Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AMPA SIKU 15 MWEKA HAZINA WA SIKONGE, APATE MAELEZO YA KUTOKUSANYA MAPATO

$
0
0
*Ataka apate maelezo kwa nini ameshindwa kukusanya mapato

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa siku 15 Mweka Hazina wa Wilaya ya Sikonge, Bw. Evans Shemdoe ajieleze ni kwa nini ameshindwa kufikisha asilimia 80 ya makusanyo ya ndani.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo asubuhi (Alhamisi, Agosti 10, 2017) wakati akizungumza na watumishi na watendaji wa wilaya hiyo, mjini Sikonge.

“Nataka maelezo yakayoniridhisha ni kwa nini hamkufikisha asilimia 80 ya makusanyo ya halmashauri ambacho ni kiwango cha chini. Nzega TC wamefikisha asilimia 112, Kaliua wana asilimia 91, Nzega DC wana asilimia 80, ni kwa nini wewe umeshindwa kufikisha kiwango hicho?,” alihoji Waziri Mkuu.

“Ninataka nipate maelezo pia ni ipi mipango yenu ya kukusanya mapato kwa maeneo mliyoshindwa kufanya vizuri, na pia mmejipangaje kwa mwaka ujao wa fedha. Niyapate maelezo hayo ifikapo tarehe 25 Agosti,” amesema.

Alipopewa nafasi ya kujieleza, Bw. Shemdoe alisema wamefikisha asilimia 76.7 na wameshindwa kufikia lengo kwa sababu ya upungufu wa mvua katika msimu uliopita, hali ambayo ilichangia kushuka kwa mavuno ya zao la tumbaku miongoni mwa wakulima.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa wilaya hiyo, washirikiane na watendaji na madiwani ili kuongeza mapato ya wilaya hiyo badala ya kuwaachia watendaji wa kata peke yao.

Jana, mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Tabora, Waziri Mkuu alizitaka Halmashauri tano kati ya nane za mkoa huo zitoe maelezo ni kwa nini zimeshindwa kufikisha asilimia 80 ya makusanyo kama ambavyo waliagizwa na Serikali.

“Halmashauri zilizovuka malengo ni tatu tu, Nzega TC, Kaliua na Nzega DC. Nataka taarifa za halmashauri zilizobakia ifikapo Agosti 25, wakijieleza ni kwa nini hawajafikia malengo ya ukusanyaji mapato yaliyowekwa ambayo ni asilimia 80,” alisema.

Taarifa ya mkoa huo inaonyesha makusanyo kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo:- Tabora Manispaa asilimia 64.1; Nzega Mji (asilimia 112); Nzega Wilaya (asilimia 80.8); Igunga (asilimia 64.6); Tabora (asilimia 77.3); Sikonge (asilimia 76.7); Urambo (asilimia 70.9) na Kaliua (asilimia 91.5).

Pia amezitaka Halmashauri zote zihakikishe zinafanyamakusanyo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki. “Ukusanyaji wote wa mapato ni lazima ufanyike kwa mfumo wa kielektroniki. Halmashauri ambazo hazijafanya hivyo, zitumie makusanyo ya mwaka jana kununulia mashine za EFD. Hatutaki kuona risiti za kuandika kwa mkono zinatumika,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa wa Tabora uhakikishe wanapatikana watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika wilaya hiyo ili waweze kusaidiana na watendaji wa halmashauri hiyo kukusanya mapato.

“Hapa Sikonge naambiwa hakuna ofisi za TRA. Lazima tupate maafisa wa TRA katika kila Halmashauri ili watoe elimu na washirikiane na madiwani, watendaji wa vijiji na watumishi wa Halmashauri juu ya ukusanyaji mapato,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 10, 2017.

