Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


RC Rukwa Azuia Tani 2143 Za Madini Kuuzwa Nje ya Nchi

0
0



Katika kasi ya kuhakikisha madini ya watanzania yanawafaidisha watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amekamata na kuzuia uuzwaji wa tani 2,143 za madini aina ya “Clinker” yanayotumika katika kuzalishia saruji kutokana na wingu la ubabaishaji uliogubika usafirishaji wa madini hayo kwenda nje ya nchi hadi hapo atakapojiridhisha na utaratibu wa uuzwaji huo.

Sakata hilo liliibuka baada ya Mh. Zelote kufanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Kasanga Iliyopo Wilayani Kalambo mpakani na nchi ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kupitia Ziwa Tanganyika.

Usafirishaji wa madini hayo umekuwa ukifanywa na kampuni ya Mbeya Cement ya jijini Mbeya tangu mwezi wa pili mwaka 2017 kuiuzia kampuni ya Burundi Cement ya jijini Bujumbura, ambapo mpaka Mh. Zelote anazuia uuzwaji huo, tayari walikuwa wameshauza tani 4,760 huku tani moja ikiuzwa kwa dola za kimarekani 128.

Wakati Mh. Zelote akiendelea na ukaguzi katika bandari hiyo aligundua kuwa kampuni hiyo ya Mbeya Cement ina mzigo wa tani 2050 za mifuko ya saruji iliyopo bandarini hapo tangu mwezi November mwaka 2016 na alipoulizwa mwakilishi wa Kampuni hiyo ya Mbeya Sabas Sokoni alisema kuwa Saruji hiyo imekosa wateja.

“Sisi tunajuwa kwamba bandari hii inapokea Simenti na kuuzwa nchi za jirani, haya ni madini, Haiwezekani tukadanya kwamba tunapeleka madini kumbe tunapeleka “raw materials” kutoka Tanzania kwajili ya kutengeneza simenti, kila siku tunazungumza suala la kuongeza thamani ya vitu vyetu ili tuuze “finished products” na sio “raw materilas.” Mh. Zelote alisema.

Na kuongeza kuwa Utaratibu uliopo ni kwamba Simenti inazalishwa Tanzania na kuuzwa nje ya nchi na sio utaratibu wa kusafirisha udongo wa kutengenezea Simenti na kuhoiji kuwa kwanini udongo huo uwe na soko zaidi kuliko Simenti yenyewe. 

Wakati Mh. Zelote akitoa zuio hilo tayari tani 800 zilikuwa zimo kwenye meli ya MV Tora yenye namba za usajili BY 0064 huku ikiwa na bendera ya Burundi.

Kwa upande wake afisa wa bandari hiyo Suleiman Kalugendo hakuona tatizo mbali na vibali vya usafirishaji wa madini hayo kuwa na mashaka.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA KIWANDA CHA DANGOTE

0
0
Mtaalam kutoka Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ya GASCO inayojihusisha na usambazaji wa gesi, Mhandisi Mwanaidi Rashid (kulia) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kituo Namba I cha gesi ambapo Kiwanda cha Saruji cha Dangote kitaunganishwa na huduma hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa tatu kutoka kulia mbele) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia ( wa nne kutoka kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na kamati hiyo wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (kulia) akimpokea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) aliyeambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uzalishaji wa Saruji cha Dangote, Hemendra Raithatha (kulia) akielezea mafanikio na changamoto za kiwanda hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti (hawapo pichani). Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Jaji Mstaafu Josephat Mackanja.

MBUNGE RITTA KABATI APOKEA KERO ZA WENYEVITI WA MITAA 192 YA MANISPAA YA IRINGA

0
0

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wenyeviti wa mitaa 192 katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wamelalamikia ufinyu wa posho wanayopata ukilinganisha na kazi wanazozifanya kuwatumikia wananchi kwa kuleta maendeleo.

Wakizungumza wakati wa mkutano mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wa kutoa kero zao na changamoto zinazowakabiri katika uwajibikaji wa majukumu yao huko mitaani.Wevyeviti hao walisema kuwa wamekuwa wakicheleweshewa posho zao toafauti na viongozi wengine na kuwasababisha kutofanya kazi kwa weledi wao unaotakiwa kwa kufikisha huduma stahiki.

Lakini wenyeviti hao walisema kuwa viongozi wa halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa kero kwao kwa kutowasaidia kutatua changamoto na migogoro zilizopo kwenye mitaa hao.

