Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

MTUHUMIWA WA IPTL SETHI ADAI ANA PUTO TUMBONI LISIPOPATIWA MATIBABU STAHIKI LINAWEZA KUPASUKA.

0
0
Bilionea wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Indeprndent Power Tanzania Limited(IPTL), Harbinder Sethi.
 
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii.
WAKILI wa utetezi, Joseph Makandege  ameiomba Mahakama itoe amri mshtakiwa Habinder Sethi akatibiwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa sababu amewekewa puto ('Balloon') tumboni ambapo asipopata Huduma stahiki linaweza kupasuka na kumpelekea kifo.

Makandege amedai  hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai kuwa mapema, mahakama ilitoa amri mshtakiwa huyo apelekwe katika hospitali ya taifa ya Muhimbili lakini ba baada ya kuwasiliana na mteja wao walibaini Magereza walimpeleka Amana badala ya Muhimbili kinyume na amri ya mahakama.

Makandege aliiomba mahakama  mshtakiwa apelekwe Muhimbili kuhakikisha afya yake inatengamaa na hatimaye aweze kuhudhuria mashtaka yake,

Amedai mahakama ya iliamuru  mshtakiwa huyo apelekwe  Muhimbili baada ya kuzingatia kuwa anaupasuaji ambao ulipelekea  kuwekewa puto(balloon) tumbo lake.

Ameongeza taarifa za kitabibu zinaeleza kuwa hali  hiyo ya mshtakiwa isipohudiumiwa ipasavyo inaweza kupelekea kifo na kudai,  Muhimbili ndiyo hospitali ya  juu ya serikali nchini ambayo inategemewa kwa kuwa na wataalam na vifaa stahiki  vinavyoweza kumtibu Sethi.

Alidai awali mahakama ilitoa amri bila  kumung'unya maneno kuwa Sethi apelekwe Muhimbili lakini magereza wakampeleka Amana huvyo in wazi amri ya mahakama  haijatekelezwa hadi leo.

"Naiomba Mahakama itoe amri rasmi mshtakiwa Sethi apelekwe hospitali ya Muhimbili kupatiwa matibabu" ameomba Mwakandege

Wakili Wa Serikali Mkuu, Vitalis Peter alipinga vikali hoja ya kuwa amri ya mahakama imekiukwa na kudai magereza ndiyo wanakaa na watuhumiwa na kwa mara ya kwanza wao ndiyo wanamuangalia mgonjwa, na kwa tatizo la Sethi
Licha ya kumpeleka Amana, walimpelekea pia mtaalam Dk Wilson kutoka hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Baaada ya kusikiliza hoja zote hizo, Hakimu Shaidi amesisitiza na  kuamuru mshtakiwa Sethi apelekwe Muhimbili kwa ajili ya matibabu

Naye mshtakiwa James Rugemalira ameiomba mahakama apatiwe nafasi ya kuonana na mawakili wake ambao wako zaidi ya 10 kwani kati ya wote hao, mawakili wawili tu ndio wanakibali cha kumuona.

 kesi imeahirishwa hadi Septemba 14 mwaka huu.

Katika kesi hiyo, washtakiwa Sethi na RugemLila wanakabiliwa na mashtaka 12 likiwemo la utakatishaji Wa fedha USD 22,198,545 na bilioni 309,461,300,158.

Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yapungua nchini, Dr. Zekeng

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Suzan Kolimba (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI (UNAIDS), Bw. Dr. Leo Zekeng ofisini kwake jijini Dar Es Salaam leo. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Zekeng alisifu jitihada zinazofanywa na Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi ambazo zimesaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 25 na pia idadi ya watoto wanaozaliwa na virusi vya ukimwi imepungua kwa kiasi kikubwa. Dkt. Zekeng alisema kuwa kutokana na mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Bi Michel Sidibe anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini mwezi Oktoba 2017 .
Dkt. Zekeng akionesha takwimu zilizopo katika ripoti ya UNAIDS zinazoonesha namna maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI yalivyopungua nchini Tanzania. 
Mazungumzo yanaendelea 
Mhe. Naibu Waziri akiagana na Dkt. Zekeng baada ya kukamilisha mazungumzo yao 
Picha ya pamoja 

WASANII NGULI NCHINI KUPIMANA MABAVU DIMBA CONCERT TRAVELNTINE MAGOMENI

0
0
Na Agness Francis,Globu ya Jamii.

