Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1851 | 1852 | (Page 1853) | 1854 | 1855 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa NHIF akipokea cheti cha ushindi Kutoka kwa  Naibu Waziri -Tamisemi Seleman Jaffo wakati wa maonesho ya nanenane Dodoma.
  Watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wakiwa katika picha ya pamoja.

  MFUKO 
  wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) umeibuka kidedea miongoni mwa mifuko ya hifadhi  ya jamii iliyoshiriki maonesho ya  kumi ya kilimo na ufugaji inayoendelea Mkoani Dodoma.

  Katika maonesho hayo yanayoshirikisha mikoa ya kanda ya kati ya  Dodoma na Singida mfuko wa NHIF ulishika nafasi ya tatu kwa utoaji wa huduma za hifadhi ya jamii.

  Akikabidhi vyeti na zawadi kwa washindi mbalimbali waliofanya vizuri katika maonesho hayo Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa (TAMISEMI), Mh.Selemani Jafo amepongeza jitihada za NHIF na mifuko mingine katika juhudi zao za kumkomboa mtanzania katika nyanja mbalimbali.

  “Lengo letu ni kuyafanya maonesho haya ya nane nane hapa Dodoma yawe ya kimataifa, hivyo tunatambua mchango wa washiriki wote katika kumsaidia mkulima na mfugaji,” amesema Mh.Jafo

  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF  Anjela Mziray amesema tuzo hiyo ni kichocheo kwa mfuko huo katika kuboresha maisha ya Mtanzania.

  Akizungumza mara baada ya kupokea cheti maalumu kutoka kwa Mh.Jafo,Bi Anjela Mziray ameshukuru kamati ya maandalizi ya maonesho hayo kutambua mchango wa mfuko wa NHIF.

  “Tuzo hii kwetu ni motisha tosha ,na pia itatukumbusha kuwa tuna deni la kuwahudumia Watanznia tulichokionesha kwenye maonesho hayo ndio majukumu yetu ya kila siku,” amesisitiza Bi.Mziray.

  Pamoja na hilo Bi Mziray amewataka wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kutembelea Ofisi ya NHIF mkoani humo iliyopo jengo la Hazina Ndogo, barabara ya UDOM ili kujipatia huduma zinazotolewa na mfuko huo.

  Maonesho ya Nane Nane kanda ya kati yamehairishwa leo lakini  kutokana na maombi ya wadau Mh.Jafo ameongeza siku mbili zaidi ili kutoa fursa zaid kwa wananchi wa kanda ya kati na maeneo jirani kuendelea kupata huduma.

  0 0

  RC Makonda aagiza CV za watendaji kata za jiji la Dar es Salaam kupitiwa upya hatua hiyo imefuata baada ya Mkuu huyo wa Mkoa D ar es Salaam  kufika katika eneo la Bunju B jijini humo kwa maelekezo ya Rais Magufuli aliyetoa siku 4 kutatuliwa kero za eneo hilo.

  Katika mkutano na wananchi wa eneo hilo, RC Makonda alilazimika kumuinua mtendaji wa kata hiyo na ndipo alipogundua wengi wao hawaelewi vizuri majukumu yao na ndipo alipomuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Ally Happi kukagua CV za watendaji wake mara moja.

  RC Makonda amedai Watendaji hao kutoelewa majukumu yao ndio imekuwa sababu kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero ndogondogo na hatimaye Wanasubiri Rais akipita wanamsimamisha kwa matatizo madogodogo yakiwemo ya Vyoo, Umeme na masoko.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Bunju B juu ya  Watendaji  wa Kata kutoelewa majukumu yao imekuwa ni   sababu kubwa ya wananchi kushindwa kutatuliwa kero zao.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Allya Hapi akizungumza na waanchi wa Bunju B akifafanua jambo katika mkutano huo.
  Sehemu ya wanchi wakimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
  Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

  0 0


  •    JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUCHUNGUZA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA MTAA WA MABATINI WILAYANI NYAMAGANA.

  KWAMBA TAREHE 08.08.2017 MAJIRA Y A SAA 22:00 USIKU KATIKA MTAA WA MABATINI KATA YA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA T.394 DJW AINA YA TOYOTA HAICE AMBALO LINADAIWA LILIKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA AMINI SHABANI SIZYA MIAKA 28, MNYAMWEZI, MKAZI WA MTAA WA MABATINI. INASEMEKANA KUWA DEREVA WA GARI HILO  WAKATI ALIPOKUWA MAHALI HAPO ALIGEUZA GARI LAKINI ENEO LILIKUWA FINYU HIVYO ALIKWENDA KUGONGA NYUMBA (PUB) ILIYOKUWA PEMBENI  MALI YA BONIFACE NTOBI NA KUVUNJA UKUTA NA KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI NA VITU VYENYE KIASI CHA THAMANI YA TSH 4,000,000/=.

