Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

WOTE SCHEME mkombozi wa Wananchi - MABULA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema " Wote scheme ni Mkombozi kwa wananchi wengi walio katika Sekta isiyo rasmi na ameushahuri Mfuko wa Pensheni wa PPF kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii kupitia Ofisi za Halmashauri ili kuweza kuwafikia kwa urahisi jamii ambayo haipo kwenye ajira rasmi na kuweza kunufaika na Mfumo huo.

Mfuko wa Pensheni wa PPF unashiriki  katika Maonesho ya Nane nane kitaifa Lindi kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi  hasa  walio katika sekta isiyo rasmi kama vile wakulima, wafugaji, Wavuvi, wajasiriamali wakubwa na wadogo na wengine wote waliojiajiri wenyewe juu ya Mfumo wa " Wote scheme " ambao unawawezesha kujiwekea akiba wakati huo huo wakipata fursa za mafao ya Uzeeni, huduma za bima ya afya, mikopo ya maendeleo na mikopo ya kujiendeleza kielimu.

Vilevile kwa wale walioajiriwa wanaweza kumtumia Mfumo huu wa "Wote scheme" kama mfumo  wa hiari wa kujiwekea akiba Zaida Mahava, Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya kusini amesema kwa kutambua kundi kubwa la jamii ambalo halipo kwenye ajira rasmi wameona ipo haja ya kutoa elimu juu Mfumo wa Wote scheme ili waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na PPF kupitia Mfumo wa Wote scheme.
 Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Angelina Mabula (Mb) akiongea jambo na Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF baada ya kupewa maelezo ya namna ya Mfumo wa WOTE SCHEME unavyofanya kazi na faida zake kwa sekta isiyo rasmi wakati alipotembelea Banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
 Meneja wa PPF Kanda ya Kusini Bi Zaida Mahava akimuelekeza Mwananchi jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfumo wa hiari wa Wote scheme baada ya kupewa elimu alipofika katika Banda la PPF lililopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
 Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula (Mb) alipotembelea banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Angelina Mabula (Mb) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la PPF lililopo chini ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya Kilimo Nane Nane 2017 yanayofanyika Kitaifa Lindi katika Viwanja vya Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

Bodi ya Korosho yatangaza upatikanaji wa mbolea ya Salfa kwa wakulima wa korosho

$
0
0
Katibu na Mwanasheria toka Bodi ya Korosho Bi. Ugumba Kilasa (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea upatikanaji wa mbolea ya Salfa kwa wakulima wa korosho mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkaguzi wa ndani wa bodi hiyo Bw. Christopher Mwaya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkaguzi wa ndani toka Bodi ya Korosho Bw. Christopher Mwaya wakati akielezea upatikanaji wa mbolea ya Salfa kwa wakulima wa korosho mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AWAAPISHA MAKAMISHNA WAPYA

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonkowakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. 
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimvisha cheo Kamishna wa Divisheni ya Operesheni Billy Mwakatage,wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akimsikiliza Msemaji wa Jeshi hilo Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi,akitoa utambulisho mfupi wa Makamishna wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. 
 Kamishna wa Divisheni ya Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, akila kiapo cha Utii mbele yaKamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye,wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. 
 Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya Moto wa Jeshi la Zimamoto na, Jesuald Ikonko, akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye(watatukulia), akiwa katika picha na Kamishna wa Utawala na Fedha, Michael Shija (wapili kulia), Kamishna wa Oparesheni Billy Mwakatage (kushoto) na Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto, Jesuald Ikonko (kulia) wakati wa hafla fupi ya kuapishwa iliyofanyika leo Makao Makuu ya Jeshi, jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, MAKAO MAKUU

MKUU WA MKOA WA LINDI ATEMBELEA BANDA YA TANTRADE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi akishika mpira uliotengenezwa na Ngozi na Kiwanda cha Tanzania alipotembelea banda la TanTrade kwenye Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayoendelea mkoani Lindi. Lengo la ushiriki wa TanTrade ni kuhamasisha wazalishaji wa bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi katika halmshauri mbalimbali kushiriki maonesho ya Viwanda vya Tanzania yatakayoanza tar 7 - 11 Desemba, 2017 ikiwa ni fursa ya pekee kutangaza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania na kutoa hamasa kwa Watanzania kununua bidhaa za Tanzania 