Wanamuziki wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini wametambiana kuoneshana uwezo wa kuimba siku ya Tamasha la Dimba Concert litakalofanyika katika ukumbi wa Traventine Magomeni Septemba 2 mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja tukio tamasha la  Dimba Concert,Mwani Nyangasa amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa  Taifa muziki bendi kupambana na wanamuziki nguli wa Bendi ya Msondo ngoma.


“ Dhumuni la tamasha hili ni  kuendeleza muziki wa dansi hapa  nchini  kwa kutumia wasanii hawa wakongwe ili waweze kuonesha vijana,wapenzi na wadau kuwa muziki huu bado upo hai.” Amesema  Nyangasa.


 Nae msanii nguli nchini Hussen Jumbe ametanabaisha kuwa wadau na mashabiki wa muziki huo wafike kwa wingi siku hiyo pale Traveltine  septemba 2 mwaka huu ili kupata radha halisi ya muziki wa dansi.


Kwa upande wake  raisi wa vijana  sauti ya simba Nyoshi El Saadat, amewaomba mashabiki wa muziki huo kufika  kwenye tamasha hilo  na kuwaahidi kutowaangusha na kuwapa burudani ya kukata na shoka.
 Meneja Tukio wa Tamasha la Dimba Concert , Mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Tamasha litakalo wakutanisha Wakongwe wa Muziki wa Dansi nchini na bendi ya Msondo Ngoma katika ukumbi wa Traventine September 2 mwaka huu kwa kiingilio cha shilingi 10,000 na 20,000 kwa VIP.
 Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Tamasha la Dimba Concert , Jimmy Chika akifafnua namna bendi hizo zitkavyotoa burudani kwa mashabiki na wadau wa Muziki wa dansi watakaofika katika ukumbi wa traventine siku ya Jumamosi
 Msanii wa Mkongwe wa Muziki wa dansi nchini, Husein Jumbe akiwatoa hofu Mashabiki wake kuwa muziki wao bado upo juu
 Mwanamuziki wa Mkongwe wa Double M Sound , Mwinyjuma Muumini akijigamba kwa tambo kuwa siku hiyo patachimbika kwa hiyo mashabiki wote wasikose kuhudhuria Tamasha hilo.

MAHAKAMA YAKATAA KUPOKEA KIELELEZO CHA USHAHIDI KESI YA WEMA.

0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo imekataa  kupokea msokoto na vipisi viwili vya bangi vilivyotolewa na upande wa mashtaka kama vielelezo vya ushahidi dhidi ya tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya imayomkabili Wema Sepetu na wenzake.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba ambaye amesema mahakama haiwezi kupokea vielelezo hivyo kwa sababu vina kasoro.

Akitoa uamuzi wake amesema anakubaliana na hoja zilizotolewa  na upande wa mashtaka kwamba msokoto wa bangi na vipisi hivyo vina kasoro kwa kuwa shahidi hakuvifafanua mahakamani.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi September 12/2017.
 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa na wafuasi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakati wakisubiri kusomewa Mashtaka yanayomkabili ya Matumizi ya Dawa za Kulevya.
Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa na Wakili wake Peter Kibatara  wakiingia katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza mashtaka yanayo mkabili ya kutuhumiwa kutumia dawa za kulevya.
 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Wakili Peter Kibatara na Kushoto ni Mama wa Wema Sepetu.

