Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Msama atangaza kiama kwa maharamia wa kazi za wasanii

$
0
0


KAMPUNI ya Udalali ya Msama, imetangaza msako wa wezi wa kazi za sanaa kwa ujumla wake ambao wamekuwa kikwazo cha wahusika kutofaidi matunda ya ubunifu, jasho na kazi zao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msama alisema kazi hiyo ngumu na muhimu kwa maslahi ya wasanii na Serikali, inaa siku yoyote kuanzia sasa.Msama alisema kutokana na wizi huo kuwanyonya wasanii pamoja na kuikosesha Serikali pato lake halali kupitia kodi, kampuni yake imepewa jukumu hilo kwa msaada wa Jeshi la Polisi.
“Naishukuru Serikali kwa kusikia kilio cha wasanii mbalimbali kuanzia wale wa muziki wa injili, Dansi, Bongo Fleva na hata  wengineo, wamekuwa wakilia kazi zao kutajirisha wajanja,” alisema Msama.Msama alisema kibaya zaidi ni kwamba, wizi huo wa kazi za sanaa  sio tu umekuwa ukiwanyonya wasanii, pia ni kuinyima Serikali mapato halali kwa ajili ya kuzitumia kwa maendeleo ya nchi.

Alisema kazi hiyo itakayofanywa na kampuni yake kwa ushirikiano wa karibu zaidi na Jeshi la Polisi, utagusa mikoa yote ya Bara kwa kukamata wote wenye kuuza kazi zisizotambulika kisheria.“Hii ni pamoja na kazi zote zisizo na stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hivyo wenye kuuza CD, DVD feki pamoja na kunyonya kazi za wasanii katika flash, wote hawatabaki salama,” anasema.

Alisema ni heri wenye kujihusisha na kazi hiyo haramu, wakatafute kazi nyingine halali kwani tayari wanayo majina, hivyo wanajua waanzie wapi siku na saa ya kuanza kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.“Tunatangaza kuwa, tunaingia kazini kusaka wote wenye kujipatia vipato kutokana na ubunifu na jasho la wengine, huku wahusika wakibaki masikini. Msako huu hautaacha mtu,” alionya Msama.

Mbali ya ukurugenzi mkuu katika kampuni hiyo ya Udalali, Msama pia ndiye mdau aliyechangia kukua kwa muziki wa injili kupitia uratibu wa matukio ya Tamasha la Pasaka, Krismas ama uzinduzi wa kazi mpya.Alisema katika hatua ya awali, msako huo utakaokuwa chini ya Polisi wapatao 100 katika maeneo mbalimbali ya nchi, utaanzia jijini Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma.
2
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Udalali ya Msama, Alex Msamaakizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake leo,jijini Dar.

TAASISI YA JKCI YATADHARISHA WATUMIAJI WA SIGARA.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa Habari(hawapo pichani) alipokuwa akizungumzia uhusiano wa matumizi ya tumbaku na magonjwa ya moyo jana Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Frank Shija -MAELEZO.

Na Agness Moshi – MAELEZO.
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imetoa taadhari kwa watumiaji wa sigara kujiepusha na matumizi ya sigara kwasababu wapo kwenye hatari ya kuugua magonjwa ya Moyo yanayo sababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye mahojiano maalum Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI  Prof. Mohamed Janabi amesema ni vyema wananchi kujiepusha na utumiaji wa sigara kwa sababu moshi unapoingia kwenye moyo huaribu na kuziba mishipa inayopitisha damu kwenye Moyo na hivyo kuusababisha kushindwa kufanya kufanya kazi yake vizuri.

 “Moyo umezungukwa na mishipa ya damu ambayo inauwezesha kufanya kazi endapo mishipa hii itaharibiwa na moshi wa sigara,damu inayozalishwa kutoka kwenye moyo itakua chache na hivyo kusababisha mtumiaji kupata matatizo ya moyo  kama vile mshituko wa moyo, kushindwa kupumua vizuri kutokana na kubanwa kwa mishipa ya damu”,alisema Prof.Janabi.

Prof.Janabi amesema kuwa, kwa kawaida Moyo wa binadamu kila unapopiga unatakiwa uzalishe milita 70 ambapo kwa mapigo 70 ni sawa na mililita 4900 ambazo ni sawa na lita 5  kwenye mwili wa binadamu ikitokea mishipa ya damu imezibwa damu itazalishwa kwa uchache hivyo kusababisha mtu kuvimba miguu, kushindwa kupanda ngazi au sehemu za miinuko na kupata maumivu makali kama amechomwa na kisu.

Prof.Janabi ameongeza kuwa kuziba kwa mishipa ya kupitisha damu kwenye moyo hakuuathiri Moyo tu bali mwili mzima ikiwa ni pamoja na ubongo, hivyo inapotokea mishipa hiyo imezibwa kunahaja ya kutafuta njia ya kusaidia damu ipite vizuri kwenye moyo kwa kupandikiza mishipa mingine ambayo itatolewa kwenye sehemu nyingine za mwili kama kwenye miguu na mikono au kwa kumuwekea mgonjwa chuma ambacho kitasaidia damu kupita vizuri.

