Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110120 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: Soga za Diaspora Episode 2


TCAA YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE MKOANI LINDI

$
0
0
Afisa Muongoza Ndege Mwandamizi, Godlove Longole akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
 Afisa Muongoza Ndege Mwanadamizi (kulia) Godlove Longole na Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Bestina Magutu wakitoa Elimu kwa watoto waliotembelea Banda la TCAA katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Adinan Mvungi (Kulia),Adinan Mvungi Akitoa Elimu kwa Wanafunzi Waliotembelea Banda la TCAA Katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
 Afisa Habari Msaidizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Ally Changwila  akitoa elimu kwa Mwanafunzi  aliyetembelea Banda la TCAA katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Afisa Habari Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Bestina Magutu(wa pili kutoka kushoto) akitoa Elimu kwa wananchi waliotembelea banda la TCAA katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto ni Afisa Muongoza Ndege Mwanadamizi Godlove Longole.
Afisa Habari Msaidizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Ally Changwila  akitoa elimu kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi –Taarifa za Hali ya Hewa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini(TMA), Dkt Ladislaus Chang’a  aliyetembelea Banda la TCAA katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Timu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja katika maonesho ya Nane nane 2017 katika viwanja vya Ngongo Lindi. 

MASAUNI ATEMBELEA KITENGO CHA POLISI CHA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA,KILWA ROAD JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Naibu Waziri wa   Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na watumishi wa Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipofanya ziara katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingizwaji na usambazaji.
 Naibu Kamishna wa Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, DCP Mkonyi, akitoa taarifa fupi ya hali ya uzuiaji wa Dawa za Kulevya mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani   ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,  alipofanya ziara katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingizwaji na usambazaji.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisomewa takwimu za matukio ya ukamataji wa Dawa za Kulevya na mmoja wa afisa wa  Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya  wakati alipofanya ziara katika kitengo hicho kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingzwaji na usambazaji.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongozana na Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Mkonyi, wakati alipotembelea  Kitengo cha Jeshi la Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya kilichopo Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanapambana na uingizwaji wa dawa hizo kupitia bandari bubu na mianya yote ya uingzwaji na usambazaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WANANCHI WAHIMIZWA KUTUNZA FEDHA NA KUTAMBUA ALAMA ZA USALAMA

$
0
0
Makamanda wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Lindi wamewataka wananchi kutunza vizuri fedha zao ili kupunguza uharibifu unaoliongezea taifa gharama za kutengeneza fedha zingine.

Aidha, viongozi hao wameelezea umuhimu wa wananchi kutambua alama za usalama wa noti zetu ili kuepuka kuangukia mikononi mwa matapeli na kupata hasara.

Viongozi hao, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, SACP Renatha Mzinga, Mkuu wa Magereza wa Mkoa, Bw. R. Nyange, na Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Mkoa wa Lindi, Bw. Nsiima Wema walisema hayo baada ya kutembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika maonesho ya Wakulima kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi. 

RPC Mzinga alisema taifa linaingia hasara kubwa kutengeneza noti zinazotokana na uharibifu unaofanywa mara kwa mara na wananchi.

“Mimi nilikuwa najua pesa chafu zinarudishwa Benki Kuu na kufanyiwa recycling na kurudishwa kwenye mzunguko; kumbe tunapata hasara. Kwa elimu hii niliyoipata, nawashauri wananchi kwa ujumla watunze fedha zetu, kwa sababu zinapoharibika ni hasara kwa taifa,”alisema RPC Mzinga.

Mkuu wa Usalama wa Taifa mkoani Lindi, Bw. Wema alieleza kwamba amefurahishwa sana kwa kupata elimu kuhusu alama za usalama za noti zetu na kuahidi kutumia elimu hiyo kuwafundisha wengine.

“Kikubwa zaidi kilichonivutia ni namna ya kutambua pesa halali na pesa zisizo halali. Kwa ajili ya kukosa uelewa wananchi wengi wanalizwa kila siku kwa kupewa pesa zisizo halali kwa kuwa hawajui kuzitambua. Elimu niliyoipata itanisaidia niwaambie na wenzangu mtaani kwamba pesa halali iko hivi na isiyo halali iko hivi,” alisema Bw. Wema.