 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu akiwa nche ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayo Mkabiri.
 Msanii wa Filamu hapa nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu  akiwa na wakili wake Peter Kibatara wakiwa nje ya Mahakama ja Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

TIMU YA PAMBA FC KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA MBAO JUMAPILI

0
0
Klabu ya Soka ya Pamba SC ya Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza inayojiandaa na ushiriki wa Ligi daraja la kwanza msimu ujao inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na Mbao Fc mchezo utakaopigwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa 10:00 jioni. 

Mchezo huo utakua mahsusi Kwa kocha wa Pamba SC Mathias King Wandiba kujaribu wachezaji wake kabla ya Ligi daraja la kwanza kuanza septemba 16 mwaka huu ambapo licha ya mchezo huo Pamba itacheza tena michezo mingine miwili ya kirafiki itakayochezwa nje ya Mwanza. 

Hali ya timu ya Pamba SC Kwa maana ya wachezaji wako katika hali nzuri kulekea mchezo huo na timu inarajia kupata ushindi baada ya kufanya mazoezi mbalimbali ikiwemo kufanya mazoezi ufukweni na mengine mengi. 

Wadau na wapenzi wa Soka katika Jiji la Mwanza na maeneo yake Jirani wanaombwa kujitokeza Kwa wingi kuisapoti timu yao katika mchezo utakaopigwa jumapili hii Uwanja wa CCM Kirumba kuanzia saa 10:00 jioni. 

Imetolewa na Idara ya Habari na mawasiliano Pamba Sports Club 

+255766527185 

" PAMBA BACK TO PREMIER LEAGUE 2017/18" .

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAHANDISI NCHINI KUFANYIKA MKOANI DODOMA

0
0
 Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akieleza juu ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 7 hadi 8 mwezi Septemba.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi (kushoto) akionesha kwa waandishi wa habari picha yenye mashine ya kushindilia barabara ambayo imegunduliwa na wahandisi wa hapa nchini na kupewa jina la Magufuli One, kulia ni Msajili Msaidizi wa bodi hiyo, Mhandisi Benedict Mukama .
Msajili Msaidizi wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Benedict Mukama  (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akieleza juu ya maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 7 hadi 8 mwezi Septemba, kushoto ni Kaimu Msajili wa bodi hiyo, Mhandisi Patrick Barozi.
Picha na Eliphace Marwa - MAELEZO

MWIGULU AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI UREJESHAJI WA WAKIMBIZI WA BURUNDI WALIO TAYARI KUREJEA NCHINI KWAO

0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi, ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi  Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akipitia nyaraka mbalimbali wakatiKikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi,Harrison mseke.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba(watano kulia), Waziri wa Mambo ya Ndani na Elimu ya Uzalendo kutoka nchini Burundi, Pascal Barandagiye, (wasita kulia), na Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi  Duniani (UNHCR) nchini Tanzania,Chansa Kapaya(wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kikao cha 19 kinachoshirikisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR),lengo ni kujadili na kuwekeana makubaliano juu ya Mpango wa Kuwarejesha Wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa katika makambi ya wakimbizi ambao wako tayari kurejea nchini kwao.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) WATAKIWA KUFANYA KAZI ZAO KWA UFANISI

0
0
Na Mwandishi Maalum

31/08/2017 Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma, kuongeza ufanisi na kutoa huduma bora kwa wagonjwa ili epukana na malalamiko yanayoweza kujitokeza.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Prof. Janabi pia aliwahimiza wafanyakazi wa Taasisi hiyo kuendelea kutunza vizuri kumbukumbu mbalimbali zikiwemo za wagonjwa na utendaji wa kazi zao za kila siku ili pale zitakapohitajika zipatikane kwa haraka.

“Mjitahidi kujaza fomu ya wazi ya mapitio na upimaji utendaji kazi (OPRAS) kwa wakati ili kusiwe na malalamiko ya upandaji wa vyeo kwani ujazaji wa fomu hizo ndiyo unaowezesha mfanyakazi kupimwa utendaji wake kwa kipindi cha mwaka mzima”, alihimiza Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Godfrey Tamba aliupongeza uongozi wa Taasisi hiyo kwa kazi wanayoifanya ya kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi zao katika mazingira bora.