MASAUNI AKAGUA UJENZI WA VITUO VYA POLISI, AFANYA MKUTANO NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI NA MADEREVA BODABODA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, wakati alipotembelea Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mjimwema, Wilayani Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Gilles Muroto na anayefuatia ni Mkuu wa Utawala Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benadict Kitalika 
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akimuonyesha eneo linapotakiwa kujengwa kituo cha Polisi Kibada, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya naibu waziri,wilayani Kigamboni, Dar es Salaam.
Muonekano wa nje wa Kituo cha Polisi cha Mwasonga kilichopo wilayani Kisarawe, kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake kukamilika.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na madereva bodaboda wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kigamboni ambapo aliwaasa madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani pindi wafanyapo shughuli zao ili kuepuka ajali.

WAHALIFU 13 WAUAWA NA POLISI KIBITI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Chini ni silaha  8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro  akionesha makasha ya risasi (magazine) ambazo  ni miongoni  mwa makasha 8 yaliyokuwa yakitumiwa na wahalifu  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto  ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na  Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13 ambao walikuwa wakifanya mauaji  Kibiti. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro  akielezea  baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu  13 waliouawa  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti   ambapo  jumla ya  silaha 8 aina ya SMG,  risasi  158, pikipiki 2, pamoja na  begi la nguo  vilivyokuwa  vikitumiwa na wahalifu hao.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro  akionesha silaha aina ya SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8  zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kulia  ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na  Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro  akiongea na wananchi wa Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka kukagua eneo la tukio walipouawa  wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi  katika eneo la Tangibovu.
 (Picha na Jeshi La Polisi.)

Tarehe 04.08.2017 huko eneo la Gari Bovu, kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti, Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Jeshi la Polisi lilimkamata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani akiwa ana majeraha maeneo mbalimbali ya mwili wake akionekana kuwa alikuwa anaendelea kujitibia mwenyewe kwa njia za kificho. Mtuhumiwa huyu, alikamatwa kutokana na kuwepo kwa taarifa za kiintelijensia kuhusu yeye kuhusika na vitendo vya kufadhili, kusaidia, kuhifadhi na kushiriki uhalifu wa ujambazi maeneo mbalimbali. Mtuhumiwa alipohojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili alikubali na alionyesha dhamira ya kwenda kuonyesha Ngome yao.


Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu  usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu.  Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake. Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha  kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:
1.  Hassani Ali Njame
2.  Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3.  Saidi Abdallah Kilindo
4.  Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5.  Issa Mohamed Mseketu @Mtawa
6.  Rajabu Thomas @Roja
7.  Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.
Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
KIELELEZO
UTAMBUZI
SILAHA, RISASI NA MABOMU
1.   
SMG = 5
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
2.   
Anti Riot Gun 38mm = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
3.   
SAR = 1
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam
4.   
MAGAZINI = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
5.   
Risasi za SMG 158
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
6.   
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea
7.   
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
VIELELEZO VINGINE
8.   
Pikipiki  = 2
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali
9.   
Vitenge na Nguo mbalimbali
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi
10.       
Begi = 1
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe

Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki  inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1.          Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2.          Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3.          Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4.          Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la  Kibwibwi – Wilaya ya  Kibiti
5.          Kuua Afisa Mtendaji,  Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti
Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:
a.           Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi  wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.
b.          Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.
c.           Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.
Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali. Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.    
Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili  waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara moja.
Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.            Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii.          Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii.       Haji Ulatule
iv.        Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v.           Rashid Mtutula

Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.

Imetolewa na;

Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
 

WAFANYAKAZI WA TANESCO KUPITIA TUICO WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KAMPENI YA "KA...TA" KWA KUONGEZA MAKUSANYO YA BILI ZA UMEME

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia chama chao cha TUICO, wamemponegza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya umeme nchini ambapo kampeni yake ya “KA..TA” imekuwa na mafanikio makubwa ambapo wale wadaiwa sugu sasa wanalipa madeni yao.

Akitoa salamu za pongezi kwa Rais leo Agosti 10, 2017, kwenye makao makuu ya TANESCO Ubungo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, tawi la TANESCO, Bw.Hassan J.M Athumani, alisema, Mhe. Rais Magufuli, amewezesha TANESCO kukusanya madeni yake hata maeneo ambayo ilikuwa vigumu sana kulipa madeni.

