Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live

UCHANGIAJI WA MIGUU BANDIA AWAMU YA KWANZA WAANZA KWA WATU 1,000

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ametangaza kuanza kwa Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwa ajili ya Wananchi 1,000 wenye uhitaji wa miguu hiyo ilikuwawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi.
Katika zoezi hilo Wananchi wataweza kutoa michango yao kwa njia ya Simu, huduma za Kibenki au kufika Ofisi za Mkuu wa Mkoa na kuwasilisha michango yao.
Hatua hii inakuja baada ya wenye uhitaji wa Miguu Bandia kuwa kubwa tofauti na ile iliyokusudiwa na Mkuu wa Mkoa ya watu 200 ambapo awamu ya kwanza jumla ya watu 650 walichukuliwa vipimo. Makonda amesema bado uhitaji wa Miguu hiyo ni mkubwa hivyo amewaomba wadau ikiwemo Makampuni, Taasisi na Watu Binafsi kujitokeze kuchangia ili kutimiza dhamira yake ya kuwafanya walemavu kutembea.
Hadi sasa Wadau mbalimbali ikiwemo CCBRT wamechangia Miguu 25 kwaajili ya Miguu ya watu wenye maradhi wa Kisukari,Msanii Mrisho Mpoto miguu mitatu huku Taasisi za MOI, Ajma Othopedics Medical Service wakiunga mkono zoezi hilo.
Baada ya kuona uhitaji ni mkubwa wa Wananchi Kituo cha Utangazaji cha EFM na TV E wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbali.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumzana na waandishi wa habari leo juu ya Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwaajili ya Wananchi 1,000 wenye uhitaji wa Miguu hiyo
Meneja Mkuu wa EFM Radio na Tv E , Denis Busulwa (SEBO), (kulia) kizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbali Tv na Radio. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii


SERIKALI KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUDHIBITI AJALI BARABARANI

$
0
0
 Serikali imetoa mwezi mmoja kwa Mamlaka zinazohusika na masuala ya usalama barabarani kuhakikisha zinakamilisha uboreshaji wa mfumo wa kielektroniki wa uwekaji wa vifaa vya kufuatilia udhibiti mwendo barabarani ikiwa lengo ni kushughulikia matatizo ya kiusalama barabarani kupitia vyombo vya usafiri.
Akizungumza hayo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kuwa mfumo huo uendane na utengenezaji wa mpango wa Taifa wa kufuatilia masuala ya kiusalama barabarani utakaohusisha wataalam kutoka Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) na Wataalam wa Idara ya Usalama na Mazingira (Sekta ya Ujenzi).

"Shirikianeni kutengeneza mfumo ambao utasaidia kutambua matatizo mbalimbali yanayoweza kujitokeza barabarani ili kubaini mwenendo wa mabasi na malori mwanzo hadi mwisho wa safari zake",  amesema Naibu Waziri Ngonyani.

Amesisitiza kuwa mfumo ambao utaandaliwa na wataalam hao unatakiwa kukidhi mahitaji ya kila mmoja ili kuleta matokeo chanya kwa manufaa ya nchi yatakayosaidia kupunguza ajali za barabarani zinazotokana na mwendo kasi, kupambana na uhalifu na kulinda usalama wa abiria.

Aidha, Eng. Ngonyani amefafanua kuwa katika juhudi za kuhakikisha serikali inapunguza ajali za barabarani wizara yake kupitia Idara ya Usalama na Mazingira tayari imesaini mkataba wa kufunga kamera za udhibiti mwendo kasi katika barabara kuu ya TANZAM (Dar es Salaam - Tunduma), ambapo sehemu ya majaribio ya mradi huo imefanyika katika maeneo ya
Dar es Salaam - Chalinze - Morogoro.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni, amesema kuwa taratibu za kutengeneza mfumo huo zinatakiwa kukamilika haraka ili kusaidia Jeshi la Polisi kutumia mfumo huo kuweza kupambana na uhalifu katika maeneo mbalimbali ya nchi. 

