Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1879 | 1880 | (Page 1881) | 1882 | 1883 | .... | 3348 | newer

  0 0


  Courtesy of Global TV

  0 0

   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Rais wa Umoja wa Mabunge ya Afrika ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Spika huyo wa Guine-Bissau alitembelea Mhe Ndugai kwa lengo la kumpa mwaliko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania wa kujiunga na Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa N’ZI Koffi.
   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea mwaliko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania wa kujiunga na Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) kutoka kwa  Rais wa Umoja huo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam anayeshuhudia kushoto  ni Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa.  N’ZI Koffi.

    Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimueleza jambo na Rais wa Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea mwaliko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kujiunga na Umoja huo.
   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Rais wa Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama (kushoto) na  Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa.  N’ZI Koffi (kulia).
   Rais wa Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama (kushoto) akimkabidhi zawadi  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia) mara baada ya mazungumzo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Bunge

  0 0

  Kuna taarifa ya ajali ya basi la kampuni ya Kimbinyiko International la kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam kwamba  limepinduka Gairo jioni ya leo jitihada za kujua madhara zinafanyika.

  0 0

  Former  President of Nigeria H.E. Olusegun Obasanjo of Nigeria  giving his key note address at the opening of the 4th African Leadership Forum which opened today in Johannesburg, South Africa. Also in attendance are Former Presidents of Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, H.E. Thabo Mbeki of South Africa, H.E. Benjamin William Mkapa and other dignitaries.


  The African Leadership Forum (ALF) is Africa’s dedicated space for open and frank discussion about the challenges facing the continent, by the continent. It is organised by the Office of the Former President of the United Republic of Tanzania, H.E. Benjamin W. Mkapa in conjunction with the Institute of African Leadership for Sustainable Development (UONGOZI Institute).


  0 0


  Na  Hussein Mohamed Bashe
   Mbunge 
  Jimbo la Nzega Mjini, Tabora.


  Mapema Januari mwaka huu nilipata nafasi ya kushirikiana na wananchi katika kazi za maendeleo Jimboni kwangu Nzega Mjini katika Kata ya Itilo ambapo nilikuwa na kazi ya kuhamasisha na kusaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Itilo.
   Nikiwa katika eneo hilo nilipata nafasi ya kukutana na mtoto mchangamfu ambaye anaitwa Suzan.

  Bahati nzuri ni kuwa Suzan alikuwa akisoma katika shule hiyo katika madarasa ya Awali, nilimkuta amekaa chini na wenzake.Suzan ni mtoto anayejiamini na huenda shule kila siku, waalimu wake walinambia Suzan huwa hakosi kwenda shule na hana udhuru wa mara kwa mara kama watoto wengine.

  Nilivutiwa sana na habari za Suzan na tabia yake ya kupenda shule hivyo tukaamua kwa pamoja na wananchi kuanza mchakato wa ujenzi wa  madarasa na sasa tumeyamaliza na nimekwisha kuyakabidhi kwa Shule na wananchi wa Itilo.
  Wiki hii nimefika tena Jimboni nimekutana na Suzan kwa mara nyingine; na nimepata nafasi ya kuongea naye zaidi; Suzan ameniambia anataka siku moja kuwa Mbunge kama mimi na anapenda namna ninavyowapenda watoto.Uwezo mkubwa na kujiamini kwa Suzan kunanipa faraja kuwa naye karibu zaidi na kumsaidia zaidi.
  Kwa sababu yake nilisukumwa kujenga madarasa mengine mawili zaidi katika Shule ya Msingi Itilo ili kuwajengea watoto wetu mazingira mazuri ya kujifunza.
  Nimemuomba Mwenyezi Mungu anipe nguvu na uwezo niendelee kumsaidia, kumlinda na kumtunza Suzan siku zote mpaka aakapotimiza ndoto zake siku moja.
  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo leo tarehe 24 Agosti, 2017 amefanya kikao cha kazi na watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO mkoa wa Mtwara mjini Mtwara lengo likiwa ni kujadili mafanikio na changamoto za utendaji kazi. Dkt. Pallangyo amewataka watendaji hao  kuwa wabunifu kwenye ukusanyaji wa mapato pamoja na kuwasilisha  taarifa za utekelezaji za kila baada ya miezi mitatu.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO mkoa wa Mtwara mjini Mtwara

