Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110105 articles
Browse latest View live

KAMISHNA WA MADINI AANZA ZIARA KANDA YA ZIWA

$
0
0
Na Veronica Simba – Mwanza.

Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, ameanza ziara ya kazi ya takriban juma moja katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli mbalimbali za sekta hiyo.
Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Agosti 28 mwaka huu, Kamishna Mchwampaka alikutana na kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Madini, Kanda ya Ziwa Viktoria-Magharibi pamoja na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Ukaguzi wa Madini Kanda ya Mwanza, iliyokuwa ikijulikana kama Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA).
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi hizo mbili, Kamishna Mchwampaka aliwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ili kufanikisha malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwaletea wananchi wake maendeleo ya dhati.
Katika hatua nyingine, akizuru Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Kamishna Mchwampaka, alipongeza jitihada za watendaji wa Mradi huo unaomilikiwa na wazawa wazalendo kwa asilimia mia moja, kwa ubia kati ya Isinka Federation 2014 Mining Cooperative Society Limited na Kampuni ya kitanzania ya Busolwa Mining Limited.
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Samwel Sweda (wa pili kutoka kushoto), alipofika ofisini kwake akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke. Wengine ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria-Magharibi, Mhandisi Yahya Samamba (kushoto kwa Mkuu wa Wilaya) na Mhandisi Rayson Nkya (wa kwanza kulia).
Mmoja wa Viongozi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, Baraka Ezekiel (wa pili kutoka kulia), akifafanua jambo kwa Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati) na Ujumbe wake. Kamishna Mchwampaka alitembelea Mradi huo Agosti 28 mwaka huu akiwa katika ziara ya kazi Kanda ya Ziwa 
Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (katikati), akiwa ameambatana na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini na wafanyakazi wa Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza, wakikagua sehemu mbalimbali za Mgodi huo.


Shughuli za uchimbaji madini zikiendelea katika Mradi wa Uchimbaji wa Kati wa Madini ya Dhahabu uliopo Ishokelahela wilayani Misungwi, Mkoa wa Mwanza.


Cheka akata rufaa BMT kupinga matokeo

$
0
0
Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Cosmas Cheka amekata rufaa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupinga matokeo na adhabu ya kufungiwa miezi sita na faini ya Sh200,000 iliyotangazwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).

Cheka alisema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa TPBC ilikuwa na njama dhidi yake ili kumtengenezea nafasi bondia Haidary Mchanjo katika ngumi za kulipwa nchini.

Alifafanua kuwa adhabu dhidi yake haikufuata sheria kwani kwanza hakupewa nafasi ya kusikilizwa kwa mujibu wa sheria, huku akimpa nafasi mwamuzi wa pambano hilo, Modest Rashid ambaye alitaka kupigana naye kuitwa na kujieleza katika kikao cha TPBC.

“Hata kwenye mahakama, lazima mtuhumiwa apewe nafasi ya kusikilizwa au kujitetea, mimi nilikuwa ulingoni na mwamuzi na mpinzani wangu Mchanjo, mwamuzi amenitolea maneno machafu sana, haikutosha akaamua kunikata pointi, niliandika barua ya kulalamika TPBC, hawajaniita na kuibuka na adhabu kwangu,” alisema Cheka.

Alisema kuwa pamoja na maamuzi hayo kutonifikia kimaandishi, nimeamua kuchukua hatua za haraka kwani tayari vyombo vya habari mbalimbali na mitandaa ya kijamii yamekwisha tangaza maamuzi hayo yaliyofanywa bila kufuata sheria kwani hawakunipa nafasi ya kusikilizwa kwa mujibu wa sheria. 


Meneja wa bondia wa Cosmass Cheka, Juma Ndambile (kulia) akizungumzia matatizo yaliyompata bondia wake. 
Cosmass Cheka akizungumzia hatua aliyochukuwa ya kukata rufaa BMT kupinga kufungiwa na matokeo ya pambano lake dhidi ya bondia Haidary Mchanjo.

