Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

AJALI ZAPUNGUA MKOANI SINGIDA, JESHI LA POLISI LAWEKA MIKAKATI KUPUNGUZA ZAIDI AJALI NA UHALIFU

$
0
0
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,
ACP,Debora Daud Magiligimba
Jeshi la Polisi Mkoani Singida, limefanikiwa kupunguza ajali za barabarani kutoka ajali 69 kwa kipindi cha mwaka 2016 hadi kufikia ajali 24 katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, ACP Debora Magilingimba wakati akitoa taarifa ya uhalifu kwa Mkoa wa Singida ambapo amesema katika ajali hizo 24 zilisababisha vifo vya watu 29 na hapajakuwepo majeruhi kabisa.

ACP Magiligimba amesema kupungua kwa ajali kumetokana na Jeshi hilo kutoa elimu ya usalama barabarani mara kwa mara hasa katika maeneo ya vijijini, mitaani na hata katika mafunzo ya udereva.

Ameongeza kuwa jeshi hilo limekuwa likithibiti mwendo kasi katika barabara kuu, kuthibiti ulevi kwa upimaji wa kilevi kwa madereva wote wa vyombo vya usafiri na hivyo kupelekea ajali kupungua sana kwa Mkoa wa Singida.

“Pia tumeendelea kutoa elimu ya usalama barabarani mashuleni, vyuoni na katika  nyumba za ibada. Lengo ni kuiongozea jamii uelewa zaidi unaohusu masuala yote ya ulinzi na usalama, na sheria za usalama barabarani”, amefafanua.

Aidha, ACP Magiligimba amesema makosa madogo yamepungua kwa asilimia 0.8 ambapo jumla ya makosa madogo 22,222 yameripotiwa katika kipindi cha januari hadi juni mwaka huu, ikilinganishwa na makosa kama hayo 22,403 yaliyotokea kipindi kama hicho mwaka jana.

“Katika makosa hayo madogo, jumla ya wakosaji 21,836 walilipa faini mbalimbali zaidi ya shilingi milioni 655. Katika kipindi kama hicho mwaka jana jumla ya wakosaji 21,778 walilipa faini mbalimbali zaidi ya shilingi milioni 653.3. Faini hizo ni sawa na ongezeko la asilimia 0.3”, amesema kamanda huyo.
ACP Magiligimba ametaja baadhi ya mikakati mbalimbali ya kukabiliana/kupunguza zaidi uhalifu, wahalifu na ajali za barabarani kuwa ni kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kupitia vyombo vya habari na kushirikiana na asasi mbalimbali katika kutoa elimu na matengenezo ya barabara.

“Vile vile tutaendelea kuimarisha ushirikiano zaidi na asasi zisizo za kiserikali, ikiwemo World Future Vocation, mabalozi wa usalama barabarani na SUMATRA. Pia tutashirikiana na TANROADS, halmashauri za wilaya na manispaa kushauriana namna ya kufanya matengenezo ya barabara katika maeneo yaliyoharibiwa au yenye kusababisha ajali za mara kwa mara”, amesema ACP Magiligimba. 

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA UJUMBE WA WATAALAMU KUTOKA MOROCCO KWA AJILI YA SHUGHULI ZA AWALI ZA UJENZI WA ENEO CHANGAMANI LA MICHEZO MKOANI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe  akizungumza  na  ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco waliofika  Mkoani  Dodoma kwa ajili ya kuanza shughuli za awali za ujenzi  wa  eneo  changamani  la Michezo .Kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Morocco waliofika Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuanza shughuli za awali za ujenzi wa eneo changamani la Michezo.Wengine pichani  ni  Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw.Petro Lyatuu.Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

RAIS WA MISRI AWASILI NCHINI LEO KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi akishuka kwenye ndege yake baada ya kuwasili nchini mchana huu, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake,  Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere, Jijini Dar es salaam mchana huu, ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili Agosti 14-15, 2017. 

Rais wa Jamhuri ya Misri Mhe. Abdel Fattah el-Sisi akisalimiana na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili nchini hivi punde kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

RC MAKONDA AWAGUSA WENYE MAHITAJI MAALUM.

$
0
0
Mamia ya watu wenye Ulemavu wa Miguu wamejitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, kuchukuwa vipimo kwanajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa, huku wengine wakitokea Mikoani.

