Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1857 | 1858 | (Page 1859) | 1860 | 1861 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Pichani ni dereva wa gari la mwendokasi la DARTS  namba za usajili T.124 DGW akihojiwa baada ya kufanya kosa la kupita taa nyekundu eneo la Kibo barabara ya Morogoro jijini Dar es salaam leo asubuhi wakati akitokea Kimara kuelekea Kivukoni. Baada ya kukamatwa  hatua za kufikishwa mahakamani zinaendelea.
  Mkuu wa usalama barabarani kanda maalum yaDar es salaam ACP Awadhi Haji  amesema baada ya kumkamata dereva huyo kwamba baadhi ya madereva wa magari hayo wamekuwa wakifanya makosa ya usalama barabarani mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupita taa nyekundu, kutosimama kwenye vivuko vya waenda kwa miguu na kadhalika wakidhani kuwa wao hawawezi kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
  "Hivyo naelekeza kuwa madereva hao wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali kama madereva wengine pindi wanapobainika kuvunja sheria za barabani" ameamuru ACP Awadhi Haji ambaye huwa hana masikhara awapo kazini.


  0 0
  0 0  Kumpigia kura KARIM MICHUZI ashinde tuma SMS neno V10 kwenda namba 0746 520 610

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bw.Bernard Hezron Konga
  0 0

  Na Ahmed Ally .

  Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imetupilia mbali ombi la bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba la kutaka kuzuia mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika August 13 mwaka huu. 

  Hakimu Mkazi amesema haitokua busara kuzuia mkutano huo kwani Agenda za mkutano  hazionyeshi kama kuna agenda ya mabadiliko ya mfumo kama ambavyo wadhamini wanadai. 

  Pia Mahakama imesema sio busara kuzuia Mkutano kwani tayari baadhi wanachama wa Simba wanaoishi mikoani wameshawasili hivyo kuzuia mkutano huo ni kuwatia hasara, lakini pia uongozi wa klabu umeshafanya maandalizi.

  Na mwisho kabisa mahakama imesema kwa kuwa mlalamikaji ambae ni Mzee Kilomoni ana haki ya kuhudhuria Mkutano Mkuu ni vema akaenda kwenye mkutano huo akaeleza maoni yake.

  0 0


  .
  Na Honorius Mpangala.

  Ni katika utawala wa Rais wa awamu ya tano Dodoma imerejesha Hadhi yake kama makao makuu ya nchi tangu ilivyokuwa hivyo kwa zama za Mwalimu J. K. Nyerere. Hadhi ya Dodoma inamfanya kila mmoja atamani kuishi Dodoma.

  Ni katika utawala wa awamu ya tano ambapo uchaguzi wa TFF unawaingiza viongozi wapya madarakani. Hakuna asiyeijua kasi ya kiutendaji pamoja na heshima ya ofisi za umma zilivyo kwa sasa.

  Viongozi watakao chaguliwa moja kwa moja wataingia madarakani kwa kutambua kiongozi mkuu wa nchi ni nani. Hakuna kiongozi ambaye atakuja kufanya tofauti katika utawala huu kama ikitazamwa viongozi watangulizi hadi niandikapo wako rumande.

  Wanataka kutufikisha sehemu fulani wanatuhaidi mabadiliko lakini kitu pekee ambacho tutapaswa kujiandaa nacho ni pale tutakapo ambiwa mambo yanayohusu fedha lazima yakaguliwe na CAG.Hili ni jambo la kujipanga nalo na kwa viongozi watakao ingia madarakani naamini lazima akili yao itakuwa imesoma alama za nyakati na kutambua mahitaji yaliyopo sasa.

  Ikiwa kama shirikisho linahitaji mchango wa serikali katika kufanikisha Yale matarajio basi wasisite kutoa ushirikiano pia itakapofika wakati wa kuhitaji ukaguzi wa kiofisi.Miongoni mwa mambo yanayoendelea katika shirikisho letu ni upatikanaji watu mwenye weredi katika kusukuma maendeleo ya soka letu.

