Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1858 | 1859 | (Page 1860) | 1861 | 1862 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya asili.Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.

  Katika Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi ya Saccos ya Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna nazi na mbio za Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.

  Makamu wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi mwakani kwani michezo hudumisha umoja na kuleta mshikamano katika jamii.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la Mkombozi Saccos lililpo Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi
  Viongozi na Wageni mbali mbali walijumuika kula chakula cha asili cha Wakizimkazi wakati wa shrehe ya Siku ya Wakizimkazi.
  Mashindano ya kukuna nazi yawa kizutio wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkaziilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja. 
  Wananchi wakimpokea mshindi wa pili katika mashindano ya Ngalawa kijana Ahmed Yusufu Hassan ambaye ngalawa yake ameipa jina la Ndio Mambo.


  0 0
  0 0

  Na Fredy Mgunda, Ileje: Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe, Haji Mnasi amefanya ziara ya kushtukiza kukagua miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kutokana na ilani ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2015/20 chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi CCM taifa.

  Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi akisikiliza maelezo ya
  mradi huo kutoka kwa wataalamu ambao pia ni
  wafanyakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
  Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi mfereji mkuu wa umwagiliaji wenye urefu wa km 6 wa sasenga maeneo ya kata ya mbebe lengo ni kuona mradi huu unakamilika kwa wakati na unawaugaisha wananchi wa vijiji vyote vya mradi.

  Mnasi aliwataka wananchi kuutunza na kuulinda mfereji huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia katika Kilimo cha mazao mbalimbali yanayolimwa katika ukanda huo.

  Aidha Mnasi aliwaomba wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe kuitumia vizuri fursa za uwepo wa mfereji mkubwa kwenye eneo hilo ambao unaweza kutumiwa kwa kuzalisha vitu vingi ambavyo vitakuwa na tija kwa maendeleo yao.

  Mnasi alitoa onyo kwa wafugaji wenye mifugo yao husani ngombe ambao wamekuwaa wakizagaa katika eneo hilo, alimwagiza mtendaji wa kata ya mwashitete kusimamia agizo hilo na kuongeza kuwa, kinyume cha hapa mifugo hiyo itatozwa faini kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani
   Songwe, Haji Mnasi akikagua mradi wa mfereji mkubwa
   wa umwagiliaji kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo kwa
  wananchi wa Ileje akiwa Sambamba na viongozi na
  wananchi wakati wa ukaguzi.
  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude aliwataka wananchi kuulinda na kuutunza mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa serikali imefanya kazi kuwa kuwaletea maendeleo ya Kilimo kwa wakulima ili kupunguza idadi ya wananchi tegemezi.

  Lakini mkude alimtaka Mkurugenzi na kamati zake kuhakikisha mradi huo unadumu kwa muda mrefu kwani serikali imetoa kiasi kikubwa cha pesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ili nao waweze kuinuka hapo walipo kwenda hatua nyingine ya kimaendeleo.

  "Mkurugenzi hakikisha kuwa huu mradi unasimamiwa vizuri na kuutunza ili uweze kudumu kwa muda mrefu kama lengo la serikali litimizwe kama ilivyopangwa"alisema mkude

  Nao baadhi ya wananchi ambao niwakulima wameishukuru serikali kwa mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa Kilimo ndio maisha yao hivyo wanatarajia kunufaika na kukuza uchumi katika maeneo hayo.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali italipa madeni yote ya watumishi ambayo yamehakikiwa na kukutwa kuwa ni halali. 

  “Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli alisitisha malipo sababu ya zoezi la kubaini watumishi hewa, sasa kazi hiyo imeshakamilika, yale yaliyobainika kuwa ni halali yatalipwa. Tunataka watumishi mfanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa bidii,” alisema.

  Ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Agosti 12, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kwenye mkutano uliofanyika kata ya Goweko, wilayani Uyui mkoani Tabora. 

  Akiwa katika wilaya za Sikonge, Urambo, Kaliua na Uyui, Waziri Mkuu alielezwa na baadhi ya wabunge wa mkoa huo kwamba kuna watumishi ambao walihamishwa kutoka manispaa kwenda wilaya za jirani lakini hawajalipwa fedha zao kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

  Kwa nyakati tofauti, Waziri Mkuu ambaye ameweka utaratibu wa kukutana na watumishi wa umma kila anapofanya ziara za kikazi mikoani, aliwaeleza watumishi wa wilaya hizo kwamba Serikali imeanzisha mfumo wa kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.

