Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MKONO WA EID al ADHA TOKA WIZARA YA AFYA


BENDI ZAANZA KUPASHA KUELEKEA TAMASHA LA MUZIKI LA DIMBA JUMAMOSI HII TRAVELTINE HOTEL MAGOMENI DAR ES SALAAM

MAENDELEO BANK YAWAZAWADIA WATEJA WAKE VIWANJA ,MABATI NA SARUJI

$
0
0
Maendeleo Bank leo imechezesha droo yake ya kwanza iliyotokana na kampeni ya Maendeleo Pamoja na Wewe iliyozinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwezi Agosti 2017.
Promosheni hiyo ina malengo kadhaa;Kuwaweka wateja wake karibu kwa kutumia huduma mbalimbali za Maendeleo Bank Kuwajengea watanzania utaratibu wa kuweka akiba kwa njia ya kibenkiKukuza utamaduni wa kujiwekea malengo ya muda mfupi na mrefu kwa kuweka fedha kidogo kidogo katika akaunti ya WEKEZA ili kufanikisha malengo yao.
Kuwajengea wazazi utamaduni wa kuwawekea watoto wao akiba
Mkuu wa Idara ya Fedha wa benki hiyo Bw. Peter Tarimo alisema “Draw yetu ya Maendeleo Pamoja na Wewe awamu ya kwanza inahitimishwa leo kwa kuchezesha draw ambayo itatupatia washindi mbalimbali ikiwemo tani za simenti, kiwanja, mabati na ada ya shule”.
Draw hiyo imeibua washindi wane (4) ambao walishinda kiwanja, mabati 64 ,tani 3 za simenti pamoja na ada ya shule na kushudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Bw. Bakari Maggid.
Promosheni ya Maendeleo Pamoja na Wewe inasitishwa kwa sasa kupisha zoezi za uuzaji wa hisa za Maendeleo Bank na itaendeleo mara baada ya kuhitimisha uuzaji wa hisa za benki hiyo.
Mkuu wa Tehama na Uendeshaji Bw. George Wandwalo akibonyeza kitufe kuashiria kuanza kwa droo iliyomuibua mshindi wa kiwanja Bi. Dora Olotu katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Bakari Maggid
Mkuu wa Tehama na Uendeshaji Bw. George Wandwalo akizungumza na mteja wa Maendeleo Bank kwa njia ya simu baada ya kuibuka kama mmoja wa washindi waliopatikana katika droo iliyoashiria kumalizika kwa awamu ya kwanza ya promosheni ya Maendeleo Pamoja na Wewe.C:\Users\EAG Group\Desktop\PRESS MAENDELEO BANK AUG 31 2017\1T4A9121.JPG
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Bw. Peter Tarimo akizungumza na waandishi wa habari juu ya shindano na promosheni ya Maendeleo Pamoja na Wewe kabla ya kuanza kwa droo hiyo Dar es Salaam leo.

POLEPOLE: TUPO TAYARI KWA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA LONGIDO

$
0
0

Chama cha Mapinduzi kimesema kuwa kipo tayari kuingia katika uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Longido Mkoani Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa jimbo hilo lipo wazi kutokana na maamuzi ya mahakama ya Rufaa iliyobainisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 haukuwa huru na haki hivyo kufuta matokeo ya uchaguzi huo.

CCM imeeleza kuwa kulikuwa na matumizi yasiyostahili kutumika kujazwa matokeo ya Ubunge, kwa kutumia fomu namba 21c za kujaza matokeo ya Udiwani na kujaza matokeo ya Ubunge, badala ya kutumia fomu namba 21b jambo lililopelekea kufungua kesi ya kupinga ushindi wa Ubunge katika Jimbo hilo.

Kauli ya CCM imetolewa na Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Polepole alisema kuwa vipo vyama vya siasa ambavyo kwa kawaida hulalamika kila vinaposikia kushindwa na mahakama kwa madai kuwa hakuna haki lakini vyama hivyo kila vinaposhinda vyenyewe husema mahakama imetenda haki.

Alisema kuwa kazi ya mahakama ni kutumia sheria zilizopo na kuamua juu ya malalamiko ya wananchi kwa kuhakikisha usawa mbele ya sheria kwa watu wote unatendeka hivyo maamuzi yaliyotolewa juu ya kuwa wazi kwa Jimbo la longido ni sehemu ya maamuzi huru na haki kwa mahakama ya Rufaa nchini.
Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.


Aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Steven Kiruswa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Katibu Wa Halmashauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KAMANDA KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM MAMBOSASA AJITAMBULISHA, AOMBA USHIRIKIANO NA KUAHIDI KUPAMBANA NA UHALIFU JIJINI

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMIS 31.08.2017

KAMATI ZA BUNGE ZA HESABU ZA SERIKALI, NISHATI NA MADINI NA MIUNDOMBINU ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA.

$
0
0
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jaffo (aliesimama)akizungumza jambo pale Watendaji wakuu kutoka ofisi hiyo walipokutana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali leo Mjini Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Ndg. Kapulya Musomba akizungumza jambo pale kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipokutana na Watendaji wakuu kutoka Shirika hilo, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na REA leo Mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia majadiliano baina yao na Watendaji wakuu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wizara ya Nishati na Madini pamoja na REA leo Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (aliesimama) akizungumza na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Watendaji wakuu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wizara ya Nishati na Madini pamoja na REA (hawapo kwenye picha) leo Mjini Dodoma. katikati ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Deo Ngalawa na kulia ni Katibu kamati wa kamati hiyo, Ndg. Felista Mgonja
 Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakifuatilia Majadiliano baina yao na Watendaji Wakuu kutoka TCRA, Vodacom, Airtel na Tigo katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UJUMBE WA CPC ULIPOKUTANA NA MANGULA DAR NA ULIPOTEMBELEA ENEO LA UJENZI WA CHUO KIKUU CHA SIASA CHA MWALIMU NYERERE, KIBAHA

$
0
0
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akiongoza mazungumzo  baina yake na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017.
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akiongoza mazungumzo  baina yake na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017
 Ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo hayo
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akimkabidhi zawadi maalum Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula (kulia) akizawadiwa na Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017.


NYOTA YA TANZANIA YAENDELEA KUNG'AA MICHEZO YA WAKUU WA MAJESHI WA AFRIKA MASHARIKI NCHINI BURUNDI

$
0
0
Nyota ya timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imeendelea kung’ara katika Mashindano ya muhula wa nne wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi wa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi. 
Leo tena timu za Basketball na Volleyball zimeendeleza dozi kama kawa. Timu ya Basketball imeifunga Uganda kwa vikapu 63-56, wakati katika Volleyball Tanzania imeshinda kwa seti 3-0.
“Tunashukuru Mungu kwamba nyota ya Tanzania imeendelea kung'ara kwenye michezo hii na vijana wana ari ya kuendeleza ushindi kwenye michezo yote ijayo", mkuu wa msafara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga amesema. 
Brigedia Jenerali Kemwaga, ambaye yeye mwenyewe ni mchezaji nguli wa zamani wa mpira wa kikapu, ameeleza kufurahishwa na vijana wake ambao wamekuwa tishio katika michezo yote wanayoshiriki. 
Kaulimbiu ya Mashindano hayo ni “Shiriki michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda Afya zetu na Kudumisha Mshikamano”, na yanahusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na wenyeji Burundi. 
Timu ya JWTZ daima imekua ikifanya vizuri kwa kuchukua nafasi ya ya tatu kwa ujumla kati ya nchi zote zilizoshiriki katika mashindano yaliyofanyika hapo awali. Na safari hii timu hiyo kabambe imepania kunyakua nafasi ya kwanza kwani wao kila walipo ni HAPA KAZI TU.

BANDARI KAVU YA KWALA –VIGWAZA KUANZA KUTUMIKA JANUARI MWAKANI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala Vigwaza Mkoani Pwani na kumtaka mkandarasi Suma JKT kuongeza kasi na kuzingatia ubora.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo ameiagiza Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuhakikisha wanaunganisha kwa haraka ili reli na barabara zinazoingia katika bandari kavu hiyo zinakamilika na hivyo kuiwezesha bandari kavu hiyo kuanza kutumika ifikapo Januari mwakani.