Mwitikio huo ni kufuatia Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda kuwatangazia wenye uhitaji ya Miguu Bandia kufika ofisini kwake kwa ajili kuchukuliwa vipimo ili wapatiwe miguu hiyo bila malipo, ambapo hadi saa nne asubuhi walemavu waliokuwa wamefika ni zaidi ya 500.

Makonda amesema licha ya idadi hiyo kuzidi ile ya watu 200 iliyokusudiwa atahakikisha wote wanapimwa na wataalamu na kupatiwa huduma bila ubaguzi wa Mikoa wanayotoka sababu wananchi wote wapo chini ya Rais Dkt.Magufuli.

Amesema wote watakaopimwa watatengenezewa Miguu yao kulingana na vipimo vilivyochukuliwa.Hata hivyo Makonda amesema kutokana na wingi wa watu wenye uhitaji ataongeza siku za upimaji na kuongeza idadi ya wataalamu ili wote watakaofika wahudumiwe.

Aidha amesema awamu hii ya kwanza walemavu 200 watapatiwa miguu ya bandia wakati akiendelea kufanya jitiada za kuwasiliana na wadau ili waweze kuchangia na kuhakikisha wananchi wote wanahudumiwa.

Mbali na miguu bandia pia Makonda amefanikiwa kupata Magongo ya kisasa 17 kutoka Nchini Marekani ambayo pia atayatoa bila malipo kwa wale wenye uhitaji.
 Baadhi ya watu wenye Ulemavu wa Miguu wakiwa wamejitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, kuchukuwa vipimo kwa ajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa, huku wengine wakitokea Mikoani.
Mkuu wa Mkoa  Mh.Paul Makonda akizungumza na baadhi ya watu wenye Ulemavu wa Miguu waliojitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi yake , kuchukuwa vipimo kwa ajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa, huku wengine wakitokea Mikoani.
Mkuu wa Mkoa  Mh.Paul Makonda akizungumza na mmoja wa  watu wenye Ulemavu wa Miguu waliojitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi yake , kuchukuwa vipimo kwa ajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa, huku wengine wakitokea Mikoani.

Ndambile aanza mikakati ya kumleta Mayweather Tanzania

$
0
0
Na Mwandishi wetu.

Promota  na meneja maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Juma “Chief” Ndambile  yupo katika mikakati ya kumleta nchini bondia maarufu wa ngumi za kulipwa Duniani, Floyd Mayweather Jr mara baada ya pambano lake Conor McGregor.

Awali, Mayweather alipanga kutembelea Ghana mwezi  Juni, lakini safari hiyo iliharishwa ili kujiandaa na pambano lake dhidi ya bondia McGregor  lililopangwa kufanyika Agosti 26 kwenye  Las Vegas' T-Mobile Arena.

Ziara ya Ghana kwa bondia huyo imeandaliwa na kampuni ya Upscale Entertainment ambapo mbali ya Ghana, bondia huyo alipanga kutembelea Nigeria.

Ndambile alisema jana kuwa amefanya mawasiliano na waandaaji wa ziara ya bondia huyo nchini Ghana na mazungumzo yanaendelea vizuri.  Ndambile alisema  baada ya kufanya mazungumzo ya awali, alilazimika kusafiri hadi Ghana ili kujadiliana jinsi ya kufanikisha ziara hiyo.

“Nilikwenda Ghana na kukutana na waratibu wa ziara hiyo, kuna mambo ambayo tulikubaliana nao kuhusiana na ziara hiyo, tunaendelea vizuri sana, tunasubiri pia menejimenti ya bondia huyo kutangaza tarehe rasmi ya kufika 
Ghana na masuala mengine yatafuatia,” alisema Ndambile.

Ndambile alisema kuwa  ameweka nia ya kufanikisha yale aliyoyapanga  mara baada ya kuhudhuria mkutano mkuu wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) uliofanyika Desemba 11-17 Marekani. Tayari promota huyo amekabidhi taarifa ya mipango yake ya kuendeleza ngumi za kulipwa kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe.

“Nikiwa Marekani, niliweza kukutana na Rais wa WBC, Mauricio Sulaimai pamoja na bondia Mayweather, mabondia Lenox Lewis, Amir Khan, Wladimir Klitschko, Evander Holyfield na mapromota maarufu kama Don King na Jay Mathews, wote hao wameonyesha nia ya kuja nchini kwa ajili ya kuona vivutio vya utalii na kuwekeza,” alisema Ndambile.