  “Hivi sasa tunadhibiti uzalishaji wa madeni mapya ya watumishi, hakuna madeni ya matibabu, ya likizo au ya masomo. Kila mtumishi anaruhusiwa kujiendeleza, lakini ni lazima kwanza aandike barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuelezea nia yake na akikubaliwa, ndipo aanze kutuma maombi kwenye vyuo. Mtumishi akiamua kuomba chuoni moja kwa moja ndipo alete madai yale, hatapewa chochote kwa sababu ni nje ya utaratibu,” alisema.

  Akifafanua utendaji kazi wa mfumo huo, Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa  na kwamba unasaidia kutunza, kutuma na kuhuisha  taarifa za watumishi kwa wakati na kwa ufanisi tangu mtu anapoajiriwa hadi inapofikia wakati wa kupandishwa madaraja ama kustaafu.

  Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu alisema Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya.

  “Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua kama hiyo hiyo,” alisema.

  “Mimi nimekuwa kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu, sijawahi kuona mtu anaandikiwa barua ya kupandishwa daraja halafu anakataa. Kikubwa ni kwa maafisa utumishi kuona kama kuna watumishi wanastahili kupandishwa madaraja, watume taarifa zao mapema (kabla ya tarehe 10 ya kila mwezi ili waingizwe kwenye mfumo huu, kisha wawaandikie barua za kuwajulisha wahusika. Hata barua ikichelewa kumfikia mtumishi, mshahara wake hautachelewa na kwa njia hii tutaepuka kuweka madeni yasiyo na tija,” alisema.

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi hao wajibu wao wa kuwahudumia Watanzania bila kujali hali zao na akasisitiza kuwa Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ambaye anatimiza wajibu wake.

  “Napenda kusisitiza kuwa malengo ya Serikali ni kuimarisha utendaji wa watumishi lakini pia Serikali hii haitamvumilia mtu mdanganyifu, mzembe, asiye mwadilifu na mla rushwa. Tukikukamata hatuundi tume kwa sababu tume nazo zinamaliza fedha tu. Tukiwa na ushahidi wa kutosha, tunamalizana hapohapo,” aliongeza.

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa TFF (hawapo pichani) baada ya kutangazwa na kuapishwa kwa viongozi wapya wa TFF Mkoani Dodoma.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF kumwezesha kushika nafasi ya urais, wakati wa Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika katika Ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiteta na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Michael Wambura (kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa TFF uliofanyika jana katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma.

   Na Genofeva Matemu - WHUSM

  Uongozi mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umetakiwa kufikia Januari mwakani kuwajibika kama mashirika mengine ya mpira wa miguu duniani yanavyowajibika kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye magazeti ili wananchi wapate fursa ya kufahamu namna fedha zinavyopatikana na jinsi zinavyotumika katika kuboresha na kuendeleza usimamizi bora wa soka nchini.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma Aidha Mhe. Mwakyembe amewapongeza viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza TFF kwa muda wa miaka minne kwa kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku huku akiwapongeza washiriki wote waliothubutu kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi Mkuu wa TFF wa mwaka huu.

  Kwa upande wake Rais mpya wa TFF Bw. Wallace Karia amewaahidi wapiga kuwa wake kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kwani nafasi aliyopewa na wajumbe hao kwa kumuamini ni deni ambalo atalilipa kwa kuleta mafanikio makubwa katika mchezo wa soka.

  Bw. Karia amesema kuwa furaha waliyonayo viongozi wote waliochaguliwa kuiongoza TFF kwa muda wa miaka minne iende kuwa furaha ya kazi kwa kufanya yale watanzania wanatarajia kutoka kwao.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017. Picha na IKULU
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakitakiana amani na watawa wakati wa Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakijumuika na waumini wengine kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakipata picha ya kumbukumbu na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Padre Vicent na baadhi ya wanafunzi shule ya Sekondari ya St. Joseph baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.
  Balozi wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete,wakizindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.

  Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
  MBUNGE wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,amewahimiza wananchi kujenga tabia ya kujitolea katika shughuli za kimaendeleo pasipo kuachia serikali/halmashauri na wahisani pekee.
  Aidha amesema ofisi yake na halmashauri wataendelea kuunga mkono juhudi za wafadhili na wadau wanaojitokeza kushirikiana nao kutatua changamoto zinazowakabili jimboni hapo ikiwemo elimu.
  Ridhiwani alitoa rai hiyo, wakati wa uzinduzi wa majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan Utete iliyopo kata ya Pera,Chalinze wilayani Bagamoyo,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan,kwa gharama ya sh.milioni.30.

  0 0


  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Inspekta Ibrahim Samwix, wakati alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (aliyevaa suti), akisikiliza maelezo jinsi uvunjaji wa sheria za usalama barabarani unavyoweza kusababisha ajali, wakati alipotembelea banda la Maaskari wa usalama barabarani, kwenye Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimkabidhi tuzo Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwa kutambua mchango wake katika suala nzima la Usalama Barabarani wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Balozi wa Usalama Barabarani, Samira Abuu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kupokea cheti cha kutambua mchango wake katika masuala ya Usalama Barabarani wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Mgeni Rasmi,Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akizungumza wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani ambapo aliwaasa watumiaji wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazosababisha ulemavu na vifo.Tamasha hilo limefanyika jana, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwakabidhi bendera ya taifa askari kumi (10) waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa kwenye picha ya pamoja na askari waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

  Na Tiganya Vincent-Tabora


  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia zoezi la kuhakiki idadi ya wakulima wa tumbaku na ukubwa mashamba ambayo wanaweza kulima kwa ajili ya kuweka mipango mizuri ya uagizaji wa pembejeo kulingana na mahitaji halisi.

  Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana mjini Tabora wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne mkoani hapo kuhimiza shughuli mbalimbali za maendeleo na vile vile kufuatilia zao la tumbaku.

  Alisema kuwa lengo kutaka kuboresha uzalishaji wa zao hilo na kuweka mazingira ambayo mkulima hataendelea kunyonywa na baadhi watu ambao hawalimi tumbaku lakini ikifika wakati wa uuzaji wanajifanya nao ni wakulima wa tumbaku.

  Waziri Mkuu aliongeza kuwa hatua hiyo pia itasaidia wataalamu wa eneo husika kuweza kujua kwa haraka mahitaji ya wakulima wa zao la tumbaku katika eneo lake na hivyo kuwasaidia ili waweze kuzalisha kwa wingi na tumbaku iliyo katika kiwango bora

  Aidha Mhe. Majaliwa alisisitiza kuwa msimamo wa Serikali ni kuwa kila mkulima atauza tumbaku yake kupitia Chama cha Msingi na atapaswa awe amesajiliwa na Chama kilichopo katika eneo lake na sio vinginevyo.

  Waziri Mkuu alisema kinyume cha hapo mtu yoyote awe Mwanasiasa au mtumishi wa umma atakayekamatwa anajihusisha na ununuzi wa tumbaku au uuzaji wa pembejeo za kilimo kinyume na maelekezo ya Serikali atakamatwa na hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.

  Mhe. Majaliwa aliziaagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kijiji kukamata watu wote bila kuwaonea huruma wale wananunua tumbaku kwa njia ya vishada na wale wanaojihusisha na uuzaji wa mbolea kwa wakulima bila kuwa na vibali.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mke wake Mary wakimjulia hali  leo August 13.2017 ,Mbunge wa Viti maalumu CCM Mkoa wa Kigoma  Mheshimiwa Josephine Ngezabuka .ambaye amelazwa kwa matibabu katika Hosptali ya Muhimbili (MOI) Baada yakupata ajali hivi karibuni Mkoani Kigoma. katikati mwenye miwani ni Naibu spika Dkt. Tulia Akson.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  Naibu Spika Dr Tulia Akson mwenye miwani  akiwa na Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako (c) pamoja na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Catherine Magige wakimjulia hali  leo August 13.2017 ,Mbunge wa Viti maalumu CCM Mkoa wa Kigoma  Mheshimiwa Josephine Ngezabuka ,ambaye amelazwa  kwa matibabu katika Hosptali ya Muhimbili (MOI) Baada yakupata ajali hivi karibuni Mkoani Kigoma.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuzindua jengo la kituo cha Maafa cha KmKm Nungwi akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo Wilaya ya Kaksazini ”A” Unguja leo,(kushoto) Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir,(kulia) Mkuu wa KMKM Komodoo Mussa Hassan Musa

