Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110111 articles
Browse latest View live

MAVUNDE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA SHIRIKISHO LA WATANZANIA WANAOSOMA NCHINI CHINA

$
0
0
 Jana tarehe 28 Agosti, 2017 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Jumuiya za Wanafunzi watanzania wanaosoma katika Jamhuri ya watu wa China (TASAFIC) Bw. Remidius Mwema Emmmanuel alikutana na kufanya mazungumzo na Naibu waziri wa Vijana, Kazi na Ajira Nchini Tanzania Mhe. Anthony Mavunde. 

 Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine yalilenga ufahamu juu ya nafasi ya vijana wa kitanzania wanaohitimu masomo yao nje ya nchi hususani China namna ambavyo wanaweza kunufaika na kutumia vema fursa mbalimbali za kiuchumi kwa manufaa ya Taifa pindi wanaporejea nchini baada ya kuhitimu masomo yao. Hata hivyo Mhe.


Mavunde alipokea maelezo mafupi juu ya mkakati wa Shirikisho (TASAFIC) kwa Vijana wa Kitanzania pindi wanapohitimu wanavyoweza kuwa chachu ya mabadiliko na kuchangamkia fursa zilizopo nchini kwa kutumia Uzoefu na taaluma wanayoipata nje ya nchi. Kwa upande wake Mhe. Mavunde alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na TASAFIC na kuongeza kuwa Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko tayari na inaendelea kuwaunga mkono Vijana wote wanaoonyesha uthubutu wa kujikwamua kiuchumi. 

Akizungumzia Upande wa kilimo, alisema baadhi ya Vijana wamekuwa na mitizamo ya kutojihusisha na Kilimo, Lakini hii inatokana na wengi wao kujaribu kilimo kwa kutozingatia kanuni na misingi bora ya Kilimo na kuona jambo hilo haliwezekani.

"Serikali sasa tuna mikakati ambayo tuna hakika itasaidia kuondoa dhana hizo na kuwafanya vijana wengi kupenda kilimo, ikiwa ni pamoja na Kutoa Elimu zaidi na kuwatumia vijana waliofanikiwa ili waweze kuaelimisha wenzao. Mfano tunao vijana wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) wanaitwa SUGECO, Serikali iliwapatia udhamini wa fedha kupitia Benki ya CRDB, wakafanya kilimo na sasa wamekuwa ni taasisi kubwa na wameanza kusaidia vijana wenzao kupitia mafunzo na misaada mbalimbali.


MASHINDANO YA URIO CUP BADO YANAENDELEA TEGETA

HAKUNA BASI KUONDOKA KATIKA KITUO CHA MABASI UBUNGO BILA KUFANYIWA UKAGUZI -SAMWIX

$
0
0
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi  wa Usalama barabarani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akizungumza leo baada ya kufanya ukaguzi amesema kuwa hakuna basi linaweza kuondoka katika kituo cha mabasi bila kufanyiwa ukaguzi.

Samwix amesema kuwa basi ambalo likibainika katika kituo cha Mabasi Ubungo lina makosa haliwezi kufanya safari zake ambapo amewataka wamiliki kufanya matengenezo ya mara mara ili kuondokana na adha ambazo watakuna nazo mara baada kufanya ukaguzi wa mabasi hayo.