Alifafanua kuwa ameamua kuwekeza katika mchezo huo na amaani endapo atafanikisha ujio wa Mayweather, Tanzania itapaa katika mchezo wa ngumi za kulipwa na vile vile kutangaza utalii.

Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau nchini Guinea Bissau kuhusu uwepo na kazi za Mahakama hiyo

$
0
0
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) yenye makao yake makuu Jijini Arusha inafanya Ziara ya kikazi nchini Guinea Bissau ili kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kwa lengo la kuitangaza Mahakama hiyo.

Katika ziara hiyo ya siku mbili inayoanza Jumatatu August 14 hadi 15 mwaka huu,Wajumbe wake ambao ni pamoja na Majaji watatu wa Mahakama hiyo na baadhi ya Maafisa wa Ofisi ya Msajili wa Mahakama watakutana na Rais wa Guinea Bissau,Waziri wa Mambo ya Nje,Waziri wa Sheria na Spika wa Bunge la nchi hiyo.

Rais wa AfCHPR, Mheshimiwa Jaji Sylvain Ore’ amesema ili kufanikisha malengo ya AfCHPR na pia kuimarisha mfumo wa Haki za Binadamu Barani Afrika,Nchi nyingi za Umoja wa Afrika hazina budi kuridhia itifaki iliyounda Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa Mujibu wa kifungu cha 34(6) na kutoa tamko rasmi la kutambua na kukubali Mamlaka ya Mahakama hiyo kuweza kupokea kesi za watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO’s).

Kwa mujibu wa Jaji Ore’,Uelewa wa wadau hao kuhusu uwepo wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu pia utaleta hamasa kwa Nchi nyingi zaidi za umoja wa Afrika kuridhia itifaki iliyoanzisha Mahakama hiyo.

Hadi sasa ni Nchi 30 kati ya Nchi 55 wanachama wa umoja wa Afrika ndiyo zimeridhia itifaki na kati ya hizo,Ni nchi 8 tu ndio zimekwisha toa tamko rasmi la kutambua Mamlaka ya Mahakama hiyo na kuruhusu Watu binafsi na Mashirika yasiyo ya kiserikali kupeleka kesi katika Mahakama hiyo.
Guinea Bissau imetia saini mkataba ulioanzisha AfCHPR mwezi June,1998 lakini haijaridhia na wala kutoa tamko la kuruhusu watu binafsi na Ngo’s kupeleka kesi Mahakamani hapo.

“Tangu mwaka 2010,AfCHPR imefanikiwa kuendesha programu mbalimbali zinazolenga kuhamasisha na kutoa elimu juu ya uwepo wa Mahakama hiyo na shughuli zake ambapo imefanya ziara katika baadhi ya Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuendesha Semina na Mikutano katika ngazi ya Kitaifa na Kikanda kwa lengo la kukuza uelewa wa wadau juu ya uwepo wa Mahakama.”Alisema Jaji Ore’.

Mwezi April mwaka huu,Mahakama hiyo iliendesha semina kama hiyo ya uhamasishaji Nchini Misri na Tunisia na tayari Tunisia imetoa tamko la kuruhusu watu binafsi na NGo’s katika nchi hiyo kupeleka kesi zao moja kwa moja katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,huku Misri ikieleza kuridishwa kwake na utekelezaji wa shughuli za Mahakama katika kipindi cha Miaka 10 iliyopita na kuahidi kuwa itaridhia itifaki husika.

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu namba 1 cha itifaki ya mkataba ulioanzisha Mahakama hiyo ambapo Itifaki hiyo ilikubaliwa juni 09,1998 nchini Burkina Faso na ikaanza kutumika Januari 25,2004 na ilianza shughuli zake rasmi Novemba 2006.