RC TABORA ATAKA MAELEZO ALIYECHOMA MOTO KATIKA CHUO CHA ARDHI

$
0
0
Na Tiganya Vincent.

SERIKALI Mkoa wa Tabora imeagiza kutafutwa na kuchukiwa hatua kali na kupata maelezo ya watu waliohusika na uchomaji moto katika maeneo ya Chuo cha Ardhi Tabora na kusababisha uharibifu mkubwa wa mistu asili na miti iliyokuwa imepandwa katika eneo hilo kama hatua za uhifadhi wa mazingira.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri baada ya kukuta eneo la Chuo hicho likiwa limeungua na moto wakati wa ziara ya ya kukagua vitalu vya kuoteshea miti ikiwa ni maandilizi ya zoezi la upandaji wa miti.

Alisema kuwa haiwezekani wananchi wanajitoa kwa moyo kupanda miti katika kampeni inayoendelea kisha watu wachache wanaamua kuua miti na kuharibu mazingira.

Mwanri aliongeza kuwa inasikitisha kuona hata sehemu za Taasisi za umma kama hiyo zinaacha moto unaunguza miti na wakufunzi wapo, wanachuo wapo bila kuchukua hatua ya kuuzima na kuwasaka waliohusika.

Alisema kitendo kinaonyesha jinsi wao nao wanahusika kwa namna moja au nyingine katika kuchangia uharibifu ulifanyika katika Chuo chako.
Kufuatia kitecho hicho Mkuu wa Mkoa alimwagiza Afisa Mazingira wa Manispaa ya Tabora kwenda kwa Mkuu wa Chuo kupata maelezo nini kilitokea na hatua zilizochukuliwa kwa wahusika na kama hawachukua hatua kwa wahusika basi Sheria za Mazingira zichukue mkondo wake.

SAID KAROLI AZIDI KUPAA

MAWAKILI WAGOMEA AGIZO LA BARAZA LA CHAMA CHA MAWAKILI LILILOTOLEWA KUPITIA RAIS WAKE TUNDU LISSU

$
0
0
 Baadhi ya Mawakili wakiendelea na shughuli zao za Uwakili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam mapema leo licha ya kuwepo  kwa Agizo kutoka baraza la Chama cha Mawakili nchini  (TLS) lililotolewa na Rais wa chama hicho, Tundu Lisu kuwataka Mawakili wote nchini kususia shughuli za Mahakama kwa muda wa siku  Mbili (Jumanne na Jumatano), baada ya kutokea Milipuko katika Ofisi za Mawakili za IMMMA ADVOCATES zilizopo upanga jijini Dar es salaam, inayodaiwa kulipuliwa na watu wasiojulikana mapema.
 Baadhi ya Mawakili wakiendelea na shunghuli zao za Uwakili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo 

  Baadhi ya Mawakili wakiendelea na shunghuli zao za Uwakili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo 
  Baadhi ya Mawakili wakiendelea na shunghuli zao za Uwakili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema leo . 

NGAO YA JAMII MPYA YA SIMBA IKO TAYARI, SASA KUKABIDHIWA RASMI SEPT 06

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BAADA ya kufanyika kwa makosa wakati wa utengenezaji wa Ngao ya Jamii, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini 'TFF' imetengeneza Ngao mpya kwa ajili ya klabu ya Simba baada ya ile ya awali kukosewa kuandikwa.


Klabu ya Simba ilifanikiwa kushinda katika mchezo wa Ngao ya Jamii August 23, 2017 baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 mahasimu wao Yanga na kukabidhiwa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya kiuandishi.


Ngao ya Jamii ya awali iliyokabidhiwa kwa washindi hao wa mwaka 2017 Simba iliandikwa ‘Community Sheild’ badala ya ‘Community Shield’ kitu ambacho kilizua mijadala kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea TFF kuomba radhi kwa wanafamilia wa mpira wa miguu nchini na kuahidi tukio kama hilo halitojirudia tena.

Afisa habari wa TFF Alfred Lucas ameionesha Ngao ya Jamii iliyofanyiwa marekebisho itakabidhiwa  kwa Simba siku ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC.