  INASEMEKANA KUWA BAADA YA TUKIO HILO KUTOKEA WANANCHI WALITOA TAARIFA KITUO CHA POLISI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA DEREVA WA GARI HILO, LAKINI IKATOKEA KUTOELEWANA KATI YA ASKARI WENGINE WALIOFIKA ENEO HILO NA MWENYE NYUMBA (PUB) PAMOJA NA WANANCHI NA KUPELEKEA KUZUKA KWA VURUGU AMBAPO WANANCHI WALIANZA KUWARUSHIA ASKARI MAWE NDIPO ASKARI WALIFYATUA RISASI KADHAA HEWANI  HALI ILIYOPELEKEA HOFU  KWA WANANCHI WA ENEO HILO.

  KATIKA VURUGU HIZO MKE WA MWENYE NYUMBA (PUB) BI BETI ATANASI ALIJERUHIWA MGUU WA KULIA JUU YA UNYAYO, LAKINI BADO HAIJATHIBITIKA KUWA JERAHA HILO NI LA KITU GANI KWANI MAJERUHI ANAONGEA NA ANAWEZA KUTEMBEA YUPO HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HIVYO TUNASUBIRI UCHUNGUZI WA KISAYANSI WA DAKTARI ILI KUWEZA KUTHIBITISHA JUU YA JERAHA HILO.

  AIDHA KUFUATIA VURUGU ZILIZOTOKEA KATIKA ENEO HILO NA KUSABABISHA ASKARI KUFYATUA RISASI. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEANZA UCHUNGUZI WA SUALA HILO ILI KUBAINI CHANZO HALISI CHA VURUGU HIZO.
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA, AKIWATAKA KUTULIA WAKATI JESHI LIKIENDELEA NA UCHUGUZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI LIWEZE KUENDELEA KULINDA USALAMA WA RAIA PAMOJA NA MALI ZAO KATIKA MKOA WETU WA MWANZA.

  IMETOLEWA NA;
  DCP: AHMED MSANGI
  KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

  0 0  AZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa magari matatu yenye thamani ya Dola za Marekani 99, 700 kutoka Kampuni ya Foton International Trade Co. Ltd ya nchini China.

  Amepokea msaada huo leo (Jumatano, Agosti 9, 2017) jijini Dar es Salaam, ambapo amesema magari hayo yatatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii nchini. Magari hayo ni Sauvana SUV moja na Tunland Double cabin mbili.

  “Nashukuru kwa msaada huu wa magari uliotolewa na Kampuni ya Foton kwa Serikali yetu. Magari haya yanaweza kutumika katika Hospitali za wilaya kwa ajili ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kutolea elimu mbalimbali kwa umma.”

  Pia, Waziri Mkuu ameikaribisha Kampuni hiyo kuja nchini kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari. Amesema mbali na utulivu wa kisiasa uliopo Tanzania, pia kuna sera na mazingira mazuri ya uwekezaji.

  Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Zhao Xiao amesema wametoa msaada huo wa magari kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Tanzania hususan maeneo ya vijijini.

  Bw. Xiao amesema Kampuni ya Foton inatengeneza magari 700, 000 kwa mwaka, ambayo yanauzwa katika nchi 125 duniani. Amesea ifikapo mwaka 2020 wanatarajia kuongeza uzalishaji na kufikia magari milioni 1.4 kwa mwaka.

  Kuhusu suala la kuja kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari nchini, Bw. Xiao amesema wanampango wa kuwekeza nchini kwa kuwa kuna fursa nzuri za uwekezaji na uhakika wa masoko katika nchi zingine za Afrika Mashariki.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, AGOSTI 9, 2017

  0 0

  Video Courtesy of MCL

  Na Georgina Misama, MAELEZO
  Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba wamekubaliana kumaliza tofauti zao na kuvitaka vyombo vya habari kuanza kuandika habari zinazomuhusu Mkuu wa Mkoa kama ilivyokuwa awali.