TYVA, UNA na East Africa Youth Club zakutana na vijana jijini Dar

$
0
0
Baadhi ya Viongozi kutoka Asasi za Vijana wakiwapungia mkiono baadhi ya vijana wenzao walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Vijana Dunia ambayo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kibasila Jijini Dar es Salaam jana. Asasi hizo ni TYVA, UNA na East Africa Youth Club. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika kudumisha amani” ambayo imetokana na lengo namba 16 la maendeleo endelevu ya millennia.
Baadhi ya vijana wa mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Vijana Dunia ambayo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kibasila Jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na viongozi a kutoka Asasi za Vijana. Asasi hizo ni TYVA, UNA na East Africa Youth Club. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika kudumisha amani” ambayo imetokana na lengo namba 16 la maendeleo endelevu ya millennia.
Baadhi ya vijana wa mkoa wa Dar es Salaam walioshiriki maadhimisho ya Siku ya Vijana Dunia ambayo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kibasila Jijini Dar es Salaam jana wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na viongozi a kutoka Asasi za Vijana. Asasi hizo ni TYVA, UNA na East Africa Youth Club. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika kudumisha amani” ambayo imetokana na lengo namba 16 la maendeleo endelevu ya millennia.

NEEC yaanika uwezeshaji kwa watakao tumia fursa za mradi wa bomba la mafuta

$
0
0
Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) limejipanga kuanza kutekeleza kwa vitendo fursa zitakazotokana na ujenzi wa mradi mkubwa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleni Tanga kwa kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi watakaotaka  kuzitumia fursa hizo.

Mradi huo mkubwa uliosainiwa mwezi mei mwaka huu na kuwekwa jiwe la msingi hivi karibu na Rais John Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda unalenga kutoa fursa za kiuchumi kwa watanzania.

 Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi Beng’i Issa alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwisho mwa juma, kwamba wamejipanga kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi kuzitumia fursa za ujenzi wa maradi huo kuanzisha shughuli za kiuchumi.

“Tuejipanga vizuri katika kuwaelimisha, kuwaonesha fursa zitakazo kuwepo na kuwapa uwezesha kupitia mifukoa ya uwezeshaji 19,” serikai imeweka fedha katia mifuko hii hivyo waahitajika kuchagamikia,aliongeza kusema Bi. Issa.

Alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutoa fursa za ajira 10,000 na baada ya hapo kutakuwa na ajira 1,000 kwa watanzania,  na pia amezitaka Taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo VETA kuendelea kuandaa vijana watakao endana na fursa za ujenzi huo.

Bi. Issa  alizitaja shughuli za kiuchumi zinatarajiwa kuwepo katika mradi huo ni biashara za usafirishaji wa bidhaa na watu, ujenzi wa miundombinu mbalimbali, huduma za chakula, uuzaji wa bidhaa za chakula, ulinzi, uuzaji wa vifaa vya ujenzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dkt. John Jingu wa pili kushoto akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumzia namna baraza litakavyo waelimisha wananchi kutumia fursa za mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania, wa pili kulia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa, kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA DYAMWALE

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Chabanga Hassan Dyamwale (76).

Mbali wa wadhifa huo katika eneo la mpira wa miguu, pia Dyamwale atakumbukwa zaidi akiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na kwa miaka ya hivi karibu alikuwa Mjumbe wa Kamati huru ya uchaguzi TFF tangu 2004 mpaka 2012.

Hayati Dyamwale aliyezaliwa Juni 01, 1941, aliondoka FAT mwaka 1978, lakini pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo nchini miaka ya mwanzo ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Handeni mkoani Tanga kuwa Ofisa Utamaduni, lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere akamrudisha Dar es Salaam.

“Nimeguswa na kifo cha Mzee Chabanga Hassan Dyamwale. Inna Lillah wainaillah Rajauun. Natuma salamu zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, majirani na marafiki wa hayati Mzee Dyamwale ambaye nimetaarifiwa kuwa amefariki dunia Agosti 13, mwaka huu kwenye Hospitali ya Muhimbili,” amesema Karia.

“Ni msiba mkubwa kwa wanafamilia ya michezo hususani soka,” amesisitiza Rais Karia na kuomba familia, ndugu, jamaa, marafiki kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kumpoteza mpendwa Dyamwale.

Rais Karia amesema: “Namfahamu Mzee wetu huyu tangu miaka mingi akiwa mteuliwa kutoka serikalini kushika wadhifa wa utendaji ndani ya FAT wakati ule (Kwa sasa ni TFF), alifanya kazi kwa uhodari mkubwa na uadilifu,” amesema Rais Karia.

Rais Karia amesema kwamba mbali ya kuwa mtendaji ambaye alifanya mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania kutoka ligi ya kituo kimoja hadi ligi ya mikondo miwili (nyumbani na ugenini). Taarifa zinasema kwamba alifanya kazi hiyo akiwa kwenye hema.

