Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1867 | 1868 | (Page 1869) | 1870 | 1871 | .... | 3348 | newer

  0 0  0 0

  This is a prayer for our beloved country Kenya and a call to all Kenyans to unite together. While many may have varied ways of championing for peace love and unity, this is my little contribution to this cause...

  Below is youtube link to the video of the song.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inayatambua na kuyathamini mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyojengwa na awamu zilizotangulia baina ya Tanzania na mataifa mbalimbali ikiwemo Jamuhuri ya Cuba na kwamba itayaendelea.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Agosti 17, 2017), alipozungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Bi Anna Teressa mara baada ya kuwasili nchini Cuba kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

  “Tanzania na Cuba zina historia ya kutosha. Tunatambua mahusiano mazuri yaliyopo kati nchi zote mbili, ambayo yalikuwepo kuanzia Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Nyerere.”

  Amesema katika ziara yake hiyo anatarajia kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali ya Cuba kwa lengo la kukuza ushirikiano katika sekta za Afya, Elimu, Utalii na Kilimo.

  Waziri Mkuu amesema Cuba ni mojawapo kati ya nchi zenye ushirikano wa muda mrefu na Tanzania kisiasa, kijamii, kiafya na kiuchumi.”Mfano katika Sekta ya Afya, madaktari wengi kutoka Cuba walikuwa wanakuja Tanzania kutibu wagonja waliokuwa na maradhi makubwa.”

  Pia Waziri Mkuu amesema katika ziara hiyo anatarajia kukutana na Jumuya ya Wafanyabiashara wa Cuba ili kuwaelezea fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania hususan  katika Sekta ya Viwanda pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

  Kwa upande wake Bi. Anna ambaye alimpokea Waziri Mkuu kwa niaba ya Serikali ya Cuba alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea ushirikiano mzuri baina ya nchi hizo mbili, hivyo alimuhakikishia kwamba wataendelea kuudumisha.

  Pia Bi. Anna ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa namna inavyopambana na rushwa, ufisadi, kuhimiza uwajibikaji pamoja na kutetea wanyonge.
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa (kulia) na Mkewe Mary Majaliwa (kushoto) wakipata makaribisho nchini Cuba, kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa CUBA, Ana Teresa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Havana kwa ziara ya kikazi nchini humo. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Ana Teresa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Havana kwa ajili ya ziara ya kikazi nchini humo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Moshi Kabengwe akisaini makubaliano ya uendelezaji wa mafunzo ya uwanagenzi kulia ni ni Mtendaji Mkuu wa Ujerumani , Reiner Nolte na wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Waechter.

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetiliana saini makubaliano yenye thamani ya Euro 900,000 (zaidi ya shilingi bilioni 2.3) na Chemba ya Baraza la Ufundi Stadi ya Ujerumani (WHKT) kwa ajili ya mafunzo ya uwanagenzi yenye lengo la kuimarisha ufundi wa zana za kilimo na teknolojia ya mitambo ya ujenzi.

  Makubaliano hayo yalitiwa saini na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Moshi Kabengwe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Leonard Akwilapo na Ujerumani aliyetia saini ni ni Mtendaji Mkuu wa Ujerumani , Reiner Nolte na kushuhudiwa na Barozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Waechter, Mwenyekiti wa Board ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi,Peter Maduki, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk. Bwire Ndazi na Maafisa wengine waandamizi wengine wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, VETA na Ujerumani.

  “ujuzi wa mafundi na wakulima utaboreshwa kupitia kozi zitakazotolewa na VETA kwa mfumo wa uwanagenzi. Kozi hizo ni pamoja ufundi zana za kilimo, ufundi mitambo ya ujenzi na mafunzo ya vitendo katika teknolojia ya kupunguza upotevu wa mavuno ya mazao ya kilimo katika maeneo yatakayoainishwa,” inaeleza sehemu ya waraka wa makubaliano.

  Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Balozi wa Ujerumani nchini Dk. Detlef Waechter alisema anatarajia kuwa ushirikiano katika mradi huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa Watanzania wengi, hususani vijana katika kupata ujuzi wa kuutumia kwenye kuongeza tija kwenye kilimo nchini.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimani watu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Moshi Kabengwe aliishukuru serikali ya Ujerumani kwa msaada na ushirikiano na kusema kuwa utawasaidia vijana wengi kuajirika na kuwa na ujuzi wa kutumia teknolojia za kisasa katika kilimo.

  Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi aliishukuru serikali ya Ujerumani kwa kuendelea kuiamini VETA na kuendeleza ushirikiano nayo katika utoaji mafunzo kwa mfumo wa uwanagenzi. Amesema, ushirikiano katika miradi ya nyuma umeendelea kuwanufaisha vijana wengi kupata ujuzi na kuweza kuajirika kwa urahisi.

  Mafunzo ya uwanagenzi uendeshwa kwa mfumo wa ngwe za mzunguko kati ya chuo cha ufundi stadi na sehemu ya kazi ambapo mwanafunzi hupata mafunzo ya ujuzi kwenye karakana za chuo na uzoefu wa hali halisi mahala pa kazi, hivyo kumwongezea umahiri pamoja na maarifa zaidi na utamaduni wa ya mazingira ya kazi husika.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akizungumza katika mkutano wa kutiliana saini ya makubaliano kati ya Ujerumani na VETA kwa ajili mafunzo ya uwanagenzi yenye lengo la kuimarisha ufundi wa zana za kilimo na teknolojia ya mitambo ya ujenzi.
  Picha ya Pamoja Balozi wa Dk. Detlef Waechter akipeana mkono Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimani watu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji, Moshi Kabengwe pamoja na watendaji wa VETA Wawakilishi Ujerumani baada ya kusaini makubaliano ya kuendeleza wanagezi.

  0 0


  0 0


  Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii

  Mfanya biashara bilionea wa Nigeria Aliko Dangote amesema jambo la kwanza atalofanya endapo atafanikiwa kuinunua klabu ya Arsenal ya Uingereza ni kumtumbua kocha Arsene Wenger. 

   Toka mwezi Mei mwaka 2015 Dangote amekuwa akikaririwa mara kwa mara kuwa ana mipango ya kuinunua klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza ambayo mshika dau mkuu wake ni bilionea wa Kimarekani Stan Kroenke anayeshikilia hisa asilimia 67 za klabu hiyo. 

   January 18 mwaka huu alipoulizwa, bilionea huyo namba moja wa Afrika alinukuliwa na shirika la habari la CNBC akisema kwamba kwa sasa jicho lake kwanza liko kwenye kuifanya kampuni yake ya Dangote Group kuwa na kiasi cha dola bilioni 100 kabla ya kuinunua Arsenal. 

  "Nitainunua (Arsenal) lakini kwanza nataka kuimarisha miradi yangu ambayo kwa sasa ni yenye thamani ya dola bilioni 18, ndipo nitaigeukia Arsenal” CNBC ilimkarriri Dangote wakati wa mkutano wa uchumi wa dunia huko Davos, Uswisi. 

   Dangote, ambaye ni shabiki wa Arsenal na sio tena wa kocha Wenger, ameteka tena vichwa vya habari karibuni kwa kusema jambo la kwanza atalofanya ni kubadili kocha. “Amefanya kazi nzuri, lakini mtu mwingine inabidi aje kujaribu bahati yake”, alisema alipohojiwa na Bloomberg. 

   Dangote amekuwa mkosoaji mkubwa wa Wenger, akimshauri kocha huyo Mfaransa ‘kubadili mfumo wake kidogo’ mnamo mwaka 2015. Lakini pamoja na kuonesha nia ya kuinunua Arsenal, bado hajaweka dau mezani. 

