Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

Waziri wa Fedha atoa ufafanuzi juu ya tathmini ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania iliyofanywa na Shirika la fedha duniani (IMF)

$
0
0
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya tathmini ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania iliyofanywa na Shirika la fedha duniani(IMF) . Wengini ni Mwakilishi Mkazi wa IMF Thomas Baunsgaard(kulia) na Naibu Waziri wa Fedha Janet Mbene(kushoto). Picha na Shakila Galus-MAELEZO-Dar es salaam

Na Heka Paul -MAELEZO-Dar es salaam

Shirika la Fedha Duniani(IMF) limepoingeza Tanzania kwa usimamizi mzuri wa kisera ambao umesaidia utulivu wa kiuchumi ambao umesaidia kuleta matumaini hatua iliyosababisha mfumuko wa uchumi hapa nchini kuendelea kushuka.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwakilishi Mkazi nchini wa IMF Thomas Baunsgaard wakati wa mkutano wake yeye na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa na waandishi wa habari jijini Dar es salam juu ya kuelezea tathmini ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania iliyofanywa na Shirika la fedha duniani(IMF) .

Alisema kuwa ni muhumu kuendelea kudhibiti sera za mapato na matumizi ya serikali na sera za usimamizi wa fedha ili kuwa na uchumi endelevu.

Bw. Baunsgaard alisema kuwa Tanzania imedhamiria kuchukua hatua za ziada ili kuhakikisha inafikiwa lengo la kupunguza mfumuko wa bei hapa nchini.

Aidha alisema kuwa Bodi ya utendaji wa shirika la IMF imeidhinisha nyongeza ya dola za Kimarekani 57 na kuifanya Tanzania kuweza kunufaika na mkopo wenye masharti nafuu toka IMF unaofikia dola za kimarekani 114.

Vilevile Bodi iliridhia ombi la Serikali ya Tanzania la kupewa msamaha wa kukuika kigezo cha madeni ya nje yenye masharti ya kibiashara kwa sababu ukiukaji huo hauwezi kuathiri uhimilivu wa deni la Taifa.

Dk Slaa azindua matawi mawili ya Chadema mjini Moshi

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Wilbroad Slaa akipandisha bendera ya Chama kuashiria uzinduzi wa tawi Jipya la CHADEMA Classic lililoko katika kata ya Longuo mjini Moshi.
Meya wa manispaa ya Moshi,Jafary Michael akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Chadema Classic lililopo kata ya Longuo mjini Moshi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Wilbroad Slaa akikata utepe wakati akizindua tawi la vijana wa CHADEMA la Aslam Garage mjini Moshi.
Diwani wa viti maalum,Hawa Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la vijana wa Chadema katika eneo la Aslam Garage mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Baraza kuu la vijana wa Chadema (BAVICHA),John Heche akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Chadema classic lililopo kata ya Longuo B mjini Moshi.Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SIKU 3 WA AFYA YA MAMA NA MTOTO,JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo Januari 15, 2013, jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya na wa Mkoa wa Arusha, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo, jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC, Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo, jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Afya wa Rwanda, Agnes Binagwaho, baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo, jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa na waratibu wa mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma ya asili wakati akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC baada ya kufungua Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo, jijini Arusha.
Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

Rais wa Benin kuwasili nchini leo kwa ziara ya kikazi

$
0
0
Rais wa Benin ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA), Mhe. Boni Yayi anatarajiwa kuwasili hapa nchini tarehe 15 Januari, 2013 saa 2.00 usiku kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Yayi atapokelewa na Mwenyeji wake Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiwa nchini Mhe. Yayi anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam tarehe 16 Januari, 2013. Mbali na kuzungumzia masuala ya ushirikiano kuhusu nchi hizi mbili, viongozi hao watazungumzia masuala muhimu kuhusu Bara la Afrika.

Mhe. Yayi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika wakati wa Mkutano wa 18 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja huo uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia mwezi Januari 2012 na atamaliza muda wake wa uenyekiti wakati wa Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Umoja huo utakaofanyika pia Addis Ababa tarehe 27 na 28 Januari 2013.