Ametanabaisha kuwa Serikali itamchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote atakaejaribu kuhujumu mfumo huo kwani serikali itatumia fedha nyingi kuutekeleza kwa lengo la kuhakikisha usalama wa raia unalindwa ipasavyo.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Gilliard Ngewe, ameeleza manufaa ya mfumo huo kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa magari ya abiria na mizigo kuwa ni itasaidia kupunguza matumizi ya mafuta, uharibifu wa matairi ya magari mara kwa mara na kupunguza gharama za matengenezo ya magari.

Mfumo huo wa kieletroniki wa usalama barabarani ni moja ya mbinu zinazotumiwa na Serikali katika kuhakikisha matumizi ya usalama barabarani yanazingatiwa kwa mujibu wa Sheria, Taratibu na Kanuni.

 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza na wataalam wa mfumo wa kieletroniki wa usalama barabarani katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Masauni.

 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni, akichangia mada katika kikao kazi na wataalam wa mfumo wa kieletroniki wa usalama barabarani, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu Mweyekiti wa Baraza hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani.

 Kamanda wa Usalama Barabarani, Jeshi la Polisi Tanzania Fortunatus Muslim, akifafanua jambo kwa watalaam wa mfumo wa kieletroniki wa usalama barabarani katika kikao kazi kilichofanyika, jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Julius Chambo akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha watalaam wa mfumo wa kieletroniki wa usalama barabarani kilichofanyika, jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), Godfrey Nsato, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Eng. Hamad Masauni (hawapo pichani), namna mfumo wa kieletroniki wa kudhibiti mwenendo wa magari ya abiria na mizigo inavyofanya kazi, jijini Dar es Salaam. 

Ujenzi wa Tazara Flyover Wafikia Asilimia 53

INTRODUCING "MAZOEA" BY SOST Ft. BEKA FLAVOUR

GOOD ADVICE

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA BRIGEDIA JENERALI JOHN JULIUS MBUNGO KUWA NAIBU MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU

JK na Mama Salma Kikwete wakamilisha msimu wa mavuno kijijini Msoga, asema Umekuwa msimu mzuri.

$
0
0
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakivuna mahindi shambani kwao kijijini Msoga, Chalinze, Mkoa wa Pwani kukamilisha msimu wa mavuno ambao amesema umekuwa mzuri mwaka huu
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea na kazi ya kuvuna
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia mavuno mema

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiendelea kuvuna mahindi shambani kwao kijijini Msoga
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakifurahia mavuno mema ya  mahindi shambani kwao kijijini Msoga
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakifurahia mavuno mema ya  mahindi shambani kwao kijijini Msoga.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN ZIARANI WILAYA YA MAGHARIBI B LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akisalimiana na Mwenyekiti wa kampuni ya Azam Group  Bw.Said Salim Bakhresa mara alipowasili katika Viwanja vya Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko Fumba wakati alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi huo akiwa katika ziara ya Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Mgharibi
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group  Bw.Said Salim Bakhresa (wa pili kushoto) alipotembelea eneo la ufukwe katika Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko Fumba wakati alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi huo akiwa katika ziara ya Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Mgharibi
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group  katika Kijiji cha Fumba  Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Mgharibi leo wakati alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi huo akiwa katika ziara Wilaya ya Magharibi"B"
 Miongoni mwa Nyumba za kisasa ambazo zinajengwa na kampuni ya Azam Group huko Fumba Wilaya ya magharibi "B" Mkoa wa Mjini Magharibi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group  Bw.Said Salim Bakhresa (wa pili kushoto) alipotembelea eneo la ufukwe katika Ujenzi wa Nyumba za kisasa huko Fumba wakati alipotembelea kuangalia Maendeleo ya Ujenzi huo akiwa katika ziara ya Wilaya ya Magharibi"B" Mkoa wa Mjini Mgharibi. 

