Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1850 | 1851 | (Page 1852) | 1853 | 1854 | .... | 3278 | newer

  0 0  0 0

   The Government has set aside 6.7 for improving teaching and learning environment at the Dar es Salaam based National Institute of Transport (NIT)
  Addressing journalists in Dar es Salaam over the weekend, NIT Rector, Prof. Zacharia Mganilwa said that the money was allocated in the  2017/18 fiscal year budget and will transform the teaching and enabling environment of the institute, hence make it it produce competent experts who can be able to compete in the competitive labour market.

  Prof. Mganilwa said NIT was determined to produce expert who meet the current national market demands, particularly at this time when the country is involving in the construction of Hoima-Tanga crude oil pipeline as well as expansion of country’s ports and other social activities.

  It is fully accredited with the National Council for Technical Education (NACTE) and provide Competence Based Education and Training (CBET) programmes at the level of Certificate, Diploma and Degree (National Technical Awards – NTA level 4 to level 8). The system gives a student the capacity to ably compete in the labour market.

  Prof. Mganilwa said the Institute offers different courses ranging from logistic and transport management, freight clearing and forwarding, aviation studies, procurement and logistics management, automobile engineering, business administration, computing information and communication technology, mechanical engineering, accounting and finance, marketing and public relations and human resources management

   Students at the college campus
   Bird's eye view of the campus
   Newly built Institute building in  the rehabilitation process
  National Institute of Transport Rector Prof. Zacharia Mganilwa

   Aviation engineering students during class 


  0 0

  Marefarii na majaji wa mchezo wa masumbwi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrisson Mwakyembe wakati wa kumpongeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Kampeni za wagombea mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika shirikisho, zinaendelea. Kwa mujibu wa kanuni 11.10 ya uchagizi wa TFF, kampeni hizo za wiki moja hadi Ijumaa wiki hii ambako Uchaguzi Mkuu utafanyika Agosti 12, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hosteli ya Mtakatifu Gasper mjini Dodoma. 
  Kwa mujibu wa kamati hiyo iliyokutana Jumamosi Agosti 5 2017, wagombea ambao wanawania urais ni pamoja na Wallace Karia, Imani Madega, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayay, Shija Richard na Emmanuel Kimbe.
  Katika nafasi ya Makamu wa Rais wanaowania ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa. 
  Kanda namba 1 ya Mikoa ya Kagera na Geita: waliopitishwa ni Saloum Chama, Leopold Mukebezi na Kaliro Samson wakati Kanda namba 2 inayounganisha mikoa ya Mara na Mwanza wamo Aaron Nyanda, Vedastus Lufano, Samwel Daniel na Ephraim Majinge. 
  Kanda namba 3 (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu) wanaowania nafasi hiyo ni Stanslaus Nyongo, Bannista Rogora na Mbasha Matutu ilihali Kanda namba 4 (Mikoa ya Arusha na Manyara) waliopitishwa ni Omar Walii, Sarah Chao na Peter Temu. 
   Katika Kanda namba 5 inayounganisha mikoa ya Kigoma na Tabora waliopitishwa ni John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael wakati Kenneth Pesambili na Baraka Mazengo – wote wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 6 yenye mikoa ya Katavi na Rukwa. Kanda namba 7 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa waliopitishwa ni Elias Mwanjala, Cyprian Kuyava na Erick Ambakisye huku Kanda namba 8 yenye mikoa ya Njombe na Ruvuma waliopitishwa ni James Mhagama, Golden Sanga, Vicent Majili na Yono Kevela. 
   Kanda namba 9 Lindi na Mtwara ambako Athumani Kambi na Dunstan Mkundi (wamepitishwa) wakati Kanda namba 10 Dodoma na Singida waliopitishwa ni Hussein Mwamba, Steward Masima, Ally Suru na George Komba.
   Kanda namba 11, mikoa ya Pwani na Morogoro waliopitishwa ni Charles Mwakambaya, Gabriel Mkwawe na Francis Ndulane wakati Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga waliopitishwa ni Khalid Mohamed na Godluck Moshi. 
   Kanda namba 13 Dar es Salaam: waliopitishwa ni Emmanuel Kazimoto, Abdul Sauko, Ayoub Nyenzi, Shaffi Dauda, Peter Mhinzi, Lameck Nyambaya, Mussa Kissoky, Said Tully, Ally Kamtande, Aziz Khalfan, Ramadhani Nassib na Saad Kawemba. 
   Hii sasa ni orodha ya mwisho baada ya baadhi ya wagombea kufanikiwa kushinda rufaa zao katika Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakipinga kuondolewa na Kamati ya Uchaguzi. 
   Kamati ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kueleza kuwa iliwakamata viongozi wa soka kutoka mikoa mbalimbali katika mazingira ya kuvunja sheria za nchi na kanuni za uchaguzi. 
   Kamati iliamua kuwaondoa wagombea hao ambao ni Shafii Dauda wa Dar es Salaam; Banista Rugora wa Shinyanga; Ephraim Majinge wa Mara na Elias Mwanjala wa Mbeya katika kuwania nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi ujao wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu kwa ukiu
  kwaji wa Kanuni ya 14 (3) inayozungumzia kampeni kabla ya wakati.

