Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

HALMASHAURI YA MERU YAONGOZA KWA USAFI WA MAZINGIRA KATI YA HALMASHAURI 185 ZA TANZANIA.

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, akizungumza na waandishi wakati akitangaza matokeo ya mashindano ya afya na Usafi wa Mazingira leo jijini leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi.

 Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya Meru uliypo mkoani Arusha inaongoza kwa asilimia 96  kwa usafi wa ujenzi wa na matumizi ya vyoo bora katika kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iliyohusisha halmashauri 185.

Hayo ameyasema leo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitangaza matokeo ya mashindano ya afya na Usafi wa Mazingira leo jijini, amesema kuwa halmashauri ya Meru imeweza kufanya vizuri usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora pamoja na kuwa na sehemu ya kunawa mikono.

Amesema nafasi ya pili kwa  usafi wa mazingira na matumizi bora ya vyoo ni Halmashauri ya Njombe kwa asilimia 95.1 ikifuatiwa na Halmashauri ya Makete kwa asilimia 80.4.

Waziri Ummy amesema  katika kutekeleza kampeni hiyo  kwa upande wa kijiji bora na mtaa kwa usafi kwa vilivyoshindaniwa ni 80 , kijiji cha Kanikale kinaongoza  wilayanii Njombe kimeongoza asilimia 95.8 , nafasi ya pili imechukuliwa kijiji cha Nambala wilaya Meru kwa asilimia 95.3 na kijiji cha tatu ni Lyalalo kwa asilimia 93.5 wilayani Njombe.

Amesema majiji na Manispaa ambazo zimefanya kampeni  ya  usafi wa mazingira, vyoo bora pamoja na udhibiti wa taka ngumu kwa Manispaa ni Manispaa ya Moshi kwa asilimia 78.5 mshindi wa Pili Jiji la Arusha kwa 78.1 ikifuatiwa na Manispaa ya Iringa kwa asilimia 67.2 

Waziri Ummy amesema kampeni ya 2018 wataongeza ofisi za serikali, shule za msingi na sekondari kushindanisha katika usafi wa mazingira na vyoo bora.

MANAHODHA WATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI WA MAKONGO

0
0

Nahodha wa Mchenga Mohamed Yusuph (kushoto) pamoja na Nahodha wa TMT (kulia) wakikabidhi mipira kwa viongozi wa timu ya mpira wa kikapu ya Sekondari ya Makongo walipowatembelea jana na kuwahamisha kushiriki michezo mashuleni na kuirejesha heshima ya mchezo wa mpira wa kikapu

Na Zainab Nyamka, GlobU ya Jamii.

Katika kukuza na kurejesha heshima ya mpira wa kikapu nchini, waandaaji wa michuano ya Sprite Bball Kings 2017 wamewahamasisha wanafunzi kuupenda na kuuthamini mchezo huo kwani elimu na michezo inaenda sambamba.

Hayo yamesemwa na Manahodha wa timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings inayoendelea wikiendi hii wakati akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari Makongo.

Nahodha wa timu ya Mchenga Bball Stars, Mohamed Yusuph amesema kuwa masomo na elimu yanaenda sambamba hivyo wanafunzi wasiwe waoga kuonesha vipaji vyao mbele ya jamii kwani wanaweza kupata nafasi za masomo kupitia mchezo wa mpira wa kikapu.

"Wanafunzi wanatakiwa kuonesha vipaji vyao kwani wasione kama watashindwa kufanya vizuri katika masomo yao, kwa ufupi elimu na michezo vinaenda sambamba," amesema Yusuph.

Aidha Yusuph amewataka wanafunzi kujiunga na timu za mpira wa kikapu kwa ajili ya kuweza kucheza mchezo huo na zaidi katika timu yao ya Mchenga kuna timu za vijana kuanzia miaka 13 na wengine wapo katika timu za taifa.

Kwa upande wa Nahodha TMT, Isihaka Masoud amewataka wanafunzi kuithamin na kuipenda michezo kwani michezo ni afya na wakipata wasaa wa kupumzika wasiache kujumuika na wenzao katika mchezo wowote.

Baada ya kumaliza kuongea na wanafunzi, manahodha hao walitoa zawadi ya mipira kutoka Sprite na t-shirt kwa uongozi wa timu ya mpira wa kikapu ikiwa ni katika kuongeza chachu ya kucheza mpira wa kikapu na kurejesha heshima ya mchezo huo.

