Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA JUKWAA LA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI NA MFUMO MPYA WA HUDUMA ZA KIBENKI WA CRDB LEO JIJINI DAR

$
0
0

  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan ( wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na Viongozi waandamizi wa benki ya CRDB ,mara baada ya kuzindua  Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,uliofanyika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijini Dar es salaam.
  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan ( wa pili kulia) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na Viongozi waandamizi wa benki ya CRDB ,akizindua mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,uliofanyika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijini Dar es salaam.
  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,uliofanyika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijini Dar es salaam.
  Mgeni rasmi  Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan  akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya kuzindua  Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililokwenda sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,uliofanyika katika viwanja vya Posta-Kijitonyama mapema leo jijini Dar es salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB,Dkt Charles kimei akizungumza na kumshukuru Mgeni rasmi ,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,viongozi mbalimbali wa serikali na wageni waalikwa kwa ujumla,katika suala zima la kufanikisha uzinduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi uliokwendaa sambamba na uzinduzi wa mfumo mpya wa huduma za kibenki kwa njia ya simu wa SimAccount,katika viwanja vya Posta-Kijitonyama jijini Dar es salaam. Habari zaidi BOFYA HAPA

TUNAISHUKURU SERIKALI YA CUBA KWA KUTAMBUA MASHUJAA WA AFRIKA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya Cuba kwa kutambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa wa ukombozi wa Bara la Afrika, akiwemo Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuwajengea mnara wa kumbukumbu.

Mnara huo umejengwa katika Manispaa ya Playa jijini Havana kwenye eneo maalumu la makumbusho ya mashujaa hao walioshiriki katika ukombozi wa Afrika, ambapo zimewekwa sanamu zao pamoja na maelezo mafupi ya historia zao na nchi wanazotoka.

Waziri Mkuu alifanya ziara katika eneo hilo jana (Ijumaa, Agosti 25, 2017) na kuweka shada la maua katika mnara huo uliozungukwa na sanamu za mashajuaa wa Bara la Afrika na kuoneshwa sehemu itakayowekwa sanamu ya Mwl. Nyerere.

Akiwa katika eneo hilo, Waziri Mkuu aliishukuru Serikali ya Cuba kwa kujenga makumbusho ya mashujaa hao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana na Cuba kuhakikisha kuwa sanamu ya Mwl. Nyerere inawekwa katika sehemu iliyotengwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Instuto Cubano De Amistad Con El Pueblo (Taasisi ya Ushirikiano wa Cuba na Nchi Marafiki), Bw. Jose’ Prieto Cintado alisema mnara huo umejengwa kwa lengo la kutambua thamani na umuhimu wa viongozi hao.

Mkurugenzi huyo alisema Serikali ya Cuba inathamini mchango mkubwa uliotolewa na mashujaa hao katika vita ya ukombozi wa Bara la Afrika, ambapo iliamua kujenga mnara wa kumbukumbu katika nchi yao.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. kushoto , akiwa na mwenyeji wake kulia ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .August 25/2017 wakiangalia Sanamu ya aliyekuwa Raisi wa Msumbiji Hayati Samora Masheli ambayo ipo katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliopo Havana Cuba Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .kulia pamoja na Mama Mary Majaliwa ,kushoto pamoja na mwenyeji wao katikati ambaye ni Mkurugenzi wa Maswala ya Africa Nnchini Cuba .Balozi Jose Prieta Cintado .wakiweka Shada la Maua August 25/2017 katika Makumbusho ya Mashujaa wa Africa yaliyopo Havana Cuba .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

TBS yapewa tuzo na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kusaidia wajasiriamali