Mkuu wa Magereza wa Mkoa, Bw. Nyange, aliwashauri wananchi wanapofikia umri wa kustaafu wajiepushe kuwekeza katika biashara wasizozijua ili kuepuka hasara na badala yake wawekeze katika dhamana za serikali zinazotoa faida ya uhakika bila wasiwasi wowote wa kuingia hasara.

“Watu wanapostaafu mara nyingi wanajiingiza kwenye miradi mbalimbali…ambayo hawana ujuzi nayo; hawajui hata hasara zake, ili mradi wanaona mtu fulani ana biashara ya magari, ana mabasi, basi naye anajiingiza huko matokeo yake anapata hasara au mwingine anajiingiza kwenye mashamba na wakati mwingine jua mwaka huo linakuwa kali, moja kwa moja mazao yanakufa, inafikia hatua mtu anaweza hata kujiua…kumbe fedha ile unaweza ukawekeza kwenye dhamana za serikali, ukaendelea kupata faida na pesa yako ikabaki kuwa salama,” alisema.

Viongozi hao wa vikosi vya ulinzi na usalama mkoani Lindi walitumia takriban saa nzima wakipata elimu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Benki Kuu na jinsi zinavyoendana na Kauli Mbio ya Maonesho ya Wakulima ya mwaka huu isemayo: Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati.

Maonesho ya Nane Nane kitaifa mwaka huu yalifunguliwa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Bw. George Simbachawene tarehe 1 Agosti, 2017, ambaye pamoja na mambo mengine aliwataka wakulima, wafugaji na wavuvi kuongeza tija kwa kuzalisha mazao na bidhaa kwa njia za kisasa.

Waziri Simbachawene alihimiza kilimo na ufugaji wa kisasa na kuwataka wavuvi kuanzisha ufugaji wa kisasa kwa kujenga mabwawa badala ya kutegemea mitego katika mito, maziwa na bahari, ambako hakuna uhakika wowote wa kipato.Maonesho kama haya pia yanafanyika katika ngazi ya kanda katika kanda za Mashariki, Kati, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na Kaskazini.

AJALI ZA BARABARANI ZINAWEZA KUPUNGUA KWA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI-KAMANDA MUSLIM

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa ajali za barabarani zinaweza kupungua kwa madereva  kufuata sheria za usalama barabarani.

Hayo ameyasema Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim wakati akizindua uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani leo katika kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa namba za simu katika mabasi hayo zitatumika kwa abiria kutoa taarifa ya dereva anaendesha bila kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo mwendo kasi.Kamanda Muslim  amesema kuwa namba hizo ni bure na kwa abiria, dereva au kondakta atakaeng’oa namba hizo atachukuliwa hatua ikiwemo kunyanganywa leseni.

Amesema uwekaji wa namba maalumu kwenye mabasi unafanyika nchi nzima ikiwa yote nikulinda maisha ya abiria katika kuwa na uhakika wa safari zao.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo amesema kuwa watasimamia maagizo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro ambapo yamekaziwa na Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim.

Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix amesema kuwa kila siku wanafanya ukaguzi na gari ambayo ina kasoro haiwezi kufanya safari zake.Amesema watahakikisha kuwa kila basi linalondoka katika kituo cha ubungo linakuwa na namba maalum za simu  katika kila basi..
 Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akizungumza na waandishi habari katika uzinduzi wa uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
 Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkazo na maagizo ya Ukaguzi wa magari katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix (katikati) akizungumza na waandishi  habari kuhusu ukaguzi magari yanayotoka kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa  Kikosi cha Usalama Barabarani  kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akiweka namba maalmu za simu katika basi itakayotumika kupiga kwa  abiria kwa dereva atakaye kiuka sheria za usalama barabani .
  Askari wa Usalama barabani  wakiwa katika ukaguzi mbalimbali wa mabasi katika kituo Kikuu cha Mabasi  Ubungo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KUBENEA ATOA MILIONI 20 ZA MFUKO WA JIMBO KUJENGA ZAHANATI KILUNGULE