WADAU WA NGO’s WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUANZA UHAKIKI WA NGO’s NCHINI

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO BIBI SIHABA NKINGA AZINDUA MPANGO WA UHAKIKI WA NGO’S NCHINI

UTEUZI WA MADIWANI 12 WANAWAKE WA VITI MAALUM

Waziri Maghembe 'kuibeba' Rock City Marathon

$
0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe mwishoni mwa wiki hii alizindua rasmi usajili wa msimu wa nane wa mbio za Rock City Marathon huku akiahidi kushirikiana na waandaaji wa mbio hizo katika kuhakikisha kuwa zinatumika vema kuutangaza utalii wa ndani.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadhamini mbalimbali wa mbio hizo, Waziri Maghembe alisema azma yake hiyo inasukumwa na malengo ya mbio hizo ambayo ni kutumia mchezo wa riadha katika kutangaza utalii hususani katika Ukanda wa Ziwa.

"Kwa kuzingatia uzito wa malengo ya mbio hizo nitamke bayana kuwa nipo tayari kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi kuhakikisha kwamba kuanzia mwaka huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa kimataifa,'' alisema Waziri Maghembe ambae pia alithibitisha ushiriki wake kwenye mbio hizo zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kupita katika barabara mbalimbali za jiji hilo kabla hazijamalizikia katika uwanja huo.

Mbali na ushiriki wake,Waziri Maghembe alitoa wito kwa mashirika mbalimbali yaliyo chini ya wizara yake ikiwemo la Hifadhi za Taifa(Tanapa), Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Makumbusho ya Taifa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kufanikisha mbio hizo.

"Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo pia kama Wizara yenye dhamana ya utalii lazima tuvigeukie na kuvitangaza kwa nguvu na kwa njia tofauti ikiwemo michezo,'' alisema Waziri Maghembe huku akivitaja baadhi ya vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Kisiwa cha Saanane, Makumbusho ya kabila la Wasukuma pamoja na tamaduni za makabila ya wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka minane iliyopita zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, PUMA, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Mwanza Hotel , Real PR Solutions Limited, Afrimax Strategic Partnerships Limited, EF Outdoor, CF Hospital na ATCL. 
 WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe akizungumza na wadau mbalimbali wa mchezo wa riadha hapa nchini pamoja na waandaaji wa mbio za Rock City Marathon kwenye hafla maalumu ya uzinduzi  rasmi usajili wa msimu msimu wa nane wa mbio hizo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Zenno Ngowi akizungumza kwenye hafla hiyo. Alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 2000 na watazamaji zaidi ya 30,000. 
 Mratibu wa mbio hizo zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International, Bi Adeline Ndesanjo akitoa maelezo kuhusu maandalizi ya mbio hizo kwenye hafla hiyo. Alisema mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuhusisha washiriki wengi zaidi kutoka kila kona ya dunia ikiwemo Afrika, Ulaya,China,Mashariki ya Kati hususani Israel na Marekani . 
 Wadhamini nao hawakuwa nyuma!Meneja Masoko wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy, Bw Machumani Shebe alisema ushiriki wao kwenye mbio hizo umechagizwa zaidi na azma ya kampuni yake hiyo kuisaidia serikali katika kuutangaza utalii wa ndani. 
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof Jumanne Maghembe akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaaji wa mbio hizo pamoja na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo  viongozi wa serikali pamoja na wadhamini wa mbio hizo.

MAGAZETI YA JUMANNE LEO AGOSTI 22,2017

Mohamed Kivugo: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumba

$
0
0
FUNDI magari mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Mohamed Kivugo mwenye miaka 45, amesema kwamba fedha zake alizokabidhiwa jana baada ya kushinda kwenye Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', atazitumia kujengea nyumba ili aondokane na changamoto ya makazi.

Kivugo aliyasema hayo jana wakati anapokea zawadi ya Sh Milioni 20 za ushindi wa Biko alizokabidhiwa katika benki ya NMB, tawi la Bank House Posta, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kivugo alisema dhamira yake kubwa ni kutatua changamoto ya makazi kwa kuzitumia fedha za Biko kujenga nyumba.

"Ingawa nimepata ushauri mzuri kutoka kwa watu wa NMB baada ya kukabidhiwa fedha zangu kutoka Biko baada ya kushinda kwenye droo ya 33 iliyochezeshwa Jumapili, lakini naamini wazo la nyumba ni zuri kwangu.