Afisa habari wa TFF Alfred Lucas akionesha Ngao ya Jami mpya iliyofanyiwa marekebisho na tayari kukabidhiwa kwa Klabu ya Simba  siku ya mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC.

Balozi Asha-Rose Migiro awatembelea Watanzania waishio Birmingham

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mheshimiwa Asha-Rose Migiro alifanya ziara ya kuwatemebelea Watanzania waishio katika mji wa Bimingham na vitongoji vyake tarehe 28/8/2017.

Pamoja na ziara hiyo, Mhe. Balozi Migiro alipata nafasi ya kushiriki katika uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania waishio katika mji huo wa Birmingham na Vitongoji vyake, ijulikanayo kama Watanzania wa Birmingham na nchi nyeusi -(Tanzanian's in Birmingham and Black Country - WBBC).

Mhe. Balozi aliwapongeza na kutoa wito kwa  Watanzania hao kuwa na kushirikiano wa karibu na Ofisi za Ubalozi kupitia Viongozi wao. Pia alihimiza umuhimu wa Wana diaspora kuwa wamoja na kushirikiana bila kubaguana.

Katika Mkutano huo, kulifanyika hafla ndogo ya kuchangia Jumuiya hiyo pamoja na chakula cha pamoja kwa kumshukuru Mhe.Balozi kwa kutenga muda wake na kuwatembelea.

Sambamba na hafla hiyo Mheshimiwa Balozi Asha-Rose Migiro pia alizindua rasmi Jumuiya hiyo, na kukabidhiwa Katiba yao itakayo tumika kuendesha shughuli za kila siku za Jumuiya hiyo.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi Migiro akiwahutubia Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo kushoto kwake ni katibu wa Jumuiya ya Watanzania waishio Birmingham na Black Country Dkt. Hassan Khalfan Hamidu, anayefuatia ni Mbunge kutoka jimbo la Stafford wa chama cha Conservative Jeremy John Lefroy na nyuma ya Balozi ni Mwambata wa Uhamiaji Ubalozini Bw. Magnus Ulungi.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi akiwa na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Birmingham Mwenyekiti wa WBBC Bw. Renatus Mgetta(Pili kulia), Katibu wa Baraza la Ushauri Brian M. Ngelangela.; Kutoka kushoto mwa picha ni Katibu Mwenenzi Dr. Dr. Othman M., Katibu wa Jumuiya Dr. Hassan Khalfan na Kiongozi wa Kamati ya Katiba, Uratibu na Mwongozo Bw. Nelson Kampa.
 Mbunge kutoka jimbo la Stafford wa chama cha Conservative Jeremy John Lefroy akihutubuia katika mkutano huo wa wanadispora.
 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Balozi Migiro akijumuika na watanzania katika kucheza muziki
 Balozi Asha-Rose Migiro akizungumza na Mwenyekiti wa British Tanzania Society (BTS) Prof. Andrew Coulson wakati wa mkutano huo.
Mheshimiwa Balozi, akijumuhika na Watanzania hao katika chakula cha pamoja

Dawasa kujenga miundombinu ya majitaka jijini Dar es Salaam.

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

UZALISHAJI wa Maji Safi kunahitaji kuwepo na miundombinu ya maji taka ambayo yanazalishwa na maji safi katika kutunza mazingira pamoja na afya kwa wananchi wanatumia maji safi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, Mhandisi Romanus Mwang’ingo amesema kuwa wameanza kufanya utekelezaji wa miradi ya ukusaji na uondoshaji wa majitaka kwa kuanzisha miradi mitatu ya kisasa ya kusafisha majitaka hayo.

Amesema Miradi hiyo itakwenda sambasamba na uzalishaji wa mabomba ya kukusanya majitaka hayo kwa kujenga miundombinu katika maeneo ya Jangwani, Mbezi Beach pamoja na Kurasini.Mwandisi Mwang’ingo amesema ujenzi wa miundombinu hiyo itaongeza kiwango cha kusafisha majitaka kwa asilimia 30 ifikapo 2020 kutoka kiwango cha asilimia 10 iliyopo sasa itakayogharimu Dola za Kimarekani Milioni 600 katika mwaka wa fedha 2017/2018.

