Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA CHUO CHA KODI NA UHASIBU

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika mkutano na Menejimenti ya Chuo cha Kodi wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kutembelea Chuo hicho kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu (TIA) cha Jijini Dar es Salaam, Dkt. Joseph Kihanda akisoma taarifa ya utekezaji wa majukumu ya Chuo hicho kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara chuoni hapo.

Vijana kujiandikisha masomo ya Tehama yanayotolewa na Airtel na Atamizi ya DTBi

$
0
0


Airtel kwa kushirikian na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi)  leo imetangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehema yatakayotolewa katika maabara  iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama na kuwaalika wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, wanavyuo na jamii yote kwa ujumla kujiandikisha  katika mafunzo yatakayowapatia ujuzi utakaochochea kuondoa umasikini na kukuza technolojia.

Maabara  ilianzia kama kituo cha kutoa elimu ya Tehama mwezi Julai 2017 kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama yatakayosaidia matumizi ya teknolojia na Tehama katika biashara.  Maabara hii kwa sasa itaanza kufanya kazi kwa kutoa masomo mbalimbali ambayo ni pamoja na  lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”    pamoja na  msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali ,mtandaousalama wa mtandao

Akitangaza program hizo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania , Jackson Mmbando alisema “ Tumeanzisha maabara hii ya kompyuta kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi na waalimu wa shule ya msingi  pamoja na vijana  wanaopenda kujikita kwenye masomo ya sayansi na Tehama kupata ujuzi wakiwa katika umri mdogo. Lengo letu ni kuendelea kuiwezesha sekta ya technolojia na Tehama kukua na kuzalisha vijana ambao wataweza kuvumbua na kutengeneza programu zitakazoleta suluhuhisho kwenye mahitaji ya biashara naustawi wa jamii.  Tunaamini maabara hii  ni jukwaa la kukuza vipaji vya vijana na Airtel inajisikia fahari kuwa sehemu ya kuleta mapinduzi na mabadiliko haya katika jamii na nchi kwa ujumla ikiwa ni mwendelezo wa program ya Airtel Fursa inayoendeshwa na Airtel”.

Mmbando alieleza kuwa maabara hii itatoa mfunzo bure kwa walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kijitonyama ila kwa  kijana yeyote asiyekua mwanafunzi au mwalimu wa shule hii atakayependa kujiandikisha ataruhusiwa kufanya hivyo.
Fomu za kujiandikisha zitapatikana kwa njia ya mtandao kwa gharama ya shilingi 20,000 kupitia www.teknohama.or.tz na  www.airtelfursa.com  au kwa kutembelea maabara  iliyopo katika shule ya msingi kijitonyama kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana. Mafunzo yatatolewa  kwa wiki 4 kuanzia tarehe 4 septemba 2017.

“natoa wito kwa vijana hususani wanafunzi wa shule ya msingi kijitonyama na maeneo ya jirani kutumia fursa hii kujiendeleza zaidi”. Aliongeza Mmbando.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mhandisi George Mulamula alisema “ pamoja na kuwa na wahitimu kutoka katika vyuo mbalimbali  lakini bado Tanzania tuna uhaba wa wataalamu wabunifu wenye ujuzi  wa kutengeneza program u zitakazotatua changamoto za kijamii  za kibiashara na zinazokuza  kipato na kuondoa umasikini”

“Maabara hii  ina malengo mawili: kuwatayarisha vijana wanaotarajiwa kwenda chuo kikuu kuwa na elimu ya kibiashara ya Tehama zaidi ya kuwa na uelewa wa kompyuta na programu za simu. Lakini pili kuwaunganisha na wadau wa kibiashara ili kuwapa mwelekeo utakaowawezesha kutoa suluhisho la kiteknolojia na Tehama zitakazosaidia nchi kufikia malengo yake ya 2015 ya uchumi wa viwanda pindi watakapohitimu shule.

 DTBi inaishukuru sana Airtel na uongozi wa shule ya Msingi Kijitonyama kwa kuungana nasi na kuwa sehemu ya kuleta mapinduzi haya ya Tehama kwa jamii na katika biashara kwa ujumla” alisema Mulamula
Aliongeza kwa kusema huu ni mwanzo tu kwani walimu, vijana na jamiii watapata ujuzi na ni  matumaini yetu programu hii pia itafika maeneo mbalimbali nchini.


DTBi kama msimamizi wa masomo wana timu ya wataalamu ambao wamejitolea kutoa mafunzo kwa vijana na kuleta mabadiliko katika jamii. Tunawakaribisha wale watakaopenda  kushirikiana nasi kujiunga sasa, alimalizia.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akiongea wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi). Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa DTBi.
Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) akiongea wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi). Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya Msingi ya Kijitonyama Mariam Said akionyesha ujuzi wa kutumia kompyuta huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).
Mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya Msingi ya Kijitonyama Karim Ramadhan akionyesha ujuzi wa kutumia kompyuta huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) Mhandisi George Mulamula (kushoto) na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) wakati wa kutangaza kuanzishwa kwa masomo ya Tehama yatakayotolewa katika maabara iliyopo katika shule ya msingi ya Kijitonyama ambayo ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania na Atimizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi).

Kesi ya Aveva, Kaburu yazidi kupigwa kalenda

$
0
0
Kwa mara nyingine tena upelelezi dhidi kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayomkabili Rais wa  Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange Kaburu umedaiwa kuwa bado kukamilika na kwamba kuna nyaraka mbalimbali zimepelekwa kwa mtaalamu wa maandishi.

Wakili wa serikali, Eatazia Wilson amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa, pindi kesi hiyo imekuja kwaajili ya kutajwa na kudai bado wanasubiri ripoti ya polisi.

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Nongwa aliutaka upande wa jamuhuri kujitahidi kuharakisha upelelezi kwasababu washtakiwa wapo ndani na kwamba
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 8 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Aveva na Kaburu  wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha USD 300,000.

