Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

UAMUZI KAMA BANGI ILIYOKUTWA KWA WEMA SEPETU IPOKELEWE AU LA KUJULIKANA MWEZI UJAO.

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
 Agosti 18 mwaka huu, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  itatoa uamuzi kama kielelezo cha msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi vipokelewe mahakamani hapo kama kielelezo au la.

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya majibishano makali kuhusu kielelezo kutoka upande wa utetezi na ule wa mashtaka.

Kielelezo hicho cha bangi kinataka kutolewa katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na wenzake wawili.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Costantine  Kakula kumuongoza ushahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka,  Mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima kuendelea kutoa ushahidi wake.

Katika ushahidi wake, shahidi huyo amidai kuwa alipima msokoto huo na vipisi hivyo vya bangi vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi.

Mbali na mambo mengine, shahidi Mulima kupitia Kakula aliomba kuitoa kielelezo cha bangi kikiwa ndani ya bahasha iliyofungwa ikiwa na muhuri juu, na kama kielelezo cha ushahidi lakini wakili wa utetezi Tundu Lissu alibisha vikali na kusema, upande wa mashtaka ulisema unataka kutoa bangi lakini sasa wanatoa bahasha.

Wakili Lissu alipinga na kusema, ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.

Alidai Lissu vipisi viwili vyenye majani  ukiviangalia kwa makini ni vipisi vya sigara za kienyeji ambayo imetumika kwa sababu vina alama ya kuungua ambavyo kwao vinaitwa twagooso.

Baada ya mabishano makali baina ya pande hizo mbili, Hakimu Thomas Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 18, kwa ajili ya uamuzi kama bangi hiyo ipokelewe au la.

KIZIMBANI KWA KUJIFANYA MKURUGENZI WA HABARI IKULU.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MFANYABIASHARA Ramadhani Athumani Juma maarufu kama Elias Jeremiah Mazimbaka amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la kujifanya kuwa yeye ni Mkurugenzi wa Habari wa Ikulu, Gerson Msigwa.(Pichani Chini)

Akisoma hati ya mashtaka leo mapema, wakili wa Serikali, Jackline Nyantori amedai, kati ya Juni 28 na Julai 4, mwaka huu jijini Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya mtuhumiwa huyo alijitambulisha kwa mtu mmoja anayeitwa Ladislous Matindi kuwa yeye ni Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa HABARI wa Ikulu.

Mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa  imedaiwa, mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Mshtakiwa amekana mashtaka na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana mahakama ilimtaka kuwa na wadhamini wawili watakaoweka dhamana sh milioni moja
Kesi imeahirishwa hadi Agosti 23,mwaka huu.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA BALOZI WA UHOLANZI NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks  ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

Makamu wa Rais alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itazidi kuimarisha uhusiano wake na nchi ya Uholanzi hasa katika sekta  ya kilimo, elimu na uboreshwaji  wa  mazingira ya uwekezaji ili  kufikia lengo la Tanzania ya Viwanda.

Aidha, Mhe.Balozi aliahidi kuwa mjumbe mzuri wa Tanzania na atarejea mara kwa mara kuja kutembea kwani Tanzania ina watu wema na vivutio vingi vya utalii.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks  ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks  ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks  ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

MFANYABIASHARA KIZIMBANI KWA KUKUTWA NA SARE ZA JESHI LA WANANCHI.

$
0
0

 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MFANYABIASHARA wa Kariakoo, Casto Onyomolile Ngogo (35) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya kukutwa na sare mbalimbali za Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ.

Mshtakiwa huyo ambaye amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba anashtakiwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai Juni 15, 2017 mshtakiwa huyo anayeishi Tabata Segerea, alikutwa na Suruali 5000 za JWTZ zenye thamani ya milioni 50.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kukutwa na vifaa hivyo katika maeneo ya bandari kavu ya Galco Inland Container (ICD) iliyopo Sokota Chang'ombe.