Nahodha wa timu ya Mpira wa Kikapu ya Mchenga Mohamed Yusuph akizungumza na wanafunzi wa Sekondari Makongo na kuwahamisha kujikita katika mchezo wa mpira wa kikapu na zaidi elimu na michezo vinaenda sambamba na baadae kuwakabidhi zawadi mipira na t-shirt kutoka Sprite.

Nahodha wa timu ya Mpira wa Kikapu ya Mchenga Mohamed Yusuph akiwa na mwanafunzi wa Makongo akijaribu kumtoka na mpira.

MAGARI YALIYOTELEKEZWA BANDARINI YATAIFISHWA WATUHUMIWA WAHUKUMIWA.

0
0

Baadhi ya Magari ambayo yalitelekezwa katika bandari ya jiji la Dar es Salaam na  baadae yalikutwa na Rais Magufuli kwenye makontena, alipofanya ziara bandarini.

Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.
WATUHUMIWA waliongiza magari wakidai ni Nguo wahukumiwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyabiashara wawili kulipa faini ya Sh milioni 100 au kufungwa  jela miaka  mitatu baada ya kukiri kuingiza magari matatu nchini na kujifanya kuwa ni mitumba.

 Kitendo hicho  kiliisababishia serikali hasara ya Sh milioni 190.9.
Watuhumiwa hao, ambao ni  Sultan Ibrahim na Ramadhani Hamisi, Raia wa Uganda,  wamehukumiwa adhabu hiyo na Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Akisoma hukumu hiyo, Mkeha amesema, licha ya ushirikiano waliotoa washitakiwa ikiwemo kuomba kutaifishwa kwa magari hayo, ni matakwa ya sheria kwamba mali hizo zitaifishwe na kwamba inazingatia thamani ya magari  hayo ambayo yamevuka kodi iliyotakiwa kupata serikali.

Amesema, kila mshtakiwa anatakiwa kulipa fidia ya milioni 50 au kwenda jela miaka mitatu na magari yote yataifishwe  ili iwe onyo kwa yoyote mwingine mwenye nia ya kukwepa kodi kwa namna hiyo ya washtakiwa.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, hakimu Mkeha aliuuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ambapo, Wakili  wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameiomba mahakama kutoa adhabu kwa kuzingatia kifungu namba 203 (b) cha Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 ambayo  inataka bidhaa walizokutwa nazo watuhumiwa kutaifishwa.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Jebra Kambore aliiomba mahakama kuwaonea huruma watuhumiwa hao kwani wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kuandika barua kwa serikali na kukubali magari hayo kutaifishwa.

Aliongeza, thamani ya magari hayo ni milioni 287,777,536 fedha ambazo ni zaidi ya kodi ambayo serikali ilitakiwa kupata. 

Mapema baada ya watuhumiwa hao kukiri mashtaka, walisomewa Maelezo ya awali ambapo ilidaiwa, Desemba Mosi, 2016 na Machi mwaka huu, washitakiwa hao na wengine wanaoishi Uingereza, walikubaliana kuingiza magari nchini.

Alidai  Oktoba 13, mwaka jana, kupitia nyaraka za kuingiza mizigo bandarini, walishirikiana kuingiza kontena namba 3049836 ambayo ilibeba magari matatu aina ya Range Rover Sports, Range Rover Evock na Range Rover Vogue.
Aidha wanadiwa kutoa taarifa ya uongo kupitia nyaraka hizo za kuingizia mizigo bandarini kwamba kontena hilo lilibeba nguo za mitumba, viatu na magodoro kwa nia ya kukwepa kodi ambayo thamani Mali hizo ilikuwa  ndogo ukilinganisha na thamani halisi ya magari waliyobeba.

Nyantori alidai kutokana na uongo walioufanya, maofisa wa forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walikadiria kodi ya chini ya S milioni 31.5 badala ya kodi sahihi iliyopaswa kul

Alieleza baadae, ilibainika kuwa kontena hilo lilibeba magari yaliyokuwa yamefichwa ndani ya mitumba ya viatu, magodoro na nguo.

‘’Mshitakiwa Sultan alipekuliwa nyumbani kwake   na kukutwa na funguo tatu za magari hayo.