Tamba alisisitiza, “Wafanyakazi wenzangu tunaodai haki zetu tukumbuke kutimiza wajibu wetu wa kazi kwa wakati, kwani uongozi wa TUGHE hautawatetea watu ambao hawatimizi wajibu wao ipasavyo”.

Hiki ni kikao cha pili cha wafanyakazi wote kufanyika tangu kuanza kwa mwaka huu ambapo katika kikao hicho mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.

MASOGANGE ANAKESI YA KUJIBU KUSIKILIZWA TENA OKTOBA 12 MWAKA HUU.

0
0
Video Queen, Agnes Gerlda, maarufu kama Masogange (Kulia), akiwa na mpambe wake wakitoka katika viunga vya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu   ambapo amepatikana na kesi ya kujibu katika tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya zinazomkabili mahakamani hapo uamuzi uliotolewa na Hakimu Wilbard Mashauri.

Akisoma uamuzi huo baada ya shahidi Wa mwisho Wa upande wa mashtaka kumaliza kutoa ushahidi wake, hakimu Mashauri amesema, baada ya kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka ameridhika kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu na kumtaka ajiandae kujitetea.

Mshtakiwa Msogange amedai kuwa atajitetea kwa kiapo na pia atakuwa na mashahidi watatu watakaofika mahakamani hapo kumtetea.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 12, mwaka huu.

MABADILIKO YA UNAHODHA KATIKA TIMU NI JAMBO LA KAWAIDA

0
0
Na. Honorius Mpangala.

Ilikuwa ni katika mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi Lipuli nilipomwona Asante kwasi akiwa amevaa 'usinga' wa nahodha. Pale pale kuna vitu vikaanza kunifikirisha nikijaribu kurejea kwenye kauli za wadau na wapenzi wa soka letu.


 Kauli ambazo zinifanya akili izame huko ni katika kumbukumbu ya maneno yaliyotolewa baada ya benchi la ufundi la Simba kunadili uongozi wa wachezaji. Maneno yalikuwa dhidi ya John Rafael Bocco kupewa unahodha msaidizi nyuma ya Method Mwanjale na Mohammed Hussein. Ilikuwa katika kambi ya klabu ya Simba nchini Afrika kusini ambapo benchi la ufundi liliamua kubadili uongozi wa wachezaji. 

Mabadiliko yalifanya Method Mwanjale kuwa nahodha badala ya Jonas Gerrard Mkude na kupewa wasaidizi wake .Katika orodha ya wasaidizi ilikuwa jina la John Rafael Bocco ndilo lililowafanya wapenzi na wadau walitolee hoja tofauti.

 Maswali yalikuwa kwanini Bocco na sio Kazimoto au wengine waliokuwepo klabuni hapo Kwa muda mrefu. Ilichukuliwa kama ni kitu cha kushangaza sana katika tukio lile. Sababu kubwa ilikuwa kutokana na Kuvuliwa unahodha huo mchezaji mwandamizi wa klabu Jonas Gerrard Mkude.

 Lakini moja ya mambo yaliyo nifurahisha ni pale Mkude alipoongea kuwa hata yeye alipopewa kuna mchezaji alivuliwa hivyo amechukulia kawaida kwake. Tukio la mabadiliko ya kiuongozi sio geni Kwa wachezaji wanaojitambua. Hapa kwetu ilionekana tofauti sana kimapokeo. Wako waliofikiria mbali zaidi na kutaka kuuaminisha umma kuwa ni maajabu ya dunia.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MAMIA WAMIMINIKA KUJISAJILI KATIKA MFUKO WA FIDIA (WCF) IKIWA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI JENISTA MHAGAMA

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MUITIKIO wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema leo Agosti 31, 2017.