Pia Rais Karia alimfahamu Mzee Dyamwale alipokuwa Meneja wa Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru) aliyekuwa mtaalamu wa masuala ya ujenzi wa viwanja.

Rais Karia amesema kwamba atambukuka zaidi hayati Dyamwale kwa uhodari wake wa kazi na msimamo kwenye jambo aliloliamini lilileta mafanikio makubwa katika soka la Tanzania.Kumbukumbu nyingine zinaonesha kuwa Dyamwale ndiye aliyebuni mpango wa watoto kuingia bure uwanjani miaka ya 1980 maarufu yosso.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

RAIS WA MISRI AWASILI NCHINI NA KUPOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI

$
0
0
 Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na mgeni wake wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Misri zikipigwa uwanjani hapo.
 Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akikagua gwaride la Heshima mara baada ya nyimbo za Taifa kupigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akiangalia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili nchini. PICHA NA IKULU

RAIA WA AFRIKA KUSINI KIZIMBANI KWA MAKOSA MANNE, IKIWEMO KUTUMIA VISA YA KUGHUSHI.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
RAIA wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kujibu mashtaka ya kutishia kwa mtandao, kuishi nchini kwa muda wa miaka minne bila kibali na kutumia paspoti yenye visa ya kugushi.

Mshtakiwa huyo ambaye kabla ya kuanza kusomewa mashitaka yake alitishia kuwapiga wandishi waliokuwa wakimpiga picha kwa kujaribu kurusha mateke na ngumi. Amesomewa mashtaka yake hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambapo amekana mashtaka yote na amerudishwa rumande hadi hapo upande wa mashtaka utakapothibitisha uhalali wa Visa yake na makazi yake ya kudumu.

Akisoma hati ya Mashtaka wakili wa serikali, Nassoro Katuga amedai, Juni 22, mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa kwa kutumia mfumo wa kompyuta, alimuandia barua pepe Costa Gianna Koulos, yenye maneno ya vitisho kwa nia ya kumsababishia Koulos hisia za uoga.

Pia imedaiwa kuwa, Julai 20 Mshtakiwa Tsampos, alimuandikia barua pepe nyingine Koulos yenye maneno hayo ya kadhaaa ya vitisho na kumpa masaa 48 kumtaka wakae na kumaliza tofauti zao kinyume na hapo atamfanyia kitu kibaya. Wakili Katuga ameendelea kudai kuwa mshtakiwa huyo mwenye pasi ya kusafiria namba 246184272,  raia wa Afrika Kusini, Julai 6, mwaka huu alikamatwa akiishi nchini bila ya kuwa na kibali maalumu.

Aidha Agosti 7, mwaka huu katika kituo cha polisi cha Kati, Tsampos, alikutwa akiwa na pasi ya kusafiria yenye namba M00101612 ikiwa na Visa ya kughushi.

Mshtakiwa amekanusha kutenda makosa hayo na amerudishwa rumande baada ya mahakama kuutaka upande wa utetezi kufanya uchunguzi na kuhakikisha kama kweli mshtakiwa anaishi mbezi kama ana visa yake.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 16, mwaka huu.
Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61)  akiwafokea waandishi waliokuwa wakimpiga picha wakati akisubiri kusomewa mashtaka katika Mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaama  leo na Polisi wakimzuia kutimiza adhima yake.
Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) akisubiri kusomewa kesi yake inayomkabili katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) akitishia kuwapiga waandishi waliokuwa wakimpiga picha.
Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) akiondoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa mashtaka jijini Dar es Salaam leo.   
 Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WAZIRI MKUU: ACHENI KUAJIRI WATOTO KWENYE MASHAMBA YA TUMBAKU

$
0
0
*Ahimiza elimu kwa mtoto wa kike, akemea mimba za utotoni  

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa mkoa wa Tabora wawapeleke watoto wao shule na waache kuwatumia kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku. 

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Agosti 13, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa idara za kilimo na ushirika na viongozi wa wilaya ya mkoa huo kwenye kikao alichokiitisha ili awape maagizo maalum. 

“Ninasisitiza kuanzia sasa jamii iwapeleke watoto shule kuanzia elimu ya awali hadi sekondari na tuache kuwatumia watoto wadogo kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku. Wakuu wa wilaya simamieni eneo hili la kuondoa watoto kwenye ajira,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo pia kusisitiza viongozi wa mkoa huo wasimamie elimu ya mtoto wa kike na kuhakikisha kuwa wanahitimu elimu ya sekondari.