“Wakati kampeni ya KA..TA ilipoanza mwezi Machi mwaka huu wa 2017, deni lilikuwa shilingi bilioni 275, kati ya hizo, taasisi za serikali pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), zilikuwa zinadaiwa shilingi Bilioni 180 wakati taasisi binafsi, zilikuwa zinadaiwa shilingi Bilioni 95.

Bw. Athumani alisema ZECO pekee tayari wamelipa shilingi bilioni 18, wakati taasisi za serikali yakiwemo majeshi wamelipa deni shilingi Bilioni 18 pia, huku wadaiwa binafsi (private) wamelipa shilingi bilioni 5 na hivyo kufanya deni lililolipwa kufikia Julai 2017, kufikia shilingi bilioni 41.

“Kampeni hii ya rais ya KA..TA, imewezesha TANESCO sasa kukusanya bili za umeme hadi asilimia 104 kwa mwezi kutoka asilimia 90 kwa mwezi kabla ya kuanza kwa kampeni hii.” Alifafanua Mkuu wa Fedha wa TANESCO Bw.Philidon Siyame


Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, Tawi la TANESCO, Bw. Hassan JM. Athumani, akizungumza wakati wa kutoa tamko la Wafanyakazi wa TANESCO kupitia chama chao cha TUICO kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kampeni aliyoianzisha ya ukusanyaji wa madeni ya bili za umeme ijulikanayo kama "KA..TA". Tamko hilo alilitoa mbele ya wajumbe wa kamati kwenye ukumbi wa mikutano wa TANESCO makao makuu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 10, 2017.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO tawi la TANESCO, kutoka kushoto, Bw.Ahmed Mwinyi, ayewakilisha wafanyakazi upande wa uzalishaji umeme kwa njia ya mafuta (Themo Generation), Bw.Felix Lyimo, anayewakilisha wafanyakazi kutoak Kanda ya Dar es Salaam na Pwani na Bi.Asha Mtola, anayewakilisha wafanyakazi wanawake wa Shirika hilo wakisikiliza wakati tamko hilo likitolewa na Mwenyekiti wao. .
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.Tito Mwinuka, (wapili kushoto), Naibu Mkurugenzi Mtendaji (uwekezaji), Mhandisi Khalid James, (wakwaza kushoto) na baadhi ya wajumbe wa TUICO, wakinakili yaliyokuwa yakisemwa na Mwneyekiti wa TUICO Bw. Athumani.

Dkt. Chamuriho, MAB wakagua ujenzi Kiwanja cha ndege cha Songwe

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Serkta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho leo kwa kushirikiana na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), wamefanya ukaguzi wa miundombinu ya barabara ya kutua na kuruka kwa ndege na jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe Mbeya.

Tayari ujenzi wa barabara ya kutua kwa ndege yenye urefu wa km. 3.3 umekamilika ambapo inaruhusu kutua kwa ndege zenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 90 hadi 300, ambapo ndege za mashirika mbalimbali ikiwemo ya ATCL, Precisions na Fastjet zimekuwa zikifanya safari zake mara kwa mara kwenye kiwanja hiho.
Kiwanja hicho kipi daraja la sita (category 6), ambapo mbali na ndege za abiria pia kinaruhusu kutua kwa ndege za mizigo ya mazao ya kilimo yakiwemo maua, matunda, nyama, mchele na maharage kupelekwa maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (wa pili kutoka kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), Prof. Ninatubu Lema (wa pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wa MAB wakisikiliza maelezo yanayohusu jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa Songwe kutoka kwa wahandisi, walipotembelea ujenzi huo leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Drk Leonard Chamuriho (kulia) akitoka ghorofa ya kwanza ya jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe, Mbeya, mara baada ya kufanya ukaguzi na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB). Wanne ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi.
 Katibu Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (aliyechuchuma) akishika upana wa barabara ya kuruka na kutua ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe baada ya kupata maelezo kutoka kwa Wahandisi Washauri wa Kampuni ya UNETEC. Mhandisi Roupina Jambazian na Geofrey Asumenye (walioinama), baada ya kufanya ziara pamoja na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege (MAB) ya kukagua maendeleo ya ujenzi  wa miundombinu.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB) na Katibu Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (wa kwanza kushoto)  wakikagua barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe. Wa pili kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vyua Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TSN & TBC KUWAKUTANISHA PAMOJA WAGOMBEA URAIS TFF KATIUKA KIPINDI MAALUM