$
0
0
Mbunge wa Ubungo ,Saed Kubenea akihutubia wakazi wa Kimara kata ya Kilungule wakati wa mkutano wa hadhara mara baada ya kumaliza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika eneo hilo na kuwashukuru wapiga kura wake kupitia mkutano huo,ambapo aliahidi kutoa Milioni 20 za Mfuko wa jimbo kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kata hiyo.
Wananchi wa kata ya Kilungule Kimara jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Ubungo Saed Kubenea katika mkutano wake wa hadhara
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea akizungumza na mmoja wa wazee Maarufu wa kata ya Kilungule mara baada ya kumaliza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika eneo hilo
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea akifurahi na wakazi wa kata ya Kilungule mara baada ya kumaliza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika eneo hilo
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Saed Kubenea akifurahi na wakazi wa kata ya Kilungule mara baada ya kumaliza kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika eneo hilo
Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akifuatilia mkutano wa Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea Kimara Kilungule.

DKT. MENGI ATAKA EAC KUTUMIA UTAJIRI WAKE KUTENGENEZA MABILIONEA

$
0
0
MWENYEKITI wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi amezitaka Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kutumia utajiri wake mkubwa wa raslimali kunufaika kiuchumi. Ushirikiano huo ni pamoja na kuzindeleza raslimali hizo na kutumia nembo moja ya kibiashara ili kuzalisha mabilionea wakubwa duniani. 

Mwenyekiti huyo alisema hayo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili. Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi akizungumza wakati akifungua mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 Pamoja na kutoa wito huo Dk Mengi pia amempongeza Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli pamoja na serikali yake kwa kuwa mstari wa mbele kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya. Aidha alisema dhamira yake ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda itasaidia kuwakwamua Watanzania kutoka katika umaskini. Katika mazungumzo hayo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania –TPSF Dr Reginald Mengi na Ujumbe wa Kenya umeongozwa na Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor. Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi kwa kutoa risala nzuri ya ufunguzi wa mkutano huo.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye amesema mkutano huo umeitishwa kutokana na kujitokeza vikwazo vya kufanya biashara baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, jambo linalokwamisha malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kujenga uchumi unaoongozwa na sekta Binafsi. Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa KEPSA Bw. George Owuor amesema Wafanyabiashara wa Kenya wanapenda sana kushirikiana kibiashara na wenzao wa Tanzania, na wangependa kuona vikwazo vinavyokwamisha mahusiano ya kibiashara vinaondolewa. Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor akiwasilisha mada kuhusu kupunguza pengo la biashara kati ya Tanzania na Kenya na kutumia fursa zilizopo na kutanua biashara nje ya mipaka katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Meneja anayeshughulikia Utafiti, Uchambuzi na Sera wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA, Victor Ogalo (kushoto) akitoa mada kuhusu changamoto za kisera za Tanzania na Kenya katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia walioketi ni Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi wakifuatilia kwa umakini mada hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alaska Tanzania, Jennifer Bash wakifuatilia mada mbalimbali zikizokuwa zikiwasilishwa ukumbini hapo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ujumbe wa Tanzania na Kenya ulioshiriki mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Muhimbili Yaadhimisha Siku ya Wakunga Duniani kwa Kupima Afya Wananchi Leo

$
0
0
Mgeni rasmi, Flora Kimaro ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi Taasisi ya MOI akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika Tawi la Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. Pamoja na maadhimisho hayo Chama cha Wakunga Nchini (TAMA) kimepongezwa kwa kutoa huduma za afya ambapo watu wanapima afya leo katika hospitali hiyo. Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa Mei 5, kila mwaka, lakini TAMA tawi la Muhimbili imeamua kuadhimisha siku hii katika wiki ya unyonyeshaji duniani. 
Baadhi ya wananchi waliofika katika siku ya maadhimisho hayo wakimsikiliza mgeni rasmi,
Mgeni rasmi akikakata utepe akiashiria kuanza kwa shughuli za maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kupima watu mbalimbali afya
Mmoja wa wauguzi, Gladisia Kessy akimpima afya mmoja wa watu waliofika Muhimbili leo kwa ajili ya kushuhudia maadhimisho hayo. 


MHANDISI MAKANI ASISITIZA UHIFADHI SHIRIKISHI WA MALIASILI ZA TAIFA

$
0
0

NA HAMZA TEMBA -WMU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo makani amesema  jukumu la uhifadhi wa Maliasili za taifa sio la Serikali pekee kwakua Maliasili hizo ni urithi wa taifa na kila mwananchi anapaswa  kujua kuwa ana jukumu la kulinda urithi huo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Makani amesema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mshiri, Jimbo la Vunjo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa ajili kuona changamoto za uhifadhi na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.