Prof.Janabi alisema kuwa, gharama zinazotumika kwa ajili ya kusaidia mishipa iliyoharibiwa ni kubwa ukilinganisha na faida mtumiaji wa sigara anayoipta kutokana na utumiaji wa sigara kwa sababu vifaa vyenyewe viavyotumika ni ghali, gharama za uchunguzi na matibabu, pia muda wa kumuokoa ni muhimu kuzingatiwa endapo  mgonjwa ameathirika sana.

“Kama mishipa ya damu imebana kwa asilimia 90 au 100 Mgonjwa anatakiwa afike Hospitalini ndani ya lisaa limoja na nusu endapo atachelewa hakuna kitakachoweza kufanyika zaidi ya Kifo unaweza ukawa na uwezo lakini muda hautakuruhusu”,alisisitiza Prof.Janabi.

Aidha, Prof.Janabi amesema kuwa ,tatizo la uvutaji wa sigara nchini si kubwa sana ukilinganisha na Nchi za magharibi japo linakua kwa kiasi kwenye miji mikubwa  ambapo watu watumiaji na watu wanaokaa karibu na mtumiaji kwa muda mrefu wanaathiriwa na Moshi unaotokana na sigara  ambapo athari zake huonekana kwa nyakati tofauti.

“Wagonjwa wengi tunapokea hapa wanakua na sababu nyingine kama uzito mkubwa,Kisukari na presha na kwa uchache tunapokea wagonjwa wanaumwa kwa sababu ya matumizi ya sigara kwa wingi ,unakuta wanatumia pakiti moja hadi tatu kwa siku pia mara nyingi tunapowafanyia uchunguzi wa awali wagonjwa ni ni lazima tuwaulize kama wanatumia sigara kwa sababu sigara ni moja ya kisabishi cha ugonjwa wa Moyo”, alisema Prof.Janabi.

Hata hivyo, Prof.janabi  ametoa wito kwa Wananchi kuhakiksha wanapima Afya zao mara kwa mara ili waweze kugundua matatizo mapema kabla hayajaleta na madhara makubwa kwenye mwili pia amewataka watumiaji wa sigara kujiepusha na matumizi ya sigara kwani madhara yake ni makubwa.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MAKAO MAKUU YA KAMISHENI YA KISWAHILI YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Maryam Kidiko na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.
KUANDALIWA kwa kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki ni miongoni mwa juhudi za kuendeleza lugha ya Kiswahili katika ukanda huo na Duniani kwa jumla.
 Hayo ameyasema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko katika ukumbi wa  Hoteli ya Golden Tulip iliopo Malindi Mjini Zanzibar.
 Alisema kongamano hilo lililowashirikisha wataalamu wa lugha ya Kiswahili wa nchi wananchama wa Afrika Mashariki  lina umuhimu mkubwa katika historia ya maendeleo ya Kiswahili duniani pamoja na kupanga mikutano na kubadilishana utalaamu .
  Hivyo Alieleza kuwa ni muhimu kwa kamisheni kusimamia kwa makini hadhi ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ikitambuwa kwamba ukanda wa Afrika Mashariki ni sehemu ya Dunia yenye lugha tofauti.
 Samia alisema uratibu na uendelezaji wa Maendeleo na matumizi ya Kiswahili utaimarisha mchakato na utengamano wa Jumuiya kwa maendeleo endelevu. “Utengamano wa Jumuiya sio tukio bali ni mchakato ambao unapaswa kuendeshwa na watu wenye kuelewa vizuri matumizi endelevu ya Kiswahili “Alisema Makamo wa Rais.

04  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwaonyesha wajumbe walioshiriki  Kongamano la kwanza la Kimataifa la Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mpango mkakati wa miaka mitano wa Kamisheni hiyo (kulia) Mtendaji Mkuu wa Kamisheni Prof. Kenneth Simala na (kushoto) Rais Mstaafu wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi.


TFF YAUNDA KAMATI YA TUZO ZA WACHEZAJI CHINI YA MSAFIRI MGOYI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeunda Kamati ya Tuzo za Wachezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, chini ya Mwenyekiti, Ahmed Iddi Mgoyi, maarufu kama Msafiri Mgoyi.

Katika Kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti atakuwa Almasi Kasongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam, wakati Katibu Mkuu ni Amir Mhando, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu itakuwa inachagua wachezaji bora wa mwezi, goli  bora, mwamuzi bora, kocha, kipa bora na mchezaji bora wa msimu. 

Ahmed Iddi Mgoyi maarufu kama Msafiri Mgoyi ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wachezaji Bora wa Ligi Kuu

Wajumbe wa Kamati hiyo ni Katibu Mkuu wa zamani wa Simba SC, Patrick Kahemele, Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula, mchezaji wa zamani wa kimataifa nchini, Said George na Waandishi wa Habari Ibrahim Masoud, Fatma Likwata, Salehe Ally, Gift Macha na Zena Chande.


 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Alfred Lucas


ROTARY YAZINDUA MPANGO WA KUHIFADHI MAZINGIRA NCHINI

$
0
0
Shirika la kimataifa la huduma la Rotary nchini Tanzania limezindua mpango maalumu wa miaka mitano wa kuhifadhi mazingira. Mpango huo ulizinduliwa rasmi katika shule ya secondary ya Tambaza jijini Dar es Salaam kwa tukio la upandaji miti 70 katika eneo la shule hiyo hivi karibuni.