  Yeye anasema atafanya hivyo mara tu ujenzi wa mradi wake mkubwa wa mitambo ya kuchakata mafuta wenye thamani ya dola bilioni 11 jijini Lagos utapokamilika. Kampuni yake ya Dangote Group ilianzishwa mwaka 1977 ikiwa kampuni ndogo ya biashara, lakini leo imekuwa kubwa na yenye matawi nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Tanzania, Benin, Ghana, Nigeria na Togo. 

  Hivi sasa pamoja na kuzalisha saruji kampuni hiyo inazalisha pia sukari na vyakula. Bilionea wa Kirusi Alisher Usmanov mwenye hisa asilimia 30 katika Arsenal aliweka dau la dola 2.6 billioni ili kuinunua Arsenal mapema mwaka 2017 lakini bilionea Kroenke mwenye hisa zaidi ya 67 aligoma.  0 0

  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema mchango wa Cuba katika kuimarisha afya za wananchi wa Bara la Afrika unaimarika kila siku kutokana na misingi imara ya ushirikiano wa karibu na kiundugu ulioanzishwa na muasisi wa taifa hilo Fidel Castro Balozi Seif ameyasema haya Leo mjini Havana wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Afya ya umma mheshimiwa Roberto Morales Ojeda. 
   Amesema kutokana na uhusiano mzuri na kiundugu uliopo kati ya Tanzania na Cuba, Zanzibar imeweza kutoa madaktari wasiopungua 50 ambao wamefundishwa na madaktari kutoka Cuba. Amesema kupatikana kwa madaktari hao kumeiweka Zanzibar nafasi nzuri ya kufikia malengo yake ya kuwa na kituo cha afya chenye daktari kwa kila kilometa nne. 
   Balozi Seif ameiomba Serikali ya Cuba kuipatia Zanzibar madaktari 3 mabigwa katika fani ya figo (Nephrologist); masikio, pua na koo (ENT) na mionzi (Radiologist). Aidha ameitaka Cuba kuwapatia vijana waliomaliza mafunzo ya udaktari chini ya madaktari wa Cuba nafasi za mafunzo ya juu katika fani mbali mbali. 
   Naye Waziri wa Afya ya umma mheshimiwa Roberto ameeleza kuridhishwa kwake na uhusiano ulipo wa sekta ya afya kati ya Zanzibar na Cuba. Amesema Cuba iko tayari kuwapatia mafunzo ya juu vijana wa Zanzibar kwa gharama nafuu na kuitaka Wizara ya Afya ya Zanzibar kupeleka maombi yake mapema iwezekanavyo.
  Kwa upande wa wataalamu wa Afya Waziri wa Cuba Mheshimiwa Roberto amesema Serikali yake itarifikia ombi hilo na itatoa jawabu hivi karibuni

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakipata makaribisho Nchini Cuba jana Agosti 17, 2017 kutoka kwa Naibu  Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bibi Ana Teresa mara baada ya kuwasili  katika Uwanja wa  Ndege wa  kimataifa wa Havana   kwa  ziara ya kikazi nchini humo.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim  Majaliwa  akiwa na mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa CUBA Bibi Ana Teresa mara baada ya kuwasili jana  Agosti 17, 2017 katika Uwanja wa  Ndege wa kimataifa wa Havana   kwa ajili ya ziara ya kikazi Nchini Cuba. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  The main purpose of UNTOLD is to Educate, Inspire and Entertain. The show features Tanzanians from different walks of life, in and outside of Tanzania. With a large Diaspora community in the US and other parts of the world, we believe that we all have a contribution to where our great nation is going. 
   The show will explore these individual’s lives; their moments of triumph and failure , decision patterns, their motivation and inspiration, beliefs, leadership style, family, relationships etc. With these candid conversations we hope that others will be able to relate, be inspired and take something away that they can apply to their personal lives. 
  We hope to remove the barriers that most of us create in ourselves – redefining possibilities, expose patterns and remove the notation that success only belongs to a select few. In life your response to events is what determines the outcome.  
  Like, subscribe and make sure you don't miss our premiere on the 26th!

