Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1860 | 1861 | (Page 1862) | 1863 | 1864 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo wamefanya ziara katika miradi ya barabara inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa lengo la kujua Maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.
   
  Miradi iliyotembelewa ni Barabara ya Watani kwa Jongo Kata ya Makurumla ambayo ina Urefu wa kilomita 1 na inajengwa kwa kiwango cha changarawe kwa kutumia fedha za Ndani (own source), Barabara ya Ubungo Msewe kutokea  Kimara Baruti yenye urefu wa Kilomita 2.6 inasimamiwa na TAN ROADS, Pia Barabara ya Kifuru – Msigani yenye urefu wa kilomita 4.0 ambayo ina simamiwa na TAN ROAD na inajengwa kwa kiwango cha lami.

  Wajumbe wa bodi ya Barabara hiyo wamedhamiria kuhakikisha miradi iliyopangwa  inatekelezwa kwa wakati na kwa ubora ili kuboresha miundo mbinu ambayo itawanufaisha na kuwaletea maendeleo wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

  Wajumbe hao kwa Upande wa Manispaa ya Ubungo ni Mhe. Mbunge wa viti maalumu Suzan Lymo, Mkururugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo, Katibu tawala wa Wilaya Ndg James  Mkumbo  na Wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa ni ziara ya kukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Leo Agosti 14
  Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua daraja lililopo kwenye barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa ni ziara ya kukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. 
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) akiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo wakati wa ziara ya Wajumbe wa bodi ya barabara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wakikagua barabara ya Watani kwa Jongo katika Kata ya Makurumla,leo Agosti 14


  Muonekano wa Barabara ya Kifuru-Msigani ikiwa katika hatua za awali za ujenzi,leo Agosti 14.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro amezindua mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia ‘GBV Prevention Project’ unaotekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC) la mjini Shinyanga linalotoa huduma za kijamii kwa vijana ,watoto na wanawake na makundi yasiyojiweza. 

  Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatatu Agosti 14,2017 katika ukumbi wa Diamond Field Hotel mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake na watoto wakiwemo wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali,maafisa watendaji wa kata,maafisa tarafa,afisa maendeleo ya jamii,ustawi wa jamii,afisa utamaduni na dawati la jinsia na watoto. 

  Akizungumza wakati wa kuzindua mradio huo,Matiro alilipongeza shirika hilo kwa kuelekeza nguvu zake katika mapambano dhidhi ya ukatili wa kijinsia ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii husika kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola pale wahusika wanapobainika. 

  “Serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali,ili mfanikiwe mnatakiwa mshirikishe wadau kwenye maeneo husika,mmefanya jambo jema kujitambulisha badala ya kuanza kutekeleza mradi kimya kimya kama baadhi ya mashirika vile yamekuwa yakifanya hali inayowafanya washinde kufanikiwa”,alieleza Matiro. 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC). Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud,kushoto ni Afisa Mtendaji kata ya Usanda,Emmanuel Maduhu. 
  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TVMC,Japhet Daud akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
  Mkurugenzi wa Shirika la lisilo la kiserikali la The Voice of Marginalized Community (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akitambulisha mradi wa kuzuia ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na shirika hilo.


  0 0
 • 08/14/17--13:01: Article 4


 • 0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.


  Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza suali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
  Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio.Picha na Makame Mshenga.

  0 0  Kumpigia kura KARIM MICHUZI ashinde tuma SMS neno V10 kwenda namba 0746 520 610

  0 0

  Na Mathias Canal, Pemba

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 amewasili Visiwani Pemba-Zanzibar kwa Ziara ya kikazi.