Itakumbukwa ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.

“Kwakweli tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa agizo alilolitoa kwani limetoa msukumo mkubwa, waajiri wengi wamejitokeza kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko.” Alisema Bw. Luvena

K-VIS Blog ilishuhudia idadi kubwa ya waajiri wakiwa wamejitokeza leo Agosti 31, 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho kwa waajiri kutekeleza agizo la Mheshimiwa waziri, wakiwa wamejazana kwenye ofisi za WCF kujisajili na kuwasilisha michango, ambapo kazi hiyo ya kuwahudumia ilikuwa ikiongozwa na Meneja Matekelezo - WCF, Bw.Victor Ruvena.
Waajiri, wakihudumiwa na maafisa wa WCF, leo Agosti 31, 2017.

HII NDIO SABABU YA EID-AL-ADHA KUITWA 'SIKUKUU YA KUCHINJA

0
0
Eid al-Adha ni miongoni mwa sikukuu kubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu ukiachana na Eid- al-Fitr inayosherehekewa kila mwaka duniani kote. Kwa mwaka huu sikukuu hii inatarajiwa kusherehekewa siku ya Ijumaa ya Septemba mosi ambapo kwa waumini wa dini hiyo ni kipindi cha kujitolea, kuonyesha ukarimu kwa marafiki, familia na watu wenye uhitaji.

Kama zilivyo sikukuu nyingine kuna baadhi ya watu huwa hawajui ni kwa nini huwa zinaseherehekewa namna zinavyosherehekewa. Jumia Travel kupitia makala haya imekukusanyia mambo ya msingi kuhusu maana ya sikukuu hii na namna ya kusherehekea.

Waislamu huisherekea sikukuu ya Eid al-Adha kwa kuchinja mnyama ikiwa ni kuheshimu kitendo alichokifanya Ibrahim au Abraham (anavyoitwa na Wakristu na Wayahudi). Ibrahim aliamriwa na Mungu kumtoa mtoto wake pekee kiume kama sadaka kwa kumchinja ambapo alikubali kutii amri hiyo bila ya kupinga. Kabla ya kumtoa sadaka mtoto wake sadaka, Mungu aliingilia kati kwa kumtuma Malaika wake ambaye altaka amchinje kondoo badala ya mtoto wake.
Katika kuadhimisha tukio hilo kubwa la kiimani, kila mwaka sikukuu hii inaposherehekewa waumini wa Kiislamu huchinja mnyama halali kwa mujibu wa imani. Mnyama huyo anaweza kuwa ni ng’ombe, ngamia, mbuzi au kondoo inategemea na uwezo wa mtu. Baada ya kuchinja, nyama hugawanywa katika mafungu matatu ambapo la kwanza hubakia kwa familia; la pili hugawiwa kwa ndugu, jamaa na marafiki; na kisha la tatu hugawiwa kwa watu masikini na wenye uhitaji.
Hivyo basi sikukuu hii husherehekewa kama ni ishara ya kukumbuka utiifu wa Ibrahim mbele ya Mungu lakini pia huashiria tamati ya safari ya Hijja. Kila mwaka Waislamu wote duniani huenda kuhiji mjini Macca uliopo nchini Saudi Arabia. Eid al-Adha ni tofauti na Eid al-Fitr ambayo yenyewe husherehekewa baada ya kuisha kwa mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan.

