Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

DAWASCO App yaingia mtaani

$
0
0
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro akitoa elimu juu ya matumizi ya mfumo wa DAWASCO kwa kwa njia ya simu kwa watumiaji wa vyombo vya Moto hususani Bajaj na Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam. Mfumo huo umezinduliwa rasmi jana ili kutoa nafasi kwa wananchi kupata na kutoa taarifa sahihi za dawasco.


DKT. SHEIN AKUTANA NA MENEJA WA CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na mgeni wake Meneja wa China Harbour Engineering Company Ltd Nd,Xu Xinpei alipowasili katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na mgeni wake Meneja wa China Harbour Engineering Company Ltd Nd,Xu Xinpei wakati alipowasili katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akifuatana na mgeni wake Meneja wa China Harbour Engineering Company Ltd Nd,Xu Xinpei baada ya mazungumzo yao wakati alipowasili katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.Picha na Ikulu, Zanzibar.

WADAU WA NISHATI KUTOKA UMOJA WA ULAYA NA TANZANIA WAKUTANA KUJADILI MFUMO WA NISHATI KATIKA MAJENGO MAKUBWA NCHINI

$
0
0
Mtoa mada kutoka Mradi wa Matumizi bora ya Nishati katika Majengo Makubwa Kutoka Umoja wa Ulaya,Margareta Zidar akizungumza na Wadau wa Nishati katika semina Maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini juu ya Matumizi ya Nishati katika Majengo Makubwa.
Mtoa mada kutoka Mradi wa Matumizi bora ya Nishati katika Majengo Makubwa Kutoka Umoja wa Ulaya, Lena Lampropoulou, akizungumza na Wadau wa Nishati katika semina Maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini juu ya Matumizi ya Nishati katika Majengo Makubwa.
Wadau mbalimbali wa Masuala ya Nishati katika Majengo Makubwa wakiwa wanafuatilia mada katika Semina hiyo ya Nishati katika Majengo Makubwa
Wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi Binafsi wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo muhimu kwa ajili ya Nishati za Mjengo Makubwa
Wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi Binafsi wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo muhimu kwa ajili ya Nishati za Mjengo Makubwa
Wadau wa Masuala ya Nishati ya Majengo Makubwa kutoka nchini Tanzania na Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya ufunguzi wa Semina yao ya masuala ya Nishati katika Majengo Makubwa iliyofanyika Serena Hotel Dar es Salaam.

'MARUFUKU VIONGOZI KUFANYA BIASHARA YA PEMBEJEO KAMA HAWANA MASHAMBA'.

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku viongozi wa Serikali kufanya biashara ya pembejeo na vishada kama hawana mashamba ya tumbaku.

“Kuna baadhi ya viongozi wa Serikali hapa mkoani wamejiingiza kwenye biashara ya vishada na uuzaji wa pembejeo. Hii ni dosari. Hatutaruhusu hili hata kidogo,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 9, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora.

Alisema: “Kiongozi wa Serikali ni lazima uwe shamba na ulilime kisasa ili liwe ni shamba darasa kwa wakulima walio jirani nawe. Usifanye biashara ya pembejeo kana huna shamba. Nanyi viongozi wa AMCOS msikubali kuuza vishada vya viongozi wa Serikali, tukikukamata, utaenda jela.”

Alisema endapo viongozi wataamua kulima mashamba ya zao hilo, watalazimika kujiunga na vyama vya msingi (AMCOS) vya kwenye maeneo yao ili waweze kuuza kupitia huko kutokana na agizo la Serikali linalokataza makampuni kununua tumbaku bila kupitia kwenye vyama vya msingi.
 
Aprili 15, mwaka huu, akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Tabora, Waziri Mkuu aliagiza wakulima wa kujitegemea (Indepenent Farmers) na wale wa kwenye vikundi (Associations) wote wauzie tumbaku yao kupitia kwenye vyama vya ushirika ili kuzuia utoroshaji wa zao hilo na wakulima wasio na madeni kulazimika kuwalipia wenzao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 10, 2017.

WIZARA YA AFYA YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO YA JAMII NCHINI KUFANYA THATHIMINI YA MABORESHO YA SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

WIZARA YA AFYA MAENDELEO YAJAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO YA JAMII NCHINI KUFANYA THATHIMINI YA MABORESHO YA SERA YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA JINSIA JIJINI DAR ES SALAAM.

SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa Kanuni za taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha taslimu kutoka na kwenda nje ya nchi (Crossborder Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments Regulations) ambapo wasafirishaji wa fedha taslimu na wasafiri wote wanaotoka au kuingia nchini, watatakiwa kutoa taarifa za fedha taslimu wanazosafirisha ikiwa fedha hizo zinalingana au zinazidi kiasi cha dola za kimarekani elfu kumi (USD 10,000).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni hizo, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe alisema utekelezaji wa kanuni hizi, pamoja na mambo mengine utaiwezesha nchi kuwa na takwimu za usafirishaji fedha taslimu.

“Takwimu hizo zitakazosaidia pamoja na mambo mengine kubaini vitendo vya kihalifu, kupunguza utoroshaji wa mitaji na kuhakikisha kuwa tunapunguza kama siyo kumaliza kabisa usafirishaji wa fedha zitokanazo na uhalifu au/na fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi” alisema Bw. Makombe

Aidha kanuni hizo zimeweka adhabu zitakazochukuliwa dhidi ya wale watakabainika kutaka kupita na fedha zinazolingana au zinazozidi kiwango kilichowekwa bila kutoa taarifa au watakaotoa taarifa za uongo. Alizitaja adhabu hizo kuwa ni pamoja na kukamatwa kwa fedha taslimu walizonazo na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kama vile kufunguliwa mashtaka.

“Wahalifu pamoja na mambo mengine, wanapenda kusafiri na fedha taslimu kwani wanaogopa kutumia benki kutuma fedha kutokana na umakini unaoongezeka katika benki na udhaifu unaoweza kuwepo mipakani” Alisisitiza Bw. Makombe.Kamishna huyo amewaasa washiriki wa warsha hiyo kutekeleza jukumu hilo kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ili kuziba mianya yote ambayo wahalifu wanaweza kuitumia kutimiza kusudi lao ovu na kuhatarisha usalama wa nchi.

Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakifuatilia kwa makini mjadala katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).



MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA TEHAMA KUANDA MIPANGO YA BAJETI ZA MAMLAKA ZA SERIKALI WAFUNGULIWA MOROGORO

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, akifungua mafunzo ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma nchini, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID). Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA, Ofisi ya Rais Tamisemi, Baltazar Kibola, akiwasilisha mada juu ya mfumo mpya wa Tehama ulioboreshwa ujulikanao kama ‘PlanRep’ utakaoanza kutumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Meneja Mifumo ya TEHAMA kutoka Mradi wa PS3, Revocatus Mtesigwa, akizungumza na washiriki wa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama (hawapo pichani) utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa, mkoani Morogoro jana 
Washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma, wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa na wataalam kutoka Tamisemi na Mradi wa PS3, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA YASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA KAMATI YA LAAC

$
0
0
Na Jumbe Ismailly IRAMBA 

HALMASHAURI ya wilaya ya Iramba,Mkoani Singida imeshindwa kutekeleza agizo la kamati ya kudumu ya Bunge la kutenga asilimia kumi kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya wanawake pamoja na vijana katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha wa 2012/2013 hadi 2014/2015.

Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,CARROLINE DALULI aliyasema hayo kwenye taarifa aliyotoa kwenye mkutano wa Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo lilipokutana kujadili hoja za Ukaguzi na Mpangokazi wa utekelezaji wa maoni yaliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2015/2016.

“Kamati iliagiza Halmashauri kuchangia asilimia kumi kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana kwa miaka hiyo iliyotajwa na kiasi kilichoonekana”alifafanua kaimu Mweka Hazina huyo.

Kwa mujibu wa Kaimu Mweka hazina huyo kwa mwaka 2012/2013,2013/2014 na 2014/2015 Halmashauri ya wilaya ya Iramba haijatekeleza agizo la kamati ya kudumu ya Bunge kwani hakuna fedha yeyote ile iliyotengwa na iliyopelekwa kwenye vikundi hivyo.

