Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1888 | 1889 | (Page 1890) | 1891 | 1892 | .... | 3278 | newer

  0 0  0 0  0 0


  0 0


  0 0

  Katika kuboresha huduma za afya mkoa wa ruvuma kupeleka wanafunzi wanaosomea masomo ya sayansi katika vyuo vya afya ili kuboresha huduma za afya mkoani hapo hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya songea POLOLETH MGEMA habri kamili hii hapa video yake ...

  0 0  0 0


  0 0

  Na Neema Mathias na Paschal Dotto- MAELEZO.
  Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) imeanza rasmi utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kutoa leseni kwa vyombo vya machapisho yakiwemo Magazeti na Majarida.  

  Akizungumza katika makabidhiano ya leseni hizo Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema  utoaji wa leseni ni utekelezaji wa agizo rasmi lililotolewa Agosti 23, 2017 lililowataka wamiliki wote wa machapisho kujisajili upya na kupewa leseni kwa lengo la kuifanya tasnia ya Habari kuwa taaluma rasmi kama zingine.
  “Leseni hizo zimeanza kutolewa rasmi Agosti 23 na zoezi hilo litaendelea hadi Oktoba 15, 2017 na baada ya hapo wale amabo watachapisha magazeti  na majarida bila kuzingatia Sheria hiyo watakuwa wametenda kosa la jinai”, alisema Dkt. Abasi.
  Katika zoezi hilo Dkt. Abbasi alitoa leseni kwa vyombo vinne ambavyo ni Jarida la Nchi Yetu linalomilikiwa na Idara ya Habari MAELEZO, gazeti la Daily News, Habari Leo pamoja na Spoti Leo ambayo ni magazeti ya Serikali.
  Dkt. Abbasi ametoa wito kwa vyombo vingine vya habari ambavyo bado havijaanza taratibu za upataji wa leseni visisubiri hadi dakika za mwisho za mchakato huo ili kuepuka msongamano na usumbufu usio wa lazima.
  “Nitumie fursa hii kuwaalika ambao hawajapata leseni wafanye haraka, Tanzania Standard Newspaper (TSN) walitimiza masharti ndani ya siku tatu ndio maana leo wamepata leseni hizo, hakuna urasimu wala nia mbaya ya kufungia baadhi ya machapisho kama wengi wanavyodai bali ni katika kutekeleza matakwa ya Sheria”, alisisitiza Dkt. Abbasi.
  Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa TSN Dkt. Jim Yonazi ameviasa Vyombo vingine vya Habari kutekeleza agizo hilo ili kupata uhuru mpana katika uwajibikaji pamoja na kuwa mfano wa kutii Sheria bila shuruti ili taaluma ya habari iendelee kuheshimika kwa jamii.
  “Ukifanya kazi kihalali unakuwa na uhuru wa kufanya kazi vizuri, ubunifu unaongezeka na unafanya biashara bila wasiwasi”, alisisitiza Dkt.Yonazi.
   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la Daily News mwakilishi wa gazeti hilo Bi. Pudenciana Temba. Idara ya Habari imetoa imetoa leseni nne kwa ambapo leseni namba moja imetolewa kwa Jarida la Nchi Yetu linalotolewa na Idara hiyo, namba mbili imetolewa kwa HabariLeo, namba tatu Dailynews na nne imetolewa kwa Spotileo.Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Usajili Bw. Patrick Kipangula.
   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la HabariLeo mwakilishi wa gazeti hilo mhariri wa gazeti hilo Bw. Amir Mhando leo Jijini Dar es Salaam. Leseni hiyo imetolewa kufuatia kuanza kwa matumizi ya sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayomiliki magazeti ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Dkt. Jim Yonaz kwa Kampuni yake kuzingatia matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016  kwa kujisajili upya na kupatiwa leseni.
  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa magazeti ya HabariLeo, DailyNews, SpotiLeo yanayomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na uongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya kukabidhiwa Lesini za usajili wa magzeti hayo leo Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Frank Shija - MAELEZO

