Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

MADEREVA KITUO CHA SIMU 2000 WAGOMEA TOZO YA SHILINGI 1000

$
0
0
Mpiga picha wa Globu ya Jamii mapema leo asubuhi amekumbana na adha ya usafiri,kufuatia Madereva katika kituo cha mabasi simu 2000 Manispaa ya Ubungo jijini Dar kugoma kutoa huduma ya usafiri,kwa kile walichodai kupandishiwa tozo kutoka shilingi 500 hadi 1000.

Akizungumza zaidi mmoja wa Madereva wa dala dala katika mgomo huo (hakutaka kujitambulisha jina),alisema kuwa wao hawawezi kulipa tozo hiyo wakati miundombinu ya kituo hicho si rafiki na hairidhishi kabisa kwa vyombo vyao vya usafiri.

"ni vyema wakazirekebisha kwanza changamoto kadhaa zilizopo hapa kituoni,kisha baadae waje na huo mkakati wao wa kutupandishia hiyo tozo yao,lakini kwa sasa itakuwa vigumu kulipa kwa sababu kama unavyoona mazingira yalivyo hapa kituoni",alisema mmoja wa Madereva.

Mpiga picha wa Globu ya Jamii pamoja na kuonja joto ya jiwe ya kukosa usafiri,pia alijionea adha waliokuwa wakiipata abiria wengine waliokuwepo kituoni hapo,huku baadhi ya abiria wakilazimika kutumia usafiri wa piki piki kuwahi kwenye shughuli zao na wengine wakitembea kwa Miguu. 

Mpaka Globu ya Jamii inaondoka kituoni hapo ufumbuzi bado ulikuwa haujapatikana.
 Madereva na Makondakta wakijadiliana kufuatia mgomo huo
Baadhi ya mabasi (dala dala) yakiwa yamepaki kituoni hapo yakisubiri mgomo huo upatiwe ufumbuzi.
 Baadhi ya abiria wakisubiri usafiri kituoni hapo mapema leo asubuhi


TANZIA;MSIBA MKUBWA NJENJE -BABU FRANCIS AFARIKI DUNIA

$
0
0


 


MWEKA HAZINA wa miaka mingi wa Kilimanjaro Band, ambaye alijulikana kwa wapenzi wengi kutokana na kuwa mkata tiketi wa bendi wa miaka mingi sana, Francis Mnguto, maarufu kwa jina la Babu Francis amefariki leo alfajiri nyumbani kwake Ilala Flats Dar es Salaam. 
 
Kwa miezi kadhaa Babu Francis amekuwa akisumbuliwa na tatizo la figo. Taarifa kutoka kwa familia ni kuwa mazishi yatakuwa Dar es Salaam Jumatano 23 Agosti. Msiba upo nyumbani kwake Ilala Flats Dar es Salaam.

 
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN. 

GARI LAACHA NJIA NA KUPARAMIA MAWE SEGEREA NJIAPANDA BONYOKWA

$
0
0
 Wakazi wa Tabata Segerea Wilaya ya Ilala wakiwa wanashangaa gari aina ya Land Cluser Prado ambayo imecha barabara na kuvamia Vigingi Vilivyopo kwenye barabara ya kukatisha kwenda Kimara Bonyokwa
 Gari aina ya toyota Land Cluser Ikiwa ipo juu ya mawe mara baada ya kuruka na kuacha njia katika eneo la tabata Segerea njia panda ya kwenda Bonyokwa, gari hiyo imepanda mawe hayo katika harakati za kumkwepa mtu aliyekuwa anakuja mbele yake kwa speed kali hata hivyo katika ajali hiyo Hakuna majeruhi wala mtu aliyefariki wote walitoka Salama
 Gari aina ya toyota Land Cluser Ikiwa ipo juu ya mawe mara baada ya kuruka na kuacha njia katika eneo la tabata Segerea njia panda ya kwenda Bonyokwa, gari hiyo imepanda mawe hayo katika harakati za kumkwepa mtu aliyekuwa anakuja mbele yake kwa speed kali hata hivyo katika ajali hiyo Hakuna majeruhi wala mtu aliyefariki wote walitoka Salama
Gari aina ya toyota Land Cluser Ikiwa ipo juu ya mawe mara baada ya kuruka na kuacha njia katika eneo la tabata Segerea njia panda ya kwenda Bonyokwa, gari hiyo imepanda mawe hayo katika harakati za kumkwepa mtu aliyekuwa anakuja mbele yake kwa speed kali hata hivyo katika ajali hiyo Hakuna majeruhi wala mtu aliyefariki wote walitoka Salama