Mhe. Yayi anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 16 Januari 2013.

Imetolewa na: 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam.

14 Januari, 2013.

Kilimo Kwanza ni moja ya vipaumbele vyetu—Dkt. Turuka

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na technolojia, Dkt. Florens Turuka akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam jana, namna wizara yake ilivyojipanga katika utekelezaji wa dhana ya kilimo kwanza.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia imesema mkakati wa Kilimo Kwanza unaolenga kufikia mapinduzi ya kijani Tanzania ni moja vipaumbele vyake katika juhudi za kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Hii ni kwa sababu sekta hiyo ya kilimo inabeba maisha ya watu wengi hapa nchini na ikiendelezwa vizuri ina uwezo wa kubadilisha maisha ya wananchi wengi katika nchi hii ambayo ina ardhi kubwa yenye kufaa kwa kilimo.

MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU NA WAKUU WA MIKOA WATOA MAONI KATIBA MPYA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Jospeh Warioba (kulia) akiongea na Mawaziri leo katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam katika mkutano uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Nyamrunda akiongea katika mkutano kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatilia mkutano kati yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea katika mkutano kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yaokuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Mawaziri Steven Wassira, Kapteni (Mstaafu) George Mkuchika na Prof. Sospeter Muhongo wakifuatilia mkutano kati yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiongea katika mkutano kati ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali (Mstaafu) Joseph Simbakalia akiongea katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa uliolenga kupata maoni yao kuhusu Katiba Mpya. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abass Kandoro, Dkt. Rehema Nchimbi (Dodoma) na Bi. Chiku Galawa (Tanga).
Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa nchini wakipata maelezo kuhusu mfumo wa uhifadhi wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya yanayowasilshwa katika Tume kwa maandishi kutoka kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bi. Flora Mkonya leo (Jumanne, Jan 15, 2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Kanali (Mstaafu) Joseph Simbakalia(Mtwara), Bw. Abass Kandoro (Mbeya), Bi. Chiku Galawa (Tanga).na Dkt. Rehema Nchimbi (Dodoma).Wakuu hao wa mikoa pia waliwaslisha maoni ya Wakuu wa Mikoa kuhusu Katiba Mpya.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Al-Shymaa Kway-Geer, Bw. Humphrey Polepole na Bi. Riziki Mngwali wakifuatilia mkutano kati ya Tume na Mawaziri uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.

HOJA YA MDAU KUHUSIANA NA TATIZO LA USALAMA KIGAMBONI

$
0
0

Naomba kuwasilisha mtazamo wangu juu ya suala la Usalama wa Raia kwa watu wa Kigamboni
 
Kufutatia kitendo cha wanafunzi wa IFM kuandamana na kusimamisha shughul;i za kivuko kwa muda, tatizo hili sasa limepata sura mpya, na limepata kufika kwenye masikio ya watu ambao wamepewa dhamana ya kulinda raia na mali zao. 

Wimbi la uhalifu kigamboni limekuwa kubwa sana na haswa suala la hawa vijana wanaoshinda Beach (Beach Boys) kufanya mambo ambayo kimsingi yangeweza kuzuiliwa na polisi wetu. Tatizo ni "business as usual attitude" kwa askari wetu. 

Tumeshuhudia watalii wakiibiwa vitu vyao na kujeruhiwa vibaya na vijana hawa, tumeshuhudia vijana hawa wakipora mabegi ya wanafunzi, wakiwa na malengo ya kuibia wanafunzi hawa laptop zao. Askari wanafahamau vyema kabisa mambio haya. Ni askari gani wa kigamboni asiyejua kijiwe cha minazi mikinda? 

Bhangi, unga na aina zzote za dawa za kulevya zinuzwa na kutumiwa hapo. Ni askari hawa hawa wanawahi kwenda huko pindi ukitokea uporaji wa vitu hivyo (nimepata kusikia wanawahi mgao!!!????). Sasa leo tunasikia wanafunzi wanavamiwa wakiwa vyumbani mwao, wanaporwa na kudhalilishwa.