Awali ilidaiwa, kati ya Desemba Mosi, mwaka jana na Machi 4, mwaka huu, Makao Makuu ya Bandari wilayani Temeke, washitakiwa walitengeneza nyaraka za uongo kuonesha kuwa kontena hilo lilikuwa na mitumba ambayo ni nguo, viatu na magodoro na kuficha ndani yake magari hayo matatu.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kuficha utambuzi wa bidhaa waliyokuwa wakiingiza na kusababisha hasara ya Sh milioni 190.9.

IGP AFANYA KIKAO NA MAOFISA WA MAKAO MAKUU NA WAKUU WA VIKOSI NA VYUO

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akitoa maelekezo kwa  Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini katika kikao kazi cha maelekezo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania salama isiyo na uhalifu.
  Mkuu wa Utawala wa Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Leonard Paulo, akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kikao kazi cha Inspekta Jenerali wa polisi nchini IGP Simon Sirro na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania salama isiyo na uhalifu.
 
Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Zarau Mpangule, akitoa mada wakati wa kikao kazi cha Inspekta Jenerali wa polisi nchini IGP Simon Sirro na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania isiyo na uhalifu. 
Picha na Jeshi La Polisi.

PROFESA MBARAWA ATOA MWEZI MMOJA KWA WAFANYABIAASHARA JNIA.

0
0
 Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akizungumza na wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (Kulia), wakati alipokagua sehemu ya kuingilia abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa Mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) kulipa kodi ya Majengo kama mikataba yao inavyolekeza.

Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo leo wakati alipokutana na wafanyabiashara hao ili kujadili changamoto mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzitatua ili kuendelea kutoa huduma bora katika uwanja huo.

“Kulipa kodi za majengo hapa ni suala la lazima, hivyo ifikapo Septemba mwishoni nataka kuona wafanyabiaashara wote mmeshalipa kodi ya pango, makusanyo haya ni muhimu kwetu ili tuendelee na hatua nyingine za uboreshaji wa viwanja vya ndege na huduma nyinginezo.” Amesisitiza Profesa Mbarawa.

RPC SHANNA: TUTATAIFISHA MALI ZA WANAOFANYA BIASHARA YA KUSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU KUJA NCHINI.

0
0

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani.
KAMANDA wa polisi mkoani Pwani,(ACP) Jonathan Shanna (Pichani Kulia), amesema kuanzia sasa watataifisha mali zote za watu wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Aidha amewatahadhalisha wale wanaotoa vyombo vyao vya majini na nchi kavu kusafirisha wahamiaji hao  kwani navyo vitataifishwa .

Akizungumzia hatua walizozichukua kwa wahamiaji haramu 72 waliokamatwa mapema wiki hii,kamanda Shanna alisema kushiriki kwenye biashara hiyo ni kosa la kubwa la kijinai.

Amesema wanaojihusisha kusaidia na kuwawezesha kufika wahamiaji haramu watawachunguza mali mbalimbali walionazo kama imetokana na utakatishaji fedha na endapo itabainika imetokana na biashara hiyo zitafilisiwa.

Kamanda Shanna alibainisha,wataiomba mahakama kutaifisha mali zote za wale watakaobainika kuhusika kupata mali hizo na fedha na biashara haramu.

Amesema sheria ipo wazi inasema watu hao wapewe kifungo ama kupigwa faini hivyo itapendeza na itafurahisha jeshi la polisi kama watakuwa wanapewa adhabu zote na kufungwa .

Kamanda Shanna ,alisema taarifa ikifika makwao kuwa wanafungwa na kupewa adhabu kali ndipo wataacha kuingia nchini kwani watajua Tanzania sio mahala pa mchezo wala kukimbilia.

“Hii kuwakamata kuwapiga faini na kuwarudisha kwao ndio maana wanafanya mchezo mchezo kukimbilia huku,ukiwapiga faini wanakwenda wanarudi ni mchezo wa kuigiza”alisema .

Kamanda Shanna alielezea kwamba,Tanzania ina sheria zake endapo sheria zitawabana wahamiaji hao na kukoma kugeuza nchi kuwa lango lao la kupita kwenda nchi jirani ikiwemo Afrika ya kusini.

Hata hivyo ,kamanda huyo alisema wahamiaji waliokamatwa wameshawafikisha ofisi ya uhamiaji mkoani hapo na watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.