Alisema askari pekee na mitutu ya bunduki haitoshi kulinda maliasili hizo kutokana na ukubwa wa maeneo yaliyopo ukilinganisha na rasilimali zilizopo. "Maliasili hizi zipo kwa faida ya kila mwananchi, tunawaomba muendelee kuiunga mkono Serikali katika kulinda Maliasili tulizonazo, tunahitaji kufanya uhifadhi shirikishi, utalii uimarike na nchi yetu ipate mapato zaidi tuweze kufikia uchumi wa kati", alisema Makani.

Akitaja miongoni mwa faida hizo, Makani alisema maliasili za misitu husaidia upatikanaji wa mvua, kuweka mazingira bora kwa ajili ya kilimo na upatikanaji wa hewa safi. Kwa upande wa faida za kiuchumi alisema sekta hiyo kupitia utalii inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimi 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Betrita Loibooki alisema hifadhi hiyo imejenga mahusiano mazuri na wananchi wa vijiji jirani na kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kukabiliana na ujangili ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hakuna tukio lolote la ujangili wa tembo lililoripotiwa katika hifadhi hiyo.


Niabu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mshiri wilayani Moshi ,alipotembelea kijiji hicho kusikiliza Changamoto zinazo wakabili hususani katika eneo la Nusu Maili lililopo chini ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.


KAMPUNI YA UMEME WA ZOLA YAZINDUA DUKA JIPYA MWENGE JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
DUKA jipya linalouza vifaa na kutoa hudumaza umeme wa ZOLA lazinduliwa Mwenge jijini Dar es Salaam leo. Akizungumza wakati uzinduzi wa Duka hilo Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimea ametoa wito kwa Taasisi za Serikali ambazo hazina huduma za umeme hasa vijijini kushirikiana nao ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa kwenye vituo vya afya ili kuwasaidia wagojwa pamoja na kinamama wajawazito.
  
Amesema kuwa kampuni hiyo inayotoa umeme wa ZOLA hapa nchini imeshatoa huduma hiyo kwenye vituo vya Polisi pamoja na vituo vya huduma za afya na umeme upo vizuri.

Hata hivyo amesema kuwa utakapo nunua  mtambo wa umeme waZOLA  utatengenezewa mfumo wa umeme katika nyumba yako kwa bei nafuu na wengine kwani huduma zao zinalingana na maisha ya Mtanzania.

Amesema kuwa umeme wa ZOLA unaweza kutumika katika vifaa mbalimbali kama kuchaji simu, mashine za kunyolea, televisheni pamoja na kuwasha taa sita za ndani. 
Pia ukinunua vifaa vya ZOLA utapata dhamana(Warrant) ya miaka mitano endapo kifaa chochote kitaharibika mteja utatengenezewa bila gharama yeyote ile. 
Katikati ni Meneja Masoko  wa ZOLA Tanzania, Irene Mbowe akikata utepe kuzindua Duka linalouza  na kutoa huduma za ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Mkuu wa kitengo cha mauzo wa ZOLA, John Amach na Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa ZOLA, Steve Kimea wakishrikiana kukata utepe kuzindua duka hilo.
 Duka la ZOLA lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Steve Kimea wa ZOLA akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya uzinduzi wa duka hilo ambalo watakuwa wanatoa huduma pamoja na kuuza vifaa mbalimbali vitakavyotumika kupata umeme wa ZOLA.

HAKUNA AJIRA ZILIZOTANGAZWA NA JESHI LA POLISI.

$
0
0
Katika siku za hivi karibuni kumejitokeza kikundi cha watu wanaotumia vibaya jina la Jeshi la Polisi kwa kujifanya ni Maafisa wa Jeshi la Polisi na kuwatapeli watu kwa kigezo cha kuwapatia ajira.

Watu hao wamesambaza taarifa kupitia mitandao ya kijamii inayosomeka ‘Vigezo sifa za kujiunga na Jeshi la Polisi’, huku ndani yake ikitaja sifa ambazo kwa mujibu wa kikundi hicho ndizo anazopaswa kuwa nazo mtu anayeomba nafasi ya kujiunga na Jeshi la Polisi.

