Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1878 | 1879 | (Page 1880) | 1881 | 1882 | .... | 3348 | newer

  0 0

  TAASISI za Umma zimeshauriwa kujikita zaidi katika utekelezaji wa mipango iliyojiwekea badala ya kutumia muda mwingi kupanga mipango isiyotekelezwa.

  Ushauri huo umetolewa leo kwenye warsha ya kuwajengea uwezo watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuingiza Mpango kazi wa utelezaji wa APRM kwenye mipango ya maendeleo ya nchi kama vile Dira ya Zanzibar 2020, MKUZA III na Mipango ya Matumizi ya Muda wa Kati. 

  Warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa na APRM Tanzania na inafanyika katika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 24 na 25 Agosti 2017.

  Mgeni Rasmi kwenye warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Kubingwa Mashaka Simba ambaye alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Haroun Ali Suleiman aliwahakikishia washiriki kuwa Serikali ya Zanzibar imejipanga vema kutekeleza changamoto zote zilizobainishwa kwenye ripoti ya APRM iliyowasilishwa rasmi kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan mwanzoni mwa mwezi Agosti 2017.

  Bw. Simba alieleza kuwa tayari Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishachukua hatua za kuimarisha Utawala Bora ikiwemo kuunda taasisi za kusimamia suala hilo ambazo baadhi yao ni Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tume ya Kupambana na Rushwa pamoja na ugatuzi wa madaraka.

  Wadau wanaoshiriki warsha hiyo walibainisha kuwa changamoto kubwa katika taasisi za umma ni utekelezaji wa mipango iliyowekwa, Hivyo kuna umuhimu wa APRM kuangalia namna ya kujenga uwezo wa watumishi katika kutekeleza mipango ya Serikali kwa kuzingatia namna ya kupata rasilimali zinazohitajika na zenye uwezo wa kutekekeza mipango iliyopo pamoja na muda wa kutekeleza mipango hiyo.

  Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa APRM, Tanzania, Bi. Rehema Twalibu alisema warsha hiyo ni muhimu kwa watumishi wa Serikali ya Zanzibar kwa kuwa itawapa uwezo wa kuandaa taarifa ya utekelezaji wa changamoto zilizoainishwa kwenye ripoti ya APRM iliyowasilishwa miaka mitano iliyopita kwa Wakuu wa Nchi zilizoridhia Mpango wa APRM. 

  Taarifa ya utekelezaji itakayoandaliwa na Serikali ya Zanzibar itajumuishwa na taarifa ya Tanzania Bara ili kupata ripoti moja ambayo inatarajiwa kuwasilishwa na Mhe. Rais kwa Marais wenzake wanaounda APRM baadaye mwaka huu.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Zanzibar, 24 Agosti 2017.
  Katibu Mtendaji wa Mpango wa Afrika wa Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tanzania, Bi. Rehema Twalib akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Kubingwa Mashaka Simba (hayupo pichani) kwenye ufunguzi wa Warsha ya kuunganisha mipango ya APRM na Mipango ya Serikali inayofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, mjini Zanzibar. 
  Naibu Katibu Mkuu, Bw. Kubingwa Mashaka Simba akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika ufunguzi wa Warsha ya ya kuunganisha mipango ya APRM na Mipango ya Serikali
  Sehemu ya viongozi waliohudhuria kwenye Warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini Mhe. Simba.

  0 0

   Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Sekretariati ya ajira kwa utumishi wa umma Bi.Riziki Abrahamu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam  kuhusu kuwahamasisha walemavu kuchangamkia fursa za ajira zilizotolewa na Serikali, kulia ni Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya ajira kwa utumishi wa umma Bw. Malimi Muya.
  Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya ajira kwa utumishi wa umma Bw. Malimi Muya akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) mapema leo Jijini Dar es Salaam kuhusu upatikanaji wa fursa za ajira kwa walemavu kulia ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika sekta hiyo Bi.Riziki Abrahamu
  Picha Na Paschal Dotto-MAELEZO

  Na. Georgina Misama, Agness Moshi - MAELEZO
  Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Sekretariati ya Ajira Katika Utumishi wa Umma imewashauri walemavu kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa Serikalini kwani ni haki yao ya msingi kama ilivyo kwa watanzania wengine.

  Akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi Wa Umma Riziki Abraham amesema Serikali inawahamasisha walemavu kuchangamkia fursa za ajira zinazotangazwa na Ofisi hiyo kwa sababu ni wachache wanaojitokeza.