KINANA AWASILI TANGA KUSHIRIKI UZINDUZI WA UJENZI WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA UGANDA

$
0
0
 Katbu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza alipoalikuwa kuzungumza wakati wa mkutano huo.
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
 Rais Dk John Magufuli na viongozi wengine wa meza kuu akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo
 mamia ya watu wakiwa wamefurika kwenye mkutano huo.
 Kinana akifuatana na viongozi wa CCm mkoa wa Tanga kumsikiliza Rais Nagufuli alipozungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika eneo la Pongwe
 Kinana na baadhi ya viongozi wa CCM wakimsikiliza Rais Magufuli katika eneo la Pongwe
 Rais akizungumza na wananchi katika eneo la Pongwe PICHA ZAIDI/> BOFYA HAPA

SSRA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE YANAYOENDELEA KWENYE VIWANJA VYA NZUNGUNI MKOANI DODOMA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde Msika (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa wageni waliotembelea banda lao wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kikanda katika viwanja vya Nanenane Mkoani Dodoma.
Afisa wa Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Aminah Kisisa akigawa vipeperushi kwa moja ya wadau waliotembelea Banda la SSRA kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati.
Afisa wa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlama ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ally Masaninga akifafanua kwa mmoja ya wadau waliotembelea banda la Mamlaka hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati. 

MHANDISI RAMO MAKANI AKAGUA SHUGHULI ZA UTALII NA MFUMO WA UKUSANYAJI MAPATO KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa nne kushoto) akizungumza na watalii kutoka Marekani wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame ndani ya Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro jana. Alipowauliza watalii hao ni wapi walipata habari za mlima huo, walijibu kuwa kila mtu anajua kuhusu mlima Kilimanjaro!. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba, Mhifadhi Mkuu wa KINAPA, Betrita Loibooki na nyuma yake ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia.

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa KINAPA, Steven Moshi (wa pili kulia) namna mfumo wa ukusanyaji mapato unavyofanya kazi katika Hifadhi ya Taifa Mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo, James Mbatia.
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akipanda mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana. Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Vunjo, James Mbatia, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba (kulia kwake), Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Zahoro Kimwaga (kushoto) na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (kulia).
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akisikiliza na kujibu kero mbalimbali za wapagazi wanaopandisha mizigo ya watalii katika mlima Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii na mfumo wa ukusanyaji mapato katika geti la Machame jana
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Betrita Loibook akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahifadhi, mtalii na waongoza watalii. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

TAASISI ZA KIFEDHA ZASHAURIWA KUWA NA MASHARTI NAFUU YA UTOAJI MIKOPO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akimtazama mnyama aina ya kakakuona wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi akinunua moja ya mkoba uliotengenezwa na kikundi cha Jauki kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya kutembelea banda hilo wakati wa Maonesho ya 24 ya kilimo na sherehe za Nanenane katika Viwanja vya Ngongo nje kidogo ya Manispaa ya Lindi.


BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI AGOSTI 3, 2017

Kwa simu toka :London- Mahojiano Mafupi Kuhusu Kenya London

Washiriki kutoka Tanzania wa “Young African Leaders Initiative (YALI) 2017” watembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C

$
0
0
Tarehe 2, Agosti 2017) Washiriki 42 wa Mandela Washington Fellowship 2017 kutoka Tanzania waliofika mwezi Juni, 2017, walitembelea Ubalozi wa Tanzania, Washington, D.C. na kukutana na Balozi Wilson M. Masilingi. 

YALI, ni programu iliyoanzishwa na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama kuwasaidia vijana wa Afrika kutembelea Vyuo vikuu vya Marekani kujifunza, kwa ufadhili wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani (U.S. Department of State). Baada ya kumaliza mafunzo katika vyuo mbalimbali Watanzania hao walitembelea Washington, D.C. kupokea vyeti na kutembelea Ubalozi wa Tanzania.