MKUU WA WILAYA UBUNGO KISARE MAKOLI AINGILIA KATI MGOMO WA DALADALA SIMU 2000,AWEKA MAMBO SHWARI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ,Kisare Makoli (pichani kati) akiwa ameongozana na baadhi ya madereva wa dala dala wakielekea  kwenye kituo cha daladala cha Mawasiliano simu 2000 mara baada ya madereva wa Daladala kupinga tozo ya shilingi 1000 kama Ushuru wa magari ambapo awali walikuwa wanalipa shilingi 500
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ,Kisare Makoli, akizungumza na Madereva Daladala waliopo katika eneo la Simu 2000 mara baada ya kuweka mgomo kupinga tozo ya Shilingi 1000 na kudai kuwa barabara hiyo ni mbovu,Mhe.Makoli ameagiza kuendelea kulipwa tozo hiyo ya zamani ya shilingi 500 badala ya 1000 iliyokuwa imeongezwa,na kwamba madereva waendelee na shughuli zao kusafirisha abiria kama kawaida.

 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ,Kisare Makoli, akizungumza na Madereva Daladala waliopo katika eneo la Simu 2000 mara baada ya kuweka mgomo kupinga tozo ya Shilingi 1000 na kudai kuwa barabara hiyo ni mbovu


 Askari wa kikosi cha Kutuliza Ghasia wakiwa wanaimarisha ulinzi katika eneo la kituo cha Daladala cha Simu 2000

 Askari wa kikosi cha Kutuliza Ghasia wakiwa wanaimarisha ulinzi katika eneo la kituo cha Daladala cha Simu 2000
 Askari wa kikosi cha Kutuliza Ghasia wakiwa wanaimarisha ulinzi katika eneo la kituo cha Daladala cha Mawasiliano Simu 2000.

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA VITU MBALIMBALI GEREZA LA SEGEREA JIJINI DAR.

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa wapili kushoto akikabidhi, khanga ambazo kwaajili ya kinamama na watoto waliopo gerezani  kwa mkuu wa gereza la Segerea, Kamishna Msaidizi wa magereza, Godfrey Kavishe kulia ikiwa ni moja ya vitu vyenye thamani ya milioni nane (8,000,000) vilivyotolewa kwa wafungwa wanawake na watoto wa gereza hilo na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Katikati ni Mkaguzi msidizi wa magereza, Esther Mpotola, Mrakibu wa Magereza, Adeline Mgamtwa na Meneja Uhusiano wa Wawekezaji wa Benki hiyo, Hilda Rwanshane.
 Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa wapili kushoto akiwa katika pichaya pamoja na mkuu wa gereza la Segerea, Kamishna Msaidizi wa magereza, Godfrey Kavishe mbele ikiwa ni moja ya vitu vyenye thamani ya milioni nane (8,000,000) vilivyotolewa  na benki ya CRDB kwa wafungwa wanawake na watoto wa gereza hilo.Katikati ni Mkaguzi msidizi wa magereza, Esther Mpotola, Mrakibu wa Magereza, Adeline Mgamtwa na Meneja Uhusiano wa Wawekezaji wa Benki hiyo, Hilda Rwanshane.
 Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa wapili kushoto akikabidhi  boksi la maziwa ya unga na baadhi ya vitu vya michezo ya watoto  kwa mkuu wa gereza la Segerea Kamishna Msaidizi wa magereza Godfrey Kavishe kulia ikiwa ni moja ya vitu vyenye thamani ya milioni nane (8,000,000) vilivyotolewa kwa wafungwa wanawake na watoto wa gereza hilo na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Katikati ni Mkaguzi msidizi wa magereza, Esther Mpotola, Mrakibu wa Magereza, Adeline Mgamtwa na Meneja Uhusiano wa Wawekezaji wa Benki hiyo, Hilda Rwanshane.
 Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa wapili kushoto akikabidhi, Mashine za dawa ya kuulia wadudu  kwa mkuu wa gereza la Segerea, Kamishna Msaidizi wa magereza, Godfrey Kavishe kulia ikiwa ni moja ya vitu vyenye thamani ya milioni nane (8,000,000) vilivyotolewa kwa wafungwa wanawake na watoto wa gereza hilo na wafanyakazi wanawake wa benki hiyo. Katikati ni Mkaguzi msidizi wa magereza, Esther Mpotola, Mrakibu wa Magereza, Adeline Mgamtwa na Meneja Uhusiano wa Wawekezaji wa Benki hiyo, Hilda Rwanshane.