Kupitia mpango wa mazingira wa Rotary unaoitwa Rotary Mission Green, shirika hilo limedhamiria kuwekeza katika mazingira kwa kipindi cha miaka mitano kupitia mikakati miwili wa kwanza ukiwa ni kuhamasisha kupunguza matumizi ya nishati itokanayo na miti katika taasisi kubwa kwa kutambulisha nishati mbadala. Na pia kwa kuhamasisha na kushiriki katika zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na serikali za mitaa, mashirika binafsi na jamii kwa ujumla.

Akizungumza katika tukio hilo, mgeni rasmi ambaye alikuwa Mhe. Prof. Faustin Kamuzora, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira alihakikishia Rotary ushirikiano wa serikali katika utekelezaji wa mpango huu ambao uko sambamba na malengo ya serikali katika uhifadhi wa mazingira.

“Katika ngazi ya serikali tunaahidi Rotary kuwa tutashirikiana nanyi kwa kuwapa msaada wa kiufundi, maeneo, miche, elimu kwa umma na pia ufuatiliaji na tathmini wa mradi. Hivi sasa tunahamasisha wananchi waishi maisha yanayohifadhi mazingira, kila mmoja wetu ana jukumu la kushiriki katika mpango huu sio tu kwa kupanda mti bali kwa kuishi kwa kufikiria mazingira. Elimu kwa umma ni muhimu sana kwa sababu tunaamini kila mmoja wetu akielewa anachotakiwa kufanya katika kuhifadhi mazingira basi atafanya maamuzi yaliyo sahihi akiwa katika utekelezaji wa shughuli zake za kila siku,” aliongeza Mhe. Kamuzora.

Naye kiongozi wa Rotary Gavana Kenneth Mugisha akizungumzia mpango huo wa Rotary alisema kuwa shirika hilo mara zote hujihusisha katika miradi ya kusaidia jamii yenye malengo ya muda mrefu.

“Mpango huu wa Rotary Mission Green ni moja ya miradi mikubwa sana ambayo tumewahi kufanya katika jamii. Hapa Tanzania pekee tunategemea kupanda miti takribani milioni 5 au zaidi na pia kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala. Tunapiga hatua muhimu sana leo hii katika uhifadhi wa mazingira kwa kizazi kijacho cha wajuukuu zetu na watoto wao,” alielezea Rotary Gavana Mugisha.

Kupitia mradi huu Rotary pia itachangia katika uchumi kwa kuwezesha wapandaji miche ya miti ambao miche hiyo itatumika katika mradi na vile vile baadhi ya miti inayopandwa pia kutakuwa na miti inayoweza kutumika katika biashara kama vile za matunda au bidhaa za mbao, na hivyo kuongeza kipato kwa familia na jamii.

Katika mradi wa Rotary wa mazingira, miti itapandwa katika maeneo mbali mbali nchini ikiwemo, pembeni mwa barabara, sehemu za maegesho ya magari, katika taasisi mbali mbali za srikali na binafsi, mahospitali kwa nia ya kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi, kupendezesha mazingira, kupunguza kelele na magonjwa.

Mradi wa Rotary wa mazingira pia unategemea kushirikiana na mashirika na taasisi mbalimbali katika kuwezesha mradi kifedha, au kushiriki kupanda miti katika maeneo yao na watakaohakikisha miti inayopandwa inatunzwa hadi kukua.

Rotary Tanzania imechukua hatua hii ya kuhifadhi mazingira ikiwa kama agizo la Rais wa Rotary Kimataifa Ian Riseley ambaye ameagiza kila mwanachama wa Rotary duniani kote ashiriki kupanda hata mti mmoja na hivyo kuhakikisha katika mwaka huu miti milioni 1.2 inapandwa duniani.

BEN POL KUACHIA ALBAMU YAKE YA "THE BEST OF BEN POL' KESHO KUTWA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol ' maarufu kama kidume ameamua kuachia albamu yenye nyimbo 15, iitwayo The Best Ben Pol' itakayoanza kuwa mtaani keshokutwa ikiwa ni siku yake maalum ya kuzaliwa.

Mkali huyo wa R n B kesho kutwa Septemba 8 atasheherekea siku yake ya kuzaliwa huku akiachia albamu hiyo, ambayo itakuwa ikimfikisha miaka 8 toka kuanza kwake muziki wa kizazi kipya hapa nchini. 

Akizungumzia ujio wa albamu hiyo pamoja na wimbo wake mpya unaoitwa 'Kidume' ambao amemshirikisha mwanamuziki maarufu wa kike kutoka nchini Nigeria Chidinma, alisema kuwa uamuzi wake wa kutoa albamu ni kutaka kuendelea kuwa karibu na mashabiki wake ambao bila ya wao asingefika hapo alipo. 

Ben Pol alisema albamu mpya itatolewa rasmi kesho kutwa ambayo ni siku yake ya kuzaliwa na itakuwa na nyimbo 15, ikiwa na mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali ambazo amezifanya kwa kushirikiana na wasanii wenzake wa muziki huo. 

