Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YANG'ARA SABASABA.

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga (kushoto aliyesimama) akijibu maswali mbalimbali ya mteja ambaye alitembelea banda la Wizara hiyo katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa tayari kwa kujibu maswali mbalimbali ya wananchi wanaotembelea banda la wizara hiyo katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi likionekana kwa nje. (Picha na Felix Mwagara)

MAPITIO YA MAGAZETI LEO

TEMBEA UJIONEE...

$
0
0
Kamera ya Globu ya Jamii hivi karibuni ilikutana na taswira hii ya kuanwikwa kwa mahindi kwenye Kituo cha Mabasi katika kijiji cha Hale huko Mkoani Tanga,kitu ambacho ni tofauti na matumizi yake.

Wazee wa Feva Mnawaowa hawa wanachokifanya???

$
0
0
 Haya jamaa wa Boda Boda wakileta mchezo Barabadani wakati wakiipita gari hii,kama walivyonaswa na Kamera ya Globu ya Jamii huko Bagamoyo.
walipopita waliendelea tena kucheza barabarani kwa kwenda kushoto na kulia.

hii imekaaje wadau??

$
0
0
Mara nyingi Madereva wengi wa Magari ya Masafa marefu hupenda kuweka matawi ya miti mabarabarani pindi wapatapo matatizo kwenye magari yao ikiwa ni kama ishara ya tahadhali kwa magari mengine yatumiayo njia hiyo,lakini utaratibu huu umekuwa ni mbaya sana hasa pale ambapo gari husika likiwa limepona na kuondoka katika eneo hilo.kwani matawi haya huachwa hapo hapo barabarani. 

Mkurugenzi wa NBC atoa somo Mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika

$
0
0
Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada katika Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa VIA Aviation, Susan Mashibe, jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mizinga Melu (wa pili kushoto) akitoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Balozi Mark Green Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Global Development (IGD), Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Group Loid Engenharia SGPS, Loide Monteiro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIA Aviation, Suzan Mashibe.
Rais wa zamani wa Marekani, George Bush (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Mwelu na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu Kampuni VIA Aviation, Susan Mashibe. Wengine ni maofisa wa NBC, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Clara Rubambe na kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Flora Lupembe na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale.
Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kulia) akipozi kwa picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu wakati wa Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, jijini Dar es Salaam jana. Mizinga alikuwa mmoja wa watoa mada katika mkutano huo.

TAMASHA LA Grand Malt Tanzania Open Film Festival laendelea JIJINI MWANZA.

$
0
0
Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakitazama moja ya filamu iliyokuwa ikioneshwa jana usiku kwenye viwanja vya Nyamagana,ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Filamu ya wazi lililojulikana kwa jina la  ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’.Tamasha hilo lilizinduliwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya na kusababisha shangwe tupu kwa wote waliokuwepo ndani ya uwanja huo.
 Katika uzinduzi wa tamasha hilo,kuna burudani mbalimbali zikitolewa ikiwemo na wakazi wa Mwanza wenye vipaji vya kucheza na kuimba,walipewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kama ionekanavyo pichani,ambapo mwisho wa mashindano hayo kuna atakaeibuka na kitita cha shilingi laki mbili.
 Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza jana kushuhudia muenedelezo wa tamasha la filamu,lijulikanalo kama   ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ kwenye uwanja wa Nyamagana.

HATIMAYE SERIKALI YA KABIDHIWA RASMI UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Kulia) akishuhudia Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging akiweka sahihi katika hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa.Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga(Kushoto) akitia sahihi katika hati ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa,kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Habib Mkwizu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Katikati) akishuhudia Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging akibadilishana hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa na Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga (Kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi Habib Mkwizu (Kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya sherehe ya makabidhiano ya Uwanja kukamalizika.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Assah Mwambene (Kulia) akizungumza akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa TFF Angetile Oseah walipokutana katika sherehe za makabidhiano ya Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangaraka (kulia) akipokea Ufunguo wa mfano kutoka kwa Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging kuashiria kukabidhiwa rasmi kwa Uwanja wa Taifa.PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA - MAELEZO.

MTU ANAEDAIWA KUWA NI JAMBAZI AUWAWA NA POLISI JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mahmoud Ahmad Arusha

MTU mmoja anaedaiwa kuwa ni Jambazi afariki katika majibishano ya silaha na polisi katika tukio tofauti la kujibishana risasi na askari wa jeshi la polisi baada ya kumfyatulia askari risasi na kumkosa huko maeneo ya Sokon 1 jijini hapa jana majira ya jioni.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani hapa Kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa mnamo majira ya saa11;15 huko mtaa wa Onjaftian jeshi hilo lilifanikiwa kumuuwa baada ya majibishano ya risasi na askari wa jeshi hilo jambazi sugu aliyefahamika kwa jina la Lembris Taiko au kwa majina mengine doctor mbushii,general mwarusha, mwenye umri wa miaka32-35 mkazi wa sokon 1 jijini hapa.