NSSF YATOA MKOPO WA BILIONI 8.9 KUFUFUA KIWANDA CHA USINDIKAJI WA NAFAKA MWANZA

$
0
0
Mwanza, Agosti 20, 2017: Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF) limetoa mkopo wa Tshs bilioni 8.99 kwenda kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ya Tanzania kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda cha usindikaji wa nafaka katika jiji la Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za mfuko huo kutekeleza kwa vitendo sera ya uchumi wa viwanda hapa nchini.

Mkopo huo unalenga kuiwezesha Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuweza kuvifufua vinu vyake viwili vya usindikaji wa mazao ya mpunga na mahindi vilivyopo mkoani humo kwa  kununua vifaa na mitambo mipya na hatimaye kuanza uzalishaji baada ya kusimamisha uzalishaji huo mapema miaka ya 1990.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya hundi ya mkopo huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mwanza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama alitoa wito kwa Wizara yenye dhamana ya kulimo hapa nchini kuisimamia vyema bodi hiyo kiutendaji ili iweze kuijendesha kwa ufanisi utakaoiwezesha kurejesha mkopo huo unaotarajiwa kulipwa ndani ya kipindi cha miaka sita (6) ikijumlisha kipindi cha mpito yaani (grace period) ya mwaka mmoja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (wa pili kushoto) Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia) ikiwa ni mkopo kutoka Shirika hilo kwenda bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kwa ajili ya ufufuaji wa kiwanda cha usindikaji wa nafaka kilichopo jijini Mwanza. 

"Mbali na Wizara yenye dhamana ya kilimo, pia niwaombe sana uongozi wa mkoa wa Mwanza chini ya Mkuu wa mkoa kutambua kuwa ufanisi wa kiwanda hiki unategemea sana uwepo wa malighafi ya kutosha hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha uwiano kati ya uzalishaji wa malighafi na uzalishaji wa kiwanda vinakwenda sambamba,'' alisisitiza. 

Alilipongeza Shirika la NSSF  kwa uwekezaji wa viwanda vyenye tija kiuchumi ndani ya muda mfupi ambapo kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja uliopita hadi sasa shirika hilo limewekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kiwanda cha kutengeneza viuadudu vya kuua vimelea vya mbu kiitwacho Tanzania Biolarvicide Limited kilichopo Kibaha, mkoani Pwani.

"Uwekezaji wa NSSF pia unaonekana kwenye bodi ya nafaka na Mazao mchanganyiko ya Tanzania, Mkoani Dodoma, viwanda vipya vya kuzalisha sukari Mkulazi, mkoani Morogoro, kiwanda cha chaki Maswa (Maswa Chalk & General Enterprises) ambacho kipo Simiyu...hongereni sana!'' alipongeza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa hundi hiyo kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba (kushoto) huku wadau wengine wakishuhudia.

Waziri Mhagama alitumia wasaa huo pia kuwataka  waajiri wasiolipa michango ya wanachama kuwasilisha michango hiyo kwa wakati na kwa usahihi kwani  kutofanya hivyo ni kosa kisheria na  kuanwanyima haki wanachama hao huku akisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa wale wasiotekeleza sharia hiyo.


Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba alimuhakikishia Waziri Mhagama kuwa mbali na kuisimamia kwa ukaribu bodi hiyo ili iweze kurejesha mkopo huo, wizara yake imejipanga kuhakikisha kwamba miradi yote ya kilimo inayohusisha uwekezaji kutoka kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini inasimamiwa kwa umakini, ufanisi na weledi mkubwa ili kulinda pesa ya wanachama wa mifuko hiyo.

"Kwa kutambua kwamba ufanisi wa viwanda hivi unategemea zaidi kilimo kuna mipango na mikakati mizuri kuhakikisha mnyororo wa thamani unaohusika kuzalisha malighafi za viwanda hivi haukatiki,'' alisema Waziri Tizeba.
Kabla ya makabidhiano hayo Waziri Mhagama alipata wasaa kukugua mitambo ya kinu cha kukoboa mchele kinachotarajiwa kufufuliwa kupitia mkopo huo ambapo Mtendaji mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko Bw. John Maige (mbele) alimuhakikishia Waziri Mhagama na wadau wengine kuwa kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutawezesha jumla ya tani 96 za mchele kukobolewa kwa siku kupitia kinu hicho.