“TPA, TRL na TANROADS uzuri wote mko kwenye wizara moja shirikianeni na hakikisheni kilomita 15 za barabara inayoingia kwenye bandari kavu hii na kilomita moja ya reli zinajengwa haraka,” Amesema Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko kuhakikisha ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza unazingatia ubora na viwango vilivyopo katika mkataba ili kuiwezesha kuhudumia zaidi ya makontena milioni moja kwa mwaka na hivyo kupunguza msongamano katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

“Hakikisheni eneo la bandari kavu linakuwa na maegesho ya kutosha, taa, maji ya uhakika, gari la zimamoto, uzio na mashine ya ukaguzi wa mizigo scanner itakayowezesha kupima kila mzigo unaopandishwa na kushushwa katika eneo hili,” amesisitiza Profesa Mbarawa.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akifafanua jambo wakati akikagua mchoro wa Bandari kavu ya Kwala –Vigwaza Mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Eng. Charles Salu Ogare anayesimamia ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza Mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Eng. Deusdedit Kakoko akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa bandari kavu ya Kwala –Vigwaza Mkoani Pwani.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasilino, Profesa Makame Mbarawa mwenye kofia ya njano akiwa katika majukumu ya ukaguzi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwala-Vigwaza inayojengwa mkoani Pwani.
Muonekano wa bandari kavu inayojengwa na mkandarasi Suma-KJT katika eneo la Kwala-Vigwaza inayotarajiwa kuanza kutumika Januari mwakani ikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.


MAAFISA WA WIZARA YA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA UJERUMANI WATEMBELEA MAHAKAMA YA AFRIKA

$
0
0
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki  za Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chatbar(kulia)akiwaongoza wageni kutoka Wizara ya ushirikiano wa maendeleo ya Ujerumani kupitia taasisi zake GIZ na AGA waliotembelea mahakama hiyo wamekua ni wadau wakubwa katika kusaidia miradi mbalimbali ya mahakama hiyo.
Mkutubi wa Maktaba ya mahakama hiyo,Revina Moshi akizungumza na maafisa kutoka
shirika la maendeleo ya kimataifa ya Ujerumani(GIZ),kutoka kushoto ni Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Addis Ababa,Ethiopia,Barbara Schaefer,Janina Hasse kutoka Berlin,Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs 
Mkuu wa taasisi za GIZ na AGA,Hartmut Krebs akiangalia sehemu ya machapisho kwenye maktaba ya AfCHPR. 
Msajiliwa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno(kulia)akizungumza na ujumbe kutoka taasisi za Wizara ya maendeleo ya Ujerumani waliotembelea mahakama hiyo. 
Msajili wa mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR),Dk Robert Enno akimkabidhi zawadi  Afisa wa Wizara ya maendeleo ya Ujerumani anayehusika na Umoja wa Afrika(AU) ofisi ya Ethiopia,Barbara Schaefer. 

DKT PALLANGYO AKUTANA NA KAMPUNI YA M & P EXPLORATION PRODUCTION TANZANIA LIMITED

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji kutoka Kampuni inayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi ya M & P Exploration Production Tanzania Limited, Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akizungumza na Meneja Mkuu kutoka Kampuni inayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi ya M & P Exploration Production Tanzania Limited, Christophe Maitre ( kushoto) katika kikao hicho.
Sehemu ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho


…………………..


Leo Agosti 31, 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amekutana na Kampuni inayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi ya M & P Exploration Production Tanzania Limited kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini zilizopo jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujadili namna ya kuendeleza gesi ya Mnazi Bay. Kikao hicho pia kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)

MKEMIA MKUU WA SERIKALI: HUDUMA ZETU ZINAPATIKANA KOTE NCHINI

$
0
0
Na. Georgina Misama – MAELEZO

Serikali kupitia Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inafanya maboresho katika maabara zake za kanda zilizopo kote nchini ili kusogeza huduma hiyo kwa wananchi.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja kutoka Mamlaka hiyo Cletus Mnzava alisema kwamba Mamlaka inafanya maboresho katika Ofisi zake za kanda kwa kuboresha miundombinu na kuzipatia vifaa vya maabara vya kisasa.“Lengo kuu la kuimarisha Maabara zetu za kanda ni kusogeza huduma karibu na wananchi kote nchini ili kuwaondolea ulazima wa kuja kufuata baadhi ya huduma kwenye ofisi zetu za Dar es salaam”. Alisema Mnzava

Mnzava amesema sehemu ya maboresho hayo ni pamoja na kujenga majengo ya kudumu ya Ofisi za Mamlaka katika kanda ili kuwekeza katika mitambo ya kisasa na ya kudumu. Aidha, ujenzi wa jengo la Ofisi za Kanda za Nyanda za Juu Kusini unatarajiwa kukamilika mwaka huu wa fedha.