  0 0

  Na Eliafile Solla

  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.

  Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.

  Majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.

  Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.

  Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.

  Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.

  Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.

   Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumika.

  Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0
  0 0


  Na Fredy Mgunda, Mbeya

  Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani iringa imeshika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane ambao huhusisha maswala ya kilimo yaliyofanyikia jijini mbeya kwa kanda ya nyanda za juu kusini na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka mikoa yote ya nyanda za juu kusini.

  Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi ya kuwa washidi wa tatu wa maonyesho hayo ya nane nane  mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah aliwapongeza wananchi na viongozi wa wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika maonyesho hayo kwa kile walichokifanya na kuonyesha kuwa Kilolo Kilimo kinasaidia kuinua kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

  "Mimi niwashukuru sana kwa zawadi waliyotupa wananchi na viongozi wa Wilaya ya Kilolo maana ushindani ulikuwa mkubwa mno hasa ukiangalia wilaya zote za nyanda za juu kusini zinasifika sana kwa Kilimo cha mazao mbalimbali na ufugaji hivyo haikuwa rahisi sana kufika hapa mwaka huu"alisema Abdallah

  Abdallah alisema kuwa atakaa na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Kupanga mikakati madhubuti ili mwakani waweze kushika nafasi ya kwanza na kuwa wilaya ya mfano huku nyanda za juu kusini hata Tanzania kwa ujumla.

  "Sasa kazi imeanza na nitahakikisha kila kitu mwakani kitakuwa vizuri na tutafanya vizuri sana kwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ina maeneo mengi mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo na ufugaji hivyo lazima tutatafuta njia mbada ya kuinua Kilimo cha wilaya ya Kilolo" alisema Abdallah

  Aidha Abdallah alisema mikakati yake ni kuboresha pale walipokwama ili kupata matokeo chanya katika maonyesho yajayo.

  "Mikakati iliyopo ni kwamba mwisho wa maonesho haya ndiyo mwanzo wa maonesho mengine, tumegundua vitu vilivyotufanya kuwa namba tatu ni pamoja na ubunifu, hivyo tutazidi kuwa wabunifu kwa maonesho yajayo ili tufikie ushindi mnono zaidi" alisema Abdallah


  Mgeni rasmi katika kilele cha Maonyesho haya alikuwa waziri wa ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za Mitaa MHE. George B. Simbachawene akimkabidhi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah tuzo ya mshindi wa tatu sambamba na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Aloyce Kwezi.Katikati DC wa kilolo Asia Abdallah , kushoto aliyeshika hati, Mkurugenzi Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi na mwishoni kwa Mkurugenzi ni Dkt. Mwingira Afisa Mifugo mkuu Wilaya na kulia tena huku ni Afisa Kilimo mkuu Wilaya ndgu. Kuziwa..