Alitaja baadhi ya mipango na mikakati hiyo kuwa ni pamoja na ujio wa Mpango maalumu wa kuandaa mbegu bora unaotekelezwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Bill Gates. Alikili kuwa kwasasa taifa linakabiliwa na uhaba wa mbegu bora unaotakona na utegemezi wa mbegu hizo kutoka nje ya nchi huku taifa likizalisha asilimia 35 tu ya mbegu hizo.

VIDEO: WANAKIJIJI WA UFYAMBE WAJIKWAMUA NA KERO YA UMBALI WA ZAHANATI KWA KUANZA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI

OPERESHANI MAALUMU YA KUPAMBANA NA KILIMO CHA BANGI, WATANO MBARONI MVOMERO … EKARI 25 ZATEKETEZWA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika dumu) akimimina mafuta ili kuchoma lundo la bangi iliyokuwa imeng’olewa Augosti 19, 2017 na kikosi kazi maalumu katika moja ya mashamba ya bangi katika kitongoji cha Lufuna, Kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta, wilaya ya Mvomero .

Na John Nditi, Globu ya Jamii - Morogoro

POLISI mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maofisa wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini wamefanikiwa kuteketeza mashamba ya bangi ya ukubwa wa zaidi ya ekari 25 na kuwatia mbaroni watu watano akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lufuna , Asteri Telesphor (27). Watu hao miongoni mwao ni Mwenyekiti wa Kitongoji hicho baada ya kukutwa wakijihusisha  na  kilimo  bangi kwa njia ya umwagiliaji kando kando ya mto Mgeta, katika kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , wilayani Mvomero.

Operesheni hiyo maalumu ya kupambana na dawa za kulevya hasa kilimo cha bangi iliyofanyika  Augosti 19, mwaka huu   na kuongozwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama  mkoa , Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe akiwa na  Maofisa wa mamlaka ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya  pamoja na viongozi wa wilaya ya Mvomero.
Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoa wa Morogoro na wilaya ya Mvomero walioongozwa na Mkuu wa mkoa Dk Kebwe Stephen Kebwe pamoja na askari Polisi wakiwa katika zoezi la kung’oa na kufyeka miche ya bangi kwenye moja ya mashamba ya bangi katika kitongoji cha Lufuna , Kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta, wilaya ya Mvomero .

Timu ya Opereshani hiyo ililazimika kuacha magari eneo la kijiji cha Homboza , Kata  Mlali  na kutembea kwa miguu kwa  muda wa zaidi  ya saa mbili kufika katika   vitongoji vya Lufuna na Tagata  vilivyopo kijiji cha Masalawe , kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta , wilayani Mvomero  kwa ajili ya kutekeleza mashamba hayo. Kugundulika kwa mashamba hayo ni kufuatia   Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mkoa kupata  taarifa kutoka kwa wasiri juu ya uwepo wa uzalishaji mkubwa wa bangi eneo hilo.

Akizubngumza katika eneo la mashamba hayo , Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka hiyo, Mihayo Msikhela alisema  , opereshani za kutekeleza dawa za kulevya hasa mashamba ya bangi  ni endelevu  kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama vya mikoa husika .

“ Serikali imekataza matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo bangi na ili kutokomeza jambo hii opereshani za kushitumiza zitaendelea kufanyik maeneo mbalimbali nchini na kwamba serikali haijaribiwi” alisema Mihayo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( mbele ) akivuka mto Mgeta akifuatiwa na Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Mihayo Msikhela , Aug 19, 2017 ili kushiriki na kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kuteketeza shamba la bangi iliyolimwa kwa njia ya kilimo cha umwagiliaji kando kando mwa mto huo , katika kitongoji cha Lufuna , Kijiji cha Masalawe, Kata ya Luale , Tarafa ya Mgeta, wilaya ya Mvomero .

Naye  Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema ,  watu watano walikamatwa katika opereshani hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lufuna , Kijiji cha Masalawe , Kata ya Luale Tarafa ya Mgeta , Asteri Telesphor (27) baada ya kukutwa  na kiroba cha bangi iliyoivuna kutoka shambani mwake.


MKUTANO WA 37 WA SADC WAMALIZIKA KWA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI KUMPONEZA RAIS DKT. MAGUFULI

NHIF yatakiwa kuongeza wanachama wasio waajiriwa

$
0
0
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetakiwa kuongeza jitahada za kuwasajili wanachama wengi wa mfuko huo ili vituo vya serikali viweze kutoa huduma kwa wananchi wengi. Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kituo cha afya cha Mazwi kilichopo katika Manispaa ya Wilaya ya Sumbawanga mwishoni.