NAIBU KATIBU MKUU-BARA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA, LEO

$
0
0
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping (kulia), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo (wapili kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping (kulia), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa KIanali mstaafu Ngemela Lubinga.
 Ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM_Bara Rodrick Mpogo na ujumbe wa Naibu Waziri wa mamambo ya Nje wa CPC, wakishangilia baada ya mazungumzo kumalizika. 
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).

KAMANDA WA KANDA MAALUM JIJINI DAR AHIDI KUPAMBANA NA UHALIFU DAR,ATAKA JIJI LA DAR KUWA MAHALI SALAMA PA KUISHI

WAZIRI MWIGULU KUONGOZA MKUTANO KUJADILI WAKIMBIZI WA BURUNDI KESHO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba kesho ataongoza mkutano wa siku moja utakaozungumzia suala la wakimbizi raia wa Burundi ikiwemo maandalizi ya kuwarejesha kwao wakimbizi raia wa nchi hiyo waliojiandikisha kwa hiari kurejea nyumbani.

Mkutano huo utakaofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam utahudhuriwa na nchi za Tanzania, Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR). 

Mkutano huo unafanyika kwa mujibu wa matakwa ya Sheria za kimataifa zinazohusu wakimbizi ambazo zinazilazimu pande tatu katika suala hilo kukutana na kukubaliana kuhusu namna ya kuwarejesha wakimbizi hao waliohiari kurejea nyumbani.

Katika mnasaba huo, makubaliano ya mkutano huo yataipa fursa kwa upande mmoja Serikali ya Burundi kuingia katika makambi ya wakimbizi kuhamasisha kurejea nyumbani na kwa upande wa pili yatawapa fursa wakimbizi kupitia wawakilishi wao kutembelea Burundi kuangalia hali halisi ili kujiridhisha kabla ya kurudi nchini humo.

Baada ya hatua hizo kukamilika, imeelezwa kuwa Jumuiya ya Kimataifa itatekeleza jukumu lake la kuwarudisha wakimbizi hao nyumbani kwa ‘heshima’ ambapo chini ya utaratibu huo wa ‘heshima’, Jumuiya hiyo itapaswa kuwawezesha wakimbizi hao kuanza maisha mara wanaporejea ikiwemo huduma za chakula na makaazi kwa wale ambao makaazi yao yatakuwa yameathirika.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba 

RAIS DKT MAGUFULI ASITISHA UBOMOAJI WA NYUMBA 300 TUANGOMA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli amesitisha zoezi la bomoabomoa la nyumba 300  zilizojengwa katika bonde la Tuangoma wilayani Temeke jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa agizo la kusitisha ubomoaji wa nyumba zilizopo katika mtaa wa masaki kata ya tuangoma  mchana huu ikiwa ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

RC Makonda amesema kuwa zoezi la bomoa bomoa linapaswa kufanywa kwa kufuata taratibu za Ardhi na sheria za nchi,amesema na kuongeza kuwa atamwomba Rais Dkt Magufuli na Wizara ya ardhi kuweka Afisa ardhi katika kila kata ya mkoa waDar es Salaam ili kuepusha migogoro ya ardhi inayosabisha na viongoz wa mitaa. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Tuangoma wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam  na kusitisha bomoa bomoa iliyokuwa ikiendelea katika eneo hilo. Pia  amewaomba kujiepusha na kujenga nyumba za kuishi katika maeneo hatarishi.
Baadhi ya wananchi wa Tuangoma Wilayani Temeke wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam leo (hayupo pichani),Mhe. Paul Makonda  mara baada ya kutembelea eneo lao na kuzungumza nao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa amezungukwa na wananchi mbalimbali wa eneo la Tuangoma,akitembelea maeneo ambayo nyumba zake zilikuwa zikitarajiwa kukumbwa na zoezi  la bomoa bomoa.
Baadhi ya Nyumba ambazo zilitakiwa kubomolewa,ambapo kwa sasa hazitabolewa kufuatia agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli kusitisha zoezi hilo na kuwataka wahusika wafuate taratibu na sheria za Ardhi .

MIVARF yawezesha Halmashauri 73 kupunguza umasikini wa kipato

$
0
0
Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji thamani na Huduma za Kifedha Vijijini(MIVARF), imefanikiwa kupunguza umasikini wa kipato na kuimarisha uhakika wa chakula katika Halmashauri 73 zinazotekeleza program hiyo kwa Tanzania Bara na Visiwani.

Akiongea wakati wa Mkutano wa wadau wa MIVARF wa siku mbili tarehe 29 hadi 30, Agosti, 2017  mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Idara ya uratibu wa shughuli za serikali Ofisi ya Wazir Mkuu, Obey Assery alifafanua kuwa lengo la Program hiyo inalenga kuongeza uzalishaji na tija kwa walengwa.

“Program imelenga kuwajengea uwezo wazalishaji ambao huwa katika vikundi kwa kuvifiki vikundi 2,331 vyenye walengwa 81,677. Kimsingi Programu imelenga kumuwezesha mkulima aweze kufanya  kilimo cha kibiashara” alisema Assery.

Naye Mratibu wa Program Kitaifa, Walter Swai alibainisha kuwa Program imelenga kuwajengea uwezo walengwa kuyafikia masoko ya uhakika ili waweze kupunguza umasikini wa kipato.

“Programu imelenga kuboresha 1,000km za  barabara hadi sasa 9991.8km zimeshakamilika sawa na asilimia 92. Lakini pia kwa upande wa miundo mbinu ya masoko tunajenga maghala, hadi sasa kati ya maghala 29 yaliyo kwenye malengo tayari tumekamilisha maghala 24 sawa na asilimia 83 ” alisistiza Swai.

Swai aliongeza kuwa Program hiyo imepanga kukarabati maghala 6 ambapo tayari yote yamekamilika, pia tumelenga  kujenga masoko 16 ambapo hadi sasa masoko 7 yamekamilika ambayo ni asilimia 44.

MIVARF;  ni Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini  iliyobuniwa  na serikali ya Tanzania  kwa  kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za serkali Obey Assery akisistiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa MIVARF Agosti 30, Agosti, 2017  mjini Dodoma.
 Wataalamu kutoka Program ya MIVARF wakifuatilia majadiliano ya wadau wa Program hiyo wakati wa mkutano wa wadau wa MIVARF Agosti 30 Mjini Dodoma.
Baadhi ya wadau wa MIVARF wakifuatilia mkutano wa wadau wa MIVARF unaofanyika mjini Dodoma Agost, 2017.

SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA MICHEZO KATIKA MASHINDANO MBALIMBALI.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imejipanga katika masuala ya michezo  kutoa nguvu pamoja na kuenzi michezo ya shule za misingi na Sekondari ili kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ya Kikanda na Dunia na wachezaji kurudi medali za dhahabu.

 Hayo ameyasema leo Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati akipokea bendera ya Taifa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo ambao walishiriki mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) hivi karibuni, amesema wanafunzi wameonesha vipaji na kuweza kushika na nafasi ya tatu katika mashindano hayo.

Amesema kuwa shule zilizoshiriki zimeweza kutangaza Tanzania hivyo katika mashindano yajayo nguvu itaongezeka  kwa sekondari nyingi kushiriki na kasha kuweza kupata wachezaji mbalimbali ikiwemo timu ya taifa pamoja na riadha.

Dk. Mwakyembe amesema kuwa katika Wizara hiyo atahakikisha wanafnaya vizuri katika michezo kwa kuweza kupata ushindi  ikiwa kwa vilabu vyote vya michezo kujipanga.
Amesema katika michezo hakuna uchawi kinachohitajika ni juhudi na maarifa kwa wachezaji wanavyoshiriki mashindano yeyote ya ndani na ya nje ya nchi.

Aidha amesema wanafunzi walioshiriki na kushika nafasi ya tatu waongeze juhudi katika mashindano yajayo waweze kuwa washindi wa kwanza katika mashindano ya (FEASSSA).
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akimvisha medali mwanafunzi wa Shule ya  Sekondari Makongo, Winfrida Makenji aliyepata medali nne za mshindi wa tatu katika mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) leo jijini Dar es Salaam.

 Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza baada ya kupokea Bendera kwa wanafunzi wa  Shule ya Makongo walioshiriki mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akipokea bendera kwa wanafunzi wa sekondari Makongo walioshiriki mashindao ya Shule za Sekondari za Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Uganda (FEASSSA) leo jijini Dar es Salaam.

WADAU WA MAJI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA MAJI KWA WANANCHI WA DAR.

$
0
0
WADAU wa maji na Mazingira washauriwa kushirikiana ili kukidhi mahitaji ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam pia washauriwa kutoa namba maalumu ya simu kwaajili ya wananchi waonapo tatizo la maji au maji kutiririka katika maeneo mbalimbali ili kuondoa upotevu wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam.

Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema wakati akizungumza na wadau wa maji pamoja na wadau wa Mazingira jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Wadau wamaji wanatakiwa kushirikiana na ili kupunguza upotevu wa maji kutokana na ubovu wa miundo mbinu ya maji.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi,  usambazaji wa maji

Haruni Josef Kwa upande wake DAWASCO wamewaomba wadau wa maji ili kuendeleza na kukuza maendeleo ya kwaajili ya kujenga mtandao wa maji kwaajili ya kuyasafirisha ili yamfikie kila mwananchi wa jiji la Dar es Salaam.

Wadau waliokutana leo ni Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), wizara ya Afya, DAWASCO,DAWASA, WATERAID na wadau wa mazingira kwa pamoja wakiwa na kauli mbiu ya maji ni uhai na usafi ni utu.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na wadau wa maji safi pamoja na wadau wa maji taka ili kutatua changamoto za maji katika jiji la Dar es Salaam.Pia ameshuhudia kusaini makubaliano kati Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Taasisi ya Borda ya hapa nchini.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akishuhudia taasisi ya Borda na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya wadau ya maji wa maji safi na wazingira walipokutana leo leo kufanya mazungumzo ya wadau wa maji pamoja na wadau wa mazingira.
Wawakilishi wa Kampuni ya Jamka Enterprise Company wakipokea hundi ya shilingi milioni Tano ambazo wamekopeshwa na  Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) leo mara baada ya kikao cha Wadau wa Maji na Mazingira kufunguliwa jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kuzungumza masuala ya maji na mazingira. 

Serikali Yaanza kukabidhi Leseni kwa Kwa Machapisho.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni ya usajili wa Gazeti la HabariLeo mwakilishi wa gazeti hilo mhariri wa gazeti hilo Bw. Amir Mhando leo Jijini Dar es Salaam. Leseni hiyo imetolewa kufuatia kuanza kwa matumizi ya sheria mpya ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
 
Na. Neema Mathias na Paschal Dotto- MAELEZO.
Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) imeanza rasmi utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari kwa kutoa leseni kwa vyombo vya machapisho yakiwemo Magazeti na Majarida.  

Akizungumza katika makabidhiano ya leseni hizo Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema  utoaji wa leseni ni utekelezaji wa agizo rasmi lililotolewa Agosti 23, 2017 lililowataka wamiliki wote wa machapisho kujisajili upya na kupewa leseni kwa lengo la kuifanya tasnia ya Habari kuwa taaluma rasmi kama zingine.

“Leseni hizo zimeanza kutolewa rasmi Agosti 23 na zoezi hilo litaendelea hadi Oktoba 15, 2017 na baada ya hapo wale amabo watachapisha magazeti  na majarida bila kuzingatia Sheria hiyo watakuwa wametenda kosa la jinai”, alisema Dkt. Abasi.

Katika zoezi hilo Dkt. Abbasi alitoa leseni kwa vyombo vinne ambavyo ni Jarida la Nchi Yetu linalomilikiwa na Idara ya Habari MAELEZO, gazeti la Daily News, Habari Leo pamoja na Spoti Leo ambayo ni magazeti ya Serikali.

Dkt. Abbasi ametoa wito kwa vyombo vingine vya habari ambavyo bado havijaanza taratibu za upataji wa leseni visisubiri hadi dakika za mwisho za mchakato huo ili kuepuka msongamano na usumbufu usio wa lazima.