  0 0

  Timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imeendelea kung’ara katika Mashindano ya muhula wa nne wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi wa nchi za Afrika Mashariki yanayofanyika mjini Bujumbura, Burundi. 
   Baada ya jana timu ya Mpira wa kikapu ya JWTZ kuwafunga mabingwa watetezi Ulinzi Kenya kwa vikapu 68-58, mori wa vijana wetu uliochagizwa na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU, ulipanda tena leo katika mpira wa kikapu ambapo vijana hao hodari wa CDF Mabeyo wameibugiza Burundi kwa vikapu 94-18 bila huruma.  Na katika kabumbu pia JWTZ iliibuka kidedea kwa kuwapiga tena Warundi kwa mabao 2-1. 
  “Tunashukuru Mungu kwa matokeo hayo yote”, mkuu wa msafara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga, ameiambia Globu ya Jamii leo kwa njia ya mtandao. 
  Brigedia Jenerali Kemwaga, ambaye yeye mwenyewe ni mchezaji nguli wa zamani wa mpira wa kikapu, ameeleza kufurahishwa na vijana wake ambao wamekuwa tishio katika michezo yote wanayoshiriki. 
  Kaulimbiu ya Mashindano hayo ni “Shiriki michezo kama sehemu ya kazi, Kulinda Afya zetu na Kudumisha Mshikamano”, na yanahusisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na wenyeji Burundi. 
  Timu ya JWTZ daima imekua ikifanya vizuri kwa kuchukua nafasi ya ya tatu kwa ujumla kati ya nchi zote zilizoshiriki katika mashindano yaliyofanyika hapo awali. Na safari hii timu hiyo kabambe imepania kunyakua nafasi ya kwanza kwani wao kila walipo ni HAPA KAZI TU.
  Timu ya Mpira wa kikapu  ya JWTZ  ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuwafunga mabingwa wa mwaka jana Ulinzi Kenya kwa vikapu 68-58 jana mjini Bujumbura, Burundi.
  Kiongozi wa safara wa timu ya JWTZ ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga akifurahia ushindi wa timu ya mpira wa kikapu jana mjini Bujumbura, Burundi.
  Kiongozi wa safara wa timu ya JWTZ ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMATA) Brigedia Jenerali Martin Amos Kemwaga akihojiwa na mwandishi wa ITV wa Bujumbura Bw. Balen.

  0 0

  Kipanya sasa amejiunga rasmi na Vodacom RED na atakuwa anakuletea mfululizo wa maisha anayoishi sasa baada ya kujiunga na huduma hii mpya inayotolewa na kampuni ya simu nchini Vodacom Tanzania. Hatujui atatuletea nini lakini tunaimani atawapa wafuasi wake faida anazozipata akiwa na Red RLX, endelea kufuatilia hapa kuona nini atatuletea.


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Morogo Dkt Kebwe Stephen akimsikiliza Mwanasayansi Susan Rumisha aliyekuwa akitoa maelezo mbalimbali kuhusu juu ya umuhimu wa utafiti wa vifo vinavyotokea katika Hospitali za Tanzania,
  uliofanyika hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na mrejesho unaoendelea. Dkt Kebwe aliwatembelea na kuzungumza nao washiriki wa Warsha hiyo iliyofunguliwa hivi karibuni mkoani Morogo.
   Mwanasayansi Peter Emanuel akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen wakiwemo na washiriki wengine wa Warsha hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Morogo Dkt Kebwe Stephen (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mbalimbali wa Warsha hiyo mkoani humo.

  =====   ===== ====== ======

  MUKHTASARI WA TAARIFA YA UTAFITI WA VIFO VINAVYOTOKEA KATIKA HOSPITALI YA TANZANIA

  Utangulizi

  Taarifa za vifo ni moja ya vyanzo muhimu vya takwimu katika kupanga mipango na kuandaa sera ya afya. Kuainisha vyanzo vya vifo katika hospitali zetu ni muhimu ili kufuatilia ongezeko la matukio ya vifo na kuweka vipaumbele katika kuboresha huduma za afya. Hata hivyo, kumekuwa na uhaba mkubwa wa takwimu za vifo vinavyotokea katika hospitali zetu zilizoainishwa kama inavyostahili.

