Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 184 | 185 | (Page 186) | 187 | 188 | .... | 3270 | newer

  0 0

  DSC03960Kutoka kushoto Mary Mgawe,Khadija Riyami,Shilole,Sunday Shomari,Mkuu wa idhaa Mwamoyo Hamza, Ilya,Massanja na Raymond Maro. ???????????????????????????????Wakiwa na balozi wa Vijana Raymond Maro. DSC03967"Shilolist" ???????????????????????????????Shilole akiwa balozi Raymond Maro. DSC03966Ndani ya studio za VOA.

  0 0

  Ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji linalojengwa katika shule ya msingi Maulu kata ya Kipagalo wilayani Makete ukiendelea kwa kasi kubwa, kutokana na shule hiyo kukumbwa na uhaba wa maji hasa wakati wa kiangazi hali inayopelekea wanafunzi kupata tabu ya kujisaidia kutokana na vyoo kuwa ni vya kutumia maji. Ujenzi huo umefadhiliwa na AMREF
   Hapa mafundi wakiwa kazini kama uonavyo
   bado kidogo tuu ujenzi huo utakamilika
  Jamaa akiwa jikoni mwenyewe kujipikia ugali kwa ajili yake na mafundi wenzake wanaojenga tanki hilo(Picha zote na mdau Edwin Moshi)

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi (kushoto) katika hafla maalumu ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi hilo ambayo itatumika kufugia nyuki katika Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma.
  Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi kabla ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi la Magereza ambayo itatumika kufugia nyuki katika Mkoa wa Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi akitoa hotuba kwa maafisa wa Jeshi la Magereza kabla ya makabidhiano ya mizinga ya nyuki 85 iliyotengenezwa na jeshi hilo. Katika hotuba ake hiyo, Dk Nchimbi alimshukuru Mkuu wa Jeshi hilo nchini. Kamishna Jenerali John Minja kwa msaada huo mkubwa ambao utawahamasisha wakazi wa Mkoa wa Dodoma waweze kufuga nyuki. Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, mjini Dodoma. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).

  0 0

  IMG_8869

  Muonekano wa Banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  IMG_8862
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji wakati alipotembelea Banda la Kampuni hiyo kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  IMG_8866
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea kuzungukia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Kampuni ya MeTL Group kwenye banda hilo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akiwa pamoja na baadhi ya wageni wa meza kuu wakati wa ufunguzi wa  Mkutano wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde leo jijini Mbeya. Kulia kwa Waziri wa Maji ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe.Abbas Kandaro.

   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro akitoa taarifa  rasmi ya hali ya Maji Mkoani Mbeya kwa wajumbe wa  Mkutano watano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde (hawamo pichani)  jijini Mbeya leo asubuhi.

   Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akifungua rasmi Mkutano wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde leo jijini Mbeya.

   Baadhi ya wadau wa sekta ya maji wanaoshiriki Mkutano wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde ulioanza leo jijini Mbeya.  Wadau wa sekta ya maji wanaoshiriki katika Mkutano wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde  wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Mbeya.
  =====  ======  ======


  WAZIRI WA MAJI AFUNGUA MKUTANO WA MWAKA WA BODI ZA MAJI ZA MABONDE JIJINI MBEYA.

  Waziri wa Maji Pro.Jumanne Maghembe amefungua Mkutano wa tano wa mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde  leo jijini Mbeya katika ukumbi wa Hoteli ya Mtenda Sunset and Conference Centre.

  Katika mkutano huo, Prof. Maghembe alisisitiza kuweka mkakati wa utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla, kwa kuandaa mpango maalum wa taifa wa utunzaji wa vyanzo vya maji wa miaka mitano.

  Pia, alishauri kuanzisha Mfuko wa Vyanzo vya Maji kwa ajili ya jamii zinazoishi karibu na vyanzo hivyo, maalum kwa kuwezesha utunzaji wa vyanzo hivyo ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa ufanisi mzuri. Na akapendekeza kiasi cha Sh. bil. 3-5 kwa kuanza mfuko huo.                
                                              
   Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya maji ili kupitia utekelezaji wa malengo na mikakati katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji kwa nia ya kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinatumika kwa uwiano mzuri kwa sekta zote na kwa njia endelevu. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Jitihada za Pamoja katika Kutunza na Kulinda Vyanzo vya Maji ni Muhimu ili Kuhakikisha Upatikanaji wa Maji.