   Sehemu ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO- Mtwara wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo akisisitiza jambo katika kikao hicho

   Afisa Rasilimaliwatu wa Kanda ya Kusini, Bonus Msuha (kushoto) akieleza jambo katika kikao hicho. Kulia ni Meneja wa TANESCO-Mtwara Mhandisi  Aziz Salum

  Sehemu ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Kusini na Ofisi za TANESCO- Mtwara na Wizara ya Nishati na Madini  wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kikao hicho.


  0 0

  Na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
  WANAFUNZI watatu wa shule  za Sekondari katika Manispaa ya Morogoro wamefariki dunia na wengine 30 kujeruhiwa miongoni mwao watu wazima baada ya basi dogo aina ya Coaster kugonga treni ya abiria iliyokuwa inatokea mikoa ya kanda ya Ziwa kuelekea Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha  tukio hilo mapema leo kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi  karibu na eneo la Ofisi za Mkoa za Tanesco ambapo kipo  kizuizi cha kivuko cha treni  inapokatisha barabara ya kutoka mjini kwenda Msamvu , Manispaa ya Morogoro.
  Alisema dereva aliyekuwa anaendesha basi hilo lenye  namba za usajili T438 ABR  alikatiza kwenye barabara bila kuchukua  tahadhari katika kivuko cha Treni wakati ikiwa inapita kitokea mikoa ya kanda ya Ziwa kwenda Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi wa mkoa huo alisema basi hilo ndogo linalofanya  safari zake kati ya Mjini na Kihonda  iligonga  treni hiyo ya abiria.
  Kamanda Matei alisema kuwa katika ajali hiyo  wanafunzi watatu, wawili wa wakiume na mmoja wa kike walipoteza maisha na kwamba walikuwa wanasoma Shule za sekondari Tushikamane  na Mji mpya.
  Kufuatia ajali hiyo  alisema polisi inamshikilia dereva wa basi hilo ndogo, Charles Damian Petro (39) mkazi wa Kihonda kutokana na kusababisha ajali iliyopoteza maisha ya wanafunzi  hao  na kujeruhi wengine kadhaa  baada ya kukatiza kwenye  kizuizi cha treni bila kuwa na tahadhari.
  Kamanda Matei aliwataka wamiliki na madereva wa vyombo vya usafiri kuwa makini wakati wanapokuwa wakivuka njia za reli ili kuepusha ajali ambazo mara kadhaa zimekuwa zikisababishwa na uzembe wa madereva kwa kuzigonga treni.
  Naye Mganga  mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk  Frank  Jacob  alisema , kuwa walipokea  walipokea majeruhi 33  na kati yao watatu walifariki dunia wakipatiwa matibabu  ambao ni wanafunzi , mmo akiwa ni wa kike na wawili wakiume. Alisema majeruhi 30   wamelazwa katika hospitali hiyo kati yao wanaume ni 10 na wanawake ni 23 na  hali zao zinaendelea vizuri.
  Kwa mujibu wa mganga mkuu mkoa huyo  kuwa baadhi ya majina ya majeruhi waliolazwa katika wodi  namba tatu ya wanawake  ni Asha Masud, Rehma Mashaka, Fatuma Aman , Zena Shabani,  Salma Said na  Asha Omari.