“Nitumie fursa hii kuwaalika ambao hawajapata leseni wafanye haraka, Tanzania Standard Newspaper (TSN) walitimiza masharti ndani ya siku tatu ndio maana leo wamepata leseni hizo, hakuna urasimu wala nia mbaya ya kufungia baadhi ya machapisho kama wengi wanavyodai bali ni katika kutekeleza matakwa ya Sheria”, alisisitiza Dkt. Abbasi.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa TSN Dkt. Jim Yonazi ameviasa Vyombo vingine vya Habari kutekeleza agizo hilo ili kupata uhuru mpana katika uwajibikaji pamoja na kuwa mfano wa kutii Sheria bila shuruti ili taaluma ya habari iendelee kuheshimika kwa jamii.

“Ukifanya kazi kihalali unakuwa na uhuru wa kufanya kazi vizuri, ubunifu unaongezeka na unafanya biashara bila wasiwasi”, alisisitiza Dkt.Yonazi.

WAKAZI WA MBEYA WAASWA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.

$
0
0

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

Aidha Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na matukio makubwa ya uhalifu pamoja na wahalifu. Jitihada zinaendelea kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha mkoa wetu unakua mahala salama. Hata hivyo kumekuwa na tukio moja la unyang’anyi wa kutumia silaha wilaya ya Chunya kama ifuatavyo :-

Mnamo tarehe 29.08.2017 majira ya saa 06:00hrs katika kitongoji cha Logia, kijiji na kata ya Upendo, tarafa ya Kiwanja wilaya ya Chunya, mkoa wa Mbeya, dereva HERI ELIA RUBIENO [32], mkazi wa Ilemi – Mbeya akiendesha gari T.767 DDN aina ya Isuzu basi la abiria liitwalo SAFINA mali ya ISAYA SAMWEL MTITU, mkazi wa Njombe ikitokea kijiji cha Mamba kwenda Mbeya mjini njiani ilizuiwa na watu wapatao sita ambao waliweka magogo njiani wakiwa na silaha bunduki moja idhaniwayo kuwa ni shortgun na silaha nyingine za jadi [panga, rungu, na shoka]

Katika tukio hilo abiria waliporwa simu aina mbalimbali zenye thamani ya Tshs 410,000/= pamoja na pesa taslimu Tshs 2,771,000/=. Aidha wakati wa tukio abiria kadhaa walipata michubuko na mikwaruzo na walipatiwa matibabu katika zahanati ya Makongolosi na kuruhusiwa. Watu hao mara baada ya tukio walifyatua hewani  risasi mbili na kutokomea kusikojulikana kwa kutumia usafiri wa pikipiki.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata majambazi watatu ambao pia walitambuliwa na wahanga pamoja na pikipiki moja MC 388 BFZ aina ya Kinglion. Watuhumiwa hao ni

i.    JUAKALI MBALAMWEZI [65], mkazi wa Sumbawanga
ii.    GASPAR MAHINI [22], mkazi wa Sumbawanga
iii.    PETRO JUMA [21], mkazi wa kijiji cha Mamba [A].

Ufuatiliaji zaidi kuhusiana na tukio hili bado unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa wengine pamoja na silaha.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu  Kamishna wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA  anatoa  wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria, badala yake wahakikishe wanawafikisha katika mamlaka husika watu wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali ili sheria ichukue mkondo wake.

 Aidha Kamanda MPINGA  anatoa rai kwa yeyote mwenye taarifa juu ya  watu wengine waliohusika katika tukio hilo  azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake vinginevyo wajisalimishe mara moja. Pia anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kuwa na tamaa ya kujipatia utajiri wa haraka kwa kutumia njia mkato zisizo halali, badala yake wafanye kazi halalli ili kupata kipato halali.

Pia  Kamanda MPINGA anawatakia Heri ya sikukuu ya EID EL HAJI wakazi wa Mkoa wa Mbeya washerehekee kwa amani na utulivu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi. Watumiaji wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara wazingatie  Sheria za usalama barabarani.

[MOHAMMED R. MPINGA - DCP]
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

PROF. JANABI AIELEZA MAHAKAMA KUWA MANJI ANA VYUMA KWENYE MOYO

$
0
0
Na Karama Kenyunko,  blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeelezwa kuwa, mfanyabiashara Yusuf Manji amewekewa vyuma kwenye moyo wake na pia  anasumbuliwa na maumivu makali na tatizo la kukosa usingizi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amesema hayo leo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mshitakiwa Yusuf Manji amewekewa vyuma kwenye moyo wake na kwamba anasumbuliwa maumivu makali na kukosa usingizi.

Profesa Janabi amesema hayo wakati akitoa ushahidi wake kama shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi kwenye kesi matumizi ya dawa za kulevya inayomkabikli Manji.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula, Profesa Janabi amdai, Februari na Julai mwaka huu, mshitakiwa Manji  alifikishwa katika taasisi hiyo kati kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo, ambapo kwa mara ya kwanza kulazwa ilikuwa Februari.

Amedai kuwa, mara ya kwanza Manji kupelekwa JKCI alipelekwa  kama mgonjwa wa nje,  ambapo alitoa historia ya matatizo yake na kupatiwa matibabu, lakini baadae alienda tena kuchunguzwa ndipo ikagundulika kuwa moyo wake ulikuwa na tundu hivyo aliwekewa vyuma kwa ajili ya kusaidia msukumo wa damu lakini baadae Julai mwaka huu alifika tena hospitalini hapo akilalamikia maumivu ya moyo upande wa kushoto ambapo walipochunguza waligundua kuwa vyuma vilivyowekwa kwenye moyo wake vinafanya kazi vizuri na kumpatia dawa za maumivu.

Shahidi huyo alidai kuwa, Manji aliwaeleza kuwa kabla ya kwenda JKCI alikuwa anapatiwa matibabu nchini Marekani , lakini pamoja na tiba mbalimbali walimpatia tena dawa kutoka makundi matatu ambazo hazikumbuki na pia kwa tatizo la kutolala vizuri hatukumtibu sisi bali wakati anachukuliwa historia yake alieleza kuwa alipatiwa dawa za kupunguza maumivu na sindano.