  “Mwamko wa walemavu katika uombaji wa ajira ni mdogo, ninawahamaisha kutuma maombi yao endapo wametimiza vigezo bila kuogopa changamoto zinazowakabili kwa sababu mchakato wote wa ajira unafanywa kwa kufuata kanuni na Sheria za Nchi ambayo inampa kila mtu haki ya kupata ajira”,Alisema Riziki.

  Sheria namba 9  ya Ajira ya mwaka 2010 inasema “ Mwajiri yoyote awe wa Umma au Binafsi mwenye waajiriwa kuanzia 20 na kuendelea lazima asilimia 3 ya waajiriwa hao iwe kwa ajili ya watu wenye ulemavu” hii  inaonyesha kuwa walemavu wana haki ya kuajiriwa mahali popote.

  Bi.Riziki amesema ni vyema walemavu kuzitaja changamoto zao kweye fomu za maombi ili Ofisi iweze kuwaandalia mazingira rafiki kwa ajili ya mchakato mzima wa upatikanaji wa ajira na baada ya kupata ajira waweze kupangiwa sehemu ambazo hazitakua changamoto kwao.

  Aidha Serikali inawapa kipaumbele walemavu kuanzia wakati mchakato wa usajili hadi wakati wa kupanga ajira hivyo basi walemavu wenye vigezo vilivyoanishwa kwenye matangazo ya ajira wajitokeze kutuma maombi ya nafasi hizo.

  Naye, Katibu Msaadizi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi Wa Umma Malimi Muya amesema kuwa Walemavu wanahaki kisheria hivyo waachane na mawazo ya kudhani wakitaja changamoto zao kwenye maombi hawatapatiwa nafasi.

  “Serikali yetu haina ubaguzi kwenye utoaji ajira ukiwa na vigezo tutakuchukua, kuna upendeleo tunawapa walemavu kulingana na changamoto zao kama vile kuwaongezea muda wakati wa usaili, kuwatafutia wataalam wa mawasiliano na kuwaandalia mazingira rafiki wakati wa usaili kwa kuzingatia changamoto zao”, alisema Malimi.

  Aidha Bw.Muya ameongeza kuwa Serikali inatambua nafasi ya Walemavu katika kuchangia maendeleo ya Nchi na ina wahamasisha kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kujikwamua kiuchumi.

  Ofisi ya Rais, Sekretariati ya Ajira Katika Utumishi wa Umma ina jukumu la msingi la kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi wanaofaulu usaili.

  0 0

  Jonas Kamaleki- MAELEZO.

  WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ameridhia mwekazi kupewa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kijijini Msoga, Wilayani Chalinze, Mkoa wa Pwani.


  Waziri Lukuvi amesema kuwa wanakijiji wana uwezo wa kutoa ardhi hadi ekari hamsini tu zaidi ya hapo ni Mhe. Rais mwenye uwezo wa kutoa hati kwa mwekazaji, hivyo alikwenda Msoga kujiridhisha kabla ya kumshauri  Rais kutoa hati kwa mwekezaji.


  Aliwauliza wananchi katika mkutano uliofanyika kijijini Msoga kama walikubaliana kumruhusu mwekazaji wa Region Recycling East Africa Limited kujenga kiwanda kijijini hapo, nao wananchi kwa pamoja walisema kuwa ndiyo walitoa ardhi yao kwa ajili ya uwekezezaji huo.


  Kiwanda hicho kitakuwa kinatumia betri mbovu za gari na za umeme jua  (Recycling) kama malighafi ya kutengeneza betri nyingine kwa ajili ya matumizi ya magari na mitambo ya umeme jua. Mwekezaji huyo alipewa jumla ya ekari 56 na wanakijiji wa Msoga kwa ajili ya uwekezaji huo.

  “Vijiji vilivyopimwa kimji vitaiingizia Serikali mapato na wananchi pia watapata fursa za kupata mikopo kwenye mabenki na kufanya biashara kubwa,”alisema Lukuvi na kuongeza kuwa anazishauri Halmashauri zote nchini kupandisha hadhi vijiji vya namna hiyo.


  0 0

  FAMILIA YA DR. REHEMA NCHIMBI, MKUU WA MKOA WA SINGIDA, INASIKITIKA KUWATANGAZIA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI KUWA IMEFIKWA NA MSIBA WA BI. SELIDA DAUDI AMBAYE NI MAMA MZAZI WA DR. REHEMA NCHIMBI HUKO MAGUGU BABATI, MKOANI MANYARA. TARATIBU ZA MAZIKO ZINAFANYWA MAGUGU BABATI MANYARA. TAARIFA ZIWAFIKIE NDUGU NA JAMAA WOTE POPOTE PALE WALIPO.

  BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
  -AMIN

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akiwa katika mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, alipokutana nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akiwa na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, baada ya mazungumzo nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini. 
  PICHA: BASHIR NKOROMO. KWA PICHA ZAIDI ZA KIKAO HICHO

  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU-Ughaibuni yenye maskani nchini ujerumani,inatarajiwa kulitingisha jiji la Bremen siku ya jumamosi 9.09.2017.

  Katika ukumbi wa Wisserterasse kuanzia saa mbili usiku,bendi hiyo iliyojijengea umaarufu katika kila kona kwa tabia zake za kuwadatisha akili washabiki wake katika majukwaa ya kimataifa kwa kutumia mdundo wake "Extraordinary Bongo Dansi" ndio bendi pekee ya kigeni barani ulaya inayodumu katika tasnia ya muziki kwa muda mrefu barani ulaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 na kiongozi wake mwanamuziki Kamanda Ras Makunja wa himaya yake ya viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com au wape hai at www.facebook.com/ngomaafricaband.

  0 0

   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliokutanisha Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kupata elimu juu ya Sheria ya Usalama wa Mitandao, Utekelezaji wake na namna ya kuchukua tahadhari, jijini Dar es Salaam.
   Mwanasheria Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Philip Filikunjombe akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayohusu Sheria ya Usalama wa Mitandao. Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na lengo la kutoa elimu juu ya Sheria ya Usalama wa Mitandao, utekelezaji wake na namna ya kuchukua tahadhari.
  Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza mada iliyokuwa inawasilishwa na Msemaji wa Jeshi la PolisiBarnabas Mwakalukwa (hayupo pichani), wakati wa ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar es Salaam.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 

  NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ametoa onyo kali kwa wale wanaofanya uhalifu kwa njia ya mtandao kuchukua tahadhari kwani hawapo salama na kuahidi kuwashughulikia kwa mujibu wa Sheria.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, katika mkutano uliokutanisha uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Naibu Waziri Ngonyani amesisitiza kuwa serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamendelea kufanya doria katika mitandao  ili kubaini watu ambao wanatumia vibaya mitandao.

  "Tutumie mitandao kwa ajili ya kuleta maendeleo na si kinyume chake kwani ukifanya uhalifu wowote kwa njia ya mtandao tutakukamata popote ulipo na kukuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria", amesema Eng. Ngonyani.

  Aidha, Naibu Waziri Ngonyani amewataka wananchi kutumia kikoa cha Tanzania (.tz), na Kituo Mahiri cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zao ili zisiingiliwe kwa urahisi na kuweza kuibiwa.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Hamza Juma, ameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa jamii kuhusu masuala ya matumizi ya mtandao kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.
  "Nawaomba TCRA na vyombo vya habari nchini msaidie kusambaza elimu hii kwa wanachi ili waweze kupata uelewa wa masuala ya matumizi salama ya mtandao na changamoto zake”, amesisitiza Mhe. Juma.

  Kwa upande wake Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Barnabas Mwakalukwa, ametoa onyo kali kwa wale wanaotumia mitandao vibaya katika kuleta uchochezi wa kidini, kisiasa na kutumia majina ya viongozi na watu maarufu kwa ajili ya kufanya utapeli kuacha mara moja kwani Jeshi la Polisi litahakikisha linachukua hatua kali za kisheria dhidi yao.

  Amewataka wananchi kuwa tayari kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zinazohusu uhalifu wa kimtandao ili kuweza kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kwani suala la ulinzi na usalama ni letu sote.

  Tangu kuanzishwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 kumewezesha Jeshi la Polisi nchini kufuatilia kwa karibu na kushughulikia uhalifu mtandaoni ambapo kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni, 2017 Jeshi la Polisi limeweza kukamata watuhumiwa 315, kufikisha mahakamani kesi 153, kesi 19 zilipatikana na hatia na zingine zipo chini ya upelelezi. 
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kushoto) alipokuwa akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari ya Chokocho Wilaya ya Mkoani lenye madarasa manne na Chumba cha Maabara leo akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba (kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoku wa akiuliza suala na kutoa maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Chokocho Maalim Abdalla Mohamed Abdalla (kushoto) wakati alipoikagua maabara katika skuli hiyobaada ya kuifungua rasmi pamoja na madarasa manne ya kusomea (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma,Rais akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Chokocho Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ili kuzungumza na Wazee,Wananchi hao pamoja na Walimu katika uzinduzi wa jengo la madarasa manne (4) na Chumba cha maabara leo katika Skuli ya Sekondari ya Chokocho  akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba.
  [Picha na Ikulu.] 24/08/2017.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Shirika lisilo la kiserikali la AESH linalojishughulisha na utoaji wa elimu kuhusu matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na serikali kupitia miradi mbalimbali ikiwemo elimu,utuzaji wa mazingira,kilimo na ujasiriamali,kutoka wilaya ya TUNDURU mkoani RUVUMA linatarajia kuanza kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali kupitia mfuko wa elimu.