  Ambapo hii Leo atakuwa katika Wilaya ya Chakechake, katika Ziara hiyo Katibu Mkuu UVCCM Taifa atakagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kipindi hiki Cha Miaka mitano 2015-2020

  Aidha, Shaka atashiriki shughuli Mbalimbali za kijamii sambamba na kuzungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 akisalimiana na Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake mara baada ya kuwasili Visiwani Pemba-Zanzibar kwa Ziara ya kikazi.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 akisalimiana na Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake mara baada ya kuwasili Visiwani Pemba-Zanzibar kwa Ziara ya kikazi.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 akisalimiana na Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake mara baada ya kuwasili Visiwani Pemba-Zanzibar kwa Ziara ya kikazi.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 akisalimiana na Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake mara baada ya kuwasili Visiwani Pemba-Zanzibar kwa Ziara ya kikazi.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 akisalimiana na Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake mara baada ya kuwasili Visiwani Pemba-Zanzibar kwa Ziara ya kikazi.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 15, 2017 akisalimiana na Wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake mara baada ya kuwasili Visiwani Pemba-Zanzibar kwa Ziara ya kikazi.

  0 0


  Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii

  SERIKALI inatoa sh. bilioni 18.77 kwa ajili ya kugharamia elimu bure ili kila mtanzania apate elimu bora na faida yake kwa serikali hiyo, ni kuona wanafunzi wanafaulu darasa la Saba na Kidato cha Nne na kuendelea na elimu ya kidato cha tano na hadi chuo kikuu.

  Hayo ameyasema leo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati wa uzinduzi mabweni katika shule ya sekondari Nasibugani ambayo ujenzi wake uko katika hatua ya mwisho pamoja na Shule ya Sekondari Mwinyi, ambayo ujenzi umekamilika kwa kuingia wanafunzi katika mabweni hayo wilayani Mkuranga mkoani Pwani .

  Profesa Ndalichako amesema serikali ya awamu ya tano imeondoa gharama katika shule ya msingi na sekondari ili kuondosha mzigo kwa wazazi wengine ambao walikuwa wanashindwa kugharamia elimu hiyo.

  Amesema mabweni katika shule ya sekondari Nasibugani na Mwinyi zenye Kidato cha Kwanza hadi Sita ni kuongeza sehemu ya kumwezesha mwanafunzi kusoma kwa muda mrefu na pa kondokana na vishawishi vinavyopatikana mtaani.

  Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha shule mbalimbali ikiwemo pamoja na makazi ya walimu yaliyo bora pamoja na huduma zingine ikwemo umeme katika shule ya Sekondari Nasibugani.

  Amesema kuwa Mkuranga iko nyuma kielimu ni ukweli usiofichika hivyo walimu pamoja na watendaji kuhimiza suala la elimu ili viwanda vilivyopo na wanamkuranga wanufaike na sekta hiyo.

  Waziri Profesa Ndalichako amempongeza Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega kuanzisha Program kwa wanafunzi wa sekondari kuwa Hakuna Kufeli.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizindua mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Nasibugani iliyopo Wilaya ya Mkuranga.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akipanda mti katika shule ya Sekondari Nasibugani.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi katika shule ya Sekondari Nasibugani.
  Sehemu ya mabweni na nyumba za walimu ambazo zimefikia hatua ya boma


  0 0

  Lengo ni kuwafikia waliowengi na huduma za kibenki kwawasio na akaunti za benki.

  Dar es Salaam Tanzania, Jumatatu 14 Agosti 2017 – Ikiwa ni moja kati ya mikakati yake ya kuendelea kuboresha huduma zake kwa kutoa huduma kwa kila mtanzamia hasa kwa wale wasio na akaunti za Benki, Benki ABC Tanzania leo imezindua huduma za wakala itakayowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki hiyo wakiwa katika mazingira yeyote yale.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja binafsi Bi.Joyce Malai alisema Benki ABC inaendelea kuja na teknolojia mpya katika utoaji huduma ili kukidhi mahitaji ya kibenki kwa wateja wake nchini Tanzania.

  Changamoto ya Kipato kidogo na kuhitajika kwa vielelezo vingi wakati wa kufungua akaunti za Benki pamoja na uhaba wa huduma za kibenki kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini yamefanya Watanzania wakose huduma za kibenki na hivyo kufanya maendeleo ya kiuchumu ya nchi kuwa finyu. Sisi Benki ABC tumejiandaa kuhakikisha kwamba huduma za uwakala za Benki yetu zinakuwa ni suluhisho kwa Watanzania kupata huduma bora za kifedha wakiwa popote bila ya kupata shida, alisema Joyce.