Aidha amesema kuwa madereva wanatakiwa kuwa mabalozi wa kukataa kufanya safari zao pale wanapobaini kuwa basi lina ubovu wowote ili kupukana na ajali ambazo zinatokana na ubovu wa mabasi hayo.
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi  wa Usalama barabarani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akiwa ndani ya uvungu wa basi la Smart akifanya ukaguzi kabla ya basi hilo kuondoka leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi  wa Usalama barabarani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi wa basi kabla halijaondoka kituo hicho leo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI NCHEMBA AZINDUA UJENZI WA MABWENI KATIKA CHUO CHA POLISI MOSHI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mhe. Mwigulu Nchemba (mb) wane kulia, akiwa ameongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (watatu kulia), Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, pamoja na viongozi wengine wakielekea kwenye eneo la uzinduzi wa ujenzi wa upanuzi wa madarasa na mabweni ya wanafunzi yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya mia nane (800) kwa wakati mmoja ujenzi unaofanywa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiweka saini mara baada ya kuwasili katika viwanja vya chuo cha Polisi Moshi CCP mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuzindua rasmi ujenzi wa upanuzi wa madarasa na mabweni ya wanafunzi yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya mia nane (800) kwa wakati mmoja ujenzi unaofanywa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Baadhi ya maofisa na askari wa Jeshi la Polisi wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (hayupo Pichani) wakati wa tukio la uzindua rasmi ujenzi wa upanuzi wa madarasa na mabweni ya wanafunzi yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya mia nane (800) kwa wakati mmoja ujenzi unaofanywa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, katika chuo cha Polisi Moshi kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mhe. Mwigulu Nchemba (mb, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, pamoja na viongozi wengine wakizindua rasmi ujenzi wa upanuzi wa madarasa na mabweni ya wanafunzi yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya mia nane (800) kwa wakati mmoja ujenzi unaofanywa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, katika chuo cha Polisi Moshi CCP kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mhe. Mwigulu Nchemba (mb), Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa upanuzi wa madarasa na mabweni ya wanafunzi yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya mia nane (800) kwa wakati mmoja ujenzi unaofanywa kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, katika Chuo cha Polisi Moshi CCP kilichopo mkoani Kilimanjaro. Picha na Jeshi la Polisi.

DC WA BUHIGWE KANALI GAGUTI AFANYA UKAGUZI WA KUSHITUKIZA MPAKANI MWA TANZANIA NA BURUNDI

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel

MKUU wa wilaya Buhigwe mkoa Kigoma, Kanali Marco Gaguti ameendesha zoezi la kustukiza la ukaguzi wa hali ya ulinzi na usalama wa mpaka wa Tanzania na Burundi na kuridhika kwamba hali ya ulinzi na usalama katika mpaka huo ni ya kuridhisha.

Katika ukaguzi huo uliofanyika juzi usiku, kiongozi huyo akiambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo alitembelea vijiji vya Kibande,Nyamugali na Mnanila ambako aliambaa ambaa na ukingo wa Mto malagarasi unaotengenisha nchi za Tanzania na Burundi kuona hali halisi ya ulinzi na usalama na kuona hali ya usafirishaji wa bidhaa za magendo kupitia maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari majira ya saa tisa alfajiri baada ya kukamilisha zoezi hilo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa ulinzi shirikishi uliowekwa kuanzia ngazi za vitongoji na uelimishaji jamii kuhusu hatua za kuimarisha ulinzi maeneo ya mpakani imekuwa na mafanikio makubwa na kwamba ofisi yake itaendelea kusimamia hali hiyo kuhakikisha ulinzi na usalama wa kudumu unakuwepo wakati wote.

Sambamba na kuangalia hali ya ulinzi na usalama pia zoezi hilo lilihusisha upekuzi katika baadhi ya nyumba zilizokuwa zinahisiwa kuhifadhi wahamiaji haramu na kutembelea maeneo ya mpaka ambayo yanatuhumiwa kwa usafirishaji wa bidhaa za magendo kwenda nchini Burundi na zinazotoka huko kuingia mkoani Kigoma.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa amekuwa akifanya ukaguzi huo mara kwa mara na kwamba mafanikio ni makubwa ingawa alikiri kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji katika maeneo hayo ya mpakani kushirikiana na wahalifu kutenda makosa ya uingizaji wa bidhaa zamagendo na wahamiaji haramu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Buhigwe, Anosta Nyamoga alisema kuwa zoezi la ukaguzi wa mpaka wakati wa usiku limesaidia kupunguza vitendo vya usafirishaji wa bidhaa mbalimbali hasa mazao kwenda nchini Burundi bila kulipiwa ushuru.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa vitendo vya usafirishaji wa mazao na bidhaa bila kulipiwa ushuru vimekuwa vikiiokosesha mapato halmashauri yake na kwamba mkakati wa kuziba mianya ya upotevu huo wa mapato ya serikali inaendelea kufanyiwa kazi.

TPA YATOA MSAADA WA MASHUKA 900 KWA HOSPITALI ZA WILAYA YA TEMEKE

$
0
0
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa mashuka 900 yenye thamani ya Sh. Milioni Kumi kwa Hospitali za Temeke, Mbagala Zakheim na Round zilizopo katika Wilaya ya Temeke.

Msaada huo umekabidhiwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva ikiwa ni sehemu kutambua na kuthamini dhamira na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli, ya kufikisha huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wote na hasa wa hali ya chini.