Amesema mfumo wa majitaka wa Jangwani utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kusafisha majitaka hayo mita za ujazo 200,000 kwa siku.Mabomba yenye urefu wa kilomita 376 yatajengwa katika mradi utakaonzia kunazia Ubungo hadi Jangwani,Kinondoni, Mwananyamala, Msasani Katikati ya Jiji na Ilala.

Mhandisi Mwang’ingo amesema kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi itahusisha sehemu sehemu itakayoweza kusafisha mita za ujazo 25,000 kwa siku na mabomba yenye urefu wa kilomita 17.43 yatakayojengwa eneo la magomeni.

Aidha katika awamu ya kwanza,bomba linalomwaga majitaka baharini litaacha kutumika na badala yake majitaka hayo yatakwenda kusafishiwa katika mtambo huo ambapo mtambo huu unajengwa kati ya ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Korea kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Exim ya Korea unaotarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani milioni 90 ambazo tayari zimepatikana.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, Mhandisi Romanus Mwang’ingo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati Dawasa ya maji safi na majitaka leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maelezo,Rodney Thadeus kulia ni Meneja Mawasiliano Dawasa, Neli Msuya.
Meneja wa Mawasiliano wa Dawasa, Neli Msuya akizungumza juu miradi inajengwa na Dawasa katika maeneo mbalimbali Dar es Salaam na Sehemu ya mkoa wa Pwani leo jijini Dar es Salaam

PATAKUWA HAPATOSHI TRAVERTINE HOTEL-MAGOMENI

VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYAITIKIA WITO WA RAIS MAGUFULI KUNUNUA BUTI KATIKA KIWANDA CHA VIATU KARANGA, MOSHI

$
0
0
Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili katika ziara Maalum ya kukagua maboresho mbalimbali katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi leo Agosti 29, 2017(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Gereza Kuu Karanga – Moshi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Leonard Mushi.
Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akiongea na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Kilimanjaro katika Kiwanda cha viatu cha Karanga Moshi(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Hassan Mkwiche.
Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akiangalia Buti la Jeshi lililotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi.
Viatu aina ya Buti za Jeshi zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu Karanga Moshi.
Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akikagua eneo la mradi wa Ubia kati ya Jeshi la Magereza na Mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF ambapo katika eneo hilo kutajengwa mradi wa Kiwanda kipya cha viatu na bidhaa za ngozi katika eneo hilo.
. Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila akifyatua tofali zitakazotumika kujengea nyumba za askari katika Gereza Kuu Karanga, Moshi kama inavyoonekana katika picha.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAKAMU WA RAISI WA KAMPUNI YA UTENGENEZAJI MELI UFARANSA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watu wote wenye nia ya kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 29, 2017) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais (Uendelezaji Bishara) wa kampuni ya PIRIOU, Bw. Michel Perrin. Waziri Mkuu amekutana na Bw. Perrin jijini Paris nchini Ufaransa kupitia ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Kampuni ya PIRIOU inataka kuja nchini kuwekeza katika utengenezaji na ukarabati wa meli.

Akizungumza na muwekezaji huyo Waziri Mkuu alimshukuru kwa nia yake ya kutaka kuwekeza nchini, ambapo alimtaka afuate sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji nchini. “Tanzania ni sehemu nzuri ya uwekezaji kwa sababu kuna fursa nyingi. Pia ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo nakukaribisha sana.”

Kwa upande wake Bw. Perrin amesema ameamua kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi salama na kwamba anauhakika wa kupata soko ndani ya nchi pamoja na mataifa jiraji. Amesema anaamini uwekezaji wake nchini Tanzania utakuwa na tija, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali na pia atahakikisha anafuata sheria zote za nchi.

