Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1862 | 1863 | (Page 1864) | 1865 | 1866 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Na fredy Mgunda, Iringa.

  Watanzania wametakiwa kuanza kuutumia mtandao wa simu wa TTCL kwa kuwa umeboreshwa kwa kiwango kikubwa na huduma zao zinazingatia wateja wake ili kuendelea kiinufaisha serikali kwa kuwa mtandao huo unamilikiwa na serikali.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa TTCL 4G mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono mtandao huu wa kizalendo ambao unahuduma nyingi nzuri.

  “Ukiangalia utagundua kuwa mtandao wa TTCL inahuduma ya pesa ambazo zina makato madogo sana kulinganisha mitandao mingine hivyo nawasiii wananchi wa mkoa wa iringa kuanza kutumia huduma za mtandao huu wa kizalendo” alisema Abdallah

  Abdallah aliwataka wananchi kuanza kuvithamini vitu vya wazawa kwanza ili kuleta maendeleo ya maendeleo kwenye kampuni na taasisi za kizalendo  ndio maana mkuu wa mkoa wa Iringa na wakuu wa wilaya wote wa mkoa huu wameamua kujiunga na mtandao huu wa TTCL.

  “Mimi,mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya Richard Kasesela  na viongozi wengine wamejiunga na mtandao huu wa TTCL 4G ambao unakasi kubwa kwenye upande wa internet na huduma nyingine ziboreshwa na zimekuwa bora sana” alisema Abdallah.


   Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi wa mitandao wa TTCL 4G LTE katika Mkoa wa Iringa eneo la ofisi za kampuni hiyo.
   Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizindua huduma ya mtandao wa simu wa TTCL kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa bi Amina Masenza
  Picha ya Pamoja.

  0 0


  Na Mary Gwera
   JUMLA ya Kesi za Mauaji 24 zimepangwa kwa ajili ya kusikilizwa kuanzia Agosti 14 hadi Agosti 25 Mwaka huu katika Kikao maalum cha kusikiliza mashauri ‘Court session’ kitakachofanyika  Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma. 
  Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, Naibu Msajili Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Mhe. Messeka John Chaba alisema kuwa mashauri manne (4) kati ya mashauri hayo 24 yamepangwa kusikilizwa ‘hearing’ huku mashauri 20 yakiwa yamepangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali ‘Plea taking.’ 
  Kufuatia maandalizi ya kikao hiki maalum Mhe. Chaba ametoa wito kwa mashahidi  muhimu ambao wametumiwa wito wa kuitwa shaurini ‘summons’ kufika Mahakamani na kutoa ushahidi wao ili haki iweze kutendeka. 
  Kwa upande wa Waendesha Mashtaka - Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, Mhe. Chaba amewasihi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Mashahidi wote wanapatikana na kufika Mahakamani ili kuiwezesha Mahakama kusikiliza mashauri hayo na kuyatolea uamuzi kwa mujibu wa sheria. 
  “Miongoni mwa mashauri hayo 4 yatakayosikilizwa, mashauri 2 yalisikilizwa na Mahakama ya Rufani Tanzania na kuamuliwa yaanze upya,” alifafanua Mhe. Chaba. Aliyataja mashauri hayo kuwa ni “Crim. Sess. Case No. 52/2014 Mshtakiwa - Adrian Francis na Crim. Sess. Case No.39/2012 Mshtakiwa - Wylife Salumu@Nyendo & 2 Others. 
  Kikao hicho kitaendeshwa na Majaji watatu wa Mahakama Kuu Dodoma, ambao ni;  Mhe Jaji M.A. Kwariko, Jaji Mfawidhi, Mhe Jaji H.H. Kalombola, na Mhe Jaji L. Mansoor. 
  “Matarajio yetu ni kwamba kikao hiki kitasaidia kumaliza/kuondoa mashauri ya jinai ambayo ni mlundikano.  Aidha, kikao hiki kitatoa fursa kwa washtakiwa 20 kufika Mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa awali/uchukuaji wa kiri (plea taking) na huenda baadhi yao wakakiri makosa yao na kupunguza ama kuongeza idadi ya mashauri ambayo yatakuwa yameamuliwa na Mahakama Kuu kwa mwaka huu 2017,” alibainisha Mhe. Chaba. 