$
0
0
KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) kesho Ijumaa (Agosti 11, 2017)wameandaa kipindi maalum kwa wagombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kitakachofanyika mjini Dodoma kuanzia majira ya saa 3 usiku.

Kipindi hicho maalumu kitarushwa mubashara kupitia TBC pamoja na ‘TSN Online’ kitawakutanisha wagombea urais; Ally Mayay, Fredrick Mwakalebela, Wallece Karia, Shija Richard, Iman Madega na Emmanuel Kimbe ikiwa ni saa chache kabla ya siku ya uchaguzi yaani kesho kutwa Jumamosi.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kipindi hicho, Enock Bwigane alisema kuwa ili mpira wa miguu uendelee kukua nchini TBC na TSN iliona ni vyema ikawakutanisha wagombea kwenye jukwaa moja ili waweze kuwaambia wananchi ni kwa njia gani wataweza kuinua soka la Tanzania kama wakipewa dhamana hiyo.

Alisema, “Kuna takribani wapiga kura 130, wagombea urais ni sita lakini mmoja ndiye atakayeshinda na kuongoza shirikisho hilo kwa miaka minne kabla ya uchaguzi mwingine hivyo tumeona haja ya kuwakutanisha na kuwawezesha wananchi waweze kuwafahamu...

“…Naamini fursa ya kuwakutanisha na kuwapa nafasi ya kuwaeleza watanzania sera na mipango yao ya kuboresha soka ni jambo la msingi na ni haki yao ukizingatia kuwa leo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni,” alisema Bwigane.

Naye Katibu wa kamati hiyo, Alfred Lasteck alisema kuwa TSN ikishirikiana na TBC inatambua nini watanzania wanataka kufahamu kuhusu mpira wa miguu na ndiyo maana imepanga kuwakutanisha wagombea ili waweze kuzungumza na umma kabla ya uchaguzi hapo kesho.

“Kuna zaidi ya Watanzania milioni 50 ambao wangependa kufahamu ni nini kitasaidia soka la Tanzania ili liweze kuendelea kutoka lilipo sasa hadi kufikia mafanikio.

“Hivyo ni nafasi ya kipekee kwa kila mtanzania kufuatilia matangazo mubashara yatakayorushwa na TBC1 pamoja na TSN Online kipindi kile ambacho wagombea wote wa Urais watakapokuwa wakielezea mipango yao kuhusu mpira wa miguu nchini,” alisema Lasteck.

WAZIRI UMMY MWALIMU, WAZIRI SIMBACHAWENE NA BILIONEA BILLGATE WAZINDUA MFUMO WA MATUMIZI YA KIELEKTRONIKI KATIKA SEKTA YA AFYA

$
0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam katikati ni Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Simbachawene.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akimkabidhi zawadi Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akionyesha kitabu cha mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam pamoja na Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates katikati na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Simba Chawene.
Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates wa kwanza kushoto akisaini kitabu cha wageni wakati alipokutana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa pili kushoto katika ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es salaam ili kuzindua mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya.

KATIBU WA CCM MKOA WA DODOMA AHIMIZA UMOJA,UPENDO NA USHIRIKIANO KATIKA KUITEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM.