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kuhusu mawasiliano ya KMKM wakati wa kutoa huduma inapotokea maafa baharini ,baada ya  kuzindua jengo la kituo cha Maafa cha KmKm Nungwi akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo Wilaya ya Kaksazini ”A” Unguja leo,(kushoto) Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir,(kulia) Mkuu wa KMKM Komodoo Mussa Hassan Mussa.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia  kuzindua jengo la kituo cha Maafa cha KmKm Nungwi akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo Wilaya ya Kaksazini ”A” Unguja leo,(kushoto) Waziri wan chi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir,(kulia) Mkuu wa KMKM Komodoo Mussa Hassan Musa.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  alipokuwa akizungumza na Wanchama wa Chama cha Mapinduzi CCM alipokuwa akisalimiana nao leo baada ya kuwekaji wa  Jiwe la msingi Maskani ya CCM Tushikamane,katika Kijiji cha Nungwi Wilaya ya Kaskazinmi “A” Unguja  akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya Mendeleo katika Wilaya hiyo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein  (katuikati) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndg. Maneno Mohamed Maneno (kushoto) wakati alipotembelea kukagua Jengo la Ofisi ya Bandari Mkokotoni leo pamoja na Eneo Litakalojengwa Tuta la Bandari ya Mkokotoni akiwa katika ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Kaskazini “A”Unguja leo. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA  0 0


  Courtesy of Global TV

  0 0

  Na. Hassan Mabuye

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amezindua ujenzi wa Mji wa Safari pamoja na kuwapa hati wakazi 100 wa mji wa Arusha.

  Safari City ni mji wa kisasa uliopangwa vizuri kwa kufuata sheria na kanuni za mipango miji uliopo Jijini Arusha.Eneo hili limepangwa viwanja vya nyumba za makazi, ofisi, biashara, hoteli, shule na viwanda vidogo vidogo. 

  Viwanja hivi vina huduma zote muhimu kama vile miundombinu ya maji, umeme, barabara na mfumo wa maji taka.Mauzo ya viwanja hivi yanakwenda sambamba na mauzo ya nyumba za mfano ambapo viwanja vya makazi vinaanzia Tsh 7M na kuendelea.

  Katika ziara hii Waziri Lukuvi alipokea taarifa ya ufutwaji wa mashamba kumi na mbili (12) yaliyoko Halmashauri ya Meru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

  Baada ya kupokea taarifa hiyo Mhe. Lukuvi alitembelea eneo la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano ambazo kati ya nyumba 10 zilizojengwa na NHC, nyumba saba zimeishanunuliwa.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikabidhi hati kwa wamiliki wa awali wa eneo la Safari City wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano na makabiadhiano ya Hati Miliki za Viwanja 100 kwa ajili ya Uendelezaji.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikabidhi hati kwa wamiliki wa awali wa eneo la Safari City wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano na makabiadhiano ya Hati Miliki za Viwanja 100 kwa ajili ya Uendelezaji.

   Baadhi ya Nyumba zilizokamilika ujenzi wake katika Eneo la Safari City mkoani Arusha.
   Waziri Lukuvi akipokea taarifa ya ufutwaji wa mashamba kumi na mbili (12) yaliyoko Halmashauri ya Meru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
  0 0

  Wakwanza kutoka kushoto ni Ditha Nyoni na Nancy Mbogoro watangazaji wa RUVUMA TV, Kama ulipitwa na matkio ya wiki yaliyo jili mkoani ruvuma kuanzia tarehe 07-13 August 2017 basi tumekusogezea matukio hayo kama ilivyo kawaida yetu.

  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole (wa pili kushoto) akiongoza nyimbo ya hamasa mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana kuwasili kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

  Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana akifunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani (kulia) ni  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo(kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi .

  Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana akifunga mafunzo elekezi ya  siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ndg:Humphrey Polepole akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela  ubinga,akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa
  Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.


  0 0


  · Yasajili wateja wapya 132,826 kwa kipindi cha miezi mitatu
  · Wateja wapya 1.038 milioni wa Airtel Money wasajiliwa

  Airtel Tanzania ndio kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania ambayo imefanikiwa kuongeza wateja wengi kwenye robo ya pili ya mwaka huu huku makampuni ya simu za mkononi wakishindania kuongeza wateja wapya na watumiaji wa huduma za kifedha kulingana na ripoti ya Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA).