  Akiongea na waandishi wa habar jijini Dar es salaam leo, Mwenyekiti wa TEF Theophil Makunga alisema kwamba wiki chache zilizopita viongozi wa jukwaa la Wahariri walikutana na Mkuu wa Mkoa ili kumsikiliza na kufikia muafaka kwa suala la Vyombo vya Habari kususia kazi zake.


  “Adhabu tuliyoitoa haikuwa na muda maalum (Open ended) hivyo tusingeweza kuendelea kukaa katika mgomo huu kwani tayari muda mrefu ulishapita. Tulipoenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, alitueleza mazingira yaliyopelekea yeye kufanya tukio lile Clouds na kwa pamoja tulikubaliana kuyamaliza kwani yaliyopita si ndwele sasa tugange yajayo”. Alisema Makunga.

  Makunga alisema haikuwa rahisi kufikia muafaka huo, kwani walifanya majadiliano na Makonda zaidi ya mara moja hatimaye Alhamisi ya wiki iyopita walihitimisha mazungumzo yao na wote walikubaliana kufanya mkutano huu wa pamoja ili kuujulisha Umma kukoma kwa kifungo cha vyombo vya habari katika kuripoto kazi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.

  Kwa upande wake Makonda alisema kwamba waandishi wote wanafahamu upendo wake kwa vyombo vya habari, jambo ambalo kamwe halitokaa libadilike. Amekuwa tayari kukaa mezani na viongozi wa TEF kwa maslahi ya Umma kwani wote wanafanya kazi moja kwa maendeleo ya Taifa.

  “Tumekubaliana na viongozi wenzangu baada ya kuja ofisini kwangu, kunisikiliza na kunihoji maswali sio chini ya masaa matatu. Mwishoni waliona hakuna haja ya kuendelea na kifungo kwa manufaa ya watanzania, pande zote mbili tumejifunza kutokana na tukio lile, na hatutegemei jambo lile kujirudia tena” Alisema Makonda

  Akiongelea mahusiano yake na  Mutahaba, Mkuu wa Mkoa alisema kwamba wao ni marafiki wa siku nyingi nje ya kazi, na kwa heshima ya Mhe. Rais, wamekubali kuweka tofauti zao pembeni, kusameheana na kupendana ili kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana kama ilivyokuwa awali.

  Akitolea ufafanuzi jambo hilo, Mutahaba alisema kwamba kwake yeye anajiona kama abiria katika lori ambalo Rais ni dereva, anajua tofauti zao na Makonda zimekuwa kero kwa Mhe. Rais hivyo bila kujali kauli yoyote ya Makonda, haoni sababu ya kuendeleza tofauti zao.

  “Mhe. Rais ameshasema jambo hili liishe na tuendee na kazi, sioni sababu ya kuendelea kwa heshima ya kauli yake. Kwangu mimi haijalishi kama Makonda ameomba radhi au hajaomba, lakini naona umuhimum wa kulimaliza jambo hili ili kuruhusu mambo mengine yaendelee kwa maslahi ya Taifa. Alisema Mutahaba.
  Takribani miezi 5 sasa imepita toka TEF kutoa tamko la kususia kazi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es saam Paul Makonda ikiwa ni adhabu baaba ya Makonda kudaiwa kuvamia kituo cha utangazaji cha Clouds.   


  0 0


  0 0

   Mratibu wa Idara ya huduma za jamii wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)  Jimbo la Kusini Mchungaji  Andrew King’omela akizungumza na Mwinjilisti kiongozi wa Mtaa Mwapemba Usharika wa Mtoni Nicolas Mtali wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Mtaa huo iliyofanyika hivi karibuni. Zaidi ya milioni 17 zilipatikana katika harembee hiyo ambayo ilikadiriwa kukusanya kiasi cha milioni 50.
   Mratibu wa Idara ya huduma za jamii wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)  Jimbo la Kusini Mchungaji  Andrew King’omela (kushoto) akizungumza na Mchungaji wa Usharika wa Mtoni Moses Sozigwa (kulia) ambaye ni mlezi wa Mtaa wa Mwapemba wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la Mtaa huo.
    Kwaya ya Uinjilisti ya Mtaa wa Kemete usharika wa Kijitonyama ikiimba wakati wa harembee ya kuchangia ujenzi  wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kusini  Mtaa wa Mwapemba Usharika wa Mtoni iliyofanyika hivi karibuni. Zaidi ya milioni 17 zilipatikana katika harembee hiyo ambayo ilikadiriwa kukusanya kiasi cha milioni 50.
   Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kusini  Mtaa wa Mwapemba Usharika wa Mtoni lenye uwezo wa kuchukuwa waumini 400  na vyumba vya ofisi vitano kama linavyoonekana katika picha.
  Picha na Anna Nkinda.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite BBall Kings 2017 imezidi kupamba moto baada ya timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya fainali   kutambiana.