“Menejimenti ya TPA, chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, inaunga mkono kwa dhati kabisa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu, TPA inayo Sera ya Misaada kwa Jamii ambayo imejikita katika kusaidia jamii kwenye nyanja za Afya, Elimu na Maendeleo ya Kijamii,” amesema Mhandisi Kakoko.

Mhandisi Kakoko ameongeza kuwa pamoja na kwamba TPA kazi yake kubwa ni kuhudumia shehena mbalimbali zinazopita kwenye bandari zote nchini, lakini pia ina wajibu wa kurudisha kile inachokipata kutokana na huduma zake kwa kuisaidia jamii inayoizunguka na ndio maana imeamua kutoa msaada huo kwa Wilaya hii ya Temeke ilipo Bandari ya Dar es Salaam ambayo kiutendaji ndiyo bandari kubwa kuliko bandari zote hapa nchini.

Hivi karibuni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alizindua rasmi kuanza kwa kazi ya maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam na mara itakapokamilika mwaka 2022 itaiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli zenye uwezo wa kubeba kontena 8,000 kutoka kontena 2,500 za sasa na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya ushindani na kuliongezea Taifa mapato. 
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva (wanne kushoto) akishukuru kupokea msaada wa Mashuka 900 yenye thamani ya Tshs Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (watano kushoto)

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva (wapili kushoto) akishukuru kupokea msaada wa Mashuka 900 yenye thamani ya Tshs Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng Deusdedit Kakoko (watatu kushoto).

MAWAKILI MBEYA WAENDELEA NA KAZI

Tulia Trust yatoa msaada wa televisheni na maziwa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete


KIKAO CHA KAMATI YA TIBA KUFANYIKA JUMATANO AGOSTI 30, 2017

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Dkt. Paul Marealle ameitisha kikao cha Kamati ya Tiba kitakachofanyika kesho Jumatano Agosti 30, mwaka huu kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Kikao hicho kitakachofanyika Ukumbi wa Ofisi za Makao Makuu TFF, yaliyoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kitarejea shughuli zake kwa mujibu wa Katiba ya TFF sambamba na Kanuni zinazoongoza mashindano mbalimbali ya TFF.
Katika kikao hicho, pia kamati itapitia fomu za afya za utimamu wa mwili za wachezaji wote wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL).
Miongoni mwa majukumu ya kamati hiyo ni kupitisha wachezaji wanaopaswa kucheza/kushiriki katika ligi baada ya kujirisha juu ya utimamu wa mwili wa wachezaji kwa michuano tajwa hapo juu.

KAMATI YA NIDHAMU KUKETI KESHO
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, kinatarajiwa kuketi kesho Jumatato Agosti 30, mwaka huu.
Kamati hiyo itakuwa na ajenda kadhaa ikiwamo ya mashauri yanayohusu wachezaji mbalimbali, viongozi na klabu.

Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
……………………………………………………………………..……………..……
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

WAZIRI MKUU AWATAKA WAWEKEZAJI KUFUATA SHERIA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watu wote wenye nia ya kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu. Ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Agosti 29, 2017 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais (Uendelezaji Bishara) wa kampuni ya PIRIOU, Bw. Michel Perrin. 
 Waziri Mkuu amekutana na Bw. Perrin jijini Paris nchini Ufaransa kupitia ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Kampuni ya PIRIOU inataka kuja nchini kuwekeza katika utengenezaji na ukarabati wa meli. Akizungumza na muwekezaji huyo Waziri Mkuu alimshukuru kwa nia yake ya kutaka kuwekeza nchini, ambapo alimtaka afuate sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji nchini. “Tanzania ni sehemu nzuri ya uwekezaji kwa sababu kuna fursa nyingi. 
Pia ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo nakukaribisha sana.” 
 Kwa upande wake Bw. Perrin amesema ameamua kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi salama na kwamba anauhakika wa kupata soko ndani ya nchi pamoja na mataifa jiraji. Amesema anaamini uwekezaji wake nchini Tanzania utakuwa na tija, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali na pia atahakikisha anafuata sheria zote za nchi. 
 Pia Bw. Perrin alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Balozi Samwel Shelukindo kutokana na ushirikiano anaompa kuhusu masuala ya uwekezaji nchini. Naye Balozi Shelukindo amesema atahakikisha anaendelea kutafuta wafanyabiashara mbalimbali na kuwashawishi waje kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini.