"Nawashauri Watanzania wenzangu wacheze Biko mara nyingi na wasikate tamaa ili waweze kuibuka na ushindi kama nilivyoibuka mimi, ukizingatia kuwa biko ni bahati nasibu inayotoa ushindi na kukabidhi fedha kwa Jataka, "Alisema.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, aliwataka Watanzania kucheza Biko ili wavune utajiri mkubwa kutoka kwenye bahati nasibu yao inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea katika Tigo Pesa, MPesa na Airtel Money huku namba ya Kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.

"Kushinda Biko ni rahisi pamoja na kupokea zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwenye simu za washindi wanazotumia kuchezea Biko bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 inayotoka kila Jumatano na Jumapili kama aliyoshinda mshindi wetu Kivugo wa Tabata," Alisema.

Kwa mujibu wa Melles, zaidi ya Sh Bilioni mbili zimelipwa kwa washindi katika miezi mitatu ya Mei, Juni na Julai, huku akiwataka Watanzania wacheze kwa wingi na mara nyingi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kuibuka mamilioni ya bahati nasibu ya Biko.
Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia mwenye fulana ya Biko akimkabidhi fedha zake mshindi wao wa Bahati Nasibu, Mohamed Kivugo aliyeibuka kidedea katika droo ya 33 iliyochezeshwa Jumapili. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Bank House, Posta jijini Dar es Salaam akishuhudia makabidhiano hayo.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU AGOSTI 21, 2017


RC SHINYANGA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MJINI SHINYANGA

$
0
0
Jumatatu Agosti 21, 2017, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (aliyesimama pichani) alifanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zimamoto karibu na soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kusikiliza kero za wananchi. 

Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa,na watumishi mbalimbali wa serikali alisikiliza kisha kujibu kero za wananchi huku pia akitoa nafasi kwa watumishi kutoka idara mbalimbali kujibu hoja na kero za wananchi. 

Miongoni mwa kero zilizoibuka eneo la mkutano huo ni pamoja na ardhi ambapo baadhi ya wananchi walieleza kutoridhishwa namna ardhi inavyotolewa na jinsi migogoro ya ardhi inavyotatuliwa. 

Kero nyingine ni ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari polisi waliodaiwa kutowajali wananchi wanaofika katika kituo cha polisi huku askari polisi wakiendelea kufanya mambo yao ikiwemo kuchat kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuhudumia wananchi wanaofika kituoni.
Mkutano unaendelea,viongozi wakiandika dondoo muhimu/maswali ya wananchi

Suala la vumbi katika barabara ambazo ujenzi wake haukamiliki mjini Shinyanga nalo likiibuka kwamba afya zao ziko hatarini kutokana na vumbi hilo. Pia wananchi wakaomba kuwekewa taa za barabarani pamoja na askari wa usalama barabarani katika eneo la Japanese Corner mjini Shinyanga ambapo panadaiwa kutokea ajali za mara kwa mara. 

Kero ya bei kubwa ya maji nayo haikusahaulika,wananchi walieleza kuwa bei ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA). Hali kadhalika wananchi wakaomba kuwekewa sehemu ya kupumzikia walau wawekewe mwamvuli katika mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule akizungumza

Wananchi pia waliomba kuongezwa kwa waganga katika kituo cha afya Kambarage ambacho kinadaiwa kuzidiwa na idadi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma. Wazee nao wakatoa kilio chao cha kutaka huduma bora ya afya wakiomba kuingizwa kwenye bima ya afya badala ya kupewa tu dawa bure. 

Akijibu hoja mbalimbali za wananchi, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack aliwataka watumishi wa umma kuzingatia maadili yao ya kazi katika kuwatumikia wananchi huku akiwasisitiza kutatua kero za wananchi kwa wakati.
Katibu tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akijibu hoja za wananchi


Telack alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa pale inapotokea mkandarasi anayejenga barabara mjini hajamwaga maji kwenye barabara kwani wamemwagiza kuwa anamwaga maji ili kuepusha vumbi. Aidha baada kusikiliza kero za wananchi, mkuu huyo wa mkoa aliagiza kupewa taarifa ya utekelezaji wa mambo mbalimbali waliyokubaliana wakati wa mkutano huowa hadhara ifikapo Septemba 15,2017 ili kuhakikisha kero za wananchi zinapungua. 