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma kimewakutanisha viongozi wa serikali na wa Chama ngazi ya Tarafa katika semina ya siku moja lengo likiwa ni kuwapa uelewa wa pamoja wakati wa  kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Akifungua semina hiyo katika kata ya Nzoisa wilayani Kongwa Katibu CCM mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph  amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa pamoja ili kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kama ilivyoahidiwa.

Ili hilo litekelezeke amewaasa kujenga umoja na maelewano katika sehemu zao za kazi kwa kuelezana ukweli pale wanapoona kuna jambo haliendi sawa na kutatua kero za wananchi kama walivyoahidi.

Alisema viongozi wa Chama na Serikali wakiwa tofauti ilhali kazi ya kupeleka maendeleo kwa wananchi kutokana na Ilani iliyopo inapaswa kufanya kwa ushirikiano wanakuwa wanawakosea wananchi walioichagua CCM na kuiweka madarakani.
 PICHA (1)
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali wa Tarafa ya Nzoisa wilayani humo katika semina ya kujenga uelewa wa namna ya kutekeleza majukumu yao kwa pamoja.
PICHA (2)
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph akifungua semina hiyo kwa viongozi wa chama na serikali ngazi ya Tarafa ambapo amesisitiza ushirikiano,upendo na umoja katika kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliyopo.
PICHA (4)
Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma akiongoza viongozi wa Chama na Serikali wa wilaya ya Kongwa kuimba wimbo wa Chama katika semina hiyo,miongoni mwa viongozi hao yupo mkuu wa wilaya hiyo Deogratius Ndejembi,katibu wa CCM wilaya Mfaume Kizigo na mwenyekiti wa halmashauri White Zubeir.


SERIKALI YAFUTA UMILIKI WA VIWANDA AMBAVYO HAVIJAENDELEZWA

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU IKULU.

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji

Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo ya Elimu ya Juu puia Katibu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nd,Iddi Khamis Haji alipokuwa akitoa taarifa ya Uongozi wa Wizara ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wengine (katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Maalim Kombo Hassan Jumaakifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Said Hassan Saidi,[Picha na Ikulu.] 10/08/2017.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Elimu Bi.Sada Thani (kulia) alipokuwa akitoa taarifa yake wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi hiyo na Uongozi wa Baraza la Elimu,wengine ni Wajumbe wa Bodi,[Picha na Ikulu.] 10/08/2017. 

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA MHE PATRICIA SCOTLAND IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JIONI HII

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe Patricia Scotland Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Agosti 10, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe Patricia Scotland Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Agosti 10, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe Patricia Scotland Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Agosti 10, 2017 akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe Patricia Scotland Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Agosti 10, 2017 akiwa kaongozana na  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro.

Picha na Ikulu

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA MASHIRIKA YA KIPAPA YA VATICAN BABA ASKOFU PROTAS RUGAMBWA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Sanamu ya  Bikira Maria wa Fatima kutoka kwa Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa wapili kutoka kushoto Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza na kumuaga mgeni wake Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na  mgeni wake Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 10.08.2017

MICHUZI TV: KOCHA WA ZAMANI WA TAIFA STARS MARCIO MAXIMO AMMWAGIA SIFA FREDRICK MWAKALEBELA URAIS TFF

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZUNGUMZIA SAKATA LA kiwanda cha Ngozi cha AFRICA TANNERIES


INTRODUCING "NAVIMBA" BY LILLIAN INTERNET

INTRODUCING "NAKUONA" BY KENNEDY

MAMA GRACA MACHEL AZINDUA KITABU CHA WANAWAKE WALIOFANIKIWA KIUCHUMI AFRIKA

$
0
0
 Mjane wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela , Mama Graca Marshel  akipiga makofi mbele ya Wanawake waliofanikiwa kiuchumi ambao wameandikwa katika kitabu  cha wanawake Afrika kuashiria uzinduzi wa Kitabu hicho katika Mkutano wa Advance Women Africa
 Mwandishi wa Kitabu cha Wanawake waliofanukiwa kiuchumi Afrika , Lisa O'Donoghue akifanya marejeo ya kitabu hicho kabla ya kuzinduliwa
 Mwandishi wa Habari kutoka Tanzania akitoa stori fupi ya Maisha na Mtoto wake , Ester Karin