Kamanda alisema kuwa awali walipata taarifa kwa wasamaria wema kuwa kuna watu3 wanaosadikiwa majambazi na kufuatilia maeneo ya tukio na kuizingira nyumba walipojaribu kuingia ndani na kuwataka watu wote kujisalimisha ghafla risasi zilianza kutoka ndani kupitia ukutani na kumkosa askari hali iliyowalazimu askari kujibu mapigo na kufanikiwa kumuua jambazi huyo.

Sabas alisema kuwa uchunguzi uliofanya na askari wa jeshi hilo umebaini kuwa ni jambazi sugu huyo alikuwa akitafuta na jeshi hilo na akishiriki kwenye matukio ya ujambazi maeneo mbali mbali ikiwemo Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam na alikutwa akiwa na bastola mmoja,aina ya bereta iliyofutwa namba risasi moja chemba,ganda moja la risasi iliyofyatuliwa,risasi 3za bunduki aina ya shortgun,na funguo mbali mbali 26 na mordem ya kampuni ya Airtel.

“Jambazi huyu alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi letu kwa kushiriki kwenye matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha za moto tukio ambalo lilitokea28\08\2012 huko maeneo ya olasiti jijini hapa ambapo walipora bastola yenye no.T0620-11J00491 aina ya tisas”alisema kamada sabas.

Katika tukio lingine jambazi huyo alijeruhiwa mguuni akafaniwa kutoroka lakini jeshi la polisi lilifanikiwa kumua jambazi aliefahamika kwa jina la peter Toshi katika majibizano hayo jambazi huyo alikutwa na bastola aina tisas inayoaminiwa kuwa ndio ilioporwa ikiwa imefutwa namba zake.

Kamanda sabas alisema kuwa kutoka eneo la tukio anabainisha kuwa mmiliki wa nyumba aliokuwa jambazi huyo anaefahamika kwa jina moja la Swalehe au baba Amiri ambaye hakuwepo wakati wa tukio hili jitihada za kumtafuta zinafanyika ili aweza kuhojiwa juu ya uhusiano wao na jambazi aliyeuwa na wapangaji wengine kwenye nyumba hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

Hata hivyo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount meru kwa uchunguzi zaidi na juhudi za kuasaka majmbazi wengine badao zinaendelea kufanyika.

BUNGE LAENDELEA KUTOA SOMO KUHUSU KAZI ZAKE KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

$
0
0
Afisa wa Bunge Ndg. Christopher Kanonyele akifafanua kwa wananchi majukumu ya msingi ya Bunge kama yalivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwal Nyerere.
Mwananchi akisikiliza kwa hisia maelezo kuhusu siwa ya Bunge na umuhimu wake katika vikao vya Bunge, kwenye maonesho ya sabasaba.
Afisa Habari wa Bunge Prosper Minja akifafanua hatua kwa hatua namna miswada inavyowasilishwa Bungeni hadi inapokuwa sheria kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Bunge wakati wa Maonesho ya Sabasaba.
Wananchi wakifuatilia kwa makini maelezo ya picha za waliowahi kuwa maspika wa Bunge tangu kuanza kwake lilikiwa baraza la kutunga sheria mwaka 1926 kutoka kwa afisa wa Bunge Ndg. Ismail Jimrodger.
Muonekano wa Banda la Bunge kwa nje katika viwanja vya sabasaba. Picha zote na Owen Mwandumbya

TAMKO LA CCM DMV

Twanga Pepeta na Ben Paul kusindikiza Redd's Miss Temeke 2013

$
0
0
Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Temeke Beny Kisaka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la Redd’s kanda ya temeke linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa ya juma hili.Kulia ni mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye.
Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la Redd’s kanda ya temeke linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa Julai 5,2013.Wengine Pichani ni Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Temeke Beny Kisaka na Msanii Ben Paul pamoja na Warembo watakao shiriki kinyang'anyiro hicho.
Warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa shindano hilo sambamba na wasanii watakaotumbuiza siku hiyo Ben Paul na Luiza Mbutu wa bendi ya Twanga pepeta ambapo shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa Julai 5,2013.