  Utafiti huu ulifanywa kuainisha matokeo ya vifo katika hospitali 39 za Tanzania ili kubaini maradhi yanayoathiri jamii yetu. Utafiti huu pia ulichunguza uwepo, upatikanaji na ubora wa takwimu za vifo hospitalini.

  Mbinu za utafiti: Utafiti huu ulifanyika kati ya Julai na Desemba 2016 na ulihusisha jumla ya hospital 39. Hospitali hizo ni pamoja na hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Kanda na Mikoa, Hospital Maalum na hospitali za Wilaya. Takwimu hizi zilipatikana kutoka kwenye rejesta za hospitali na za Wakala wa Vizazi na Vifo katika ofisi za Mikoa na Wilaya. Taarifa zilizokusanywa zilihusu wasifu wa jinsia ya mgonjwa na chanzo cha kifo.

  Vyanzo vya vifo viliwekwa katika makundi 45 kulingana na utaratibu wa makundi ya magonjwa uliowekwa na Shirika la Afya Duniani.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0

  ZAIDI ya wakazi 3000 wanaoishi katika eneo la Jaribu tena na Mwisho wa Shamba kata ya Maweni Jijini Tanga wanatarajiwa kuepukana na adha ya uhaba wa maji safi na salama iliyodumu kwa muda mrefu baada ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Jijini Tanga kuwa pelekea mradi wa maji.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungenzi Mtendaji wa Tanga UWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema kuwa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
   
  Alisema kuwa gharama za mradi huo hadi kukamilika kwake ni kiasi cha sh Mil98,lakini kutoka na gharama kuwa kubwa waliwashauri  wananchi ili kuona namna watakavyoweza kufanya kazi za kujitolea ili kukamilika kwa wakati.
   
  Alisema kuwa ndipo wananchi walipoamua kushiriki katika kazi za kuchimba mitaro ambayo itaweza kutumika kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya mabomba kutoka Pongwe hadi katika maeneo hayo yenye uhitaji.“tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano waliounyesha wa kushiriki kwenye uchimbaji huo kwani wameweza kuokoa kiasi cha sh Mil 10 ambazoingebidi tuwalipe vibarua kwa ajili ya uchimbaji wa mitaro hiyo”alisema Mgeyekwa.
  Alisema kuwa mradi huo umegawanyika katika awamu ambapo katika awamu ya kwanza unatarajiwa kusambaza maji katika umbali wa Km 5.5 kutoka eneo la Pongwe hadi katika mitaa ya Jaributena na Mwisho wa shamba.Nae Mbunge wa Jimbo la Tanga Mussa Mbaruku alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kwa haraka kutaweza kusaidia wananchi hao kuepukana na adha ya ukosefu wa maji iliyodumu kwa muda mrefu.
  “Niwapongeze wananchi wa kata ya Maweni namna walivyoweza kujitolea kushirikina na serikali yao katika kumaliza changamoto zinazowakabili kwani hii inaonyesha kuwa ili kuharakisha maendeleo ya sehemu husika kunahitaji ushirikishwaji wa pande zote”alisema Mbunge Mbaruk.

  Kwa upande wake Mtendaji wa Kata wa mtaa wa kichangani Ziada Ali alisema kuwa wakazi wa mtaa huo walilazimika kutembea umbali wa Km 5kwa ajili ya kutafuta huduma hiyo kila siku.
  Alisema kuwa mradi huo utakapo kuwa umekamilika itakuwa ni faraja kwa wananchi wa mitaa ya Jaribu tena na Mwishi wa shamba pamoja na kuwapunguzu adha ya kwenda mwendo mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma ya maji.

  Vile vile Mwenyekiti wa Kamati ya Maji  Lucas Nyengo alisema kuwa kwa takribani miaka minne wamekuwa wakiomba kupatiwa huduma hiyo lakini wanashukuru kwa awamu hii kupatiwa mradi huo.
  Alisema kuwa kufuatia shida ya maji ilidumu kwa muda mrefu waliamuakuunga mkono jitihada za mamlaka kwa kushiriki katika uchimbaji wa mtaro ili kuharakisha mradi huo.
  Alisema kuwa kutokana na shida ya maji iliyokuwa inawakabili
  walilazimika kununua  ndoo moja kwa kiasi cha sh 500 jambo ambalo ni gharama kubwa ukilinganisha na uhitaji wa huduma hiyo
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Serikali imesema kuwa imetumia shilingi Bilioni 85 kupeleka mawasiliano vijijini kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuzipatia ruzuku kampuni za simu za mkononi ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za mawasiliano.