Katika kalenda ya mwezi wa Kiislamu, sikukuu ya Eid al-Adha hutukia siku ya 10 ya mwezi wa 12 na hudumu kwa muda wa siku nne mpaka siku ya 13. Kwa mwaka huu itaanza siku ya Ijumaa ya Septemba mosi na kufikia ukomo siku ya Jumanne ya Septemba 5. Maadhimisho ya sikukuu hii hubailika kila mwaka kulingana na mabadiliko ya kalenda, hivyo haimaanishi mwaka ujao sherehe zitaangukia tarehe sawa na za mwaka huu.
Kama ilivyo kwa Eid al-Fitr, Waislamu huanza kusherehekea Eid al-Adha asubuhi kwa kwenda msikitini kwa ajili ya sala, kusikiliza mawaidha kisha kufuatiwa na kutakiana heri ya sikukuu pamoja na kugawiana zawadi. Baada ya hapo wanyama huchinjwa ikiwa ni sehemu ya sherehe na kisha nyama hugawiwa kwa ndugu, jamaa na marafiki ikiwemo masikini na watu wasio na uwezo. Lakini pia watu wenye uwezo huwagawia pesa watu masikini na wasio na uwezo ili nao waweze kusherehekea kwa furaha kama watu wengine.
Kwa mfano, kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ni rahisi kugundua kwamba ni sikukuu kutokana na shamrashamra zinavyoonekana. Mitaa, maduka, migahawa, sehemu za kutembelea kama vile fukwe ya bahari ya Hindi hufurika watu wakifanya manunuzi, kula chakula na kufurahia kwani mara nyingi huwa ni mapumziko ya kitaifa. Jumia Travel inaamini kwamba utakuwa umeelewa ni nini maana ya Eid al-Adha na namna inavyosherehekewa ili kutopoteza maana yake. 

RC makonda azidi kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu

0
0
Mkuu wa mkoa wa dar es salaam, Paul Makonda leo ametambulisha kamati ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za walimu kwa shule za msingi na sekondari zilizobainika kukosa ofisi hizo.

Kamati ya ujenzi wa ofisi za walimu itaongozwa na Mwenyekiti Kanali Charles Mbunge kutoka JKT, Makamu Mwenyekiti ACP Solomon Urio kutoka Jeshi la Magereza, Katibu wa kamati ambaye pia ni afisa elimu wa mkoa  Hamis Lissu, Katibu Msaidizi SACP Juma Hamis kutoka jeshi la polisi pamoja na wajumbe wengine.

Makonda amesema ujenzi wa ofisi hizo utaanza september 5, 2017 chini ya vyombo vya ulinzi na usalama kutoka JKT, Polisi na Magereza walioamua kuunga mkono juhudi za mkuu wa mkoa.

Amesema kuwa hadi sasa JKT wametoa vijana 300 kwajili ya ujenzi huo huku jeshi la magereza likitoa wafungwa watakaofanya kazi ya kutengeneza matofali.

Aidha makonda amewaomba wadau na wananchi kuchangia fedha na vifaa ikiwemo mabati, nondo, saruji, kokoto, mchanga, mbao na nguvu kazi ya watu ilikuwafanya walimu wafanye kazi katika mazingira mazuri.

Amesema kuwa wananchi wanaweza kuchangia fedha kupitia account ya
Crdb namba 0150296180200 au kuwasilisha michango yao ofisi ya mkuu wa mkoa.

Katika ujenzi huo channel ten wameamua kumuunga mkono rc makonda kwa kuhamasisha jamii katika uchangiaji.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za walimu kwa shule za msingi na sekondari zilizobainika kukosa ofisi hizo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA ULINZI NA USALAMA WASASA NA WASTAAFU IKULU JIJINI DAR

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika chumba cha Mkutano kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na na viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wasasa na wastaafu Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo yao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Omar Mahita(IGP Mstaafu), Said Mwema(IGP Mstaafu) pamoja na Ernest Mangu(IGP Mstaafu) Ikulu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Omar Mahita Ikulu jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

HUKUMU YA UCHAGUZI KENYA KUTOLEWA KESHO IJUMAA

0
0
Na   Bashir   Yakub.

1. WAHUSIKA
Walalamikaji(petitioners) ni wawili. Wa kwanza Raila Amolo Odinga na wa pili Stephen Kalonzo Musyoka, mgombea mwenza.
Walalamikiwa(respondents) ni watatu, wa kwanza ni tume huru ya uchaguzi IEBC. wa pili mwenyekiti wa tume hiyo ndg Wafula Chebukati na watatu ni ndg Uhuru Muigai Kenyatta.

