Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1841 | 1842 | (Page 1843) | 1844 | 1845 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Wananchi 365 wa kijiji cha Chongoleani watafidiwa shilingi bilioni 3,035 kwa ajili ya kutoa maeneo yao, ili kupisha ujenzi wa bomba la mafuta linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga.

  Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Usimamizi wa Bandari Tanzania TPATanga, Bibi Janeth Rwuzangi katika mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.

  Bi Ruzangi amesema kuwa kwa hapa Chongoleani mradi una ukubwa wa hekta 200 zikiwemo hekta 100 zitakazotumiwa kuweka miundombinu ya mafuta ghafi. Hekta 100 zilizosalia zitatumika kwa ajili ya shughuli za TPA) kuwekeza miundombinu ya kupokea mafuta yaliyosafishwa. Vile vile eneo hili limezingatia maendeleo endelevu ya biashara ya mafuta na gesi katika siku zijazo.

  Aliongeza kuwa TPA itakuwa na wajibu wa kuhudumia meli, kuhakikisha usalama wa bidhaa, vyombo na watu pamoja na kusimamia masuala ya afya bandarini. Aidha, Majukumu la TPA yanatarijiwakujikita katika shughuli za uendeshaji wa majini ikiwemo kuwa na vyombo na boti maalumu kwa ajili ya kuongozea meli wakati wa kuingia na kutoka kwenye gati la mafuta ghafi.

  Akitoa ufafanuzi, Bi Ruzangi amesema vile vile, TPA ina jukumu la kuhakikisha inahudumia shehena ya vifaa vyote vya ujenzi katika Bandari ya Tanga kwa kushirikiana na Bandari Kuu ya Dar es Salaam. Shughuli nyingine ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya majini pamoja na usalama wa eneo la Bandari ambalo limegawanyika katika sehemu kuu mbili; ardhini kwenye gati la mafuta na majini kwenye lango la kuingilia meli na nangani.


  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akiwasili Tehran kushiriki hafla ya kuapishwa kwa Rais wa 12 wa Iran ambapo kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, Rais huapishwa Bungeni na Spika. Mheshimiwa Spika yuko Tehran kwa mwaliko wa Spika wa Bunge la nchi hiyo akiwawakilisha Maspika wa Afrika
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii katika Bunge la Iran, Mhe Dkt, Abdolreza Aziz,wakati alipotembelea Bungeni hapo kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa 12 wa Iran.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea amevipongeza vikundi saba vilivyoiwezeshwa na Mfuko wa Mbunge kwa kuweza kujiendeleza na kuanza kufikia malengo waliyojiwekea.

  Aliyasema hayo katika ziara ya vikundi saba katika kata nne za Wilaya ya Temeke akiwa ameongoza na wawakilishi kutoka Taasisi ya Global Patner ya nchini Uingereza.

  Katika kata nne alizotembelea, Mtolea amewaonyesha wageni hao namna wananchi wanavyojikita katika kujiiunua kiuchumi kwa kuunda vikundi vyao binafsi na kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ufugaji wa kuku wa mayai, kutotoa mayai, upandaji na uuzaji wa miti aina mbalimbali,  na sanaa za mikono kama batiki, vikoba na masuala ya sanaa ya uigizaji.

  Mtolea allitembelea kata ya Mtoni, Azimio, Vituka, Makangarawe na Kilakala 
   Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea  akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kata ya Mtoni katika Kikundi cha Mfendengeni wanaojishughulisha na shughuli za upandaji wa vitalu vya miti ikiwa ni katika mradi unaosimamiwa na ofisi ya Mbunge.
   Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kata ya Azimio katika kikundi cha Saccos ya Vijana kinachojishughulisha na mradi wa utotoleshaji wa mayai ya kuku.

   Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mtongani Unguja Kata ya Azimio akishuhudiwa na Mweyekiti wa Mtaa huo Zainab Liganja wakati wa ziara ya Mbunge huyo katika Miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata saba za Wilaya ya Temeke.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi eneo la Michungwani Kwa Mkonga akiwa njiani kuelekea Mkoani Tanga, kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi eneo la Kwa Mkonga akiwa njiani kuelekea Mkoani Tanga, kwa ziara ya kikazi ya siku tano.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

  Licha ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa amri ya mshtakiwa Harbinder Singh Sethi kutibiwa hospitalini hapa nchini, mpaka leo mshtakiwa huyo bado hajapata huduma yoyote ya matibabu.