 Ni nani asiyejua kuwa ili kuondoa wimbi hili ni lazima kuboresha doria kwenye fukwe hizi za kigamboni? Ni aibu kwa nchi kwa ujumla kufuga kundi kubwa la vijana wala unga nje tu ya uwanja wa Ikulu, pale karibu na soko la samaki? Nje ya ikulu vijana wanavuta unga. Je usalama wa kilometre 1000 kutoka ikulu ilipo ukoje?
 
Maandamano ya wanafunzi Kigamboni yafungue macho ya wahusika kuhusu hali halisi ya usalama kigamboni. Wananchi wa kibada wamepitia kipindi kigumu kiasi kwamba karibu kila mwanannchi aliishia kumiliki silaha, na sio moja kwani hali ilikuwa mbaya kupita kiasi. Walinzi wa Bar wanauwawa, madereva wa taxi wanauwawa. 

Nyumba zinavamiwa kila leo. nk. Tunaona polisi wakipita kufanya doria usiku, lakini basically doria hii hulenga bar ambazo hazijafungwa baada ya saa tano (saa sita weekends). Kweli nguvu hii ya kukamata wahudumu wa bar ikielekezwa kusaka wahalifu hatutapata nafuu ya kiusalama? Nadhani bado tuna nafasi kubwa sana ya kuboresha usalama kabla hali haijawa mbaya. 

Kila wakati polisi wanawakumbusha wananchi kuwa wasichukue sheria mkononi. Tunategemea nini kama wananch wanamawazo kuwa Polisi wanashirikiana na wezi?Unawezajae kuelewa unapoambiwa kuwa wezi walitumia zaidi ya saa mbili ndani ya hostel ya wanafunzi huku wanafunzi wakike wakipiga kelele kuomba msaada?
 
Ndugu zetu polisi, kodi zetu zinapaswa kutulinda, na si kushiriki katika vitendo viovu pamoja na waovu. Wezi wote wa ferry, na haswa hawa beach boys wanajulikana. Shukeni kule chini, fanyeni doria, tumieni mbinu zenu za kiupelelezi mlizofunzwa kwa kodi zetu kuwafichua na kuwafikisha waovu hawa sehemu inayostahili na sio huku mitaani. Huku sisi tunahitaji amani, na tunahitaji kufanya mipango ya maendeleo, na sio kulala na hofu kila siku.
 
Naomba mamlaka zitekeleze wajibu wao wa kikatiba, kulinda maisha ya raia na mali zao. Sio kulinda tu maisha ya watawala kwa misafara mirefu isiyo na sababu wala tija kwa taifa letu.
 
Naomba kuwasilisha

WADAU WAZIDI KUMIMINIKA KUCHUKUA FOMU ZA UCHAGUZI WA TFF

$
0
0

Idadi ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia 26.

Hata hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.

Waliochukua leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, Titus Osoro na Zafarani Damoder.

Idadi kamili ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).

Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).

AFRICOM General Carter Ham Visits Tanzania, Commends Partnership Between United States and Tanzania

$
0
0
Commanding General for the United States Africa Command (USAFRICOM) General Carter F. Ham, (left), with His Excellency, President Jakaya Mrisho Kikwete, (center), and U.S. Ambassador Alfonso E. Lenhardt, (right), at the State House in Dar es Salaam on January 14, 2013.  General Ham made a one-day visit to Tanzania, which included a meeting with Chief of Defense, General Adolf Davis Mwamunyange, and a guest speaker lecture at the National Defense College.  His visit, in which he commended the partnership between the United States of America and the United Republic of Tanzania, was part of a nine-day trip across Africa to further AFRICOM's engagement programs with several critical partners.

Commanding General for United States Africa Command (USAFRICOM) General Carter F. Ham made a one-day visit to Tanzania on January 14.  He was accompanied by Ambassador Christopher Dell, Deputy to the Commander for Civil-Military Activities.

  During his visit, he met with President Jakaya Mrisho Kikwete and commended the strong partnership between the United States and the United Republic of Tanzania.  General Ham's visit to Tanzania was part of a nine-day trip across Africa to further AFRICOM's engagement programs with several critical partners.