  Michuano hiyo itakayoendelea wikiendi hii katika Viwanja vya Don Bosco imekuwa ya ushindani mkubwa ikiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza hatua ya fainali.

  Manahodha kutoka timu hizo wametambiana kwa kila mmoja kumuambia mpinzani wake kuwa ajipange katika mchezo huo wa raundi ya kwanza  katika kushindania lile taji la Sprite BBall kings ili kumpata mfalme wa kikapu kwa mwaka 2017.
  Kwa upande wa timu ya mpira wa kikapu ya Mchenga Bball Stars, nahodha wao Mohamed Yusuph amesema kuwa watahakikisha mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya wapinzani wao TMT unamalizika Kwa wao kuwapiga vikapu vya kutosha wapinzani wao.

  Nahodha wa TMT Isihaka Mzinga  ametamba na kuwatahadharisha Mchenga kuwa wajipange vyema, kwani kwa mchezo wa kwanza tu watahakikisha wanaonyesha uwezo wao wa kuibuka wafalme wa kikapu katika  Mashindano ya Sprite BBall kings 2017.

  Mchezo wa kwanza wa Sprite BBall kings 2017, utachezwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay na mshindi wa kwanza wa mashindano haya ataondoka na kitita cha shilingi milioni 10 ,mshindi wa pili milioni 3, na mchezaji bora milioni 2.
  Sprite BBall kings 2017, ni kwa udhamini mkubwa kabisa wa kinywaji cha Sprite.

  0 0


  Na Karama Kenyunko Globu ya jamii.

  Mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ali Mayay amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha dira ya mpira wa miguu inarejea katika mstari na  kuiwezesha nchi kupata maendeleo makubwa katika sekta hiyo.

  Mayay amesema hayo leo alipokuwa ananadi sera zake katika siku ya kwanza ya uzinduzi wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF utakaofanyika Agosti 12, mkoani Dodoma. Amesema kuwa kwa sasa hakuna dira ya mpira wa miguu na ndio chanzo cha kuwa na maendeleo duni ya mpira kulinganisha na nchi zingine ambayo kwa sasa zinafaidi matunda baada ya kuanzisha na kutekeleza dira hiyo.

  “Kwa sasa wachezaji wengi wa Zambia wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi, timu yao Taifa inafanya vizuri, Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, lakini hakuna dira na kusababisha wao pia kukosa dira katika fani yao,” alisema Mayay.

  Alisema kuwa akiwa kama mchezaji, ameweza kuona changamoto mbalimbali za mpira wa miguu na kuamua kugombea nafasi iliyo ili kuzitatua na  lengo lingine ni kujenga taasisi imara kwa kutumia rasilimali zilizopo kwani tatizo si vipaji, bali ni aina gani ya uongozi unaosimamia mpira wa miguu.

  Wachezaji mbalimbali waliong’aa katika medani ya soka hapa nchini, wamepigia chapuo mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Ali Mayay kuchaguliwa katika nafasi ya urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

  Mgombea huyo ambaye ni chaguo la wachezaji wa zamani nchini aliungwa mkono na mshambuliaji nyota wa zamani wa Klabu ya Simba,  Zamoyoni Mogella ambaye alisema TFF inahitaji mtu kama Mayay anayejua matatizo ya mpira wa miguu kwani ameucheza huo mpira.

   Mogella ambaye enzi zake alipewa jina la “Golden Boy” na “Morgan” alisema kuwa wanahitaji kuurudisha mpira kwa wenyewe huku wakiwaomba wagombea kumchagua Mayay kwani ni wakati wa mabadiliko kwa wadau wa soka nchini kwa kumchagua Mayay ambaye anavigezo vyote katika masuala mbalimbali ya soka na uongozi.

  “Mayay ni dira ya soka Tanzania, amecheza soka kuanzia shuleni, katika hatua ya vilabu mpaka timu ya Taifa, anajua nini cha kufanya ili kuleta maendeleo ya soka nchini,” alisema Mogella.

  Mchezaji wa zamani wa Yanga Mohamed “Adolph” Rishad naye alisema kuwa  Mayay ni suluhisho sahihi kwa maendeleo ya soka nchini na si wagombea wengine zaidi wachezaji wa mpira wa miguu wametengwa katika soka na kukosa mwamko katika mchezo ambao wanaupenda.