Aidha Daluli aliweka bayana pia kwamba kwa mwaka 2016/2017 Halmashauri hiyo imechangia shilingi milioni mbili,zikiwemo shilingi milioni moja kwa Mazega Kisimba na shilingi zingine milioni moja kwa kikundi cha Maendeleo Shelui na itaendelea kuchangia kadri fedha zitakapopatikana.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi akimkabidhi mmoja wa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba cheti cha mafunzo ya udiwani aliyopata na ambayo yatawawezesha madiwani wote kutambua majukumu pamoja na mipaka yao ya kazi.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi akisisitiza juu ya maafisa watendaji wa vijiji 30 walioiba fedha za chakula cha njaa kuhakikisha wanazirejesha ifikapo aug,30,mwaka huu na kupendekeza njia rahisi ya fedha hizo kurejeshwa kuwa ni kuanzishwa kwa Mahakama tembezi itakayomtembelea kila mdaiwa na kuuza mali alizonazo ili kulipia deni la chakula hicho cha njaa walizokula.


Seven Opportunities in the Uganda-Tanzania Pipeline Project and How to Participate.

$
0
0
7 Opportunities in the Uganda-Tanzania Pipeline Project and How to Participate.
THE EAST African oil pipeline (or the Uganda-Tanzania pipeline is the talk of the town now. Not only in East Africa but all over the globe.
The construction of this pipeline is officially on. Social and resettlement planning services have been undertaking it in Tanzania.

The sad reality is that people don’t know about the business opportunities available in the project.
More and more people keep wondering what the opportunities emerging in this project are and how they can be part of it.
“Do they offer equipment or provide services?” they ask themselves.
If you are among these people seeking to do business in this projects but have no idea how to get started, then no need to worry.
This article shows you some opportunities available in the project and how you can participate so that you can reap a substantial profit.
The Tanzania-Uganda Pipeline Opportunities
  1. Pipes and connection supplies: One of the opportunities in this project is to supply and manufacture seamless tubes and pipes (LSAW) and also supplying steel pipes.
  2. Chemical Supplies: For the construction of the pipelines, there are a lot of specialty chemicals needed, from corrosion inhibitors additives to scale remover to chemicals that reduce paraffin build up. You cannot run a pipeline without these things, and you can get them from China really cheap. Which means your profit margin may increase by 30-50 percent.
  3. Pipeline equipment supplies: These cover all materials that are required in the pipeline transportation system. It includes fittings, valves, scraper traps, insulating flanges, flow tee, pumping station, etc.
  4. Civil engineering works: These include building construction work, construction and maintenance of roads, construction and maintenance of drainage system, etc.
  5. Pipeline inspection services.
  6. Food supply.
  7. Security services.
Are you ready to utilize opportunities in this project? Here is how to grab the opportunities:
1. Identify the decision makers and influencers in this Uganda-Tanzania pipeline project.
The first step in pursuing opportunities in the Uganda-Tanzania pipeline is determining who the decision makers are.
Decision makers are the people who can approve or disapprove your proposal.
No matter how big a company is, there are decision makers who can approve or disapprove documents.
This can be easily achieved by making a list of key players in the project and starting to build long term relationship with them.
2. Demonstrate your experience.
You should demonstrate that you are the right person to execute the project you’re proposing.
You should demonstrate your capability and your experiences in executing similar project.
“What if my business is small and new n the industry?” you may ask.
Well, the answer is pretty simple. You still have a chance to tap opportunities in the Uganda-Tanzania pipeline project.
If your business is small and new, and you don’t have any experience or working history to be taken as references to the service you want to render, you should consider going into a joint venture with an experienced contractor in the oil and gas industry in such bidding venture. However inexperienced, you still have a chance to participate in this work.
You have learned the opportunities in the East Africa pipeline project and you now know how to access them.
If you want to learn more about the opportunities in the Tanzanian oil and gas sector and how you can grab them, click here to know more.

SERIKALI YAMALIZA SINTOFAHAMU YA TANI 3,700 ZA TUMBAKU.

$
0
0
 SERIKALI imefanikiwa kumaliza sintofahamu ilikuwepo baina ya wakulima na wanunuzi wa tumbaku mkoani Tabora juu ya uwepo wa tani 3,700 zilizokosa soko.

Tani 3,700 zilikuwa zimekosa wanunuzi kwa sababu hazikuwa na mkataba kati ya wakulima na wanunuzi na hivyo kuhitaji utatuzi wa haraka wa Serikali ili kuinusuru tumbaku hiyo.