  0 0

  Courtesy of NBS

  0 0

  Bang na nako 2 nako is the song of appreciation to NAKO 2 NAKO (MUSIC GROUP) for everything they did to take it to the top and the impact they brought back to the streets(society) through their music, which was mostly preaching love ,unity ,self esteem ,hard work as the only means to success and having fun as a life style.
  here attached is the song cover art and the link to download
           +255 756 564 364

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
  Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetiliana saini makubaliano yenye thamani ya Euro 900,000 (zaidi ya shilingi bilioni 2.3) na Chemba ya Baraza la Ufundi Stadi ya Ujerumani (WHKT) kwa ajili ya mafunzo ya uwanagenzi yenye lengo la kuimarisha ufundi wa zana za kilimo na teknolojia ya mitambo ya ujenzi.
  Makubaliano hayo yalitiwa saini na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Moshi Kabengwe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk Leonard Akwilapo na Ujerumani aliyetia saini ni ni Mtendaji Mkuu wa Ujerumani , Reiner Nolte na kushuhudiwa na Barozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Waechter, Mwenyekiti wa Board ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi,Peter Maduki, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk. Bwire Ndazi na Maafisa wengine waandamizi wengine wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, VETA na Ujerumani.
  “ujuzi wa mafundi na wakulima utaboreshwa kupitia kozi zitakazotolewa na VETA kwa mfumo wa uwanagenzi. Kozi hizo ni pamoja ufundi zana za kilimo, ufundi mitambo ya ujenzi na mafunzo ya vitendo katika teknolojia ya kupunguza upotevu wa mavuno ya mazao ya kilimo katika maeneo yatakayoainishwa,” inaeleza sehemu ya waraka wa makubaliano.
  Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo, Balozi wa Ujerumani nchini Dk. Detlef Waechter alisema anatarajia kuwa ushirikiano katika mradi huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa Watanzania wengi, hususani vijana katika kupata ujuzi wa kuutumia kwenye kuongeza tija kwenye kilimo nchini.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimani watu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Moshi Kabengwe aliishukuru serikali ya Ujerumani kwa msaada na ushirikiano na kusema kuwa utawasaidia vijana wengi kuajirika na kuwa na ujuzi wa kutumia teknolojia za kisasa katika kilimo.
  Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi aliishukuru serikali ya Ujerumani kwa kuendelea kuiamini VETA na kuendeleza ushirikiano nayo katika utoaji mafunzo kwa mfumo wa uwanagenzi. Amesema, ushirikiano katika miradi ya nyuma umeendelea kuwanufaisha vijana wengi kupata ujuzi na kuweza kuajirika kwa urahisi.

  Mafunzo ya uwanagenzi uendeshwa kwa mfumo wa ngwe za mzunguko kati ya chuo cha ufundi stadi na sehemu ya kazi ambapo mwanafunzi hupata mafunzo ya ujuzi kwenye karakana za chuo na uzoefu wa hali halisi mahala pa kazi, hivyo kumwongezea umahiri pamoja na maarifa zaidi na utamaduni wa ya mazingira ya kazi husika.  Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Moshi Kabengwe akisaini makubaliano ya uendelezaji wa mafunzo ya uwanagenzi kulia ni ni Mtendaji Mkuu wa Ujerumani , Reiner Nolte na wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire na Balozi wa Ujerumani nchini, Dk. Detlef Waechter.


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Bwire Ndazi akizungumza katika mkutano wa kutiliana saini ya makubaliano kati ya Ujerumani na VETA kwa ajili mafunzo ya uwanagenzi yenye lengo la kuimarisha ufundi wa zana za kilimo na teknolojia ya mitambo ya ujenzi.
  Picha ya Pamoja Balozi wa Dk. Detlef Waechter akipeana mkono Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimani watu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji, Moshi Kabengwe pamoja na watendaji wa VETA Wawakilishi Ujerumani baada ya kusaini makubaliano ya kuendeleza wanagezi.

