Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1897 | 1898 | (Page 1899) | 1900 | 1901 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

  Watahiniwa 917,030  kutoka shule za msingi 16,581, za Tanzania Bara wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE 2017)  Septemba 6 hadi 7 , mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George Simbachawene amesema kuwa maandalizi ya uendesheji na usimamizi wa mtihani huo yamekamilika katika ngazi zote ikiwemo kusafirishwa kwa mitihani na wasimamizi kutoka ngazi ya Halmashauri kwenda kwenye vituo vya kufanyia mtihani.

  “Jumla ya shilingi , 29,474,964,600 zitatumika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na usimamizi wa mtihani huo kwenye mikoa na Halmashauri” ameongeza George Simbachawene.

  Aidha, Waziri Simbachawene amewataka viongozi wa Serikali kushirikiana kwa hali na mali na kuhakikisha zoezi hilo muhimu na nyeti  linafanyika kwa utulivu na ufanisi kwa kuwataka wanajamii wote, wazazi na walezi wawaruhusu wanafunzi kuhudhuria na kufanya mtihani huo kwa amani.

  “Ndugu walimu, jiepusheni na udanganyifu au kusaidia kutekeleza udanganyifu. Natoa wito kwenu mkasimamie vema vijana wetu ili waweze kufanya mtihani wao kwa usalama haki na usawa ili tuweze kuwapata vijana watakaojingana kidato cha kwanza wenye sifa zinazostahili na si vinginevyo” amesisitiza Simbachawene.

  Waziri Simbachawene amewaagiza viongozi wanaohusika na mtihani huo kuanzia ngazi za mikoa na Halmashauri wahakikishe wanakamilisha kwa wakati upelekaji wa mitihani na vifaa kulingana na mahitaji kwa wakati.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama  ametoa mwezi mmoja kwa wavamizi wa eneo la hifadhi ya msitu wa Dutumi kuondoka mara moja ifikapo Oktoba 4 mwaka huu.

  DC Assumpter amesema hayo baada ya kwenda kuutembelea msitu huo eneo la Tengefu la hifadhi lililopo katika Mkoa wa Pwani baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu ambao wamevamia na wameweka makazi katika eneo hilo isivyo rasmi.

  Akizungumza na waandishi wa habari  katika eneo hilo DC Assumpter  amesema kuwa ndani ya msitu huo kuna watu kutoka katika mikoa mbalimbali jumla ya wananchi 3,000 ambao wanaishi ndani ya msitu huo huku wakifanya uharibifu wa kukata miti hovyo na kuichoma kwa lengo la kufanya biashara ya kuchoma mkaa bila ya kuwa na vibali halali kutoka serikalini.
   Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza na wakazi waliovamia eneo la hifadhi ya msitu wa Dutumi mara baada ya kukagua msitu huo na kukuta uharibifu mkubwa ndani ya Msitu huo.
   Mkuu wa Wilaya Assumpter akimshika mtoto mmoja wapo anayeishi  na wazazi wake kwenye kambi ya watu wanaokata misitu na kuchoma mkaa , hapo alikuwa akiwauliza wazazi hao kuwa hawawatendei haki watoto wao kwani ndani ya kambi hizo hakuna mahitaji muhimu kama hispitali, shule, maji safi  pamoja na malazi yenye hadhi ya kuishi binaadamu
  Sehemu ya msitu wa Dutumi ambao umefyekwa miti yote mikubwa na wananchi waliovamia msitu huo


  0 0

   Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili kulia) wakiweka saini katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.
   Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (wa pili kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda (wa pili kulia) mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Michael John na kulia ni Kaimu Meneja wa Sheria toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Martha Charles.
   Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) wakiweka saini katika mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 
  Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) mkataba wa utendaji kazi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma na Taasisi za Serikali pamoja Watendaji Wakuu wa taasisi hizo wakimsikiliza Msajili wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuweka saini mikataba ya utendaji kazi kwa taasisi na Mashirika ya Umma mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0
  WINGA wa Klabu ya Azam FC Joseph Kimwaga akiwa katika chumba cha matibabu katika Hospitali ya Vincent Palloti iliyopo jijini Cape Town nchini Afrika Kusini.