  Amesema kuwa kwa sasa Tanzania ina matokeo mabaya katika soka la kimataifa ni kukosa uongozi wenye mapenzi ya mchezo pamoja na Tanzania kuwa na vipaji vingi vya soka.
  Mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ali Mayay akizungumza na waandishi wa habari akinadi sera zake za kuelekea Uchaguzi  Mkuu wa TFF utakaofanyika Agosti 12, mkoani Dodoma, Kushoto ni  mshambuliaji nyota wa zamani wa Klabu ya Simba,  Zamoyoni Mogella

  0 0

  --
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Majadiliano ya Ngazi za Juu kati ya Serikali na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR).Majadiliano hayo yamehusu masuala ya uhifadhi wakimbizi   na suluhisho la kudumu la wakimbizi walioko katika Kambi mbalimbali nchini.Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam
    Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya, akichangia hoja wakati wa Kikao cha Majadiliano ya Ngazi za Juu kati ya Serikali na Shirika hilo .Majadiliano hayo yamehusu masuala ya uhifadhi wa wakimbizi na suluhisho la kudumu la wakimbizi   walioko katika Kambi mbalimbali nchini.Kushoto ni Makamu Kamishna Mkuu wa Shirika hilo, Volker Turk .Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam
   Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani,   akichangia hoja wakati wa Kikao cha Majadiliano ya Ngazi za Juu kati ya Serikali na Shirika hilo. Majadiliano hayo yamehusu masuala ya  uhifadhi wakimbizi na suluhisho la kudumu la wakimbizi   walioko katika Kambi mbalimbali nchini..Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam
   Mratibu wa Mpango wa Kuwahudumia wakimbizi  ,Dkt. John Jingu, akizungumza wakati wa Kikao cha Majadiliano ya Ngazi za Juu kati ya Serikali na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR).Majadiliano hayo yamehusu masuala ya wakimbizi   na suluhisho la kudumu la wakimbizi walioko katika Kambi mbalimbali nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa CSFM, Prof. Bonaventure Rutinwa. Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wanne kulia waliokaa), Makamu Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Volker Turk(watano kulia waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na washriki wa Kikao cha Majadiliano ya Ngazi za Juu kati ya Serikali na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR).Majadiliano hayo yamehusu masuala ya  uhifadhi wakimbizi   na suluhisho la kudumu la wakimbizi walioko katika Kambi mbalimbali nchini.Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo , Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZBC pamoja na Uongozi wa ZBC leo   katika kikao cha siku moja kilichofanyika katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
   Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBC Bi. Nasra Mohamed (kulia)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo na Uongozi wa ZBC, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),(kushoto) Mjumbe wa Bodi Nd,Ali Bakari
   Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Nd,Iman Othman Duwe (kulia) alipokuwa akitoa maelezo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo  katika kikao cha siku moja cha  Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo, Bodi ya Wakurugenzi ya ZBC na Uongozi wa ZBC,ambacho kikao hicho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji ya ZBC na Bodi kwa pamoja, (kushoto) Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikalini Mhe.Mohamed Fakih.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,Bodi ya  Wakurugenzi  ya ZBS pamoja na Uongozi wa ZBS     katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
   Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBS Prof Ali Seif Mshimba (kushoto)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Biashara,Viwanda na Masoko na Uongozi wa  ZBS, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), (kulia) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Nd,Said Hassan Said
  Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBS Prof. Ali Seif Mshimba (kulia)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Biashara,Viwanda na Masoko na Uongozi wa  ZBS, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), wengine ni baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya ZBS wakisikiliza kwa makini taarifa hiyo (Picha na Ikulu).

  0 0

  Wanachama wa klabu ya simba kutoka hapa songea wamejitokeza kwa wingi katika hospitali ya rufaa ya songea kwa lengo la kuwa fariji wagonjwa,lakini walipata nafasi ya kufanya usafi katika maeneo hayo na kutoa damu kwa watu wenye mahitaji.

  0 0

  Dk. Kigwangalla aagiza TAKUKURU kuwahoji waliokuwa viongozi wa TASO Kanda ya Mashariki Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro kuwakamata mara moja waliokuwa viongozi wa chama cha wakulima Tanzania TASO kanda ya mashariki kutokana na ubadhirifu wa fedha walioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

   Dk Kingwangala alitoa agizo hili mara baada ya kupokea taarifa za kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Mh. Dk. Steven Kebwe juu ya walioukuwa viongozi wa Taso kanda ya Mashariki kushirikiana kuuza baada ya maeneo kwa wananchi ndani ya uwanja wa maonyesho ya mwalimu Juliaus Nyerere nanenane ulipo mkoani Morogoro. 

  Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele hicho cha Nane nane akimwakilisha Makamu wa Rais Mama Samia Salum, ameagiza kuchukuliwa hatua za haraka viongozi hao huku akieleza kuwa kutokana na usajili wamashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuwa ndani ya wizara yake ni, vyema viongozi hao wakatafutwa na kukamatwa ili waweze kujibu tuhuma zinazowakabili. “Kwa mamlaka, tunawaagiza Mkuu wa TAKUKURU kuhakikisha wanawakamata viongozi wa TASO haraka ilikuweza kurudisha mali zote ikiwemo walizowauzia wananchi viwanja ndani ya maeneo haya. 

  Taasisi ama NGO’s zikifilisiwa mali zote ni za Serikali na zinakuwa chini ya uangalizi wa Serikali hivyo hatua kali zitachukuliwa kwa wale waote waliohusika” alieleza Dk. Kigwangalla katika tukio hilo la kufunga kilele cha maadhimisho ya Nane nane, Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar e s Salaam, katika Banda la Mwalimu Julius Nyerere. Dk. Kigwangalla pia ameweza kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwemo Vyeti, hundi za fedha pamoja na vikombe vya ushindi kwa taasisi na mashirika na wadau walioshiriki maonyesho hayo. 

  Hata hivyo Dk. Kigwangalla ameongeza siku mbili zaidi kuendelea kwa maonyesho hayo ambayo yaendelea leo na kesho Alhamisi Agosti 10,2017. Awali amepata Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea mabanda mbalimbali ndani ya viwanja hivyo huku akijionea mazao ya kilimo na ufugaji wa kila aina pamoja na bidhaa zitokanazo na kilimo za wadau wa ndani. 
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia namna mashine ya kukoboa mahindi ya kisasa inavyofanya kazi ambayo itakuwa msaada kwa wakulima hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia bidhaa za usindikaji kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia bidhaa za usindikaji kutoka kwa wakulima wa ndani hapa nchini kwenye viwanja vya maonyesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki inayohusisha mikoa ya Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi kilele cha Nane nane, 8 Agosti 2017
  Baadhi ya viongozi wakiangalia bidhaa za ngozi kutoka kwa Mjasiriiamali kutoka Tanga kwenye maonyesho hayo.


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Majadiliano ya Ngazi za Juu kati ya Serikali na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR).Majadiliano hayo yamehusu masuala ya uhifadhi wakimbizi   na suluhisho la kudumu la wakimbizi walioko katika Kambi mbalimbali nchini.Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam
    Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Tanzania, Chansa Kapaya, akichangia hoja wakati wa Kikao cha Majadiliano ya Ngazi za Juu kati ya Serikali na Shirika hilo .Majadiliano hayo yamehusu masuala ya uhifadhi wa wakimbizi na suluhisho la kudumu la wakimbizi   walioko katika Kambi mbalimbali nchini.Kushoto ni Makamu Kamishna Mkuu wa Shirika hilo, Volker Turk .Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (wanne kulia waliokaa), Makamu Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Volker Turk(watano kulia waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na washriki wa Kikao cha Majadiliano ya Ngazi za Juu kati ya Serikali na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR).Majadiliano hayo yamehusu masuala ya  uhifadhi wakimbizi   na suluhisho la kudumu la wakimbizi walioko katika Kambi mbalimbali nchini.Kikao hicho kimefanyika leo, jijini Dar es Salaam.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi. Sophia Mjema mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere akitokea mkoani Lindi ambako alifunga maadhimisho ya 24 ya sherehe ya Siku ya Mkulima (Nane Nane) kwenye viwanja vya Ngongo jana. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Na Erasto Ching’oro- WAMJW.

  Katika kuhakikisha Taifa linakuwa na Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ambayo ni shirikishi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeandaa kikao kazi kwa ajili ya kukusanya maoni zaidi yatakayosaidia kuhuisha sera hiyo.

  Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga mara baada ya kikao na wadau kutoka taasisi mbalimbali katika mwendelezo wa mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya ambayo yatasaidia kubaini mapungufu, na changamoto zilizopo katika Sera iliyopo na hivyo kusaidia uboreshaji wa Sera hiyo kwa kuzingatia mahitaji ya kijinsia kwa ajili ya maendeleo ya wanawake, wanaume, wavulana wasichana na watoto.