Balozi Masilingi aliwaasa kuwa wazalendo, kupendana na kuwa waadilifu katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu kwa kuanzisha na kukuza biashara. Aliwashauri pia kushirikiana na Ubalozi na Diaspora ya Watanzania waliopo Marekani, kukuza sekta ya utalii, biashara, elimu na ujenzi wa viwanda.
Balozi Tanzania nchini Marekani, Wilson M. Masilingi akizungumza na Washiriki wa YALI, Mandela Wahington Fellows. (kulia) Afisa wa Ubalozi, Dismas Assenga.
Yali Mandela Washington Fellows 2017 wakiongea na Mhe. Balozi.
Balozi Wilson M. Masilingi akiwa na washiriki wa YALI Mandela Washington Fellows, 2017.

A CLIMATE CHANGE INSPIRED PROJECT LAUNCHES IN DAR ES SALAAM

$
0
0
The Kilimanjaro Project, a climate change inspired project, held a meeting with environment stakeholders and members of the press to introduce the project. A prominent business leader, Mr. Ali Mufuruki was the guest of honor during the meeting which also served as the official launch of the project.

The Kilimanjaro Project is an art for change campaign for sustainable futures and climate change awareness, using Mount Kilimanjaro as an indicator that we are experiencing rapidly changing climates and environmental degradation. Through active partnerships, The Kilimanjaro Project will raise awareness through a communications campaign that will inspire sustainable behavioral change.
The Kilimanjaro Project Launch at Seacliff Hotel Dar es Salaam. From left are; An Advisory Board Member, Kelvin Twissa, Project Lead, Sarah Scott and Guest of Honour, Ali Mufuruki.

  The project will use Khangas as a tool to send message and raise awareness. In an installation planned to take place in October 2018, the kilimanjaro project lay six khangas up the six hiking trails of the mountain, each carrying a different message around key aspects of the environment; reforestation, waste management, conservation, water stewardship, and renewable energy. The six khangas will meet at the top of Mount Kilimanjaro, calling for people to come together.   

The Kilimanjaro Project is driven by the vision of better futures for coming generations. The main goal of the project is to raise awareness, enter dialogue, and create solutions around sustainable futures and climate change.

The Guest of Honour, Ali Mufuruki, addresses invited guests during the launch.

Other goals are participating in the Sustainable Development Goals by supporting conservation, tree planting, education and social enterprise / small business development in Tanzania; engaging local communities to participate in solutions for creating a climate resistant future; fundraising for related projects - conservation, reforestation and water resource management and creating active partnerships.

The first edition of the khangas, Tuje Pamoja- Let Us Come Together is available for sale in Dar es Salaam. Dar es Salaam residents can pay for the khangas through Mpesa 5588080 - The Kili Project and pick up khangas at selected points; The Novel Idea bookshop at Slipway, Masaki and at Clouds Media’s offices in Mikocheni. The event which was sponsored by Cool Blue Pure Drinking Water took place at Sea Cliff Hotel in Dar es Salaam on the morning of 3rd August and later in the day followed by a cocktail reception at Kilimanjaro Wonders Hotel in Marangu, Kilimanjaro.
The Project Lead, Sarah Scott, addresses invited guests during the launch. please upload a press release bellow

NBM yafungua tawi lake jipya mji mdogo wa Haydom Mkoani Manyara

$
0
0
 KILIO cha wakazi wa jimbo la Haydom wilaya ya Mbulu mkoani Manyara cha kukosa huduma za kibenki toka Tanzania ipate uhuru,kimepata ufumbuzi wa kudumu baada ya NMB benki, kufungua tawi katika mji mdogo wa Haydom. 
Kwa mujibu wa mbunge wa jimbo la Haydom, Flatei Massay, katika kipindi chote hicho, wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakilazimika kufuata huduma za kibenki Mbulu mjini, umbali wa zaidi ya kilometa 90.  
Mbunge Massy alisema kitendo cha kufuata huduma za kibenki umbali mrefu kiasi hicho, kumekuwa na madhara mengi na makubwa, ikiwemo gharama kubwa ya usafiri na pia usalama wa fedha. “Umbali huo umesababisha wakulima, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, kutunza fedha zao majumbani. 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Sara Msafiri Ally ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang (wa tatu kulia) kikata utepe kuashiria uzindua wa jengo la tawi la NMB lililopo katika mji mdogo wa Haydom. Wa pili kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati, Straton Chilongola.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Sara Msafiri Ally ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Hanang akizindua jengo la tawi la NMB lililopo katika mji mdogo wa Haydom.