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Utalii,Prof Kitila Mkumbo akizindua tenki la Maji katika eneo la Shabaha kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakuruenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Prof Faustine Bee na kushoto mwa katbu Mkuu ni Mjumbe wa Bodi hiyo ,Bi Hajira Mmambe.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Prof Kitila Mkumbo akiwabebesha maji wawakilishi wa wananchi wa kijiji cha Newland mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika eneo hilo.


  0 0

  Na ELIAFILE SOLLA

  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.

  Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.

  Majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.

  Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.

  Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.

  Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.

  Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni. Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumika. Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. 

  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akizungumza na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto), wakati wa ziara ya kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, lengo ikiwa ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu,Utolewaji wa visa,udhibiti uingiaji wa dawa za kulevya  na uingiaji na utunzaji kumbukumbu za watalii wanaoingia nchini.Kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza swali Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wan DEGE wa Kimataifa Julius Nyerere, Fulgence Mutarasha,  wakati wa ziara iliyowajumuisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, lengo ikiwa ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu,Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
   Mkuu wa Kitengo cha Uzingatiaji Viwango wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, Paul Rwegasha, akifafanua jambo wakati wa ziara iliyojumuisha  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani(kushoto), Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wapili kushoto)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).Lengo la ziara hiyo ni kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu,Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
   Meneja Huduma za Abiria wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Damas Temba, akielezea jinsi huduma ya kukagua mizigo inavyofanyika katika sehemu ya mizigo wakati wa ziara ya Manaibu Waziri, Mhandisi Hamad Masauni (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi), Mhandisi Ramo Makani(Wizara ya Maliasili na Utalii) na Mhandisi Edwin Ngonyani(Wizara ya UIjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), ikiwa na lengo kukagua masuala mbalimbali ikiwemo Ulinzi, Usalama, Miundombinu, Utolewaji wa visa, uingiaji na utunzaji kumbukumbu za Watalii wanaoingia nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Lindi.

  WANANCHI wa Mkoa wa Lindi wamehamasishwa kutumia mashine ya kukatia mbao  (WOODMISER ) ili kurahisha kazi pamoja na muda kwa kutumia mashine za zamani.

  Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya Nanenane mkoani Lindi, Meneja wa Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za  Misitu nchini, Grlory Mziray amesema kuwa mashine hiyo ni nzuri kwa matumizi ya kukatika magogo  na kuzalisha mbao nyingi kutokana na mabaki yake kuwa madogo ukilinganisha na mashine zingine.

  Amesema kuwa huduma zinazosimamiwa na wakala za misitu unahamasisha wananchi kuwa uhifadhi wa misitu ni jukumu la kila mtanzania katika kuitunza na kuisimamia ili kuhakikisha faida zake zinatumika kwa kwa kizazi kilichopo na cha baadae.

  “Misitu ni hewa tunayovuta misitu ni maji pamoja na rutuba ya ardhi yetu inategemea misitu , misitu hiyo hiyo inategemea kuitunza”amesema Glory

  Amesema nyuki ni bidhaa isiyohitaji kulindwa lakini inatoa bidhaa tano zinazoweza kusaidia kutunza misitu hiyo wananchi wanahitaji kupatiwa elimu ya ufugaji nyuki kutoka kwa wakala wa huduma za misitu ambazo ziko katika kila wilaya ili waweze kutumia fursa zilizopo zitokazo na asali katika kwenda katika uchumi wa viwanda wa serikali ya awamu ya tano kutokana na kuwepo kwa masoko makubwa ya asali.

   Wananchi wakiangalia mashine ya kukatia magogo katika maonesho ya Nanenane yaliyofikia mwisho jana katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Paul Nyelu akiwapa maelezo wananchi  na wanafunzi waliotembelea banda Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya vipindi vya historia ambayo nchi imepita  katika katika maonesho ya Nanenane yaliyofikia mwisho jana katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Afisa wa Misitu, Ahazi Shayo akitoa maelezo juu ya huduma za wakala wa misitu inavyofanya kazi katika maonesho ya Nanenane yaliyofikia mwisho jana katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Wananchi wakiwa  katika sherehe za Nanenane katika maonesho yaliyofikia mwisho jana katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Suleiman Jafo amezitaka halmashauri zote nchini kutekeleza jukumu lao la kuwapelekea wakulima wa vijijini teknolojia na pembejeo bora ili kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji mali.