"Mimi kama msanii nguli hapa nchini na Afrika Mashariki niliyefanya kazi yangu kwa miaka minane sasa, naona si vibaya kuendeleza muziki wangu kwa kutoa zawadi kwa mashabiki wangu kwa kutoa albamu yangu ya “Best of Ben Pol” ikiwa na nyimbo 15 nilizoshikirisha wasanii mbalimbali wkiwemo Darasa na Rama Dee” alisema Ben Pol. 

Alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu sasa ni mwaka wake wa nane katika safari yake ya muziki ikiwa ni pamoja na kuungana na mashabiki wake ambao wamekuwa wakimuunga mkono kila anapotoa nyimbo zake mpya. 

Albamu hiyo yenye mchanganyiko wa nyimbo mbalimbali ambazo amezifanya na kuweza kufanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya hapa nchini,ikiwa na nyimbo ijulikanayo kama Kidume, Tatu na Tuliza Boli, ambazo amewashirikisha Darasa na Rama Dee.

Katika kuhakikisha mashabiki wake wanapata vitu vizuri Ben Pol amehakikisha anafanya kazi nzuri katika nyimbo zake hizo mpya kama zile zilizopita ambazo mpaka leo zinaendelea kufanya vizuri na baadhi zikiwa Nikikupata, Maneno,Jikubali, Yatakwisha, Sophia, Moyo Mashine, Pete na Phone na kama msanii mwenye uwezo katika ukanda wa Afrika Mashariki anaamini kila mshabiki atapenda kupata albamu yake. 

NMB yazinduwa matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Amos Makalla akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi la NMB Uyole uliofanyika jijini Mbeya. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.
 Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Ndani – Augustino Mbogella akizungumza na wateja wa NMB waliokusanyika kushuhudia uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni wilayani Songwe katika mkoa wa Songwe. Ufunguzi wa tawi hili unafanya idadi ya matawi ya NMB 31 kwa mikoa ya kanda ya Nyanda za juu yaani Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Katavi.

BENKI ya NMB Imefungua matawi saba kwa mpigo katika mikoa sita ikiwa ni juhudi za kujiimarisha zaidi na kuwa karibu na Wateja wake wa kanda ya nyanda za juu.

Matawi hayo yamefunguliwa katika mikoa ya Njombe, Mbeya,Songwe, Rukwa na Katavi. Matawi ambayo yamefunguliwa na yanatoa huduma kwa jamii ni pamoja na NMB  Kasumulu, NMB Uyole, NMB Mkwajuni, NMB Wanging’ombe, NMB Laela na NMB Kalambo lililopo Mlele.

Idadi hii ya matawi mapya inafanya jumla ya matawi ya NMB 31 katika kanda ya Nyanda za Juu huku yakifikia matawi ya NMB 207 nchi nzima.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la NMB Uyole lililopo mkoani Mbeya, Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu - Badru Iddy amesema kuwa lengo la Benki hiyo ni kusogeza huduma zaidi kwa wananchi ili kuwa karibu na wateja wake.

“Kuzinduliwa  kwa tawi hili la NMB Uyole mahali hapa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wetu wa Uyole kupata tawi la NMB lenye nafasi ya kutosha .Aidha  eneo hili ni karibu zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wetu wakubwa na wananchi kwa ujumla. Tawi hili  kama yalivyo matawi yetu mengine nchini linatoa huduma zote za kibenki zitolewazo na benki yetu," alisema Badru.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Uyole, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya - Amos Makalla alisema kuwa Wananchi wanapaswa kufungua akaunti katika Benki hiyo na kuitumia kwa kuwa serikali ina hisa ya asilimia 32 katika Benki hiyo.

“Hapa tuelewane, Serikali na Benki ya NMB ni sawa na mapacha kwa kuwa kila mahala ambapo serikali imepeleka huduma zake za kijamii Benki hiyo hufuatia kwa kuweka huduma za kifedha ili kuwahudumia wananchi wa eneo husika,” alisema Mheshiwa Makalla.

Huko Mkoani Songwe Mkuu wa Wilaya ya Songwe  - Samwel Jeremiah ambaye alimwakilisha mkuu wa Mkoa huo  - Chiku Galawa kwenye uzinduzi wa tawi la NMB Mkwajuni, aliwataka wananchi kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha na hivyo kutumia fursa zinazotokana na benki ya NMB kukuza uchumi wao na mwisho kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa ujumla. Alisema desturi ya kuhifadhi fedha  Benki kunajenga nidhamu ya matumizi ya fedha kuepuka madhara ambayo yanaweza kutokea.

MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha pili cha Bunge la nane leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala akijibu swali wakati wa kikao cha pili cha Bunge la nane leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura (kushoto) na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Seleman Jaffo (kulia) wakifuatilia kipindi cha Maswali na Majibu wakati wa kikao cha pili cha Bunge la nane leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa kikao cha pili cha Bunge la Nane leo Mjini Dodoma.


MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI SITA YENYE THAMANI YA SH. 1.2 BILIONI WILAYANI MONDULI

$
0
0
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Amour Hamad Amour amezindua miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya Sh.1.2 Bilioni.

Miradi hiyo ni wa maji katika Kijiji cha Meserani Juu ambao usanifu wake ulianza mwaka 2013 na umekamilika kwa gharama ya Sh 513 milioni wakati serikali imechangia Sh 444.5 milioni ,halmashauri ya Monduli imechangia Sh 66.6 milioni na wananchi Sh 2.2 milioni.