Pia Bw. Perrin alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Balozi Samwel Shelukindo kutokana na ushirikiano anaompa kuhusu masuala ya uwekezaji nchini. Naye Balozi Shelukindo amesema atahakikisha anaendelea kutafuta wafanyabiashara mbalimbali na kuwashawishi waje kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMANNE, AGOSTI 29, 2017.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Raisi wa Kampuni (Uendelezaji Bibiashara) wa Kampuni ya PIRIOU ya utengenezaji na ukarabati wa meli nchini Ufaransa. Bwana Michel Perrin .kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa Bwana Samweli Shelukindo.Waziri Mkuu amekutana naye leo Agost 29/2017 Parisi Ufaransa.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

MultiChoice Yafyeka bei za vifurushi vyote! Wapenzi wa Kandanda ‘meno nje’

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akitangaza punguzo kubwa la bei kwa vifurushi vyote vya DStv bei zitakazoanza kutumika rasi Septemba mosi 2017.

Katika kuhakikisha kuwa wateja wake wote na watanzania kwa ujumla wanaendelea kufurahia huduma za DStv, kampuni ya Multichoice Tanzania imetangaza neema kubwa kwa wateja wake kwa kufyeka bei za vifurushi vyake vyote, huku pia ikiboresha maudhui na vipindi katika vifurushi vyake hususan vile vya bei ya chini!

Habari hiyo njema imetangazwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema bei hizo mpya zitaanza kutumika rasmi Septemba mosi 2017.

“Kumjali na kumsikiliza mteja ni nguzo ya uendeshaji wa biashara yetu. Tumesikia maoni ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla kutusihi tuangalie uwezekano wa kupunguza bei, tumechanganua kwa kina na tumeamua kutekeleza matakwa yao, leo hii tumepitisha panga kwenye bei za vifurushi vyetu vyote!” alisema Maharage. 

Akifafanua kuhusu punguzo hilo, Maharage amesema  kumekuwa na punguzo la hadi asilimia 16, ambalo ni punguzo kubwa sana na litakalowapa ahueni kubwa watumiaji wa DStv. Amezitaja bei mpya kuwa ni; 
Mara baada ya kutaja bei hizo Maharage aliwaambia waandishi wa habari; “Kwa lugha ya mtaani wanasema ‘Vyuma Vimekaza’ – ikimaanisha hali ya kifedha imebana… Multichoice imelisikia hilo na kuamua kuwapa wateja wote wa DSrv ahueni kubwa! Sasa kwa wateja wetu wa DStv, ‘Vyuma vimeachia’”

Maharage amesisitiza kuwa Multichoice itaendelea kuwasikiliza wateja wake na kuhakikisha kuwa inatekeleza kile wanachohitaji wateja wake pale inapowezekana.

“Wateja wetu walituomba tuongeze maudhui ya kitanzania kwenye king’amuzi chetu, tukawasikia, tukaweka chanel maalum kabisa ya Maisha Magic Bongo ambayo ina asilimia 100 ya maudhui ya Kitanzania; wakatuomba tupunguze bei ya vifurushi, tukafanya hivyo mwishoni mwa mwaka jana, na leo tena kwa mara ya pili tumepunguza bei, wakatuomba tuongeze chanel kwenye vifurushi vya bei ndogo, tukafanya hivyo, tukaleta Laliga na Ligi kuu ya uingereza hadi kwenye kifurushi cha chini kabisa cha Bomba”.

“Kipekee kabisa Wananchi kupitia serikali wakatuomba tuongeze nguvu kwenye kuinua vipaji vya vijana wetu wa kitanzania, tukasikia, tukaitikia, tukaanza katika riadha ambapo tumemdhamini mwanariadha wetu Alphonce Simbu. Sote tunajua matokeo yake, sasa Tanzania inahofiwa kwenye ulingo wa riadha kimataifa! Haya yote tumefanya kwa sababu tunawasikiliza wateja wetu, tunawasikiliza wadau wetu, tunawasikiliza Watanzania” alisema Maharage.