  Wakati Rais mstaafu Bemjamini William Mkapa anatoweka madarakani mwaka 2005 alicha Uwanja wa taifa. Wakati Rais mstaafu pia Jakaya Kikwete anatoweka madarakani mwaka 2015 aliacha utaratibu wa Kocha mkuu wa timu ya taifa akilipwa mshahara na serikali. 

  Awamu ya nne licha kufanikisha kwa kuzisaidia timu zetu za taifa kwa kuwaleta walimu toka nje ya Tanzania lakini tulikosa watu wa kuwachunguza watu tuliowapa mamlaka ya kusimamia vyama hivyo vya Michezo.

  Alikuja kocha wa ngumi toka nchi ya Cuba hadi Leo hakuna mwenye majibu yaliyonyooka aliondoka vipi. Sio kocha wa ngumi tu bali hata kocha wa Netball alikuja hapa nchini lakini Uswahili wa viongozi wetu hakuna ambaye alielewa.

  Awamu hii Rais kafanikiwa kumshawishi mfalme wa Morocco kuweza kufanikisha upatikanaji wa uwanja wa Michezo pale Dodoma. Ni kitu kikubwa sana kufanyika ambacho kitaifanya Dodoma kujikuta ikimpa heshima ya juu Rais wetu kwa maamuzi yake na Uzalendo wake kwa taifa lake.

  Katika kipindi hiki ndipo niligundua Waziri wa wizara ya Michezo anawasiliana na watu wa FIFA na kuwaeleza kila wafanyalo kwa shirikisho la Mpira la Tanzania ni lazima serikali ifahamishwe. Hali hii itapelekea kufanikisha mambo mengi yaliyokuwa yanaelekeza katika utekelezaji wa miradi ya TFF.  Kwa viongozi watakao ingia madarakani watakuwa na uwepesi wa kazi kutokana na kuzisoma nyakati na kujua mahitaji na kiu ya watanzania katika msuala ya Michezo. Nina hakika kwa kiongozi yeyote atakaye fanikiwa kuingia katika uongozi atakuwa amesoma nyakati vyema.Utendaji wa shirikisho utakuwa na ufanisi sana.

  Soka letu linahitaji MTU amayeweza kujitoa kwaajili ya watu ili kufanikisha ndoto zao. Tunahitaji MTU anatakaye tambua uwezo na kipaji cha vijana walioko kwenye mfumo wa kimakuzi katika soka. Hadi sasa ilikuwa inashangaza vijana waliokuwa wamepelekwa katika vituo vya kulelewa kisoka kutotumika. Wako waliopelekwa Nchi ni Ghana na mwingine pale Dakar Senegal lakini hakuna anayeonekana kuwakumbuka vijana wale.

  Ni kama tunapiga konzi kwenye kinyago na hatimaye tunaumia wenyewe. Tunahitaji atakaye tujuza kuwa hiki ni kinyago na tuachane nacho kukipiga makonzi. Shirikisho lenye uthubutu katika utendaji ndio mafanikio ya soka letu.Natamani kuona serikali ikiwa na mamlaka ya kushirikiana na TFF katika kufanikisha kila jambo. Kwa taasisi iliyo chini ya serikali ingekuwa safi kuona mkaguzi wa hesabu za serikali akifanya kazi katika nyanja mbalimbali katika masuala ya Michezo.

  Hoja ya kusambaza mpira nchi nzima itaweza kusaidia hata kufanya hata baadhi ya maeneo yanayo onekana hayana soka basi watacheza soka. Kuto kuwa na soka ni hali ya mikoa kutokuwa vilabu kwa daraja la kwanza la pili hata ligi kuu.

  Rais wa TFF unayekuja pamoja na wajumbe wako jambo pekee la kuweka kichwani ni kwamba Rais Wa jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli anakusubili mfanye kazi mfanikishe ujenzi wa Uwanja wa Michezo pale Dodoma.