"Huku mitaani watoto wadogo wanabakwa hovyo ukipeleka kesi polisi wanadai ushaidi haujakamilika na watuhumiwa wanakuwa nje kwa dhamana kitu kinachosababisha kudhohofisha utendaji wa kazi zao,mitaani kwenu kunawizi unaendelea lakini bado viongozi wa polisi wamekuwa kero kwa kutotatua kero hizo na swala jingine ni wenyeviti kudharauliwa na watumishi wa manispaa ya Iringa "walisema wenyeviti
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza na wenyeviti wa mitaa yote ya manispaa ya Iringa wakati wa kusikiliza kero zinazowakabili viongozi hao wakati wa utendaji wao huko wenye mitaa yao. 
Hawa ni baadhi ya wenyeviti wa mitaa ya halmashauri ya manispaa ya Iringa waliohudhuria mkutano huo wa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta kabati 


MBUNGE MUSSA NA MKEWE WASHIRIKI ZOEZI LA MSARAGAMBO WA MTARO KATA YA MAWENI JIJINI TANGA

0
0
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni ambao utapitisha maji kutoka Pongwe
 Mke wa Mbunge wa Jimbo la Tanga nae akishiriki zoezi la Uchimbaji wa mtaro huo
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kichangani Kata ya Maweni wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea na kushiriki nao uchimbaji wa mtaro wa kupitishia maji
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.

Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.

Dkt. Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu. Alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika jamii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017.

 Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.
Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.

STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO

0
0
Wakati pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017-2018 likitarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Agosti 27, mwaka huu kwa timu zote 16 kuingia viwanjani,Kampuni ya Michezo ya Bahati Nasibu Mtandaoni – BIKO imeidhamini Klabu ya Stand United ‘Chama la Wana’ shilingi milioni 100 kuanzia mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Ijumaa,Agosti 25,2017mjini Shinyanga, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele (CCM) alisema BIKO wameamua kuidhamini timu hiyo baada ya kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo. 

“Baada ya Stand United kupoteza mwelekeo na wadhamini wake Kampuni ya Acacia kujiondoa katika udhamini,hivi sasa nimeamua kuwa msimamizi mkuu wa timu hii,nimetafuta udhamini mwingine,nimeiomba kampuni ya Kitanzania ya BIKO,imekubali kuwa wadhamini wakuu na imetupatia shilingi milioni 100 kwa mwaka huu”,alieleza Masele. 

Mbunge huyo alisema ameamua kuwa msimamizi mkuu wa timu hiyo ili kuhakikisha kuwa timu hiyo inafanya vyema katika michezo mbalimbali. 
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza katika mkutano wa hadhara leo Mjini Shinyanga ambapo alisema kampuni ya BIKO imedhamini timu ya Stand United kwa kuipatia shilingi milioni 100. 
 Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United,Dkt. Ellyson Maeja akielezea jinsi timu hiyo ilivyojipanga kufanya vizuri katika michezo mbalimbali huku akiomba wadau kuendelea kujitokeza kuisadia timu hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa katika mkutano huo. 

MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO AGOSTI 26,2017


INTRODUCING TRA'S ONLINE TV

Introducing Casso ft Dogo janja nitamisI official video

INTRODUCING "ZILIPENDWA" BY WASAFI

Introducing KambaKochi Beach Cottage at Kimbiji in Dar-Es-Salaam,Tanzania

0
0
Kambakochi Beach cottage located at Kimbiji Village in Kigamboni district on the South coast of Dar es Salaam,Tanzania,   is a self catering beach cottage, only steps away from the Indian Ocean. Nestled in a quaint, sleepy fishing village of Kimbiji.
It boasts of a private stretch of white sands ideal for long walks and spectacular sunrise. The cottage is a self catering round rock house with two bedrooms ensuite. Sleeps 6/8 comfortably. Chef included to assist you with meals. 3 bbq stands and coolers provided. Full kitchen amenities, open plan downstairs, dinning and living room area. 
An open outdoor terrace, entire cottage facing the magnificent Indian Ocean, giving you a full view of the beach full of charm and character due to its Coral Reef barrier. The Coral Reef creates a mini pool when the tide is out, making it ideal for snorkeling and super safe for children to swim in.
For More CLICK HERE

KINANA AMWANDALIA BALOZI WA CHINA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KUMUAGA

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, jana  Agosti 25, 2017. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Naibu Spika Tulia Akson, Mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Mawaziri Kadhaa, Makatibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Makatibu wa Jumuia za Chama. Picha zote na Bashir Nkoromo.
 Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kupokea zawadi maluum, ambayo Kinana alimzawadia wakati wa chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kumkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia), wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, jana Agosti 25, 2017.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa hafla hiyo.
  Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing wakiinua glasi za vinwaji kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, jana Agosti 25, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson. Picha zote na Bashir Nkoromo.

