More Channels
Showcase
Articles on this Page
(showing articles 37841 to 37860 of 65640)
- 08/31/17--23:00: _Wakili: Sethi kupot...
- 08/31/17--23:09: _KUZIONA TANZANIA VS...
- 08/31/17--23:40: _ KAMISHNA WA MADIN...
- 09/01/17--02:00: _MAGAZETI YA IJUMAA ...
- 09/01/17--00:58: _SWALA YA EID EL HAJ...
- 09/01/17--01:00: _MUDA WA KUJISAJILI ...
- 09/01/17--01:22: _LADY JAY DEE: WABON...
- 09/01/17--02:09: _FAIDA ZA KUTUMIA LI...
- 09/01/17--02:10: _Diary Of A Vocal Co...
- 09/01/17--02:15: _BREAKING NYUZZZZ......
- 09/01/17--02:18: _WATANZANIA WAMETAKI...
- 09/01/17--03:56: _WANAJESHI WA JESHI ...
- 09/01/17--10:27: _JESHI LA WANANCHI W...
- 09/01/17--10:29: _MBUNGE MAJI MAREFU ...
- 09/01/17--10:54: _MWAMY: MKULIMA WA K...
- 09/01/17--10:54: _DKT SHEIN AONGOZA B...
- 09/01/17--11:04: _SPIKA NDUGAI ANAWAT...
- 09/01/17--11:05: _Zulia Jekundu S1 Ep...
- 09/01/17--12:35: _JAPAN YAIPATIA TANZ...
- 09/02/17--10:44: _JESHI LA WANANCHI W...
(showing articles 37841 to 37860 of 65640)
Channel Description:
Most read Swahili blog on earth

Makandege alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na kueleza mahakama kuwa mshitakiwa huyo alifanyiwa upasuaji na kuwekwa puto tumboni.
Alidai kuwa katika mashauri yaliyopita, mahakama ilitoa amri mara mbili, zote zikielekeza mshitakiwa huyo apelekwe Hospitali ya Muhimbili lakini haijatekelezwa.
Aliomba mahakama izingatie ugonjwa wa mshitakiwa na iamuru apelekwe moja kwa moja Muhimbili kwani ndio hospitali ya juu ya serikali nchini ambayo inategemea kuwa na wataalamu na vifaa stahiki vya ugonjwa unaomkabili.
"Upande wa jamhuri unatambua haya lakini kwa ridhaa yao wao wamempeleka mshitakiwa Amana hospitali. Swali ambalo mahakama isaidie kujibu pamoja na jamhuri, ni je, kumpeleka mshitakiwa wa kwanza hospitali ya Amana, magereza na jamhuri wameshindwa kutii amri ya mahakama?," alihoji Makandege.
“Mahakama haikumungunya maneno katika kutoa amri yake, ambapo ilitamka kwenye amri hiyo kwamba mshitakiwa huyo apelekwe katika hosipitali ya taifa ya Muhimbili, wao kumpeleka Amana wametekeleza amri gani?” Makandege aliendelea kueleza.
Alidai amri ya mahakama haijatekelezwa hivyo upande wa mashitaka umekaidi amri hiyo."Mahakama ndio mahala amri zote zitaheshimiwa kwa pande zote mbili kwa kuwa nchi inafuata demokrasia na utawala wa sheria," alidai Makandege.
Makandege alidai kuwa kilichofanyika ni kinyume na amri ya mahakama na kinyume na sheria za magereza kifungu cha 53 (1) ambacho kinatoa fursa kwa mtu yoyote aliyeko gerezani kama anaumwa kufikishwa hospital ili apate matibabu.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Botswana utakaofanyika Jumamosi Septemba 2, mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) viingilio vitakuwa Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko.
Wakati huo huo, Kiungo Taifa Stars, Simon Msuva tayari amejiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya Difaa El Jadidah ya Morocco baada ya Shirikisho la Soka Morocco na timu yake kumfanyia mpango wa visa ya muda mrefu iliyomwezesha kusafiri.
Mchezaji ambaye imeshindikana kuja ni Orgenes Mollel wa FC Famalicao ya Ureno. Sababu ni taratibu za ruhusa za kimataifa zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za nchi ya Ureno ambako anacheza soka la kulipwa.