Pia kiongozi huyo amezindua mradi wa barabara yenye urefu wa kilometa 11kutoka Monduli hadi Kijiji cha Lendikinya uliofadhiliwa na Mfuko wa Barabara(Road Fund) kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa jumla ya Sh 272.6 milioni.Imeelezwa kukamilika kwa wa mradi huo kutarahisisha usafiri na kutachochea shughuli za wananchi kujiletea maendeleo na kusadifu azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati wa Tanzania ya viwanda.

Pia kiongozi huyo amefungua nyumba ya wafanyakazi wa afya katika Kijiji cha Mswakini Juu iliyojengwa kwa ushirikiano wa nguvu za wananchi na halmashauri ya wilaya ya Monduli kwa gharama ya sh 53 milioni.

Miradi mingine iliyozinduliwa ni kiwanda kidogo cha kuchakata chakula cha mifugo katika Kijiji cha Mungure na uzinduzi wa mradi wa MMES II (SEDP II)katika shule ya Sekondari Oltinga kwa gharama ya Sh 225 milioni
Imeandaliwa na mtandao wa www.rweyemamuinfo.blogspot.com
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa,Salome Mwakitalima akivalishwa Skafu na mmoja wa watoto wa chipukizi wakati wakiingia wilaya ya Monduli kutoka wilaya ya Arusha. 
Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta(kulia)akimpokea mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru,Amour Hamad Amour akitoa ujumbe wa Mwenge baada ya kufungua nyumba ya watumishi wa Afya katika Kijiji cha Mswakini Juu wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha kwa gharama ya Sh 53 milioni. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru,Amour Hamad Amour akimkabidhi mmoja wa wananchi Chandarua kwaajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa Malaria wakati kufungua nyumba ya watumishi wa Afya katika Kijiji cha Mswakini Juu wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha iliyojengwa kwa gharama ya Sh 53 milioni,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta. 
Wananchi wa kijiji cha Mswakini Juu wakishangilia ujumbe wa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 

Wakulima washauriwa kutumia mbegu bora kuongeza uzalishaji.

$
0
0

Na Mwandishi Wetu,Songwe.
WAKULIMA wa zao la maharage Mkoani Songwe wameshauri utumia vyema fursa ya mafunzo kutoka Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) kupitia mradi wa uhakika wa mbegu kwa chakula na kipato ili kuweza kuongeza tija ya uzalishaji na kipato katika kaya.

Hayo yamesemwa hivi karibuni Wilayani Momba na Mkuu wa Idara ya Kilimo toka shirika la Action for Development Program (ADP) Mathius Lisso ambaye pia ni bwana shamba wa mradi wa  uhakika wa mbegu kwa chakula na kipato unaotelekezwa na shirika la PELUM Tanzania kupitia ufadhili wa Taasisi ya Bread for the World.

Lisso amesema kupitia mradi huo wakulima katika vikundi hivyo watawezesha mbegu hizo kutumiwa na wakulima wengine nje ya vikundi hivyo kwa kuwa mbegu zimekidhi ubora unaotakiwa kwa mujibu TOSCI.

 “Wakulima hawa kwa sasa mbali na kufanikiwa kuandaa mbegu zao wenyewe kupitia wataalamu toka TOSCI l pia jamii inayowazunguka wameanza kunufaika na uwepo wa mbegu hizi baada ya kuona uzalishaji wake uko tofauti kulinganisha na mbegu za asili” amesema Lisso.

Ameongeza kuwa ambapo kupitia mbegu hizo mkulima atakuwa na uwezo wa kupata gunia sita hadi nane kwa heka moja iwapo atazingatia  kanuni, ikilinganisha na mbegu za asili ambapo kwa kwa ekari moja mkulima ana uwezo wa kupata debe tatu hadi  tano pekee.

Lisso amesema mbegu ambazo wakulima hao wanazozalisha ni aina ya Njano Uyole na Uyole 96 ambazo maharage yake yana soko kubwa katika nchi ya DRC Kongo na Tunduma na hivyo kuwataka wakulima kuchangamkia fursa hiyo ambayo imeanza kuleta matokeo chanya kwa wakulima kupitia uzalishaji wake.

Aidha Lisso amelipongeza shirika la PELUM Tanzania kwa kutambua mchango wa wakulima wadogo katika kukuza sekta ya kilimo na kutafuta fursa za miradi mbalimbali na kupanua wigo wa ushirikiano Maafisa kilimo na ugani wa Serikali.

Kwa mujibu wa Lisso amasema miongoni mwa malengo ya mradi huo ni kuunganisha mtandao wa wakulima nchini kupitia vikundi hatua itakayosaidia kuongeza uzalishaji hivyo ni wajibu wa TOSCI kutoa utambulisho wa vyeti kwa wakulima walio kwenye vikundi ili waweze kuwafundisha wakulima.

Kwa upande wake, mmoja wa wanakikundi cha Motomoto Erasto Mauli mmoja wa amesema mbali na mbegu hizo kuanza kutumiwa na wakulima wenzao ndani ya kata pia wameweza kupanua wigo wa masoko hadi maeneo ya Tunduma.