“Kuna tatizo la mimba kwa watoto wa shule. Eneo hili pia linahitaji usimamizi ili kuwalinda watoto wa kike wamalize elimu yao. Tuwalinde wanaposoma elimu ya msingi na sekondari, wakishafika vyuo vikuu watakuwa wamepevuka na kuweza kufanya maamuzi ya kujilinda,” alisema.

Akihutubia kwenye mikutano ya hadhara wakati wa ziara yake ya siku nne moani Tabora, Waziri Mkuu aliwaasa vijana wa kiume wasithubutu kuwaoa mabinti wanaosoma, kwani kwa kufanya hivyo, wataishia kufungwa jela miaka 30.

Pia aliwaasa wazazi wanaoamua kuwaoza mabinti zao ili wapate mahari, nao pia wana hatari kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 endapo watabainika kushirikiana na waoaji.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, AGOSTI 14, 2017.

TANESCO YAOMBA RADHI

$
0
0
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi kwa Wateja wake waliounganishwa katika Gridi ya Taifa kwa katizo la umeme lililotokea majira ya Saa 7:32 Mchana.


Jitihada za kutatua tatizo hili zinaendelea,   hadi kufikia saa 8:00 mchana baadi ya Mikoa imeanza kupata umeme.

Taarifa rasmi kuhusu tatizo hilo itatoloewa pale uchunguzi wa tatizo  utakapo kamilika. 

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu


IMETOLEWA NA:- OFISI UA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

WAZIRI MKUU AKEMEA KUAJIRIWA WATOTO KWENYE MASHAMBA YA TUMBAKU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa mkoa wa Tabora wawapeleke watoto wao shule na waache kuwatumia kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Agosti 13, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa idara za kilimo na ushirika na viongozi wa wilaya ya mkoa huo kwenye kikao alichokiitisha ili awape maagizo maalum.

“Ninasisitiza kuanzia sasa jamii iwapeleke watoto shule kuanzia elimu ya awali hadi sekondari na tuache kuwatumia watoto wadogo kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku. Wakuu wa wilaya simamieni eneo hili la kuondoa watoto kwenye ajira,” alisema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo pia kusisitiza viongozi wa mkoa huo wasimamie elimu ya mtoto wa kike na kuhakikisha kuwa wanahitimu elimu ya sekondari.

“Kuna tatizo la mimba kwa watoto wa shule. Eneo hili pia linahitaji usimamizi ili kuwalinda watoto wa kike wamalize elimu yao. Tuwalinde wanaposoma elimu ya msingi na sekondari, wakishafika vyuo vikuu watakuwa wamepevuka na kuweza kufanya maamuzi ya kujilinda,” alisema.

Akihutubia kwenye mikutano ya hadhara wakati wa ziara yake ya siku nne moani Tabora, Waziri Mkuu aliwaasa vijana wa kiume wasithubutu kuwaoa mabinti wanaosoma, kwani kwa kufanya hivyo, wataishia kufungwa jela miaka 30.

Pia aliwaasa wazazi wanaoamua kuwaoza mabinti zao ili wapate mahari, nao pia wana hatari kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 endapo watabainika kushirikiana na waoaji.

UZINDUZI WA UTOAJI WA HATI YA HAKIMILIKI YA KIMILA KUFANYIKA KESHO MKOANI MOROGORO


HAKUNA VIBALI KWA AJILI YA KUUZA SHEHENA YA VIROBA ILIYOBAKI- MAKAMBA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amesema kuwa Serikali haina mpango wa kutoa vibali kwa ajili ya kuuza shehena ya kinywaji aina ya viroba vilivyopo stoo kwenye maghala ya Wafanyabiashara wa pombe hiyo.

Aliongea hayo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika ghala la kampuni ya usambazaji wa vinywaji aina ya kiroba ya Temani iliyopo Kimara Temboni jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa Serikali ilitoa muda mrefu kuanzia mei 2016 mpaka machi 2017 kwa wenye shehena hiyo ya viroba kuuza na kumaliza mzigo wote uliopo stoo hivyo basi baada ya Serikali kupiga marufuku pombe hiyo, hakuna kibali kitakachotolewa kwa ajili ya kuuza shehena ya mzigo wa viroba uliobaki. 