Aidha shahidi huyo amedai, mtu yoyote anayewekewa vyuma akitumia vitu vyovyote kama vile sigara, vyakula vya mafuta au dawa kama Heroine anaweza kuathiri utendaji kazi wa vyuma hivyo  na kwamba kabla ya kuwekewa mgonjwa hupewa maelekezo nini atumie  na vitu gani asitumie  lakini maamuzi ya kutumia dawa za kulevya si ya daktari.

Alipoulizwa juu ya madhara anayoweza kupata mgonjwa wa moyo akitumia dawa za kulevya alisema, Vyuma vinavyowekwa kwenye moyo husaidia kuzibua mishipa ili damu izunguke mwili mzima na kuna masharti kwa mtu anayewekewa vyuma. Athari moja wapo ni kujirudia kwa tatizo na kuziba kwa mishipa.

Kesi hiyo itaendelea kesho.

WAJUMBE WA KAMATI YA ARDHI NA MAWASILIANO WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WASIFU KAZI NZURI INAYOFANYWA NA TMA KATIKA KUTOA HUDUMA ZA HALI YA HEWA ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi na Mawasiliano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma (mwenye koti jeusi) akielezea jambo wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipokutana na mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri-TMA na menejiment ya TMA (hawapo pichani), kwenyea ukumbi wa mikutano wa TMA, Ubungo Plaza.

NA MONICA MUTONI

Siku ya Ijumaa, tarehe 25/08/2017, Kamati ya Ardhi na Mawasiliano wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ilitembelea Makao Makuu ya Ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yaliyopo jengo la Ubungo Plaza Dar es salaam ili kuona na kupata taarifa mbali mbali za taasisi hiyo.

Taarifa ya utendaji ya TMA iliwasilishwa na ndugu Selemani Selemani (Mchumi) pamoja na mambo mengine aliwafahamisha wajumbe wa kamati hiyo kuwa Mamlaka imepokea ‘Certificate of Appreciation’ toka Idara ya kukabililiana kamisheni ya kukaliana na maafa na Mamlaka ya usafiri wa majini (ZMA) kwa kazi nzuri inayofanywa ya kutoa huduma za hali ya hewa katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe, Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Ardhi na Mawasiliano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma alisifu kazi nzuri inayofanywa na mamlaka katika kutoa huduma za hali ya hewa Zanzibar. Aliielezea menejiment ya TMA kuwa, huduma za hali ya hewa nchini zinazidi kuimarika hususan kwenye usahihi wa taarifa zinazotolewa kama vile utabiri wa kila siku na tahadhari, hivyo kuongeza imani kwa wananchi katika ufuatiliaji wa taarifa za hali ya hewa ukilinganisha na hapo awali ambapo jamii ilikuwa na hulka ya kupuuzia taarifa hizo.

Mhe. Juma alifahamisha mchango wa TMA unatambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) akitolea mfano wa pongezi zilizotolewa kwa Mamlaka na Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Balozi Seif Ali Iddi kwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Kwa upande mwengine, Mwenyekii wa Bodi ya Ushauri ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi aliwashukuru wajumbe hao kwa pongezi zilizotolewa na kuahidi kuisaidia Mamlaka kufikia malengo ya juu zaidi katika utoaji huduma kwa kuboresha miundo mbinu. Aidha aliwaeleza wajumbe hivi karibuni alikuwa na ziara ya kutembelea vituo vya hali ya hewa vya unguja na pemba ili kujionea hali halisi, hivyo wananchi wategemee huduma bora zaidi kwa kuwa lengo la Mamlaka ni kuongeza na kuviboresha vituo vyake na kuongeza usahihi wa takwimu za hali ya hewa zinazokusanywa.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi aliwashukuru wajumbe na kueleza utendaji kazi wa Mamlaka kwa kuzingatia weledi na ushirikiano uliopo baina ya wafanyakazi wenyewe na wadau wa hali ya hewa, Aidha, Dkt. Kijazi alijivunia uwepo wa wataalam wa sayansi ya hali ya hewa wenye sifa za kitaifa na kimataifa ambao mchango wao mkubwa umeonekana katika kuongeza usahihi wa taarifa zitolewazo.

ALICHOKIFANYA KIPANYA KUHUSIANA NA VODACOM RED RLX

$
0
0
Kipanya rasmi sasa amejiunga na Vodacom RED na atakuwa anakuletea mfululizo wa maisha anayoishi sasa baada ya kujiunga na huduma hii mpya inayotolewa na kampuni ya simu nchini Vodacom Tanzania. Hatujui atatuletea nini lakini tunaimani atawapa wafuasi wake faida anazozipata akiwa na Red RLX, endelea kufuatilia hapa kuona nini atatuletea.

SERIKALI KUUZA MALI ZA WADAIWA SUGU WA KODI YA ARDHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabulla ameziagiza halmashauri zote kuwafikisha mahakani na kuuza mali zao wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi wenye madeni ya muda mrefu. Dkt. Mabulla ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya kukagua mifumo ya makusanyo ya kodi ya ardhi mkoani Geita mara baada ya kukuta majina 100 ya wadaiwa wa kodi ya ardhi ambao hawajalipa kwa zaidi ya miaka 10.

Mhe. Naibu Waziri wa Ardhi alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita kuhakikisha wadaiwa hao wa muda mrefu wanaandikiwa notisi ya muda wa siku 14 na wasipolipa ndani ya muda huo wafikishwe mahakamani bila kuchelewa na kama wasipolipa basi mali zao zipigwe mnada. Mara baada ya kubaini hayo Mhe. Mabulla amefanya upekuzi wa nyaraka za umiliki wa ardhi katika masijala ya ardhi ya Halmashauri ya mji wa Geita na kugundua uhifadhi mbovu wa hati na ucheleweshwaji utoaji hati za wamiliki kwa muda mrefu.

Naibu waziri alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita kutembelea mara kwa mara katika ofisi na masijala za ardhi ili kuhakikisha maafisa wa idara ya ardhi wanatoa hati kwa wakati na kwa mpangilio mzuri bila kuleta migogoro. Aidha, Naibu Waziri huyo alitembelea eneo lenye viwanja vilivyowekwa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita ambavyo vimepangwa kujengwa ofisi za serikali, shule, hospitali, makazi, maeneo ya kuzikia, na huduma nyingine za kijamii.