 Wanawake Mashuhuri nchini wakiwa katika mkutano huo wakijadili jambo kabla ya uzinduzi wa kitabu
Mjane  wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela , Mama Graca Marshel , akiteta na Wanawake wajasiliamali nchini ambao  wameshiriki Mkutano wa Women Advance Afrika
 Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini.
Picha na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

MAGAZETI YA IJUMAA LEO AGOSTI 11,2017

WAFUGAJI LONGIDO WAANZA KUNUFAIKA NA UJENZI WA SOKO LA KISASA LA MIFUGO

$
0
0
 

Benny Mwaipaja, WFM, LONGIDO-ARUSHA.

WAFUGAJI wilayani Longido Mkoani Arusha wameanza kunufaika na ujenzi wa soko la kisasa la mifugo linalojengwa na Serikali katika kijiji cha Worendeke kata ya Kimokouwa, kupitia mkopo wa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB.

Baadhi ya wafugaji wamesema kuwa Soko hilo linalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 650, limewaondolea adha kubwa waliyokuwa wakiipata walipokuwa wakiuza mifugo yao nchini Kenya kutokana na gharama kubwa ya kusafirisha mifugo kwenda huko pamoja na kulipa kodi na ushuru mbalimbali.

Wamesema kuwa kujengwa kwa somo hilo ni mkombozi mkubwa kwao na kwamba hali hiyo itasisimua uchumi wao kwa kuwa wafanyabiashara wa ndani na kutoka Kenya wamekuwa wakiwafuata kwenye soko hilo kununua mifugo yao hatua inayowafanya wapate faida kubwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido, Bw. Toba Nguvila, amesema kuwa soko hilo ambalo ujenzi wa miundombinu yake umekamilika kwa asilimia 85 limeanza kuiingiza Serikali mapato yake ambapo kwa wastani Halmashauri ya wilaya inakusanya wastani wa shilingi milioni 1 kwa siku.

“Asilimia 95 ya wakazi wa wilaya yetu ni wafugaji wa kimaasai ambao kwa kipindi kirefu wameteseka kusafirisha mifugo yao kwenda Kenya na kutopata faida kutokana na gharama kubwa ya kusafirisha, kupitisha mifugo kwenye maeneo ya watu hivyo kulazimika kulipa ushuru, halikadhalika kulipia tozo mbalimbali wakati wakisubiri kuuza mifugo yao” alieleza Bw. Nguvila .

Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Bw. Toba Nguvila (kushoto), akimweleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (katikati) kabla ya kutembelea Soko la Kisasa Mifugo linalojengwa katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido, mkoani Arusha, linalojengwa kutokana na mkopo wenye masharti nafuu wa sh. Milioni 650 kutoka Benki hiyo. Kulia ni Afisa anayeshughulikia Dawati la Beni ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Mifugo katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido mkoani Arusha, unaogharimu shilingi milioni  650, ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akisisitiza jambo baada ya kusikiliza maelezo ya mradi huo wa Soko la Kisasa la Mifugo linalojengwa katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa wilayani Longido mkoani Arusha. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (wapili kulia) akimweleza jambo Katibu Tawala wa wilaya ya Longido mkoani Arusha, Bw. Toba Nguvila, wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Mifugo, linalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 650 kupitia mkopo nafuu wa Benki hiyo kwa Serikali ya Tanzania. 
Baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido mkoani Arusha, wanaonufaika na uwepo wa soko hilo ambapo wameanza kuuza mifugo yao kwa faida kubwa badala ya kupeleka mifugo yao nchi jirani ya Kenya ambako walikuwa wakipata adha kubwa na faida ndogo kutokana na gharama kubwa walizokuwa wakitumia kufikisha mifugo yao nchini humo. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango) .

Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images