  Mahakama ya Tanzania imedhamiria kusikiliza na kutoa uamuzi kwa wakati kwa mashauri yote ya muda mrefu na yanayoendelea kufunguliwa Mahakamani ili haki ipatikane kwa wakati  na pia kurejesha imani ya jamii.

  0 0

  Shirika la Rafiki Social Development Organization – SDO la mkoani Shinyanga leo Jumanne Agosti 15,2017 limezindua Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili katika kata 30 kwenye halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Shinyanga Vijijini na Kahama Mji.

  Uzinduzi wa mradi huo umefanyika katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro. 

  Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo,Matiro alilitaka shirika hil0 kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa jadi la sungusungu,serikali,viongozi wa dini,kimila na wananchi. “Niwapongeze sana Rafiki SDO kwa kupata mradi huu muhimu kwa ajili ya ulinzi wa watoto,sote tunatambua kuwa vitendo vya ukatili wa watoto vimekithiri katika jamii,serikali pekee haiwezi kumaliza vitendo hivi,lazima tushirikiane ili watoto wetu wawe salama”,alisema Matiro. 

  “Natamani kusikia mashirika yanajitokeza kuanzisha miradi kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ulawiti wanavyofanyiwa watoto wetu,taarifa nilizo nazo ni kwamba baadhi ya watoto wa kiume waliopo katika shule za msingi wanafanyiwa mchezo mbaya wa kulawitiwa,tena wanafanyiwa na watu wazima,hili halikubaliki lazima tushirikiane kumaliza tatizo hili”,aliongeza Matiro. 

  “Naomba mashirika yanayojihusisha na masuala ya watoto yajitokeze na kuanzisha miradi ya kusaidia watoto wanaolawitiwa,tunapaswa kuwalinda watoto hawa,kinachotakiwa ni ushirikiano japo changamoto katika kesi za ukatili ni wazazi na walezi kumaliza kesi kienyeji”,alisema Matiro. 
  Wa kwanza kushoto ni Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Shinyanga John Nhabi,akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,Mkurugenzi wa Shirika la RAFIKI SDO,Gelard Ng’ong’a na Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima (wa kwanza kulia) wakiwa katika ukumbi wa Ibanza Hotel Mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala .
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala utakaotekelezwa na Shirika la Rafiki SDO kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kuhudumia watoto “Save The Children International” kwa hisani ya shirika la Maendeleo la nchini Sweeden – SIDA. 
  Wadau wakiwa ukumbini wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
  Wadau mbalimbali wa masuala ya watoto kutoka kata 30 za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini,Manispaa ya Shinyanga na Kahama Mji ambako mradi huo utatakelezwa wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini. 


  0 0

  Karibu na asante kwa kujiunga nasi
  Kanisa la Umoja International Outreach lililopo jijini Dallas Texas limeandaa mikutano ya injili katika maeneo ya Texas na Washington DNV.
  Mwanzilishi na Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Mch Absalom Nasuwa alizungumza nami kuhusu mkutano huo
  KARIBU

  Pia Mch Nasuwa alizungumzia huduma yake

  0 0

  Natoa pole kwa wote walioathirika na janga la moto kwa wafanyabiashara soko la Sido. SOKO la sido lilianza kuungua saa 21.32 Hrs jana usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko la sido.

  Pamoja na kutoa pole niwashukuru wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano na kazi kubwa YA kudhibiti moto usiendelee kuleta madhara makubwa zaidi.

  Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Mbeya imeunda kamati  ya kufanya tathmini ya kujua hasara na chanzo cha Moto huo .