Alisema Mkoa wa Rukwa umefikia asilimia 27 ya wananchi wanaotumia bima ya afya Kitaifa,hivyo waongeze kuwashawishi wananchi wengi zaidi kujiunga na mfuko huo pamoja na mfuko wa afya ya jamii(CHF).

“nimesema kuanzia sasa ninaanza kuwapima kwa kusajili wananchi ambao hawapo kwenye mfumo rasmi wa ajira,ninataka vijana wengi wajiunge kwa wingi kwa kwa kujiunga kama kikundi na kujiunga na bima inayojulikana kama  ‘Kikoa” kwa kujiunga kikundi cha kuanzia watu kumi,wafikieni huko huko walipo.

Kwa upande wa Mfuko wa Afya ya jamii(CHF) waziri huyo hivi sasa kuna CHF iliyoboreshwa hivyo kadi hiyo inatumika kwenye vituo vyote vya halmashauri  na si pale mwanachama alipokatia,”ni bora tuwachangishe elfu kumi kumi za watanzania ili tuweze kufikia usajili wananchi wengi na kupata huduma za afya bila vikwazo.

Hata hivyo alishauri Manispaa hiyo kutengezea kadi ambayo itakua rafiki kwa mwanachama kuweza kuiweka kwenye waleti au mahali pengine ambayo itakua rahisi kwa kutunza na siyo kadi za hivi sasa ambayo ni mzigo kwa mwanachama kuibeba kwani kadi hiyo ni kubwa. 

Aidha,alisema wizara yake inataka kuongeza gharama ya CHF iliyoboreshwa ya  shilingi elfu ishirini ambapo mwenye kadi hiyo ataenda kupata huduma hivyo hadi  hospitali ya mkoa.

“ tunazungumzia kila mtu apate huduma za tiba bila kikwazo,leo una hela,kesho huna na una umwa bora tunasema utoe elfu kumi na utibiwe ndani nya manispaa tena siyo peke yako bali na watu wako watano,alisema waziri ummy. Hata hivyo alisema ni  marufuku  kwa mtu mwenye kadi ya CHF anapoenda kwenye vituo vya huduma ya afya kuambiwa akanunue kipimo au dawa bali wanatakiwa kupata vipimo vyote.

MEYA MANISPAA YA DODOMA ATOA RAI KUBORESHA MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI MAARUFU NANENANE

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe (wa kwanza kulia) akishuhudia mmoja ya banda la maonesho alipotembelea Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati katika Viwanja vya Nzuguni Manispaa ya Dodoma hivi karibuni.

Na Ramadhani Juma, Dodoma

HALMASHAURI za Manispaa na Wilaya katika mikoa ya Kanda ya Kati unayoundwa na mikoa ya Dodoma na Singida kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaounga mkono shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi wameshauriwa kubuni njia rahisi inayoweza kuwafikishia kwa wakulima na wafugaji elimu inayopatikana kwenye viwanja vya Maonesho ya Wakulima maarufu kama Nanenane.

Rai hiyo imetolewa na Meya wa Manispaa ya Dodoma Mstahiki Profesa Davis Mwamfupe kufuatia maenesho ya Nanenane yaliyomalizika hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo amesema bado Maonesho hayo hususan Kanda ya Kati hayajafanikiwa kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi wetu kwa kiasi kinachoridhisha na kuwawezesha kubadili shughuli zao na kuzifanya kuwa na tija inayoridhisha.

Alisema Maonesho ya Nane Nane yamekuwepo kwa miaka mingi katika Kanda mbalimbali nchini na yamekuwa na mambo ya kuvutia sana hususani Teknolojia na mbinu bora za uzalishaji katika kilimo na mifugo ambazo zinauwezo wa kuleta tija kubwa lakini bado changamoto kubwa ni kwamba mambo yote bora na mazuri yanayopatikana kwenye Maonesho hayajaweza kumfikia mkulima kwenye ngazi za msingi kwa maana ya ngazi ya kaya na vijiji.

Alisema kuwa, unaweza kutoka umbali usiozidi kilomita mbili tu kutoka kituo (Uwanja) cha Maonesho kilipo utashangaa kukuta mkulima analima kilimo cha kienyeji ambacho hakina manufaa.

“Teknolojia inayooneshwa kwenye Maonesho haya bado haijaweza kuwafikia wakulima na wafugaji wetu kwenye vijiji vyao wanakoendesha shughuli zao za kilimo na mifugo” alisema Profesa Mwamfupe na kuongeza kuwa, bado teknolojia na ubunifu unaopatikana kwenye Maonesho haya unahitaji kuwafikia wakulima wa chini kabisa.