   Hayo yamesemwa na wakili wa Utetezi, Alex Balomi, mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi  wakati kesi  hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama mshtakiwa amepatiwa matibabu kama amri ya mahakama ilivyotolewa wiki iliyopita. Alidai, siku mshtakiwa Seth anakamatwa, alikuwa njiani kwenda South Africa kwa matibabu.

  Hata hivyo wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Leornad Swai alidai mshtakiwe huuo atibiwe katika Hospitali ya Amana na Lugalo.

  Akijibu hoja hiyo, Swai alikiri kuwepo kwa amri ya Mahakama ya mshtakiwa kupatiwa matibabu lakini hakuna ushahidi kuwa siku mshtakiwa alipokamatwa alikuwa anakwenda Afrika Kusini kutibiwa.

  Pia alidai suala la mshtakiwa kupelekwa nje ya nchi kutibiwa nje ya nchi bado si sahihi, kwa sababu utaratibu wa mgonjwa kupelekwa nje unafahamika na kwamba haendi kwa sababu ya amri ya Mahakama.

  Aliendelea kudai kuwa, madaktari wa hapa  hawajakiri kushindwa na hakuna uthibitisho wa madaktari kwamba wameshindwa kumtibu.

  Pia aliongeza kuwa, hakuna utaratibu wa mgonjwa kupelekwa Muhimbili moja kwa moja anatakiwa kuanzia hospitali ya Amana ama Lugalo wao ndio watafanya utaratibu wa kumuhamishia Hospitali ya Muhimbili.

  Alidai Magereza ambapo Sethi anatibiwa ndio wanatakiwa kuthibitisha na kufanya utaratibu apelekweHospitali ya Amana.

  Alibainisha kuwa Amana nao hawajasema wameshindwa kumtibu hivyo aliomba aendelee kutibiwa katika Hospitali ya Amana.

  Kuhusu ombi la Wakili wa Sethi,Alex Balomi kuomba kesi itajwe ndani ya siku saba kwa ajili ya kuangalia kama amepelekwa hospitali, Swai aliomba ipangwe ndani ya Sikh 14.

  Alidai kutajwa ndani ya Siku saba ni kumsumbua mgonjwa na kwamba muda huo autumie kwenda hospitali na siyo mahakamani, aliomba ipangwe ndani ya Siku 14 kama utaratibu ulivyo.

  Pia alibainisha kuwa ndani ya Siku 14, atakuwa amefikishwa katika hospitali ya Amana ama Lugalo kupatiwa matibabu, utaratibu za Magereza zimekamilika na wao watasimamia.

  Hakimu Shaidi katika uamuzi wake alisema hajasema apeleke kutibiwa nje ya nchi, bali atibiwe hapa nchini.

  Pia aliwapa siku 14 Takukuru kama walivyoomba awali, ili kuangalia kama atakuwa amefikishwa katika hospitali ya Amana ama Lugalo kupatiwa matibabu.

  Kesi imeahirishwa Agosti17,2017.

  Katika kesi hiyo, Sethi na James Burchard  Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

  0 0

  WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, leo wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20, mshindi wao wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, aliyetangazwa jana Jumatano, jijini Dar es Salaam.

  Matagili anakuwa mshindi wa droo ya 28 ya Biko, inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.

  Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Matagili anayejishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba, alisema amepokea ushindi wake kwa furaha, baada ya kuuwazia kwa muda mrefu na kuamua kuwa mchezaji mzuri wa Biko.

  Alisema makabidhiano hayo ya fedha yamefanyika haraka, tofauti na matarajio yake, ikiwa ni siku moja baada ya kupigiwa simu ya ushindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

  “Nashukuru kwa kushinda na kukabidhiwa fedha zangu mapema, nikiamini kuwa nitapiga hatua kubwa kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa ndio matarajio yangu.