“Tumefanikiwa kuongea nao na tutauza zile tani 3,700 kwa wanunuzi,” alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuamsha shangwe ukumbi mzima.

Waziri Mkuu alitoa ahadi hiyo jana jioni (Jumatano, Agosti 9, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora.

Aliwashukuru wanunuzi kwa kukubali kumaliza tatizo hilo kwani litaleta ari mpya kwa wakulima na kuwafanya wajipange vizuri kwa msimu ujao. “Makampuni ya ununuzi yatapita kwenye maeneo yenu, WETCU watafuatilia na tumekubaliana nao kuwa tutafanya kazi pamoja,” alisema Waziri Mkuu.

Kufuatia sintofahamu hiyo, wiki iliyopita, wakazi wa mkoa huo waliomuomba Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli aingile kati ili kuwanusuru na adha ya zao hilo kukosa soko. Naye akawaahidi wananchi hao kwamba suala hilo atalikamilisha Waziri Mkuu.

Mapema, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Aggrey Mwanri wakati akiwasilisha muhtasari wa taarifa ya mkoa huo alisema katika masoko ya tumbaku yanayoendelea, kuna tatizo la tumbaku kukosa  wanunuzi kwani hapakuwa na mkataba kati ya wakulima na wanunuzi.

“Tumbaku inayofikia kilo milioni 3.7 kwa sehemu kubwa ililimwa kwa ufadhili wa WETCU Ltd, kwa fedha ambazo zilikuwa ziende APEX. WETCU walinunua pembejeo na kuwapa wakulima waliokuwa chini ya vyama sinzia, na sasa haina wanunuzi. Tunaomba ulisemee hilo ili tupate ufumbuzi wa suala hili,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni mbunge wa Urambo, Mheshimiwa Margareth Sitta aliiomba Serikali ikubali kuliangalia suala hilo la tani za ziada 3,700 kwani wakulima wamejaza tumbaku majumbani mwao na kwenye maghala.

“Wakulima wetu wanahitaji kuuza hii tumbaku ili wapate fedha za kuanzia msimu ujao wa kilimo. Lakini pia tunaomba liangaliwe suala la upangaji madaraja ya tumbaku, wasaidiwe kukabili bei isiyotabirika na kutatua ukosefu wa soko la uhakika,” alisema Mama Sitta.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 10, 2017.

ALI MAYAYI ATOA VIPAUMBELE VYAKE ENDAPO ATAPATA URAIS TFF

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA WANANCHI WA WILAYA SIKONGE TABORA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Sikonge Mjini leo Agosti.10.2017 katika viwanja vya Tasaf   Waziri Mkuu yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya Kikazi.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.

WHC WAFUNGUA DIRISHA JIPYA LITAKALOWEZESHA WATUMISHI WA SEKTA BINAFSI KUWEZA KUNUNUA NYUMBA.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC),  Dkt. Fred Msemwa (Katikati)akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufungua dirisha jipya  litakalowezesha watumishi wa sekta binafsi  kuweza kununua nyumba zake kwa garama nafuu na kuwainua kiuchumi. Kushoto  ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde na Kulia ni Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC),  Maryjene Makawia.
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde akifafanua jambo wakati wa kufungua dirisha jipya  litakalowezesha watumishi wa sekta binafsi  kuweza kununua nyumba zake kwa garama nafuu na kuwainua kiuchumi. katikati ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC),  Dkt. Fred Msemwa na kulia ni Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC),  Maryjene Makawia.
kulia ni  Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC),  Maryjene Makawia akizungumza na waandishi wa ahabari jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC),  Dkt. Fred Msemwa.

Kulia ni Afisa Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Irene Kasanda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC),  Dkt. Fred Msemw na Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC),  Maryjene Makawia.
Picha na Avila Kakingo, Blog ya Jamii.
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.
WATUMISHI Housing Company (WHC),  wamefungua dirisha jipya  litakalowezesha watumishi wa sekta binafsi  kuweza kununua nyumba zake kwa garama nafuu na kuwainua kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa WHC,  Dkt. Fred Msemwa, amesema, dirisha hilo ambalo litajumuisha Watumishi wote wale wa umma na wa binafsi, litawawezesha wafanyakazi wote kuwa na makazi bora kupitia umiliki wa nyumba kwani nyumba hizo wanaweza kuzitumia kwa kukopa kuanzisha miradi mbali mbali ya uchumi.