Simbachawene ahamasisha Teknolojia ya Kilimo Ihamishiwe kwa Wakulima

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akitembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed Co kabla ya kufungua maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa kampuni hiyo,Philemon Mushi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akitembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu ya Seed Co kabla ya kufungua maonesho ya wakulima na wafugaji Kanda ya Kaskazini(Taso) kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mtaalamu wa ardhi na mimea wa kampuni hiyo,Philemon Mushi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(kulia)akipewa maelezo ya namna ya kulima bila kutumia udongo na Mtalaamu wa kilimo wa kampuni ya Rijk Zwaan alipotembelea maonesho kwenye vipando vya kampuni ya mbegu hiyo kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,George Simbachawene(wa pili kushoto)akiangalia namna kikundi cha Nronga Women Dairy cha wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kinavyojishughulisha na uuzaji wa maziwa kwenye banda la halmashauri ya Hai kwenye viwanja vya Themi,Njiro jijini Arusha,kushoto ni Mkuu wa Hai,Gelasius Byakanwa.

Nteghenjwa Hosseah - Arusha
Nane nane ni miongoni mwa maonyesho maarufu Nchini Tanzania ambayo huwagusa na kuwakutanisha wakulima, wafugaji, wavuvi wa Mjini na Vijijini, Taasisi za Serikali na binafsi zinahusika na sekta hiyo zilizopo ndani na nje ya Nchi pamoja na Wadau wa Kilimo.

Maonyesho ya Nane nane hutoa fursa kwa wadau wote wa sekta ya Kilimo kuonyesha bidhaa mbalimbali za Kilimo, kuuza bidhaa hizo, kubadilishana uzoefu na kujifunza teknolojia mbalimbali zia kuboresha Sekta ya Kilimo ili kuondokana na Kilimo cha kufa na kupona na kuwa Kilimo chenye Tija kinanachofaa kwa biashara na kutosheleza kwa chakula.

Katika historia ya maonyesho haya ambayo wakulima kutoka Halmashauri mbalimbali Nchini hushiriki ili kujifunza teknolojia hizo mpya za Kilimo kumekuwa na mabadiliko kidogo katika eneo la utekelezaji wa Teknolojia hizo katika maeneo yao.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

COSTECH YATOA MAFUNZO YA KILIMO CHENYE TIJA KWA WAKULIMA KATIKA MAONYESHO YA NANENANE MKOANI LINDI

$
0
0

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), akiwaelezea wakulima hao umuhimu wa matumizi ya MB katika siku zao katika kuinua kilimo na utafutaji wa masoko katika maeneo mengine ya ndani na nje ya nchi.

Na Dotto Mwaibale, Lindi

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetoa mafunzo ya siku moja kwa wakulima wa Mkoa wa Lindi yenye lengo la kuwasaidia kulima kilimo chenye tija. Mafunzo hayo yametolewa na mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk. Hamalord Mneney katika maonyesho ya kitaifa ya wakulima Nanenane yanayoendelea Viwanja vya Ngongo mkoani hapa leo.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo Dk. Mneney alisema Serikali imeona itoe mafunzo kwa wakulima hao ili wajifunze kilimo cha kisayansi chenye tija badala ya kuendelea na kilimo cha mazoea.


Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk. Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija kwa wakulima wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani hapa leo.

"Serikali siku zote inawajali wakulima ndio maana tukaona ni vizuri kuleta mafunzo haya kwa hawa wakulima ili kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo katika shughuli zao za kilimo" alisema Dk.Mneney.

Wakulima walionufaika na mafunzo hayo ni kutoka wilaya za Lindi, Lindi vijijini, Rwanga, Kilwa na Nachingwea ambapo kulikuwa na washiriki zaidi ya 20. Wakizungumza katika mafunzo hayo wakulima hao walisema changamoto kubwa waliyonayo ni mabadiliko ya tabia nchi na ukame unaotokana na mvua kutopatikana kwa wakati pamoja na pembejeo za kilimo kutowafikia kwa wakati.