  “Sera iliyopo ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 imechukua muda mrefu kufanyiwa tahmini kutokana na ukweli kuwa zoezi la tathmini linahitaji muda wa kutosha sanjari na uhakikika wa upatikanaji wa rasimali fedha kufanikisha kazi hii” alisema Bibi Sihaba.

  Kwa upande wake Msauri Mwelekezi Profesa Linda Muhando aliipongeza Wizara kwa kuridhia mchakato wa kutathmini sera hiyo na kujumuisha wadau hatua amabyo itasaidia kupata mchango wa wananchi wengi zaidi na kuwezesha kupata masuala mapya amabyo hayako kwenye sera hiyo na kuyajumuisha katika rasimu ya sera inayofanyiwa mapitio.

  Kikao kazi cha tathmini ya Sera hiyo kinatoa fursa kwa wadau kuibua changamoto, mapungufu yaliyopo na kuimarisha uzingatiaji wa mahitaji ya wanawake na wanaume ili kutoa fursa sawa ya upatikani haki na usawa kwa watu wote.

  Maandalizi ya uboreshaji wa Sera hii utajumuisha usambazaji wa sera kwa wananchi, kutoa elimu kwa umma ili kufahamu mwongozo wa kisera, na kuiweka katika lugha nyepesi ili kujenga ufahamu wa wananchi katika wigo mpana zaidi. Aidha, ukusanyaji wa maoni ya wadau utasaidia kupanua ushirikishaji wa wananchi katika kuandaa sera na kufanikisha utekelezaji wake kwa kuzingatia wakati.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) akifungua kikao kazi cha wadau (hawapo pichani) waliokuta kutathmini Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kilichofanyika katika ukumbi wa jengo la Wizara Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017 kulia  ni Mkurugenzi wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba (kulia) na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi.
    Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi (aliyesimama) akibainisha malengo ya kikao cha wadau (hawapo pichani) wanaokutana kutathmini Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia katika ukumbi wa Ofisi ndogo za Wizara ulioko Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017 Kulia ni Katibu Mkuu Sihaba Nkinga.
  Baadhi ya wadau wanaoshiriki kikao kazi cha kutathmini Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia kutoka taasisi mbalimbali wakifuatilia mada mbaimbali katika kikao kinachofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ulioko Magogoni Jijini Dar es salaam leo 9 Agosti, 2017.
  Picha na Erasto Ching’oro WAMJW.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

  Mgombea wa Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Shija Richard ameanza rasmi harakati za kufungua kampeni yake ya kuwania nafasi ya urais wa shirikisho hilo hapa nchini. 

  Shija amezungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam nia na madhumuni ni kufungua rasmi zoezi la kampeni yake ambayo imejikita  kuzungumzia sera zaidi ya TFF  badala ya  maswala ya kiutendaji

  Mgombea huyo amesema kuwa atahakikisha  kunakuwepo na sport Academi katika kanda sita hapa nchini, hii itaongeza vipaji vingi vya kabumbu na  kuwashawishi  wazazi wanapeleka watoto wao wenye vipaji katika  shule hizo za mafunzo ya mpira.

  Hata hivyo Shija amesema kumekuwa na tatizo kubwa kwa klabu kukosa kuwa na uwanja, na hilo pia husababisha kutofanya vizuri kimataifa hivyo amesema atahakikisha anatafuta wadhamini kujikita katika swala zima la miundo mbinu ili kila klabu kujengewa kiwanja chake

  Amesema ili kucheza mpira kwa amani na utulivu bila kupendelea upande mmoja wa timu  ataweka mkakati kwa kushirikiana na vyama vingine vya michezo duniani kote ili kuleta ufanisi kwenye mchezo huo hapa nchini.

  Uchanguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti  mwaka huu mjini Dodoma ambapo wagombea hao wa  kiti cha urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) ni Shija Richard, Wallace Karia, Iman Madega, Ally Mayay,  na Emmanuel Kimbe.
  Mgombea urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Shija Richard akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna atakavyofanya kampeni zake alizozizundua leo rasmi na akiahidi maendeleo ikiwemo na kujenga shule za akadeni ya kabumbu katika kanda sita 6 nchini.

  0 0


  0 0

  ⁠⁠⁠Na Agness Francis, Globu ya Jamii 

  Mgombea nafasi ya urais wa shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF),Iman Omary Madega amesema atashirikiana na klabu za soka kwa ajili ya kuleta maendeleo ya soka ya nchini pamoja na kuhakikisha wanapatikana wadhamini watakaosaidia maendeleo zaidi.