Mauli alisema uwepo wa mizani feki kutoka kwa umesababisha wengi wao kutopata faida hali inayochangia mkulima kunyonywa, kwani mbali na dalali kupata faida ya shilingi 5000-7000 kwa kila debe bado anakuwa na faida ya kilo tatu hadi nne kwa kila debe kutokana na madebe yao kuwa makubwa.

Mradi wa uhakika wa mbegu kwa uhakika wa chakula na kipato unaofadhiliwa na wa Bread for the World na kusimamiwa na Shirika la PELUM Tanzania na kutekelezwa katika ya Mikoa Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Kigoma, Songwe, Mbeya, Manyara na Shinyanga.

LIGI YA WANAWAKE KUANZA NA LIGI NDOGO

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeagiza Makatibu wa Vyama vya Mikoa kutuma haraka majina ya timu mabingwa wa mikoa wa soka la wanawake wa msimu wa 2016/17. 

Viongozi wa mikoa wamekumbushwa kutuma timu ili kufanya maandilizi ya haraka ya Ligi Ndogo itakayofanyika Septemba 22 hadi 29, mwaka huu. Ligi Hiyo ndogo inachezwa kutafuta timu mbili zitakazopanda daraja kucheza Ligi Kuu soka ya wanawake msimu wa 2017/2018. Huu ni msimu wa pili wa ligi ya wanawake kwani msimu uliopita, timu shiriki zilikuwa 12 na Mlandizi Queens ya Pwani iliibuka bingwa wa kwanza katika historia ya soka hapa nchini. 

Mara baada ya kumalizika kwa Ligi Ndogo, TFF itaanza taratibu za kupanga kuanza kwa Ligi Kuu kwani wakati huo tayari tutafahamu timu ambazo zimepanda. Ligi Ndogo haitahusisha timu ambazo zimecheza Ligi Kuu msimu wa 2016/17.

BARAZA LA MADIWANI TEMEKE LAMVUA UDIWANI YUSUF MANJI KWA KUKOSA VIGEZO

$
0
0
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Temeke Mhe; Abdallah Chaurembo amvua udiwani Mhe; Yusufali Mehbub Manji ambaye alikua diwani wa kata ya Mbagala Kuu. 

Utenguzi huo ulifatia uvunjwaji wa kanuni za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke za Mwaka 2015 kifungu cha 72(C) ambacho kinamtaka Diwani pamoja na majukumu mengine aliyonayo lazima ahudhurie mikutano ya Halmashauri na kamati ndogo ambayo yeye ni mjumbe bila kukosa.

Aidha sheria ya serikali za Mitaa sura ya 8 ya 1982 kifungu cha 25(5) (a) (b) kinaeleza kuwa mjumbe wa Baraza la Madiwani ambaye hakuhudhuria vikao vitatu mfulULIZOzo bila taarifa yeyote ya maandishi kwa Mwenyekiti atakuwa amejiondoa katika nafasi hiyo. 

Lakini pia kanuni za kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Temeke za mwaka 2015 zinaeleza wazi kuwa kiti cha mjumbe wa Halmashauri kitakuwa wazi endapo mjumbe bila sababu ya kuridhisha au bila idhini au kibali cha maandishi cha Mwenyekiti, atakosa kuhudhuria mikutano mitatu (3) ya kawaida ya Halmashauri inayofuatana au kamati ambayo yeye ni mjumbe, nafasi yake inatakiwa kuwa wazi (kifungu cha 73(1) (m).

Kutokana na vifungu hivyo vya kanuni vinamlazimu Mstahiki Meya kuengua nafasi hiyo ya Diwani wa kata ya Mbagala Kuu. Pia mstahiki Meya amemwandikia barua yenye viambatanishi ya utenguzi huo kama sehemu ya utaratibu unaojulikana katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe; George Simbachawene kuwa nafasi hiyo sasa ipo wazi, ili taratibu zingine zifuate.

Awali Tarehe 20/2/2017 Mhe; Yusufali Mehbub Manji aliandika barua kwa Mkurugenzi yenye Kumb.Na. YM-MBGKUU/51/2017 akitoa taarifa ya kutoweza kuhudhuria vikao vya Halmashauri kutokana na sababu za kiafya bila ya kuwasilisha uthibitisho wa daktali. Vikao alivyo vikosa baada ya kuandika barua yake ni vile vya tarehe 3-4/3/2017, 18-19/5/2017 na 24-25/8/2017. 

Tarehe 22/3/2017 Mkurugenzi alimwandikia barua yenye Kumb. Na TMC/MD/K.11/58/57 akimtaka awasilishe taarifa za kidaktari kuthibitisha matatizo ya kiafya kama alivyoeleza kwenye barua yake jambo ambalo hakulitekeleza. Aidha tarehe 22/5/2017 aliandika barua yenye kumb na. YM/MBGKUU/64/2017 ambayo ilinakilishwa kwa Mkurugenzi akieleza kutohudhuria vikao vya Halmashauri kwa sababu za kiafya bila kuweka uthibitisho wowote lakini pia akiweka wazi nia yake ya kutaka kujiuzulu kama hali yake ya afya haitaimarika.