$
0
0
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limepata tuzo na kushika nafasi ya pili kwa taasisi za kiserikali zinazosaidia wajasiriamali wadogo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mkuu wa TBS Profesa Egid Mubofu alisema tuzo hiyo intoka Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC), katika mwaka wa fedha 2016/2017 TBS na wameshika nafasi ya pili kwa taasisi zinazosaidia wajasiriamali kujimudu kiuchumi.
“Tuzo hii ni chachu kwetu, inatukumbusha kufanya kazi zaidi kwa ajili ya kuiua wajasiriamali wadogo. Hivyo tunawakumbusha wajasiriamali waje kwa wingi nasi tupo tayari kuwasaidia ili azma ya serikali ya viwanda itimie,” alisema Profesa Mubofu na kuongeza:
“Shirika limekuwa likitenga fedha kwa ajili ya kuwahudumia wajasiriamali wadogo, kwa mwaka huu tumetenga kiasi cha Sh milioni 100 kwa ajili hiyo.”
Akizungumzia utaratibu huo unavyofanya kazi Profesa Mubofu alisema: “Tunawasaidia wajasiriamali kupata alama ya ubora bila kulipia gharama yoyote. Utaratibu huu umekuwa ukifanyika kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).
“Ambapo mjasiriamali hutakiwa kwenda SIDO kupewa elimu ya msingi ya uzalishaji kisha anatambulishwa kwetu ili tuendeleze elimu na pia kumsaidia katika kuanzisha na kukuza kiwanda. TBS tunamgharamia mjasiriamali huyo kila kitu kuanzia ukaguzi hadi kumpatia leseni ya kutumia alama ya ubora.”
Aidha, wajasiriamali wadogo wanafanikiwa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora kupitia mpango huu huendelea kuhudumiwa bure  na shirika kwa kipindi cha miaka mitatu: “kuanzia mwaka wan ne watatakiwa kuchangia asilimia 25 ya malipo, mwaka wa tano asilimia 50 na mwaka wa sita asilimia 75 hadi ikifika mwaka wa saba watatakiwa kulipia asilimia 100 ili kupata fursa ya kusaidia wajasiriamali wanaochipukia.”
Vilevile ili kuimarisha na kurahisisha utendaji kazi katika mkakati huu, TBS na SIDO wanatarajia kusaini hati ya makubaliano ili kurahisisha utendaji kazi wa kuwahudumia wajasiriamali.
TBS kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakishirikiana na taasisi na mamlaka nyinyine za kiserikali  kuhakikisha wajasiriamali wadogo wanaanzisha viwanda vidogo kabisa, vidogo na vya kati ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe na uchumi wa kati utokanao na viwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Prof. Egid Mubofu akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kufuatia kupata tuzo iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) kutokana na mchango wa Taasisi hiyo katika kuchangia maendeleo na uakuaji wa wajasiriamali nchini jijini Dar es Salaam.

COCO BAND YAWAPA RAHA MASHABIKI WA MUZIKI WA TANZANIA JIJINI KAMPALA

BODI YA CHAKULA DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAHARIBU BIDHAA MBOVU NA ZILIZOPITWA NA MUDA WAKE

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo 

Wafanyabiashara wa Zanzibar wanaoagiza bidhaa kutoka nje wametakiwa kuwa waadilifu na kuwahurumia wananchi wenzao wakati wanaponunua bidhaa kwa kuangali ubora na kuacha tabia ya kuchukua bidhaa dhaifu zenye bei ndogo kwa lengo la kutafuta faida kubwa.
Mkuu wa Kitengo cha ufuatiliaji madhara ya chakula kutoka Bodi ya Madawa na Vipondozi Zanzibar Bibi Aisha Suleiman alitoa ushauri huo wakati bodi hiyo ilipofanya zoezi la kuangamiza tani 27.5 za mchele ulioharibika na chakula mchanganyiko kilo 400 kilichomaliza muda ikiwemo tende na juice katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Unguj.
Bi. Amina ambae alikuwa msimamizi mkuu katika zoezi hilo alisema mchele ulioharibika uliingizwa nchini na Kampuni ya Zenj General Machandise na uliingia maji wakati wa kusafirishwa na chakula kilichomaliza muda wa matumizi kiligundulika katika maduka mbali mbali ya Zanzibar baada ya kufanyika ukaguzi katika maduka hayo.
Alisema kwa mujibu wa sheria bidhaa zinapoharibika wakati wa kusafirishwa na ikagundulika wakati wa ukaguzi bandarini kabla ya kuingia sokoni mmiliki wa bidhaa hiyo huwa hanakosa na hulazimika kutoa gharama za kuangamiza bidhaa hiyo yeye mwenyewe.
Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar wakishusha bidhaa zilizoharika katika Dampo la Kibele tayari kwa kuangamizwa.
Moja ya gari lililobeba mchele ulioharibika likishushwa na Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Unguja.
Gari la kijiko kutoka Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano likiangamiza mchele tani 27.5 ulioharibika katika Dampo la Kibele Mkoa Kusini Ungua.