Jeshi la polisi linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa taarifa hizo ni za uongo na zenye lengo la kupotosha Umma kwa madhumuni wanayoyajua wao wenyewe. Pia zipo taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa wapo watu wanaoombwa kutoa fedha na matapeli hao ili waweze kuwapatia nafasi ya ajira hizo.

Wananchi watambue kuwa Jeshi la Polisi lina utaratibu wake mzuri na wa wazi wa kuajiri. Pale Serikali itakapotoa idhini ya kuajiri watumishi wapya  utaratibu huo utatangazwa kwa  wananchi ili waweze kuufuata kuomba nafasi hizo.

Jeshi la Polisi linawataka wananchi kutoa taarifa juu ya kikundi hicho kupitia kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nawe au ofisi za Serikali ili watu hao waweze kukamatwa na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Wananchi mnashauriwa kupata taarifa sahihi za Jeshi la Polisi kupitia website yake ambayo ni www.policeforce.go.tz au akaunti ya twitter www.twitter.com/tanpol pamoja na Facebook www.facebook.com/tanpol

Imetolewa na:
Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
Dar es Salaam.

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI, DKT. SASABO ASISITIZA MATUMIZI YA TEHEMA MKOANI DODOMA.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Maria Sasabo,(kushoto) amezungumzia umuhimu wa taasisi za umma zilizo chini ya mradi wa Benki ya Dunia kuhakikisha mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), iliyofungwa inafanyakazi mara moja ili kuongeza tija na ufanisi katika kuhudumia wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ufanisi wa matumizi ya TEHAMA katika hospitali ya rufaa ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Dkt. Sasabo  amewataka viongozi wa taasisi hizo kuhakikisha mifumo hiyo inakamilika na kuanza kazi mara moja.

“Hakikisheni ifikapo mwezi Septemba mawasiliano yenu na huduma zenu zilizounganishwa kwenye mifumo ya TEHAMA inafanyakazi ili kurahisisha utendaji na kuiongezea Serikali mapato”, amesema Dkt. Sasabo.

Dkt. Sasabo amemtaka Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya rufaa ya Dodoma Dkt. Samweli Seseja, kuhakikisha hospitali hiyo inakuwa na mfumo maalum wa mawasiliano utakaowezesha kuboresha huduma katika hospitali hiyo na kumudu ongezeko la watu katika Manispaa ya Dodoma.

Akiwa wilayani Bahi, Katibu Mkuu huyo wa mawasiliano  amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya  wilaya ya Bahi Bi, Rachel Chuwa kuhakikisha mifumo ya Tehama iliyofungwa  katika ofisi za halmashauri hiyo na katika shule za sekondari wilayani humo inafanyakazi mara moja ili kuendana na malengo ya serikali katika utoaji wa huduma bora, za kisasa na kwa wakati kwa wananchi wake na hivyo kuiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Serikali imekuwa ikihamasisha matumizi ya TEHAMA katika taasisi zake zikiwemo ofisi, shule, hospitali na vituo vya polisi  ili kuboresha huduma na kuwezesha uwazi katika ukusanyaji wa mapato na hivyo kuhamasisha wananchi kuchangia huduma kwa hiari.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

NANENANE IWE NA FAIDA INAYOONEKANA KWA MKULIMA, MFUGAJI NA KILA MSHIRIKI- DKT NCHIMBI

$
0
0
Maonyesho ya nane nane yanatakiwa kuweka alama chanya na kuwa na sura ya mabadiliko yanayoonekana kwa macho kwa wakulima na wafugaji wanaoshiriki pamoja na wananchi wanaopata huduma na bidhaa katika maonyesho hayo.

Mgeni rasmi katika Ufunguzi wa maadhimisho ya nanenane kanda ya kati ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Chimbi ametoa rai hiyo mapema jana kwa wakulima, wafugaji na washiriki wakati akifungua rasmi maonyesho hayo huku akiwataka washiriki hao kuitumia fursa hiyo kwa manufaa zaidi.

“Ni vizuri maadhimisho ya Mwaka huu yakaonesha mabadiliko chanya kwa washiriki mliojitokeza katika kuonesha bidhaa zenu mbalimbali na pia kwa wale wote waliofika kwaajili ya kununua au kupata maelezo ya matumizi ya bidhaa hizo, wapate kitu tofauti kitakachooneka katika maisha yao”, amesema.