  0 0

   Brigedia Jenerali John Julius Mbungo aliyeapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo akila kiapo cha maadili ya Viongozi wa serikali baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.  
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Mhe. Angela Kairuki  baada ya kuongea machache  baada ya kumuapisha  kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kumuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Mhe. Angela Kairuki, Waziri wa sheria na Katiba Profesa palamagamba Kabudi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju, katibu Mkuu Kiongozi Balozi  John Kijazi, wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Brigedia Jenerali John Julius Mbungo baada ya kuapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   PICHA NA IKULU.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Stephen Wasira leo ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


  0 0


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ametoa onyo kali kwa wale wanaofanya uhalifu kwa njia ya mtandao kuchukua tahadhari kwani hawapo salama na kuahidi kuwashughulikia kwa mujibu wa Sheria.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, katika mkutano uliokutanisha uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Naibu Waziri Ngonyani amesisitiza kuwa serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamendelea kufanya doria katika mitandao ili kubaini watu ambao wanatumia vibaya mitandao.

  “Tutumie mitandao kwa ajili ya kuleta maendeleo na si kinyume chake kwani ukifanya uhalifu wowote kwa njia ya mtandao tutakukamata popote ulipo na kukuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria”, amesema Eng. Ngonyani.

  Aidha, Naibu Waziri Ngonyani amewataka wananchi kutumia kikoa cha Tanzania (.tz), na Kituo Mahiri cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC), kwa ajili ya kuhifadhi taarifa zao ili zisiingiliwe kwa urahisi na kuweza kuibiwa.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliokutanisha Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kupata elimu juu ya Sheria ya Usalama wa Mitandao, Utekelezaji wake na namna ya kuchukua tahadhari, jijini Dar es Salaam. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Hamza Juma (wa pili kulia), akizungumza na wajumbe wa Kamati na watendaji wa TCRA katika ziara ya kikazi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani. 
  Mwanasheria Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Philip Filikunjombe akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar inayohusu Sheria ya Usalama wa Mitandao. Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ulikuwa na lengo la kutoa elimu juu ya Sheria ya Usalama wa Mitandao, utekelezaji wake na namna ya kuchukua tahadhari .
  Wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza mada iliyokuwa inawasilishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Barnabas Mwakalukwa (hayupo pichani), wakati wa ziara ya kikazi katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), jijini Dar es Salaam.   0 0


  0 0

  JUMLA ya nchi Sita leo zimeanza mchuano mkali katika mashindano ya gofu ya kanda ya tano ya Afrika yaliaonza kutimua vumbi katika Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

  Mashindano hayo ya siku tatu yaliyoanza jana yanazishirikisha nchi za Rwanda,Burundi,Ethiopia,Uganda, Kenya na wenyeji Tanzania. Katika mchezo uliochezwa jana upande wa ‘Singel’s kati ya Amani saidi kutoka Tanzania na John Karicho kutoka Kenya wachezaji hao walitoka sare katika mashimo 18 waliyocheza. 

  Akizungumza baada ya mchuano huo kumalizika, Karicho kutoka Kenya, alisema kuwa mchuano ulikuwa mzuri na wenye upinzani mkubwa kutokana jinsi alivyokuwa nyuma kwa viwanja 3-0 kati ya viwanja 9 walivyocheza. 

  Aidha Karicho, alisema kuwa uchezaji wa mpinzani wake, Saidi ni mzuri sana na katika mchezo huo alidai alicheza kwa uangalifu mkubwa katika viwanja 9 vya mwisho kuhakikisha anasawazisha matokeo hayo. 
  MCHEZAJI wa Timu ya Gofu ya Tanzania, Amani Said, akipiga mpira katika Shimo Namba 9, wakati akichuana na mpinzani wake John Karichu, kutoka nchini Kenya, katika mashindano ya Tano ya Kanda ya Afrika Mashariki yanayoshirikisha Nchi Sita za Tanzania, Ethiopia, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda, yaliyoanza jana katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofika kushuhudia mchuano huo. 


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo. 