  Kulingana na ripoti ya robo ya pili ya 2017 (TRCA’s Quarterly Communication Statistics Report), makampuni ya simu za mkononi Tanzania yaliongeza watumiaji wapya wa huduma za kifedha 1,059,163 milioni kwa kipindi cha April mpaka Juni.

  Kutokana na idadi hiyo, Airtel Tanzania ilisajili wateja wapya 1,038,193. Hii inamaanisha ya kwamba kwa kipindi hicho asilimia 98 ya wateja wa huduma za kifedha za simu za mkononi wapya waliojiunga na Airtel Tanzania.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema ‘Hii ni ishara nzuri kuwa Airtel inatoa suluhisho sahihi kwa huduma za kifedha kwa makampuni ya simu za mkononi hapa Tanzania. Kwa mfano tuangalie huduma ya mikopo rahisi ya Timiza inayotolewa kupitia Airtel Money, hatimaye imeanza kuzaa matunda’.

  Huduma ya mikopo ya Timiza inadhihirisha juhudi zetu za kutoa suluhisho inapokuja suala ya huduma za kifedha kwa kutumia simu za mkononi. Pia inaenda samba samba na juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wafanya biashara wadogowadogo na wakati wanapata huduma ya mikopo yenye marshati nafuu, alisema Singano.

  Ikiwa na ongezeko la 1.038 milioni, Airtel Tanzania kwa sasa ina jumla ya wateja milioni 5.9 wa Airtel Money kwenye soko ambalo jumla ya makampuni matano ya simu za mkononi yanashindania wateja milioni 20. Airtel Tanzania pia imefanikiwa kusajili laini mpya 132,826 kwenye robo ya pili ya mwaka na hivyo kufikisha jumla ya watejakuwa milioni 10.3. Kwa ujumla, jumla ya wateja wapya wa simu za mkononi waliongeza na kufikia 40.358 milioni mwishoni mwa mwezi Juni kutoka 39.856 mwishoni mwa Machi mwaka huu.

  Kwa kuendeleza uwekezaji zaidi nchini kwa mujibu wa Singano anathibitisha kuwa Airtel Tanzania inazidi kukua vizuri huku kampuni hiyo ikiendelea kuwekeza zaidi kwenye miradi mbali mbali ili kufuta wateja wengi wapya.

  Moja ya mradi mkubwa wa uwekezaji ni mradi wa U900. Kulingana na Singano, Mradi wa U900 unatafuta kuboresha miundombinu ya kiufundi kwa nia ya kuongeza kiasi cha data na kuboresha kasi ya data

  "Hii mikakati yetu ya kuimarisha maisha ya Tanzania kupitia huduma za kidigitali. Katika jiji la Dar es Salaam zaidi ya maeneo 300 tayari yamebadilishwa, mpango wetu ni kueneza mradi wetu wa U900 kwa mikoa ya Mwanza, Morogoro, Dodoma, Arusha na kisha katika masoko mengine yenye uwezo mkubwa hapa nchini Tanzania, "aliongeza Singano.

  0 0

  Wanafunzi wote wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje wametakiwa  kuwa na kibali cha Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) bila kufanya hivyo wanafunzi hao hawatatambulika kutokana na viwango walivyoweka.

  Hayo ameyasema Afisa Habari Mwandamizi wa TCU, Edward Mkaku katika Mkutano wa Wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya Nje ya Nchi uliokuwa umeandaliwa na Global Link Education Link (GEL), kwa ajili ya kupeana maelekezo kwa Wanafunzi wanaokwenda nje kusoma vyuo Vikuu vya Nje ya Nchi mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Mkaku amesema GEL inafuata taratibu na huwa haipeleki wanafunzi vilaza ambao hawapati vibali kutotaka TCU. Amesema kuwa TCU ndio inafanya utambuzi wa vyuo ambavyo wanafunzi wanakwenda kusoma ikiwa ni kuangalia ubora wa vyuo hivyo.