Dkt Rehema Nchimbi ambaye ametumia muda usipungua dakika 45 kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kilimo na ufugaji wenye tija ili kuendana na falsafa ya serikali ya awamu ya Tano inayo himiza zaidi Uchumi wa Viwanda.

Aidha ameliomba Jeshi la Magereza na wawekezaji wote wa ndani na nje ya Nchi wafike kuwekeza katika mikoa ya Singida na Dodoma na kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma watahakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa kila atakayekuwa tayari kuwekeza katika Mikoa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama bidhaa za mbogamboga katika banda la Wilaya ya Kondoa katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mkoa wa Singida katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Julius Sang’udi alipotembea banda la jeshi la magereza kujionea bidhaa wanazotengeza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.

Waziri Mwakyembe alipokutana na Wasanii wa Filamu nchini.

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akieleza mikakati ya Serikali katika kutatua changamoto za wasanii wa filamu nchini wakati alipokutana nao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipokutana nao ili kujua changamoto zinazoikabili tasnia ya filamu mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa filamu nchini mara baada ya kumaliza mkutano wao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.


Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

AfDB YAISAIDIA SERIKALI KUWAONDOLEA WAKAZI WA ARUSHA ADHA YA UMEME KUKATIKA MARA KWA MARA

$
0
0
 Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Kupoozea Umeme cha Njiro Mkoani Arusha, Mhandisi Lembrice Mollel, akitoa maelezo kuhusu mitambo ya Kituo hicho kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt Nyamajeje Weggoro (kulia) alipotembelea Kituo hicho kukagua mradi wa kusambaza umeme uliofadhiliwa na AfDB, uliogharimu Dola milioni 4.2, Jijini Arusha
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt Nyamajeje Weggoro (wa pili kulia) akipewa maelekezo ya namna mitambo ya usambazaji umeme katika Kituo cha Njiro Jijini Arusha inavyoendeshwa kwa mfumo wa Kidigitali. Mitambo hiyo imefadhiliwa na Benki ya AfDB ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu.

Na Benny Mwaipaja, WFM-Arusha
WAKAZI  wa Jiji la Arusha wameondokana na  na adha ya umeme kukatika mara kwa mara  baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme katika Kituo cha kupoozea umeme cha Njiro kilichoko Mkoani Arusha chenye uwezo wa kuzalisha megawati 130.

Hali hiyo inatokana na Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kuwekeza kiasi cha Dola milioni 4.2, ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili kuongeza uwezo wa Kituo hicho kuzalisha umeme unaotumika kwa ajili ya makazi ya watu, maeneo ya biashara na viwanda.

Msimamizi Mkuu wa Kituo cha Usambazaji umeme cha Njiro Mhandisi Lembrice Mollel amesema mradi huo   umesaidia kuongeza Megawati 130 za umeme ambao umekidhi mahitaji ya Jiji la Arusha linalo hitaji Megawati 60 hivyo kubakiwa na Umeme wa ziada kiasi cha Megawati 70.

Alisema kuwa tatizo la kukatika katika kwa umeme katika mji huo wa kitalii na kibiashara litakuwa historia na kwamba umeme unaozalishwa kituoni hapo unasafirishwa kwenye maeneo mengine yenye uhitaji ikiwemo mikoa ya Kilimanjaro na Tanga.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Umeme wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mhandisi Frorence Gwang’ombe amesema kuwa lengo la mradi lilikuwa kupatikana kwa umeme wa uhakika na kuimarisha miundombinu ya usambazaji na kupooza umeme jambo ambalo limefikiwa kikamilifu.

Alisema kuwa uboreshaji wa Kituo hicho cha kupoozea Umeme cha Njiro ni sehemu ya utekelezaji wa uboreshaji wa Sekta ya Umeme nchini kupitia mradi ujulikana kamaElectricity V, uliofadhiliwa na AfDB kupitia mkopo nafuu wa kiasi cha Dola milioni 8, ukihusisha pia mkoa wa Dar es Salaam, Vituo vya kupooza umeme vya Sokoine na Ilala.