  Tunaomba wananchi waendelee kuwa watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo cha moto na hasara iliyopatikana
  Aidha vyombo vya ulinzi vinaendelea kuchunguza kujua kama moto huo utakuwa umesababishwa na mtu/ watu uchunguzi huo bado unaendelea
  Nirudie tena kuwapa pole wote walioathirika na janga na mungu awatie nguvu ktk kipindi hiki Kigumu
   

  Amos G.Makalla
  Mkuu wa mkoa wa Mbeya

  0 0

  Baadhi ya wafanyabiashara katika Soko la Sido lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, wakiangalia namna mali zao zilivyoteketea bila kujua cha kufanya. Moto huo ulioanza jana usiku umeteketeza eneo kubwa la soko hilo ambapo mali zilizoteketea bado thamani yake haijafahamika. chanzo cha moto huo pia bado hakijafahamika. PICHA ZOTE NA FADHIL ATICK A.K.A MRPENGO
   Muonekano wa eneo yalipokuwepo mabada ya wafanyabiashara hao baada ya kuteketea kwa moto.
   Kila kitu kimeungua.   Mmoja wa wafanyabiasha akiwa amebeba sehemu ya mali za dukani kwake alizobahatika kuziokoa.


  0 0

  Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wamefanya ziara ya mafunzo kwenye Msitu wa asili wa Hifadhi wa Mlima Rungwe mkoani Mbeya na kujionea jinsi wananchi wanavyoshirikishwa katika uhifadhi wa pamoja.

  Akizungumza Mwenyekiti wa kamati hiyo, Welani Chilenga amesema lengo la ziara hiyo ni kutaka kujifunza jinsi Wakala wa Huduma Misitu Tanzania (TFS) wanavyofanya uhifadhi kwa kuwashirikisha wananchi katika kuzilinda hifadhi zao.

  Amesema nchini Malawi wao wamekuwa wakitumia mitutu katika kulinda Misitu jambo ambalo halijawawezesha kufanikiwa katika uhifadhi hivyo sehemu kubwa ya miti yao imekatwa.

  Chilenga amesema wamejionea vyanzo vya maji ambapo mlima huwa ni chanzo cha mito 21 na wameiomba TFS kuendelea na juhudi za uhifadhi kwani nao wamekuwa wakifaidika na Mlima huo kama chanzo chao cha maji kupitia ziwa Nyasa Katika hatu nyingine, Wabunge wa Kamati hiyo walifanikiwa kupanda mlima huo mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko.

  Awali, Mhifadhi Mkuu wa Mlima Rungwe, Innocent Lupembe amewataka watanzania kutembelea hifadhi hiyo ili waweze vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo wakiwemo ndege na wanyama wa aina mbali mbali.

  Aidha, Aliwataka watafiti wa ndani na nje ya nchi wafanye tafiti katika hifadhi hiyo kwa kuwa ina amali ambayo haipatikani mahali popote pale duniani nisipokwa katika Mlima huo.
  Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wakiwa wanapumzika baada ya kupanda Mlima Rungwe mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko, lengo la ziara hiyo ikiwa ni kujifunza jinsi Wakala wa Huduma Misitu Tanzania (TFS) wanavyofanya suala la uhifadhi kwa kuwashirikisha wananchikatika kuzilinda hifadhi hizo.
  Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka nchini Malawi wakiwa wanapanda Mlima Rungwe ambapo waliweza kupanda mlima huo mpaka kituo cha kwanza cha mapumziko

  0 0


  0 0

  Kampuni ya Simu Tanzania TTCL imezindua huduma ya teknolojia mpya ya 4G LTE mkoani Iringa ili kuongeza kasi ya maendeleo na kuimarisha mawasiliano katika mkoa huo.

  Hafla hiyo ya uzinduzi ilihudhuriwa na Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mkuu wa Wilaya Iringa, Richard Kasesera, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Meneja wa TTCL –Iringa, Mhandisi Ekael Manase.

  Akizindua huduma hiyo Mgeni rasmi alisema Mkoa wa Iringa ni maarufu kwa mazao ya kilimo na biashara hivyo huduma hiyo itawanufaisha wananchi kuwasiliana na kupeana taarifa kuhusu shughuli mbalimbali za maendeleo.

  Aidha amesema kuanzishwa kwa huduma hiyo mkoani humo ni fursa nyingine kwa wananchi kwani itatoa mchango mkubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, usafiri, biashara, utalii, huduma za jamii na sekta nyingine mbalimbali.