Pia kuna walioomba kuingia katika kesi hiyo na kukubaliwa. Wa kwanza mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ameingia kama rafiki wa mahakama(amicus curiae) , wa pili chama cha wanasheria kenya "Law Society of Kenya LSK," nao kama rafiki wa mahakama.

Wa tatu  na  nne  ni Dr Ekuru Aukot na Mr. Michael Wainaina ambao wameingia kama wahusika wenye maslahi(interested parties). Hawa nao walikuwa wagombea urais.

2. MUDA WA KESI.

Kwa katiba ya Kenya mlalamikaji anazo siku 7 tu za kufungua shauri tokea siku matokeo yalipotangazwa. Na mahakama inazo siku 14 tu za kusikiliza na kutoa hukumu tokea siku shauri lilipofunguliwa.

Kesi  hii  imekuwa  ikisikilizwa  mpaka  usiku  saa  tano  zikiwemo  siku  za  jumamosi  na  jumapili  ili  kuendana na  muda wa  katiba.

3. MAHAKAMA NA MAJAJI.
Mahakama inayosikiliza ni mahakama ya juu( the supreme court).
Majaji wanaosikiliza ni 7 wakiomgozwa na Jaji mkuu David Maraga na naibu wake mwanamama Philomena Mwilu. Wengine ni Jackton Ojwang, Mohammed Ibrahim, Njoki Ndung'u, Smokin Wanjala na Isaac Lenaola.


LEO KATIKA KUMBUKUMBU: NI YULE YULE WA MEI 18, SAID SUED 'SCUD'

0
0
PICHANI:  Mshambuliaji wa Yanga, Said Sued 'Scud', wanne kulia.


Tarehe kama ya leo, 1991, mshambuliaji wa Yanga, Said Sued 'Scud', alifunga bao pekee na la ushindi dhidi ya Simba kwenye mchezo wa raundi ya pili ya ligi daraja la kwanza(sawa na ligi kuu siku hizi).

Bao hilo la dk ya 59(14 kipindi cha pili) lilifuatia lile la mchezo wa raundi ya kwanza wa Mei 18 mwaka huo ambapo 'Scud' pia alifunga bao pekee na la ushindi dhidi ya Simba.

Mtangazaji wa mchezo huo, Ahmed Jongo wa Radio Tanzania Dar Es Salaam, alisikika akisema, "Gooooooo...ni yule yule wa Mei 18". Msemo huu ukajipatia umaarufu sana mitaani hasa pale mtu akirudia kufanya kitu alichowahi kukifanya hapo kabla.

Mabao haya yanamfanya Scud awe mchezaji pekee kufunga peke yake mabao pekee na ya ushindi katika mechi mbili mfululizo za watani wa jadi kwenye ligi ya Bara.

Dua Said wa Simba naye aliwahi kufunga kwenye mechi mbili mfulizo; 
Julai 17, 1993, Simba wakishinda  1-0, bao la dk ya 69 na 
Septemba 26, mwaka huo huo, Simba wakishinda 1-0 tena, bao la dk 13. Hata hivyo, mechi hizi zilikuwa za ligi tofauti; ya kwanza ilikuwa ligi daraja la kwanza na ya pili ilikuwa ligi ya Muungano.

Ligi ya Muungano ilikuwa muendelezo wa ligi ya Bara na ya Zanzibar na bingwa wake ndiyo alikuwa akihesabiwa kama bingwa wa Tanzania huku bingwa wa Bara na yule wa Zanzibar wakiishia kucheza Kombe la Kagame pekee. Hii ndiyo sababu FIFA wanaitambua Yanga kama bingwa mara 22 wa Tanzania badala ya mara 27 kama wanavyojitambua wao. Kwa sababu, mara tano kati ya 27 zao, walishinda ubingwa wa Bara ambao kuanzia 1982 mpaka 2003, ulikuwa hautaambuliki na FIFA.