  Madega ambaye ni mwanasheria wa kujitegemea, pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga amenadi sera zake leo Jijini Dar es salaam  kuelekea uchaguzi mkuu wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 Mkoani Dodoma.

   Akinadi Sera zake ambazo zinalenga hasa katika uadilifu,utendaji na uwazi amesema kuwa atakuwa bega kwa bega na klabu zote bila kubagua endapo atachaguliwa kuwa Rais wa shirikisho la kabumbu nchini kuachilia mbali kuwa aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga mwaka 2005-2010 chini ya uongozi wa Leodger Tenga na kuwataka wapenda soka kuondoa shaka kwa hilo.

   Madega amesema ili kuweza kuongoza vizuri tasnia hii ya soka inaitaji muda ili kufanikisha utendaji mzuri wa kazi na kupiga hatua mbele zaidi katika soka.

   Mgombea huyo amesema lengo lake ataakikisha analeta mafanikio katikan sekta ya soka nchini kwa kuwapandisha Tanzania kutoka viwango vya sasa 120 vilivyopo kwa sasa na kushuka zaidi chini ili kuwa katika viwango bora duniani.

  Katika soka la wanawake, Madega amehakikisha kuwa atatenga bajeti ya kutosha itokanayo na wadhamini ili waweze kucheza soka la mikoa yote nchini ili kukuza vipaji zaidi na ili kuwa na maendeleo hayo na kufikia hatua ya kimataifa atahakikisha anaboresha mahusiano mazuri kati ya TFf na serikali yetu,kuboresha viwanja vya mpira nchini, pamoja makocha wazuri na waamuzi wenye uwezo mkubwa wa kuchezesha mechi za kimataifa.

   Madega ametoa wito kwa wapiga kura kumchagua kuwa kinara katika uchaguzi huo wa shirikisho La soka Tanzania (TFF) utakaofanyika tarehe 12 agosti mwaka huu mjini Dodoma.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa magari matatu yenye thamani ya Dola za Marekani 99,700 kutoka Kampuni ya Foton International Trade Co. Ltd ya nchini China.

  Amepokea msaada huo leo (Jumatano, Agosti 9, 2017) jijini Dar es Salaam, ambapo amesema magari hayo yatatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya jamii nchini. Magari hayo ni Sauvana SUV moja na Tunland Double cabin mbili.

  “Nashukuru kwa msaada huu wa magari uliotolewa na Kampuni ya Foton kwa Serikali yetu. Magari haya yanaweza kutumika katika Hospitali za wilaya kwa ajili ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kutolea elimu mbalimbali kwa umma.”

  Pia, Waziri Mkuu ameikaribisha Kampuni hiyo kuja nchini kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari. Amesema mbali na utulivu wa kisiasa uliopo Tanzania, pia kuna sera na mazingira mazuri ya uwekezaji.

  Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Zhao Xiao amesema wametoa msaada huo wa magari kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Tanzania hususan maeneo ya vijijini.

  Bw. Xiao amesema Kampuni ya Foton inatengeneza magari 700,000 kwa mwaka, ambayo  yanauzwa katika nchi 125 duniani. Amesea ifikapo mwaka 2020 wanatarajia kuongeza uzalishaji na kufikia magari milioni 1.4 kwa mwaka.

  Kuhusu suala la kuja kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari nchini, Bw. Xiao amesema wanampango wa kuwekeza nchini kwa kuwa  kuna fursa nzuri za uwekezaji na uhakika wa masoko katika nchi zingine za Afrika Mashariki.
                                                     
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, AGOSTI 9, 2017
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Funguo za Magari matatu yenye thamani ya Dola za kimarekani 99,700 ambayo amekabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano Kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo nchini Tanzania, wanaoshuhudia kutoka kushoto  ni Meneja masoko wa kampuni ya Simba Motors Taanzania Bibi Ifigenia Salazar na kutoka kulia ni Afisa masoko wa Foton International, Bwana Fan Liang. Makabidhiano hayo yamefanyika leo ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia moja ya magari aliyokabidhiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Foton International kutoka China Bwana Zhao Xiano Kwa ajili ya kusaidia shughuli zamaendeleo nchini Tanzania Makabidhiano hayo yamefanyika leo ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es salaam.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


older | 1 | .... | 1851 | 1852 | (Page 1853) | 1854 | 1855 | .... | 3285 | newer