  “Nawaomba Watanzania wote waendelee kucheza Biko mara nyingi zaidi na wasikate tamaa, kwa sababu kushinda kwangu kumeniongezea imani kubwa kwa waendeshaji wa Biko,” Alisema.
  Moses Matagili mshindi wa Biko wa Milioni 20 mkazi wa Goba, katikati akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia, huku akishuhudiwa na afisa wa NMB, tawi na Bank House, jijini Dar es Salaam leo mchana.
  Mshindi wa droo ya 28 ya Biko, Moses Matagili, kushoto akipokea fedha zake jumla ya Shilingi Milioni 20 kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia katika benki ya NMB leo jijini Dar es Salaam.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi Mkuu  wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakitia saini karatasi ya makubaliano ya udhamini wa timu ya Singida wenye thamani ya Milioni 250.
  Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga  (kushoto) na  Mkurugenzi Mkuu  wa kampuni ya YARA Alexander Macedo wakibadilishana nyaraka za mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Timu ya Singida United imeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250  na kampuni ya uzalishaji mbolea ya YARA ikiwa ni katika mikakati ya kuongeza vyanzo vya mapato ya timu hiyo.

  Mkataba huo umesainiwa leo mbele ya waandishi wa habari ukishuhudiwa na kocha mkuu wa timu ya Singida United Hans Van De Pluijm.

  Akizungumza kabka ya utiaji saini wa Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga amesema kuwa mkataba huu wa mwaka mmoja utaizidi kmuimarisha timu yao katika masuala ya kifedha na zaidi wataendelea kuwakaribisha makampuni mengine kwa ajili ya kufanya nao kazi.

  Sanga amesema kuwa, katika moja ya makubaliano yaop wameshapata shamba la ekari 10000 kwa ajili ya kilimo cha Mahindi na zitasimamiwa na kamouni ya YARA ikiwemo uwekezaji wa mazao hayo ndani na nje ya nchi.

  Pia mbali na hilo, Singida United wameingua makubaliano ya kibiashara ya kusambaza bidhaa za YARA ndani ya nchi ikiwemo na kuzitangaza.

  Kwa upande wa kampuni ya YARA,  Mkurugenzi Mkuu Alexander Macedo amesema kuwa wameamua kuidhamini timu ya Singida United kwani wameona ni timu nzuri na hata nembo ya timu yao ina ua la Alizeti ambalo linatumika sana kwa ajili ya utengenezaji mafuta hayo.

  Macedo mwenyeji wa Brazili amesema watashirikiana na timu yya Singida ili waweze kuendeleza kilimo cha Mahindi nchini pampja na kuhakikisha wanawapatia wataalamu wazui wa soka kwa ajili ya mafunzo mbalimbali.
   Mkurugenzi Mkuu  wa kampuni ya YARA Alexander Macedo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.
    Mkurugenzi Mtendaji wa timu ya Singida United Festo Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.

  Wachezaji wa Simgida United wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya YARA Alexande Macedo (kulia)
  kocha mkuu wa timu ya Singida United Hans Van De Pluijm (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United Festo Sanga wakati wa utiaji saini wa makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja kwa timu ya Singida United wenye thamani ya kiasi cha Milioni 250.

  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza jambo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mtango Mtahiko akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani wakati wa kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).
  Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibook akifanya uwasilishaji wa taarifa kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa Naibu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani.
  Madiwani kutoka kata mbalimbali za jimbo la Vunjo pamoja na Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia pia wameshiriki katika kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.


  0 0


  0 0

  Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanga
  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Idara ya Uhamiaji Nchini imethibitisha kuwa  Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace John Karia ambaye ni Mgombea Urais wa TFF  katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika August 12  mwaka huu ni Raia halali wa Tanzania.

   Akizungumza na waandishi habari makao makuu ya Idara hiyo, Msemaji Mkuu wa Uhamiaji,  Ally Mtanga amesema kuwa mmoja wa wagombea wa Urais wa TFF alimkatia rufaa mgombea mwenzake Wallace Karia kuwa si raia wa Tanzania  hali ambayo inafanya akose sifa ya kuwa mgombea wa kiti hicho.

