Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1852 | 1853 | (Page 1854) | 1855 | 1856 | .... | 3286 | newer

  0 0  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP) Lucas Mkondya, alipowasili nchini akitokea nchini Rwanda kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kujadiliana juu ya njia za kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa binadamu na biashara ya dawa za kulevya. 
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akisalimiana na baadhi ya maofisa wa Jeshi hilo, waliofika kumpokea alipowasili kutoka nchini Rwanda alipokwenda kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kubadilishana uzoefu pamoja na kujadiliana juu ya njia za kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka, usafirishaji wa binadamu na biashara ya dawa za kulevya. 
   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (watano kulia) na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, Emmanuel Gassana(wanne kulia), wakiwa katika picha ya na Maofisa wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, baada ya kumaliza kikao kazi. Picha na Jeshi la Polisi


  0 0

  KATIKA kuhakikisha inarahisisha upatikanaji wa huduma ya majisafi na kwenda na mfumo wa kisasa wa mawasiliano ya kiteknolojia, Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limezindua mfumo mpya wa mawasiliano ambao unalenga kumrahisishia mteja kupata na kutoa taarifa zinazohusu huduma hiyo kwa haraka zaidi.

  Huduma hiyo mpya sasa itapatikana kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) wa DAWASCO, Kiula Kingu amesema lengo kuu la mfumo huu ni kumweka mteja karibu kihuduma na kila mwananchi ana uwezo wa kutumia mfumo huo katika simu yake kupitia mitandao yote ya simu za mikononi nchini.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) wa DAWASCO, Kiula Kingu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati akitangaza uwepo wa mfumo mpya wa mawasiliano ambao unalenga kumrahisishia mteja kupata na kutoa taarifa zinazohusu huduma hiyo kwa haraka zaidi. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro.

  Kingu ameongeza kuwa ili mteja kunufaika na mfumo huu anatakiwa kuhakikisha ana simu ya mkononi ya “Smartphone” ambayo itamwezesha kupakua mfumo huo mpya wa DAWASCO, kisha kujisajili kwa kuingiza akaunti namba yake ya DAWASCO ambapo baada ya kufuata hatua zote za kujisajili mteja atatumiwa neno la siri ambalo litamwezesha kuingia na kupata taarifa husika. “Sisi Dawasco tumeona haja ya kujiboresha na kwenda sawa na teknolojia kwa kumletea mteja wetu mfumo rahisi ambao utamwezesha kupata taarifa zetu kupitia simu yake ya mkononi muda wowote,”alisema Kingu.

  Naye, Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya maji ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.

  “Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Lyaro.
  Anasema kwa sasa wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO itatumia taarifa hizo kumtafuta mteja na kukamilisha taratibu nyingine hadi kuhakikisha mteja anapata huduma ya maji.

  Katika kutimiza agizo la Waziri wa Maji na Imwagiliaji, Mhandisi Greyson Lwengwe la kuhakikisha wakazi wa Dar es salaama, Miji ya Kibaha na Bagamoyo wanapata huduma ya maji safi, DAWASCO imekua ikijitahidi kuwafikia wananchi kwa njia na mbinu tofauti, kampeni tofauti kama 'mama tua ndoo ya maji kichwani' huku maunganisho ya maji kwa mkopo yakisaidia upatikanaji na uboreshaji wa huduma ya maji kwa maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam.

  Mpaka sasa takribani watumiaji 25,000 wa mitandao ya simu jijini Dar es Salaam wameshapakua mfumo huu na lengo la DAWASCO ni kuwafikia wakazi wengi zaidi kwa kipindi kifupi.

  0 0

   Katibu tawala msaidizi utumishi na utawala katika sekretarieti ya mkoa wa Ruvuma  Bw. Biseko Bwai (kushoto) akiangalia maziwa yaliyosindikwa na mjasilimali mdogo aliyefahamika kwa jina moja la mama Tarimo wakati wa kilele cha siku ya wakulima nane nane mkoani Ruvuma jana.