Article 2

RAIS DK. SHEIN AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MTENDAJI WA KAMISHENI YA KISWAHILI AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  Prof Kenneth Linyani  Simala wakati  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe alliofuatana nao .
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  Prof Keneth Linyani Simala wakati  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar  jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  Prof Keneth Linyani Simala wakati  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar  Jana  29/08/2017. (Picha na Ikulu) 

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WANAFUNZI MSALATO GIRLS WAJIPANGA KUINGIA 10 BORA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA.

$
0
0
Wanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya wasichana ya Msalato Manispaa ya Dodoma wamemuahidi Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo kwamba watapambana ili katika matokeo ya kidato cha sita mwakani shule yao iwe miongoni mwa shule kumi bora nchini. 

Ahadi hiyo ilitolewa na wanafunzi hao katika ziara ya Naibu Waziri Jafo alipotembelea shule hiyo kukagua ujenzi wa miundombinu inayojengwa na serikali ili kuirudisha shule hiyo katika hadhi yake.

Shule hiyo ni miongoni mwa shule kongwe 88 zilizo katika mpango wa ukarabatiwa na serikali ambapo ndani ya miaka 4 shule hizo zitakuwa ni shule zenye ubora wa hali ya juu kwa kuboreshewa mazingira yake yakiwemo mabweni, madarasa, vyoo, mabwalo, mifumo ya maji na umeme, pamoja na nyumba za walimu. 

Katika shule hiyo, serikali hadi sasa imeshakamilisha ukarabati wa mabweni nane, mfumo wa umeme na maji.Aidha Serikali imejipanga kuendelea na ukarabati wa madarasa na ujenzi wa madarasa mengine manne mapya, ukarabati wa bwalo la chakula, majengo ya utawala, na nyumba za walimu. 

Kufuatia uboreshaji huo, Wanafunzi wameishukuru serikali na wamemuahidi Naibu Waziri huyo kwamba watahakikisha wanajitahidi ili mwakani shule yao iwe miongoni mwa shule kumi bora katika matokeo ya kidato cha sita.

Akizungumza na wanafunzi hao, Naibu Waziri Jafo amewahakikishi watanzania kwamba mpango wa serikali ni kuboresha shule za umma ili ziweze kutoa elimu bora hapa nchini.Mwaka jana, Naibu Waziri Jafo alitembelea shule hiyo na kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kuhakikisha wanafanya vizuri katika mitihani yao ili shule hiyo itoke kutoka shule ya 21 katika matokeo ya kidato cha sita mwaka jana ili waingie 10 bora. Jambo ambalo katika matokeo ya mwaka huu shule hiyo imeshika nafasi ya namba 14 kitaifa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua maeneo ya vyoo na mifumo ya maji iliyokarabatiwa katika shule ya Sekondari ya wasichana Msalato.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelezo ya ukarabati wa mabwene kutoka kwa mmoja wa wakandarasi wanaofanya ukarabati huo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akifanya ukaguzi wa mabweni nane yaliyofanyiwa ukarabati katika shule ya Sekondari ya wasichana.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa shule hiyo pamoja na maafisa wengine wakifanya ukaguzi wa majengo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Msalato Dodoma.
Miongoni mwa mabweni yaliyokarabatiwa na serikali

Wakazi wa Shinyanga na Geita kunufaika na uwekezaji mradi wa umeme

$
0
0

Kampuni ya Acacia, kwa ushirikiano na TANESCO, imejenga kituo cha kupozea umeme kilichopo katika mgodi wake wa dhahabu wa Bulyanhulu ambacho kimeweza kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya mgodi huo.

Acacia imewekeza shilingi bilioni 5.5 katika mradi huo ambao utanufaisha maeneo yanayozunguka migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na maeneo mengine ikiwa ni pamoja na Kahama, Shinyanga, Msalala, na sehemu nyingine za Geita.

Ujenzi wa Kituo hicho ulianza Desemba 2016 na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Haya ni maendeleo makubwa kwa viwanda na biashara zinazozunguka eneo hilo ambazo zitafaidika na uwepo wa umeme wa uhakika jambo litakalosaidia kuboresha ufanisi na kuongeza uzalishaji.