Nyota wengine walikwisha kuripoti ni pamoja na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya) wakati Farid Mussa wa CD Tenerif ya Hispania anatarajiwa kutua leo.
Wengine ambao wako kambini Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Pia wamo Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao – Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Young Africans).
Katika hatua nyingine, Botswana inatarajiwa kuingia usiku wa saa 3.00 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) na watafikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Botswana inayonolewa na David Bright inakuja na wachezaji 18 wakiwamo makipa Mampule masule, Noah Maposa na Antony Gouws.
Walinzi ni Letsweletse, Mosha Gaolaolwe, Simisane Mathumo, Thabang Mosigi, Lesenya Ramorake, Tapiwa Gadibolae na Bokani Leeton.
Viungo ni Alphonse Modisaotsile, Maano Ditshupo, Katlego Masole, Gift Moyo, Segolame Boy, Lemponye Tshireletso, Thero Setsile, Kabelo Seakanyeng,Jackson, Lemogang maswena.
Washambuliaji ni Tumisang Orebonye, Jarome Ramathakwane, Tebogo Sembowa, Hendric Moyo na Boipelo Oaitse.
Na Veronica Simba – Geita
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameshuhudia na kushiriki katika zoezi la kuhakiki na kufunga madini ya dhahabu katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Kamishna Mchwampaka alishiriki zoezi hilo hivi karibuni, akiwa katika ziara ya kazi mkoani Geita kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya madini.
Zoezi la uhakiki na ufungaji wa dhahabu inayosafirishwa, hufanyika katika chumba maalum kijulikanacho kama gold room kilichopo mgodini na hushirikisha maafisa mbalimbali wa Serikali kutoka Jeshi la Polisi, Wizara ya Nishati na Madini na Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na maafisa wa Mgodi.
Akizungumzia lengo la maafisa wa Serikali kutoka sekta husika kushiriki katika zoezi hilo; Kamishna Mchwampaka alieleza kuwa ni kwa Serikali kujiridhisha na thamani ya dhahabu inayosafirishwa ili kuhakikisha inapata mapato stahiki na kuepusha udanganyifu wowote unaoweza kujitokeza.
“Katika hili, tuko imara na makini. Ni lazima tuhakikishe kuwa Serikali inapata mapato stahiki kulingana na dhahabu inayosafirishwa. Ndiyo maana unaona maafisa wetu kutoka sekta zote muhimu wanashiriki kikamilifu katika zoezi hili.”
Aliwataka watanzania kuondoa hofu na kuiamini Serikali ya Awamu ya Tano inayowaongoza kuwa iko makini na imejipanga kusimamia kikamilifu maslahi ya wananchi.Kamishna wa Madini yuko katika ziara ya kazi Kanda ya Ziwa kukagua shughuli mbalimbali za sekta husika.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti), akihakiki uzito wa Mkuo wa Dhahabu, katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kabla ya kufungwa na kusafirishwa nje ya nchi. Wengine pichani ni baadhi ya maafisa wa Serikali na GGM.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (mwenye koti-kulia), akishuhudia Mkuo wa Dhahabu wenye uzito wa kilogramu 26, ukiwekwa ndani ya mfuko maalum kabla ya kufungwa kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi. Wengine pichani ni baadhi ya maafisa wa Serikali na GGM.
Afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Anuari Fadhili akiweka ‘seal’ maalum ya Serikali kwenye Kasha lenye Mkuo wa Dhahabu baada ya ukaguzi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi. Wanaoshuhudia ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na maafisa wengine wa Serikali na GGM.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislam wakiwa kwenye ibada ya swala ya Eid el Hajj iliyoswaliwa katika Uwanja wa Msikiti wa Kigogo, Jijini Dar es salaam leo. Sikukuu ya Eid el Hajj husherehekewa na waislam duniani, ambapo Waislamu huisherekea sikukuu ya hii kwa kuchinja mnyama ikiwa ni kuheshimu kitendo alichokifanya Nabii Ibrahim (vitabu vya dini vimeeleza).
Ibada ya Eid el Hajj iliyoswaliwa katika Uwanja wa Msikiti wa Kigogo, Jijini Dar es salaam ikiendelea.
Waumini wakisikiliza mawaidha.