Pia mshtakiwa huyo alikutwa na alikutwa na maofisa wa polisi akiwa na tisheti 50 za JWTZ zenye thamani ya Sh 500, 000 pia Juni 17, mwaka huu huko African Inland Container Deport mshtakiwa alikutwa na polisi akiwa na pea 20 za viatu vya JWTZ bila ya kuwa na uhalali.

Mshtakiwa huyo hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Pia (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana chini ya kifungu cha 36 (2) cha sheria ya uhujumu uchumi. Kesi imeahirishwa hadi Agosti 29,mwaka huu.

TAMASHA LA MIAKA 40 YA BIA YA SAFARI LAGER LILIVYOBAMBA JIJINI DAR

$
0
0
 Msanii  Mkongwe wa Muziki Bongo Fleva, Juma Nature akiongoza kundi la TMK Wanaume Family katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Msanii wa Bongofleva Barnaba akiimba kwa kutumia Live band katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
Msanii Mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva , Rehema Chalamila (Ray C) akitoa Burudani katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Dj Maarufu kutoka kituo cha Radio cha Clouds Fm, Dj Zero akionyesha ufundi wa kuchezea Santuri katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam
 Dj Mkongwe katika uchezeshaji wa Santuri, John Dilinga (DJ JD) akionyesha ufundi kwa kupiga nyimbo za Zamani katika Tamasha la Miaka 40 ya Bia ya Safari Lager lililofanyika katika Viwanja vya Readers Club Jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Culture of secrecy still embedded in public officials

$
0
0
The culture of secrecy is still embedded in public officials especially in the central government as opposed to Local Government despite improvement in service delivery and access to information, a recent study has revealed.

A study which was conducted by the Media Institute of Southern Africa (MISA) Tanzania Chapter with support from the Collaboration on International ICT Policy for East and Southern Africa (CIPESA) aimed at looking at Access to Information in Local Government Authorities (LGAs) and Central Government offices in Tanzania. The LGAs were represented by the City and Municipal Councils and the Central Government was represented by the Regional Commissioners’ Offices.

This study wished to find out how central government and local government authorities are transparent and accountable to citizens. The study also strived to find out how the general public do/can access information in public offices.

Practical experience from Journalists who conducted the study shows that there is an improvement in service delivery and access to information in some of the public offices especially in Local Government as opposed to Central Government.

However, they say laxity among public servants is still a big problem in public service. “If you received someone’s documents, while would you say you can’t see them just a week later?” questions Haika Kimaro, Mwananchi Correspondent in Mtwara. 

Similar sentiments were echoed by George Binagi, a Radio Journalist in Mwanza. “I submitted my questions in writing to the Regional Commissioner’s Office. I went back 10 days after and yet I did not get the answers , they looked for my letter and they never saw it” .

FOR MORE NEWS CLICK HERE

NAIBU WAZIRI MHANDISI NGONYANI ATEMBELEA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA, AZUNGUMZA NA UONGOZI, WAFANYAKAZI WA SHIRIKA

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akipatiwa maelezo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, wakati alipotembelea vitengo mbalimbali vya shirika hilo, kuongoea na Uongozi pamoja na wafanyakazi, Dar es Salaam leo. Wa tatu ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhura Pinde.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akipatiwa maelezo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo kuhusu utendaji kazi wa kitengo cha utumaji na upokeaji wa fedha cha Western Union, katika ziara hiyo. 
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo (kulia), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani kuhusu idara mbalimbali za Posta Kuu, wakati alipotembelea sehemu hiyo katika ziara hiyo. Kushoto ni Meneja wa Posta, Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, akisalimiana na kuagana na wafanyakazi mara baada ya kumaliza kuzungumza nao, leo jijini Dar es Salaam. 

MSHINDI WA TATU MBIO ZA DUNIA (LONDON MARATHON) FELIX SIMBU AWASILI NCHINI LEO

$
0
0

MSHINDI wa tatu wa Mbio za Dunia za London Marathon mwaka huu, Felix Simbu amesema kuwa ushindi huo alioupata si wapeke yake bali wa wanariadha wote ambao walienda kushiriki kutokana walijitoa muhanga hadi kufanya vizuri.