TBL YANOGESHA SIKU YA WAKULIMA WA SHAYIRI KARATU

$
0
0
 Mtafiti wa Mbegu,Geremiah Mrimi  (wa pili kushoto) akimuonesha Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi mbegu aina ya Shayiri zilizokubaliwa na Wizara ya Kilimo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Shayiri, wilayani Karatu, Arusha mwishoni mwa wiki. Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.

Mtaalamu wa Kilimo cha Shayiri, Joel Msechu (kulia) akitoa maelezo juu ya mbegu za Shayiri kwa Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi (katikati) na Mhasibu wa Mashamba, Optaty Minja.Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia TBL, shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.
 Mtaalamu wa Kilimo cha Shayiri, Joel Msechu (kulia) akitoa maelezo juu ya mbegu za Shayiri kwa Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi (katikati) na Mhasibu wa Mashamba, Optaty Minja.Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia TBL, shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.
 Anatoly Lohay,mkulima wa Rhotia kati Karatu.
Editha Temu,Afisa Ughani kiwanda cha TBL akielezea umuhimu wa zao hilo

MEYA WA MANISPAA YA ILALA ATEMBELEA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA - SABASABA LEO

$
0
0
IMG_8364
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar ambapo alitembelea mabanda mbalimbali.
IMG_8735
Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed (kushoto) akimkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwenye Banda la HSC kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8808
Mtsahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya jinsi Mfuko wa Fursa sawa kwa wote unavyopambana na kutokomeza Ugonjwa wa Saratani ya Matiti kwa wakina mama nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
IMG_8797
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal walipokutana kwenye Banda la Mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar.
IMG_8830
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa akiagana na Mstahiki Meya Jerry Silaa mara baada ya kutembelea Banda la (EOTF) linalotoa fursa kwa wajasiriamali nchini Tanzania kuonyesha bidhaa zao katika maonyesho hayo kila mwaka.
IMG_8558
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipata maelezo jinsi ya kutumia Kizimamoto Fanisi cha kurusha (Fire Extinguisher) ambacho ni rahisi kutumia na hakihitaji matengenezo na hudumu kwa miaka mitano pia Kifaa hicho ni rafiki wa mazingira na mvumbuzi bora kwa uokoaji wa dharura wakati alipotembelea Banda la GreenBat Fire Solutions katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea.
IMG_8542
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika banda la Arusha International Conference Centre (AICC) wanaoshughulika kutoa huduma za kumbi za Kimataifa za mikutano na Utalii jijini Arusha.
IMG_8531
Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia jinsi mtoto Range Jackson ( wa pili kushoto) mwenye ulemavu wa Ubongo akionyesha ramani ya Tanzania na Sehemu ya mipaka yake iliyotumika kumfundishia kujua kusoma na kuandika na ufundi stadi kupitia kituo cha VETA. Kulia ni Mkufunzi wa kuchomea (Welding Instructor) na Mwalimu wa watu wenye mahitaji maalum Bw. Kintu Kilanga na Wa tatu kulia ni Baba mzazi wa kijana huyo Bw.Jackson Range.(Picha na Zainul Mzige).

VUNJA MBAVU : KUTOKA KWA ANKAL CHIBIRITI

$
0
0
Bili ilivyomchanganya Masawe; Masawe alienda na rafiki zake Bar kunywa, baada ya kumaliza kunywa bili ikaletwa kama ifuatavyo;

1). Manka       = sh.35,000.
2). Marieta      = sh.20,000.
3). Kekuu        = sh.30,000.
4). Kitime        = sh.10,000.
5). Kinabo       = sh.15,000.

TOTAL           = SH.110,000.

Masawe akaicheki bili akasema; wote nitawalipia lakini huyo TOTAL ''Yesuu'' simlipii kabisa. Kwansa anamiliki sheli kibao sa mafuta hapa Bongo...shensi taaip! na amekunywa nyingi kuliko wote, alipe mwenyewe.

Morogoro yailaza Temeke 5-2 michuano ya Airtel Rising Stars

$
0
0
Timu za Airtel Rising Stars zikiingia kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam tayari kwa ufunguzi rasmi wa ARS ngazi ya Taifa jana Jumanne Julai 2, 2013.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano – Mallya akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana Jumanne Julai 2, 2013.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana Jumanne Julai 2, 2013.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Kassim Majaliwa akikagua timu za mikoa ya Mwanza na Ilala ambazo zilichuana kwenye hafla ya kufungua rasmi mashindano ya Taifa ya Airtel Rising Stars kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam jana Jumanne Julai 2, 2013. Mwanza ilishinda 3-1.
Mashabiki wa soka wakishuhudia vipaji vya soka wakati wa mechi ya Airtel Rising Stars kati ya Mwanza na Ilala kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Jumanne Julai 2, 2013. Mwanza ilishinda 3-1.

chemsha bongo: waweza tambua ni wapi hapa??