Picha na Makame Mshenga.

PROFFESA MSAMBICHAKA ASISITIZA NIDHAMU KWA WANAFUNZI NA WALIMU ILI KUINUA ELIMU WAKATI AKIZINDUA KAMPENI YA 3D

$
0
0
WALIMU, Wanafunzi na Wafanyakazi katika shule mbalimbali wametakiwa kuzingatia nidhamu shuleni ili kuweza kuchochea maendeleo ya ufaulu kwenye shule zao.Wito ulitolewa jana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist iliyopo Boko Basihaya jijini Dar es Salaam, Aspiter Kibona wakati wa mahafali ya 10 ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya '3D' yenye maana ya !Nidhamu, Nidhamu, Nidhamu!.

Kibona alisema wameamua kuzindua kampeni hiyo ikiwa ni kauli mbio yao kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na walimu na wafanyakazi wengine kuzingatia nidhamu muda wote ambayo itaendelea kuchochea maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
"Nidhamu si kwa wanafunzi pekee bali inatakiwa kuanzia hata kwangu mimi mkuu wa shule pamoja na walimu na wafanyakazi wengine katika shule yetu hii, hivyo tumezindua kampeni hii ikiwa ni kauli mbio yetu ya kuendelea kuhamasisha nidhamu katika shule yetu kwa nia kuendelea kuchochea maendeleo ya wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao darasani, " alisema Kibona.
Alisema nidhamu inapoanzia kwa viongozi wa juu, walimu na wafanyakazi wengine inasaidia nidhamu hiyo hiyo kuingia hadi kwa wanafunzi ambayo inawachochea kufanya vizuri katika masomo yao darasani.

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo, Jalia Mayanja aliwataka wahimu 53 wa kidato cha nne kuzingatia nidhamu mahali popote watakapokuwa mara baada ya kutoka shuleni hapo kwa faida yao ya huko waendako.

Mayanja alisema nidhamu ndiyo siri ya mafanikio ya shule hiyo katika ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.Alisema ni vema wahitimu hao wa kidato cha nne wakaendeleza nidhamu waliyokuwa wakiionyesha shuleni hapo huko wanapokwenda ili iweze kuwasaidia katika maisha yao ya baadae.Aliongeza kwa kuwataka wazazi wanaopeleka watoto wao katika shule hiyo kukaa kwa amani kutokana na kwamba wapo katika mikono salama.

Article 19

$
0
0
Walete watoto wafurahi wakati wa Mkulima Soko na Sikukuu ya Eid kuanzia 30 Agosti hadi 2 Septemba 2017 kwenye Maegesho ya Magari ya Research Flats, mbele ya Jengo la Ndaki ya Kilimo na Teknolojia za Uvuvi (CoAF) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.A

SIMBACHAWENE AAGIZA BARABARA YA LUMUMA-MBUGA MPWAPWA ITENGENEZWE KWA KIWANGO KINACHOTAKIWA.

$
0
0

Na Fred Kibano, Mpwapwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B. Simbachawene (Mb) amemwagiza Msimamizi wa Wakala wa barabara za Vijijini (TARURA) Mhandisi Geophrey Mwamkinga kuhakikisha barabara ya Lumuma hadi Mbuga wilayani Mpwapwa inatengenezwa kwa kiwango kinachotakiwa na kwa thamani halisi ya fedha za Serikali.