  Wengine ni Azama Rajab , Umi Mohamed , Magdalena Mgina , Ratifa Hassani, Florah Clemence, Eveline Mtelani, Asia Omary, Sada Seif . Lucy Lyamba, Nuru Shaban , Eliopa Paulo, Rehema Azizi na Monica Julias.
   Mbali na wodi ya wanawake majehuri wengine wanaume walilazwa katika wodi namba mbili  akiwemo Yasin Khalid Mkinngiye wanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Tushikamane.
  Naye Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Mhe. Regina  Chonjo ambaye alifika eneo la tukio hilo alisema, mashuhuda anaeleza kuwa ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva huyo.
  Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya kuwa, askari wa reli alizuia magari kwa kunyosha alama ya kibendera chekundu kusimamisha  magari  lakini dereva huyo aliamua kuyapita yaliyosimama mbele na kufika kizuizi hicho na kabla ya kuvuka  akigonga treni hiyo.
  Gari hilo liliburuzwa  umbali wa  zaidi ya mita 200  kutoka eneo la tukio na kuangukia pembezoni  na kusababisha majeruhi na vifo hivyo.
  Alisema treni hiyo ya abiria  haikuwa  katika  mwendo mkali kitendo ambacho kimepunguza madhara mengi licha ya kupoteza wanafunzi watatu.
  Umati mkubwa ulijitokeza eneo la ajali ambao pia walienda  kuwangalia majeruhi  wa ajali hiyo katika Hospitali hiyo ili kuwatanmbua watoto ama ndugu zao wakiwemo walimu wa shule za Sekondari na Msingi.
  Basi dogo Daladala lenye  namba za usajili T 438 ABR lililokuwa  limeigonga  treni ya abiria likipelekwa kituo cha polisi
  Mamia ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakwa eneo  la karibu na Ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro wakiangalia basi dogo Daladala lenye  namba za usajili T 438 ABR likiwa limeganga  treni ya abiria   yenye  kichwa namba 88U08  iliyokuwa inatokea  mikoa ya kanda ya Ziwa  kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu,  daladala hiyo ilikuwa inatokea kituo cha Masika kwenda Kihonda  ndani yake ikiwa na idadi kubwa  wanafunzi wa msingi na sekondari na wananchi.
  Basi dogo Daladala lenye  namba za usajili T 438 ABR lililokuwa  limeigonga  treni ya abiria   yenye  kichwa namba 88U08  iliyokuwa inatokea  mikoa ya kanda ya Ziwa  kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu, iliyokuwa inatokea kituo cha Masika kwenda Kihonda  ndani yake ikiwa na idadi kubwa  wanafunzi wa msingi , sekondari na wananchi ikiwa juu ya gari la kubeba vitu vizito la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kupelekwa Kituo cha Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.
  Basi dogo Daladala lenye  namba za usajili T 438 ABR lililokuwa  limeigonga  treni ya abiria   yenye  kichwa namba 88U08  iliyokuwa inatokea  mikoa ya kanda ya Ziwa  kwenda Dar es salaam katika eneo la kivuko chake karibu na ofisi za Tanesco mkoa wa Morogoro Augosti 24, mwaka huu. 
  Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii

  0 0


  0 0


  The main purpose of UNTOLD is to Educate, Inspire and Entertain. The show features Tanzania’s from different walks of life, in and outside of Tanzania. With a large diaspora community in the US and other parts of the world, we believe that we all have a contribution to where our great nation is going.
  The show will explore these individual’s lives; their moments of triumph and failure , decision patterns, their motivation and inspiration, beliefs, leadership style, family, relationships etc. 
  With these candid conversations we hope that others will be able to relate, be inspired and take something away that they can apply to their personal lives. We hope to remove the barriers that most of us create in ourselves – redefining possibilities, expose patterns and remove the notation that success only belongs to a select few. In life your response to events is what determines the outcome.
  Untold Season 1 premieres 8.26.17. 
  Like, subscribe and make sure you don't miss our premiere on the 26th!

  UNTOLD

  Ni kipindi kinachohusu mambo ambayo hayajawahi kuelezwa.
  Lengo kuu la kipindi hiki ni kufundisha, kuhamasisha na kufurahisha. The show inahusu Watanzania katika nyanja tofauti za maisha ndani na nje ya Tanzania. Tunaamini kila mtu ana mchango mkubwa wa mwelekeo wa nchi yetu kutokana na ukweli kwamba kuna jamii kubwa ya wanzania nchi za nje hususani Marekani.
  Kipindi cha UNTOLD kinatafiti maisha ya watu katika mafanikio na mapungufu yao, mfumo wao katika kufanya maamuzi, motisha na msukumo wa mafanikio yao, Imani zao, aina za uongozi wanazo kubaliana nazo, familia, mahusiano n.k. Kwa mwongozo wa maongezi haya yakinifu tunategemea wengine watajifunza kitu/ vitu na kuhamasika na hatimaye kutumia mawazo hayo kuboresha hali zao. Tunategemea kuondoa vikwazo binafsi katika maisha. Kwa Mara nyingine kufafanua uwezo/ uwezekano, kuonyesha miundo na kuondoa mawazo kuwa mafanikio ni kwa kundi fulani tu. Katika maisha matokeo ya jambo yanategemea sana ushiriki wako.
  Tegemea UNTOLD tarehe 26/08/2017

  0 0
  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa

  Halmashauri ya wilaya ya kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka mingi katika mji mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha dola za kimarekani 9,548,827 kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji yatakayo weza kutatua changamoto hiyo.

  Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi  wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa wameamua kutafuta chanzo kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa Ilula.

  “Leo nimefika hadi huku kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa kitafanikiwa kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani ya chama na kuhakikisha kuwa wanatatua  matatizo ya wananchi”alisema Masenza

  Aidha Masenza alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania dr John Pombe Maguli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alivitaja baadhi ya vyanzo ya maji na uwezo wa uzalishaji ambavyo vinatoa huduma kwa mji mdogo wa Ilula ni Ilomba kutoka kijiji cha Imalutwa na Idemule kutoka kijiji cha Mazombe kwa ujumla vinazalisha wastani wa uzalishaji wa maji wa mita za ujazo 1,142 kwa siku.
   Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula
   Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula
  viongozi wa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa wakiwa wanaelekea kwenye chanzo cha maji kwa ajili ya kujua jinsi gani kitaweza kutatua kero za wananchi wa mji wa mafinga.


  0 0


  Na Mathias Canal, Zanzibar

  Kongamano lilodumu kwa siku mbili kwa kuwakutanisha watanzania waishio Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limehitimishwa hii leo Agosti 24, 2017 huku likiwa limehudhuriwa na Diaspora 350 na kuchagizwa na wahudhuriaji wengine ambao ni watendaji kutoka taasisi za serikali na wadau katika uwekezaji na uchumi.

  Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) lilifunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan ambapo limefikia ukomo kwa kupatikana majibu ya changamoto mbalimbali ziwahusuzo Diaspora ikiwemo uraia pacha na sera ya utambuzi wao nchini Tanzania.

  Akihutubia mamia ya watanzania walioshiriki katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Idd alisema kuwa serikali inawatambua Diaspora kama mabalozi muhimu katika kutangaza utalii Duniani kote jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaongeza kipato cha nchi.

  Alisema kuwa serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Diaspora katika kuitangaza nchi ya Tanzania na vivutio vyake hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo pia kuwatangaza viongozi wa serikali kwa weledi mpana pasipo kueneza chuki dhidi ya viongozi wao.

  Mhe alozi Seif alisema kuwa kumekuwa na watanzania waishio nje ya nchi wasiokuwa na weledi na nidhamu dhidi ya viongozi wa serikali kwani wamekuwa wakiwasema vibaya kwa kuwatukana na kejeli jambo ambalo linarudisha nyuma heshima yao waliyonayo na kutia doa serikali.