“Mradio huu umelenga kuwahudumia wananchi takribani 8,400 hivyo kukamilika kwa mradi huo ni neema kwa wananchi wengi kwa kuwa utasaidia kuimarisha uwezo wao wa kibiashara ndani ya Jiji la Arusha na maeneo mengine ya nchi” alisema Mhandisi Gwang’ombe.

MAOMBI YA DHAMANA YA MANJI KUSIKILIZWA AGOSTI 7 MWAKA HUU.

$
0
0
Mfanyabiashara Yusuf Manji akirudishwa mahabusu baada ya kesi yake ya maombi ya dhamana kuahirishwa hadi Agosti 7mwaka huu.

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Leo imeahirisha kesi maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na   Mfanyabiashara maarufu Tanzania Y usuf Manji, hadi Agosti 7 mwaka huu kwa kuwa Jaji Isaya Arufani anayesikiliza kesi hiyo anaudhuru.

Kesi hiyo imeahirishwa na  Msajili wa Mahakama kuu, Siani..
Hata hivyo kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, upande wa Mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Paul Kadushi akisaidiana na Simon wankyo wamesilisha kiapo kinzani kupinga maombi hayo ya dhamana wakiwa na hoja tatu.

Hoja hizo ni kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo ya dhamana, na kwamba upande wa utetezi umewasilisha maombi hayo ya dhamana kwa kutumia vifungu ambayo siyo sahihi kisheria na pia viapo walivyo viwasilisha vina dosari kisheria.

Hata hivyo, kwa kuwa Jaji husika anayesikiliza kesi hiyo hayupo, kesi hiyo itakuwa tena Agosti 7 (Jumatatu).

Katika maombi hayo ya dhamana, Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Julai 5 mwaka huu aliposomewa Mashtaka ya uhujumu uchumi.

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Farces Salaam Leo imeahirisha kesi maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na   Mfanyabiashara maarufu Tanzania Yusuf Manji, hadi Agosti 7 mwaka huu kwa kuwa Maji Isaya Arufani anayesikiliza kesi hiyo anaudhuru.

Kesi hiyo imeahirishwa mbelw ya Msajili wa Mahakama kuu, Siani.
Hata hivyo kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, upande wa Mashtaka ukiongizwa na Wakili wa Serikali Paul Kadushi akisaidiana na Simon wankyo wamesilisha kiapo kinzani kupinga maombi hayo ya dhamana wakiwa na hoja tatu.

Hoja hizo ni kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo ya dhamana, na kwamba upande wa utetezi umewasilisha maombi hayo ya dhamana kwa kutumia vifungu ambayo siyo sahihi kisheria na pia viapo walivyo viwasilisha vina dosari kisheria.

Hata hivyo, kwa kuwa Jaji husika anayesikiliza kwai hiyo hayupo, kesi hiyo itakuwa tena Agosti 7 (Jumatatu).

Katika maombi hayo ya dhamana, Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurgenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

Kwa mujibu wa hati ya maombi hayo, Manji anadai kuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo  na kwamba ameambatanisha vyeti vya daktari katika maombi yake.

Katika kesi ya msingi,  Manji na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na mihuri ya mbalimbali ya JWTZ isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.

Mbali na Manji, washtakiwa wengine ni,  Ofisa Rasilimaliwatu Deogratias Kisinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Mtunza Stoo msaidizi, Thobias Fwele (43).

MSIGWA ATOA SOMO LA KUTAMBUA BIDHAA FEKI ZA NISHATI JADIDIFU NCHINI.

$
0
0
  Mjumbe wa bodi ya Terea Godwin Msigwa  akitoa somo juu ya kutambua bidhaa feki  za nishati Jadidifu ambazo zinaingizwa nchini kwa njia za panya na kusababisha kupotea kwa fedha na kuleta athari kubwa katika uchumi wetu.
 Muwezeshaji kutoka Tanzania Media Foundation Dustun Kamanzi akizungumza na Waandishi wa habari walioshiriki katika mafunzo ya uandishi Nishati Jadidifu.
 Waandishi  walioshirikikatika mafunzo hayo wakitazama moja ya bidhaa feki ya Nishati Jadidifu ambayo ilikwisha ingia sokoni.
KWA PICHA ZAIDI BOFY HAPA.