  WINGA wa Klabu ya Azam FC Joseph Kimwaga, anatarajia kukaa nje ya dimba kwa muda miezi minne baada ya kubainika ya kuwa amechanika mtulinga wa kati ‘meniscus’ kwenye goti lake la mguu wa kushoto.

  Kimwaga hivi sasa yupo nchini Afrika Kusini tokea Ijumaa iliyopita akifanyiwa matibabu ya goti lake hilo, aliloumia wakati Azam FC ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Ndanda ulioisha kwa matajiri hao kushinda bao 1-0 wiki mbili zilizopita.

  Kwa mujibu wa Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwankemwa, aliyeambatana na Kimwaga nchini humo, amesema kuwa mchezaji huyo alifanyiwa vipimo jana Jumatatu na Dr. Nickolas kwenye Hospitali ya Vincent Palloti iliyopo jijini Cape Town nchini humo.

  “Jumatatu (4/9/2017)alifanyiwa vipimo na kuthibitika amechanika Meniscus upande wa kati pia  

  ameumia mtulinga wa kati ACL(Anterior Cruciate Ligament),” alisema kwenye ripoti aliyoipokea kutoka kwa Dr. Nickolas.

  Mwankemwa alisema baada ya kufanyiwa kipimo hicho, Kimwaga anatarajiwa kulazwa kesho Jumatano saa 9.00 Alasiri, huku akitarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo (athroscopy) siku inayofuata Alhamisi kabla ya kutoka hospitalini Septemba 9 mwaka huu na kurejea nchini siku nne baadaye (Septemba 13) .


   Amesema Upasuaji wa kwa njia ya Athroscopy ni ule wa kisasa kabisa ambao wataalamu hutumia vifaa maalum, ambavyo huingizwa kwenye goti ambavyo hufanya matibabu na kuondoa matatizo yote katika eneo hilo, faida yake humfanya mchezaji kurejea mapema uwanjani kuliko ule wa kupasuliwa goti zima.

  Winga huyo mara baada ya kufanyiwa upasuaji Alhamisi anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi minne kutoka siku ya upasuaji.

  Azam FC inamtakia kila kheri Kimwaga katika matibabu yake hayo, yaweze kwenda salama kama yalivyopanga na hatimaye aweze kurejea dimbani mapema.

  0 0

  Jeneza lenye Mwili wa marehemu, Muhingo Rweyemamu aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilayaka katika Serikali ya awamu ya nne na Mwandishi wa habari mkongwe nchini, ukiwa kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuagwa, mchana wa leo kabda ya mazishi yake yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza kabla ya kuongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa marehemu, Muhingo Rweyemamu mcahan wa leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Marehemu Muhingo Rweyemamu amezikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa neno wakati wa  kumuaga Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu yaliyofanyika leo Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Mtoto wa marehemu akisoma risala.
  Mwili wa marehemu mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu ukiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelewa Ofisini kwake na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zuber na kufanya Mazungumzo.

  Katika Mazungumzo hayo Mufti amemtia Moyo Makonda na kumsihi asikate tamaa sababu kazi anayoifanya ni Njema na inagusa watu wa makundi  yote hususani Wanyonge.

  Aidha Mufti amemuunga mkono RC Makonda kwa kumletea mdau atakaejenga Ofisi za Walimu kwenye Shule tatu.

  "Nimeona nisikae kimya ndio maana nimeona niunge mkono Kampeni yako ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu kwa kutafuta mdau ambae atajenga Ofisi kwenye Shule Tatu ili Walimu wafanye kazi kwenye mazingira mazuri" Alisema Mufti.

  Makonda amemshukuru Mufti kwa kumtembelea na kusema kuwa ataendelea na jitiada zake za kufanya kazi kwa bidii ilikutatua changamoto za Wakazi wa Dar es salaam.