Mheshimiwa Simbachawene ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kutembelea Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya vijiji kujionea maendeleo ya vijiji katika sekta za Afya, Elimu, Maji, Ardhi na eneo la Utawala bora ngazi ya vijiji.

Amesema Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kampuni ya M/S Besta Holding Co Ltd ya Jijini Dar es Salaam bado haijafanya kazi nzuri ijapokuwa ujenzi wake umefikia asilimia 70 kwani wembamba wa barabara hiyo ambao hauruhusu magari kupishana, kuwa na mitaro midogo ya kutupa maji, uvunjaji wa miamba kwa mita chache pembeni mwa barabara hiyo ya milima ya Kizi haujafanyika ipasavyo, ikiwa ni pamoja na mitaro ya kinga mita kwa pembeni na kujaza kifusi ambacho hakitelezi.

“Kwa hiyo, barabara lazima itanuliwe, mlima huu hapa hakati, huyu jamaa (Mkandarasi), anagusagusa tu lakini hakati, Yule mwenzake wa kule Wotta (kata nyingine wilayani Mpwapwa) anakata, tena ni jiwe tu kutoka chini, yeye huyu ni udongo anafanya hivi, lakini hakati (mlima kwa upande wa pembeni), hivi vifereji ni utapeli mtupu, hivi vifereji wakati wa mvua vitaondoka vyote kwa sababu hujaandaa vizuri njia yenyewe, ukijenga mfereji unacheza (ni kama utani)”

Barabara ya kata za Lumuma na Mbuga yenye urefu wa kilomita 21 inahusisha matengenenezo makubwa, ni barabara ya siku nyingi ambayo haikuwahi kuwa chini ya Halmashauri ambapo ni wananchi pekee na Wamisionari wa Kanisa katoliki ndio walioianzisha na kuikarabati kuweza kupita kwa shughuli zao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George B. Simbachawene (Mb) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Geophrey Mwamkinga na Wataalam wengine juu ya marekebisho ya barabara ya Lumuma hadi Mbuga yenye urefu wa kilomita 21 ambapo alimtaka kuchukua hatua kwa mkandarasi kampuni ya M/S Besta Holding Co Ltd ya Jijini Dar es Salaam kufanya marekebisho ya upanuzi wa barabara, kumwaga kifusi kisicho tereza, kujenga kingo imara za barabara na marekebisho maalum sehemu korofi kabla ya msimu wa mvua. 

RC TABORA: MA-DED NUNUENI VIFAA VYA KUPIMIA UBORA WA UDONGO ILI KUWASAIDIA WAKULIMA

$
0
0
Na  Tiganya Vincent – TABORA

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Manispaa na Halmashauri kuhakikisha wanawanulia Maafisa Ugani vifaa vya kupimia ubora wa udongo(soil kits ) kwa ajili ya kuwawezesha kutoa huduma ya ushauri kwa wakulima ili waendeshe kilimo kulingana na hali ya udongo wa eneo husika.

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya siku saba ya Maafisa Ugani kutoka Halmashauri zinazolima zao la tumbaku kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutoa huduma nzuri kwa wakulima. Alisema kuwa vifaa hivyo ni lazima vinunuliwe walau vichache vya kuanzia ili Maafisa Ugani katika ngazi za kuanzia kijiji hadi Kata waweze kuwasaidia wakulima juu ya matumizi sahihi ya pembejeo ikiwemo mbolea katika udongo husika kwa ajili kuwafanya wazalishe mazao mengi.

Mwanri aliongeza kuwa wakulima wamekuwa hapati mafanikio wakati mwingine kwa sababu ya kukosa wataalamu wa kuwashauri jinsi ya kuendesha kilimo cha kulingana na udongo walionao katika eneo lao na matumizi sahihi ya pembejeo kulingana na hali halisi ya udongo.