   "Wallace Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357(Rejeo la 2002) na kanuni zake, wakati huo huo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi".

  Mtanga amesisitiza  utambuzi wa uraia upo kisheria sura ya 357 (rejeo la 2002} uraia hauangaliwi Rangi, kabila wala dini.
   Idara hiyo imevitaka vilabu vyote na taasisi za michezo kuhakikisha wafanyakazi wote na wachezaji ambao raia wa kigeni wanatimiza taratibu zote za kisheria za kukaa nchini  bila kufanya hivyo sheria itashika mkondo wake .

  0 0


  0 0  Wananchi 365 wa kijiji cha Chongoleani watafidiwa shilingi bilioni 3,035 kwa ajili ya kutoa maeneo yao, ili kupisha ujenzi wa bomba la mafuta linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Tanga.

  Hayo yamesemwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Usimamizi wa Bandari Tanzania TPATanga, Bibi Janeth Rwuzangi katika mahojiano maalum na  Idara ya Habari (MAELEZO) leo.

  Bi Ruzangi amesema kuwa  kwa hapa Chongoleani mradi una ukubwa wa hekta 200 zikiwemo hekta 100 zitakazotumiwa kuweka miundombinu ya mafuta ghafi. Hekta 100 zilizosalia zitatumika kwa ajili ya shughuli za TPA) kuwekeza miundombinu ya kupokea mafuta yaliyosafishwa. Vile vile eneo hili limezingatia maendeleo endelevu ya biashara ya mafuta na gesi katika siku zijazo.

  Aliongeza kuwa TPA itakuwa na wajibu wa kuhudumia meli, kuhakikisha usalama wa bidhaa, vyombo na watu pamoja na kusimamia masuala ya afya bandarini. Aidha, Majukumu la TPA yanatarijiwakujikita katika shughuli za uendeshaji wa majini ikiwemo kuwa na vyombo na boti maalumu kwa ajili ya kuongozea meli wakati wa kuingia na kutoka kwenye gati la mafuta ghafi.

  Akitoa ufafanuzi, Bi Ruzangi amesema vile vile, TPA ina jukumu la kuhakikisha inahudumia shehena ya vifaa vyote vya ujenzi katika Bandari ya Tanga kwa kushirikiana na Bandari Kuu ya Dar es Salaam. Shughuli nyingine ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya majini pamoja na usalama wa eneo la Bandari ambalo limegawanyika katika sehemu kuu mbili; ardhini kwenye gati la mafuta na majini kwenye lango la kuingilia meli na nangani.

  Kwa upande wa ajira za TPA Ruzangi amesemawafanyakazi ambao wataajiriwa ni pamoja na mabaharia, wahandisi, mafundi, wahasibu, wachumi, watakwimu, vibarua mbalimbali kwa ajili ya nguvu kazi n.k. Sehemu ya wafanyakazi hawa watatokana na waliopo sasa kwenye Bandari watakaopangiwa kazi hizo. Hata hivyo TPA inatarajia kuajiri wengine ambao watalazimika kufanya kazi hizo kulingana na taratibu za ajira za TPA.


  0 0


  Timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom tanzania bara zimekabidhiwa vifaa mbalimbali na mdhamini mkuu wa ligi hiyo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni 500/=

  Akikabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa kampuni hiyo, Hisham Hendi, alisema kuwa  kwa mara nyingine tena katika kuhakikisha ligi ya soka nchini inaenda vizuri Vodacom inakabidhi  vifaa mbalimbali vya ligi ambavyo ni jezi mbalimbali, viatu vya mazoezi na mechi, soksi, vilinda ugoko, nguo za mazoezi, nguo za kawaida, gloves, mabegi ya kusafiria, nguo za marefa, bendera, substitution boards  na vifaa vingine vingi vinavyohitajika. “Tunajisikia furaha  kukabidhi vifaa hivi siku ya leo tukiwa tunatekeleza  matakwa ya mkataba wa udhamini, ni imani yetu kwamba timu zitakazoshiriki ligi zimejiandaa vya kutosha kwa msimu mpya wa ligi  wa 2017/2018”Alisema Hendi.