Naibu Waziri alimtaka mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale kihakikisha mji huo unapangwa vizuri na kuwekwa miundombinu ya barabara, maji safi na taka na umeme ili kuepusha migogoro ya ardhi ambayo mara nyingi huibuka kutokana na wilaya kutokuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi ya muda mrefu. Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabulla ametembelea eneo la Bombambili mkoani Geita lililojengwa nyumba 48 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo nyumba 14 tayari zimenunuliwa na Halmashauri ya mji wa Geita.

Mhe. Mabulla alizitaka halmashauri nyingine nchini kuiga mfano wa halmashauri ya mji wa Geita kwa kuwashirikisha NHC katika kujenga nyumba bora badala ya kutumia wakandarasi wa nje wakati Shirika la Nyumba la Taifa lipo na linajenga nzuri na kwa gharama nafuu. Naye Meneja wa NHC Mikoa ya Mwanza, Geita na Simiyu Eng. Benedict Kilimba alimeishukuru Halmashauri ya mji wa Geita kwa kuwa wakwanza kununua nyumba hizo 14 katika hatua ya awali.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla anaendelea na ziara yake ya mikoa ya kanda ya ziwa ambapo anataria kufanya ziara Mkoa wa Shinyanga hasa katika wilaya ya Kahama na Shinyanga Mjini.

LIBYA YAIPATIA ZANZIBAR MSAADA WA MATREKTA

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid (kulia) akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania, Bw. Saleh Kusa Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam leo. Wawili hao walijadili namna ya kukamilisha taratibu za kukabidhi msaada wa matrekta 10 yenye thamani ya zaidi ya milioni 250 za Tanzania kutoka Libya kwa ajili ya Serikali ya Zanzibar. Matrekta hayo yashawasili jijini Dar es Salaam na wiki ijayo yanatarajiwa kukabidhiwa Serikali ya Zanzibar. Aidha, Kaimu Balozi alisema kuwa Libya imetenga Dola Bilioni 20 kupitia Mfuko wa "Libyan-Africa Investment Portfolio" kwa ajili ya nchi za Afrika. Aliahidi kuwa atahakikisha kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zinaletwa Tanzania. 
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Bw. Suleiman Saleh na Afisa Dawati wa Libya, Bw. Nicolas wakifuatilia mazungumzo.
Kulia ni Mkalimani wa Kaimu Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Serikali ya Zanzibar wakifuatilia mazungumzo hayo 
Nazungumzo yanaendelea.
Picha ya pamoja

Waziri Mbarawa aridhishwana kasi ya ujenzi TBIII

$
0
0
Mkurugenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Wolfgang Marschick (kushoto) akiwa na Mhe. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akikagua mradi wa jengo hilo.

Na Neema Harrison, TUDARCO

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambapo sasa utakamilika Oktoba 2018. Mhe. Prof. Mbarawa aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya mradi huo ulianza 2013, na sasa kuridhishwa na hatua waliyofikia. Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo, Prof. Waziri Prof. Mbarawa amesema kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 64, na hatua iliyobaki ni ujenzi wa wa mifumo ya ndani ya jengo.

“Sote tumekuwa mashahidi nimekuwa nuikitembelea mara kwa mara ujenzi wa jengo hili na ninaridhika kwa kasi ya ujenzi wake, ambapo sasa tumefikia kwenye hatua nzuri na vitu vilivyobaki sio vikubwa kama ilivyokuwa wakati wanaanza, hivyo ni matumaini yangu hadi Oktoba mwakani (2018) jengo lote litakuwa limekamilika na serikali kukabidhiwa,” amesema Mhe. Prof. Mbarawa. Hatahivyo, Prof. Mbarawa amesema serikali inatarajia kupata watalii wengi na serikali itapata mapato kupitia kodi na tozo za abiria wanaosafiri kutumia kiwanja hiki, pia wapangaji wanaotoa huduma mbalimbali yakiwemo maduka na usafiri wa magari.

Amesema serikali itaendelea kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo linalosimamiwa na mkandarasi BAM International ya Uholanzi, ambapo pia likikamilika litatoa ajira kwa Watanzania wengi.

“BAM wamekuwa wakifanya kazi nzuri nawapongeza sana na tunatarajia hadi kukamilika tutapata mradi bora utakaoliingizia taifa faida kubwa kutokana na kodi na tozo mbalimbali,” amesema Prof. Mbarawa. Amesema jengo hilo likikamilika linatarajia kuchukua abiria milioni sita (6) kwa mwaka, na kupunguza msongamo ulipo katika jengo la pili la abiria (JNIA-TBII)
Mhe. Prof. Makame Mbarawa mwenye miwani mkononi, akiendelea leo na ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kushoto ni Mkurugenzi wa mradi huo Bw. Wolfgang Marschick na kulia ni Meneja wa Mradi Bw. Ray Blumrida.
Meneja wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Ray Blumrida (wa pili kulia) akielezea ujenzi wa ngazi zinazotumia umeme (escalator) kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Prof. Makame Mbarawa (katikati), akimsikiliza Meneja wa mradi wa jenzi la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Ray Blumrida akielezea ujenzi wa madaraja (bridges) ya kupitia abiria wanaowasili na wanaoondoka.
Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akifurahia jambo na Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi wa Viwanja vya Ndege cha Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Emmanuel Raphael wakati wakitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

MAKALA MICHEZO: BUSWITA NA OBI KOSA MOJA ADHABU TOFAUTI

$
0
0
Na Honorius Mpangala 

Ilikuwa ni mwaka 2006 klabu ya Manchester United ilipofanya ujanja kumsainisha John Michael Nchekwube Obinna. Obi kama anavyojulikana na wengi akiwa klabu ya FK Lyn ya Norway alijikuta akiingia tamaa ya kuvaa jezi ya United na kuingia mkataba wa awali bila wakala wake na klabu yake kujua. 