Wakati habari hii ikiwa ni njema kwa watanzania wote, washabiki na wanazi wa kandanda wameonekana kufurahia Zaidi kwani kwa punguzo hilo kuwa wataweza kushuhudia ligi kuu ya uingereza PL pamaja na ligi nyingine kubwa ulimwenguni na makombe maarufu kama UEFA kwa bei nafuu zaidi. 

Kwa maelezo Zaidi kuhusu bei mpya na vipindi mbalimbali katika vifurushi vya DStv tembelea; www.dstv.com

MIVARF yafanikiwa kupunguza umaskini wa kipato na kuimarisha uhakika wa Chakula

TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI KUJIANDAA NA BOTSWANA JUMAMOSI, 'MAPRO' WAANZA KUTUA

$
0
0
Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza kujifua leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Wachezaji wote kutoka klabu za Tanzania wamefika kadhalika baadhi kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile Nahodha Mbwana Samatta na Elias Maguli. Mazoezi hayo yataendelea kila siku hadi Ijumaa wiki hii.

Kikosi hicho kinachofanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga kinajindaa kucheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 28 hadi Septemba 5, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2, 2017.

Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemwita upya Mlinzi wa Young Africans, Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wakiwa ni saba.

Kikosi hicho kinachopiga kambi hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).

Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).

Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).

Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman).

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
 Kocha Mkuu  wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Shabani Mayanga 
.

WAGOMBEA NANE WAPITISHWA UCHAGUZI WA BODI YA LIGI OKT 15

$
0
0
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza majina manane ya wagombea ambao yamepita katika mchujo wa awali kuwania nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Waliopitishwa ni kuwania uenyekiti wa Kamati ya Uongozi (Management Committee) ni Clement Sanga na Ahmed Yahya wakati Shan Crysostoms ameiptishwa kuwania nafasi ya makamu mwenyekiti. 

Kwa mujibu wa kamati hiyo, Ramadhan Mahano na Hamisi Madaki wamepitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. James Bwire na Almas Kasongo wamepitishwa kuwania Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu hakuthibitishwa na klabu yake. 

Edga Chubura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni marais au wenyeviti wa klabu husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti au Marais wa klabu husika. Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee. 

Uchaguzi huo wa kamati hiyo utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017 jijini Dar es Salaam na unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013. 

MCHUNGAJI KUTOKA NCHINI GHANA KUTOA HUDUMA KWA SIKU TATU KATIKA KANISA LA PURE FIRE MIRACLES LILILOPO TABATA SEGEREA.

$
0
0
MWAZILISHI na mchungaji Mkuu wa kanisa  la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International'), lililopo Tabata Segerea kwa Bibi
,Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana amewasili hapa kwaajili ya
  kuwaletea siku tatu za huduma ya ujazo wa upako.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha hapa nchini mchungaji huyo kutoka nchini Ghana, Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwu amesema kuwa wananchi wajitokeze ili kupata maada mbalimbali za ukombozi na mafanikio.

Amesema huduma zitatolewa kwa siku tatu kuanzia leo Jumanne saa 11:00 jioni hadi alhamisi ambapo wahapingani kabisa na muda wa kazi hapa nchini kutokana na muda huo watu wengi watakuwa wametoka makazini.

Huduma hiyo itatolewa kwa lengo la kusaidia wanachi wenye matatizo mbalimbali, ili kupata upanyaji na kumtumaini Mungu,pamoja na Ukombozi na Mafanikio ambapo wanawaalika watu mbalimbali kuhudhulia mkutano huo ambapo mtoa maada katika siku tatu mfululizo ili kujipatia huduma za ukombozi na mafanikio.
 Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuwasili katika Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi jijini Dar es Salaam.
 Mchungaji Mwenyeji, Innocent Ikechukwuakizungumza wakati wa kumkaribisha  Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada alipo wasili kanisani hapo jijinio Dar es Salaam leo.
Pia amemshukuru kwa kuitikia wito wake kuja hapa nchini kutoa huduma ya neno la Mungu pamoja na ukombozi wa Mafanikio ya wanajamii watakao hudhuria katika huduma kanisani hapo.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Moto halisi (Pure Fire miracles Ministries International') lilopo Tabata Segerea kwa Bibi wakimuaga Mkuu wa Kanisa hilo, Dk. Enoch Aminu kutoka nchini Ghana mara baada ya kufika na kuongea na waumini hao.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI, KARANI WA MARAZA MAREHEMU HASSAN RASHID SHEBUGE AKUMBUKWA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi pamoja na mawaziri wakisimama kwa heshima kumkumbuka aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Marehemu Hassan Rashid shebuge aliyefariki mwezi Julai mwaka huu, kabla ya kuanza kwa kikao hicho kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha baraza la Mawziri kulu jijini Dar es salaam leo Agosti 29, 2017.