JINA LA SCUD

Mwaka huo, 1991, kulikuwa na Vita ya Ghuba iliyosababishwa na Iraq chini ya Sadam Hussein kuivamia Kuwait. Majeshi ya umoja wa mataifa yakiongozwa na Marekani, yaliingilia kati kuing'oa Iraq, vita ikazuka.

Sadam Hussein alijivunia mabomu ya Scud ambayo yalikuwa tishio kweli kweli.

Katika mchezo wa 'kutesti mitambo' kati ya Yanga na Reli ya Morogoro uwanja wa Karume, Yanga walikuja na mtambo mmoja uliokuwa ukipiga mashuti kama mabomu ya Scud. Hapo ndipo mashabiki wakambatiza jina hilo mshambuliaji wao mpya ambaye alikuwa hafahamiki sana hapo kabla.

CHUO CHA USAFIRI WA ANGA CATC, KINACHOMILIKIWA NA TCAA CHATUNUKIWA TENA CHETI CHA TRAINAIR PLUS

0
0
Mkurgenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari (Kati Kati) Akionyesha  Cheti cha Trainair Plus Kilichotunukiwa kwa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Kinachomilikiwa  na TCAA. CATC Imefuzu kuwa  Mwanachama Shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).
Watumishi wa Chuo Cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) wakifurahia kutunukiwa Cheti cha Trainair Plus. CATC imetunukiwa Cheti hicho baada ya kufuzu kuwa  Mwanachama shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). 
Mkurgenzi Mkuu,Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari (Kati Kati) Akifungua Cheti cha Trainair Plus Kilichotunukiwa kwa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Kinachomilikiwa  na TCAA. CATC Imefuzu kuwa  Mwanachama Shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO). 

Kwa mara nyingine  Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania( CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kimefuzu na kutunukiwa cheti cha kuwa  mwanachama Shirikishi wa wa Umoja wa Vyuo Vya Mafunzo ya Usafiri wa Anga Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).

Cheti hicho ambacho maarufu kama TrainAir Plus, kimetolewa na Shirikisho la  TrainAir Plus, wiki hii baada ya CATC kufuzu vigezo na masharti ikiwa ni pamoja na kuandaa mitaala inayokubalika na shirikisho. Kwa mara ya kwanza CATC ilitunukiwa cheti hicho mwaka 2012 na muda wake uliisha mwaka 2015.

Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea cheti hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza S. Johari amewachagiza watumishi wa chuo cha CATC kufanya kazi kwa bidiii na kuhakikisha CATC inaendelea kujiimarisha  na kutoa mafunzo  bora zaidi.

Hiki ni chuo cha kimataifa kwa kuwa kinatoa mafunzo  kwa wanafunzi wa  kutoka nje ya nchi,  lengo letu tuhakikishe tunakuwa wanachama kamili wa TrainAir Plus, Amesema Hamza . Ameahidi kutoa msaada unaohitajika katika kukiimalisha chuo hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa  Chuo cha CATC, Aristide Kanje, Amemuhakikishia Mkurugenzi Mkuu kuwa timu yake itaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha chuo hicho  kinatakeleza majukumu yake kama inavyotakiwa.

Pamoja na faida nyingine, vyuo wanachama  wa TRAINAIR PLUS wana fursa ya chuo kutambulika kimataifa,  kupata, kubadilishana  mitaala ya masomo  ya usafiri wa anga inayoandaliwa kwa kufuata viwango vinavyokubalika kimataifa.

BENDI ZAANZA KUPASHA KUELEKEA TAMASHA LA MUZIKI LA DIMBA

WAKUU WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA WASTAAFU WAMFAGILIA RAIS DKT MAGUFULI

TRA YAKAMATA SUKARI YA MAGENDO BAGAMOYO

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images