  Alisema kuwa Diaspora wanapaswa kuendelea kushiriki katika makongamano mengine yajayo kwani kufanya hivyoi kunatoa fursa kwao kuishauri serikali na kuona namna bora ya utambuzi wao.
  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akihutubia wakati wa kufungaKongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara. (Picha zote na Mathias Canal)
  Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu Mhe Issa Haji Gavu akitoa salamu kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
  Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia hotuba ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddykatika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara.
  Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy (Kushoto) akifatilia burudani mbalimbali wakati wa kufunga Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Mwingine ni Balozi Anisa Mbega Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya namtumbo luckiness amlima amekagua ujenzi wa mabweni, vyumba vya madarsa na vyoo katika shule ya sekondari NASULI na NANUNGU iliyopo wilayani hapo na kuridhishwa na ujenzi wake ambao hadi kukamilika kwake itagaharimu kiasi cha shilingi milioni mia tano na kumi na nane.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kutafuta mbinu bora za kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ili kukuza sekta hiyo.

  Amesema licha ya Tanzania kuwa na vivutio vingi vya utalii lakini idadi ya watalii wanaoingia nchini kwa mwaka ni ndogo, hivyo kuna haja ya kuboresha matangazo.Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatano, Agosti 23, 2017) wakati alipofanya ziara katika mji wa kitalii wa Varadero ulioko kwenye mkoa wa Matanzas nchini Cuba.

  Alisema mji wa Varadero tu unaingiza watalii zaidi ya milioni moja kwa mwaka na unategemea kivutio kikubwa kimoja tu cha fukwe ambayo ina urefu wa kilomita 22.Alisema idadi hiyo ni tofauti na Tanzania ambayo imejaliiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii huku watalii wanaovitembelea ni wachache. “Tunatakiwa kujitangaza zaidi.”Waziri Mkuu alitaja baadhi ya vivutio vya utalii ambavyo ni mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, miji ya kihistoria ya Kilwa, Bagamoyo, Stone Town pamoja na Mikindani.
  “Vivutio vingine ni eneo la Oldvai George ambako binadamu wa kwanza aliwahi kuishi, hifadhi ya Gombe ambako kuna sokwe ambao wanaishi kama binadamu.”

  Alisema Serikali itahakikisha jitihada zinafanyika katika kukuza sekta ya utalii ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vilivyoko nchini ili kuweza kuongeza idadi ya watalii.Pia Waziri Mkuu aliwahamasisha Watanzania kujenga tabia ya kutembelea vivutio vyeo vya utalii na kujifunza mambo mbalimbali na si kuwaachia wageni pekee.Kwa upande wake, Kiongozi wa Sekta ya Utalii katika mkoa wa Matanzas, Bw. Luis Martinez de Armas alisema mji wa Varadero ni kivutio kikubwa cha utalii nchini Cuba.

  Alisema kivutio kingine cha utalii ni hoteli zilizojengwa ndani ya bahari, maeneo ya kihistoria na migahawa inayouza vyakula vya asili vya nchi hiyo.
  Bw. Luis alisema mwaka 1990 ndio walianza kuendeleza sekta ya utalii katika mkoa wao na ulikuwa na hoteli 4,436 ambazo kwa sasa zimeongeza na kufikia hoteli 20,696.

  Hata hivyo Bw. Luis alisema Tanzania inavivutio vingi vya utalii na kwamba anavutiwa na mlima Kilimanjaro pamoja na wanyama na viumbe vingine vilivyoko katika mbuga mbalimbali. Alisema wako tayari kushirikiana na Serikali katika kukuza sekta ya utalii.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, 
  ALHAMISI, AGOSTI 24, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ,kushoto akikabidhi Jarida lakutangaza Utalii wa Tanzania Kwa Kiongozi wa maswala ya Utalii katika Mkoa wa Matanzas .Bwana Luis Marines ,jana August 23/2017 wakati alipokuwa katika Ziara ya kikazi kwenye Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nchini Cuba, katikati katika picha ni Mama Mary Majaliwa
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (mwenye miwani)na Mama Mary Majaliwa (kulia) .pamoja na Ujumbe wa Serekali ya Tanzania wakipata maelezo jana August 23/2017kutoka kwa Kiongozi wa Utalii katika Mkoa wa Matanzas ,Bwana Luis Martines. jinsi fukwe za Bahari zinavyo tunzwa nakuwa kivutio kwa Watalii wanao tembelea Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nnchini Cuba
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (mwenye shati jeupe) na Mama Mary Majaliwa (kushoto)pamoja na ujumbe wa serekali ya Tanzania jana August23/2017. wakipata maelezo kutoka kwa muongoza wa Talii Bibi Yanseli Marrero kuhusu biashara ya Boti za Utalii kwenye fukwe za Bahari katika Mji wa Varadero Mkoa wa Matanzas Nnchini Cuba