Alitoa wito kwa Mamlaka zinazohusika kuhakikisha Kiwanja cha Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati kilichopo katika Kata ya Nzuguni Manispaa ya Dodoma kinakuwa kituo cha Shamba Darasa la kilimo mifugo na uvuvi cha kudumu ili wataalamu wa kilimo na mifugo wawepo kituoni hapo kipindi chote cha mwaka wakisimamia shughuli za kilimo na mifugo kituoni hapo na Halmashauri zilete Wakulima na Wafugaji wao kujifunza na kupata suluhisho la changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za uzalishaji.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA MAENDELEO LA JAPAN (JICA) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea jambo  na  Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka aliyekutana na kufanya mazungumzo naye leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo  na Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Mhe. Masaharu Yoshida leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale kwa Rais wa shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) Bw. Shinichi Kitaoka aliyekutana naye leo agosti 21, 2017 Ikulu jijini Dar es salaam.

MAKALA YA ELIMU: Kishapu yaendelea kuboresha sekta ya elimu

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akimkabidhi msaada wa vifaa vya maabara, stuli za kukaliwa wanafunzi wakati wa mazoezi kwa vitendo kwa aliyekuwa mkuu wa shule ya sekondari Kishapu ambaye sasa ni mratibu elimu kata ya Sekebugora, mwalimu Hosea Somi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akikagua mojawapo ya vyoo va nyumba za walimu katika shule ya sekondari Kiloleli kata ya Kiloleli wilayani humo.
Sehemu ya nyumba za walimu katika shule ya sekondari Kililoli kata ya Kiloleli wilayani humo ambazo ni mojawapo ya mpango wa halmashauri kuboresha sekta hiyo muhimu.

Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga inaendelea na mkakati wake wa kuboresha mazingira ya sekta ya elimu kwa kujenga miundombinu katika shule zake mbalimbali. Inafanya hivyo kupitia programu mbalimbali zikwemo Mpango wa kuboresha Miundombinu katika shule za sekondari (SEDP) ili kumpa mwanafunzi mazingira mazuri ya kujifunza.

Pia halmashauri hiyo kupitia Idara ya Elimu Sekondari ina jukumu kubwa la kuhakikisha shule zake zinafanya vizuri katika mitihani ya kitaifa na hatimaye kuitoa kimasomaso wilaya kitaaluma. Imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ikiwa na lengo la kupanua wigo wa elimu katika shule mbalimbali za sekondari na hivyo wanafunzi kuwa na mazingira mazuri ya kujifunza.

Wanafunzi wanapokuwa na mazingira mazuri ya elimu ikiwemo miundombinu rafiki kwao wanakuwa na ari ya kujifunza na hatimaye kufaulu. Vile vile walimu nao wanapokuwa na wamewekewa mazingira mazuri ya kufundishia huweza kufanya kazi kwa nguvu moja na kwa moyo wote. Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, maabara na vyoo endapo vikiwa katika ubora vinakuwa motisha kubwa kwa walimu na wanafunzi.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Kampuni ya Kansai Plascon Tanzania sasa rasmi Arusha

$
0
0
Arusha: Kampuni ya Kansai Plascon Afrika ltd. Ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya rangi ya Kansai iliyoko Japan, imehitimisha makubaliano yake ya kununua shughuli za rangi za Sadolin nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki.  Hii ilitangazwa na Deodatus Makumpa Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Plascon Tanzania wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Hotel ya Arusha Jijini Arusha

Kampuni ya rangi ya Kansai ni kampuni ya kimataifa ambayo inaendesha shughuli zake nchini Japan, China, Mashariki ya Kati, Ulaya na Afrika. Bidhaa zake inazotoa zinajumuisha upambaji, Viwanda, rangi za kulinda na mitambo, ina vituo vya utafiti na maendeleo nchini Japan, India na Afrika Kusuni.

“Tumefurahishwa na mafanikio haya. Kupitia haya, tutaweza kutumia nembo yenye nguvu ya urithi wa Kansai, uwezo wa kimataifa wa kiufundi, na utendaji wa kuaminika, kutupatia uwezo mpya, kuweza kupata teknolojia mpya na utambuzi ambao ni muhimu zaidi katika kuendelea kukuza nembo hii,” alisema Makumpa
 
Akiongea kuhusu sababu za kuinunua, Gary van der Merwe, Rais wa Kampuni ya Plascon Afrika Mashariki alisema kwamba makubaliano haya yanadhihirisha nia ya Kansai Plascon katika kujiendeleza zaidi duniani. “Afrika Mashariki ni moja kati ya ukanda ambao unakuwa haraka zaidi kiuchumi barani Afrika. Kwa ukuaji wa kasi wa daraja la kati, kuongezeka kwa nguvu ya utumiaji na kukua kwa miji, huu ni muda muafaka wa kuingiza sokoni bidhaa zetu mbali mbali kwaajili ya kuboresha zaidi mtindo wa maisha yao wakati huo huo tukiwa tunaongeza kuenea kwetu duniani”.