“Vifaa hivyo vitasaidia wao kujua ni virutubisho gani vinapungua katika udongo na hivyo waweze kumshauri mkulima jinsi ya kuongeza virutubisho hivyo ili apate mafanikio na kuachana na kilimo cha kukisia katika matumizi ya pembejeo”alisisitiza Mkuu wa Mkoa huyo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAENDESHA BODABODA WOTE KUNUNUA KOFIA NGUMU NDANI YA MWEZI MMOJA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza waendesha bodaboda wote nchini kuhakikisha kuwa wanakuwa na kofia ngumu ‘Helmet’ ndani ya mwezi mmoja baada ya hapo hatua kali zitachukuliwa. 

Mheshimiwa Nchemba ametoa agizo hilo jana Agosti 26,2017 mjini Shinyanga wakati akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli 'daladala' zaidi ya 300 wanaofanya shughuli zao katika manispaa ya Shinyanga. 

Alisema kosa la kutovaa kofia ngumu litawahusu wamiliki wa bodaboda,waendesha bodaboda pamoja na abiria ambao kwa pamoja watawajibika kila mmoja kwa nafasi yake. 

“Hili litafsiriwe vizuri kila eneo katika nchi yetu,kwanza kabisa kama mmiliki hajaweka kofia mbili,bodaboda ikikutwa haina kofia mbili,tatizo lile linaenda kwa mmiliki,pili kama mwendesha bodaboda amepewa kofia mbili halafu akaamua kuziacha huyo ana kosa”,alieleza. 


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli 'daladala' jana mjini Shinyanga.Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule.Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho.
Mkazi wa Shinyanga Mjini akieleza shida yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba baada ya kikao kufungwa.


CAR BUYERS AND SELLERS TO SAVE MILLIONS AS LOCAL INNOVATION DISRUPTS TANZANIAN VEHICLE MARKET

$
0
0
 Autofair is a weekly Sunday market that will be held at Mlimani City every Sunday from 07h30 to 16h00 from 27 August 2017. Autofair presents a space where individuals can sell and buy vehicles directly from each other. Only a small fee of TZS20,000 is paid by the seller to exhibit their vehicle. Buyers can come and select their dream car from the cars on display and entry is free for buyers. The benefits to the seller is that they can see many serious buyers all at once. 
Buyers will benefit by being able inspect the vehicle, save time by not having to drive around town in search of a vehicle. Savings on Both Sides. A great feature of a deal between a buyer and a seller of a car at Autofair is that the middleman will be cut out of the transaction. 
This means that the seller can now achieve more in return for his vehicle and at the same time the buyer will pay less. This means of transacting maximizes the transaction for both the buyer and the seller. Only the commission agent will not benefit from this transaction. Said Erica Msenga, Operations Manager of Autofair Tanzania, “We are very excited to provide a space where citizens of Dar es Salaam can come and buy or sell vehicles, cut out the middle man and save time and money. This innovation will become a weekly institution of the City.” The weekly Autofair will be held in the grounds of the Mlimani City shopping centre. The benefit of the venue is that it is central and well known in Dar es Salaam. There is also very little traffic on Sunday so buyers and Sellers should easily be able to attend the Autofair whilst at the same time having time for their other Sunday activities. 
 Pastory Mrosso General Manager of Mlimani City Holdings remarked “Mlimani City Holding is proud to be associated with this weekly event; not only will the Autofair bring add more variety to the shopping experience on offer at Mlimani City on Sunday but we also believe that this event will make Mlimani City the premium destination for buyers and sellers of cars in Dar es Salaam” Autofair has an affiliation with Kupatana.com. thorough this affiliation, buyers will be able to have their vehicle advertised on the Kupatana platform and at the same time sellers will be able to see what vehicles are available online. 
Mark Tesha of Kupatana.com said “Kupatana finds that Autofair provides a perfect meeting place for serious buyers of sellers of cars. Now you can find your car on Kupatana and then finalise the deal on Sunday at Autofair.” Buyers and sellers are urged to come every Sunday to Autofair at Mlimani City between 07h30 and 16h00. It is expected that at least 20% of all vehicles on offer will be sold each week. For more information please visit www.Autofair.co.tz. Autofair Tanzania can also be found on Facebook and Instagram. Direct enquires can be directed to +255 712 2120 19.