Dkt. Mwakyembe: MCL endeleeni kusimamia maadili na kuhabarisha Jamii

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akibofya kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Muonekano Mpya wa Gazeti la Michezo la Mwanaspoti Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni baadhi ya Viongozi waandamizi wa Kampuni ya Uchapishaji Magazeti ya Mwananchi Communications Ltd (MCL).

Na Benedict Liwenga.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza Kampuni ya Uchapishaji Magazeti ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kusimamia maadili kwa kuhabarisha na kuielimisha jamii ya Kitanzania. Pongezi hizo amezitoa jana wakati wa Uzinduzi wa Muonekano Mpya wa gazeti pendwa la michezo la Mwanaspoti linalochapishwa na Kampuni hiyo.

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa, mara kwa mara MCL imekuwa ikiisaidia jamii kwa kujihusisha katika masuala mbalimbali ya kijamii kama vile wakati wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera imeweza kutoa mchango wake mkubwa kwa jamii na daima imekuwa ikilinda maadili na weledi wa kazi ya uandishi kwa wafanyakazi wake jambo ambalo linaonyesha ushirikiano mzuri baina ya Serikali, Kampuni na jamii.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na baadhi ya Viongozi waandamizi wa Kampuni ya Uchapishaji Magazeti ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa Muonekano Mpya wa Gazeti la Michezo la Mwanaspoti Jijini Dar es Salaam.

“Mimi nawapongeza na kuwashukuru sana MCL kwakuwa mstari wa mbele katika kulinda maadili katika kazi zenu, endeleeni kulinda maadili kwa kuhabarisha na kuielimisha jamii, sijaona mkivunja maadili ya kazi zenu na hakika mnajijengea sifa nzuri kwa wengine”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa, kwa sasa kumeibuka wimbi kubwa la Waandishi wa habari (Makanjanja) ambao hawana vyeti wala weledi wa kufanya kazi ya uandishi wa habari na hao wamekuwa kila wakati wakirusha taarifa zisizo sahihi hususani katika mitandao ya kijamii jambo ambalo Serikali haiwezi kulifumbia macho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akichomoa gazeti jipya la Michezoa la Mwanaspoti ambalo lina muonekano mpya wa kisasa zaidi mara baada ya kulizindua Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bw. Francis Nanai amesema kwamba lengo la kampuni hiyo kuja na muonekano mpya wa gazeti hilo ni kuwapa ladha mpya wasomaji wake nchini kote, na hiyo ni mara ya sita kwa gazeti hilo kubadilishwa muonekano wake tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001.

“Sisi kama wadau wa michezo tumewasikiliza wasomaji wa gazeti letu na tukayafanyia kazi mawazo yao na ndiyo maana tukaamua kuja na muonekano mpya wa gazeti hili ambao uko kimataifa zaidi”, alisema Nanai.

Aliongeza kuwa, gazeti hilo lilianzishwa na waandishi wa tatu mwaka 2001 na lilikuwa likitoa nakala 3,000 kwa siku ambapo kwa sasa kuja kwa muonekano mpya wa gazeti hilo kutaongeza idadi ya wasomaji tofauti ilivyokuwa mwanzo na idadi ya uchapishaji imeongezeka hadi kufikia nakala 60,000 kwa siku.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchapishaji Magazeti ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Bw. Francis Nanai (kulia) wakiwaonyesha Waandishi wa habari muonekano mpya wa gazeti la michezo la Mwanaspoti mara baada ya uzinduzi Jijini Dar es Salaam.

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELA MIRADI YA UMEME WA GESI YA KINYEREZI II NA ULE WA UPANUZI KINYEREZI I

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (Mb), wapili kulia, akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, kutembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2018. Kamati hiyo pia ilitembelea kituo cha kupkea gesi asili kilicho jirani na Miradi hiyo.