  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwenye Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu mjini Dodoma.


  “Mfuko huu unaendelea kuhakikisha kuwa mawasiliano bora yanafika katika maeneo mengi nchini hususan vijijini na kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara ambapo Takwimu zinabainisha kuwa, tayari mawasiliano   yamefikishwa kwenye kata 443, vijiji 1,939  kuanzia mwezi Machi 2013 hadi Julai mwaka huu”, amefafanua Naibu Waziri Ngonyani.


  Ameongeza kuwa tayari Mfuko umetiliana saini mkataba na kampuni za simu za mkononi mwezi Agosti mwaka huu kuhakikisha kuwa zinapeleka mawasiliano kwenye kata nyingine 75 na vijiji 154.


  Aidha, ametanabaisha kuwa hadi hivi sasa asilimia 94 ya wananchi wanapata huduma ya mawasiliano nchini na kuongeza kuwa, Serikali kupitia mkataba wake na Kampuni ya Simu ya Halotel imefikisha mawasiliano kwenye jumla ya vijiji 3,069 kati ya vijiji 4,000 tangu walipoanza utekelezaji wa jukumu hilo mwezi Novemba, 2015 na wanatarajia kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.


   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo katika kikao na Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Kakoso na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo Eng. Angelina Madete. 

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Eng. Angelina Madete akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu miradi ya maendeleo ya mawasiliano vijijini katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma.

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kasoso, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kamati hiyo katika kikao kilichowakutanisha na uongozi wa Wizara ya  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mjini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani.

  Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu maeneo ya vijijini yaliyofikiwa na mawasiliano katika kikao na Kamati hiyo mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Dua Nkurua na kushoto ni Mhe. Rita Kabati wajumbe wa Kamati hiyo.


  0 0

  Na: Veronica Kazimoto-Mororgoro.

  Jumla ya wakufunzi 52 wakiwemo Mameneja Takwimu wa mikoa yote nchini wamepewa mafunzo juu ya mbinu mbalimbali zinazotumika kufundishia wadadisi kwa ajili ya kupata takwimu bora za kilimo na mifugo.

  Mafunzo hayo ya wiki moja yanayoendelea kufanyika mkoani morogoro, yanalenga kuwajengea uwezo wakufunzi hao ili waweze kuwafundisha wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa Mwaka 2017 kwa ajili ya kupata takwimu rasmi zitakazotumika katika kupanga mipango ya maendeleo.

  Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya amewataka wakufunzi wao kuzingatia kwa makini mafunzo hayo ili waweze kuwafundisha kwa ufanisi wadadisi wakaokusanya taarifa za utafiti huo wa kilimo na mifugo.

  "Ili kuiwezesha nchi yetu kupata takwimu bora za kilimo na mifugo inatakiwa ninyi wakufunzi kuzingatia kwa makini mafunzo haya ili muweze kuwafundisha kwa ufanisi mkubwa wadadisi ambao watazunguka nchi nzima kukusanya takwimu za kilimo na mifugo", amesema Ruyobya.

  Utafiti wa Kilimo na Mifugo hufanyika kila mwaka ambapo utafiti wa mwaka huu utafanyika kuanzia mwezi Oktoba, 2017 chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda na Biashara.
   Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Irenius Ruyobya akizungumza leo na Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 wakati wa mafunzo ya wakufunzi hao yanayoendelea kufanyika mkoani Morogoro. Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.

   Mtalaamu wa Kilimo na Mifugo kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Zanzibar Mzee M. Mzee akiwafundisha Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya wakufunzi hao yanafanyika mkoani Morogoro ambapo utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.

   Mmoja wa Wakufunzi akiuliza swali wakati wa mafunzo ya Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 yanayofanyika mkoani Morogoro.  Utafiti huo wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017 unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.