Akizitaja Ofisi hizo za kanda Mnzava anasema kuna kanda ya Ziwa ambayo inahudumia mikoa ya Mwanza, Bukoba, Simiyu, Mara, Shinyanga, Geita na Kigoma, na kanda ya Kaskazini kwa ajili ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara. Kwa mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Tabora na Iringa inahudumiwa na ofisi za Kanda ya Kati, wakati Kanda ya Mashariki ni kwa ajili ya Mikoa ya Dar es salaam na Pwani.

Vilevile kuna Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya Mikoa ya Mbeya, Katavi, Songwe, na Rukwa na Kanda ya Kusini kwa ajili ya kuhudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Songea.Mamlaka pia imejipanga kuanzisha Maabara yenye vifaa vya kisasa kwa kanda ambazo bado hazina maabara hizo ili kutoa huduma kwa weledi na ufanisi kulingana na mahitaji ya eneo husika.

Mzava anasema ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano, Mamlaka imeimarisha shughuli zake za ukaguzi kwa mipaka yote nchini, ambapo kwa mipaka mikubwa kama vile Namanga na Tunduma huduma hizo za ukaguzi hutolewa kwa masaa 24.

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inawaasa watanzania kujenga utamaduni wa kuzitumia Ofisi zake za Kanda kwa lengo la kufanya kazi zinazoweza kufanyika kwa haraka kwenye Kanda husika badala ya kutegemea zaidi Maabara zilizoko Ofisi za Dar es salaam.

Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemi Mkuu wa Serikali Bw.Cletus Mnzava akiwasomea Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya mikakati ya mamlaka ya hiyo kuhusu uimarishwaji wa ofisi zao hapa nchini, kulia ni Afisa Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bw. Silvester Omary katika mkutano uliofanyika katika ukumbI wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemi Mkuu wa Serikali Bw.Cletus Mnzava akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari( hawapo pichani) katika mkutano wa mamlaka hiyo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemi Mkuu wa Serikali Bw.Cletus Mnzava katika mkutano wa Mamlaka hiyo ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Paschal Dotto(31.08.2017

International Karate Seminar & Grading (Gasshuku) kuanza leo ukumbi wa Don Bosco Dar es salaam

$
0
0

Japan karate Association/World Federation - Tanzania (JKA/WF-TZ), ni shirikisho la mchezo wa karate wa asili ya Japani tawi la Tanzania, lenye usajili wa kimataifa toka makao makuu ya shirikisho hilo Tokyo Japan na pia hutambuliwa na Shirikisho la Karate la Dunia (World Karate Federation). JKA/WF-TZ ilipata usajili rasmi mwaka 2006, na ilishafanya semina na mashindano mengi ya kimataifa ndani na nje ya nchi. Hivi sasa shirikisho lina timu ya Taifa ya karate inayojindaa na mashindo ya Afrika mwakani (2018), Mashindano ya Dunia (2019), Mashindano ya Olympics (2020), na pia mashindao mengine ya ndani na nje ya nchi.
Pamoja na kuendelea na maandalizi ya Timu ya Taifa sisi (JKA/WF-TZ) tunarajia kuendesha Mafunzo ya Karate na kufanya mitihani ya Kimataifa (International Karate Seminar & Grading ama Gasshuku), yatakayofanyika katika ukumbi mkubwa wa Don-Bosco Upanga, kuanzia  tarehe 1-4 Septemba 2017. Saa 6:00 Mchana hadi saa 9:00 Alasiri.
Mafunzo na Mitihani hiyo itaongozwa na Mkufunzi (Master) Shihan Koichiro Okuma, kutoka Makao Makuu ya JKA Tokyo Japan, ambaye aliendesha mafunzo kama haya mwaka jana mwezi wa tisa, eneo lile lile la Don-Bosco Upanga. Mafunzo haya yatajumuisha nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kati, zikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zimbabwe, Zambia, DRC, Angola, Afrika Kusini, Ufaransa, nk. Hadi sasa mataifa ya Kenya, Uganda, Malawi, Zimbabwe, Angola, Afrika kusini na Japan, yameshawasili nchini  kuhudhuria mafunzo haya. Na tunatarajia kupata wageni wengi zaidi kadri muda unavyosogea.
Katika mafunzo hayo tunatakuwa na sherehe za ufunguzi siku ya kwanza (tar 1/9/2017 ) na sherehe kubwa siku ya mwisho (tar 4/9/2017) ambapo watahiniwa waliofuzu mafunzo watakabidhiwa vyeti na leseni zao siku hiyo ya mwisho, na wahudhuriaji watakabithiwa vyeti. Katika sherehe hizo, tunatarajia kuwa na Mgeni Rasmi toka BMT ambaye ni Katibu Mkuu, Bwana Mohamed kiganja. na pia tutakuwa mgeni toka Ubalozi wa Japani nchini.