  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0


  Waziri wa michezo nchini Tanzania Mh.Dk Harrison Mwakyembe amewatakia safari njema watoto waliochaguliwa na kampuni ya Tecno mobile kwenda kufanya majaribio ya kucheza mpira wa miguu katika academy ya klabu ya Manchester City nchiniUingereza.
  Malimi Majaliwa wa kwanza kushoto na Daudi DAmasi wakiwa katika picha ya pamoja baada yakupewa Baraka za safari na Mh. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe)

  Akiongea katika hafla hiyo fupi kutambulisha mbele ya waziri mpango huo, Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Tecno Mobile Bwana, Eric Mkomoya alisema kua kampuni ya Tecno Mobile ndio wadhamini pekee wa safari hiyo kupitia simu yao mpya Tecno Camon Cxto leo maalumu la machester city ambapo watoto hao wawili wataenda kupewa mafunzo yenye kiwango cha kimataifa lakin pia endapo watafanya vizuri wanaweza kuchaguliwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo. ,(wadhamini wa kuuwa safari

  (Wazazi na walezi wa vijana wanaokwenda Manchester city wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa kuu kutokea Tecno Mobile.)

  Alisemaa . ”Tumefurahi kukutana na serikali hasa Waziri wa michezo na kuamua kuwapa Baraka zake vijana wetu wanaokwenda huko wataondoka usiku wa tarhe 23 na kurudi tarehe 30 mwezi wa nane”.

  Akikaribishwa na mkurugenzi wa michezo, waziri wa michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kua serikali ina furaha kuona wadau wanajitokeza kukuza vipaji nchini Tanzania, hasa kwa watoto wanao chipukia.

  Dk Harrison Mwekyembe pia amesema “niwaombewa dau katika sekta ya michezo tushirikiane katika kukuza michezo, na washukuru kampuni ya Tecno Mobile kwa kuonesha juhudi za wazi katika kufanikisha hili, serikali pia inafanya jitihada kwa nafasi kuhakikisha viwango vya soka na michezo kwa ujumla vinakua.”alimaliza.)

  Mzazi wa mtoto mmoja wapo Malimi, Majliwa Mbasa amesema anafuraha kuona kijana wake amepata nafasi hiyo anaamini atafanya vizuri liafungue milango kwa vijana wengine wadogo wa kitanzania walioko nchini waweze kwenda kucheza soka la kulipwa nchini uingereza.

  Watoto wawilli Daudi Damasi pamoja na Malimi Majaliwa wanaocheza nafasi ya kipa na ushambuliaji wamepata nafasi hizo kutokana na ushirikiano wa Tecno Mobile naasasi ya michezo ya Magnet, watoto hao ambao wote wana miaka kumi na mbili wataondoka kuelekea manchster city mnamo tarehe 23 mwezi wa nane na kurudi nchini tarehe 30.