Walitaja changamoto nyingine kuwa ni mazao ya chakula kushambuliwa na wadudu waharibifu, kukosekana kwa masoko ya mazao yao na magonjwa kama batobato na michirizi kahawia yanayoshambulia mihogo pamoja na mbegu bora.
Usikivu katika mafunzo hayo yaliyofanyika Ukumbi wa Mikutano katika Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Kilwa lililopo katika viwanja hivyo vya Ngongo.


Mkulima Omari Kijuwile kutoka Wilaya ya Kilwa alisema wakulima wana ari ya kulima lakini wanakosa mtaji baada ya taasisi za kifedha kushindwa kuwakopesha kwa kuwa hawana kitu cha kuweka dhamana ambapo aliomba umilikishwaji wa mashamba yao kwa hati za kimila ambazo zitatambuliwa na taasisi hizo ili waweze kupata mikopo hiyo.

"Tunaomba tumilikishwe mashamba yetu kwa hati za kimila ili tuweze kuaminika na kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha" alisema Kijuwile.

Mkulima Dadi Uredi Chibwana kutoka Kijiji cha Kiwalala Lindi vijijini ni vizuri wakulima wakajenga tabia ya kufuata ushauri wa maofisa ugani kuhusu kilimo badala ya kutegemea kilimo cha mazoea. Zarafi Mahamudu mkulima wa Manispaa ya Lindi alisema wakulima wamekuwa wakijitahidi lakini masoko yamekuwa ni changamoto kubwa kwao hivyo aliiomba serikali kuangalia jambo hilo kwa undani zaidi.
Mkulima kutoka Wilaya ya Kilwa, Omari Kijuwile akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.


Mkulima kutoka Wilaya ya Kilwa Anastazia Lai aliomba serikali na wadau wengine itoe msaada wa kukabiliana na wadudu waharibifu wa mazo badala ya kuacha nguvu zao kupotea bure kutokana na wadudu hao.

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Dk.Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), aliwataka wakulima hao kutumia simu zao kutafuta masoko badala ya kutumia kwa matumizi yasiyo na tija.

"Wenzenu wa nchi zingine wamekuwa wakitumia MB katika simu zao kuwasiliana na wakulima wa nchi zingine katika masuala ya kilimo na kutafuta masoko ya mazo yao badilikeni nanyi mnaweza kufanya hivyo" alisema Dk. Nyinondi.


Dadi Uredi Chibwana mkulima kutoka Kijiji cha Kiwalala Lindi Vijijini akielezea changamoto mbalimbali walizonazo wakulima katika mkoa huo.

DStv yazindua Msimu Mpya wa Soka, Ligi ya Uingereza kutangazwa kwa Kiswahili

$
0
0
Wakati vuguvugu la soka ulimwenguni likizidi kupanda, Kampuni ya Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi cha DStv imezindua kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka ijulikanayo kama ‘Full vyenga Bila Chenga’  ambapo watanzania kupitia DStv wataweza kushuhudia mubashara michuano mikubwa ya soka ulimwenguli inayotarajia kuanza hivi karibuni ikiwemo Ligi kuu ya Uingereza (PL) na ligi ya Hispania (La Liga) pamoja na makombe mengine maarufu Duniani.

Pazia la ligi kuu ya uingereza litafunguliwa jumapili Agosti 6 kwa mtanange wa ngao ya jamii kati ya Arsenal na Chelsea mchezo ambao utaonyeshwa  mubashara kupitia DStv.
 Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya Msimu mpya wa Soka ijulikanayo kama ‘Full vyenga Bila Chenga’, Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande  amesema kuwa msimu huu wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika muonekano bora zaidi huku wakiweza kufuatilia michuano hiyo kwa matangazo yatakayorushwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Msimu huu watanzania, kupitia DStv, siyo tu kwamba wataona michuano mbalimbali ya soka ulimwenguni mubashara, bali pia watayaona katika ubora wa hali ya juu yaani High Definition na zaidi ya yote, tutawapatia fursa watanzania kufuatilia ligi kuu ya Uingereza kwa lugha ya Kiswahili”.