  0628994409

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Ulyankulu waache kujihusisha na matukio ya uhalifu.

  Ametoa onyo hilo leo mchana (Ijumaa, Agosti 11, 2017) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Ulyankulu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya VETA, wilayani Kaliua mkoani Tabora.

  Amesema matukio ya ujambazi, mauaji na umiliki wa silaha yanayofanyika kwenye tarafa hiyo ni mengi ikilinganishwa hali ilivyo kwenye maeneo mengine ya mkoa huo.

  "Taarifa nilizonazo zinaonyesha katika kipindi cha miaka miwili kumekuwa na matukio ya mauaji 35, ujambazi matukio 12, umiliki wa silaha nao unatisha. Yamekamatwa magobole 11, bunduki aina ya SMG saba na Mark Four mbili."

  "Tulikamata pia risasi 714 za SMG zikiwa kwenye ndoo za mafuta na juu yake wamepaka mafuta ya mawese. Pia risasi mbili za Mark Four zilikamatwa," amesema Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu amewataka wakazi hao ambao baadhi yao wamepewa uraia na wengine bado ni wakimbizi waonyane wanapokutana kwenye vikao vyao kwa sababu matendo yao yanaikwaza Serikali ambayo iliamua kuwapa hifadhi. "Ni vema mkikutana kwenye vikao vyenu muelezane na kuonyana," amesema Waziri Mkuu.

  "Ninawasihi matukio haya myadhibiti la sivyo mtaharibu nia njema iliyoleta uwepo wenu.  Bunduki na risasi zinakuja kufanya nini wakati nyie mko maeneo salama? Mauaji ya nini?  Kama kuna tatizo limekupata, muone mwenyekiti wa kijiji,  atakusaidia," alisisitiza.

  Alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi yao ambao wamegeuka mawakala na wameanza kuwaleta ndugu zao bila kufuata utaratibu. "Hatuzuii mtu kutembelewa na ndugu yake, lakini ni lazima mfuate taratibu. Tunataka tudumishe amani iliyopo nchini lakini pia tudumishe urafiki wa nchi zetu mbili za Burundi na Tanzania," aliongeza.

  Mapema, Mbunge wa jimbo la Ulyankulu, Bw. John Kadutu alimuomba Waziri Mkuu afuatilie suala la upatikanaji wa maji kwenye tarafa hiyo, pia aliomba wasaidiwe ili kata tatu za Kanindo, Igombenkulu na Milambo ziwezeshwe kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo hilo zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Ridhiwani, amesema kuwa atawapatia washindi wa pili wa michuano hiyo pikipiki ya miguu miwili na jezi kwa timu zote tatu za juu.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga,ambaye pia ndio muaandaji wa mashindano hayo ametoa zawadi ya pikipiki ya Toyo ya miguu mitatu kwa mshindi wa kwanza ili itumike kwa shughuli za kuwaingizia kipato kwa vijana.

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na mchezaji anayeshiriki katika mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akitoa vifaa kwa washiriki wa mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akitoa vifaa kwa washiriki wa mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa tatu kutoka kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo wa pili toka kulia Majid Mwanga wakiangalia mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akionyesha moja ya jezi zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete.

  0 0

  Na Vero Ignatus.Arusha

  Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .

  Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho ).

  Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa serekali Penina Joakim amesema kuwa Mnamo May 18 katika hotel ya Skyway iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .

  Wakili Penina alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria .

  Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Nestory Barro alisema dhamana ipo wazi iwapo wathamini watakithi vigezo vinavyotakiwa na mahakama hiyo.
  Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akiwa nje ya mahakama mara baada ya kuachiwa kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Akizungumza na mwenyekiti wa CCM katika kata ya Sambasha Lesion Letionoki Njoki.Picha na Vero Ignatus Blog.   0 0

  Mjane wa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Mama Graca Machel akihutubia wakati wa kufunga Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika
  Mjane wa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Mama Graca Machel akihutubia wakati wa kufunga Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika
  Mjane wa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Mama Graca Machel akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Zamani Nchini ,Jaji Joseph Sinde Warioba kabla ya kufunga Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika
  Baadhi ya Wanawake kutoka nchi Mbalimbali Walioshiriki Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika
  Waziri Mkuu Mstaafu ,Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza jambo na Mwanaharakati wa siku nyingi Getrude Mongela wakati wa Kufunga Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika 
  Baadhi ya Wanawake kutoka nchi Mbalimbali Walioshiriki Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika

  0 0

    Mshindi  wa shindano la Miss Grand Tanzania, Batul Mohamed akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kazi atakazozifanya za kijamii katika kipindi cha mwaka mmoja na matarajio yake katika kuwania taji la Dunia. Wengine pichani ni Mrembo wa Dunia  wa shindano la Miss Grand International 2016,Ariska Mchammed (katikati) pamoja na Makamu wa Rais wa Shindano la Miss Grand International,Teresa Chaivisut. 
    Mrembo wa Dunia  wa shindano la Miss Grand International 2016,Ariska Mchammed akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kazi za Missgrand International hapa nchini.
    Muandaaji wa Shindano la Miss Grand Intarnational hapa nchini, Happyness O'shen  akizungumza juu ya Safari ya mrembo huyo kwenda Thailand.

  0 0

  Uhuru Kenyatta hatimaye ametangazwa mshindi wa kiti cha Urais nchini Kenya, jambo ambalo limehitimisha siku kadhaa za sintofahamu kufuatia uchaguzi mkuu uliojaa ushindani mkubwa.
  Rais mteule Uhuru alitangazwa mshindi kwa kujipatia jumla ya kura 8, 203,290  au asilimia 54.27 na Mwenyekiti wa Tume y Uchaguzi Wafura Chebukati wakati mshindani wake wa karibu  Raila Odinga wa  NASA akimfuatia kwa kura 6, 762, 224 ambazo ni asilimia 44.74% siku ya Ijumaa Agosti 11, ikiwa ni siku tatu baada ya kura kupigwa.
   "Naomba kumtangaza Uhuru Kenyatta kuwa Rais mteule na William Ruto Naibu Rais Mteule," alisema  Chebukati huku akishangiliwa na wafuasi wa washindi hao.
  Uhuru alijizolea asilimia 25 ya kura katika majimbo 35 ambapo Raila alifanya hivyo katika majimbo 29.
  Chebukati alisema jumla ya  Wakenya 15,073,662 walipiga kura ikiwa ni sawa na asilimia 71.91 ya waliojiandikisha.

  0 0  0 0

  Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF umehitimishwa kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia  (kulia) kushinda kwa jumla ya kura 95 na kuwabwaga wapinzani wake.
  Uchaguzi huo umefanyika leo mkoani Dodoma ukiwa wa amani kwa wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na wagombea wenyewe.

  Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli akitangaza matokeo hayo ambapo alimtangaza Wallace Karia kama mshindi wa kinyang'anyiro kwa kura 95 kati ya kura 127 zilizopigwa.

  Wagombea Urais wa TFF na kura zao ni: Emmanuel Kimbe (1). Frederick Mwakalebela (3), Imani Madega (8), Richard Shija (9)  Ally Mayai  (9) na Wallace Karia  (95).

  Kuuli ametangaza kuwa, katika nafasi ya makamu wa Rais, Michael Richard Wambura (kushoto) ameshinda nafasi hiyo kwa kura 85.