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa GEL , Abdulmalik Mollel amesema kuwa katika vitu wanavyofanya ni uhakika kwa wanafunzi kwenda kusoma katika vyuo vikuu vya nje ya nchi.Amesema mkutano huo wanaoufanya ni kujiweka wazi kuwa hakuna kificho kwa kile ambacho wanakifanya kwa wanafunzi wanaokwenda vyuo vikuu vya nje.

  Waziri zamani wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Mbunge wa Bagamoyo, Mhandisi Dk. Shukuru Kawambwa amesema kuwa wanafunzi wakasome na kuweza kuleta maendeleo.

  Amesema kuwa wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje wakapepelushe bendera kwa kufanya vizuri na kuweza kurudi vyeti.
   Mkuruegenzi  Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza  na Wanafunzi  wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya  nje ya nchi  wakiwa na  wazazi wakipata taarifa juu taarifa mbalimbali kabla ya safari ya kwenda katika vyuo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Zamani wa Elimu, Mbunge wa Bagamoyo, Mhandisi Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje katika Mkutano ulioandaliwa na Global Education Link (GEL) 
   Afisa wa Habari Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU),Edward Mkaku akizungumza juu ya Global inavyofanya  kazi kwa ukaribu  na TCU kwa wanafuzi wanaokwenda  kuwa  taarifa za  tuume hiyo.
   Mwanasaikolojia ,Chris Mauki akizungumza juu ya masuala ya Saikolojia katika kuwajenga wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje ya nchi.
   Baadhi ya wazazi wakichangia maada zinazohusiana na wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya Nje ya Nchi.


  0 0

  Na Mary Gwera

  JUMLA ya Kesi za Mauaji 24 zimepangwa kwa ajili ya kusikilizwa kuanzia Agosti 14 hadi Agosti 25 Mwaka huu katika Kikao maalum cha kusikiliza mashauri ‘Court session’ kitakachofanyika  Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

  Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, Naibu Msajili Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, Mhe. Messeka John Chaba alisema kuwa mashauri manne (4) kati ya mashauri hayo 24 yamepangwa kusikilizwa ‘hearing’ huku mashauri 20 yakiwa yamepangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali ‘Plea taking.’

  Kufuatia maandalizi ya kikao hiki maalum Mhe. Chaba ametoa wito kwa mashahidi  muhimu ambao wametumiwa wito wa kuitwa shaurini ‘summons’ kufika Mahakamani na kutoa ushahidi wao ili haki iweze kutendeka. 

  Kwa upande wa Waendesha Mashtaka - Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, Mhe. Chaba amewasihi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Mashahidi wote wanapatikana na kufika Mahakamani ili kuiwezesha Mahakama kusikiliza mashauri hayo na kuyatolea uamuzi kwa mujibu wa sheria. 

  “Miongoni mwa mashauri hayo 4 yatakayosikilizwa, mashauri 2 yalisikilizwa na Mahakama ya Rufani Tanzania na kuamuliwa yaanze upya,” alifafanua Mhe. Chaba. Aliyataja mashauri hayo kuwa ni “Crim. Sess. Case No. 52/2014 Mshtakiwa - Adrian Francis na Crim. Sess. Case No.39/2012 Mshtakiwa - Wylife Salumu@Nyendo & 2 Others. 

  Kikao hicho kitaendeshwa na Majaji watatu (3) wa Mahakama Kuu Dodoma, ambao ni;  Mhe Jaji M.A. Kwariko, Jaji Mfawidhi, Mhe Jaji H.H. Kalombola, na Mhe Jaji L. Mansoor.

  “Matarajio yetu ni kwamba kikao hiki kitasaidia kumaliza/kuondoa mashauri ya jinai ambayo ni mlundikano.  Aidha, kikao hiki kitatoa fursa kwa washtakiwa 20 kufika Mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa awali/uchukuaji wa kiri (plea taking) na huenda baadhi yao wakakiri makosa yao na kupunguza ama kuongeza idadi ya mashauri ambayo yatakuwa yameamuliwa na Mahakama Kuu kwa mwaka huu 2017,” alibainisha Mhe. Chaba.

  Mahakama ya Tanzania imedhamiria kusikiliza na kutoa uamuzi kwa wakati kwa mashauri yote ya muda mrefu na yanayoendelea kufunguliwa Mahakamani ili haki ipatikane kwa wakati  na pia kurejesha imani ya jamii.

older | 1 | .... | 1858 | 1859 | (Page 1860) | 1861 | 1862 | .... | 3286 | newer