”kwa kuwa Mhe. Yusufali Mehbub Manji hakuhudhuria vikao na mikutano ya Halmashauri inayofuatana bila kutoa taarifa (mikutano ya tarehe 3/2/2016,24/3/2016,1/6/2016,25/8/2016, 24/11/2016, 14-15/2/2017) na vikao vya kamati ambavyo yeye alikua mjumbe vya tarehe 18/3/2016, 17/8/2016, 8/11/2016, 2/2/2017,(hata vikao na mikutano aliyo toa taarifa alishindwa kuthibitisha taarifa za ugonjwa) pia amevunja kanuni za Halmashauri pamoja na sheria ya Serikali za Mitaa sura ya 8 ya mwaka 1982 kifungu 25(5) (a) (b) kama kinavyosomeka hapo juu, hivyo nawasilisha taarifa rasmi kuwa Bwana Yusufali Mehbub Manji amekosa sifa ya kuendelea kuwa Diwani wa kata ya Mbagala na kwamba kata hii itangazwe kuwa iko wazi". alisema Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mhe; Abdallah Chaurembo.

MKUU WA WILAYA KIBAHA ASSUMPTER MSHAMA AFUNGA MACHINJIO YA PANGANI KIBAHA KWA MUDA USIOJULIKANA

$
0
0
MKUU wa Wilaya  ya Kibaha  Mkoani Pwani  Bi Assumpter Mshama  ametoa amri ya kufungia  machinjio mapya yaliyopo  Mtaa wa Mtakuja Pangani  Kibaha  Mkoani Pwani kwa muda usiofahamika  kutokana na kukithiri kwa uchafu  unaotishia  afya za walaji  wa eneo  la Kibaha na Vitongoji vyake

Bi Assumpter ametoa amri hiyo muda mfupi uliopita baada ya kufanya ziara ya kushtukiza machinjioni hapo.

Aidha  Bwana Afya Ramadhan Mohammed  ambaye husimamia  shughuli za machinjio hayo amekiri  kuwa  machinjio hayo yanakabiliwa na changamoto nyingi  ikiwa hi pamoja na ukosefu wa maji na umeme.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WADAU WA ZAO LA KOROSHO OFISINI KWAKE DODOMA , AWATAKA WAFANYENI TATHMINI YA ZAO LA KOROSHO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa zao la Korosho kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma Septemba 5, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Bodi ya Korosho Tanzania zifanye tathimini ya maandalizi ya msimu ujao kwa wakati na zimpatie taarifa mara moja.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana usiku (Jumanne, Septemba 5, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao la korosho kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma kujadili mwenendo wa zao la korosho na ununuzi wa pembejeo.

“Lipo tatizo la tathmini ya maandalizi ya msimu kutofanyika kwa wakati na kusababisha matatizo kutotatuliwa kwa wakati. Bodi na Wizara zitoe tathimini ya maandalizi ya msimu ujao kuhusu vyama vya ushirika vilivyojipanga, upatikanaji wa vifaa kama magunia na nyuzi, maghala, masoko, mizani, minada, malipo na mfumo wake,” alisema.

Waziri Mkuu pia alizitaka Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Korosho zitoe tathimini ya maandalizi ya msimu ujao katika maeneo ya mashamba, miche, pembejeo na viatilifu. Alisema tangu Serikali iamue kusimamia mazao makuu matano ya pamba, chai, kahawa, korosho na tumbaku hajapata muda wa kukaa na kuongea na wadau wote. “Serikali imeamua kufuatilia usimamizi wa mashamba; kusimamia upatikanaji wa mbegu, miche na pembejeo; kufuatilia uvunaji na mfumo wa masoko ya korosho na pia kufuatilia mfumo wa ushirika katika baadhi ya mazao,” alisema.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

WAZIRI MKUU APOKEA RIPOTI ZA UCHUNGUZI WA BIASHARA YA ALMASI NA TANZANITE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti mbili za kamati ya Maalumu ya Bunge ya kuchunguza biashara ya madini ya almasi na tanzanite na kuahidi kuiwasilisha kwa Rais Dkt. John Magufuli kesho asubuhi.

Pia amesema Serikali haina mchezo katika usimamizi wa rasilimali za Taifa, hivyo amewataka viongozi  na watendaji wote waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia sekta ya madini hakikisha wanatimiza vyema wajibu wao.

Waziri Mkuu amepokea ripoti hizo leo (Jumatano, Septemba 6, 2017) kutoka kwa Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai ambaye alikabidhiwa ripoti hizo  na Wenyeviti wa kamati Bw. Mussa Zungu (Almasi) na Bw. Dotto Biteko (Tanzanite).

“Kesho saa 4.30 asubuhi nitaziwasilisha ripoti hizi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli. Hakuna ucheleweshaji katika jambo hili na Mheshimiwa Spika (Job Ndugai) kesho twende tukakabidhi wote.”

Waziri Mkuu amesema kamati hizo zimefanya kazi nzuri na kwamba Serikali inaimani  na ripoti hizo na ushauri uliotolewa utawezesha Taifa kunufaika na rasilimali zake, hivyo mapendekezo na hoja zote zilizoibuliwa zitafanyiwa kazi katika kipindi kifupi.

Amesema taarifa hiyo zimewasilishwa katika kipindi muafaka na zimeonyesha  dhamira ya dhati ya Bunge, kuunga  mkono juhudi za Rais Dkt. Magufuli  na Serikali yote kwa ujumla katika kulinda rasilimali za Taifa.