  “Natumia fursa hii kutoa rai kwa Wana Iringa na Wananchi kwa ujumla kutumia TTCL kwani ni Mtandao wa wenye huduma bora na tozo nafuu, zenye kukidhi mahitaji ya Makundi yote katika jamii” Alisema Mkuu wa Wilaya ya Kilolo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dc Asia Abdallah.

  Aidha, mgeni rasmi amewataka Wakazi wa Iringa kuziona fursa za kibiashara zinazotolewa na TTCL kama vile kuwa Wakala wa kuuza vocha, wakala wa TTCL PESA na huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hii ili waweze kujipatia kipato.

  Katika hatua nyingine alitoa changamoto kwa TTCL kupanua wigo wa huduma zake ili kuyafikia maeneo ya vijijini ambako zinafanyika shughuli nyingi za kiuchumi hasa Kilimo na biashara ambavyo vinahitaji sana Mawasiliano ya uhakika.

  Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba aliwataka wananchi kutumia huduma za TTCKL ambazo zimeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu.

  “Uzinduzi wa huduma hiyo, ni utekelezaji wa mpango mkakati ambao TTCL imejiwekea kwa kusambaza huduma za mawasiliano bora nchini kote. Uzinduzi wa huduma ya 4G, ni miongoni mwa hatua za utekelezaji wa mpango mkakati huo, ambao unaongeza idadi ya mikoa iliyofikiwa kuwa 15 kati yake 13 ya Tanzania Bara na miwili ya Tanzania visiwani ”amesema Bw. Waziri Kindamba.

  Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu aliwahakikishia wananchi kuwa TTCL imejipanga vyema katika kuhakikisha inatoa huduma bora ya mawasiliano ya simu ya Mkononi, mezani na huduma bira ya Intaneti.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Iringa, Amina Masenza (wa tatu kulia), akiwa ameshika bango sambamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba (wa pili kushoto) pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchunaji Peter Msingwa (kushoto), wakiashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL 4G mkoani Iringa na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya Iringa, Richard Kasesera (wa pili kulia) pamoja na Meneja wa TTCL Mkoa wa Iringa, Mhandisi Ekael Manase.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba (katikati) akimuonesha matumizi ya Simu ya Mezani isiyotumia waya, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Juma Abdallah katika uzinduzi wa huduma ya 4G mkoani Iringa.
  Afisa Mtendaji Mkuu Bw.Waziri Kindamba akimuonesha Mbunge wa Iringa Mjini, Mchunaji Peter Msingwa jinsi huduma ya 4G ilivyobora na spidi kubwa ya Intaneti, katika hafla ya uzinduzi wa 4G Iringa.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba akihutubia kwenye hafla ua uzinduzi wa huduma ya TTCL 4G Mkoani Iringa.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba (wa pili kushoto) akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Juma Abdallah namna huduma hiyo inavyofanya kazi wakati wa huduma ya 4G mkoani Iringa. Wengine pichani toka kushoto ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mchunaji Peter Msingwa, Mkuu wa Wilaya Iringa, Richard Kasesera (wa pili kulia) pamoja na Meneja wa TTCL Mkoa wa Iringa, Mhandisi Ekael Manase.

  0 0

  Na Robert Hokororo, Kishapu DC.

  Wananchi wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Afya (CHF) iliyoboreshwa ili wapate huduma na kuboresha afya zao na hivyo kuweza kushiriki shughuli mbalimbali za uzalishaji.

  Wito huo ulitolewa jana na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji shughuli za afya wilayani hapa.

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo katika kijiji cha Malwilo, Mheshimiwa Nyabaganga Taraba, Kangese aliwataka viongozi wa serikali za vijiji kuonesha mfano kwa kujiunga na mfuko huo mapema.Kangese pia aliwataka viongozi hao kuhamasisha kaya zingine zijiunge ifikapo Oktoba mwaka huu wakiwemo walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). 

  Alisema huduma hiyo ni muhimu kwa wananchi wasiojiweza na wenye kipato cha chini ambapo kwa sh. 10,000 humuwezesha kuhudumiwa yeye na watu wengine sita katika kaya kwa mwaka mzima.