Akili aliyoitumia Obi ni ya wachezaji wetu wa kiafrika ambao wana teswa na ile methali "tamaa mbele mauti nyuma".Akiwa mzaliwa wa mji wa Jos katikati ya Nigeria alianza safari yake ya soka katika klabu ya hapo nyumbani kwao ya Plateau United.

Akiwa Norway Obi alipotea ghafla katika klabu yake na kusemekana kuwa ametekwa. Kumbe iligundulika alikuwa na Watu wa Manchester United ndipo alifanya 'uswahili' wa kusaini kandarasi ya kuitumikia United. Baadae picha zikasambaa kwenye mitandao akiwa na jezi ya United.

Kwa mapungufu yaliyofanywa na United iliwafanya Chelsea,kupita njia halali ya kumsajili. Uhalali na uwazi walioutumia Chelsea ukaonekana kuwa Manchester walimlazimisha Obi na kutokana na ukubwa wa klabu yao alijikuta anashindwa kukataa kuichezea klabu yao.

Baada ya sakata kufikishwa mbele ya Uefa maamuzi yanatolewa kuwa Manchester United walimsajili Obi kwa njia zisizo sahihi. Hawakumtumia wakala wake walimteka kijana wa watu lakini katika mazingira ambayo hata klabu yake inasemekana walijua ila hawakutaka kuwa wawazi. Maamuzi yalimnufaisha Chelsea na hatimaye Obi mwenyewe kwa kinywa chake akasema nataka kucheza Chelsea na sio Manchester United. Akakazia kuwa huko nilisaini kwa kushinikizwa.

Hatimaye Obi akaanza kuitumikia Chelsea katika makubaliano ambayo ilitakiwa klabu ya Chelsea ilipe fidia kwa Manchester united. Fidia hiyo ni kutokana na mkataba wa awali ambao Mchezaji aliusaini kuitumikia United.

Katika sula hilo hilo la Obi lilifanana na kile walichokifanya Klabu ya Simba kwa mchezaji wa Yanga Pius Buswita. Akiwa ni kijana mwenye umri wa Miaka 21 tu subira ambayo ingempa heri anaiweka kando. Anaamua kutumia tamaa mbele ambayo inampa majibu ya mauti ya Soka lake. 

Alichokifanya Buswita sio kigeni kwa wanasoka wa Afrika.Ziko rejea nyingi ambazo unaweza kuzitumia katika kutatua au kulinganisha matukio kwa wachezaji wa kiafrika inapokuja suala la Usajili.

Wakati FIFA wakitoa Adhabu kwa Didier Kavumbagu ya kutocheza soka miezi sita baada ya kusaini Klabu mbili tofauti kule Vietnam. Sisi hapa Tanzania shirikisho lilimpa adhabu ya kosa la kuwa na mkataba na Prisons na kusaini Mbeya city Mchezaji Mohammed Mkopi.Adhabu ya Mkopi ilikuwa ni mwaka mmoja.

Wakati klabu ya Simba inampa 'kishika uchumba' Mbuyu Twite pale Kigali hawakufanya mazungumzo na klabu yake. Walichokifanya Simba ni kumwendea moja kwa moja Mbuyu.Wenzao Yanga wakaenda mbali zaidi Baada ya kugundua Mchezaji huyo alikuwa kwa mkopo katika klabu ya APR lakini ni Mali ya Fc Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika jiji la Lubumbashi.

Sakata la Mbuyu likamalizwa kwa Shirikisho kuwataka Yanga kuwalipa Simba Fidia ya Gharama walizoingia kwa Mbuyu na ndio uuwangana. Uungwana huo ndio waliotumia Uefa kumtambua Obi ni wa Chelsea na kuwataka walipe fidia ya gharama walizo tumia United kwa Obi.

Ikiwa ligi kuu Tanzania haijaanza Shirikisho lilitoa muda wa kupitia pingamizi mbalimbali. Pingamizi zilihusu wachezaji katika soko la usajili. Hatimaye TFF walipokea pingamizi nyingi zilizohusu klabu nyingi zile za madaraja ya chini na ligi kuu na pia hata vituo vya kulelea wachezaji.

Katika pingamizi zilizopelekwa TFF hakukuwa na pingamizi lililomhusu Pius Charles Buswita aliyesajiliwa na Yanga akitokea Mbao Fc .Baada ya siku kadhaa kupita na kufanyika kwa mapitio ya pingamizi kabla ligi haijaanza TFF wanatangaza kufungiwa kwa Buswita mwaka mmoja.

Wakiwa wanatekeleza moja ya vifungu vilivyowekwa na bodi ya ligi wako sahihi Kwa Adhabu ya mchezaji mwenye mikataba miwili timu tofauti. Lakini suala hilo linachukua sura tofauti na lile la Mohammed Mkopi aliyekuwa akiitumikia Prisons na mkataba ukiwa umebaki mwaka mmoja akaamua kusaini Mbeya city. Utofauti ninao usema hapa ni kwamba Buwita hakuwa mchezaji wa Simba kama ilivyokuwa Kwa Obi hakuwa mchezaji wa Manchester united ila alishikishwa kishika uchumba cha mkataba wa awali. Wakati simba wakifanya hayo Buswita alikuwa na mkataba na Mbao. Ukianza kufuata mnyoyoro wa makosa unagundua Simba walifanya mazungumzo na Buswita kimakosa. Yanga wao wakafanya kama Chelsea ikawa kama walivyofanya Kwa Mbuyu wakaenda Kufanya mazungumzo na Mbao wenye mkataba na mchezaji. 

Mbao wanamruhusu Buswita kusajiliwa Yanga halafu Simba wanaweka mezani mkataba wao wa kishika uchumba. Maamuzi yaliyofanyika Kwa Mbuyu ndiyo ingekuwa halali zaidi kwasababu waliotoa ruhusa ya kuuza ni klabu yake ya awali yaani Mbao na mkataba wa Mbao na Buswita ulikuwa TFF. Sasa anapoibuka mwingine kusema Nina mkataba nae unajiuliza uliingia nae mkataba lini na ulipata idhini ya klabu yake maana bado ana mkataba na klabu. Jibu linabaki kuelea kama ngalawa ya Mzee chipumu Nyasa.