Mkuu wa kitengo cha miradi ya maendeleo wa mgodi wa Bulyanhulu, Jiten Divecha ameeleza kuwa tatizo la mabadiliko ya nguvu ya umeme limekuwepo kwa muda mrefu na limekua likisababisha uharibifu mkubwa wa mashine.“Ujenzi wa kituo hiki utasaidia kupunguza athari zinazotokana na kuongezeka au kupungua kwa nguvu ya umeme katika migodi yetu hivyo kuboresha shughuli za uzalishaji. Wakazi na viwanda vinavyotumia umeme katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga na wilaya zingine za mkoa wa Geita zitafaidika na uwekezaji huu pia,” alisema Jiten.

Aliongeza: "Acacia inajitahidi kuleta manufaa ya kiuchumi ya pamoja kwa jamii zinazotuzunguka na wadau wake kupitia miradi endelevu."
Wakati wa ujenzi wa kituo hicho, ajira mbalimbali zilitolewa kwa jamii zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu.
Akizungumzia fursa hiyo, David Nyanda alisema: “tunathamini sana ujenzi wa mradi huu kwa sababu tumepata fursa za ajira. Japokuwa fursa hizi ni za muda, tunaweza kupata mapato ili kuendesha familia zetu hasa katika kipindi hiki cha ukame.”

MPANGAJI APEWE NOTISI YA MUDA GANI KUONDOKA KWENYE NYUMBA ?.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Kuna  matatizo  sana   kati  ya  wapangaji  na  wenye  nyumba  kuhusu  notisi  ya  kuondoka  au  kuondolewa.  Wako  wanaosema  notisi  ni  mwezi mmoja,  wako  wanaosema  ni  miezi  mitatu  n.k.  Kama  ni kweli  ama  hapana  tutaona hapa   sheria  inasemaje. 

Masuala  ya  pango  yanaongozwa  na  sheria  kuu  mbili.  Moja  sheria  ya  ardhi  namba  4  ya  mwaka  1999  na  pili  sheria  ya  mikataba  sura  ya  345.  Kwa  pamoja  sheria  hizi  mbili  husimamia   jambo  hili.

1.MIKATABA YA  PANGO.                
Mikataba ya pango  inahusisha  makubaliano  ya  upangaji  kati  ya  mwenye  nyumba  na  mpangaji  au  mpangaji  na  mpangaji  mwingine  wa  pili.  Pango  laweza  kuwa   la  nyumba  ya  kuishi,   kwa  ajili ya  biashara,  nyumba  ya  ibada  au  shughuli  nyinginezo.   Yote  haya  yataingia  katika  maana  ya  pango.

2.   AINA   ZA  MIKATABA  YA   PANGO.
Sheria  ya ardhi   vifungu  vya  78  na  79  inatambua   mikataba ya  upangaji  ya  muda  mrefu  na  vipindi  vifupi. Inatambua  pango  la  wiki,  mwezi,  miezi,  mwaka  na  miaka.  Imetoa  uhuru  kwa  wahusika  wenyewe  kuamua  ni  muda  gani  wangependa  kuingia  mkataba. 

3.   NOTISI  YA  KUONDOKA.
Katika  vitu  muhimu  sana  katika  suala  la  pango  ni  notisi ya kuondoka   au  kuondolewa  katika  pango.  Jambo  la  kuzingatia awali  kabisa  ni  kuwa   notisi  hii  ni  muhimu  pande  zote  mbili.  Upande  wa  mwenye  nyumba  na  upande  wa  mpangaji.  Kila  mmoja  kwa  nafasi  yake  anawajibika  kutoa  notisi  kwa  mwenzake  panapo  mahitaji  ya  kuondoka  au  kuondolewa.

Ikumbukwe  notisi  si  kwa  ajili  tu  ya kuondoka  na kuondolewa   bali  pia   hutakiwa  yanapotokea mabadiliko  yoyote  katika  masharti  ya  mkataba. Hii  ina  maana  hata  kuongeza  kodi, kupanga  kukagua  nyumba, kufanya  marekebisho  n.k.  notisi  yafaa  itolewe. 

KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com




MAGAZETI YA JUMATANO LEO AGOSTI 30,2017

WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Nkololo wilayani Bariadi (hawapo pichani) katika Mkutano wa Hadhara, wakati wa ziara yake aliyofanya kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ziara aliyofanya katika Kata ya Nkololo wilayani Bariadi, kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Nkololo wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika Mkutano wa Hadhara aliofanya katika Kata hiyo wakati wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Wananchi wa Kata ya Nkololo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wametakiwa kutambua wajibu wao katika kuchangia ujenzi wa Vyumba vya madarasa ili kupunguza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari. Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka wakati alipokuwa akijibu kero mbalimbali za wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nkololo Kata ya Nkololo Wilayani Bariadi.

Mtaka amesema ni vema wananchi wakahamasika kuchangia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kama wanavyochangia katika masuala mengine ili watoto wao wawe na mazingira mazuri ya kusomea. “Kujenga vyumba vya madarasa siyo wajibu wa walimu wetu ni wajibu wenu wenu wazazi, ni lazima wananchi wa Nkololo mjenge vyumba vya madarasa kama mnavyojitoa katika mambo mengine, najua hamuwezi kushindwa kutoa angalau mfuko mmoja wa saruji kila kaya; Nkololo itajengwa na wana Nkololo wenyewe” amesema Mtaka.

Aidha, Mtaka ametoa wito kwa wananchi hao kuzingatia suala la uzazi wa mpango kwa kuwa ongezeko kubwa la watoto ndio linalopelekea idadi kubwa ya wanafunzi ikilinganishwa na vyumba vya madarasa. “Mhe.Diwani nikuombe tengeneza utaratibu hapa na watu wako, Nkololo ni moja ya centre(kituo) kubwa wachangie, wala wasiseme tumechangia sana ni lazima wachangie; na kama hatutajirekebisha kwenye kuzaana, tutachanga, tutachanga, tutachanga” amesema Mtaka.

Naye Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Doreen Rutahanamilwa amesema, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya elimu vikiwemo vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo, hivyo wananchi wanao wajibu kuunga mkono jitihada hizo ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.

Kuhusu kero ya uharibifu wa mazao unaofanywa na wanyamapori hususani Tembo, ambayo ilitolewa na Luja Masala Mkazi wa Kijiji cha Bubale, Mkuu huyo wa Mkoa amesema, Serikali kupitia watalaam wake wa Wanyamapori watakabiliana na tatizo hilo, hivyo akawataka wananchi wasiache kulima na wazingatie ushauri wanaopewa na watalaam hao.

Akitoa ufafanuzi wa kitaalam juu ya kero hiyo, Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili, Ndg.Mazengo Sabaya amesema, Halmashauri imekuwa ikipeleka askari wa Wanyamapori katika maeneo yanayovamiwa na tembo na akawataka wananchi kuendelea kufuata ushauri wa kutumia uzio wa pilipili katika mashamba yao ili kuwazuia tembo hao.

Katika suala la upatikanaji wa mbegu bora, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka Serikali kupitia kwa wakala wa mbegu ina mpango wa kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora katika bei wanayoweza kuimudu. Katika hatua nyingine Mtaka ametoa maelekezo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuhakikisha inaweka mipango ya ujenzi wa stendi, soko na barabara katika kituo cha Nkololo ambacho ni moja vituo vikubwa vya kibiashara wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa ameanza ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi katika Kata ya Nkololo na baadaye atafanya ziara katika kata za Dutwa na Ngulyati ambapo atafanya mikutano ya hadhara na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.

KAMISHNA WA MADINI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA

$
0
0
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati), akikagua sehemu ya chini (underground) ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM). Pamoja naye ni maofisa kutoka wizarani na GGM.

Na Veronica Simba – Geita

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, amefanya ziara katika Mkoa wa Geita, ambapo ametembelea maeneo mbalimbali ukiwemo Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Kijiji cha Nyakabale, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.

Ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake rasmi ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kamishna Mchwampaka, jana, Agosti 29, alifanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali mstaafu, Ezekiel Kyunga, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Selestine Gesimba na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi ambapo walikubaliana kuendeleza ushirikiano katika kusimamia shughuli za sekta ya madini kwa manufaa ya wananchi wa Geita na Taifa zima.

Akiwa katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Kamishna Mchwampaka ambaye alifuatana na Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria-Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba, Afisa Madini wa Mkoa wa Geita Ali Said Ali na maafisa wengine kutoka wizarani, alipokea taarifa ya utendaji kazi wa Mgodi huo na kukagua maeneo na shughuli mbalimbali zinazofanyika mgodini.