WATU SITA WAFARIKI KWA AJALI YA LORI KIJIJI CHA KATIKA KIJIJI CHA KIJOTA, SINGIDA.

$
0
0
Watu sita wamefariki dunia huku wengine 42 wakijeruhiwa baada ya lori lenye namba za usajili T.806 AEL aina ya scania mali ya Abdalla Mussa (39) mfanyabiashara mkazi wa Mwenge mjini Singida, kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Kijota, Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema ajali hiyo imetokea Agosti 27 mwaka huu saa 1.30 usiku katika kijiji cha Kijota wakati likitokea mnadani katika kijiji cha Mtinko Singida vijijini, likielekea Singida mjini.

ACP Magiligimba ametaja chanzo cha ajali kuwa ni uzembe wa dereva wa lori hilo Jumanne Kidanka (32) Kamanda huyo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva ambaye hakuwa makini akiwa anaendesha lori hilo lililosheheni abira na mizingo mingi.

Amewataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Haji Jumanne (35), Mikidadi Mohammed (40) wote wawili wakazi wa kijiji cha Mrama na Musa Salimu (30) mkazi wa kijiji cha Mwakiti.

ACP Magiligimba amewataja wengine kuwa ni Allen Mwangu (38) mkazi wa wilaya ya Ikungi, Lucas Stephano (40) mkazi wa kijiji cha Mrama na Sharifa Omari (19) mkazi wa kijiji cha Ilongero.

Ameongeza kuwa majeruhi 20 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida, kumi wamelazwa hospitali ya misheni ya Mtinko na wanne ambao hali zao ni mbaya, wamelazwa katika hospitali ya misheni ya Hydom mkoani Manyara.

Ameeleza kuwa baadhi ya majeruhi walipatiwa matibabu na kurejea makwao huku wengine waliolazwa wamevunjika mikono, miguu na sehemu mbalimbali ya miili yao.

“Hawa wenye hali mbaya ni Fadhili Jumanne (33) mkazi wa Kibaoni mjini Singida, Mikidadi Hamisi, Jafari Hamisi na Idrisa Ibrahimu, wote wamevunjika miguu. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali misheni Mtinko”, amesema.
 Mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
 Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa huku akiendelea kupatiwa matibabu ya mkono katika hospitali ya Mkoa wa Singida mara baada ya kupata ajali ya lori iliyoua watu 6 katika kijiji cha Kijota Singida.
Baadhi ya ndugu na jamaa wa majeruhi wa ajali ya lori iliyoua watu sita wakiwa nje ya wodi za wagonjwa katika hospitali ya Mkoa wa Singida.

NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, ASISITIZA UKUSANYAJI WA MAPATO YA ARDHI NA MAJENGO

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akikagua mafaili kwenye ofisi za Ardhi za Wilaya hiyo. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akiangalia ramani ya Kijiji cha Bukandwe ambacho kipo kwenye Wilaya ya Mbongwe Mkoani Geita. Mkuu wa Wilaya ya Bukombe ,Josephat Maganga akisoma taarifa fupi ya Wilaya ya Bukombe kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akikagua na kupatiwa maelezo na afisa ardhi mteule Joseph Kimondo .

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DIMBA MUSIC CONCERT INAKULETEA MPAMBANO WA NGUVU

Viewing all 110105 articles
Browse latest View live




Latest Images