   Afisa kilimo kutoka halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Bw. Jibinza Masaba (kushoto)  akiwaeleza baadhi ya wananchi waliofika katika maonesha ya siku ya wakulima nane nane nyanya ambazo zinaweza kuishi na kuzaa kwa muda wa miezi sita tofauti na nyanya nyingine ambazo zinaishi kwa miezi miwili.
   Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea wakiangalia kibao kinachoonesha aina ya mbegu ya ngano na mahindi yenye uwezo wa kutoa gunia 40 kwa ekari moja katika viwanja vya nanenane  wakati wa kilele cha mnaadhimisho ya siku ya wakulima mkoani Ruvuma. Picha na Muhidin Amri

  0 0


  0 0


  0 0

  Na Thobias Robert- MAELEZO

  Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola Mh. Patricia Scotland (picahni) anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima amesema leo wakati alipokuwa  akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Dkt. Mlima. Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya Madola  atafanya ziara  ya siku tatu nchini kuanzia  Agosti 10 hadi 12 mwaka huu, ambapo atakutana na viongozi wa juu wa serikali ya Tanzania.


  “Lengo la ziara hiyo nchini  ni kuelezea viongozi wa ngazi za juu wa Tanzania kuhusu mageuzi yanayofanywa na Sekrtarieti ya Jumuiya ya Madola na  vipaumbele  vya Jumuiya hiyo  kwa sasa, hatua zinazochukuliwa ili kuimarisha kazi za Jumuiya hiyo na kutoa taarifa kuhusu  Mkutano wa Wakuu wa Nchi na serikali wa Jumuiya unaotarajiwa kufanyika jijini  London nchini Uingereza  mwakani mwezi April” alisema Dkt. Mlima.

  Alifafanua kuwa mageuzi yanayotarajiwa kufanywa na Jumuiya hiyo ni pamoja na kuondoa vyeo vya Naibu Makatibu wakuu watatu na kupunguza idadi ya Wakurugenzi kutoka 12 hadi 6, kuanzisha nafasi tano za Maafisa Waandamizi kutoka maeneo ya kijiografia ya Jumuiya hiyo kwa maana ya Afrika, Ulaya, Amerika, Karibeani, Asia na Pacific Kusini kwa lengo la kuziba nafasi ya Makatibu Wakuu.

  “Mageuzi haya yataiwezesha Jumuiya ya Madola kuokoa kiasi cha Pauni milioni 3 kwa mwaka ambazo zitafanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo,” alifafanua Dkt. Mlima.

  Katika ziara yake nchini,  Katibu Mkuu huyo  wa Jumuiya ya Madola anatarajiwa kukutana na  kufanya  mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Mbali na kukutana na Rais Magufuli,  Katibu Mkuu Scotland  atafanya mazungumzo  na Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.


  Jumuiya ya Madola ilianzishwa karne ya 20 kwa lengo la kuikutanisha Uingereza na yaliyokuwa makoloni yake duniani kwa jukumu la kuhakikisha wanachama wanajikwamua  katika nyanja za Kisiasa, Kiuchumi, kijamii, Michezo na Burudani huku Malkia wa Uingereza ndiye Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo.


  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa tatu kulia), akizungumza na Rais wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Cooporation (CCECC) Bw. Zhao Dianlong kuhusu maendeleo ya ujenzi wa  barabara za maingiliano katika eneo la Ubungo (Ubungo interchange), leo jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia), akizungumza na Makamu wa Rais wa kampuni ya China Harbour Engineering Company Ltd Bw. Liyi .. kuhusu upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Leo Jijini Dar es Salaam.

   Makamu wa Rais wa kampuni ya China Harbour Engineering Company Ltd Bw. Li-yi (Wa tatu kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kushoto), kuhusu shughuli za Upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, leo jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Tanzania  Bw. Song Geum-young (Kulia), kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na nchi yake hapa nchini.