Akiongea kwa Mh. Waziri , Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bi Elizabeth Massawe alisema wanaiomba Serikali iwasaidie ili waweze kupunguza mzigo mkubwa wa viroba ambao wanao katika ghala lao sababu wanapata hasara kubwa na wanatakiwa kulipia kodi ya magahala waliyokodi. .

Katika ziara hiyo ya kutembelea ghala la vinywaji la kampuni ya Tema Enterprise Waziri alikuta shehena kubwa ya katoni 150,000 za viroba zilizofungashiwa katika vifuko vya plastiki.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Temani ambayo wana ghala la kuhifadhia vinywaji aina ya viroba lililoko Kimara Temboni Bibi Elizabeth Massawe (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ghala hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ghala la kuhifadhia vinywaji la Kampuni ya Temani lililopo Kimara Temboni.


Sehemu ya vinywaji aina ya viroba na vifungashio vilivyopo katika ghala la kuhifadhia vinywaji la Kampuni ya Temani.

ANNA ABDALLAH AWAPONGEZA GIRL GUIDES KWA KUIWAKILISHA VIZURI TANZANIA NJE YA NCHI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha  Tanzania Girl Guides (TGGA), Anna Abdallah (katikati) akiwa na Girl Guides waliorejea nchini kutoka kwenye programu ya Yess ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya uongozi, utamaduni na maadili  katika nchi za Uganda, Madagascar,  Zimbabwe na Zambia. 

Hapo ilikuwa wakati wa hafla maalumu iliyoandaliwa na TGGA  Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapongeza na kupata mrejesho wa walichojifunza walipokuwa kwenye programu hiyo inayodhaminiwa na Norwey.Anna Abdallah aliwapongeza wasichana hao wanne kwa kuiwakilisha vizuri TGGA  na Tanzania katika programu hiyo nje ya nchi.

Kutoka kulia ni Ummy Mwabondo alikwenda Zambia, Farida Mjoge aliyekuwa Uganda,  Elizabeth Betha (Madagascar) na Edna Chembele (Zimbabwe)
 Girl Guides hao wakipata msosi wakati wahafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa kwa ajili yao kwenye Hoteli ya Golden Tulip, Oysterbay, Dar es Salaam.
 Anna Abdallah akiotoa nasaha na pongezi kwa Girl Guides kwa kuiwakilisha vizuri TGGA NA Tganzania kwa ujumla, ambapo aliwataka watumie mafunzo waliyoyapata kwa kutoa mafunzo kwa wasichana wenzao nchini.
 Wakiwa na furahani Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi (kushoto), Anna Abdallah (katikati) na Mjumbe wa TGGA, Agnes Makenya
 Katibu Mkuu wa TGGA Tanzania, Grace Shaba akitoa neno la ukaribisho muda mfupi kabla ya Girl Guides waliorejea nchini kutoka nje ya nchi kwenye programu hiyo kuelezea mambo mbalimbali waliyoyafanya na kujifunza.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa  Bodi ya TGGA, Sophia Mjema akitoa ufafanuzi wakati Girl Guides wakielezea mafanikio na changamoto ya mafunzo yao nje ya nchi.

TUFANYE HAYA KULETA MAPINDUZI YA SOKA TANZANIA

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Soka la nchi yetu linaenda 'halijojo' halina mtiririko wenye mwendelezo makini.Tangu kuanzishwa kwa Taifa hili ni Mara moja tu nchi yetu ilishiriki michuano mikubwa kwa ngazi ya Afrika yaani Afcon.



Ilikua mwaka 1980 ambao tulinyanyaswa sana katika uwanja wa Sululele pale Nigeria. Sululele ndio mtaa aliozaliwa msanii nguli wa Nigeria Wizkid,na anatanbulika kama mfalme wa Sululele.

Vizazi Vingi vimepita tangu mwaka 1980 hadi sasa. Na imekua kama ni suala la kawaida kila nyakati zimekuwa zikilalamikiwa. Na nyakati zikipita waliolalamikiwa kwa viwango vyao nao wanawalalamikia wale wanaocheza kwa wakati ambao waliolalamikiwa hawachezi.