Jeshi hilo,linaendelea kudhibiti wahamiaji haramu ili kupungua wimbi kubwa linaloingia kupitia njia za panya mkoani hapo hasa bandari bubu 18 zilizopo Bagamoyo .

Pamoja na hilo,Kamanda Shanna alisema wanafanya oparesheni kusaka wahalifu mbalimbali ,zoezi ambalo ni endelevu.

BENKI KUU YA TANZANIA YASAJILI KAMPUNI YA KUTOA MIKOPO YA NYUMBA

0
0

Benki Kuu ya Tanzania imetoa leseni kwa kampuni mpya ya kutoa mikopo ya nyumba inayoitwa “First Housing Company (Tanzania) Limited”.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Sera na Leseni katika Kurugenzi ya Usimamizi wa Mabenki imeeleza kwamba leseni hiyo inaipa nafasi kampuni hiyo mpya kufanya biashara ya kutoa mikopo ya nyumba nchini. Makao makuu ya kampuni hiyo ni jijini Dar es Salaam. 

Hii ni mara ya kwanza kwa Benki Kuu kutoa leseni kwa kampuni ya mikopo ya nyumba nchini. 

Benki Kuu pia inatoa leseni na kusimamia benki, taasisi za fedha, maduka ya kubadilisha fedha, kampuni za karadha na zinazotunza kumbukumbu za ukopaji za wananchi (credit reference bureaus).

HASHEEM THABEET AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI

0
0


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mtanzania anayecheza mchezo wa kikapu nje ya nchi, Hasheem Thabeet (kushoto), walipokutana kwa ajili ya Maandalizi ya Tamasha la Usalama Barabarani, linalotarajiwa kufanyika kesho Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mtanzania anayecheza mchezo wa kikapu nje ya nchi. Hasheem Thabeet (wapili kushoto), baada ya mazungumzo ya Maandalizi ya Tamasha la Usalama Barabarani, linalotarajiwa kufanyika kesho Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.Wengine ni ujumbe ulioongozana na mchezaji huyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKLALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MAKONDA AFUNGUA MKUTANO WA USAJILI MUHIMU WA MATUKIO YA BINADAMU KWA NJIA YA TEHAMA

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na katika ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Afisa Mtendaji  Mkuu (RITA) Emmy Hudson akizungumza na waandishi  wa habari katika mkutano wa viongozi wa gazi ya Mkoa na Wilaya kuhusu usajili wa matukio muhimu ya Binadamu na kutambulisha majaribio ya mfumo wa Tehama katika ukumbi wa Arnautoglou, jijini Dar es Dalaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

WAZIRI MKUU MAJALIWA - WANANCHI WALIOPEWA URAIA MUHESHIMU SHERIA ZA NCHI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Ulyankulu waache kujihusisha na matukio ya uhalifu. 

Ametoa onyo hilo leo mchana (Ijumaa, Agosti 11, 2017) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Ulyankulu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya VETA, wilayani Kaliua mkoani Tabora. 

Amesema matukio ya ujambazi, mauaji na umiliki wa silaha yanayofanyika kwenye tarafa hiyo ni mengi ikilinganishwa hali ilivyo kwenye maeneo mengine ya mkoa huo. 

"Taarifa nilizonazo zinaonyesha katika kipindi cha miaka miwili kumekuwa na matukio ya mauaji 35, ujambazi matukio 12, umiliki wa silaha nao unatisha. Yamekamatwa magobole 11, bunduki aina ya SMG saba na Mark Four mbili."

"Tulikamata pia risasi 714 za SMG zikiwa kwenye ndoo za mafuta na juu yake wamepaka mafuta ya mawese. Pia risasi mbili za Mark Four zilikamatwa," amesema Waziri Mkuu. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa CUF Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya Agosti 11. 2017, Waziri Mkuu yupo wilayani Kaliua kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Tabora 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mwamnange kilichopo Wilaya ya Kaliua leo Agosti 11, 2017 .Wananchi hao walisimamisha msafara wake ili kumuomba serekali iwasaidie kupata umeme. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihotubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Veta Jimbo la Ulyankulu wilayani Kaliua mkoani Tabora leo August 11, 2017, ambapo amewataka wananchi waliopewa uraia kuheshimu sheria za nchi vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JAFO: ZOEZI LA HOSPITALI TEMBEZI LIFANYIKE MIKOA YOTE

0
0
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Makatibu tawala wa mikoa yote Tanzania bara kuratibu zoezi la Hospitali tembezi katika mikoa yao ili kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kupata huduma ya kibingwa. 