  Msafara huo utaongozwa na wazazi na walezi wa watoto hao akiwemo kocha mwenye utalaamu wa kulea vipaji vya vijana kocha Juma Maswanya. Tecno mobile ndio wadhamini wakuu wa safari hii wanajumuisha vijana kutoka nchi za afrika ambako kampuni hii inapofanyakazi hivyo Nigeria, misri ,Tanzania, Ghana pamojana Kenya.
  Afisa Mahusiano wa Tecno Mobile Eric Mkomoya wa kwanza kushoto, meneja Masoko Franck Luo, wa kwanza kulia)
  aziriwaHabari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na watoto wawili Daudi Damasi na Malimi Majaliwa wanaokwenda kufanya Majaribio,

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), ameziagiza Halmashauri nchini, kuyatambua na kuyatolea taarifa maeneo yanayohodhiwa na watu bila kuendelezwa na yale ambayo hayakupatikana kihalali ili Wizara iweze kuchukua hatua stahiki.

  Naibu Waziri huyo ameyasema hayo alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, kisha Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu kuanza ujenzi wa mradi wa maji katika eneo hilo utakaonufaisha vijiji vinne vya kata ya Lamadi.

  Mhe.Mabula amesema Halmashauri zinapaswa kutambua maeneo yasiyoendelezwa na yanayomilikiwa kinyume cha sheria na kuwasilisha taarifa katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili yaweze kuyarejesha kwa wananchi na kupangiwa matumizi mengine yenye manufaa zaidi kwa jamii.
  Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
  Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali .
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya wakati alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kushoto) akimkaribisha mmoja wa washiriki katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Sehemu ya washiriki katika mkutano ulioandaliwa na Benki ya NMB na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance.

  0 0

  Marehemu Mzee Paul Joseph Maro

  14.03.1931 - 23.08.2017

  Familia ya Mzee Paul Joseph Maro ya Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha Baba yao Mpendwa Mzee Paul Joseph Maro kilichotokea katika hospitali ya Muhimbili juzi alfajiri Jumatano tarehe 23.08.2017.
  Mzee Paul Joseph Maro ni baba mzazi wa:
  1. Happiness Paul Maro, 2. Gabriel Paul Maro,3. Edwin Paul Maro na 
  4. Simon Paul Maro.Maandalizi ya Mazishi yanafanyika nyumbani kwa marehemu Tandika Maghorofani karibu na Chuo cha Bandari. 
  Habari ziwafikie ukoo wote wa Maro , Mawalla, Marealle na Mandara, ndugu jamaa na marafiki wote wa familia.

  Mazishi yatakuwa kesho Jumamosi 
  tarehe 26.08.2017 katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.


  0 0
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Yusuph Ndemango ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na Pantoni kuelekea  katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya Kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine wakati akivuka kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama mmoja mara baada ya kuvuka upande wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana pamoja na kuzungumza na abiria mbalimbali wakati akisubiri kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni kuelekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kigamboni mara baada ya kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni wakati katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Bodi na Menejimenti ya NBC na Mabenki mengine kuwa kuanzia sasa Taasisi zote za fedha ziweke kipaumbele cha kwanza katika kuwezesha kuendeleza viwanda nchini hasa viwanda vidogo vidogo na vya kati vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.Pia viwanda ambavyo vinatumia teknolojia ya kati na nguvu kazi zaidi ( labour intensive technology).
  Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubua kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya NBC.

  Mhe. Samia alisema mabenki mengi yameendelea kutoza riba ubwa hivyo kupelekea wananchi wa kipato cha chini hivyo aliwataka Wataalamu wa NBC na Sekta za Fedha kwa ujumla kutafuta suluhisho la riba zisizo rafiki kwa walio wengi ili amana pamoja na mikopo iweze kuongezeka.

  Makamu wa Rais aliziagiza Bodi na Menejimeni ya NBC na Mabenki yote nchini kuzingatia Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha, alisema " Serikali ya Tanzania haitomuonea mtu haya na itachukua hatua kali dhidi ya benki au Taasisi yeyote itakayobainika kukiuka matakwa ya sheria hiyo."

  Mwisho Makamu wa Rais aliipongeza benki ya NBC kwa kuweza kutoa gawio la Shilingi Bikioni 1.2 mwaka huu 2017 kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.

older | 1 | .... | 1879 | 1880 | (Page 1881) | 1882 | 1883 | .... | 3348 | newer