IGP SIRRO AFANYA ZIARA MKOANI MANYARA

0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Manyara, wakati alipowasili katika mkoa huo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kulia), akifurahia jambo na Mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera (Kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymond Mushi, wakati alipowasili katika mkoa huo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akipokea salamu ya heshima ya kijeshi wakati alipowasili mkoani Manyara, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akiwa ameongozana na kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, ACP Francis Jacob, wakati alipowasili mkoani Manyara, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari na maofisa wa Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.

BRIGEDIA JENERALI MBUNGU AWATAKA ASKARI WA SUMA JKT GUARD KUWA MABALOZI WAZURI WA MAPAMBANO YA RUSHWA MAKAZINI

0
0
 Askari wa ulinzi binafsi wa Suma Jkt Guard wakila kiapo cha uaminifu mbele ya  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akizungumza na askari wa ulinzi binafsi wa kampuni ya Suma JKT wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya sita kwa askari wapya wa kampuni hiyo iliyopo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT). na kuwaasa kuwa mabalozi wazuri katika mapambano ya rushwa katika kazi yao na hasa katika ofisi watakazopangiw akufanya kazi
 Mkurugenzi wa kampuni ya Ulinzi ya Suma Jkt Guard Limited, Meja Alfred Mwaijande akizungumza kabla ya kukamribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga mafunzo ya askari wa kundila sita wa Suma jkt
 wakionyesha umahiri wao wa kuchez amchezo wa Karate mbele ya mgeni rasmi  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu.
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU),Brigedia Jenerali .John Mbungu akiwa katika picha ya pamoja na askari wa ulinzi binafsi wanaomaliza mafunzo yao .


WOTE WENYE MATATIZO YA ARDHI ARUSHA MKUU WA MKOA ATAFANYA MKUTANO NANYI AGOSTI 29, 2107 KATIKA UKUMBI WA OFISI YA JIJI ARUSHA

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNT DOWN AUGUST 26TH 2017

KOCHA MAYANGA ATAJA TAIFA STARS MPYA KUIVAA BOTSWANA

0
0
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga ametangaza kikosi kipya kitakachocheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 28 hadi Septemba 2, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2, 2017.
Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemwita upya Mlinzi wa Young Africans, Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wakiwa ni saba akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.
Kikosi hicho kinachotarajia kuingia kambini kesho Jumapili kuanzia saa 2.00 usiku ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman).

Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
…………………………………………………………………………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

Azam TV – Mabao yote 7 ya mnyama Simba Vs Ruvu Shooting

TOWN PLANNERS REGISTRATION BOARD (Under Act No.7 of 2007) ANNOUNCING THE 4TH ANNUAL GENERAL MEETING ON 26TH – 27TH OCTOBER, 2017

0
0
The Town Planners Registration Board announces the Fourth Annual General Meeting which will take place on 26th - 27th October, 2017.


Venue:                           Bank of Tanzania (BOT) - Kilimanjaro Auditorium,

Dar es Salaam. 
Participants:                Town Planners, Surveyors, Land Officers, Architects, Valuers and other Land Development Stakeholders.

Participation Fee:         Tanzanian shillings 200,000.00 per participant; those paying after 15th October 2017 will be required to pay Tanzanian shillings 250,000.00 
Mode of payment:        Through Bank Account of the Board, or M-Pesa or in cash at the Office of the Board which is located in the 2ndfloor, Matasalamat Building, Samora Avenue in Dar es Salaam

Account Details:         Name: Town Planners Registration Board, Account Number: 20101000085 (NMB); M-Pesa No: 0753504222 

The Registrar,

Town Planners Registration Board,

Matasalamat Building – Samora Avenue,

P. O. Box 77496, Dar es Salaam,


Tel: 2127976, 0753 504222.

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live


Latest Images