Amesema DStv imeendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vipindi na kurekebisha bei za vifurushi ili kuhakikisha kuwa watanzania wengi zaidi wanapata fursa ya kujionea matukio mbalimbali muhimu katika Nyanja zote za maisha ikiwemo michezo na burudani. Ametoa mfano wa ligi ya Hispania La Liga ambayo inaonekana yote katika kifurushi cha Bomba. Pia baadhi ya mechi za ligi kuu ya Uingereza (PL) pia zitaonekana katika kifurushi cha Bomba.
Kwa upande wake, Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Alpha Mria amesema kampeni ya Full Vyenga bila Chenga inamaanisha kuwa wateja wa DStv, msimu huu wa soka wataweza kuliona soka kwa muonekano bora zaidi, yaani bila chenga. “Tunatambua kuwa washabiki wa soka sasa wanataka walione soka vyema, kana kwamba nao wapo uwanjani. Kwa DStv, sasa hata mtu akilambwa chenga utaiona vyema, hata kama mtu anatoka jasho utaliona. Hakuna wingu wala ukungu, ni ‘full vyenga bila chenga’  alisema Alpha.

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA NORTHAMPTON, UINGEREZA, KUFANYIKA JUMAMOSI AGOSTI 19, 2017

$
0
0

Ndugu wana Northampton kwa mujibu wa taratibu na kanuni tulizojiwekea na matarajio yetu ya muda mrefu, Kwa niaba ya kamati ndogo ya maandalizi naitisha Mkutano Mkuu na wa Uchaguzi wa Viongozi Wapya wa Jumuiya yetu ya Watanzania wote waishio Northampton na maeneo ya Wellingborough, Kattering na Corby (NORTHAMPTONSHIRE)  utakaofanyika siku ya Jumamosi tarehe 19/08/2017 katika ukumbi wa Norfolk Terrace, Semilong, Northampton NN2 6HS - Kuanzia saa kumi kamili jioni (4pm) mpaka saa mbili usiku (8.00pm).


Kamati ya maandalizi  inaomba ushirikiano wenu ili Kuepuka kupoteza muda siku ya mkutano, Tunaomba kila mjumbe mwenye ajenda ya ziada yeyote ambayo angependa iwepo katika kikao chetu basi asisite kunipatia siku nne kabla ya mkutano kwa njia ya Barua Pepe kwenda; suleimansalum160@yahoo.com au kwa kupiga simu ya Mkononi nambari 07963549935.
Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa  Tanzania Diaspora Community/Association in the United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland Ndugu Abraham Sangiwa, ambaye atatoa ufafanuzi wa jinsi Jumuiya zetu hapa Northampton zitakavoshirikiana na Jumuiya hii kuu katika malengo muhimu yanayotugusa wote Kama Watanzania tunaoishi Ughaibuni ili kupata ufumbuzi wenye nguvu zaidi kwa ushirikiano wetu.



Tujitahidi kuzingatia muda siku hiyo.  
UMOJA NA NGUVU
Suleiman Salum
Mwenyekiti Jumuiya ya Watanzania Northampton

RAIS DKT MAGUFULI APOKEWA KWA SHANGWE NA NDEREMO MKOANI TANGA, ATOA MAAGIZO MBALIMBALI KUHARAKISHA MAENDELEO YA MKOA

$
0
0
 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga pamoja na maelfu ya wananchi wa Mkata wakati akiwasili mkoani Tanga.
 Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkata wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi aliposimama eneo la Komkonga.
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukisimamishwa na maelfu ya wananchi kila alipopita.
 Wenyeji kwa wageni wakifurahia ujio wa Rais Magufuli.
 Rais Magufuli akiongea na wananchi eneo la Hale
 Wananchi wenye furaha wakimsikiliza Rais Magufuli.






MAGAZETI YA LEO IJUMAA AUG 4,2017

Mahojiano ya Mubelwa Bandio na Maduhu Emmanuel ndani ya Kilimanjaro Studios

$
0
0
Emmanuel Maduhu ni mtangazaji wa Morning Star Radio na Televisheni jijini Dar Es Salaam Mwezi Julai 2017 alifanya ziara ya kikazi nchini Marekani, ambapo alitembelea majimbo kadhaa. Mwishoni mwa ziara yake, alipata fursa kuketi na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production ndani ya Kilimanjaro Studios na kujadili mambo mbalimbali kuhusu kazi, ziara, maisha nk Karibu ujiunge nasi

Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images