Aliwataka watendaji na viongozi wa Mgodi kuendelea kuimarisha mahusiano na jamii inayowazunguka ili kuondoa migogoro iliyopo na kuepusha migogoro mingine kujitokeza.

Akizungumza na viongozi wa Kijiji cha Nyakabale, Benard Kazuri (Mtendaji) na Ndalahwa Elias (Mwenyekiti), aliwataka kuwaelimisha wananchi wao kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi, hususan zinazohusu masuala ya madini kwa kuachana na tabia ya uvamizi na kuiba katika Migodi ya wawekezaji wakubwa badala yake waendelee kujiunga na vikundi mbalimbali vya uchimbaji mdogo na kuendesha shughuli hizo kwa kufuata taratibu husika ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (wa pili kutoka kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Huduma za Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Manase Ndoroma (wa kwanza kushoto). Wengine ni maofisa kutoka wizarani na GGM.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (wa tatu kutoka kulia), akikagua moja ya maeneo kunakofanyika uchenjuaji wa dhahabu za wachimbaji wadogo katika kijiji cha Nyakabale wilayani Geita.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na timu yake wakikagua Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), katika shimo la wazi (Open pit).
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Meja Jenerali mstaafu, Ezekiel Kyuga (kushoto), akizungumza na Kamishna wa Madini na Timu yake, walipofika kumtembelea ofisini kwake.

MBUNGE ULANGA ATOA FEDHA KWA WAATHIRIKA WA AJALI YA BASI

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mh. Amina Seif na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Yusuf Semuguruka wakimsikiliza mmoja wa majeruhi wa ajali ya basi la Mfundo iliyotokea katika Mlima Ndororo hivi karibuni.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mh. Amina Seif akimkabidhi Mganga Mkuu wa Wilaya fedha zilizochangwa na Waheshimiwa Madiwani wa kamati ya Fedha, Utawala na Mipango na Wakuu wa Idara kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu yaliyotolewa kwa majeruhi wa ajali ya basi la Mfundo.

Na Sekela Mwasubila – Afisa Habari

Mbunge wa Ulanga Mh. Goodluck Mlinga ametoa kiasi cha shilingi milioni tano na laki tano kwa ajili ya kuwafariji majeruhi  na wafiwa wa ajali ya basi la Mfundo iliyotokea hivi karibuni katika mlima Ndororo.

Fedha hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Jacob Kassema ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maafa wilaya ili awasilishe kwa walengwa ikiwa kwa ajili ya kuwapa pole familia za waliopoteza maisha na majeruhi  wa ajali hiyo.

Akipikea fedha hizo Mkuu wa Wilaya Ndugu Kassema alimshukuru mbunge kwa msaada alioutoa kwani utawasaidia sana wafiwa na majeruhi na kuwafariji kutokana na kupoteza mali zao katika eneo la ajali.

Wakati huo huo madiwani wa kamati ya fedha, Utawala na Mipango na Idara nao walitoa mkono wa pole kwa wafiwa na majeruhi ambapo mchango huo ulikabidhiwa kwa Mganga Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Ulanga Mh. Amina Seif na kusema kuwa fedha hiyo imetolewa kwaajili ya kugharamia matibabu ya majeruhi waliopo wodini na waliotibiwa na kuruhusiwa.

Aliongeza kuwa waheshimiwa madiwani wameguswa sana na ajali hiyo na kuona kuwa kuna haja ya kuwasaidia kuwalipia matibabu kwani wengi wao wamepoteza vitu sehemu ya ajali hivyo ingewahuia ugumu wa kulipia matibabu na kuamua kuwachangisha madiwani wa kamati ya fedha na wakuu wa Idara na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs. 327,000.

Akipokea fedha hizo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Dkt. Rajabu Risasi amewashukuru waheshimiwa madiwani kwa msaada huo na kueleza kuwa fedha hiyo itawasaidia katika kufidia madawa yaliyotumika siku ya ajari kwani majeruhi wote walitibiwa bila kujali kama wana fedha za matibabu.

Basi la Mfundo lilipata ajali siku ya alhamisi katika mlima Ndororo na kujeruhi watu thelathini na tatu na kusababisha vifo vya watu saba.
Viewing all 110111 articles
Browse latest View live




Latest Images