  Jafo ametoa rai hiyo jana wakati wa kilele cha maonyesho ya nanenane kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Singida na Dodoma ambapo alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali yalioonyesha shughuli za kilimo na ufugaji pamoja na sekta binafsi zinazosaidia katika kukuza uchumi.

  Amesema kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa mwaka huu ni “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” hivyo basi halmashauri zinatakiwa kuhakikisha mazao ya wakulima na wafugaji yanapata soko kwa kutoa elimu ya kuchakata na kufungasha bidhaa zao katika ubora unaokubalika sokoni ili mazao hayo yawe na thamani zaidi.

  Jafo amesema halmashauri zote zinapaswa kutekeleza wajibu wao kwa kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na kuhakikisha maeneo hayo yanakuwa na huduma zote za msingi kama vile miundombinu ya Barabara, Umeme na Maji ili kuwavutia wawekezaji na hivyo kumsaidia mkulima na mfugaji kufikia uchumi wa kati.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Ole Nasha ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa kuendelea kuwezesha shughuli za kilimo nchini huku akitoa angalizo la kutowasahau wakulima wasio na uwezo.

  Ole Nasha amesema Benki hiyo isitoe mikopo kwa wakulima wakubwa na wenye uwezo tu bali isisahau jukumu la kuwafikia wakulima wasio na uwezo ili waweze kupata mikopo na kuweza kulima kisasa kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi.

  Wakati huo huo Naibu waziri Jafo ametoa Wito kwa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuamua kuufanya Mkoa wa Dodoma hasa Viwanja vya Nzuguni kuwa Kituo cha Kudumu cha Maonesho ya nanenane kitaifa kutokana na Kijiografia kuwa katikati na Makao Makuu ya nchi na hivyo kuwa rahisi kwa Kanda zote nchini na hata nchi za jirani kuja kushiriki Maonesho ya Nane Nane.

  Jafo amesema hayo akiunga mkono kauli iliyotolewa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dkt. Charles Tizeba aliyesema Serikali inafikiria kuachana na utaratibu wa kuhamisha  hamisha Maonesho ya kitaifa ya Nane Nane kwenye Kanda mbalimbali na badala yake kuwa na kituo kimoja cha Kitaifa kama ilivyo kwa maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanavyofanyika Dar es Salaam pekee.

  Jafo amesema Uwanja wa Nane Nane Nzuguni unahitaji kufanyiwa uwekezaji na uendelezaji wa miundombinu yake kama barabara, umeme na maji na kuboreshwa huduma mbalimbali na kuzitaka Mamlaka za Serikali za Mikoa ya Dodoma na Singida kuweka mkakati wa kuendeleza miundombinu hiyo kwa kuwa baada ya uwekezaji mkubwa uwanja huo utarejesha mapato mengi.

  Ameongeza kuwa Serikali za Mikoa ya Singida na Dodoma inaweza kufanikisha ukarabati huo kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Taasisi kama Benki ya Uwekezaji TIB na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB.

  Washindi wa Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati yaliyoanza tangu Agosti Mosi ni Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) lililoibuka kuwa Mshindi wa jumla wa Maonesho ya Mwaka huu, likifuatiwa na Benki Kuu ya Tanzania ikiwa mshindi wa pili na Mshindi wa tatu akiwa ni Jeshi la Magereza.
   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Suleiman Jafo akimkabidhi mshindi wa pili wa maonyesho ya nanenane kanda ya kati ambaye ni Benki Kuu ya Tanzania.
  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Suleiman Jafo akimkabidhi mshindi wa tatu wa maonyesho ya nanenane kanda ya kati ambaye ni Jeshi la Magereza.