Faida za ujio wa Shihan Koichiro Okuma (Toka Japan) na kuendesha mafunzo haya nchini:
Kwanza kama Taifa, tutakuwa tumeitangaza nchi yetu (Tanzania) kimataifa kutokana na wageni wanaokuja kutoka nje na kwenda kusambaza habari zetu huko kwao, pia kuangaziwa na  vyombo vya habari vya kimataifa, hasa katika suala na michezo, utalii nakibiashara.

Pili sisi kama JKA/WF-Tanzania, tutaongeza ujuzi kwa Wakufunzi/Walimu (Instructors), Waamuzi (Judges) wa  Wachezaji (Karatekas) wa huu mchezo hapa nchini. Pia Shihan Okuma ataangazia matayarisho ya timu yetu ya Taifa inayojiandaa kwa mashindano ya Afrika mwakani (2018), mashindano ya Dunia (2019) na mashindano ya Olympics (2020). Sisi JKA/WF-Tanzania tutatumia fursa hii kuvuna mbinu mbinu mabalimbali za kushinda mashindano ya kimataifa na namna kuindaa timu kisaikolojia na kimwili/kimazoezi pia, katika hali ya kiutaalam zaidi.
Wenu katika michezo,

Nestory Fedeliko (FEDE)
Katibu Mtendaji, JKA/WF-Tanzania.

BOT YAKANUSHA TAARIFA KUHUSU KUBADILISHA FEDHA

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kupuuza taarifa zinazozunguka katika mitandao ya kijamii kwamba kutakuwa na ‘mabadilisho ya fedha zote za zamani kuanzia tarehe 04/09/2017 hadi tarehe 01/12/2017’.



Taarifa hizo ni za uongo na hazijatolewa na Benki Kuu ya Tanzania. Wananchi mnaombwa kuendelea na taratibu zenu za kawaida za kufanya miamala yenu mbalimbali kwa kutumia fedha zetu kama kawaida.



Aidha, Benki Kuu ya Tanzania inawaasa watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia vizuri nyenzo hiyo ya kupashana habari na kuacha kuzusha uongo ambao unaleta usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.


Imetolewa na:

Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki

Barua pepe: info@bot.go.tz


Simu: +255 22 2233167


WANANCHI WAONDOLEWA WASIWASI KUHUSU FIDIA YA MALI ZAO ZITAKAZOPITIWA NA BOMBA LA MAFUTA

$
0
0
Wananchi Mkoani Singida wameondolewa wasiwasi kuhusu fidia ya mali au ardhi yao ambayo itapitiwa na mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga kwakuwa hawatapunjwa bali itazingatia vigezo vya kimataifa na kitaifa.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema hayo mapema leo wakati wa kikao na wataalamu wanaofanya uthamini wa mali na ardhi ambayo itapitiwa na mradi huo.

Tarimo amesema wananchi na taasisi zote wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutaja gharama kulingana na thamani halisi ya mali zao na sio kuongeza gharama za juu kwakuwa vigezo vya kitaifa na kimataifa vitazingatiwa.