  Alisema Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kutengeneza miundombinu, kutoa vifaa tiba na kuongeza wataalamu wa sekta hiyo ili waweze kuhudumia wananchi kwa ufanisi.Katibu Tawala huyo aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi wa CHF iliyoboreshwa ulianza rasmi Machi 2016 kwa kuimarisha mfumo wa fedha na uoreshaji dawa na vifaa tiba.
   Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akizungumza wakati wa kampeni ya afya aliyoizindua kijiji cha Malwilo kata ya Somagedi.
   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Dk. Josephat Shani ambaye pia mganga mkuu wa wilaya akizunguza wakati wa uzinduzi huo.
   Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Maguja Daniel akitoa neno wakati wa uzinduzi huo. 

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Guinea Bissau Mheshimiwa Jose Mario Vaz ameahidi kuwa, nchi yake itaridhia itifaki iliyoanzisha mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu (AfCHPR) mapema iwezekanavyo .

  Akizungumza na ujumbe wa mahakama hiyo ulioko katika ziara ya kikazi nchini Guinea Bissau, Rais Vaz alisema hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba Guinea Bissau ilikuwa miongoni mwa nchi za mwanzo za umoja wa Afrika kutia saini itifaki iliyoanzisha AfCHPR mwaka 1998.

  Katika mazungumzo yake na ujumbe huo ulioongozwa na rais wa AfCHPR mheshimiwa Jaji Sylvain Ore kiongozi huyo wa Guinea Bissau alielezea kuridhishwa kwake na madhumuni ya kuanzishwa kwa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu na kuongeza kuwa masuala ya haki za binadamu yana umuhimu mkubwa katika kufikiwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi za Afrika na kuwaondoa wananchi wake katika lindi la umaskini na ufukara.

  “Ahadi yangu ni kuhakikisha kuwepo kwa haki za binadamu katika nchi yangu” alisisitiza Rais Vaz.

  Ujumbe wa AfCHPR pia ulikutana na waziri mkuu wa Guinea Bissau Mheshimiwa Umario Sissoco Embalo ambaye alisema mamlaka husika za nchi yake zitaandaa nyaraka zinazohitajika ili kuzipeleka katika bunge la taifa nchini humo kwa lengo la kuridhia itifaki iliyoanzisha mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu.
  Raisi wa Mahakama akitambulisha Jaji Matusse kwa Raisi was Guinea Bissau Ikulu. Kushoto wa pili ni Makamu wa Raisi wa Mahakama Jaji Ben Kioko.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

     Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Samsung (kushoto) akikabidhi zawadi ya jumla (inayojumuisha Samsung microwave oven, friji na TV inch 42 ) kwa Bw Rajabu Kassim Mchatta (kulia), mshindi wa  bahati nasibu ya ‘Nunua, Sajili na Ushinde’ iliyolenga kupambana na bidhaa feki nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika makao makuu ya Samsung jijini Dar es salaam ikihashiria hitimisho ya promotion hiyo.
  Bw Rajabu Kassim Mchatta (kulia), mshindi wa zawadi ya jumla ya  bahati  nasibu ya ‘Nunua, Sajili na Ushinde’ akikagua zawadi yake mara baada ya  Makabidhiano. kushoto ni Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Samsung.
  Rayton Kwembe Mkuu wa kitengo cha bidhaa za majumbani Samsung Tanzania (katikati kulia) akishikana mkono na mshindi wa zawadi ya jumla ya bahati nasibu ya ‘Nunua Sajili na ushinde’ Bw Rajabu baada ya Makabidhiano yalifanyika makao makuu ya Samsung jijini Dar es Salaam. Kulia Meneja Bidhaa wa Samsung, Bw. Elias Mushi na Bi Lailatu Jethwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Samsung (kushoto)

  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakimpongeza Mwanariadha Alphonce Simbu kwa kuibuka mshindi wa tatu ambapo alijinyakulia medali ya shaba. Hafla hiyo ilikuwa ni maalum ya kumpokea yeye pamoja na wanariadha wengine wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere toka nchini Uingereza kwenye Mashindano ya Marathon ya 2017.
    Mwanariadha Alphonce Simbu akiwashukuru Viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea na kumpongeza kwa ushindi wake katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017 ambapo aliweza kujinyakulia medali ya shaba.
  Wazazi wa Mwanariadha Alphonce Simbu wakiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba aliyoshinda mtoto wao katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017. 
  Mwanariadha Alphonce Simbu akiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba aliyoshinda katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017.