  0 0

   Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano, juu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inafanya kazi katika vitengo mbalilmbali ndani ya maonesho ya Nanene yalifikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
    Makamu wa Rais, Samia Suluhu  Hassan  akipokea mfuko wenye taarifa mbalimbali kutoka kwa Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Vicky Msina  katika  maonesho ya Nanene yalifikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika  maonesho ya Nanene yalifikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi, Charle’s Tizeba akipata maelezo kutoka Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Bestina Magutu juu Mamlaka hiyo inavyofanya kazi katika  maonesho ya Nanenane yaliyofikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Afisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa na Meneja wa Kanda ya Kusini (TFDA), Dogratius Ngatunga akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la TFDA katika maonesho ya Nanenane mkoani Lindi juu ya madhara ya vipodozi.
   Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu  akipata  maelezo  kutoka kwa  Meneja Masoko wa PBZ, Aisha Mohamed wakati Makamu wa Rais alipotembelea banda  la PBZ  katika maonesho ya Nanenane yaliyofikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu  akimpa kikombe cha mshindi wa jumla wa maonesho ya Nanenane mkoani Lindi, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenaerali , Michael Isamuhyo.

  0 0

  Ungana nasi killa Ijumaa kwa Maombi haya ya Kivita, katika Kupambana na Shetani ana kwa ana katika Ulimwengu wa roho.
   Waefeso 6:10-18.

  Familia nyingi zimefunguliwa kwa Jina la Yesu, Kupitia Maombi haya ya Mkesha wa USIKU WA VITA.Usikose Kuungana nasi katika Ufunguzi wa Maombi haya Kimataifa;

  Ingia kwenye Maombi haya na Mahitaji yako, Famila yako, Yesu atakwenda kukufungua Usiku huo 

   Kama wewe unaishi USA na CANADA  
  Dial : (319)-527-9613 (NO CODE)
  Time: 11:pm - 4:am (Eastern Time)


    Walio nje ya USA* huwa 
  Kila Jumamosi Asubuhi.

  Tafadhali
  Dial namba Kutoka nchi uliyopo👇👇👇

  Tanzania: Tel: 041 120 1000
  *Access CODE: 172963#*
  *Time: 7:00am - 11:00 am* 

  UK: Tel:  0330 998 1254
   Access CODE: 172963#*
   *Time: 5:00am - 9:00am* 

  Kenya:Tel: 020 7653263
  Access CODE: 172963#*
    Time: 7:00am - 10:00am* 


  S-Africa:Tel: 087 825 0143
   Access CODE: 172963#*
   *Time : 6:00am - 10:00am* 

  Italy :Tel: 051 092 0292
    Access CODE: 172963#*
   *Time: 6:00am - 10:00am*

  Denmark :Tel: 78 73 09 22
  *Access CODE: 172963#*
   *Time: 6:00am - 10:00am* 

  Bwana Yesu akushindie VITA yako:
  Unaweza kuwasilia na 
  Mtumishi. 
  Minister -John Kazilo
  USA.

  Pastor-Peter Igogo
  Tanzania
  Bishop Boniface Rweikiza
  Tanzania 

  0 0

  JUKWAA la wahariri Tanzania (TEF) laondoa zuio la kutokutoa habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda jijini Dar es Salaam leo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga amesema kuwa " Mgogoro huu kati ya Jukwaa la wahariri wa habari na tasnia ya habari  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda umefika mwisho tunarusu sasa habari zake ziandikwa  mgogoro ule uliokuwepo yaliyopita si ndwele tugange yajayo"

  Tamko hilo la TEF limekuja mara baada ya Machi 22 mwaka huu kutoa tamko lao kwa vyombo vya habari  lililokuwa likisema "Zinalaani vikali vitendo vya Mkuu wa Mkoa katika kuvamia chombo cha habari cha Clouds Media akiwa ameambatana na Askari wenye silaha.
   Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuondoa adhabu aliyopewa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambayo alikua nayo ikiwa Jukwaa hilo la wahariri lilimfungia kwa  kutokutoa habari yoyote kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
  Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akizungumza na waandishi wa  habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Jukwaa la wahariri kuondoa zuio kutotoa habari zamkuu wa ,Mkoa wa Dar Es Salaam leo.
  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) wakiondoa zuio la kutokutoa habari yoyote kwenye chanzo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenye vyombo vya habari  sasa kuanzia leo habari za mkuu wa Mkoa wa Mkoa zitakuwa zikitoka kwenye vyombo vya habari. katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile  na kushoto ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
  Katikati ni  Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile  akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kushoto ni  Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
   Picha na Avila Kakingo, Blog ya Jamii.