Kama ilivyo kawaida ya siku hii, hapa ni baadhi ya waumini wakinunua mbuzi kwa ajili ya kuchinja.
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Flava, Lady Jay Dee amesema wabongo wanapenda sana kushobokea wasanii wa nje kuliko wale walionao ndani, Jay Dee ametoa kauli hiyo kupitia kipindi cha The Finest kinachorushwa na Redio 92.9 A. FM yenye maskani yake mjini Dodoma.
Lady Jay Dee alisema, Madj na Mapresenter wa Tanzania, wanapiga sana nyimbo za nje kuliko za bongo, na pia Wasanii wa Tanzania wamekuwa wanafuata upepo ulipo katika kazi zao, ukija mtindo wa Nigeria wanaimba kama nigeria, ikija ya south wanaimba kama wao, hivyo bongo flava haijui identity yake ni ipi.
Lady Jay Dee amesema hataki mazoea na watu asiowajua na ndio mana watu wengi wamekuwa wakisema kuwa anaringa ila si kweli.
Jay Dee ameongeza kuwa yeye sio muongeaji na huwa ni vigumu sana kwake kupiga mastory na mtu ambaye hajamzoea, japo salamu anatoa.
Hata hivyo kwa mara nyingine tena mwanadada huyu atafanya vitu vyake akiwa na mpenzi wake Spicy and the band Siku ya leo Eid mosi ndani ya kiota kipya cha Burudani Dodoma Capetown , akisindikizwa na mkali wa singeli Msaga Sumu na Nay wa Mitego.
Tangawizi , manjano, tui la nazi na manjano ni vyakula vyenye faida lukuki za kiafya pindi vinavyo tumika kiafya.
Moja kati ya faida kuu za kiafya zinazo tokana na kutumia vyakula hivi kwa wakati mmoja ni pamoja na kusaidia katika kurekebisha kiwango cha sukari mwilini, kuondoa sumu kwenye ini , kuondoa mafuta yasiyo faa mwilini ( lehemu /cholesterol) pamoja na kuondoa sumu mwilini kwa ujumla wake. Kufahamu jinsi na namna ya kutayarisha lishe hii, yenye faida nyingi za kiafya kwenye mwili wa mwanadamu BOFYA HAPA
0 |
|
0 |
|
MAHAKAMA Kuu nchini Kenya (Supreme Court), imebatilisha ushindi wa uRais wa Rais wa sasa Uhuru Kenyatta, dhidi ya mpinzani wake mkuu Raira Odinga, na kuamuru uchaguzi huo urudiwe ndani ya siku 60 kuanzia leo Septemba 1, 2017.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo, kufuatia maombi ya Mgombea Urais wa Muungano wa upinzani wa NASA, Raila Odinga baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, uliompa ushindi Rais Kenyatta.
Katika maombi yake, Odinga alisema, kura zake zilipunguzwa kwenye baadhi ya vituo na kuongezewa mpinzani wake, lakini kubwa zaidi ni kukiukwa kwa taratibu za uchaguzi ambapo baadhi ya fomu muhimu za matokeo ya uchaguzi kama vile fomu namba 34A,B na C, hazikupatikana siku ya kutangazwa kwa matokeo.
Katika uamuzi wa mahakama hiyo, majaji wanne kati ya sita (6), wamekubaliana kuwa tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya, (IEBC), imeshindwa kusimamia vema uchaguzi huo na hivyo kusababisha kasoro kadhaa ambazo zinakwenda kinyume na katiba ya Kenya. Hata hivyo, Mahakama hiyo imesema, hakuna ushahidi wowote, ulioonyesha kuwa Rais Uhuru Kenyatta, alitenda makosa katika mchakato huo wa uchaguzi.