“wananchi wengine wasio waaminifu wananweza wakataja pesa kubwa au hata kuvamia maeneo ambayo siyo yao ilimradi wapate tu pesa, nawasihi wasifanye hivyo kwakua watakuwa wanakwamisha mradi huu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa letu na majirani zetu Uganda”, amesema na kuongeza kuwa
Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akizungumza katika kikao na wataalamu watakaofanya uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.


Mthamini wa ardhi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Chiku Mkina (aliyevaa miwani) na wataalaamu wengine wakisikiliza kwa makini mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina M Lutambi akichangia mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mkurugenzi wa kampuni ya Dighy Welly Dkt Jan Perold akiwasilisha mada katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.


Mwakilishi wa Serikali katika zoezi la Uthamini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Linus Kinyondo akizungumza na wataalamu wa mkoa wa Singida katika kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.
Mhandisi wa Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Simwela Nuru Martin akifuatilia kwa makini kikao kilichohusu uthamini wa mali na ardhi kwa ajili ya fidia katika mradi wa bomba la mafuta la Kutoka Uganda hadi Tanga.

CAG ATOA SEMINA KWA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akiwasilisha mada kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika semina iliyohusu Ripoti za CAG kuhusu kaguzi za taarifa za fedha kwa mwaka ulioshia tarehe 30 Juni, 2016.

MBUNGE COSATO CHUMI AKABIDHI BESENI 100 KWA KINAMAMA WAJAWAZITO NA WALIOJIFUNGUA KATIKA HOSPITAL YA MJI WA MAFINGA

$
0
0
Na Fredy Mgunda-Mafinga.

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mabeseni mia moja kwa akina mama waliopata watoto kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya Mafinga.

Mabeseni hayo yalikabidhiwa kwa kina mama waliojifungua na ambao wanatarajia kujifungua hivi karibuni hospitalini hapo.Msaada huo wenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni nne, umetolewa na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini mapema wiki iliyopita.

`ndugu zangu zawadi hii tumepewa na Balozi wa Kuwait hapa Nchini kwa ajili yenu kina mama kama sehemu ya mwanzo wa ushirikiano kati ya Mafinga na Ubalozi wa Kuwait' alisema Chumi.

Akifafanua, alisema kuwa msaada huo ni uthibitisho wa upendo alionao Balozi wa Kuwait hapa nchini kwa watu wa Mafinga.`Mheshimiwa Balozi Jasem Al- Najem hajawai kufika Mafinga lakini kwa upendo mkubwa akasema, naomba hiki kidogo uwafikushie kina mama wa Mafinga' alisema Chumi na kuongeza kuwa ushirikiano kwenye jambo dogo ndio mwanzo wa ushirikiano wa mambo mengine makubwa.

Akishukuru wakati wa kukabidhi msaada huo wa mabeseni, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mhe Charles Makoga alipongeza ushirikiano wa Mbunge na wadau mbali mbali na kuwasihi watendaji kuendelea kufanya kazi kwa kujituma.`sisi halmashauri tuko bega kwa bega na mbunge, na ninyi watumishi kwa pamoja tuendelee kushirikiana na kufanya kazi kwa kujituma' alisisitiza Makoga.

Wakati akikabidhi msaada huo wiki moja iliyopita kwenye ofisi za Ubalozi wa Kuwait Masaki Jijini Dar es Salaam, Balozi Jasem Al-Najem alisema kuwa lengo la Ubalozi ni kugawa jumla ya mabeseni elfu moja kwa ajili ya mama na mtoto.`katika awamu ya kwanza ya kutoa msaada huu wa mabeseni haya ya mama mtoto kits, tumeona tuwakumbuke na kina mama wa Mafinga japo kwa mabeseni mia moja'

Ubalozi wa Kuwait umekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada ya kijamii na kibinadamu ambapo mpaka sasa wameshachimba visima arobaini kwenye shule mbali mbali za Mkoa wa Dar na Pwani.

Aidha Ubalozi umeshatoa msaada wa vifaa vya theatre katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na pia kuendesha zoezi la kuchangia damu miezi sita iliyopita.
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwapa akina mama waliojifungua mabeseni kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma ya afya kwa kinamama wa jimbo la mufindi na wananchi wote wanotumie hospitali ya mafinga mjini lakini mabeseni hayo yametolewa kwa msaada wa ubalozi wa kuwait hapa nchini Tanzania.
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na mmoja wa kinamama alifanikiwa kupewa msaada wa beseni

Migogoro mingi ya Ardhi ni kutokujituma kwa watu wetu - RC Gambo

$
0
0
"Migogoro mingi ya Ardhi ni kutokujituma kwa watu wetu" RC Gambo
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati anahitimisha mkutano wake na wananchi wa wilaya ya Karatu wenye kero mbalimbali za Ardhi,Nyumba na Makazi.