  0 0

  Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa kampeni yake Mwakalebela amesema kuwa kwa kwanza ataanza na Utawala bora kwa Kuweka misingi ya wazi katika mapato na matumizi ya TFF, Kuzifanya kamati za TFF kuwa huru na kufanya kazi bila kuingiliwa,uingalia upya Agenda ya kupunguza idadi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ili tuweze kupanua wigo wa wadau wa mpira wa miguu kutuwakilisha kwa wingi katika mkutano mkuu.
  Amesema kuwa pia ataweza kusimamia matakwa ya katiba ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kwa kufanya vikao na mikutano inayotambuliwa kikatiba, kuwa na vyombo imara vya usimamizi ndani ya shirikisho ili kuleta matokeo chanya yenye ufanisi katika soka.
  Mwakalebela amesema ataweza kusaidia Timu za Taifa ,wanaume,Wanawake na Vijana kwa Kuwa na makocha wenye viwango vya juu ikiwa ni pamoja na Kurudisha hamasa kwa watanzania kuzipenda timu za Taifa kwa kuongeza idadi kubwa za wachezaji wa ndani kucheza nje ya nchini pamoja na kucheza FIFA date zote na Kuziweka timu kambini kwa wakati


   
  Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandihi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa akinadi sera zake. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.
   Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumikaElimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
  Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

  NA ELIAFILE SOLLA
  WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini. 

  Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo. 

  Majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.

  Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.
  Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.

  Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.

  0 0  Mambo wapenzi wa sanaa! 

  Join us on Thursday 17 August at 6.30pm for the opening of Misambwa, an exhibition of sculpture by Congolese artist Agxon. Agxon creates abstract and expressive portraits with materials he collects on the shores of Lake Tanganyika. 
  With inspirations ranging from ancient Greek writings to 1970s funk culture, his artwork explores the complex post-independence history of Congo. 
  This is the first time Agxon’s work will be displayed in Tanzania – don’t miss out! You may have seen posters advertising the opening for 10 August. Unfortunately, due to unforeseeable circumstances, the date of the exhibition opening has changed from this week to next Thursday 17 August. We apologise for any inconvenience caused and hope to see you on the 17th!


  0 0

  Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Jeshi la Polisi kikosi cha Bandari pamoja na Jeshi la Uhamiaji wametakiwa kuhakikisha wanakagua abiria na mizigo yote inayopita katika bandari zote nchini ili kuhakikisha abiria na mizigo yote inafuata taratibu zote zilizowekwa kwa mujibu wa sheria jambo ambalo litaimarisha usalama bandarini. 
  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masaun katika ziara ya kukagua namna watalii wanavyopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam. 
  Katika ziara hiyo aliambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhandisi Ramo Makani na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasiliano Mhandisi Edwini Ngonyani. Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani amesema ni muhimu kuweka takwimu vizuri za watalii wanaopita katika bandari zote ili kujua idadi kamili ya watalii wanaokuja kwa kutumia njia ya maji. 
  Akielezea jinsi wanavyowapokea watalii wanaokuja kwa meli katika bandari ya Dar Es Salaam, Meneja wa Operesheni amesema wamekuwa wakikutana na wadau kila siku ili kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya ujio wa watalii nchini. Manaibu Waziri hao pia walitembelea Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal II na kukagua ujenzi wa Terminal III unaoendelea.


older | 1 | .... | 1850 | 1851 | (Page 1852) | 1853 | 1854 | .... | 3278 | newer