  0 0

  William Henry Gates III maarufu kama Bill Gates na Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft iliyomfanya kuwa mtu tajiri namba moja  duniani na mwanzilishi wa mashirika lukuki yasiyo ya kiserikali yenye kusaidia jamii yupo nchini. Leo ametembelea kijiji cha Kicheba wilayani Muheza katika mkoa wa Tanga kwa lengo la kuangalia maswala mbalimbali ya afya ikiwemo utumiaji wa dawa za mabusha, matende ili kuangalia ni namna gani anaweza kusaidia kwenye sekta hiyo ya Afya.
   Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo (kushoto) akiwa na Bill Gatesbpamoja na mmoja wa viongozi wa kinamama wa wilaya hiyo katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo
  Bill Gates akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa wilaya ya Muheza akiwamo Mkuu wa Wilaya Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo na Mbunge Mhe Adadi Rajabu (wa nne kulia) katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo
  Bill Gates akiwasili na kusalimiana na uongozi wa wilaya ya Muheza katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga leo. 
  Kujua mengi kuhusu Bill Gates BOFYA HAPA


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa kampeni yake Mwakalebela amesema kuwa kwa kwanza ataanza na Utawala bora kwa Kuweka misingi ya wazi katika mapato na matumizi ya TFF, Kuzifanya kamati za TFF kuwa huru na kufanya kazi bila kuingiliwa,uingalia upya Agenda ya kupunguza idadi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ili tuweze kupanua wigo wa wadau wa mpira wa miguu kutuwakilisha kwa wingi katika mkutano mkuu.


  Amesema kuwa pia ataweza kusimamia matakwa ya katiba ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kwa kufanya vikao na mikutano inayotambuliwa kikatiba, kuwa na vyombo imara vya usimamizi ndani ya shirikisho ili kuleta matokeo chanya yenye ufanisi katika soka.


  Mwakalebela amesema ataweza kusaidia Timu za Taifa ,wanaume,Wanawake na Vijana kwa Kuwa na makocha wenye viwango vya juu ikiwa ni pamoja na Kurudisha hamasa kwa watanzania kuzipenda timu za Taifa kwa kuongeza idadi kubwa za wachezaji wa ndani kucheza nje ya nchini pamoja na kucheza FIFA date zote na Kuziweka timu kambini kwa wakati


   
  Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandihi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa akinadi sera zake. 
  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa ni marufuku kuweka bei ya tumbaku kwa dola za Marekani kwa sababu imechangia kuwaumiza wakulima wa zao hilo. 
   Amesema wanunuzi wa zao hilo wana uhuru wa kuweka bei zao kwa dola lakini bei hiyo itafsiriwe kwa shilingi za Kitanzania ili wakulima waweze kutambua bei elekezi tangu mwanzo wa msimu. Ametoa kauli hiyo Jumatano, Agosti 9, 2017 wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora. 
   Hivi sasa bei elekezi kwa msimu huu wa tumbaku ni dola mbili za Marekani kwa kilo moja ya tumbaku sawa na sh. 4,400 hadi sh. 4,500 za Tanzania. 
   Hata hivyo, Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani hapa, alionya juu ya mkanganyiko unaowapata wakulima na viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) kwenye kutafsiri bei ya zao hilo kutoka dola za Marekani. 
   “Kwa mfano, mkulima anapouza tumbaku anaambiwa kilo zake zina thamani ya dola za marekani 90. Wakati anapokuja kulipwa bei ya shilingi inakuwa imebadilika, kwa hiyo kama aliuziwa wakati thamani ya dola moja ikiwa ni sh. 1,500/- na wakati wa kulipwa imefikia sh. 2,000/- hatalipwa kwa bei ya sasa. Bali atalipwa kwa bei ileile ya zamani jambo ambalo linamuumiza mkulima,” amesema. Akiwa hapohapo ukumbini, Waziri Mkuu aliwauliza wawakilishi wa benki za CRDB na NMB bei ya dola moja ni sawa na shilingi ngapi kwa hapo Tabora, alijibiwa kwamba katika benki ya CRDB, dola moja ya Marekani inauzwa kwa sh. 2,200 ilhali katika benki ya NMB, dola moja inauzwa kwa sh. 2,167.