In talks with General Adolf Davis Mwamunyange, the Chief of Defense, General Ham praised the professionalism of the Tanzanian military and applauded the TPDF for its support to peacekeeping missions, its active role and leadership in regional security matters and openness to partnering with the United States through extensive security cooperation programs. General Ham said, "AFRICOM remains committed to strengthening the relationship between the TPDF and the United States." 

General Ham also provided a guest speaker lecture at the National Defense College where he discussed with the class of professional military and civil sector students U.S. national defense strategy and its relationship to United States military engagement, partnership and security cooperation programs across Africa. 

The United States recognizes and applauds Tanzania's leadership and important role in the African Union and both East and South African regional associations.  The United States assists Tanzania in bringing its competencies and influence to bear on resolving conflicts in Africa and beyond.  

The United States provides support of Tanzanian peacekeeping capacity including military education, training and equipping, in addition to assisting Tanzania in strengthening its borders and addressing maritime insecurity, piracy, illicit trafficking and other transnational challenges.

bus la champion lamgonga mtembea kwa miguu na kumsababisha kifo

TOVUTI YA KULIPIA MAHOTELI NA PACKAGE ZA UTALII TANZANIA YAZINDULIWA

$
0
0

Kutokana na mahitaji ya muda mrefu ya watalii na watanzania, kupata huduma ya kuwezeshwa kulipia vyumba vya mahoteli na huduma za kitalii kwa njia ya mtandao kwa bei nafuu, kampuni ya Vinjari imeanzisha huduma hiyo kwa kupitia tovuti yake ya www.vinjari.co.tz


Kwa kupitia mtandao wa Vinjari sasa mtu yeyote mwenye kadi ya VISA (iliyowezeshwa kufanya manunuzi kwenye mtandao) na yule mwenye akaunti ya M-Pesa (Tanzania) anaweza kulipia huduma hizo sasa kwa kupitia www.vinjari.co.tz. Huduma hii imetengenezwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na kuthibitishwa na taasisi  inayoidhinisha mitandao inayotoa huduma za malipo mbalimbali duniani.


Katika kuperuzi mtandao wa vinjari, mteja ataweza kuchagua aina ya hoteli, mkoa anaotaka kwenda,tarehe anayotaka kwenda pamoja na kiasi ambacho ana uwezo wa kulipia. Mtandao huu kwa sasa unatoa huduma katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha,  Mwanza,  Kilimanjaro, Pwani, Mbeya, Kigoma, Kagera pamoja na Zanzibar.


Vinjari inawakaribisha watu wote katika ulimwengu wa kiteknolojia unaorahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali popote ulipo. Pia unaweza kufuatilia huduma za Vinjari kwa kupitia Facebook (www.facebook.com/vinjari) na Twitter (https://twitter.com/VinjariTanzania).

introducing libeneke la bongomovieTZ

$
0
0
Naomba uwajulishe watembeleaji wa mtandao wako, kutoka nje na ndani ya nchi kwamba hivi sasa kuna mtandao mpyawww.bongomovietz.com special kwa ajili ya tasnia ya filamu Tanzania. Humo kuna interviews, videos kama trailers ya movie mpya, movie reviews,picha za matukio na habari kuhusu mastaa wa bongomovie na tasnia nzima kwa ujumla. Karibuni mperuziwww.bongomovietz.com    Pia tupo facebook search bongomovietz na twitter @bongomovietz  ::SPECIAL KWA AJILI YA BONGOMOVIE NA MASTAR WAKE::

Hoja: daraja la Selander nako si salama...

$
0
0

Ahsante kaka kwa uwanja huu wa kutoa maoni.
 
Mdau aliyeandika kuhusu kigamboni amenifanya niandike hili pia. Ahsante mdau kuliona hilo.

Ukizungumzia 'beach boys' sio kigamboni peke yake, daraja la Selander sasa limekuwa hatari. Hao vijana wanajificha baharini, pande zote za daraja, wakiona upenyo kidogo tu wanakuja kwa kasi ya ajabu na kupora kwenye gari, iwe ni sight mirror au chochote wanachoweza kukifikia. 