"Toka nianze mikutano mikutano hii na wakazi wa Jiji la Arusha na leo nipo hapa Karatu migogoro mingi si mikubwa kama inavyoonekana bali inachangiwa na uzembe wa watu wetu katika mabaraza ya Ardhi na mahakama kutokutimiza wajibu wao ipasavyo" alisema Gambo.

Katika mikutano hiyo maalum ambayo mkuu huyo wa mkoa ameshaifanya katika jiji la Arusha na Karatu amekutana na migogoro mingi ambayo kiuhalisia imeshasuluhishwa katika hatua mbalimbali za kimaamuzi lakini wananchi hao hawajapewa mrejesho.

"Tatizo letu sisi watendaji ni kutokuwaandikia watu hawa wa nini tumekifanya katika maamuzi yetu na kutokuweka kumbukumbu sahihi, kama mmeshughulikia tatizo la mtu mpeni mrejesho kwa maandishi na kama ataona hajaridhika mshaurini hatua zaidi za kufuata na jambo hilo liwekwe kwenye kumbukumbu zetu ili akija wakati mwingine tusipate shida kwa kudhani ni jambo jipya" alisisitiza Mhe Gambo.

Vilevile amemuagiza Kamishna wa Ardhi kutuma timu maalum itakayoshughulikia kero hizo ndani ya muda mfupi na kuyafanyia ukaguzi mabaraza yote ya Ardhi wilaya za Arusha mjini na Kararu.

"Kamishna nitakutana mara baada ya ziara ya mwenge kupita mkoani mwetu ulete timu maalum itakayopiga kambi hapa kumaliza kero hizi kwani hapa kuna wengine wala hawana migogoro ya ardhi bali wamevamiwa kwenye maeneo yao watu kama hawa polisi ndio sehemu husika na sio kwenye mabaraza ya ardhi, vilevile ukayafanyie ukaguzi mabaraza ya Ardhi ya Arusha mjini na Karatu kwani nayo sioni kama wanafanya kazi zao sahihi sana" aliagiza mkuu huyo wa mkoa.

Katika mikutano hiyo maalum aliyoianza tarehe 29/08/2017 kwa Jiji la Arusha na tarehe 30/08/2017 kwa wilaya ya Karatu Mkuu huyo wa mkoa ameambatana na wataalam wa Ardhi toka ofisi ya Kamishna wa Ardhi,Msajili wa hati Kanda, wataalam wa Ardhi mkoa wa Arusha, mwanasheria toka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na wataalam mbalimbali toka halmashauri husika.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kua na migogoro mingi ya Ardhi na ya muda mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo(katikati) akiendesha mkutano wa kuwasikiliza wanachi wa Jiji la Arusha kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fabian Daqqaro na kulia ni Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bwana. Chitukuro .
Baadhi ya wananchi wa Jiji la Arusha wakisubiri kumuona mkuu wa mkoa wa Arusha na kumweleza kero zao
Wananchi wa wilaya ya Karatu wakiwa katika makundi kusubiri kuonana na RC Gambo na kutoa malamimiko yao.

Sheikh Shariff Majini kufanya Dua nzito Magomeni.

$
0
0
Sheikh Shariff Majini kwa siku mbili mfululizo atafanya Dua maeneo ya Magomeni wilayani Kinondoni Jiji la Dar es salaam.

Dua itafanyika katika viwanja vya Mtambani jirani na ofisi za Serikali ya Mtaa na Dua hiyo itakuwa ni ya hadhara lakini pia ni ya pamoja ili kuifanya kuwa na nguvu.

Huu ni mfululizo wa Dua za Sheikh maeneo mbali mbali Nchini.

Kabla ya Magomeni Sheikh amefanya DUA katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Tanga, Temeke, Viwanja vya TP Darajani na Ukumbini STARLIGHT.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images