  0 0

  Hivi Karibuni, Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kwa pamoja waliweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania. Katika Makala hii pamoja na mambo mengine Mwandishi Said Ameir wa Idara ya Habari- MAELEZO anaeleza kwani nini mradi huu ni kipimo cha utayari na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa.

  Mradi huu unaojulikana kama Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) unatekelezwa kwa ubia kati ya washirika wa sekta binafsi na sekta za umma za nchi za Tanzania na Uganda.

  Washirika hao ni Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Taifa ya Petroli ya Uganda (UNOC), Kampuni ya Mafuta ya Total ya Ufaransa, Kampuni ya TULLOW yenye makao makuu yake London nchini Uingereza na Kampuni ya China National Offshore Oil Company (CNOOC).

  Bomba ambalo litagharimu dola za kimarekani 3.5 bilioni, sehemu yake kubwa yaani kilomita 1,115 kati ya kilomita 1,445 litajengwa katika ardhi ya Tanzania na kupita mikoa 8, wilaya 24 na vijiji 184.

  Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa, mradi huu wakati wa ujenzi na utakapokamilika, utatoa na fursa nyingi za kiuchumi ambazo zitasaidia sana kuchangamsha shughuli za kiuchumi hivyo kuchangia ukuaji uchumi na kuinua kiwango cha maisha ya watanzania kwa namna mbalimbali.

  Mradi huu ni mfano wa ushirikiano kati ya nchi za Tanzania na Uganda na kwa upande mwingine ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta za umma katika nchi hizi. 

  Katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake, mradi huu utahitaji ushiriki wa sekta binafsi katika nchi zote mbili na wakati mwingine hata taasisi nyingine za umma ambazo zinatoa huduma zitakazohitajika na mradi.

  Kwa hiyo, wakati tukisifia kuwa ni mfano wa mradi wa ubia wa sekta ya umma na sekta binafsi katika nchi zetu, watanzania hawana budi kuelewa kuwa wana wajibu mkubwa wa kuzitumia vyema fursa za mradi huu.

  Kwa Tanzania, mradi huu unaweza kuonesha picha halisi ya ushirikiano wa sekta hizo kwa kuzingatia namna makampuni na taasisi za humu nchini zitakavyoweza kushiriki na kufanikisha mradi huu.

  Kwa maana nyingie ni mradi ambao unaweza kutumika kupima utayari, umakini, uwezo na ujasiri wa watanzania katika kuchangamkia fursa za kiuchumi.


  0 0

   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

  Taasisi ya Wajibu imezindua Ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na maoni yake katika ukaguzi wa 2016 katika maeneo ambayo ni muhimu kwa kila mtanzania kuweza kujua ripoti hiyo kwa mstakabali wa maendeleo ya taifa. 

  Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kabla ya uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo, Lodovick Utouh amesema kuwa ripoti hiyo imeangalia maeneo matatu ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) na maoni yake katika ukaguzi wa 2016  ambayo  ni Serikali Kuu, serikali za Mitaa pamoja na Mashirika ya Umma.

  Amesema kuwa katika ripoti hiyo kwa deni la taifa linatakiwa kwa serikali kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza kulipa na shughuli zingine za maendeleo ziendelee bila kuongeza mapato na kulipa deni kutafanya shughuli hizo za maendeleo kukwama.

  Utouh amesema katika ripoti hiyo agizo la serikali kwa Halmashauri kutenga asilimia 10 ya kuwawezesha vijana na wanawake inatakiwa kuwa ni mikopo wanayopata inatakwa kuwa katika mzunguko na  kuweza kila mtu kumfikia mkopo huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesababu za serikali na maoni yake iliyoangalia maeneo matatu ya ripoti hiyo leo.
   Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya Taasisi ya  wajibu. 
   Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert akizindua ripoti ya taasisi ya wajibu  leo jijini Dar es Salaam.
  Picha pamoja Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert, Watendaji wa Taasisi ya wajibu pamoja na wadau mbalimbali.