Jafo ametoa agizo hilo leo alipokuwa akizindua huduma za hospitali tembezi kwa wilaya ya Chemba na Kondoa zoezi ambalo limefanyikia mjini Kondoa.Mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika katika wilaya ya Kongwa, Mpwapwa, Chamwino na sasa linaendelea kwa wilaya za Chemba na Kondoa.

Akizindua huduma hiyo, Jafo ameumwagia sifa uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa kuratibu vyema zoezi hilo ambapo zaidi ya wagonjwa 8,000 wamefanyiwa uchunguzi huku 500 wakifanyiwa upasuaji mdogo na mkubwa.

Amewataka wananchi wa wilaya hizo kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa huku akiwataka kupima tezi dume kwa kuwa umekuwa ugonjwa tishio kwa wanaume.

Ameeleza kuwa huduma hizo za kibingwa zinatolewa kwa gharama nafuu na hivyo kuwawezesha wananchi wasio na uwezo kupata matibabu.Jafo amewapongeza madaktari bingwa wa mkoa wa Dodoma kwa kazi kubwa wanayoifanya na amewataka wengine waige mfano wa Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya ya Kondoa na Chemba.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.James Kiologwe na viongozi wa wilaya ya Chemba na Kondoa.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya za Kondoa na Chemba.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wagonjwa na viongozi katika uzinduzi wa Hospitali tembezi.
Wananchi waliofika katika uzinduzi wa hospitali tembezi.

SHAKA AKAGUA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA KUKIFUFUA CHUO CHA MAFUNZO IHEMI

0
0
Katibu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Iringa ndg:James mgego akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya uchaguzi wa jumuiya ya Umoja wa Vijana kwa Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka alipowasili kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi za CCM Mkoa .

Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akitazama baadhi ya
nyaraka na vitabu mbali mbali vilivyokua vikitumika wakati wa mafunzo
katika chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa.
Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka (wa tatu)akielekea kukagua baadhi ya majengo ya Chuo cha mafunzo Ihemi Mkoan Iringa.
Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akikagua majengo ya madarasa katika chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa.
Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akipata maelekezo katika mchoro wa ramani wa kubadilisha majengo na muonekano wa chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa.

Zulia Jekundu S1 Ep 135: Beyonce, Rihanna, Neymar Jr, Shakira na RM Show

Rais Magufuli amteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Seriakli Dkt.Hassan Abbas.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUHUDHURIA SHEREHE YA SIKU YA KIZIMKAZI KESHO ZANZIBAR

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Zanzibar jioni ya leo tayari kuhudhuria sherehe ya Siku  ya Kizimkazi itakayoadhimishwa kesho tarehe 12 Agosti, 2017.

Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa  Abeid Amani Karume, Makamu wa Rais amekutana na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland ambaye alikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam.

Bi. Scotland alikuwa mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland ambaye alikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam jioni ya leo. Pichani kati ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha-Rose Migiro 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland ambaye alikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam jioni ya leo. Pichani kati ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha-Rose Migiro .

MISS TANZANIA 1996 SHOSE SINARE ALALAMIKIA WAPELELEZI WA KESI YAO.