DKT. SHEIN KATIKA HAFLA YA KUCHANGIA MFUKO WA MAENDELEO YA UWT ZANZIBAR.

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika hafla ya Chakula cha Hisani kuchangia Mfuko wa maendeleo ya UWT Zanzibar iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 27/08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika hafla ya Chakula cha Hisani kuchangia Mfuko wa maendeleo ya UWT Zanzibar iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 27/08/2017.
Baadhi ya Viongozi mbali mbali na Wafanyabishara waliohudhuria katika hafla ya Chakula cha Hisani kuchangia Mfuko wa maendeleo ya UWT Zanzibar iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja,mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 27/08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akipokea zawadi maalum kutoka kwa Dkt.Maua Abeid Daftari Mwenyekiti wa kamati ya kuhamasisha uchangiaji wa mfuko wa maendeleo ya UWT katika hafla ya Chakula cha hisani cha kuchangia Mfuko wa maendeleo ya UWT Zanzibar katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja jana,[Picha na Ikulu.] 27/08/2017.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

:DC TUNDURU APIGA MARAFUKU NGOMA ZA UNYAGO.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Tunduru JUMA HOMERA ,amepiga marafuku kwa wazazi wote kuto kujihusisha na masuala ya kimila hususani katika kushiriki ngoma za usiku hali inayopelekea kutokea kwa mimba za utotoni.

MFUKO WA MAENDELEO WA JUMUIYA YA UWT ZANZIBAR WACHANGIWA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein iliyochorwa ikipigwa mnada kwa Viongozi na Wafanyabiashara mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya Kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya UWT Zanzibar iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 26/08/2017.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitia saini Picha yake iliyochorwa ambayo ilipigwa mnada kwa Viongozi na Wafanyabiashara mbali mbali na kununuliwa kwa shingi za Kitanzania Milliomi tatu,ambayo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mecco Bw.Abdukadir Mohamed Bujet (kulia) ameinunua picha hiyo katika hafla ya Kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya UWT Zanzibar iliyofanyika jana katika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akikabidhi Picha ya Mji wa Zanzibar Kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ikiwa ni miongoni mwa Picha mbali mbali zilizopigwa mnada kufanikisha kuchangia Mfuko wa maendeleo ya UWT Zanzibar hafla iliyofanyika ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Unguja,(kushoto) Mama Asha Suleiman Mke Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

DKT MAHENGE KUWAFUNDA MAAFISA UGANI MKOANI RUVUMA.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma DKT BILINITH MAHENGE amewataka wadau wa kilimo na mafisa ugani kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi juu ya uzalishaji wa zao la soya ambalo limeonekana kuwa na tija katika mikoa ya mbeya,njombe na ruvuma kutokana na hali ya hewa iliyopo katika mikoa hiyo.

KUNDI LA NYOTA YA ASUBUHI KUNOGESHA WIMBO WAO NA CHRISTIAN BELLA

WIZARA YA ARDHI YATAMBULISHWA NA KOREA MRADI WA KUCHORA RAMANI ZA KIJIOGRAFIA

$
0
0
Ugeni wa Wakorea, kutoka Taasisi ya Taifa ya masuala ya kijiografia umetambulisha rasmi mradi wa kuchora ramani za kijiografia kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Ugeni huo uliopokelewa na Idara ya Upimaji na Ramani katika Wizara ya Ardhi, umehusisha timu ya Maafisa kumi kutoka nchini Korea. Akizungumza na wawakilishi wa Idara ya Upimaji na Ramani; Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Taasisi hiyo; Bwn. Hynu-Hee Joo amesema mradi huo unaojumuisha nchi tatu, yaani Tanzania, Zambia na Msumbiji unategemewa kuanza rasmi 2018.

Mradi wa kuchora ramani za kijiografia upo chini ya ufadhili wa nci ya Korea kupitia Benki ya Dunia na Umoja wa Kamisheni ya Afrika.

Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 Timu ya utambulisho wa Mradi wa kuchora Ramani za kijiografia kutoka Korea na baadhi ya watendaji wa Idara ya Upimaji wa Ramanni (Wizara ya Ardhi) katika Mkutano wa utambulisho wa Mradi. 
Ugeni kutoka Taasisi ya Taifa ya Kijiografia- Korea, waliofika kutambulisha Mradi wa kuchora Ramani za kijiografia utakaoanza 2018, katika picha ya pamoja na baadhi ya watenfaji wa Wizara ya Ardhi.

MPOGORO AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA MAKATIBU WA UVCCM MIKOA YA TANZANIA BARA NA VISIWANI.

$
0
0


Naibu katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi ndugu Rodrick mpogoro akifungua Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam.
Mwenyekiti wa umoja wa Vijana na mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Ndg:Sadifa Juma khamisi akizungumza katika Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam
Kaimu katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaam

washiriki wa mafunzo elekezi wakifuatilia mafunzo
mshiriki Katibu wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa kirimanjaro ndg; abdulrahim hamid akiuliza swali wakati wa Mafunzo elekezi kwa makatibu wa umoja wa Vijana wa CCM mikoa ya Tanzania bara na Visiwani katika ukumbi wa kamati kuu ofisi ndogo ya Ccm Lumumba dar es salaa.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI WAKATI AKITOROKA MKOANI SINGIDA.

$
0
0
Mkazi wa kijiji cha Shiponga – Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.

Amefafanua kuwa Hamisi (marehemu) alipigwa risasi na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka mara baada kuonyesha bunduki aina ya rifle yenye namba 7358 na risasi zake tano.

Amesema bunduki hiyo iliyokuwa imekatwa mtutu na risasi zake tano zilikuwa zimefichwa kwenye soksi, vitu hivyo vilikuwa vilihifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi, na kufichwa chini ya jiwe.

ACP Magiligimba amesema Agosti 23 mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na wananchi wa kijiji cha Ngamu, na kufikishwa katika kituo cha polisi cha kijiji hicho kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya ujambazi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba akionyesha bunduki aina ya rifle iliyokuwa ikimilikiwa na mtuhumiwa wa ujambazi Hamisi Athumani (32) mkazi wa Shiponga-Hanang mkoa wa Manyara anayedaiwa kuitumia kwenye matukio ya ujambazi. 
Picha/habari na Nathaniel Limu.

VIDEO Tribute: ZURIELS FILM PREMIER - "FOLLOW THE BALL" AT HILTON ABUJA IN NIGERIA

$
0
0
Los Angeles - CA
August 25th

As a globally recognized Girl Education Advocate and known as the worlds youngest film maker in many quarters, newly minted 15 year old Zuriel Oduwole has premiered her fifth film - but the second for the big screen in Abuja - Nigeria, following the success of her 2014 release - "A Promising Africa", which showed at Genesis Deluxe in Lekki and Film House Cinema in Surulere, before screening in Ghana, South Africa, the United Kingdom and Tokyo - Japan.
Attended by dozens of children, youths and representatives from governments, groups and private sector leadership, including several Ambassadors and their wives, Ford Foundation, Dangote, Tony Elumelu and 2 Governors Offices and the Nigerian Presidency, it capped her three year journey of making the film, which was shot across 5 countries [Brazil, Ethiopia, Nigeria, Mauritius and the US] on 3 continents.
It is the story of ONE girl taking TWO footballs across THREE continents and through FIVE countries, traveling 29000 miles to get the message of Girls Education out, with filming commencing during the 2014 FIFA World Cup in Brazil. The footballs were signed by people from more than 35 nationalities, and included Football Players, Pilots, Ambassadors, Governors, Football Fans, a First Lady, a Nobel Prize Winner, Corporate CEO's and ordinary people, wanting to make their voices heard.
Already critically acclaimed, the colorful film premier event at the Hilton Hotel saw speeches and tributes from several groups and supportive interests/stakeholders. One of the musical tributes was from Kenya Pop Group and winners of an MTV 2016 Award - SAUTI SOL.
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images