  0 0

  The Republic of Turkey pledged to strengthen her relationship with the State University of Zanzibar (SUZA) in matters related to higher education field, this was clarified by Mr. Mehmet Kose, the Head of Presidency for Turks Abroad and Related Communities (YTB) during his visit at SUZA main campus with his delegation on 14th August, 2017. They were hosted by Prof. Idris Rai, the SUZA Vice Chancellor and his Management team.

  The delegation was very much pleased by their visiting in Zanzibar and Tanzania in totality where Mr. Nevzat Ceylan who is a Turkish government member of Parliament and Vice President of Turkey-Tanzania Friendship Committee stated that their visit is a clear testimony that their historical relationship with Zanzibar is still influential. “Our presence here today will enhance this historical relationship between us”, he added.

  Turkey through this mission has shown interest to work in partnership and promised to establish higher learning exchange programmes and expertise in various disciplines with SUZA, also aims to initiate cooperation in teaching languages spoken in these two nations.

  Prof. Idris Rai informed his visitors that Zanzibar has significantly benefited from having relationship with Turkey through the enjoyment of various educational opportunities which are offered by Turkey; he said that Zanzibar has a variety of experts in diverse fields who obtained their education from that country.
  Delegation of Presidency for Turks Abroad and Related Communities (YTB) meets Prof. Rai (right) in his office at SUZA main Campus. Others from left are Mr. Mustafa Efe - the Advisor to YTB President, Mr. Mehmet Kose – YTB President and Mr. Nevzat Ceylan -  a Turkish government member of Parliament and Vice President of Turkey-Tanzania Friendship Committee.

  Conversation between Turkish YTB delegation and SUZA officials in progress.

  FOR MORE NEWS CLICK HERE


  0 0

   Mthibiti ubora wa Shule Wilaya ya  Kinondon, Victoria Mollel, (katikati,) akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi Perfect Mugisha wa Hazina aliyeongoza  kwenye mitihani ya majaribio iliyoandaliwa  na shule ya  Crown ya Mbezi Makonde Dar es salaam. Kushoto ni Mshauri wa shule ya sekondari ya Crown, Moses Kyando na kulia ni Mkurugenzi wa shule ya Crown Mary Shirima.

  Na Mwandishi Wetu.
  SHULE ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  katika matokeo ya mitihani ya majaribio (Mock) ya darasa la saba kati ya shule 135.

  Kwenye matokeo hayo yaliyotangazwa na Ofisa Elimu wa Wilaya Kinondoni, Kiduma Mageni yanaonyesha kuwa shule ya Hazina pia imefanikiwa kuingiza wanafunzi kumi bora kwa upande wa wavulana na kumi bora kwa upande wa wasichana.

  Wavulana waliofanikiwa kuingia kumi bora ni Perfect Ndyetabula,, Abdurahim Sagin, Hamza Almas, Maxmbwana Max, Phinny Murungu, Walter Kiunsi na Hafidh Mohamed, Derick Ignas Menelick Sanga na Brighton Lyatuu.

  Kwa upande wa wasichana waliofanya vizuri aliwataja kuwa ni Abeer Ally, Chipwe Ramson, Florensiana Simon, Ashine Mohamed, Cherish Narcis, Safina Mzuanda, Sandra lema, Evoduia Mayombo, Leyla Sagin, Najra Kimaro na Shufaa Juma.

   Akizungumzia siri ya mafanikio ya shule yake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,  Patrick Cheche, alisema kujituma kwa walimu na ushurikiano ambao wamekuwa wakiupata kwa uongozi wa shule na wanafunzi ndiyo kitu wanachojivunia.

  “Walimu wanafanyakazi kwa moyo sana, wazazi wa wanafunzi wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri sana kwa shule na uongozi wa shule unawajali sana walimu, hayo kwa pamoja yamekuwa yakisaidia ufaulu wetu kuwa juu mwaka hadi mwaka,” alisema Mwalimu Patrick

  Aliwapongeza wanafunzi kwa mafanikio hayo na kuwataka wasome kwa bidii ili hatimaye waweze kuongoza kitaifa na  Mkoa wa Dar es Salaam kwenye mitihani ya darasa la saba mwaka huu.