  Hendi alisema Vodacom inaendelea kudhamini ligi kuu kwa sababu soka ni mchezo unaopendwa sana hapa nyumbani ukiwa na washabiki wengi hivyo inapenda kuona wananchi ambao baadhi yao ni wateja wake wanapata burudani ya mchezo waupendao pia siku zote inaamini kuwa michezo ni ajira kubwa duniani kote, ikiendelezwa inaweza kubadilisha maisha ya watu wengi na taifa kunufaika kwa mapato makubwa ya kodi kutoka katika sekta hii.
  Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia) akimshuhudia Mwakilishi wa timu ya Yanga ambaye ni Afisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara(kushoto) baada ya timu hiyo kukosa mwakilishi akimtania mmoja wa vijana aliyeitambulisha jezi ya Yanga itakayotumika katika msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2017/2018 wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura akipokea keki toka kwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)kuashiria Uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)akimpongeza mmoja wa vijana aliyeitambulisha jezi ya Azam FC wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam,Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura na Mwakilishi wa Timu hiyo, Jafari Maganga.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura(kushoto)akiwashuhudia mwakilishi wa timu ya  Simba Afisa habari wa timu hiyo, Haji Manara(watatu kushoto)pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi(kulia)wakiwapongeza vijana walioitambulisha jezi ya nyumbani na ugenini ya timu hiyo wakati wa hafla iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ya  kukabidhi vifaa kwa timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo jana jijini Dar es Salaam.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Kijana Emidio Nkoma mkazi wa kijiji cha Londo kilichopo Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma, Aelezea mkasa wa baba yake mzazi pamoja na bibi yake walivyoliwa na mamba katika Daraja la mto Rwika ambalo linaunganisha kijiji cha Londo na Ngido .

  0 0

   Muwezeshaji kutoka Tanzania Media Foundation Dustun Kamanzi akizungumza na Waandishi wa habari walioshiriki katika mafunzo ya uandishi Nishati Jadilifu
    Mwandishi Mwandamizi Alan Lawa  akizungumza jambo wakati wa majadala uliokuwa ukiendelea katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na TMF na Hivos Kenya
   Muwakilishi wa Hivos Kenya , Maimuna Kabatesi akizungumza juu ya Hivos  Kenya katika kusaidia masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi
   Waandishi  walioshirikikatika mafunzo hayo wakijadili jambo wakati wa kazi za makundi.


  0 0

   Mwenyekiti wa Mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam Bw. Okare Emesi (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini waliopata toka kampuni ya Startimes na Sibuka mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa chama hicho Bw. Peter Mpangala na kushoto ni Afisa Mahusiano toka Startimes Bw. Samwel Gisayi.
  Mkurugenzi wa Masoko wa chama hicho Bw. Peter Mpangala (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu udhamini waliopata toka kampuni ya Startimes na Sibuka mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Okare Emesi na kushoto ni Afisa Mahusiano toka Startimes Bw. Samwel Gisayi.

  Picha Eliphace Marwa - Maelezo


  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-TABORA

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ameagiza kuanzia msimu ujao wa kilimo kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi ni lazima alime heka mbili za alizeti kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kujenga Viwanda vya kusindika na kuzalisha mafuta hayo kuanza ujenzi mkoani humo.

  Bw. Mwanri alitoa kauli hiyo jana wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nanenane kwa Kanda ya mikoa ya Magharibi yaliyofanyika mkoani Tabora.

  Alisema zao la alizeti katika mkoani Tabora linastawi sana na ikiwa wakazi wake watalima kwa wingi Kampuni mbalimbali zitajitokeza kwa wingi kuja kujenga viwanda vya kuzalisha mafuta hayo.

  Bw.Mwanri alisisitiza kuwa wawekezaji wengi wamekuwa wanashindwa kuja kujenga viwanda vya usindikaji wa mafuta hayo kwa sababu siku za nyuma zao hilo limekuwa halitiliwi mkazo na kufanya uzalishaji kuwa wa chini sana , lakini hivi sasa hiyo itakuwa ajenda ya Mkoa kama mkakati mojawapo wa kuwavutia watu kuja kujenga viwanda.