Simbu alishika nafasi ya tatu katika mbio za Km 42 na kuitoa kimasomaso Tanzania ambayo ilikuwa haijafanya vizuri katika mashindano hayo kwa miaka mingi.

Akizingumza mara baada ya kutua akitokea nchini Uingereza ambapo alipokelewa na mamia ya mashabiki, Simbu alisema haikuwa kazi rahisi kupata medali hiyo imetokana na wao kujitoa muhanga.

"Ushindi huu si wangu peke yangu bali ni wa wetu sote kutokana tulikuwa na umoja."Huu ni ushindi wa wote, hivyo umoja wetu utazidi kujitahidi kufanya vizuri zaidi hapo baadae," alisema.

Alisema, aliona kama maajabu kwa ushindi huo baada ya kuona bendera ya Tanzania inapandishwa kuashiria ushindi wake.Awali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harryson Mwakyembe alisema ushindi huo umewafanya Watanzania wawe na furaha kutokana hawakuwa na imani ya kufanya vizuri.

Alisema ni wakati sasa wa kuwekeza katika mchezo huo ili uweze kupiga hatua zaidi.Simbu aliwasilia saa 12:20 jioni kutokana na kuchelewa kufika ambapo awali aliyatarajiwa kufika saa 6:05 mchana.

Kufika kwake alipokelewa na vikundi mbalimbali vya ngoma, wasanii ambao waliongozwa Khadija Kopa na Riyama Ally.

RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAIS WA MISRI PIA AKUTANA NA WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati wa nyimbo za mataifa mawili zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA). Rais huyo wa Misri ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati akielekea kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza nyimbo za kikundi cha matarumbeta kilichokuwa kikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi ambaye ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Tanzania yahudhuria Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia mjini Baku, Azerbaijan

$
0
0
Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia unafanyika nchini Azerbaijan katika mji wa Baku kuanzia tarehe 14 hadi 18 Agosti 2017. Mkutano huu utajumuisha nchi zote wanachama ambao zinafikia nchi 167. Kila nchi inapaswa kutuma wajumbe 6 kuhudhuria mkutano huu, lakini pia waangalizi (Observers) wanakaribishwa.

Ni mkutano mkuu ambao unazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu mafunzo kwa vijana skauti, miradi mbalimbali, mafanikio na changamoto mbalimbali zinazokabili nchi wanachama.

Tanzania inawakilishwa na wajumbe 6 muhimu kama Katiba ya Shirikisho la Vyama vya Skauti Duniani (World Scout Bureau) inavyosema, lakini pia ujumbe huo unaongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa DK. Jakaya Mrisho Kikwete, kama Mlezi Mstaafu wa Chama cha Skauti Tanzania. Kwa kawaida Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania ni Rais wa Nchi kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania.

Mheshimiwa DK. Jakaya Kikwete amepewa Heshima ya kuwa Msemaji Mkuu (Keynote Speaker) wa ujumbe wa Chama cha Skauti Tanzania.

Ujumbe wa Chama cha Skauti Tanzania tayari umeshaondoka nchini kuhudhuria Mkutano huo, ambapo Mheshimiwa DK. Jakaya Kikwete ameomba kukutana na Viongozi wa Vyama vya Skauti nchi za Afrika kuzungumza na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu uskauti barani Afrika wakati wa Mkutano Mkuu huo.

Ujumbe wa Chama cha Skauti Tanzania ni pamoja na Skauti Mkuu Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza. Kamishna Mkuu Mheshimiwa Abdulkarim Esmail Shah. Naibu Kamishna Mkuu ndugu Rashid Kassim Mchatta. Kamishna Mtendaji Bi. Eline Kitaly. Na Kiongozi wa skauti kutoka mkoa wa Dar es salaam ndugu. Dinesh Rajah.