Amesema Watumishi hao wa sekta binafsi ambao nao wanapata fursa ya kununua nyumba hizo ni wale ambao hawako katika utumishi wa umma lakini wanachangia katika mifuko ya pensheni.

Ameongeza kuwa, wigo huo mdogo unatokana na mahitaji ya wengi kwani watu wengi ukitoa Watumishi wa umma ambao hapo awali ndio walikuwa na sifa ya kununua nyumba hizo,wanashida ya makazi bora na ya kisasa
                                              KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.

ARUSHA WAIBUKA VINARA TUZO ZA SAYANSI ZA YST.

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Simon Msanjila  akikabidhi zawadi kwa washindi wa jumla wa Shindano la Wanasayansi Chipukizi (YST) lililofanyika jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu , Simon Msanjila  akisoma Zawadi ya Washindi  shindano la Wanasayansi Chipukizi (YST)lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam Kulia ni Mkurugenzi wa Shell Afrika Mashariki  na Bg Tanzania Marc Den Hartog akishuhudia.
Wanafunzi wakishangilia mara baada ya kupata zawadi zao za ushindi katika shindano la Wanasayansi Chipukizi.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BILL GATES NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. ill Gates aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiagana na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia), Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dk Charles Tizeba (wa tatu Kushoto), Msaidizi wa rais Masuala ya diplomasia Bi. Zuhura Bundala (kushoto)  pamoja na maafisa alioongozana nao Bw. Bill Gates
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana na  Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwa katika mazungumzo na   Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiagana na  Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.PICHA NA IKULU


MASAUNI AKAGUA UJENZI WA VITUO VYA POLISI, AFANYA MKUTANO NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI NA MADEREVA BODABODA

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akimuonyesha eneo linapotakiwa kujengwa kituo cha Polisi Kibada, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya naibu waziri,wilayani Kigamboni, Dar es  Salaam.
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akikagua moja ya chumba cha mahabusu ndani ya kituo cha Polisi Mwasonga, wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya polisi wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa.
 Muonekano wa nje wa Kituo cha Polisi cha Mwasonga kilichopo wilayani Kisarawe, kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake kukamilika.

WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKI MCHEZO WA KUBAHATISHA WA TATU MZUKA.

$
0
0
Mratibu wa Mawasiliano wa Mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga, akizungumza hadi shilingi  na Waandishi  juu faida za mchezo huo na namna ya kucheza na kufanikiwa kupata Milioni 30.
Balozi wa Mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka,  Mc Ray Maharufu kama Chikunde  akizungumza juu ya yeye kuhusishwa na kampuni inayoendesha mchezo huo wa Tatu Mzuka.
Kiongozi kutoka Mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka, Mudy B akizungumza na Waandishi wa habari namna ya kushiriki kupitia simu zetu za Mkononi.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

COKE STUDIO AFRIKA YACHANGIA KUPAISHA KAZI ZA WASANII NCHINI TANZANIA.

$
0
0
 
Baadhi ya wasanii wa Tanzania waliowahi kushiriki Coke Studio. *Imetangaza pia muziki wa Bongo Fleva Onyesho maarufu la muziki la Coke Studio Africa, ambalo hivi sasa limeingia katika awamu ya tano chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola, limechangia kwa kiasi kikubwa kutangaza wasanii wa Tanzania waliofanikiwa kushiriki na kazi zao nje ya nchi hususani wanaopiga muziki wa Bongo Flava. Kazi za wasanii zimejulikana kutokana na mtindo unaotumika katika onyesho hili la kuwakutanisha wasanii nguli kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo hufanya kolabo za pamoja ambazo zinarushwa kupitia vituo vya luninga na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia mitandao ya kijamii. Baadhi ya wasanii kutoka Tanzania ambao wameshiriki onyesho hili tangu lianzishwe ni Lady Jaydee, Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Alikiba, Joh Makini, Shaa, Fid Q, Ben Pol, John Makini, Shaa, Nahreel na msimu huu wa tano wapo Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy. Misimu minne iliyopita ya Coke Studio Africa imekuwa na mafanikio makubwa katika kuutangaza muziki wa Bongo Flava barani Afrika. Wamejiongezea mashabiki, wamejifunza mambo mbalimbali kuhusu muziki kama burudani, muziki kama taaluma na muziki kama biashara na tena si tu kutoka kwa wasanii wenzao wa Afrika na Marekani pia. Vilevile wasanii wote ambao wamepita kwenye onyesho hili wameendelea kupata mafanikio makubwa ya kimuziki kutokana na kazi zao kuendelea kutamba na kukubalika kwa wengi ndani na nje ya Tanzania. Taarifa kutoka kampuni ya Coca-Cola iliyotolewa hivi karibuni imeeleza kuwa onyesho la Coke Studio Africa, ambalo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka msimu huu utakuwa na burudani za aina yake kutoka kolabo za wasanii nguli barani Afrika kuanzia Afrika Magharibi mpaka Afrika ya Kusini na litarushwa na vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya 30 barani Afrika. Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki. Katika msimu wa Coke Studio Africa unaotarajia kuanza kurushwa kwenye luninga mapema mwezi ujao unashirikisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, DRC na Cameroon.