  Aidha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mha. Bashir Mrindoko, aliongeza kuwa anategemea mbinu zaidi zitatumika katika kutekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji , ikiwemo njia ya usimamizi shirikishi ili kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.
  Mkutano huo unategemea kuendelea mpaka tarehe 5, Julai na utahusisha pia kutembelea vyanzo vya maji mkoani Mbeya, ambapo kunapatikana karibu 70% ya vyanzo vya maji nchini.
   


  0 0

   Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa. Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina laNDEGE 3.
   
  Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
   
  MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
   
  Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) akizungumza jambo na na baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini Mkoa wa Dar es Salaam walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Kushoto (mbele) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja.

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) akimsikiliza kwa makini mmoja wa viongozi wa dini (kulia) wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati walipokuwa wakijadiliana masuala mbalimbali ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akifafanua jambo katika mazungumzo hayo. Picha zote na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, atakutana na Wanahabari kesho, Ijumaa, Julai 5, 2013, kuanzia saa 4:00 asubuhi, katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume uliopo katika Ofisi za Tume, Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.
   
  Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Jaji Warioba atazungumzia mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya kujadili Rasimu ya Katiba itakayofanyika katika kila halmashauri ya wilaya. Mikutano hiyo itaanza hivi karibuni. 

  Nyote mnakaribishwa.

  0 0
 • 07/04/13--03:09: LEO MAGAZETINI

 • 0 0

   Sehemu ya Ziwa Victoria ikioneakana mapema leo kutoka eneo la Soko la Samaki Kirumba Mwaloni,ndani ya Manispaa ya Ilemela.
   Ngalawa ikiwa imesheheni mizigo ikitokea visiwani ikielekea kutia nanga kwenye bandari ndogo ya eneo la Soko la Samaki Kirumba Mwaloni,ndani ya Manispaa ya Ilemela.Globu ya Jamii ilizungumza na watu kadhaa waliokuwepo eneo hilo kuhusiana na usafiri wa Ngalawa kwa ziwa Victoria,walibainisha kuwa usafiri wa Ngalawa ni msaada mkubwa wa usafiri wa mizigo na abiria ndani ya ziwa victoria kwa asilimia kubwa,na wengi wamekuwa wakiutegemea zaidi katika suala zima la kusafirisha mizigo yao kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
  Ngalawa ya Magunila ikitia nanga tayari kwa kushusha mizigo.
  Mizigo mbalimbali ikishushwa kutoka kwenye Ngalawa hiyo,ikiwemo magunia ya dagaa ambayo yalikywa yamefunikwa kama uonavyo pichani,ukiachilia mizigo mingine iliyokuwa ikishushwa kama ionekanvyo.

  0 0

  Balozi mstaafu Charles Sanga (kulia), ambaye ni Mwenyekiti wa asasi ya vijana ya Tayoa akiwaongoza wafanyakazi wa asasi hiyo kufurahia tuzo tatu walizopata mjini Nairobi nchini Kenya wakati wa maonyesho ya matumizi ya teknolojia katika kusaidia maendeleo ya kiuchumi yaliyohusisha nchi za Tanzania, Sudani Kusini ,Uganda, Burundi, Rwanda, Kenya na Tanzania.

  0 0


  VIWANJA VILIVYOPIMWA VINAUZWA VYA UKUBWA MBALIMBALI.VIPO VIKAWE HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA,NI KARIBU ZAIDI KUPITIA BARABARA YA BAGAMOYO,SHUKA NJIA PANDA YA VIKAWE/BAO BABU SEKONDARI,NI KILOMETA 9 MPAKA KWENYE VIWANJA.KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU AMA WASILIANA KWA NAMBA HII 0782122885 KWA MAZUNGUMZO ZAIDI.
  KARIBUNI NYOTE.