HAKIMU MAKETE: ACHENI KUWALAUMU POLISI WANAPOTOA DHAMANA KWA WATUHUMIWA.

$
0
0
Zaidi Tazama video hii hapa.
Na Edwin Moshi.
HAKIMU wa Mahakama ya Mwanzo Makete Mjini ameitaka jamii kuacha kutupa lawama kwa polisi ama Mahakama pale Mtuhumiwa anapoachiwa kwa dhamana

Ameyasema hayo hivi karibuni katia kikao Maalum cha timu ya ulinzi na usalama wa Mtoto kilichoketi katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete kujadili mambo mbalimbali Kuhusu Watoto

"Kama kuna mahali unapoona huridhiki na kupewa dhamana mtuhumiwa, nenda polisi ukaulize, na kama ni mahakamani nenda mahakamani ukaulize na sio kuwalaumu polisi au mahakama mitaani" amesema hakimu huyo

EFM YAZINDUA TAMASHA LA MZIKI MNENE KWA MIKOA SITA NCHINI.

$
0
0
Balozi wa kampuni ya Noah Funishing na Mtangazaji wa Efm Radio, Swebe Santana  akizungumza juu ya kampuni hiyo ilivyojikita katika kudhamini  EFM Joging itakyofanyika katika mikoa yote sita ambapo Tamasha la Muziki Mnene litafanyika.
 Meneja Mkuu wa EFM Radio na Tv E , Denis Busulwa (SEBO), Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Tamasha Mziki Mnene litakalo fanyika katika mikoa sita nchini  Sanjari na Kampeni ya Nje Ndani ambayo itarusha vipindi vya Radio kutoka mitaani .
 Meneja Masoko kutoka kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya Biko, Good Hope Heaven , akizungumza namna kampuni yao ilivyoweza kudhamini Tamasha la Muziki Mnene kupitia bahati nasibu ya Nguvu ya Buku.
 Baadhi ya Watangazaji wa EFM Radio na Tv E Wakifatilia uzinduzi wa Tamasha la Mziki Mnene.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Mbunge Rweikiza asisitiza uwekezaji kwenye sekta ya elimu.

$
0
0
Mkurugenzi wa shule St Anne Marie iliyoko Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Salaam, Jasson Rweikiza akimpa zawadi mwanafunzi bora wa darasa la saba, Katherine Mujungi, kwenye mahafali ya darasa la saba ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki maeneo ya Mbezi kwa Msuguri jijiini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
 IMEELEZWA kuwa uwekezaji bora kwenye sekta ya elimu, ikiwamo miundombinu, maktaba na walimu walio na sifa za kufundisha, itaongeza ufaulu na uelewa kwa wanafunzi.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shule ya St. Anne Marie, Jasson Rweikiza kwenye mahafali ya 18 ya wanafunzi wa darasa la saba, yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi kwa Msuguri.

Alisema ili kuinua kiwango cha ubora wa elimu nchini, ipo haja ya kuzingatia uwekezaji huo pamoja na kuboresha maslahi ya walimu kwa kuwa watapata ari ya kufundisha.

"Shule ikiwa na mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia kama vile vifaa vya kutosha, madawati, maji, maktaba, walimu wenye ari matokeo ni elimu bora, wadau tuwekeze zaidi," alisema Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini na Mwenyekiti wa wabunge wa CCM.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Gradius Ndyetabula alisema shule binafsi ni muhimu kwa kuwa zinatoa mchango wa elimu na kuongeza fursa kwa Watanzania.

 Alisema iwapo shule za serikali pekee zingeachiwa mzigo wa elimu vijana wengi wangekosa fursa ya kujiunga na kuendelea na masomo, kutokana na uchache wa shule za serikali.

 Alieleza shule hiyo imeshika nafasi ya 32 kitaifa matokeo ya darasa la saba yaliyopita kati ya shule za msingi 16,350 na kwamba wanatarajia wahitimu 43 wa darasa la saba mwaka huu watafanya maajabu kwasababu maandalizi waliyofanya ni mazuri.