Hii ni hatari sana, kwani inaweza hata kusababisha ajali mbali ya madhara atakayokuwa ameyapata aliyeporwa. Haya yote yanafanyika mapema tu, na limekuwa ni jambo la kawaida kila siku giza likianza tu.
 
Swali la kujiuliza, wale askari waliokuwa wakilinda maeneo hayo wakisaidiwa na mbwa, wameenda wapi? Wadau tusaidiane katika hili, hali imekuwa mbaya.


Mdau Mwenge

Balozi wa Uingereza amuaga Rais Kikwete leo

$
0
0
Balozi wa Uingereza anayemaliza muda wake Mhe. Diane Corner akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Kitabu cha historia ya Uendeshaji Jeshi la Wananchi wa Tanzania kilichoandikwa kwa ushirikiano wa wataalamu wa historia kutoka JWTZ na ubalozi wa Uingereza, wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam leo bada  ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini. Picha na Freddy Maro wa Ikulu

mama salma kikwete aandaa sherry party ya mwaka mpya

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenza wa mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao hapa Tanzania pamoja na wake wa viongozi wakati wa hafla ya Mwaka mpya(New Year Cherry Party) iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia wenza wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania wakati wa hafla ya mwaka mpya(New Year cherry Party) iliyofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam . Kupata hotuba yake BOFYA HAPA

Kali TV Online: This week, meet Kalamazoo

$
0
0
This week Kali TV speaks to Steve Mokone a.k.a Kalamazoo from South Africa. Kalamazoo was the first black African soccer player to play professional soccer in Europe. From playing for Coventry City FC in England to signing for Barcelona and Valencia in Spain. He is one of the few African legends. Please follow the link below,

JOOMLA! CMS WEBSITE DESIGN AND DEVELOPMENT TRAINING FROM 18– 22 FEBRUARY, 2013

$
0
0
The University of Dar es Salaam (UDSM), Center for Virtual Learning(CVL) is organizing a 5 days training to equip participants with the skills, knowledge and techniques for designing and developing good websites without even being experts by using Open Source Content Management System (CMS) called Joomla! CMS 2.5.8

Joomla is an award-winning CMS, which enables people to build Websites, as well as Web based applications. A summary of course outline can be found from the College website: www.coict.udsm.ac.tz


Target Audience

  • Individuals who would like to have their very own website.

  • Owner of an existing Joomla website built by another 3rd party.

  • SMEs and small businesses who wish to cut down the costs of web development projects and manage their own websites.

  • Individuals who wish to be self-employed in Website development


  • Web masters, website administrator, computer systems analysts, public relationship officers, communication officers and entrepreneurs.


Training fee:  Tsh. 500,000/= (excluding breakfast and lunch)

Venue:  UDSM Kijitonyama Campus (Former TTCL Staff College), Dar Es Salaam

Registration:Please register NOW through the College website: www.coict.udsm.ac.tz

Certificate of attendance:  will be provided upon completion of the course.

For more information contact us at saganda@udsm.ac.tz; Telephone: +255715471705

WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI WILAYANI RUANGWA WAPIGWA MSASA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Iindi,Bi Agness Hokororo (katikati) akihututubia wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya wachimbaji wadogo wa madini katika wilaya ya Ruangwa.wengine pichani ni baadhi ya viongozi wilayani Ruangwa.

Na Abdulaziz Video,Ruangwa

Wachimbaji wadogowadogo wa madini Wilayani Ruangwa wametakiwa kuacha kufanya kazi katika mfumo usio rasmi badala yake wabadilike kwa kuingia katika mfumo rasmi ambao utawawezesha kukubalika na taasisi za fedha kutokana na kukua kwa sekta ya Madini Duniani ikiendana na Mabadiliko ya Uchumi hapa Nchini.

Wito huo Umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Iindi,Bi Agness Hokororo wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili ya wachimbaji wadogo wa madini wilayani hapa ambapo alibainisha kuwa uchimbaji mdogo ni sekta ya kibiashara ambayo inaweza kuongeza kipato cha wananchi kwa kuongeza ajira pamoja na uchangia na ukuaji wa pato la taifa.