  Aliongeza kuwa kama Benki inayokua kwa kasi hapa nchini, benki ABC inalengo kupanua huduma na uwepo wake kwenye miji mikubwa hivyo huduma za uwakala zitakuwa ni moja ya njia ya kufikia malengo hayo.

  Joyce aliongeza kuwa huduma za uwakala za Benki ABC itakuwa na tija kwa Watanzania ambao hawana akaunti za Benki na pia kwa wale ambao wana akaunti lakini badala ya kupoteza muda mwingi kupanga foleni kwenye matawi yao wanaweza kupata huduma hizo kwenye wakala wa Benki hiyo popote pale. Huduma za wakala zitaanza kupatikana jijini Dar es Salaam kupitia Maxcom Afrika. Wateja wa Benki ABC watapata huduma zote za kibenki kupitia wakala wote wa Maxmalipo kwa mkoa wa Dar es Salaam kabla ya huduma hiyo kusambaa nchini kote. 
   Meneja wa Kitengo Binafsi Benki ya ABC Joyce Malai akiongea na waandishi wa habari wa uzinduzi wa huduma za uwakala wa Benki hiyo kwa kushirikiana na Maxcom Africa Plc.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Maxcom Africa Plc Jameson Kasati akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari jana kwenye hafla ya kushirikiana na Maxcom Africa Plc kutoa huduma za kibenki.
   Meneja huduma za uwakala wa Benki ABC Mwita Robi akionyesha mashine ya uwakala wa huduma za kibenki jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuzindua huduma za hiyo jana.  0 0

  Mkuu wa mkoa wa RUVUMA DK BILINITH MAHENGE amemwagiza DK ANSEL MTALIMO kuhakikisha manipsaa ya SONGEA inakatiwa maji kutokana na deni wanalodaiwa na mamlaka ya maji safi na taka SOWASA kutokana na wao kuwa vinara wakutolipa akara za maji kwa muda mrefu.  

  0 0


  Makamu Mkuu wa Cho Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ,Prof,Faustine Bee akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku moja ya Elimu ya Ushirika kwa Waaandishi wa Habari wa mkoa wa Kilimanjaro.
  Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wakishiriki warsha hiyo.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ilitolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) katika Warsha ya siku moja iliyofanyika chuoni hapo.
  Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MoCU) Taaluma Dkt,Kitala Malamsha akizungumza wakati wa ukaribisho wa mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya siku moja ya Elimu ya Ushirika kwa Waandishi wa Habari.
  Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wakifuatilia mijadla katika warsha hiyo.

  Washiriki wa Warsha ya Elimu ya Ushiriki kwa Waandishi wa Habari wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Prof ,Faustine Bee.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  BENKI ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitanda na magodoro 40 katika hospitali ya Wilaya ya Temeke ikiwa ni shukrani yao katika kuadhimisha miaka 20 ya Benki hiyo ya kujali jamii ambapo msaada huo utawekeza shilingi milioni 200 katika sekta ya afya Tanzania. 

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda wakati wa kuwakabidhi vitanda 40 katika hospitali ya wilaya ya Temke jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa
   Mradi huu unalenga kusaidia upungufu wa vitanda katika hospitali nchini hivyo benki ya Exim itatoa magodoro 500 na vitanda katika hospitali za serikali mikoa 13 nchini.
   “ Mwaka huu benki ya Exim imefikia hatua muhimu sana. Tunasheherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii. Kwa miaka mingi benki ya Exim imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya, mazingira na elimu nchini. Tunatambua juhudi za serikali katika kuboresha huduma za afya hivyo basi tumejitolea mwaka huu mzima kuwekeza katika hospitali za serikali katika maeneo mbalimbali nchini.” amesema Ponda.
   Nae 
  Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Temeke Dkt. Husna Msangi amesema,kuwa  “ Upungufu wa vitanda katika hospitali ya Tememke ni changamoto kubwa. Tunahitaji vitanda  katika wodi ya watoto na wodi ya wazazi. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii katika hospitali yetu.”

  Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali, katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Mtwara, Pemba na Unguja.
  Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni zawadi kwa hospitali hiyo kwa kujali jamii na kusheherekea miaka 20 ya Benki ya Exim Tanzania. 
   Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda akizungumza katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam leo wakati wakisheherekea miaka 20 ya benki ya Exim Tanzania pamoja na kutoa msaada wa Vitanda na Magodoro 40 katika hospitali hiyo ikiwa benki hiyo inaijali jamii. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Matawi ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu. Na kutoka Kulia ni Katibu wa Afya, Sanura Kondo na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi.
  Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi(Katikati) akiwashukuru Benki ya Exim mara baada ya kutoa msaada wa Magodoro na Vitanda 40 katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam leo Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki ya Exim Selemani Ponda na Kulia ni
  Katibu wa Afya, Sanura Kondo na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Husna Msangi.

  0 0

  Na Henry Kilasila - Rukwa

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani ameendelea na ziara za uzinduzi wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA PHASE III) ambapo Agosti 14, 2017 alikuwa Mikoani Rukwa katika Kijiji cha Kabwe Wilaya ya Nkasi.

  Dkt. Kalemani alisema jumla ya Shilingi Bilioni 42.5 zitatumika kupeleka umeme katika Mkoa huo na kuongeza Mradi huo utatekelezwa katika vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 111.

  "Sehemu ya pili itahusisha vijiji 145 ambapo itaanza baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza. Kufikia mwaka 2021 vijiji vyote vya Mkoa wa Rukwa vitakuwa vimepatiwa umeme".Alisema Dk. Kalemani.

  Aidha, Dkt. Kalemani alimtambulisha Mkandarasi atakayejenga Mradi wa REA Mikoani humo Kampuni ya Kitanzania ya Nakuroi Investment Company Limited.

  Alimwagiza Mkandarasi kuhakikisha anapeleka umeme Kijiji kwa Kijiji na Kitongoji kwa Kitongoji bila kuruka na sehemu zinazotoa huduma za Kijamii kama Mashule, Zahanati, Magereza, Visima vya maji, Nyumba za Ibada na sehemu mbalimbali.

  Pia alitoa maagizo kwa TANESCO kupeleka Ofisi katika Kijiji cha Kabwe na katika maeneo yote yenye Wateja wengi lakini wapo mbali na Huduma za TANESCO.
  Naibu waziri Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani akifurahia baada ya kuzindua mradi wa REA RUKWA
  Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akiwasili eneo la uzinduzi Mkoani Rukwa, akiwa amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mheshimiwa Saidi Mtanda.
  Kutoka kushoto Mkurugenzi Mkuu REA, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. TITO E. Mwinuka katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya Nakuro Investment Company Limited inayojenga Mradi huo wa umeme Mkoani humo. 


  0 0

  MBUNGE wa jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amewataka madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,kukaa na viongozi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Saadan na Wamiliki ili kujua mapato wanayonufaika nayo kwa mwaka na changamoto zilizopo.

  Amesema zipo sheria zinazojieleza kuwa kila kijiji kinachozunguka hifadhi hupata mapato kwa mwaka kama si mwezi ambapo madiwani na halmashauri hazitambui.

  Akizungumza katika kikao cha mwaka cha baraza la madiwani Chalinze,Ridhiwani alieleza,ipo haja ya kujua sheria za maliasili zinazosaidia maeneo yao pamoja na kulinda hifadhi ili kujiongezea kipato.
  Aidha alisema kamati ndogo ya bunge ya mazingira na maliasili iliyoketi hivi karibuni kwa lengo la kujiuliza juu ya matatizo yanayoendelea kwenye bunga za hifadhi ikiwemo Wamimbiki inatarajia kufanya kikao na madiwani hao wakati wowote kuanzia sasa.

  Ridhiwani alieleza kwamba,kamati hiyo itakwenda kuzungumza na halmashauri na madiwani hao ili kujua changamoto zinazowakabili .
  “Wamimbiki ndio njia kubwa ya kupita tembo na wanyama wengine wakali kwenda Saadan na ndio njia ya wanyama wanaotoka Saadan kwenda Ruvuma na Selou”

  “Kamati itatakaizungumzie uhifadhi na kutenga mazingira yetu yakae vizuri na kutengeneza vivutio Wamimbiki ili tutengeneze fedha nyingi kwa watalii hasa wa picha”alisema Ridhiwani.