Imekua kama mbio za 'relay' kila mlalamikiwa muda ukimwacha nae husubili wa kumlalamikia. Leo twaweza kuwa na kiwango kizuri tikaridhisha mashabiki lakini kesho tunakuwa kawaida.

TUFANYE HAYA KUNUSURU SOKA LETU.

Katika masuala ya utafiti kuna jambo linaitwa kukusanya taarifa za jambo la utafiti.Pia unatakiwa kufanya mapitio ya maandishi ili kujua tatizo uchunguzalo kama limewahi kuchunguzwa. Baada ya kuchunguza unatazama kufanikiwa au kutofanikiwa kwa utafiti huo.

Katika soka tinapaswa kutumia utafiti wa wenzetu walioporomoka kisoka na wakarudi vyema. Iko mifano mingi lakini tuwatazame Wajerumani na Wabelgiji.

Katika nchi ya Ujerumani baada ya kufanya vibaya katika michuano ya Ulaya mwaka 2000 walirudi katika vitalu 'grassroots' vya soka.

Wataalamu elfu moja walisambazwa nchi nzima kutafuta vipaji vya soka. Wataalamu hao wenye elimu ya ukocha waliingia miji mbali na maeneo ya chini kabisa kufanya kazi hiyo.

Maamuzi ya kuingia vitaluni kusaka vipaji ilitokana na jicho lao kuona hawana ubabe tena Ulaya.Maeneo ya Gelsenkirchen, Bremen, Colony, Munich,Hamburg, Wolfsburg, Frankfurt,Stuttgart yalifikiwa na wataalamu hao.

Uhai wa Ujerumani ulibaki katika vilabu vyao ambapo Mwaka 2001 Bayern Munich walichukua kikombe cha ubingwa wa Ulaya. Mwaka uliofuata klabu ya Bayer Leverkusen walicheza fainali dhidi ya Rael Madrid. Mwaka 2002 wakapoteza fainali dhidi ya Brazili pale Yokohama.

MAZUNGUMZO YA PAMOJA SERIKALI YA MUUNGANO NA MISRI

$
0
0

Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi katikati na Ujumbe aliofuatana nao wakiwa katika mazungumzo na Viongozi was Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiongozwa na Rais Dkt.John Pombe magufuli leo alipokuwa katika ziara ya siku mbili mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu ya Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo ya Viongozi baina ya Ujumbe wa Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi (kulia) na Viongozi wa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam,Rais Abdel Sisi na Ujumbe wake wakiwa nchini kwa ziara ya siku mbili, [Picha na Ikulu).14/08/2017.

KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA YATOA MAFUNZO YA UTAWALA NA UONGOZI WA MICHEZO SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu.

Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) imeanza kutoa mafunzo ya siku tano ya Utawala na Uongozi wa Michezo Mkoani Simiyu, ambayo yamelenga kuleta tija katika kusimamia na kuendeleza Michezo.

Mafunzo hayo yanawahusisha Maafisa Michezo Mkoa na Wilaya, Viongozi wa Vyama mbalimbali vya Michezo  na walimu wa michezo kutoka katika baadhi ya shule za msingi na sekondari mkoani Simiyu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mafunzo hayo Ndg.Suleiman Jabir amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwasaidia Maafisa Michezo, viongozi wa vyama vya michezo ngazi ya mkoa na wilaya sambamba na walimu wa michezo kupata mafunzo ya kiufundi katika kusimamia na kuendeleza michezo, ambayo hutolewa katika mikoa yote hapa nchini, chini ya usimamizi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC).

Akizungumzia ushiriki wa wanawake Ndg. Jabir amesema Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imehakikisha kuwa wanawake wanashiriki kwa asilimia 40 katika mafunzo hayo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa la mwaka 2016 la kuwashirikisha wanawake katika masuala muhimu ya kimichezo ikiwemo suala la uongozi.
  Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(katikati) akizungumza na washiriki wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wakati alipofungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka Mjini Bariadi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kutoka Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) Ndg.Suleiman Jabir akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo kutoka mkoani Simiyu (hawapo pichani) ambayo yanafanyikwa kwa muda wa siku tano Mjini Bariadi.
 Afisa Michezo wa Mkoa wa Simiyu,Ndg.Addo Komba (kushoto) akizungumza katika mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kwa maafisa michezo, viongozi wa vyama vya michezo na walimu wa michezo yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC).
 Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania(TOC) wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo hayo kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka mjini Bariadi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images