  Kwa upande wa wajumbe wa mkutano mkuu kumekuwa na maingizo mapya kutoka kanda mbalimbali za nchini kama ifuatavyo:
  Zone 1: Saloum Chama 
  Zone 2: Vedastus Lufano 
  Zone 3: Mbasha Matutu 
  Zone 4: Sarah Chao 
  Zone 5: Issa Bukuku 
            Zone 6: Kenneth Pesambili 
  Zone 7: Elias Mwanjala 
  Zone 8: James Mhagama 
  Zone 9: Dunstan Mkundi 
                                                      Zone 10: Mohamed Aden 
                                                   Zone 11: Francis Ndulane 
                                                Zone 12: Khalid Abdallah 
                                                   Zone 13: Lameck Nyambaya

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pia Kaimu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Ali Abeid Karume wakati alipowasili katika ukaguzi wa maendeleo ya Kiwanda cha Sukari cha Mahonda na kupata maelezo mbali mbali kutoka kwa Wasimamizi wa Kiwanda hicho Kampuni ya ETG  alipofanya ziara katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja mradi  katika Kanda ya Afrika Mashariki katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Nd,Tushar Mehta  alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja wa Mawasiliano katika Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Fatma Salum Ali (kulia) wa  Kampuni ya ETG inayoendesha Kiwanda hicho wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa  Meneja mradi  katika Kanda ya Afrika Mashariki katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Ndg. Tushar Mehta  (wa pili kushoto) alipofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mkuu wa mradi   katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Bw. Mahesh  Patel (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Mohamed.
  Picha na IKULU

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha zoezi la kutoa maeneo mapya ya utawala hadi itakapotangazwa vinginevyo. 

  "Kwa sasa tumesitisha kutoa maeneo mapya ya utawala ili tuimarishe kwanza yale ya awali. Tunaimarisha kwanza miundombinu ya majengo ya ofisi,  nyumba za watumishi kwenye wilaya na Halmashauri mpya, zikitengamaa tutafanya maamuzi mapya, " alisema. 

  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa,  Agosti 11, 2017) katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Ulyankulu na Kaliua, wilayani Kaliua mkoani Tabora.  
  Alikuwa akijibu maombi ya wabunge wa majimbo ya Ulyankulu na Kaliua ambao walisema kuna haja ya kuigawa wilaya ya Kaliua ili kusogeza huduma kwa wananchi waishio kwenye kata zilizo mbali na tarafa. 

  Akizungumzia kuhusu migogoro baina ya wanavijiji na maeneo ya hifadhi, Waziri Mkuu alisema Serikali bado inafanya uhakiki wa mipaka katika maeneo ya hifadhi na ikikamilisha zoezi hilo itatoa taarifa. 

  Ili kuharakisha zoezi hilo,  Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na maeneo ya hifadhi, wasifanye upanuzi wowote hadi zoezi la kuhakiki mipaka ya hifadhi litakapokamilika.

  "Tumeamua kuweka beacons katika maeneo yote ya hifadhi ili kubaini mipaka imepita wapi.  Wananchi mkiwaona watu wa hifadhi wanapita huko msigombane nao. Ni hatua ya awali ya kubaini maeneo ya mipaka. "

  "Niwasihi wanavijiji wote, vijiji vilivyomo kwenye hifadhi visiendelee kupanua maeneo yake. Mbaki hivyo hivyo hadi Serikali itakapoamua vinginevyo, " alisema.  
  Alisema zoezi la uhakiki wa mipaka ya hifadhi likikamilika na taarifa kutolewa, Serikali itatoa uamuzi juu ya vijiji vilivyobainika kuwa ndani ya maeneo ya Hifadhi. 
  Akiwa Kaliua, Waziri Mkuu alielezwa na Mbunge wa jimbo hilo,  Mheshimiwa Magdalena Sakaya kuwa wananchi wanashindwa kujenga makazi ya kudumu katika maeneo waliyopo kwa sababu wanatishiwa kwamba wapo hifadhini.  
  Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya mapitio na ikilazimu itabidi ifanye marekebisho ya Sheria inayohusu Misitu ya Hifadhi pamoja na Sheria inayohusu masula ya Wakimbizi. 