Chama cha Skauti Tanzania kimetimiza Miaka 100 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini, na sherehe za maadhimisho hayo zilifanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 21 hadi 28 Julai 2017 ambapo Viongozi mbalimbali wa Kitaifa walialikwa wakiwemo Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu, pamoja na Skauti wenyewe kutoka ndani na nje ya Nchi.

Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa  Maadhimisho hayo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ambaye alimuwakilisha Rais DK. John Pombe Magufuli.

Tuzo na Nishani kadhaa zilitolewa kwa Viongozi mbalimbali wa Nchi, Viongozi wa Skauti, na skauti wenyewe ambao wameshiriki katika matukio ya ujasiri, michezo na mashindano za stadi za kiskauti.

Maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania yalifungwa na  Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi.

Ujumbe wa Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ambao wanahudhuria Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia  pia utapokea Tuzo na Cheti maalum cha kutimiza Miaka 100 ya uskauti Tanzania, ujumbe huo  unatarajia kurejea nchini tarehe 21 Agosti 2017.


IMETOLEWA NA HIDAN .O. RICCO.

KAMISHNA MKUU MSAIDIZI

 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa DK. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia  mjini Baku, Azerbaijan
Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa DK. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 100 ya Skauti nchini zilipofanyika mkoani Dodoma mwezi Julai. Pamoja naye ni Skauti Mkuu Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza (kushoto). Kamishna Mkuu Mheshimiwa Abdulkarim Esmail Shah (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana
Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Mheshimiwa DK. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia  huko Baku nchini Azerbaijan

POLISI: BODABODA MARUFUKU KUPAKIA WATOTO...

ZIARA YA SIKU MBILI YA RAIS WA MISRI NCHINI TANZANIA

INTRODUCING Mrisho Mpoto Ft Kassim Mganga - Kitendawili (Official Video)

BREAKING NEWZZZZZZ: MOTO MKUBWA WATEKETEZA SOKO LA SIDO USIKU HUU JIJINI MBEYA

$
0
0
Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa Ripota wetu jijini Mbeya,zinaeleza kuwa Soko la Sido lililopo mkabala na maeneo ya Mwanjelwa linateketea kwa moto hivi sasa,Taarifa zinaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.

Kwa mujibu wa Ripota wetu aliyepo eneo la tukio,anaeleza kuwa  Moto huo ulianza kuwaka mnamo majira ya saa tatu usiku huu na kusababisha tafrani kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwepo maeneo hayo,ambao nao walionesha juhudi zao za kushriki kuuzima,lakini kwa bahati nzuri kikozi cha zima moto kikawa kimeishawasili na kuendelea kupambana na moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi kubwa mpaka hivi sasa tunapoingia mitamboni.

Kama vile haitoshi katika kuongeza nguvu za kiusalama eneo hilo,Kikosi kutoka jeshi la Polisi la mjini Mbeya tayari nalo liliwasili katika eneo hilo katika suala zima la kuhakikisha ulinzi na usalama wa mali za watu unaimarika .

TAARIFA ZAIDI TUTAWALETEA 

Moto huo ukiendelea kuteketeza bidhaa mbalimbali zilizoachwa sokoni hapo usiku huu,huku Kikosi cha zima Moto kikiendelea kupambana na moto huo.

MAGAZETI YA JUMATANO LEO AGOSTI 16,2017


Uchambuzi wa ki-Ingereza wa Wimbo wa Roma, "Zimbabwe"