Mbao wangeweza kusema tumemuuza Pius kwenda Yanga na kama ana meneja naye angesema nilishirikiana na klabu kumuuza Buswita kwenda Yanga. Hili linakuwa jibu tosha Kwa makubaliano ya Yanga na Mbao kuwekwa bayana. Halafu bodi inaanza kupitia makubaliano ambayo Simba wanasema waliingia na Buswita. Baada ya kubaini kuwa Mchezaji alishikishwa kishika uchumba pasipo klabu yake ya awali kutokujua na ilihali wana mkataba naye,hii ingeliweka jambo katila sura ya suluhu kati ya Simba na Mbao.

Iko wazi mchezaji anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote kama amebakisha mkataba wa miezi Sita na klabu anayoitumikia.Kitendo cha Simba kufanya mazungumzo na Buswita kina rejesha mambo yaleyale waliyowahi kuyafanya Kwa Mbuyu ilihali mchezaji alikuwa na mkataba na Fc Lupopo. 


Kosa la Mkopi linaweza kutofautina na Buswita kwasababu Mkopi alikuwa na mkataba na Prisons. Wakati Buswita hakuwa na mkataba wowote unaomtambulisha kuwa ni mchezaji wa Simba pale Tff. Ifahamike kuwa mikataba yote ya wachezaji inakuwa sehemu mbili klabuni kwake na Tff. Sasa ukifika ofisi za shirikisho wao wanaweza kuwa rahisi kukupa mkataba wa Buswita na mbao na sio Mchezaji huyo na simba.


Mahakama ikiwa ni mhimili katika dola hupenda kutoa maamuzi Kwa kutumia rejea za Mashauri mbalimbali toka maeneo mbalimbali. Katika soka yapo mambo ambayo tunayaiga kutoka maeneo mbalimbali na yanatupa picha nzuri katika kuendesha soka letu. Utofauti wa kimaamuzi katika ligi moja na nyingine hutokea katika kanuni za ligi husika japo sheria za mpira zinabaki kuwa kama zilivyo.

Katika ligi hiyohiyo kanuni hizohizo ziliamua fidia kwa Mrisho Ngassa na Mbuyu Twite kama ilivyokuwa Kwa Obi na Chelsea yake.Fidia pia iliwahi kuwakuta Chelsea Kwa Birmingham city Kwa mchezaji Danny Sturridge ambaye Chelsea walilazimika kulipa baada ya kumchukua mchezaji huyo akiwa kinda toka Manchester city ilihali mmiliki halali alikuwa ni Birmingham city.

Fidia sio jambo geni hivyo Buswita angeweza kujitetea mbele ya kamati na kutoa maamuzi ya fidia. Lakini Kwa bahati mbaya kwake hakubahatika kuitwa mbele ya kamati na kuhojiwa.

Kanuni zetu ndio mwongozo wa maamuzi yetu Kwa kufuata misingi na taratibu za utoaji maamuzi baada ya kusikiliza pande mbili na kutazama makosa yaliko na kutoa adhabu stahiki.

0628449904

UZINDUZI RASMI WA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TAMWA

$
0
0
Na Edda Sanga, Mkurugenzi Mtendaji TAMWA
Wanaharakati wenzangu, karibuni TAMWA, mahali adhimu ambapo tumeamua kuzindulia maadhimisho ya miaka 30 ya Chama Cha Wandishi Wa Habari Wanawake Tanzania.

Jina la TAMWA si geni masikioni mwa Watanzania walio wengi, ikizingatiwa hiki ni chama kikongwe cha wanahabari Tanzania ambacho mithili ya chombo baharini, kimehimili mawimbi, makubwa na madogo, mitikisiko na misukosuko ya hapa na pale, na bado kikaweza kuelea katika bahari tulivu. Itoshe kusema, tumetoka mbali.

Mimi mbele yenu ni mmoja wa waasisi wa Chama Cha TAMWA, kwa niaba ya wenzangu kumi na mmoja, tulio hai ni kumi, ambapo wawili wametangulia mbele za haki. Namshukuru Mungu ametujalia neema ya kuuona Mwaka uliotutunuku fursa ya kuanzisha Chama hiki, japokuwa tunazindua harakati za maadhimisho haya, tukiwa na takriban siku 78 kufikia kilele hapo tarehe 17 Novemba Mwaka huu.

Tungependa ndugu zetu, marafiki zetu, wadau wetu, Watanzania wenzetu mmoja mmoja na katika ujumla wenu, muungane nasi kufurahia fursa hii ya kuadhimisha siku hii muhimu ambayo katika historia ya kuwepo kwetu, tunahesabu mafanikio lukuki tuliyoyapata.

Moja ya mafanikio hayo ambayo ni vigumu kusahau ni ushawishi, kuzengea na kuzonga kuliko fanyika kwa ustadi mkubwa , tukiwa na wenzetu TGNP, TAWLA, MEWATA, WLAC, LHRC, CRC na mashirika mengine kama hamsini hivi tukitetea kubadilika kwa sera, na sheria kandamizi zinazomnyima haki mwanamke na mtoto, hasa mtoto wa kike. Furaha yetu ilikamilika , pale Mwaka 1998 tulipofanikiwa kuongea na wabunge, wakatuelewa na kuwazawadia Watanzania SHERIA YA MAKOSA YA KUJAMIIANA , maarufu kama SOSPA. Utakumbuka pia sheria hii iliboreshwa Mwaka 2005.

Uzuri wa sheria hii ya SOSPA, ni kwamba kwa mara ya kwanza, ilitamkwa wazi kuwa ukeketaji ni kosa la jinai, ikampa mtoto wa kike ulinzi wa kutofanyiwa ukatili akiwa chini ya umri wa miaka 18.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Edda Sanga, akisoma tamko la uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho jijini Dar es salaam leo. Wengine ni wanachama wanzilishi wa TAMWA

 Bi Fatma Aloo akielezea jambo wakati wa mkutano huo
Mkutano wa uongozi wa TAMWA na wanahabari ukiendelea jijini Dar es salaam leo. Kusoma tamko kamili BOFYA HAPA
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images