$
0
0
Hili ni moja ya maeno ndani ya nchini yetu nzuri ya Tanzania,je waweza tambua ni wapi hapa??

NEWS ALERT: Morsy out in Egypt coup

$
0
0
Cairo (CNN) -- Egypt's military deposed the country's first democratically elected president Wednesday night, installing the head of the country's highest court as an interim leader, the country's top general announced.

Gen. Abdel-Fatah El-Sisi said the military was fulfilling its "historic responsibility" to protect the country by ousting Mohamed Morsy, the Western-educated Islamist leader elected a year ago. The country's constitution has been suspended, new parliamentary elections will be held and Adly Mansour, the head of the country's Supreme Constitutional Court, will replace Morsy, El-Sisi said.

Mansour will have the power to issue constitutional declarations during the interim period and will "establish a government that is a strong and diverse," the armed forces chief said. He said Morsy "did not achieve the goals of the people" and failed to meet demands to share power with opponents who thronged the streets of Cairo and Tahrir Square.
Those crowds erupted as the announcement was made on Egyptian television shortly after 9 p.m. (3 p.m. ET). But Morsy supporters gathered in another Cairo plaza vowed to oppose the coup, chanting "Down with military rule" and "The square has a million martyrs." And in statements posted on the presidential Facebook and Twitter pages, Morsy said his ouster would be "categorically rejected by all the free men of our nation."

"The president -- who is also the supreme commander of the armed forces -- tells all citizens, civilians and military, leaders and soldiers, must abide by the constitution and should not respond to the coup which brings Egypt behind," he said. "Everyone must take responsibility before God, people and history."

KUMBUKUMBU YA DR PETER ZACHARIAH KOPWE

$
0
0
Mpendwa wetu Dr Peter   Zachriah leo ni miaka miaka sita tangu umetutoka na kutangulia mbele ya haki. Tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi. Unakumbukwa na mke wako Lilian P. Kopwe watoto wako Ronald , Paul , Nancy na Gerald pamoja na Wazizi wako kaka zako Dada zako shemeji zako wote pamoja na jamaa marafiki   (Ayub 19:25 ) pumzika kwa amani

FOREVER NUTRI-LEAN PROGRAMME

$
0
0
A) FOREVER NUTRI-LEAN PROGRAMME (WEIGHT MANAGEMENT PROGRAMME) 1. Clean 9- Detoxify-leaves you clean, healthier, happy and helps you to loose between 3kg to 8kg. @ Tsh 270,000.

2. Forever Nutri-Lean (Life style 30)- burns fats, loose weight between 10kg to 15kg & maintain your weight, leaves you with good eating habits. @ Tsh 440,000.

3. Body Toning Kit- Removes cellulite and fats deposits under the skin. Wrap the arms, thighs, stomach and loose up to 2 inches per Wrap. @ Tsh 145,000.
Loose weight and improve quality of your life (Sexual desire and performance, reduce possibilities of diabetes, Cancer and Sleep apnea). FOREVER NUTRI-LEAN PROGRAMME has No Drugs (Caffeine, Topiramate, sibutramine, xenical, phentermine, methamphetamine).

B) REASONS TO DRINK ARGI+ 1. Is a marvelous daily supplement that supports better health throughout many systems of the body, delivering optimal performance.

2. Supports the immune system. Nitric oxide derived from L-Arginine, is used by white blood cells to attack bacterial etc. as it is toxic to them and makes these immune cells more lethal.

3. Helps maintain a healthy blood pressure and cardiovascular system.

4. Aids bone and tissue growth and repair, so is particularly appropriate after fractures and soft tissue injury.

5. The nitric oxide formed, permits grater blood flow and may improve sexual function.

6. Increases muscle mass and strength, whilst reducing the amount of fatty tissue. A welcome benefit for sports men and women.

7. The pomegranate and fruit components are a rich source of antioxidants, needed to fight the damaging effects of free radicals.

8. Contains an extract of red wine, which helps to reduce blood cholesterol levels.

9. Affects insulin sensitivity so is particularly useful in maintaining blood glucose control.

10. Acts to release anti-ageing hormones.

SO MUCH EXCITEMENT AT ONLY TSH 132,000.

Call 0786766028/ 0769888605 OR VISIT http://www.mariettasweke.blogspot.com/search/label/ARGI
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images