  0 0


  0 0

  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

  Na Mathias Canal, Lindi

  Serikali imesema kuwa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi itaendelea kuwa muhimili na kichocheo katika kujenga uchumi wa viwanda ambao ndio kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli. 

  Hayo yalibainishwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt Charles Tizeba wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, nane nane kitaifa, katika viwanja vya ngongo katika manispaa ya lindi jana tarehe 8/8/2017.

  Dkt Tizeba alisema kuwa kwa ushirikiano na Watumishi wote katika Wizara, amejipanga kuhakikisha kuwa, Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inaendelea kukua sawa sawa na mahitaji ya Wananchi. Alisema kuwa jambo hilo linawezekana ambapo inawezekana kwa kiasi kikubwa kuzalisha malighafi za kutosha za kuwezesha viwanda kuzalisha bidhaa mbalimbali, ambazo zitauzwa ndani na nje ya nchi kwa bei nzuri na ya ushindani. 

  Alisema kuwa kupitia mbinu hiyo wizara itakuwa imefanikisha kuongeza mchango wa Sekta hizo katika uchumi wa Taifa na pia katika kuondoa umaskini kwa Watanzania wengi. Sambamba na hayo pia Mhe Dt Tizeba alisema kuwa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, mabadiliko ya tabianchi, ambayo kwa kiasi kikubwa yanachangia kupungua kwa uzalishaji na tija ya mazao, uhaba wa malisho ya mifugo na rasilimali maji. 

  Katika kukabiliana na jambo hilo Mheshimiwa Dkt Tizeba alisema kuwa Wizara yake imejipanga kuendelea, kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora zinazovumilia ukame, magonjwa na kutoa mavuno mengi. 

  Alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na Wabia wa Maendeleo, wamekamilisha Mpango wa Kilimo Kinachohimili Mabaliliko ya Tabianchi na Miongozi ya uzalishaji mazao, ufugaji na uvuvi. Muongozo wa kilimo umetolewa kulingana na Kanda za Kilimo za Kiteknolojia. Miongozo hiyo, imezinduliwa na kuanza kusambazwa kwa Maafisa Ugani wa Kilimo Mifugo na Uvuvi na kwa wananchi, kuanzia Mwezi, Mei na Juni, 2017. 

  Alisema Mikakati mingine, inayoendelea ni pamoja na kuhakikisha kuwa mbolea bora, inapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu zaidi, sawasawa na agizo la Makamu wa Rais la kuwasaidia Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kupunguza gharama za uzalishaji ili waweze kufaidika na matunda ya juhudi zao. 

  Sambamba na hilo aliongeza kuwa wizara yake imejipanga ili kuhakikisha kuwa inaendelea kuwaelimisha na kuwasaidia Wafugaji wa Tanzania, kufuga kitaalamu zaidi ili kuepuka hali ya kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho na maji. Alisema kuwa jambo hilo litawezesha kufuga kwa tija na pia kupunguza migogoro ya Wakulima na Wafugaji.

  0 0


  0 0

   Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilionea marehemu Maleu Mrema katika ibada ya mazishi yaliyofanyika jana katika hoteli yake ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha(Habari Picha NA Pamela Mollel,Arusha)
  Waziri Mkuu mstaafu,Edward  Lowassa akiweka shada la maua pamoja na mke wake  katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema jana nje kidogo ya jiji la Arusha katika hoteli ya Ngurudoto
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Mrema kwenye ibada ya mazishi yaliyofanyika katika hoteli yake ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha
   Baadhi ya wake za marehemu wakiweka udongo katika kaburi la mpendwa wao

   Waziri Mstaafu wa mambo ya nje Benard Membe akiweka shada la maua katika kaburi la Bilionea Mrema.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Faustine Mrema.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

older | 1 | .... | 1852 | 1853 | (Page 1854) | 1855 | 1856 | .... | 3286 | newer