  Hata hivyo Ridhiwani alisema,zipo sheria zinazoruhusu ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri kuwa mwanachama kwa jambo hilo ambapo pia kila kijiji kinachozunguka hifadhi kwa mwaka inatakiwa kupata sh milioni.12.
  “Kata na vijiji vinavyozunguka Saadan na Wamimbiki lazima mjue hilo,mie ndio nilijua katika kikao hicho hivyo fuatilieni kwenye vijiji vyenu mjue kama huwa wakinufaika na mapato hayo” .  0 0

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, amesema, uwekezaji mkubwa utakaofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC baada ya kuorodheshwa rasmi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) jana utasaidia kuongeza mapato ya Serikali na kuwezesha wananchi.

  Kampuni hiyo jana ilijiorodhesha hisa zake DSE baada ya kuuza asilimia 25%  ya hisa zake ambapo kiasi cha shilingi bilini 476 kimefanikiwa kukusanywa.
  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uorodheshaji wa hisa hizo, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango,  alisema uoredheshwaji huo ni hatua muhimu ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.

   “Mgawanyo wa hisa zilizouzwa kwa umma umefanyika kwa kutoa kipaumbele kwa wawekezaji wa ndani ya Tanzania ambapo wamepata aslimia 100% ya maombi yao ya waliofanya katika ununuzi wa hisa zilizouzwa kwa umma na hivyo hivyo wawekezaji wa ndani kupata asilimia 60% na wawekezaji wa kimataifa asilimia 40%,”.

  Waziri Mpango alisema kipaumbele kimetolewa kwa wawekezaji wa ndani ili kuwezesha Watanzania kuwa washiriki katika maendeleo ya uchumi wa nchi yao badala ya kuachwa pembeni ya mageuzi na maendeleo ya kiuchumni yanayotokea hapa nchini.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao alimwambia Waziri Mpango kuwa fedha zilizokusanywa zitatumika kufanya uwekezaji zaidi na hivyo kuwafanya wawekezaji wapya kunufaika na uwekezaji wao ndani ya Vodacom Tanzania.

  “Tutaendelea kufanya uwekezaji mkubwa na wenye tija kwa ajili ya wanahisa wetu. Vodacom ndiyo kampuni ya simu za mkononi inayoongoza na kupitia uwezeshaji huu wa kimtaji tunatarajia kukuwa zaidi,”alisema
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Dk John Mduma alisema mafanikio hayo yanaleta chachu ya maendeleo na mageuzi katika sekta ya masoko ya mitaji na fedha hapa nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (kulia)akipiga kengele kuashiria kuorodheshwa rasmi kwa hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC katika Soko la Hisa la Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao na Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Moremi Marwa.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (kulia) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (katikati) kuhusiana na kufanikisha kuorodheshwa rasmi kwa hisa za kampuni yake katika Soko la Hisa la Dar es Salaam jana.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Moremi Marwa.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (wapili kulia) Mwenyekiti wa bodi ya soko la hisa, John Mduma (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Moremi Marwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao akifafanua jambo wakati wa Uzinduzi wa hafla ya kuorodheshwa rasmi kwa hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC katika Soko la Hisa la Dar es Salaam jana.


  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiongea wakati wa  hafla ya  Uzinduzi wa kuorodheshwa rasmi kwa hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania PLC katika Soko la Hisa la Dar es Salaam jana. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Moremi Marwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, alipofanya ziara ya kikazi bandarini hapo, jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akitoa maelekezo kwa Mkururgenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko wakati akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka hiyo wakati alipofanya ziara ya kikazi, jijini Dar es Salaam. 
   Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Meli kutoka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kapteni Abdullah Mwingano, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa tatu kushoto), kuhusu utaratibu wa upakuaji wa mafuta bandarini wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Bandari ya Dar es Salaam.
   Meneja Msaidizi wa Mifumo ya ukaguzi wa mizigo (Scanner), Bandari ya Dar es Salaam Bw. Jackson Paul, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, namna mifumo hiyo inavyofanya kazi wakati wa ziara yake ya kikazi bandarini hapo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi katika Bandari ya Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko. Kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Freddy Liundi.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


  0 0

  Nahodha wa timu ya Mchenga Mohamed Yusuph (jezi 10) akiwa amerusha mpira ulioleleka langoni mwa timu ya TMT katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Michuano ya Sprite BBall King.