Alisema kwenye matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa hivi karibuni, St Anne Marie ilifanikiwa kuwa ya tano  kwenye Mkoa wa Dar es Salaam kwenye matokeo hayo lakini siri kubwa ni mfumo mzuri wa ufuatiliaji wa matokeo ya wanafunzi kitaaluma kuanzia ngazi za chini.

Alisema pia shule hiyo ilifanikiwa kuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Ubungo jijini hapa na hivyo kuziacha kwa mbali shule zaidi ya 11 zenye kidato cha tano na sita wilayani humo.

Aidha, alisema mbali na kushika nafasi ya tano kwa Mkoa wa Dar es Salaam, shule hiyo ilifanikiwa kufaulisha wanafunzi 15 kwa daraja la kwanza, wanafunzi 48 daraja la pili, wanafunzi 23 daraja la tatu na mwanafunzi mmoja tu ndiye aliyepata daraja la nne.

“Dar es Salaam kuna shule 56 zenye kidato cha tano na sita na nyingi zinavifaa na zana za kufundishia hivyo sisi kupenya hadi kuwa namba tano si jambo rahisi, sisi tumejipanga kwa walimu wazuri na mazingira bora ya kusomea kama maktaba ya kisasa na tunaahidi kufanya maajabu kwenye mitihani ijayo,” alisema Ndyetabula.

WABUNGE WA MAREKANI WAIPONGEZA TAYOA KWA KUWAINUA VIJANA.

$
0
0
Ujumbe wa wabunge watano wa Bunge la Congress la Marekani wakiangalia ngoma za asili mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Shirika la Vijana Tayoa Bahari Beach Dar es Salaam.

 Kaimu Balozi wa Marekani Dk. Inmi Patterson akisailimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Vijana Tayoa, Balozi Charles Sanga alipowasili kwenye viwanja vya shirika hilo Bahari Beach Dar es Salaam pamoja na ujumbe wa wabunge watano wa Bunge la Congress la Marekani.
 Kaimu Balozi wa Marekani,  Dk. Inmi Patterson, wa kwanza kushoto akifurahia jambo na ujumbe wa wabunge watano wa Bunge la Congress la Marekani wakati wanazindua redio ya kuelimisha vijana kuhusu mbalimbali kwenye Shirika la Vijana Nchini Tayoa. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Tayoa Peter Masika.

Na Mwandishi Wetu
UBALOZI wa Marekani nchini, umesifu kazi zinazofanywa na Shirika la Vijana Nchini (Tayoa), katika kuwainua na kuwahamasiha vijana kujikwamua kiuchumi na kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson, wakati ujumbe wa wabunge watano wa Bunge la Congress la Marekani wakiwa na familia zao, ulipotembelea ofisi za Shirika hilo zilizoko Bahari Beach, jijini Dar es Salaam.

Wabunge hao wa Congress walioambatana na Kaimu Balozi wa nchi hiyo ni pamoja na Carly Paul, Bob Goodlatte, Steve King, Blake Farenthold, Mike Bishop na Sheila Jackson Lee.

 Wabunge hao walijionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo ikiwemo elimu ya bure kuhusu masuala ya Ukimwi kupitia simu za bure, ujasiriamali na miradi mbalimbali ya kuinua vijana.

Balozi alisema yeye na ujumbe wake wamefurahi kuona kazi kubwa zinazofanywa na Tayoa kwa kushirikiana na taasisi za Marekani kama Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Center for Disease Control (CDC).

“Tumefurahi sana kuona kazi zenu na hasa mnavyowashirikisha vijana katika kujikwamua kiuchumi na kutafuta maendeleo, nawapongeza sana Tayoa kwa kazi kubwa mnayofanya,” alisema

POLEPOLE AFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI HAPA NCHINI TANZANIA, LEO

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Poloepole akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Inmi Petterson, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 21, 2017.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Poloepole akilipokuwa akimkaribisha Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Inmi Petterson, katika ukumbi wa Sekretarieti kwa ajili ya mazungumzo, baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Agosti 21, 2017. Picha zote na Bashir Nkoromo.
PICHA ZAIDI>BOFYA HAPA

MICHUZI BLOG: VETA na Ujerumani watiliana saini makubaliano ya mafunzo ya uwanagenzi katika teknolojia ya ufundi wa zana za kilimo na mitambo ya ujenzi

$
0
0
MICHUZI BLOG: VETA na Ujerumani watiliana saini makubaliano ya mafunzo ya uwanagenzi katika teknolojia ya ufundi wa zana za kilimo na mitambo ya ujenzi0653416221
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images