$
0
0
Na Profesa Mbela
Roma, a Tanzanian composer and singer, has become a household name in Tanzania, albeit controversial, on account of his compositions. His latest song, "Zimbabwe," has just been released to much acclaim, but also reservations. It is a charged piece that is bound to raise sentiments and maybe ruffle a few feathers.
"Zimbabwe," is a music video that brings up seemingly disconnected and random images and references incorporating ideas, sentiments, and pleas. Clad in flowing robes, like a prophet, Roma traverses an expansive landscape proclaiming his message, which sounds like an apocalypse. I think of Yeats's vision--in "The Second Coming"... of a rough beast slouching towards Bethlehem to be born, but Roma's vision is not entirely dark and ominous.
The plight of prophets is often uncertain and Roma's is no exception. He has experienced rejection, censure and even kidnapping, which is a key theme, if not the impetus, of his "Zimbabwe" song. A prophet can be rejected, becoming a voice crying in the wilderness. 
In this video, Roma appears in the wilderness much of the time, but he has a sizable following, heading with him towards the distant horizon beyond which, presumably, Zimbabwe lies.
I have stated that this song pulls together seemingly disparate and random ideas, sentiments, and references, but there is method in the madness. Running through the song is a mood, not of celebration or joy, but sadness, which is sustained by the repetitive beat of soulful sounds. 

For more CLICK HERE

MSANII CHID BENZ NA WENZAKE WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Watu saba akiwemo msanii wa Bongo Fleva Chid Benz ambaye jina lake halisi ni Rashid Makwiro wamekamatwa na Jeshi la polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala kufuatia msako uliofanyika hivi karibuni na kubainika kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,Salum Hamduni alisema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12 majira ya saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya. 
‘’Chid Benz na wenzake wapo kituo cha polisi cha Msimbazi ambapo tunaendelea na upepelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa Mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa”,alisema Hamduni.
Kamanda huyo alisema kuwa baada ya kuwakamata vijana hao,sasa wanajikita kusaka mtandao mzima unaohusika na biashara hiyo ili kuhakikisha hatua kali zinachukuliwa dhidi yao.

INTRODUCING "SHOO SHOO" BY MKUBWA NA WANAWE Ft. NINJA

NAIBU WAZIRI WA UJENZI UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATEMBELEA TEMESA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati (aliyevaa suti) akimsikiliza Mkuu wa Kivuko/ Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe wakati akimpa taarifa ndani ya chumba cha kuongozea kivuko cha MV. KAZI alipotembelea kujionea utendaji kazi wake, wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu .
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Makao makuu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Dk. Mussa Mgwatu wakati akisoma taarifa fupi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani aliyetembelea ofisi za wakala huo kujionea utendaji kazi na kusikiliza changamoto zinazoukabili wakala huo
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu katikati akitoa ufafanuzi wakati alipokua akisoma taarifa ya wakala huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani wa kwanza kushoto. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa wakala huo Hans Lyimo. Mheshimiwa Ngonyani alitembelea ofisi za wakala huo kujionea utendaji kazi na kusikiliza changamoto zinazoukabili wakala huo.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati akimsikiliza Meneja wa Karakana ya Mt Depot Mhandisi Moses Humbe wa kwanza kushoto alipokua akimuelezea kuhusu utendaji kazi wa karakana hiyo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.

Jaji Mark Bomani na mkewe washerehekea nusu karne ya ndoa yao

$
0
0


Jaji Mstaafu Mark Bomani na mkewe wakikata keki katika hafla ndogo ya kusherehekea miaka 50 ya ndoa yao nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
 Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na mkewe Mama Sitti Mwinyi wakijiunga na Jaji Mstaafu Mark Bomani na mkewe   katika hafla ndogo ya kusherehekea miaka 50 ya ndoa yao  Mikocheni jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
 Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na mkewe Mama Sitti Mwinyi na Mama Rose Rupia wakiwa  na Jaji Mstaafu Mark Bomani na mkewe   katika hafla ndogo ya kusherehekea miaka 50 ya ndoa yao  Mikocheni jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
 Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Mama Everlyin Warioba wakiwa  na Jaji Mstaafu Mark Bomani na mkewe   katika hafla ndogo ya kusherehekea miaka 50 ya ndoa yao  Mikocheni jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma.
 Wakiwa na watoto na wajukuu kwenye sherehe ya nusu karne ya ndoa yao



Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images