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.  Timu ya mpira wa kikapu ya Mchenga Bball Stars imeanza vyema katika mchezo wa kwanza wa fainali ya Sprite BBall kings kwa kuweza kuibuka na ushindi wa alama 101 dhidi ya 71 vya TMT.

  Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay ulikuwa wa kasi kwa kila upande kwa timu ya TMT Kuonekana kuwabana na kuwalinda Mchenga Bball stars.

  Katika mchezo huo wa kwanza wa fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings,Mchenga wameweza kuibuka na ushindi wa alama 101 ambapo katika robo ya kwanza na ya pili walionekana kupewa ulinzi mkali na timu ya TMT lakini utulivu, umakini na nidhamu ya wachezaji wa Mchenga uliweza kubadili matokeo katika robo ya tatu na ya nne.
  Nahodha wa timu ya TMT Isihaka Masoud amesema kuwa wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa fainali ila bado kuna mechi zingine zinazoweza kuamua matokeo na zaidi wanaenda kuangalia wapi wamekosea ili katika mchezo wa pili wa fainali waweze kuibuka kushinda.

  "Tunaenda kuangalia wapi tumekosea, turekebishe na katika mchezo wa pili wa fainali tunataka kuhakikisha tunatoka na ushindi kwani mecho moja haiwezi kuamua matokeo ya mechi zilizobaki," amesema Isihaka.

  Fainali hiyo inayoendelea katika viwanja vya Don Bosco iliweza kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo pamoja na kutoa Burdani kwa mashabiki wa mpira wa kikapu waliojitokeza kushabikia timu hizi mbili za Mchenga BBall Stars na TMT zote zikitokea Upanga.

  Baadhi ya wasanii waliohudhuria ni pamoja na Young D, Lulu diva, Tammy the baddest, Country Boy ,Kajala, DJ choka na wengine wengi.

  Mchezo wa pili wa  fainali utapigwa tena Kesho, Jumatano katika Viwanja vya Don Bosco ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kiasi cha milion 10, mshindi wa pili milioni 3 na mchezaji bora wa michuano (MVP) atajinyakulia milioni 2.

  0 0

  Mshauri wa Klabu ya Ndanda katika masuala ya biashara Peter Simon na afisa masoko Motisun Group, Erhard Mlyansi wakibadilishana na hati ya mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wa klabu hiyo kupitia bidhaa yake zenye chapa ya Kiboko.

  Klabu ya Ndanda imesaini mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini na kampuni ya Motisun Group ambao ni watengenezaji wa bidhaa zenye chapa ya Kiboko. 

  Kwa mujibu wa afisa masoko Motisun Group, Erhard Mlyansi amesema thamani ya mkataba huo inakaribia ile ya mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania bara. 

  “Tumesaini mkataba wenye thamani kubwa lakini hatuta weka wazi ni kiasi gani cha pesa. Udhamini wetu kwa Ndanda utakuwa ukikaribiana na wa mdhamini mkuu wa ligi kuu Tanzania bara,”amesema Mlyansi. 

  "Kikubwa wanataka kuona timu ikipata matokeo mazuri na kuleta ushindani mkubwa na hatutaki kuona migogoro katika timu, ". 

  “Tumeingia mkataba wa mwaka mmoja lakini kutokana na mahusiano yaliyopo tutakuwa tukipokea maombi kutoka Ndanda juu ya mahitaji yao na kufanyia kazi yale tutakayoona tunayaweza,”amesema. 

  Mshauri wa Ndanda katika masuala ya biashara Bw. Peter Simon amesema, watahakikisha Motisun wanapata nafasi ya kujitangaza kupitia Ndanda SC. 

  “Sisi Ndanda tutawapa Motisun Group nafasi ya kujitangaza kupitia mabango ambayo yatawekwa kwenye uwanja wetu wa yumbani.” 
  Mshauri wa Klabu ya Ndanda katika masuala ya biashara Peter Simon (kushoto) sambamba na afisa masoko Motisun Group, Erhard Mlyansi wakisaini mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja kupitia kwa bidhaa zenye chapa ya Kiboko.