   Baadhi ya Wakufunzi wakijifunza mbinu mbalimbali zitazotumika kuwafundishia Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya wakufunzi hao yanafanyika mkoani Morogoro ambapo utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017.
  Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Irenius Ruyobya akitoa maelekezo kwa waratibu wa mafunzo ya Wakufunzi wa Wadadisi wa Utafiti wa Kilimo na Mifugo wa mwaka 2017. Mafunzo ya Wakufunzi hao yanafanyika mkoani Morogoro na utafiti huo unatarajia kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Oktoba, 2017. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

  0 0

  Vijana wa JKT wakijisajili majina yao kabla ya kutoa damu kwaajili ya kuchangia.
  Takataka zikiondolewa.

  Na Dotto Mwaibale

  ASKARI wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi namba 831 KJ Mgulani, wamejitolea kuchangia damu pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Zacharia Godfrey Kitani alisema kila maadhimisho hayo yanapofanyika wamekuwa wakifanya shughuli za kijamii kama kufanya usafi na mwaka huu wameona wafanye usafi na kuchangia damu katika hospitali hiyo ili kusaidia wananchi.

  "Ni kawaida yetu katika kuadhimisha siku ya kuanzishwa jeshi letu sisi kama askari kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika maerneo tofauti tofauti kwa siku kadhaa leo hii tunafanya usafi katika Hospitali ya Temeke na kutoa damu na tutaendelea katika maeneo mengine hadi siku ya kilele cha maadhimisho haya hapo kesho kutwa" alisema Kitani.

  Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Husna Msangi alisema msaada huo wa damu waliochangia askari hao utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto ya damu hospitalini hapo kutokana kuwa na mahitahi makubwa ya damu kwa wagonjwa.

  Alisema mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa hivyo amewaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu ambao wataweza kupoteza maisha kwa kukosa damu.
  Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) namba 831 KJ Mgulani, Luteni Kanali, Zacharia Godfrey Kitani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu askari wa kikosi hicho kujitolea damu na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote.
  Jengo la Utawala la Hospitali hiyo.
  Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa Hospitali hiyo, Heri Shekighenda akimtoa damu, Kijana wa JKT, Kafumu Godfrey Ambross wakati akichangia damu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  In fulfilment of its Corporate Social Responsibility, the Karimjee Jivanjee Foundation has donated a brand new ambulance to Idodi health centre through the Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, Hon William Lukuvi worth US$47,519.

  The vehicle is meant to ease the challenges faced by Idodi health centres that hinder them to offer health services to the citizen effectively. Present during the presentation was Karimjee Jivanjee Foundation Chairman, Hatim A. Karimjee and Toyota Tanzania Executive Director, Yusuf A. Karimjee.

  Speaking at the event Karimjee Jivanjee Foundation Chairman, Hatim A. Karimjee said that the Foundation is committed to support communities in Tanzania primarily through education and applauds the efforts of Idodi health centre to support the patients.

  The Hon William Lukuvi thanked the Karimjee Jivanjee Foundation and Toyota Tanzania Ltd for their generosity, said that Toyota is the world’s most successful vehicle manufacturer. For seven generation, the Karimjee Jivanjee Group has established a strong record for its philanthropic activities by contributing to the development and growth of Tanzania and East Africa.

  The Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) is an amalgamation of various Karimjee Jivanjee charitable institutions since the 1940’s. It was founded as a trust in 2006 and officially registered in 2010. Today, KJF’s core charitable and CSR focus centres on Education in Tanzania, most notably by providing annual scholarships to young Tanzanians to study at graduate level. 