  0 0


  KWAMBA TAREHE 17.08.2017 MAJIRA YA SAA 11:00HRS ASUBUHI KATIKA ENEO LA UFUKWE WA ZIWA VIKTORIA LIITWALO MURUTANGA ULIOPO KATA YA IRUGWA WILAYA YA UKEREWE MKOA WA MWANZA, MARWA MWITA MIAKA 18, MVUVI NA MKAZI WA NYAMAZARA TARIME, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI DHIDI YA MVUVI MWENZAKE AITWAYE ERNEST MAGERO, MIAKA 26, MVUVI NA MKAZI WA KIABAKARI – MARA, YALIYOTOKANA NA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KINACHOZANIWA KUWA NI KISU MAENEO YA SHINGONI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.


  INADAIWA KUWA TUKIO HILO LA MAUAJI LIMETOKEA BAADA YA KUZUKA KWA UGOMVI KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA WA MAUAJI, AMBAPO INASEMEKANA KUWA MAREHEMU ALIKUWA AKIMTUHUMU MTUHUMIWA KUWA ANATABIA YA KUJIPENDEKEZA KWA BOSI WAO ALIYEWAPA MTUMBWI WA KUVULIA SAMAKI. INADIAWA KUWA BAADA YA MTUHUMIWA WA MAUAJI KUAMBIWA KAULI HIYO ALIKASIRIKA NDIPO ALICHUKUA KITU CHENYE NCHA KALI KISHA AKAMCHOMA MAREHEMU MAENEO YA SHINGONI NA KUPELEKEA MAREHEMU KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO.


  WANANCHI/ WAVUVI BAADA YA KUONA TUKIO HILO WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI, AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA. MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA UKEREWE KWA AJILI YA UCHUNGUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATO WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA KISHERIA. AIDHA PIA ANAWAOMBA NDUGU WA MAREHEMU KUWA WATULIVU KATIKA KIPINDI HIKI AMBAPO JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI ILI BAADAE MTUHUMIWA AWEZE KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.


  IMETOLEWA NA;

  DCP: AHMED MSANGI


  KAMANDA WA POLISI (M) MKOA


  0 0


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe jana na kulifungua Tawi la CCM Kizimkazi Dimbani Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa ziara yake katika Wilaya hiyo,(kushoto) Mwandawa Said Nassor.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na WanaCCM wa Tawi la Kizimkazi Dimbani mara baada ya kulifungua Tawi hilo akiwa katika ziara katika Mkoa wa Kusini Unguja jana (kushoto) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Bw.Ramadhan Abdalla Ali.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua pazia kama ishara ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba ya Daktari katika Kijiji cha Muyuni "B" Wilaya ya Kusini Unguja alipofanya Ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Wilaya  hiyo jana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwasalimia na wananchi  katika Kijiji cha Muyuni "B" Wilaya ya Kusini Unguja baada ya kuweka   Jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba ya Daktari  katika kijiji hicho jana alipofanya Ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Wilaya   hiyo. Picha na IKULU