  0 0

  Na Ali Othman Ali

  Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri amepokea Cheti cha shukrani kutoka kwa Taasisi ya Rafiki Network kutokana na juhudi na mchango wake mkubwa aliotoa katika kufanikisha Bonanza la kihistoria la kimichezo lililoandaliwa na taasisi hiyo kisiwani Pemba.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa cheti na Rais wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Hamad Hamad ofisini kwake Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Mh Naibu Waziri amesema ipo haja ya kufufua michezo iliyosahauliwa ya Kipemba ili kuibua burudani ambazo amesema kwasasa zimekua adimu.

  “Watu wanataka burudani kwasababu zimekua adimu hivyo ni vizuri kuendelea na kufufua michezo iliyosahauliwa ikiwemo michezo ya kivita ya kipemba (martial arts) kama vile Ngware na Kirumbizi” Amesema Mh. Mmanga.

  Akielezea juu ya kuridhishwa kwake na juhudi za Taasisi ya Rafiki Network katika kuandaa na kusimamia Tamasha la kimichezo kisiwani Pemba lijulikanalo kama “Pemba Weekend Bonanza”, Mheshimiwa Naibu Waziri amesema Taasisi ya Rafiki Network imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuamsha hisia za watu kiburudani zinazohusiana na michezo yao ya kiasili.

  Aidha Mh. Waziri amesema burudani zimekua adimu kisiwani Pemba ambapo ametumia kigenzo cha wananchi kujitokeza kwa wingi katika tamasha la Pemba Weekend Bonanza kuwa ni ishara tosha ya kuadimika kwa michezo na burudani kisiwani Pemba. Ameongeza kua michezo ni muhimu sana kwa kuwaunganisha watu.

  Taasisi ya Rafiki Network iliandaa tamasha kubwa la Kimichezo Kisiwani Pemba ambalo lilifanyika kuanzia tare 28 hadi 30 Julai ambapo michenzo mbalimbali ikiwemo mchezo wa Ng’ombe, Resi za Baiskeli, Mashindano ya Kuogelea na Resi za Ngalawa yalifanyika ambapo washindi na washiriki walizawadiwa.
  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri akipokea Cheti cha Shukrani kutoka kwa Raisi wa Taasisi ya Rafiki Network Bw. Hamad Hamad huko Ofisinini kwake Mazizini.

  0 0

  Idara ya Uhamiaji inapenda kuufahamisha Umma kwamba, utolewaji wa pasipoti zenye hadhi ya Kidiplomasia (Diplomatic Passport) na Kiutumishi (Service Passport) upo kwa mujibu wa Sheria ya Pasipoti na Hati za Kusafiria Sura ya 42 ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni zake. 

  Katika Vifungu Namba 10(2) na (3) na Jedwali la Pili na la Tatu la Sheria hiyo, makundi mbalimbali ya watu wanaostahiki kupewa pasipoti hizo yameainishwa.

  Hivyo, Idara ya Uhamiaji inawataka wale wote ambao wamefikia ukomo wa Utumishi wa nyadhifa na hadhi hizo, warejeshe pasipoti hizo kwenye Ofisi za Uhamiaji ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu tarehe ya kutolewa kwa taarifa hii, kama yalivyo matakwa ya Kifungu cha 8(2) cha Sheria tajwa hapo juu; isipokuwa wale ambao kwa mujibu wa nyadhifa zao wanaruhusiwa kisheria kuendelea kutumia Pasipoti hizo hata baada ya kustaafu kwao wakiwemo Viongozi Wakuu wa Nchi wastaafu, Wakuu wa Mihimili ya dola Wastaafu na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Wastaafu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu kwenye Sheria hiyo.

  Baada ya kuisha kwa kipindi tajwa yaani mwezi mmoja baada ya kutolewa kwa taarifa hii, wasiostahiki kuwa nazo watazuiliwa safari zao mara watakapopita katika vituo vya kuingia na kutoka nchini ikiwa ni pamoja na Viwanja vya Ndege. Aidha, ieleweke kwamba, kuendelea kuwa na Pasipoti hizo kwa wasiostahiki ni kosa kisheria chini ya kifungu cha 19(2)(k) cha Sheria tajwa.