  Aidha Makonda amewaomba Viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa kujitoa kwa pamoja ili kuijenga Dar es Salaam

  0 0  José Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akiongea na wenyeji wake baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Kushoto ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero. (Imreandaliwa na Robert Okanda Blogspot)

  José Graziano da Silva Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akitambulishwa kwa Katibu wa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Joseph Rubiro baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Anayetoa utambulisho ni ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero.

  José Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akiongea na wenyeji wake baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Kushoto ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero.

  José Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akisalimiana na Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa UNDP, Alvero Rodriguez, baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Katikati ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero.

  José Graziano da Silva mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akielekea kupanda gari tayari kuanza kwa msafara wake baada ya baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziaraya kikazi. Pamoja nao ni Mratibu mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa UNDP, Alvero Rodriguez (wa pili kushoto) Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jestus Nyamanga na Mwambata wa FAO kutoka Roma Italia, Meshack Malo (kulia).

  José Graziano da Silva Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula Dunia (FAO) akitambulishwa Msaidizi wa Mwakilishi wa FAO Tanzania (Utawala) na Msaidizi Mwenza (Programu) Charles Tulahi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo kwa ziara ya kikazi. Anayetoa utambulisho ni ni Mwenyeji wake Mwakilishi mkazi wa FAO, Fred Kafeero.

  0 0

  Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Ilala ambaye pia Diwani wa Kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto ameeleza sababu zilizopelekea Zahanati ya Vingunguti kufuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali kupitia wakaguzi wake (TRN) na imekuwa miongoni mwa Zahanati tano zilizofuzu.

  Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati Ibrahim Aeshi Nduze, Naibu Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa hali ya mara ya kwanza katika zahanati hiyo haikuwa shwari lakini kwa jitihada zake na kushirikiana na Halmashauri na Serikali alifanikiwa kufanya mambo mbalimbali katika maboresho ya zahanati hiyo na hatimae imefanikiwa kupewa hadhi ya nyota nne.

  Akiyataja mambo waliyoyafanya katika Zahanati hiyo ni pamoja na Ununuzi wa Gari ya Wagonjwa (Ambulance), Mashine ya Kufulia,Jenereta, Choo kwa kinamama wanaojifungua, utanuzi wa maabara, ufungaji wa feni nne, mashne tatu za kupmia uzito kwa watoto,kipimo cha presha na kiti cha kubebea wagonjwa.

  Zahanati nyingine zilizoweza kupandishwa hadhi Halmashauri ya Ilala ni pamoja na Zahanati ya Tabata, Mhongo la Ndege, Kinyerezi na Kadlugambwa.

  Taarifa kutoka Kamati ya Zahanati imeeleza kuwa mwanzo zahanati yetu ilikua na nyota mbili ambapo hizo zahanati nyingine zilikua na nyota tatu hivyo vingunguti imepanda nyota mbili. Kamati hiyo imewashukuru wananchi kwa mawazo, maoni, na changamoto walizozitoa ambazo zimezifanyiwa kazi na ku pelekea zahanati hiyo kupata nyota mbili za ziada, kamati memshukuru pia Diwani Omary Said Kumbilamoto kwa kuwaongoza, kuwashauri, na kutoa mchango wa hali na mali ii kufikia malengo.

  0 0

  Mkoa wa Ruvuma umefikia lengo ya ununuzi wa mahindi waliyopanga kununua katika msimu huu wa mavuno kwa vituo vyote ambayo viliteuliwa rasmi na hifadhi ya chakula ya mkoa.