  0 0

  IMG_8550Rais Jakaya Kikwete (aliyenyoosha mkono) akitembelea  Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa  yanayoendelea katika viwanja  vya  Mwalimu  J. K Nyerere  jijini  Dares Salaam.kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdallah Kigoda. 
  IMG_8637 IMG_8571Rais   Jakaya   Kikwete  akipata maelezo kutoka kwa n Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo  na Makazi(UNHABITANT) Phillemon  Mutashubirwa  kuhusu wanavyofanya kazi ya kusaidia watoto wa shule  na  wanawake kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa  yanayoendelea katika viwanja  vya Mwalimu  J. K Nyerere  jijini  Dares Salaam.
   IMG_8636Rais Jakaya  Kikwete (kulia)  akiangalia  mafuta ya ubuyu  na bidhaa zingine kwenye banda la  Mfuko wa Fursa Sawa Kwa wote(EOTF) kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa  yanayoendelea katika viwanja  vya  Mwalimu  J. K Nyerere  jijini  Dares Salaam .Kutoka (kushoto)  wa pili ni Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa  (kushoto) ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Stephen Emmanuel. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Afisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Bakari Maggid akiweka karatasi zenye majina ya washiriki wa Promosheni  ya lipa kwa M pesa na Ushinde ukiwa Sabasaba na kujishindia zawadi ya shilingi Elfu 40 sanjari na muda wa maongezi wa shilingi 1000   kila siku ambapo washindi watano walipatikana,Promosheni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania wengine wanaoshuhudia  toka kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.
   Mkazi wa jijini Dares Salaam Bi.Khadija Abdallah (kushoto) akishuhudiwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw. Matina Nkurlu wapili toka kushoto na Afisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Bakari Maggid akichukua karata yenye jina la mshindi wa kwanza kati ya washindi watano waliojishindia shilingili elfu 40 sanjari na muda wa maongezi wa shilingi 1000  kila mmoja katika promosheni ya fanya malipo kwa huduma ya M PESA ukiwa Sabasaba.
   Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu akiongea kwenye simu na mmoja kati ya washindi watano waliojishindia shilingi elfu 40 kila mmoja kwenye  droo ya lipa kwa M pesa na Ushinde ukiwa Sabasaba  sanjari na muda wa maongezi wa shilingi 1000 kila siku.

  0 0

   Sehemu ya Magunia ya Dagaa yakiwa yamepangwa vyema ndani ya soko hilo tayari kwa kusafirishwa sehemu mbalimbali kwa matumizi ya binadamu na mifugo.
   Dagaa 'wachafu' wakiwa wameanikwa chini kwa ajili ya kukaushwa.!Globu ya Jamii pia ilipata nafasi ya kuzugumza na mmoja wa wafanyabishara wa dagaa,kuhusiana na bei,akaeleza kuwa dagaa wazuri kwa sasa wanauzwa kati ya elfu 8 mpaka 12 kwa ndoo ya plastiki,"Lakini pia hawa walioanikwa hapa chini sisi wakazi wa Mwanza huwa hatuli,tunatengeneza maalum kwa ajili ya kuwauzia watu wenye mifugo,lakini pia kuna baadhi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nje ya jiji la Mwanza wamekuwa wakija kuwanunua dagaa hawa "wachafu" kwa ajili ya matumizi ya chakula na kwenda kuwauza huko mikoani ikiwemo jijini dar es salaam kwa bei yao"alisema mfanyabiashara huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe hapa mtandaoni. 
   Sehemu ya soko kuu la Kimataifa la Samaki-Kirumba Mwaloni jijini Mwanza kama lionekanavyo mapema leo mchana
   Wakina mama wakijishughulisha na biashara yao ya ndizi ndani ya soko kuu la Kimataifa la Samaki-Kirumba Mwaloni jijini Mwanza
  Baadhi ya Wafanyabiashara hao wakiwa bize kuwachambua Dagaa wasiofaa na wanaofaa kwa matumizi mbalimbali. 
  Sehemu ya bango la soko hilo kama lionekanavyo pichani.

  0 0

  The fourth edition of  the Tanzania first and premier wedding show preparation are all under way slated to be held this year on 6th July at Hyatt Kilimanjaro filled with the very best of wedding suppliers and stakeholders for all wedding requirements.
   
  The founder and the organizer of this huge and remarkable annual event Mustafa Hassanali stated “Now in its Fourth year, the event is growing Bigger and Better compared to previous years and we look forward to the growth of the Wedding industry and its stakeholders”
   
  True to the quote, this years wedding show has already attracted more wedding gown designers and bridal boutique owners most of them who have been participating since its inception in 2010. The Wedding show will take place from 7pm onwards.
   