  Imetolewa na 

  KITENGO CHA UHUSIANO,
  IDARA YA UHAMIAJI, 
  MAKAO MAKUU.
  15 AGOSTI, 2017.

  0 0


  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi akiwa na Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Masijala ya Kijiji Cha Nyange ambayo itakuwa inatunza kumbukumbu ya hati.


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii , Kilombero

  Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wananchi kuacha kuuza maeneo yenye hati za kimila na kuwaonya kuwa maeneo hayo yamepimwa na serikali zaidi hawatatozwa kodi kwa wananchi wanaomiliki ardhi za kimila na maofisa ardhi wawatoze kodi wale wenye hati za miaka 99 za umiliki wa mashamba makubwa ya biashara.

  Lukuvi ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa hatimiliki za kimila zaidi ya 2000 katika Kijiji cha Nyange wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro kupitia Mradi wa Uwezeshaji Umilikishaji Ardhi (LTSP).

  Lukuvi amesema hatimiliki hizo zipo kwa lengo la kulinda ardhi ya vijiji husika na kwamba walanguzi wa ardhi hawatapata nafasi kwa kuwa ardhi iliyopimwa haitaweza kununulika kwa mtu ambaye sio wa kijiji hicho. Amesema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya udalali wa ardhi lakini kutokana na ulinzi uliowekwa katika hatimiliki hizo, hawataweza kwa kuwa ardhi haitanunulika.

  "Hili ni agizo kutoka kwa Rais Dk John Magufuli kwamba wananchi wote watakaopatiwa hatimiliki za kimila wasitozwe kodi isipokuwa wale wenye mashamba makubwa ya biashara ambao watatozwa kila ekari Sh 1,000. Kwa kuwa hamtalipa kodi, basi fedha hiyo muitumie kuzalisha zaidi kwa manufaa yenu ya baadae," alisema Lukuvi na kuongeza;

  "Ardhi iliyopangwa na kupimwa hata kama ardhi ni ndogo inathamani kubwa zaidi ya mtu mwenye eneo kubwa ambalo halina hatimiliki."

  Alisisitiza kuwa wananchi waliopewa hatimiliki za kimila wanakopesheka hivyo, benki zote zifungue milango na kuwapatia mikopo stahiki ili kuendeleza mashamba yao na kujiinua kiuchumi. Alieleza kuwa maofisa wa serikali wanapaswa kueleza namna ya kuzalisha mazao mengi kuliko awali na kwamba ardhi isibadilishwe matumizi kama ni ya kilimo au ufugaji itumike kama ilivyotakiwa.

  Lukuvi amesema katika miaka ijayo wanatarajia kutoa hati za kimila 300,000 kwa wananchi na kwamba kwa sasa asilimia 20 pekee ya ardhi ndio imepimwa na kupangwa.

  LTSP ni mradi wa majaribio wa miaka mitatu unaofadhiliwa na Mashirika ya maendeleo ya Denmark kupitia Shirika la DANIDA na nchini Sweden kupitia Shirika la SIDA na Uingereza kupitia Shirika la UKaid  ambapo kwa sasa ni katika  Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga mkoani Morogoro. Mradi huo umeanza Julai mwaka jana kwa kazi ya kupima, kubainisha mpango wa matumizi ya ardhi.
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi ,akizungumza na Wakazi wa Kijiji Cha Nyange Kabla ya kuanza zoezi la Ugawaji hati za Kimila kwa wakzi wa Kijiji Hicho ambao wamepimiwa kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi akimkabidhi hati yake Mkazi wa Kijiji Cha Nyange , Bibi Clesencia Namuhoni wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
  Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard akizungumza na wakazi wa kijijii cha nyange juu ya umuhimu wa kumiliki hati za kimila katika kujiendeleza kiuchumi wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
  Mratibu wa Programu, Godfrey Machabe mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.


older | 1 | .... | 1860 | 1861 | (Page 1862) | 1863 | 1864 | .... | 3284 | newer