  Other past projects and partnerships have included: providing scholarships to Doctors to graduate for Masters Degree in Pediatric Oncology at Muhimbili University of Health and Allied Science (MUHAS) through Tumaini la Maisha (NGO), supporting Read International in supplying text books to secondary schools, supporting Rotary International with various projects including the Muhimbili National Hospital (Cancer ward), promoting science and technology in Tanzania through the Young Scientists Tanzania (YST) programme and educational support to TESA, a Tanzanian NGO established by the Canadian alumni of the Karimjee Secondary School in Tanga. 
  MINISTER for Lands, Housing and Human Settlements Development, Mr William Lukuvi receives an ignitions keys from Karimjee Rivanjee Foundation Chairman, Mr Hatim Karimjee in Dar es Salaam August 30, 2017 for Idodi Health Centre based in Iringa region. The brand new ambulance worth 106/-m to ease the challenges faced by the centre that hinders them to offer health services to patients effectively. 
  Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, William Lukuvi tests the brand new ambulance worth 106/-m in Dar es Salaam yesterday, after receiving it from Karimjee Jivanjee Foundation Chairman, Hatim Karimjee (left) for Idodi Health Centre based in Iringa region. The vehicle is meant to ease the challenges faced by the centre that hinders them to offer health services to patients effectively. (Photos by Robert Okanda)

  0 0

  Serikali ya Marekani kupitia Taasisi ya kijeshi ya Walter Reed (WRAIR) imesaini upya makubaliano ya ushirikiano na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) siku ya Jumanne, Agosti 29, 2017 katika sherehe ya kusaini tamko la pamoja la ushirikiano katika jitihada za kupambana na VVU/UKIMWI. WRAIR ni kitengo cha kikosi cha jeshi la Marekani kinachojihusisha na tafiti za kitabibu na kimefanya kazi moja kwa moja na JWTZ tangu mwaka 2004 kutekeleza programu za VVU/UKIMWI Tanzania.

  Utiaji saini huo uliofanywa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja  Generali (Dk.) Denis Raphael Janga, unawakilisha dhamira ya pamoja katika upatikanaji endelevu wa huduma za afya na mpango mkakati wa kukabiliana na tishio la VVU/UKIMWI.
  Makubalino ya awali, yaliyosainiwa mwaka Aprili 2011 yanabainisha ushirikiano wa pande hizo mbili katika kupunguza maambukizi mapya na kuboresha matibabu na huduma za kuzuia maambukizi.

  Kupitia ushirikiano huu endelevu wa pande hizi mbili Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) unatoa nafasi kwa majeshi ikiwemo JWTZ kuelewa vizuri tishio la afya, tabia na mazingira hatarishi yanayohusiana na kuenea kwa maambukizi ya VVU.


  “Mafanikio ya ushirikiano wa WRAIR/JWTZ hayapingiki na faida zake ziko wazi.”alisema Kaimu Balozi Patterson. “Kwa pamoja tumehakikisha upatikanaji endelevu wa huduma za tiba kupitia ujenzi wa vituo vipya, ukarabati wa vituo vya zamani, vya matunzo na tiba na kutoa vifaa vya maabara.” 

  Ushirikiano huu wa pande mbili kati ya WRAIR na JWTZ umeundwa kuimarisha na kusaidia utafiti na utekelezaji wa jitihada za matunzo na matibabu ya VVU nchini Tanzania.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Matumizi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang'a , Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri, Samwel Mbuya, pamoja na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.

  MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini Tanzania leo imewapa semina baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alisema semina hiyo ni utaratibu wa TMA kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuwa mabalozi wa zuri wa kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi mazuri ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa wananchi. 

  Alisema wanahabari inabidi wazielewe vizuri, kuzichambua na kuwafikishia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kiusahihi wananchi jambo ambalo litasaidia wananchi na sekta mbalimbali kujipanga kukabiliana na ama athari zitokanazo na utabiri wa hali ya hewa. 

  "...Semina kama hizi kwanza zinasaidia wanahabari kuelewa masuala mbalimbali yatokanayo na taarifa zetu za utabiri, kisha wao kuelimisha jamii zaidi kuhusiana na taarifa zetu kupitia vyombo vyao mbalimbali vya habari. Kundi hili likielewa vizuri nao watakuwa mabalozi wazuri kufikisha ujumbe kupitia kalamu zao," alisema Dk Agnes Kijazi. 

  Aidha pamoja na mafunzo hayo, TMA pia ilipokea mrejesho na ushauri kutoka kwa wanahabari ili kuboresha zaidi namna ya utoaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa umma. Picha ya pamoja ya washiriki wa semina kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa.

older | 1 | .... | 1888 | 1889 | (Page 1890) | 1891 | 1892 | .... | 3278 | newer