  “Wedding is the union of families and communities, a once in a life time indulgence, so our plan is to give the astute bride and grooms all their requirements they need under one roof, and this is the perfect time for them and their friends and family to see and experience all the services and products for their big day” said PR and Media Manager Esi Mgimba
   
  The Harusi trade Fair brings various wedding related vendors and suppliers all together, a melting and networking point for only the best in the Tanzanian Wedding Industry thus making Harusi Fashion Show a premier Wedding Show in Tanzania. The designers and bridal boutiques showcasing at this years event are An Nisaa Abayas, Manjuu, The Wedding Kingdom, Mustafa Hassanali, Gracella Bridal Boutique, Sinta Bridal lounge, Twaiba Classic Wear and The Brand House
   
  The following will be exhibiting at Harusi Fashion Show ,Rupam Stores LTD, Wedding Kingdom Boutique, AVP, MC Luvanda, Flying Chefs, Mbezi Garden Hotel , The Cake Shop, Liquid Lab, Gogo Shop, Queens Gems & Jewellers, Asila Bridal Packages, Harusi Nzuri, Malaika Media, E – Cakes, VanRoy, Omni Studios and Shayland Photogenic
   
  We urge the public to attend this show in Large Numbers so as to appreciate creativity, and the entrance to the show will be 50,000 tsh for the front row VIP seats and 20,000 tsh for normal seats, support Tanzanian enterprises and promote Made In Tanzania products” concluded Ms. Mgimba
   
  Harusi Trade Fair 2013 is proudly sponsored by 361 Degrees, Clouds FM, Clouds TV, Events lite, Prime Advertising, Century Cinemax and Baileys Cream and Spirit.


  0 0

   Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na mabalozi Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kwenda kufanya kazi Nchi za Nje,walipofika kumuaga Rais leo  Ikulu Mjini Zanzibar. Picha ni juu Dkt Shein akipeana mikono na Balozi wa Tanzania nchini Comoro Mhe Chabaka Kilumanga, akifuatiwa na Luteni Jenerali mstaafu Abdulrahman Shimbo (China) na Balozi Wilson Masilingi (Uholanzi)
   Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na mabalozi Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kwenda kufanya kazi Nchi za Nje,walipofika kumuaga Rais leo,
  Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamja na mabalozi Wapya wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kwenda kufanya kazi Nchi za Nje,walipofika kumuaga Rais leo

  0 0

  ZAIDI ya watu 200 wamefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho bila malipo yoyote katika mkoa wa Iringa wakati wa kampeni ya upasuaji wa macho iliyofanyika kwa siku mbili mkoani hapa.

  Wagonjwa hao wenye matatizo ya kutokuona mbali na karibu na wenye upofu walijitokeza kwa wingi katika  hospitali ya misheni ifunda na hospital ya halmashauri ya wilaya ya kilolo iliyopo ilula ili kupata huduma hiyo.

  Kutokana na upofu kuwa tatizo la kidunia Shirika la Sightseves kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la kusaidia jamii la nchini Uturuki (IHH) limeendesha kampeni hiyo ya upasuaji wa macho ili kupambana na tatizo la upofu mkoani hapa.

  Akizungumza na Mwandishi wakati wa kampeni hiyo Mratibu wa macho mkoa wa Iringa, Dokta George Kabona alibainisha kuwa Iringa  upofu upo kwa kiasi kikubwa ambapo zaidi ya watu 9,412 wanakabiliwa na tatizo hilo.

  Kwa upande wao mmoja wa wagonjwa Martini Msasa ambaye alifanyiwa upasuaji katika hospitali teule ya Ilula alisema kuwa anawashukuru sana madaktari pamoja na mradi wa IHH kwa kuwakumbuka kwani umewafanya kuweza kuona na hivyo wataweza kwenda kufanya kazi mashambani na biashara ili kujikimu kiuchumi tofauti na mwanzo walikata tamaa na kuwa watu wa kukaa ndani na kuhudumiwa kwa kila kitu.

  Huduma hiyo ya upasuaji hutolewa bila malipo yeyote na hivyo watu wenye upofu na matatizo ya macho walijitokeza kwa wingi kupima katika vituo hivyo vya afya na kupata huduma wengi wao wakiwa ni wazee.