  Dkt. Nzuki amesema ipo haja sasa kwa Sekta za Umma kuona umuhimu wa kuwekeza moja kwa moja katika biashara ya utalii nchini hususani katika huduma za malazi na usafiri ili kuiwezesha Serikali kupata mapato ya moja kwa moja na kuongeza zaidi kwenye pato la taifa. 

  Alisema kwa kuimarisha usafiri wa anga kutawezesha usafiri wa watalii moja kwa moja kutoka kwenye soko na kuwaleta nchini huku wakilipia gharama zote hapa nchini tofauti na hivi sasa ambapo baadhi ya makampuni ya nje hulipwa fedha kiasi nje ya nchi na hivyo kuikosesha Serikali mapato kupitia ushuru unaotozwa na TRA. 

  Alisema sio lazima Serikali iwe inasimamia moja kwa moja utoaji wa huduma hizo kwa kuwa upo uwezekano wa kutumia makampuni makubwa hata ya nje ya nchi kuja kuendesha huduma hizo kwa ufanisi zaidi hapa nchini.  

  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na wadau wengine wa sekta ya utalii wakimsikiliza Prof. Raphael Mwalyosi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia) wakati akiwasilisha mada kuhusu Hoja ya Marekebisho ya Sera ya Utalii ya Mwaka 1999 katika warsha ya kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kupitia upya Sera hiyo iliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii mjini Dodoma leo.
  Kamu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Deograsias Mdamu akizungumza katika warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo. 
  Picha ya pamoja ya Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (katikati waliokaa) na wadau wa sekta ya utalii katika warsha ya siku moja ya kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya utalii kwa ajili ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999 iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Benki ya Dunia na Shirikisho la Utalii Tanzania mjini Dodoma leo.


  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.

  Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga SC za Dar es Salaam kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini. Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo. 

  Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri mwonekana wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.

  Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu sahihi.

  Hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa Maji ya kutosha kwa Wakazi wa Dar es Salaam.

  Katika ziara hiyo Makonda ametembelea Ujenzi wa Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.

  Makonda amesema lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ni kumtua Mama Ndoo kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia Wananchi wote.

  Amesema kukamilika kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo Vinne vikubwa vya usambazaji wa Maji vinavyojengwa maeneo ya Changanyikeni, Makongo, Wazo na Bunju*vitasaidia kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.

  Katika ziara hiyo pia Makonda ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye Ziara ya Dar Mpya ambavyo Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa kuzalisha Lita 16,000 kwa kila kisima ambavyo vitahudumia wakazi wa Wilaya ya Ubungo.

  Aidha Makonda ametembelea eneo la Jangwani ambapo 
  kutajengwa Mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 200 na eneo la Kilongawima Mbezi Beach kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 135 chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na Serikali ya Japan.

  Hata hivyo amesema bado Serikali inaendelea kufanya jitiada za kuhakikisha Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia miradi mbalimbali inayoendelea.

  Amewataka Wananchi ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za DAWASCO ili waunganishiwe Maji bila malipo ambapo baada ya hapo watawekewa utaratibu wa malipo.
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama  Ujenzi wa moja ya Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama mambo ya kupitishia maji ikiwa ni pia sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo mafupi juu ya muundo mzma mzima wa miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishiriki kuchimba mtaro wa kupitisha bomba la maji ikiwa ni sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar

  0 0


  Filbert Rweyemamu,Arusha

  Benki ya Dunia imetoa Sh 200 Milioni ili kuwezesha miradi ya elimu na ujuzi kwa ajili ya kazi zinazoleta uzalishaji wenye tija pamoja na vituo viwili vya umahiri vya kikanda vitakavyofungua ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu elimu. 

  Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta za kilimo,utalii,ujenzi ,nishati na madini.

  Alisema kuwa miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na vituo vinne vya umahiri katika masuala ya utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pia ipo miwili iliyochini ya taasisi ya Chuo Kikuu ya Nelson Mandela pamoja na vituo vingine viwili vilivyopo katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine(Sua).

  Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia, Bella Birds alisema kuwa uboreshwaji wa rasilimali watu kwa kuongeza ujuzi uliokosekana utasaidia taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa viwanda.
  Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kushoto) akiwasili katika taasisi ya Chuo cha Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) kuzindua mradi wa Vituo vya umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji zinazoleta tija uliofadhiliwa na Benki ya Dunia,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NM-AIST,Profesa David Mwakyusa na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Profesa Karoli Njau .
  Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya utendaji wa Kituo hicho 
  Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizindua mradi wa Vituo vya Umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia Bella Bird. 


  0 0


  0 0older | 1 | .... | 1878 | 1879 | (Page 1880) | 1881 | 1882 | .... | 3348 | newer