Licha ya kutokuwepo kwa taarifa sahihi za uzalishaji na uuzaji wa madini na wachimbaji wadogo kutozifanya shughuli za uchimbaji madini kama shughuli maalum ambazo zinaweza kuajiri na kuajiriwa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamewezeshwa na Wizara ya Nishati na Madini na kuratibiwa na ofisi ya Kamishna wa Madini kanda ya kusini na kuhusisisha Wachimbaji wadogo,Madiwani,Watendaji wa vijiji/kata ambapo mada mbali mbali zitatolewa zikiwamao za Sheria ya madini ya mwaka 2010,Ufafanuzi wa sera ya madini,Fursa za madini zilizopo Ruangwa na Matumizi salama ya Baruti ambapo pia watapewa Mwongozo wa kuandaa mpango wa kutunza Mazingira(EPP0).
Baadhi ya Wadau waliohudhulia Mkutano huo wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa (hayupo pichani)
Sekretarieti ikiendelea na kazi yake ya kukusanya maoni ya wadau hao.
Picha ya Pamoja.

WORLD BANK BOARD APPROVES ADDITIONAL FINANCING FOR TANZANIA'S BUS RAPID TRANSIT PROJECT

$
0
0
WASHINGTON, January 15, 2012 – The World Bank Board of Executive Directors has today approved US$100 million as additional financing for completion of the Bus Rapid Transit (BRT) system in Dar es Salaam. The initiative will save the economy billions of shillings lost daily in the jams and provide relief to at least 300,000 commuters.

The additional $100 million from the Bank’s International Development Association will bring the total cost of the Second Central Transport Corridor Project (CTCP2 to $290 million).

“Dar es Salaam is growing rapidly”, said Philippe Dongier, World Bank’s Country Director for Tanzania, Uganda and Burundi. “Traffic jams are a significant problem for the economy. They reduce productivity by wasting the time of road users; they threaten future growth prospects for the city and the country, and they pollute the environment.”

The BRT is implemented by the Dar es Salaam Rapid Transport (DART) agency and is aligned to Tanzania’s development strategy which underscores the need for improved transport infrastructure to achieve social and economic objectives. The combined works on the project including the construction of the road works, bus-passenger terminal buildings, feeder stations, utility power relocation will provide some 80,000 jobs by completion in 2015.

The BRT system will be operated by a US$40.9 million public private partnership (PPP) arrangement with two private bus operators, one fare collector and a fund manager. The modern system will provide rapid boarding and dedicated right of way for 148 buses with a capacity of 140 passengers each, providing both normal and express services.

Additionally, another 100 buses with a capacity of 60 passengers will transport passengers to the trunk system through feeder stations. The entire 20.9 kilometers will be provided with tree-shaded bicycle and pedestrian ways on both sides of the road with an average distance of 500 meters between bus stops.

“We are happy with the momentum of implementation of the BRT infrastructure as all works contracts have been awarded and the construction is proceeding,” said Yonas Mchomvu, the World Bank’s Transport Specialist in Tanzania.

DART in collaboration with the Surface and Marine Transport Authority (SUMATRA) and the Daladala Owners Association (DARCOBOA) are currently mobilizing local transport operators to form companies that are expected to participate in the bidding for the BRT bus operation through joint venture agreements and/or operation contracts with experienced international operators.

Further, preferential access to shares in the BRT bus operation will be given to the 1,800 daladalas (commuter mini-buses) that are expected to be displaced by the BRT operation.

Rais Kikwete ampokea Mwenyekiti wa AU Rais Dkt.Boni Yayi wa Benin

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin, Mheshimiwa Dkt. Boni Yayi amewasili nchini usiku wa jana, Jumanne, Januari 15, 2013, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam, Rais Boni Yayi amepokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mara ndege yake ilipotua kiasi cha saa tano unusu usiku.

Kesho asubuhi, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi kabla ya Rais Boni Yayi kuondoka nchini kuendelea na ziara yake Barani Afrika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha mgeni wake Mheshimiwa Dkt.Boni Yayi wakati alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere usiku wa jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Dkt.Boni Yayi wakifurahia jambo katika hoteli ya Kilimanjaro.(picha na Freddy Maro).
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images