  0 0


  0 0


  Na Mathias Canal, Dar es salaam
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, leo Jumanne Septemba 5, 2017 amefanya mazungumzo na waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi nchini Tanzania. 
  Katika ziara hiyo Bw. Graziano da Silva atafanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Serikali, wadau na anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein sambamba na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.
  Ziara hii ya Mkurugenzi Mkuu inajili wakati FAO ikiadhimisha miaka 40 toka kuanza shughuli zake hapa Tanzania Hafla ambayo itahudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu Hassan. 
  Katika mazungumzo na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mkurugenzi Mkuu wa FAO anabadilishana mawazo na Serikali ya Muungano wa Tanzania kwenye masuala makuu yanayohusiana na uhakika wa chakula na maendeleo ya kilimo, ikijumuisha juhudi za FAO kitaifa na kikanda.
  Pia yamejadiliwa mambo mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na FAO, pia masuala ya umuhimu kati ya pande hizo mbili.Mbali ya Maafisa wa Serikali, Mkurugenzi Mkuu atakutana na wadau wengine wa FAO hapa nchini wakiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za elimu, na taasisi za utafiti. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva (Kulia), akimpongeza Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba mara baada ya kuelezea taarifa mbalimbali zihusuzo wizara hiyo. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
  Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, kuzungumzia ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva, akizungumzia na wataalamu mbalimbali katika Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi juu ya ujio wake nchini na ushirikiano baina ya FAO na serikali ya Tanzania. Kulia kwake ni Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
  Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akipokea simu 50 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silvakwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.
  Waziri wa kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tzeba akionyesha moja ya siku kati ya 15 alizokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), José Graziano da Silva kwa ajili ya wataalamu wa kilimo kuzitumia kukusanya taarifa mbalimbali na kuziwasilisha kwa jamii. leo Jumanne Septemba 5, 2017.


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Timu ya JKT mlale inayoshiriki ligi daraja la kwanza kutoka mkoa wa ruvuma watamba kufanya vizuri kwenye kundi lake latika msimu huu wa ligi. hii inatokana baada ya kumfunga majimaji bao moja kwa bila katika mchezo wa kirafiki uwanja wa majimaji mjini SONGEA.

  0 0


  0 0

   The late Advocate Neema Lwise Kileo
   03.12.1984 - 02.09.2017

  Funeral her at Kigamboni Kisota (near Doctor Dau's residence) in Dar es salaam.
  Burial - Friday 08.09.2017
  Last respects at KKKT Usharika wa Mji mwema Church at 1pm
  Burial at Kisota (Kigamboni) cemetery in Dar es salaam  0 0
  0 0

  Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde akizungumza wakati wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco, Dar es Salaam jana.
  Baadhi ya washiriki wa semina kwa vijana kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliokuwa yanatolewa kwa ajili ya kuwahamamisha jana jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Magilatech Company Ltd. Godfrey Magila na mtaalamu wa tenklojia akitoa mafunzo kwa vijana waliodhuria semina kuhusu umuhimu wa kusoma kwa kutumia mtandao kupitia aplikesheni ya VISOMO inayotumiwa na VETA kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco, Dar es Salaam jana.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikia na VETA leo wametoa mafunzo kwa vijana mkoani Dar itakayowawezesha kuongeza ujuzi na kuenda sambamba namahitaji ya soka la ajira na kujiajiri. Mafunzo hayo yenye lengo la kutoa fursa mbalimbali zinazopatikana kupitia ushirika wa watoa huduma hao yanalenga katika kuwawezesha vijana nchnini  kujiendeleza kielimu kupitia application ya VSOMO kwa kupata masomo ya ufundi stadi ya VETA kupitia simu zao za mkononi ili kuongeza ujuzi wao.

  Akiongea wakati wa semina hiyo , Meneja Mradi wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema Tumeonelea vyema kufanya semina hii ili kuongeza uelewa kwa vijana  juu ya fursa hii muhimuinayotoa nafasi ya kijana kujitambua na kujiajiri mwenyewe mara baada ya kusoma masomo ya Ufundi kupitia simu zao za mkononi na kupata cheti.  Tunao vijana Zaidi ya wateja 30,000 ambao wamepakua application ya VSOMO kati yao 9,000 wamejiandikisha ili kusoma kwa mtandao lakini idadi ya waliopata vyeti bado ni chache, hivyo tumeonelea ni vyema kujikita katika kutoa elimu na kuwahamashisha watanzania kutumia technologia hizi za kisasa kujisomea wakati wowote mahali popote kupitia simu zao za smartphone na hatimae kufanya mafunzo ya vitendo na kupata cheti.