  0 0

  Benki ya Finca imeeleza kutoa huduma kwa wateja wake ambapo mpaka sasa  watanzania wapatao 800,000  wamepata huduma katika matawi  yake yote yaliyo katika Mikoa 24 nchi nzima. Finca inafikisha huduma kwa njia ya Mawakala wanaopatika nchi nzima, pia kutoa huduma hiyo ya kifedha kwa njia ya simu.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Issa Ngwegwe amesema kuwa wanatoa huduma za kifedha zinazowasidia wateja kuweza kutengeneza biashara ambazo zinawapatia kipato.
  Ngwegwe amesema kuwa huduma hizo pia zitawasaidia wateja hao kutengeneza ajira kwa Watanzania wengine wasio katika Sekta Binafsi.Pia, ameongeza huduma hizo kuwapatia uwezo wa kujitambua na kuwafikisha katika malengo.
  Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko wa Benki, Gershom Mpangala amesema kuwa Benki hiyo ina akaunti inayoitwa Mipango Pay Out inayolenga kwa Wastaafu zaidi ambazo zinaweza kumuingizia Mstaafu huyo Riba kubwa.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Issa Ngwegwe akizungumza na Waandishi wa Habari  kuhusu utaoaji huduma Benki ya FINCA kwa wateja wake kwenye ofisi zake jijini Dar es Salaam leo
  Mkuu wa Masoko wa Benki ya Finca, Gershom Mpangala akizungumzia Mipango Pay Out inayolenga kwa Wastaafu zaidi ambazo zinaweza kumuingizia Mstaafu huyo Riba kubwa.

  0 0


  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.  Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akimsikiliza meneja wa Karakana ya MT. Depot, Mhandisi Julius Humbe alipo kuwa akifafanua jambo, kuhusu taratibu za matengenezo ya magari ya serikali. Mhandisi Masauni alifanya ziara ya siku moja katika karakana hiyo mapema leo, ili kujionea jinsi matengenezo ya magari ya serikali yanavyofanyika.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.  Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akipata maelekezo ya jinsi kifaa cha kieletroniki cha kubaini magonjwa ya magari kinavyofanya kazi kutoka kwa Fundi Yakubu Kibingo wa karakana ya MT. Depot. Kushoto kwa Waziri ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu. Mhandisi Masauni alifanya ziara ya siku moja katika karakana hiyo mapema leo, ili kujionea jinsi matengenezo ya magari ya serikali yanavyofanyika.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.  Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akifafanua jambo kwa watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) alipotembelea karakana ya MT. Depot mapema leo, ili kujionea matengenezo ya magari ya Serikali yanavyofanyika katika karakana hiyo. Kushoto kwa Waziri ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu na kulia kwake ni Mkurugenzi wa zalishaji na matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe.
  Mafundi wa Karakana ya MT. Depot wakifanya matengenezo kwenye gari, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.  Mhandisi Hamad Masauni, aliyetembelea karakana hiyo mapema leo ili kujionea jinsi magari ya serikali yanavyotengenezwa. Picha na TEMESA

  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana , leo tarehe 18 Agosti 2017 amehudhuria Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.

  Mkutano huu umejadili zaidi hali ya Siasa nchini Lesotho na namna ya kuisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo inatarajiwa kufanya Uchaguzi Mkuu.

  Taarifa kamili ya Mkutano huu itawasilishwa kesho Jumamosi tarehe 19 Agosti 2017, katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC.

  Double Troika inahusisha nchi wanachama Sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.

  Imetolewa na
  Ofisi ya Makamu wa Rais
  Pretoria, Afrika Kusini
  18 Agosti, 2017.
   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) kabla ya Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda.
  Mkutano huo unafanyika mjini Pretoria, Afrika Kusini.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa OR Thambo mjini PretoRia,Afrika ya Kusini tayari kuhudhuria Mkutano wa Troika Mbili za Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  SADC na Troika ya SADC kwa ajili ya kujadili hali ya Siasa , Ulinzi na Usalama katika Kanda

  0 0

  Aliyekuwa Mgombea Urais wa Kenya kupitia umoja wa NASA, Raila Odinga hatimaye amefungua kesi katika Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya nchi hiyo kupinga matokeo ya urais wa Kenya saa 4:30 usiku yaani saa moja na nusu kabla ya deadline ya Saa 6 kamili ya usiku wa leo. Election Petition ina viambatanisho (annexure) vyenye kurasa zaidi 9, 000.

older | 1 | .... | 1867 | 1868 | (Page 1869) | 1870 | 1871 | .... | 3348 | newer