  “Ndugu zangu Wakuu wote wa Wilaya na Wakurugenzi kuanzia sasa akili yetu na agenda yetu kubwa iko katika kuhakikisha kuwa kila mkazi wa Tabora analima heka mbili za alizeti kuanzia msimu ujao wa kilimo ili tuwe na malighafi nyingi kwa ajili ya kulisha viwanda vitakavyoanzishwa kwa mwaka mzima” alisema Mkuu huyo Mkoa.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Wasanii wa Bongo Freva  hapa nchini wameaswa kukuzingatia matumizi ya Lunga pamoja na mavazi  ili kuepushafungia fungia ya kazi zao za sanaa hayo yamesemwa leo wakati wa mkutano wa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe na wasanii wa nyimbo za bongo Freva pamoja na wadau mbalimbali na sanaa hapa nchini jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wasanii wa nyimbo za Bongo Freva hapa nchini kuhusu maswala mbalimbali yanayowahusu wasanii hao, pia wameshauliwa kujiunga kusajili kazi zao pamoja na kulipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupata miongozo mbali mbali COSOTA pamoja na BASATA.
   Baadhi ya wasanii wa Nyimbo za Bongo Freva  hapanchini kutoka kulia ni Wastara Thomasi, msanii wa Bongo Fleva, Khadija Shaban (Keisha) na Witnes Mwajaga wakiwa katika Mkutano wa wasanii wa Bongo freva na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe jijini Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe akipokea saa ya ukutani ikiwa ni Rambirambi kutoka kwa wasanii wa Mziki wa Bongo Freva  kama pole kufiwa na Mkewe.
                     Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii. 
  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga ameagiza shughuli zote za upimaji wa ardhi kusimama kwa sasa mpaka watakapotoa kibali cha upimaji.

  Mkuu Wilaya alitoa agizo katika mkutano na wananchi wa wilaya kuhusiana na mgogoro wa ardhi, ambapo vijiji vinne vinavyodaiwa kuvamia shamba la familia ya Rajwani mwenye asili ya kihindi lenye ukubwa wa ekari 2472.

  Vijiji hivyo vinne ni Mwambaya,Lunzando,Mipeko na mlamleni vilivyopo kwenye Kata ya mipeko na Tambani.

  Sanga amesema kuwa kwa sasa hakuna mtu kutoka Halmashauri wala maafisa mipango miji kupima ardhi mpaka awe na kibali kutoka wilayani na kuongeza kuwa Madiwani na Wenyeviti wa vitongoji kutoruhusu mtu kupima ardhi mpaka awaoneshe kibali kutoka wilayani.

  Aidha amewataka wananchi wa vijiji hivyo kifanya kazi zao kwa Uhuru bila hofu yeyote kwani wilaya hiyo ipo salama."tumejipanga vizuri Mimi mwenyewe ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na wahakikisheni mupo salama,msiache kwenda mashambani,msiache mazao shambani kavuneni mazao yenu hakina wakuwabigudhi.alisema Sanga.

  Wakati huohuo ametoa wito kwa madereva wabodaboda wilayani humo wametakiwa kuvaa kofia ngumu pindi wanapoendesha pikipiki na kuacha kupakia watu wawili kwa pikipiki moja ‘Mishakaki’.

  Naye Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdalah Ulega amewatoa hofu wananchi hao kwa kuwa suala lao linashughulikiwa na wamempa notisi ya siku 90 ya kujieleza kuhusiana na eneo hilo.

  Ulega aliwaahidi wananchi hao kuwachangia kiasi cha shilingi milioni moja kama sehemu ya mchango wake katika kusaidia kutatua tatizo hilo.
   .Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungumza na wananchi wa vijiji vinne ambavyo vina mgogoro wa ardhi katika mkutano uliofanyika Mwanambaya .
   Mbunge wa jimbo la Mkuranga , Abdalah  Ulega akizungumza na wapiga kura wake juu ya mgogoro wa shamba lenye ekari 90 katika kijiji cha Mkuranga.
   .Sehemu ya wananchi wakimsikiza mkuu wa wilaya juu ya mgogoro unao wakabili

older | 1 | .... | 1841 | 1842 | (Page 1843) | 1844 | 1845 | .... | 3353 | newer