  Tunatoa wito kwa watanzania hususani vijana kuchangamkia fursa hii kwa kupakua application ya VSOMO kwenye simu zao na kusoma kozi hizi za ufundi ambazo gharama yake ni 120,000/= hadi kumaliza na kupata cheti.

  Kwa upande wake mtaaalamu wa technologia na Mkurugenzi wa Magilatech Company Ltd. Bw, Godfrey Magila alisema, Techonologia inakuwa kwa kasi sana ni muhimu kutumia Tehama katika kuleta tija katika kibiashara, kilimo , elimu na kadhalika. Kwa kuona hivyo tumeanzisha hii application ya VSOMO ambayo ni ya kwanza dunia kutoa mafunzo ya ufundi kupitia simu na Tanzania tunajivyunia kupiga hiyo muhimu.

  Naye Meneja Mradi wa VSOMO VETA , Bwana Charles Mapuli alisema, Ushirikiano wetu na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kunaongeza wito katika kutoa elimu ya ufundi na kuwafikia watanzania wengi Zaidi. Napenda kuwahakikishia kuwa masomo haya ya VETA kupitia simu yamehakikiwa na VETA kuhakikisha yanatolewa katika ubora na viwango vinavyotakiwa, na hivyo natoa wito kwa watanzania kutumia fursa hii kujiendeleza.  Lengo letu ni kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa ya kujiendeleza na kuwa na ueledi utakaomuwezesha kuajiriwa au kujiajiri. 

  Kozi zinazopatikana katika application ya VSOMO ni pamoja ni  Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta,umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani, Umeme wa magari. Vilevile Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium,  Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

  0 0

  Mwenyekiti  wa Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita) Nidrosy Mlawa akizungumza na waandishi habari juu ya changmoto ya viziwi katika upatikanaji wa taarifa pamoja na mawasiliano katika jamii kwa kusaiadiwa na Mkalimani Octavian Simba hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam. katika kufanya utendaji  katika maeneo wa ser

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  CHAMA Cha Viziwi Tanzania (Chavita) kimesema kuwa viziwi wanakabiliwa na changamoto kwenye shughuli za maendeleo ya jamii katika nyanja za siasa na kiuchumi kutokana na ulemavu huo kwa kuwa kikwanzo katika mawasiliano na upatikanaji wa habari katika jamii hiyo .

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho, Nidrosy Mlawa amesema kutokana na changamoto zinazowakabili watu wasiosikia wanatarajia kuendesha mradi katika mikoa mitatu  katika kutoa mafunzo kwa watendaji wa serikali za mitaa juu kutambua haki za watu wasiosikia.

  Mradi huo utaendeshwa kwa kipindi cha miezi sita katika Mikoa ya  Morogoro, Mwanza pamoja na Arusha ambapo watakutana na watendaji wa serikali za mitaa katika mikoa hiyo na kupata taarifa mbalimbali zinahusiana viziwi juu ya changamoto ya mawasiliano  pamoja na utumiaji wa lugha za alama katika shule ambazo zina watoto viziwi.

  Mlawa amesema mradi huo utagharimu sh. Milioni 80 ambazo wamepata ufadhili  na The  Foundation For Civil Society  katika kugusa changamoto za viziwi ikiwemo kwa watendaji wa serikali za mitaa kutambua na kufanya ufatiliaji wa matumizi ya mafungu ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya watu wenye Ulemavu katika Halmashauri zao.

  Aidha amesema kuwa Chavita kikipata ushirikiano katika mradi huo kwa watendaji katika mikoa hiyo ili kufanya Jamii ya Tanzania kuwa jamii juu jumuishi.

  Amesema kuwa sekta ya elimu haina walimu hawajui lugha ya alama na kusababisha wanafunzi viziwi kutopata elimu bora kama sera ya elimu ya 2004 inavyoanisha.

older | 1 | .... | 1897 | 1898 | (Page 1899) | 1900 | 1901 | .... | 3278 | newer