“Watanzania ni mashahidi kwamba Mwenyezi Mungu ameijalia Tanzania utajiri wa rasilimali za kila aina.  Tunayo ardhi yenye rutuba, madini ya aina mbalimbali na mengine hayapatikani katika nchi nyingine isipokuwa Tanzania tu kama vile Tanzanite.”

Amesema ni  lazima rasilimali hizo zisimamiwe na kutunzwa vizuri ili ziwezeshe kuboresha hali na maisha ya Watanzania wote na kila mwananchi ana jukumu la kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuleta mageuzi katika Sekta ya madini nchini.

Waziri Mkuu amesema suala la kusimamia rasirimali za nchi ni la Watanzania wote kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 27 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo aliinukuu Ibara hiyo kama ifuatavyo:

“27 (1) kila mtu ana wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na Wananchi na pia kuiheshimu mali ya mtu mwingine.

“(2) Watu wote watatakiwa na Sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya nchi na pamoja vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu na kuendesha uchumi wa Taifa na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao.”

Kamati hizo zilipewa jukumu la kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na Almasi Nchini, ambazo zimeishauri Serikali kuhusiana na mfumo bora wa uendeshaji na udhibiti wa biashara ya Tanzanite na Almasi  nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Spika wa  Bunge, Job Ndugai Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuchunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017.  Katikati ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Maalum iliyoundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai kuchunguza Biashara ya Tanzaniate wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza  baada ya kukabidhiwa na Spika wa Bunge Job Nduga  Taarifa hiyo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. 
Baadhi ya Wabunge walioshiriki katika hafla ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya Bunge ya Kuichunguza Biashara ya Tanzanite na Almasi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  Maalum iliyoundwa na Spika ya  Kuchunguza Biashara ya Tanzanite baada ya Spika kupokea Tarifa hiyo na kumkabidhi Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 6, 2017. Aliyekaa kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na aliyeka kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Job Ndugai. 

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  Malum iliyoundwa na Spika   Kuchunguza biashara ya  Almasi baada ya Spika kupokea Taarifa hiyo na kumkabidhi Waziri Mkuu kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septembea 6, 2017. Aliyekaa kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson na aliyeka kulia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Job Ndugai. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ASKOFU DKT. CHARLES GADI AFANYA MAOMBI KWA TAIFA LA MAREKANI JUU YA KIMBUNGA

BUSWITA RUKSA KUCHEZA YANGA, ATAKIWA KUILIPA SIMBA MILIONI 10

$
0
0
Kamati ya Sheria katiba na hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF wamemfungulia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja iliyokua inamkabili mchezaji Pius Buswita ambaye alifungiwa kutokana na kusaini mikataba miwili na timu za Yanga na Simba.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari asubuhi ya leo Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Elias Mwanjala amesema Simba,Yanga na Mchezaji mwenyewe wamekubaliana Pius Buswita alipe pesa alizochukua katika klabu ya Simba wakati akisaini mkataba wa makubaliano ya kuichezea klabu hiyo.

Wakili Mwanjala amesema kilichofanywa na klabu hizo mbili ni busara tu ili kumpa nafasi mchezaji huyo acheze kinyume cha hapo mchezaji huyo angeendelea kutumikia adhabu yake na walichokitaka Simba wao ni kulipwa tu pesa zao ili kuondoa lalamiko hilo na mchezaji mwenyewe ameahidi mbele ya kamati kwamba atalipa.

Kiasi cha milioni 10 pamoja na gharama zingine ikiwa ni pamoja na usafiri na malazi ambazo kwa pamoja zinafikia milioni 1 ndizo zilizotajwa na Simba kwenye barua yao waliyoiwasilisha TFF na ndicho kiasi ambacho Yanga na mchezaji wameahidi kulipa na kamati imetoa onyo kali la kimaandishi kwa mchezaji huyo na ataruhusiwa kucheza tu iwapo Simba watathibitisha kulipwa pesa zao.

Buswita mchezaji wa zamani wa Mbao FC ya Mwanza alijikuta akifungiwa na shirikisho la soka nchini baada ya kusajiliwa na Yanga huku pia akiwa amesaini mkataba na Simba.

VIDEO: UWANJA WA MAJIMAJI WAKARABATIWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA RUVUMA

$
0
0
Uwanja wa MAJIMAJI ambao unamilikiwa na chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma CCM umefanyiwa malekebisho ili uweze kutumika vizuri katika mashindano mbalimbali ikiwemo ,ligi kuu ya Tanzania bara ambayo imeanza hivi karibuni.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO, AAGANA NA BALOZI WA CHINA AONANA NA MZEE BUTIKU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0




  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. José Graziano da Silva  alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa  Mwakilishi Mkazi wa FAO  nchini Bw.  Fred Kafeero    na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Meshack Malo Ofisa aliyeongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea kitabu na kadi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Bw.  Bw. José Graziano da Silva alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na  Mkurugenzi Mtendaji wa Mwalimu Nyerere Foundation Mzee Joseph Butiku aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya kinyago  Balozi wa China aliyemaliza muda wake nchini Dkt. Lu Youqing    alipofika kumuaga Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2017.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Introducing "KICHAKA" by Saida Karoli, Belle 9 na G Nako - Behind the scene

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images