0 |
|
0 |
|
Katika kuadhimisha miaka 53ya kuazishwa kwa JWTZ kikosi cha 401 kutoka mkoa wa Ruvuma Brigade ya kusini wameazimisha siku hiyo kwa kuchangia damu katika hospitali ya rufaa ya mkoa
0 |
|
0 |
|
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo, Luteni Kanali Mkundi alisema kuwa wamefika hospitalini hapo ambako wamefanya usafi katika wodi mbalimbali na kugawa zawadi ikiwa ni kusherehekea maadhimisho hayo yaliyoadhimishwa nchini kote huku wanajeshi wakiungana katika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha Bwana. Robert Shilingi akipokea msaada kutoka kwa Luteni Kanali Gelda Lucas Mkundi na Kulia ni Meja Salma Shaaban Kalili wote kutoka Kambi ya Nyerere Msangani Kibaha Mkoani Pwani.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Hospitali ya Tumbi Kibaha ikiwa ni katika maadhimisho ya miaka 53 ya kuanzishwa kwa Jeshi la Wananchi nchini , sherehe hizo hufanyika kila ifikapo Septemba Mosi ya kila mwaka.
Meja Enock Wiliam Liwembe kutoka kikosi cha Kiluvya akitoa damu katika hospitali ya Tumbi ikiwa ni katika sehemu ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 53 ya JWTZ.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akizungumzia maadhimisho ya miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Jenerali wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wa kwanza kushoto pamoja na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kuzungumza kuhusu kuhusu miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Jenerali wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya wanne kutoka kushoto Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange wanne kutoka kulia Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Mwakibolwa watatu kutoka kushoto mstari wa mbele pamoja na Wakuu wa Kamandi na machifu wa Makao makuu ya Jeshi hilo.
PICHA NA MPIGA PICHA WETU
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akishiriki kufyetua matofali 10000 ambayo baadae yatagawiwa kwa kata 29 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na zahanati ikiwemo nyumba za wafanyakazi wa serikali baada ya kupata saruji mifuko 200 kutoka kwa Mohamed MO na Hoza Farm naye amempa mifuko mingine 100.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiendelea na kazi |
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu mwenye shati za njano akishiriki kufyatua matofali na viongozi wa CCM Korogwe Vijijini
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stepheni Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akiwa amebeba tofali mara baada ya kulifyetuaa(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Kwa hisani ya DW
0 |
|
0 |
|

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akisalimiana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali baada ya kutoa hutuba yake katika sherehe za Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akipungia mkono Viongozi mbali mbali kama ishara ya kuwaaga baada ya kumalizika kwa sherehe za Baraza la Eid El Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,[Picha na Ikulu.] 01/09/2017.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman alipowasili katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo.


Baadhi ya Akinamama waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo,katika ukumbi wa mkutano wa Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

Wananchi na Viongozi wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (kushoto) akiwa na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa katika sherehe za Baraza la Eid el Hajj lililofanyika leo katika viwanja vya Nyumba za Mji Mpya wa Kisasa Fumba Wilaya ya Magharibi “B” Mkoa wa Mjini Magharibi,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
0 |
|
0 |
|
Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), imeipatia Tanzania ruzuku ya Yen milioni 69 sawa na Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa awamu ya pili ya mradi wa upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Septemba 1, 2017, Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) kwa niaba ya Serikali, Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Satoru Matsuyama.
Tukio hilo limekwenda sambamba na kuingia makubaliano kuhusu muda wa kukamilisha mradi huo pamoja na kupeana taarifa ya namna mradi huo utakavyotekelezwa.
Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).
Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Dkt. Mpango amesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya msongamano wa magari kutoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (wa pili kushoto), wakisaini makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge, yenye urefu wa kilometa 4.3, ambapo Japan imetoa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa barabara hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida akibadilishana hati za makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Morocco hadi Mwenge, yenye urefu wa kilometa 4.3, ambapo Japan imetoa msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina wa barabara hiyo, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kulia) na Mwakilishi Mkuu mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama (wa pili kushoto) wakisaini Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kufanya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama wakibadilishana hati ya Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara ya Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini humo.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) na Mwakilishi Mkuu mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Bw. Satoru Matsuyama wakipeana mkono baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa makubaliano ya msaada wa Shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya Usanifu wa kina wa upanuzi wa Barabara kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.
0 |
|
0 |
|
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akizungumzia maadhimisho ya miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akizungumzia maadhimisho ya miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha na Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa kwanza Mzalendo kuliongoza Jeshi hilo Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya (kushoto} pamoja na Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kulia) mara baada ya kuzungumza kuhusu kuhusu miaka 53 tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo la Wananchi katika Makao makuu ya Jeshi hilo Ngome jijini Dar es Salaam.