KAMATI ya Bunge ya Bajeti, imetembelea miradi ya kuzalisha umeme wa gesi ya Kinyerezi II, na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I unaoendeshwa na Serikali kupitia Shrika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, pia ilitembelea kituo cha kupokea gesi asili inayotumika kuzalisha umeme kilichoko jirani na miradi hiyo.

Katika ziara hiyo, mwenyeji wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, (Mb), Mhe.Dkt.Medard Kalemani, aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa miradi hiyo inaendelea kama ambavyo Serikali ilitarajia na kwamba Watanzania wategemee ongezeko kubwa la upatikanaji wa umeme pindi miradi hiyo itakapokamilika. 
 Wajumbe wa Kamati wakipita pembezoni mwa moja ya mashine kubwa (genereta), kati ya 8 zinazofungwa kwenye mradi wa Kinyerezi II

“Mhe. Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Kamati, miradi hii kunzia ule wa Kinyerezi I unaopanuliwa ambapo kutakuwa na ongezeko la umeme Megawati 35 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 185 zitakazozalishwa kutoka Kinyerezi I, na huu wa Kinyerezi II utakapokamilika Agosti mwakani (2018) utatupatia Megawati 240 na ukijumlisha na miradi mingine itakayofuatia ya Kinyerezi III na VI, tutakuwa na jumla ya Megawati 1175.” Alifafanua Mhe. Dkt. Kalemani.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephene Manda aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa mradi huo utakuwa na jumla ya mashine 8 ambazo zitafua umeme na tayari ufungaji wa mashine hizo umeanza na unaendelea na kuongeza kuwa kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, TANESCO itaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na kufanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kadri kazi ya ufungaji wa mashine hizo utakavyokuwa unakamilika.

Alisema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.


Mhandisi Manda, (waliyenyoosha mkono), ambaye ni Meneja Mradi wa Kinyerezi II, akwapatia maelezo wajumbe wa Kamati akiwemo Naibu Waziri Dkt. Kalemani.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Washindi wa weka amana na Benki ya CBA wapatikana

$
0
0
BENKI ya CBA, jana iliendesha droo yake ya kwanza katika kampeni ya kuhamasisha umma kujiwekea  akiba inayojulikana kama ‘weka amana ushinde’ ambapo washindi wawili walipatikana na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni tatu

Jesen Anderson Mbise kutoka Arusha aliibuka mshindi kwa upande wa wateja binafsi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja, huku Hoteli ya Tiffany ya jijini Dar es Salaam wakiibuka washindi katika upande wa taasisi na kujinyakulia shilingi milioni 2.

Zaidi ya shilingi milioni 20 zimetengwa kwa ajili ya kutolewa kama zawadi katika kampeni hiyo ambayo itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ambayo ilishuhudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha,  Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa CBA Gift Shoko alisema lengo la promosheni hiyo ni kuhamasisha umma kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba.

”Kampeni hii inalenga kuwahamasisha wateja wetu waliopo na watarajiwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. Kuweka akiba ni muhimu kwa kuwa kunawezesha kufanya uwekezaji pamoja na kupambana na matukio yasiyotarajiwa ambayo yanahitaji fedha,” alisema Shoko

Alisema kujiwekea akiba ni muhimu haswa katika kipindi hiki kinachoelekea mwisho wa mwaka ambapo huwa na mahitaji makubwa ya kifedha kwa ajili ya shughuli kama kulipa ada za shuke, kodi za nyuma, likizo pamoja na shughuli nyingine. Kwa mujibu wa Shoko, benki ya CBA imerahisisha namna ya wateja wake kujiwekea akiba ambapo wanaweza kutumia simu zao za kupitia huduma ya M-PAWA, kwa kutumia njia ya mtandao pamoja na kutembelea matawi yake yaliyopo sehemu mbali mbali.