RC MAKONDA KUTOA MSAADA WA MIGUU BANDIA KWA WANANCHI WENYE ULEMAVU MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Agness Francis, Globu, ya jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  ameahidi kutoa  msaada  wa  Miguu ya bandia kwa walemavu wa miguu wasio na uwezo wa kununua Miguu hiyo.

Akizungumza  na Waandishi wa Habari leo  jijini Dar es Salaam, Makonda amesema kuwa anatoa fursa hiyo kwa walemavu  200 ambapo itakuwa ni awamu ya kwanza kuweza kufanikisha zoezi hilo.

Makonda amesema zoezi hilo litafanyika kwa  awamu kutokana na gharama. Amesema  gharama hizo ni changamoto kwa wananchi wake kwa walio makazini na hata wasio makazini na amewaomba watumie fursa hiyo kujitokeza katika zoezi hilo la upimaji  vipimo ili kufanikisha leongo

Amesema kuwa zoezi hilo  litafanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 14-15 mwaka huu katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa zilizopo Ilala Boma Jijini Dar Es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akionesha Miguu Bandia kwa Waandishi wa Habari wakati kaizungumza nao Ofisini kwake.

TFS Kukusanya maduhuli kieletroniki

$
0
0
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanza utekelezaji wa ukusanyaji wa maduhuli kwa njia ya kielectroniki kufuatia marekebisho ya sheria ya fedha ya mwaka 2017 na maelekezo ya serikali ya awamu ya tano ambao umezitaka Taasisi za serikali kujiunga na mfumo wa ukusanyaji maduhuli uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na Mipango unaoitwa Government electronic Payment Gateaway-GEPF.   
       
Akitoa ufafanuzi Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bwana Peter Mwakosya amesema Mashamba yote na ofisi za Meneja (DFM's) za Taasisi hiyo zimeunganishwa katika mfumo huo.Aidha amesema kutokana na mazingira ya vizuia(checkpoints)  kutokidhi mahitaji ya mfumo huo na hasa kushindwa kuhifadhi vitendea kazi kama kompyuta na printa kwa sasa wakala inaendelea kuunganisha kwenye mfumo vizuia vyote kwa kutumia vifaa maalum (point of sales-POS). 

  Amebainisha kwamba vifaa hivi vitatumika kukusanya maduhuli na kuhakiki uhalali wa nyaraka zinazokaguliwa katika vituo vyote vya ukaguzi wa mazao ya misitu na nyuki kwa kipindi hichi ambacho tunaendelea kuunganisha vizuia kwenye mfumo moja kwa moja. 

Bwana Mwakosya amesisitiza Maduhuli yote yanayokusanywa kwenye vizuia yanawasilishwa Ofisi ya Meneja wa Misitu wa wilaya mapema ili yaingizwe kwenye mfumo pia amewakumbusha wateja wote wa Mazao ya Misitu na nyuki kuzingatia kwamba wanatakiwa kupata hati za madai (Bill) katika mfumo kabla ya kwenda kufanya Malipo. 

Aidha amewakumbusha wateja wa bidhaa za Misitu na nyuki kwamba stakabadhi zilizokuwazinatumika kabla ya mfumo huu (ERV) hazitaendelea kutumika katika vituo vilivyounganishwa na mfumo.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images