  0 0


  Na Benny Mwaipaja, Songwe/Mbeya

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewasimamisha kazi watumishi wanne wa Idara ya Forodha, katika Mpaka wa Tanzania na Zambia, Mjini Tunduma, ili kupisha uchunguzi wa kudaiwa kuhusika na upotevu wa lakiri 10 zinazotumika kufunga kwenye shehena ya mizigo inayopita mpakati hapo kutoka nje ya nchi.

  Mpango amewataja watumishi hao kuwa ni pamoja na Harrison Mwampashi, John Makorere, Stephene Josia na Frank Kessy na kuviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama mpakani hapo viwahoji huku wakiwa wamesimamishwa kazi.

  Watumishi hao wanadaiwa kuiba lakiri hizo kumi kutoka ofisi za TRA-Tunduma wanakofanyiakazi, ambapo 4 kati ya hizo lakiri zilikutwa zimefungwa kwenye mizigo ya malori yanayoshikiliwa katika mpaka huo baada ya uchunguzi kufanyika huku malori mengine 5 yakizuiwa baada ya kuonekana lakiri zao zimechezewa.

  Taarifa zinasema kuwa baada ya uchunguzi, mawakala ama wamiliki wa malori hayo wamedai walipewa lakiri hizo na watuhumiwa na kwamba uchunguzi zaidi umebaini kuwa kiwango cha mizigo kilichomo kwenye makontena yaliyobeba mizigo ya magogo na kufungwa lakiri hizo za wizi hakilingani na idadi ya mizigo iliyoko kwenye nyaraka jambo linaloashiria kuwa wanazitumia lakiri hizo kudanganya idadi na uzito wa mizigo yao ili kukwepa ushuru na kodi mbalimbali za Serikali.

  “Hakuna kitu muhimu kama uadilifu kwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato na hatutasita wala hatutamwonei aibu mtu yeyote, tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria ili kulinda fedha za umma” alionya Dkt. Mpango

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Katibu wa Jumuiya ya madola Mhe. Patricia Scotland amefanya mazungumzo na Naibu Waziri Ofisi ya Mkamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga kuhusu suala zima la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira huku eneo la mabadiliko ya Tabianchi likipewa kipaumbele.

  Katika mazungumzo hayo Bi. Scotland alisema kuwa kuna kila sababu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuelewa zaidi suala zima la mabadiliko ya tabianchi akieleza kuwa wanasayansi wanasema ifikapo mwaka 2050 dunia inaweza kabisa kuepukana na suala la athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi endapo itawezekana kulifanyia kazi kwa pamoja.

  Kwa upande wake Naibu Waziri Mpina alieleza kuwa Tanzania imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali na jitihada zimefanyika katika kuwezesha jamii kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

  Alisema serikali inatekeleza Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012) ambapo sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nishati zimeandaa na zinatekeleza mpango kazi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.
  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Nje ya Ofisi ya Makamu wa Rais Baada ya kumaliza mkutano ulohusu suala zima la usimamizi na Utunzaji wa Mazingira.
  Mhe. Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza AshaRose Migiro, akizungumza baada ya kikao na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri Mpina na wataalaam kuhusu masuala ya Mazingira, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
  Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na wajumbe walioshiriki mkutano wa masuala ya hifadhi ya mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

    Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Mmoja wa Madereva wa Daladala ambao hufanya safari zao kituo cha River Side kwenda Makoka mara baada ya kuchonga barabara hiyo kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo .
    Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, akizungumza na Dereva wa Bodaboda katika barabara ya Riverside Makoka mara baada ya kukagua barabara hiyo iliyochongwa kwa fedha za Mfuko wa jimbo
   Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na  Wakazi wa eneo la Ubungo Makoka mara alipo fika katika kituo cha Daladala eneo la Riverside kupata maoni yao nini kifanyike kuboresha barabara hiyo ili iweze kupitika muda wote 
  Mjumbe wa shina Makoka Phinias  akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea  juu ya barabara ya Makoka River side   mara baada ya kuchonga barabara hiyo kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo 

older | 1 | .... | 1857 | 1858 | (Page 1859) | 1860 | 1861 | .... | 3272 | newer