TANGA: HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA

$
0
0
Na Agness Moshi- MAELEZO,

Ni takribani mwaka mmoja sasa tangu taarifa za kujengwa kwa Mradi wa Bomba la Mafuta litakaloanzia Hoima Nchini Uganda mpaka Tanzania kwenye bandari ya Tanga kuenea kwenye vyombo vya habari ,mitandao ya kijamii na kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga ambao ndio wahusika wakuu kwenye mradi huu japo unajengwa kwa manufaa ya mataifa haya mawili kwa ujumla.

Mradi huu ni moja kati ya miradi mikubwa ambayo Nchi imeweza kutekeleza na utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani Billioni 3.5 ambazo ni sawa na Tsh Trillioni 8 kwa fedha za kitanzania. Bomba hili linategemewa kuwa na urefu wa kilometa 1,445 likiwa na uwezo wa kusafirisha mapipa ya mafuta takribani 2,016,000 kwa siku na kutoa ajira zaidi ya 1,000 na vibarua zaidi ya 30,000.

Taarifa hizo zilianza kuwa rasmi, mnamo tarehe 14 marchi 2016 ambapo Makamu wa Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw.Javier Rielo alimhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuanza kwa ujenzi wa Mradi huo.

Nyota njema ya Mradi huu ilianza kuonekana Aprili 24 ya mwaka jana, baada ya aliyekua Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo kurejea Nchini kutoka Uganda, kuongea na waandishi wa habari kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kwa mradi huo.

Bwana Muhongo alisema kuwa, kulikua na mjadala mkubwa wa kuchagua wapi Mradi huo ujengwe na wapinzani wakubwa kwa Tanzania walikua Kenya lakini kutokana na ubora wa bandari ya Tanga ukilinganisha na bandari nyingine Tanzania ilichaguliwa kunufaika na mradi huu.

MAKAMU WA RAIS MH.SAMIA SULUHU HASSAN AMPOKEA RAIS MUSEVENI ALIYEWASILI LEO JIJINI DAR

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere Dar es Salaam tayari kuelekea jijini Tanga kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika kesho Agosti 5, 2017 katika eneo la Chongoleani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpokea Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere Dar es Salaam tayari kuelekea jijini Tanga kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika tarehe 5 Agosti 2017 katika eneo la Chongoleani.Pichani kulia ni Naibu Spika wa Bunge Mh.Dkt. Dkt Tulia Ackson Mwansasu

WAKULIMA WAASWA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA WAFANYABIASHARA

$
0
0
Na Mathias Canal, Lindi
BAADA ya kuimarisha umoja na ushirikiano wa wakulima wenyewe ni vema wakulima wakajenga mahusiano mazuri na wafanyabiashara ili kutokutoa mianya kwa madalali ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamikiwa kuwa wananunua mazao ya wakulima kwa bei ya chini huku wao wakiyauza kwa bei ya juu.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wadau wa kilimo waliozuru katika sherehe za maonesho ya Wakulima Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Wamesema kuwa Ni vema kukatengenezwa mfumo mzuri utakaowasaidia wakulima kupata taarifa sahihi za masoko na bei halisi ya bidhaa kupitia umoja wao, kuliko kuendelea kusherehekea kila mwaka wakati wakulima bado wanateseka na bei kandamizi za madalali.

Suala hili linaenda sambamba na kaulimbiu ya sherehe za Nane Nane mwaka huu ambayo ni “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati”  
Juma Msembi ni moja ya washiriki wa Maonesho ya Nanenane anasema serikali inapaswa kuzidi kuwa kiunganishi kizuri kati ya wakulima na soko, ili wakulima wasikate tamaa katika kuzalisha chakula kingi.

Anasema kuwa anaamini Sherehe hizi zitakuwa chachu ya kujadili na kutathmini maendeleo ya sekta ya kilimo na changamoto zinazowakabili wakulima na kuangalia namna ya kuzitatua.

Katika Maonesho haya wakulima watajifunza mbinu bora za kisasa za kilimo zitakazowawezesha kupata mazao mengi na kuinua kipato chao.

Msembi anatoa wito kwa wakulima na mashirika kujitokeza katika maonesho hayo kwa sababu watapata fursa ya kujifunza mambo mengi na kubadilishana uzoefu na wataalamu mbalimbali wa kilimo.
Viewing all 110120 articles
Browse latest View live




Latest Images