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Balozi Benedict Mashiba, ambapo amemtaka kuimarisha mahusiano baina ya nchi zote mbili.

  Amekutana na Balozi Mashiba leo (Jumatano, Agosti 16, 2017) katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambapo amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za Kidiplomasia kati ya Tanzania na Malawi.

  Pia Waziri Mkuu amemtaka Balozi huyo kuhakikisha anatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, ukiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama pamoja na fursa za uwekezaji zilizopo nchini hususan katika sekta ya viwanda.

  Waziri Mkuu amesema licha ya kutangaza fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii pia amemtaka kuboresha biashara baina ya Tanzania na Malawi kwa kutumia meli mbili za mizigo za Mv. Ruvuma na Mv. Njombe alizozizindua hivi karibuni.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amemtaka Balozi Mashiba kukutana na kufanya mazungumzo na Watanzania waishio nchini Malawi na kuwasisiza kuishi kwa kuzingatia sheria za nchi husika. Pia kuwaunganisha pamoja na kuwashauri waje kuwekeza nchini.

  Kwa upande wake Balozi Mashiba amesema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama pamoja na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Malawi.

  Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Balozi Benedict Mashiba wakati alipokutana naye Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es salaam leo Jumatano,( Agosti 16, 2017).

  0 0

  \

  Afisa mahusiano wa TECNO Mobile Eric Mkomoya (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya WashaCheche ns kumkabidhi Raymond Msenga (Jay Mond) wa pili kutoka kushoto zawadi ya simu toleo lao jipya kabisa la simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni iliyopewa kuifanya wiki mbili zilizopita.


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  KAMPUNI ya simu za TECNO imemzawadia zawadi ya simu mchekeshaji Raymond Msenga maarufu kama JayMondy ikiwa ni toleo lao jipya kabisa la simu aina ya TECNO SPARK, kutokana na kampeni aliyopewa kuifanya wiki mbili zilizopita.


  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo Eric Mkomoya alisema “nia na madhumuni ya kampuni yetu ni kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania kupitia simu hii mpya, vijana wanaotaka kufanikiwa wanapitia vikwazo vingi, ila Tecno inataka kuwasaidia kupitia washa cheche.”

  Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni aliomba simu kutoka Tecno Mobile kupitia video zake ili aweze kurekodi kwa ubora mzuri. Tecno Mobile walisikia kilio chake na kumpa zawadi ya simu mwaka mzima kwa kila toleo.

  “Nimefurahi kupata zawadi ya simu hii, na kikubwa na ni nafasi ya kupata mfululizo wa matoleo yote mapya ya simu zao, nawasihii vijana wenzangu wenye vipaji wawashe cheche zao na wanaweza kupata msaada kutoka Tecno Mobile.” Alisema Raymond Msenga maarufu kama Jaymond.


  Meneja wa masoko mitandaoni wa TECNO, Kelvin Boniface alisema “Namna ya kushiriki katika kampeni hii ni rahisi, Upload video au picha Kwenye mitandao ya kijamii ukitumia hashtag #WashaCheche bila kusahau kutuTag “Tecno Mobile Tanzania kwenye mitandao yetu ya kijamii ya twitter, Facebook na Instagram” alisema

  Kampeni hii itasukumwa na simu yao mpya aina ya TECNO SPARK (TECNO CHECHE) ili kuhamasisha vijana kutumia vipaji vyao kujiletea maendeleo na kujikwamua kimaisha.

  Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni akikabidhiwa simu na meneja wa masoko mtandaoni Chen Bo simu mpya aina ya TECNO SPARK.

  Afisa mahusiano wa TECNO Mobile Eric Mkomoya akiwaonyesha waandishi wa habari toleo jipya la simu zao kabla ya kumkabidhi Raymond Msenga ambaye ni mchekeshaji wa mitandaoni.

older | 1 | .... | 1862 | 1863 | (Page 1864) | 1865 | 1866 | .... | 3284 | newer