0
0
 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996  Shose  Sinare ameuomba upande wa mashitaka katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili, pamoja na wenzake wawili, walete  mawasiliano yanayofanyika kati ya Tanzania na Uingereza juu ya upelelezi dhidi ya kesi yao.
Shose amedai hivyo leo katika  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Cyprian Mkeha.
Mbali na Sinare, washitakiwa wengine ni   katika kesi hiyo ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Msamire Kitilya, na Sioi Solomon.
Sinare alidai  kuwa mpaka sasa wamekaa gerezani kwa zaidi ya mwaka na nusu hivyo upande wa mashitaka uwasilishe mawasiliano hayo.
Mapema, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi aliieleza mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika kwani bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi huo.
Kufuatia hayo, Hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 25 mwaka huu ili upande wa mashitaka ueleze muendelezo wa kile kilichowasilishwa kortini. Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550  kwa  serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Agosti 2, 2012 Sinare kwenye  Makao Makuu ya benki ya Stanbic iliyopo Kinondoni kwa  nia ya kudanganya aliandaa nyaraka  ya pendekezo akijaribu kuonyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stanbic  ya Tanzania  watatoa mkopo wa dola za kimarekani milioni  550 kwa serikali  ya Tanzania  kwa ada ya uwezeshaji ya asilimia 2.4 ya kiasi cha mkopo huo wakati akijua kuwa sio kweli.
Inadaiwa kuwa  Agosti 2, 2012 ,Sinare alitoa nyaraka za uongo za mapendekezo ya kuonyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stabic  ya Tanzania,  watatoa mkopo wa dola za kimarekani  milioni 550 na kuziwasilisha katika ofisi za Wizara ya fedha  wakati akijua kuwa sio kweli.
Aliendelea kudaiwa kuwa  Septemba 20, 2012 katika  Makao Makuu ya Benki ya Stanbic nchini yaliyopo Kinondoni, alitenda kosa la kughushi barua.
Sinare anadaiwa kughushi barua ya mapendekezo ikionyesha kuwa Benki ya Standard ya nchini Uingireza  ikishirikiana na benki ya Stabic  ya Tanzania  watatoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 550 kwa Serikali  ya Tanzania  kama ada ya uwezeshaji wa asilimia 2.4 ya kiasi cha mkopo huo wakati akijua kuwa sio kweli.
 Agosti 21,2012,  Sinare anadaiwa kuwa kwa lengo la kulaghai aliwasilisha nyaraka hizo za uongo kuiwezesha Serikali ya Tanzania kupata mkopo huo wa kiasi hicho cha ada ya uwezeshaji, katika ofisi za Wizara ya Fedha.
Washtakiwa hao kwa pamoja  wanadaiwa kughushi nyaraka za makubaliano  kwamba  Novemba 5 ,2012 katika benki ya Stanbic makao makuu Kinondoni  Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya walighushi waraka wa makubaliano wa Novemba 5, 2012.
 Inadaiwa kuwa waraka huo ulikusudia kuonesha kuwa Stanbic Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano  na kampuni ya Enterpirise Growth Market Advisors  (Egma) Limited kuwezesha upatikanaji wa mkopo wa Dola za Marekani milioni 550  kwa ajili Serikali ya Tanzania .
Wanadaiwa kuwa  Machi 2013 jijini Dar es Salaam walijipatia Dola za Marekani milioni sita, wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji upatikanaji wa mkopo  na zililipwa kupitia  Kampuni ya Egma T Ltd. Washtakiwa  hao wanadaiwa  kutakatisha fedha kwa kuhamisha, kuchukua na kuweka kiasi cha Dola za Marekani milioni sita  katika akaunti tofauti tofauti  za benki.
Kati ya  Machi 2013 na Septemba 2015, wanadaiwa  kuwa waliweka pesa hizo katika akaunti mbalimbali zilizomilikiwa na kampuni ya Egma na kwamba walipaswa kufahamu kuwa pesa hizo ni mazao ya uhalifu wa kughushi.

MAREKANI KUPITIA SHIRIKA LAKE LA MISAADA LA USAID YAIPATIA TANZANIA DOLA MILIONI 225 KWA AJILI YA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO

0
0
Siku moja baada ya Marekani kutangaza kutoa fedha za nyongeza katika mwaka ujao kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini, nchi hiyo imetiliana saini na Wizara ya Fedha na Mipango makubaliano ya kutoa Dola Milioni 225. 

Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Kilimo na Utawala bora.

Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) hapa nchini Bw. Andy Karas.

Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Bw. Doto James ameishukuru Marekani kwa kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na Tanzania na amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi.

Nae Bw. Andy Karas amesema Serikali na watu wa Marekani wanafurahishwa na kuendelea kwa ushirikiano mwema kati yao na Serikali ya Tanzania katika maendeleo na ameahidi kuwa ushirikiano huo utadumishwa.

Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson ambaye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto)akisaini mkataba wa Makubaliano (Strategic Assistance Agreement )na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas(katikati) kuhusu utoaji wa fedha hizo dola za kimarekani Millioni 225 , tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson akishuhudia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto) akibadilishana mkataba ya makubaliano (Strategic Assistance Agreement) na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto) akipiga makofi pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas(katikati), na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano (Strategic Assistance Agreement ) katika ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kusaini mkataba huo utakaowezesha Tanzania kupatiwa fedha hizo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas mara baada ya tukio hilo la mkataba wa makubaliano katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. 

DKT.SHEIN AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA BARONESS PATRICIA SCOTLAND

0
0
JUMUIYA ya Madola imeahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo kama ilivyo kwa wanachama wengine wote 52 wa Jumiya hiyo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola  Baroness  Patricia Scotland aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu mjini Zanzibar.
Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa Jumuiya ya Madola inaendelea kutekeleza mipango na mikakati kabambe ambayo imeiweka kwa wanancha wake ikiwemo Tanzania ambapo Zanzibar pia, ni miongoni mwao.


Baroness  Scotland alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Rais Dk. Shein kwa juhudi kubwa anazozichukua katika kuhakikisha Zanzibar inakuza uchumi na kuimarisha amani na utulivu na kusisitiza kuwa Jumuiya anayoiongoza haitokuwa nyuma kumuunga mkono.
Aidha, Baroness  Scotland alimueleza Dk. Shein miongoni mwa mipango ya Jumuiya hiyo kwa nchi wanachama wake wote 52 ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa katika sekta ya biashara nan uchumi, kuwasaidia wanawake, vijana, upatikanaji ajira kwa vijana, elimu, kutunza mazingira, uwezeshaji na mengineyo.
Aliongeza kuwa uchumi kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo umekuwa ukiimarika kwa kiasi kikubwa kwa zile nchi za Bara la Afrika na hata nchi za Bara la Asia uchumi wake umeimarika kwa asilimia 5 hadi asilimia 8.

 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Baroness Patricia  Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo akiwa katika ziara ya siku moja na ujumbe aliofuatana nao.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Baroness  Patricia  Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao katika ziara ya siku moja. 
/Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na mgeni wake mara baada ya kumaliza mazungumza na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola  Baroness  Patricia  Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo. 
Picha na Ikulu

The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC meets Zanzibar President, visits some Isles attractions

0
0
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Baroness Patricia Scotland QC and her entourage pose for a  group photo as she takes time off to visit various Isles attractions during her one day tour of  Zanzibar. In the background is the world famous House of Wonders.
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Baroness Patricia Scotland QC and her entourage take a guided walking tour through spice plantations in the Zanzibar suburbs
During the Spice tour the Baroness  and her entourage saw how the spices, herbs and fruits are cultivated, with the  tour guide describing in detail all about them as well as tropical fruits such as cloves, lemongrass, nutmeg, cinnamon, turmeric, vanilla, coconuts, papaya, chilli, black pepper, jackfruit, cardamom, cassava and oranges.
Some of the many tourists taking the spice tour cool off the day with coconut juice under clove trees
The Baroness and her entourage join in



SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC), KAMPUNI YA NDEGE TANZANIA (ATCL) ZATILIANA SAINI MKATABA WA MAKUBALINAO YA USHIRIKIANO WA KUTOA HUDUMA

0
0
Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, akizungumza na waandishi wa habari, wakati akielezea kuhusu makubaliano ya ushirikiano ya kutoa huduma na Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa. Makubaliano kati ya taasisi hizo, ni katika nyanja za 1. Usafirishaji wafanyakazi, wanaposafiri kikazi, 2.Usafirishaji wa mizigo, vifurushi na barua kupitia ndege za ATCL, 3. Kubadilishana uzoefu wa namna ya kuhudumia wateja, 4. Ushirikiano wa matumizi ya majengo ya Ofisi na 5. Kushirikishana kwenye tovuti kuhusu mambo yote ya Masoko.
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kulia) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kushoto), wakitia saini mkataba huo wa ushirikiano kati ya taasisi zao hizo. Kulia anayemsaidia Postamasta Mkuu ni Mwanasheria wa TPC, Bi. Zuhura Pinde.
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kushoto) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kulia), wakiuonesha kwa waandishi wa habari mkataba huo, mara baada ya kuusaini jijini Dar es Salaam leo.   
Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kulia) akimtambulisha baadhi ya watendaji wa shirika hilo, Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (wa pili kulia), mara baada ya kumalizika shughuli hiyo, Dar es Salaam leo.  



Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images