  Sambamba na hayo pia wameshauri kuwatumia wenyeviti wa mtaa kufikisha taarifa za huduma kama hiziili taarifa ziwafikie walengwa wote mara zinapojitokeza vijijini ili watu wengi waweze kujitokeza zaidi.

  0 0   Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu wa pili  kulia akitoa akiitambulisha familia ya marehemu diwani Idd Chonanga  aliyekuwa  diwani wa kata ya Nduli aliyefariki dunia  jana 


   Mtoto  mkubwa wa  marehemu  Idd  Chonanga Bw Greyson Chonanga akipewa  mkono wa pole na waziri mkuu Mizengo Pinda aliyefika  nyumbani kwao eneo la kijiji cha Nduli  kuhani msiba  huo jioni ya leo. Anayeshuhudia ni  mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu 


   Viongozi  mbali mbali wa CCM na  serikali mkoa wa Iringa  wakiwa na  waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja  na  waombolezaji  wa msiba wa aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana.


  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiweka sahihi katika kitabu cha wageni alipotembelea banda la NSSF. Kulia ni  Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Katavi, Anna Lupembe.
  Naibu Waziri wa Fedha akipata maelezo ya shughuli za NSSF.
  Mmoja wa wanachama wa NSSF akijaza fomu ya kujiunga na mpango wa hiari wa kuchangia mafao.   
  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiangalia mchoro wa jengo la Hospitali ya Apollo itakayokuwa ikitoa matibabu ya magonjwa ya moyo pamoja na Chuo cha Utabibu na Dawa eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimpa maelezo kuhusiana na hospitali hiyo. 
  Wengi walivutiwa na huduma za NSSF.
  Huduma za matibabu.
  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene  akizungumza na waandishi wa habari.
  Watu wengi walijitokeza katika banda NSSF.
  Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi, Anna Lupembe.
  Baadhi ya watoto waliotembelea banda la NSSF wakipata zawadi ya madaftari kutoka kwa Ofisa wa NSSF, Silvia Mashuda.
  Wateja wa Sh,irika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakisubiri kupata huduma katika banda la shirika hilo katika viwanja vya Sabasaba.

  Na Mwandishi Wetu


  NAIBU Waziri wa Fedha, Janet Mbene amesema lengo la kuzitembelea taasisi za kifedha na nyingine zilizoko chini ya Wizara hiyo ni kutaka kujua mafanikio na changamoto za taasisi hizo.


  Mbene amesema hayo wakati alipotembelea banda la maonesho la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.


  Alisema baada ya kutembelea na kuangalia banda hilo, alibaini kuwa changamoto kubwa ni fedha ambazo zinahitajika kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za mfuko huo, kwa kutumia teknolojia ya kisasa.


  Mbene alisema baada ya kubaini hayo serikali inao wajibu wa kutafuta kila njia lengo likiwa ni kuzipatia ufumbuzi wake.

  Unajua hivi sasa kila kazi zote zinafanywa kwa kutumia mfumo wa teknolojia ambao kwa kawaida ni mahususi katika kurahisisha kazi na kuifanya iwe bora zaidi”alisema Mbene.


  Mbene alisema ukiachilia mbali uhitaji wa teknolojia bado pia wataalam ambao wangetumika kusimamia mifumo hiyo hawatoshi, serikali kwa kuliona hilo itahikikisha kuona wanapatikana.


  Akizungumzia kuhusu mafanikio ya Mfuko wa NSSF, Eunice Chiume alisema mfuko huo hivi sasa umepiga hatua katika kuwafikishia huduma mbalimbali wateja wake kila kona ya nchi na nje.


  Aidha, Mfuko huo katika kuboresha maisha ya wafanyakazi wake inatoa mikopo, hata hivyo masharti ya kupata mkopo huo ni lazima muombaji awe mwanachama wa SACCOS.


  Mbene aliongeza kuwa SACCOS itawajibika kupokea maombi iwapo SACCOS hiyo imesajiliwa kikamilifu na imeendesha shughuli zake kwa kipindi cha miaka mitatu na si chini ya hapo.

older | 1 | .... | 184 | 185 | (Page 186) | 187 | 188 | .... | 3270 | newer