Benki ya CBA kwa sasa ina matawi 11, matano yakiwepo jijini Dar es Salaam huku matano yakiwepo Arusha, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Moshi, na Tunduma. 
Mkurugenzi wa benki ya CBA, Gift Shoko, ( watatu kushoto) akimshuhudia Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo, Mussa Kitambi(Kushoto) alipokuw akimpigia simu mkazi wa Arusha Jesen Mbise aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 1/- wakati wa uzinduzi wa droo ya kwanza ya promosheni ya akiba inayojulikana kama ‘Weka amana ushinde’ zaidi ya milioni 20 zitashindaniwa na wateja wa benki hiyo.wapili kushoto ni Msamimamizi wa michezo wa kubahatisha nchini ,Abdallah Hamedi.
Mkurugenzi wa benki ya CBA, Gift Shoko( kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi Promosheni ya ‘Weka amana Ushinde’ ambapo zaidi ya milioni 20 zitashindaniwa na wateja wa benki hiyo. Katikati ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo,Mussa Kitambi na msimamizi wa michezo ya kubahati nchini Abdallah Hamedi.
Mkurugenzi wa benki ya CBA, Gift Shoko,( kulia) akibofya kitufe cha kompyuta kuashiria Uzinduzi wa droo ya kwanza ya promosheni ‘Weka amana Ushinde’ zaidi ya milioni 20 zitashindaniwa na wateja wa benki hiyo. Katikati ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo,Mussa Kitambi na Msamimamizi wa michezo wa kubahatisha nchini Abdallah Hamedi.

MBUNGE CHALINZE AKEMEA UFUGAJI HOLELA AMBAO UHARIBU RUTUBA

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze

MBUNGE wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekabidhi pikipiki kumi, zilizogharimu sh. Mil. 22.5 kwa maafisa mifugo wa kata, ili waweze kuwafikia wafugaji wote, kupeleka sera ya kufuga kisasa na kuondoa migogoro na wakulima. Aidha amekemea tabia inayofanywa na baadhi ya wafugaji ya kufuga kizamani kwa kuswaga makundi ya ng’ombe kwenye eneo moja hali inayosababisha kuharibu rutuba.

Akikabidhi pikipiki hizo, huko Lugoba Ridhiwani alieleza, vyombo hivyo vya usafiri vikatumike kusimamia majukumu waliyonayo badala ya kuvitumia kwa matumizi yao binafsi. Aliwataka jamii ya wafugaji kuachana na mtazamo hasi wa kufuga kizamani mifugo lundo isiyo na tija pamoja na kuingia katika maeneo ambayo hayajatengwa kwa ajili yao.

Ridhiwani, alieleza kuwa wafugaji hasa wa kimasai wanaamini kuwa na ng’ombe wengi ndio utajiri, waondoe dhana hiyo kwani sio sifa, wajaribu kufuga mifugo michache na kujiwekea kasumba ya kufuga kwenye mazizi. Hata hivyo, alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa kwa kusimamia na kuyafanyia kazi maazimio ya madiwani ambayo huwa wakitoa.

Ridhiwani, alito mafuta  lita tano kwa kila pikipiki na kuahidi kuangalia uwezekano wa kufanya utaratibu kila mwezi kwenye posho zinazokwenda katika kata maafisa mifugo hao wataongeza japo 5,000 kwa ajili ya mafuta ya pikipiki hizo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Lukoa alisema pikipiki hizo zimenunuliwa kutokana na mapato ya ndani ya halmashauri. Alizitaja kata zilizokabidhiwa usafiri huo kuwa ni sanjali na Vigwaza, Kibindu, Mbwewe, Talawanda, Msata, Kimange, Kiwangwa, Miono, Ubena Zomozi na Mandela.
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifurahi jambo na baadhi ya watendandaji wakati wa zoezi la kukabidhi pikipiki hizo.

Lukoa  alieleza kwa msimu wa bajeti 2017/2018 wanatarajia kununua pikipiki nyingine 15 kwa ajili ya watendaji na nyingine nane kwa ajili ya maafisa mifugo wa kata na vijiji. Aliwashukuru madiwani kwa ushirikiano na CMT kwa mchango  wao mkubwa katika kutoa maazimio yaliyotakiwa yatekelezwe na halmashauri na sasa yamefanikiwa. 

SOMA ZAIDI HAPA
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live




Latest Images