Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1840 | 1841 | (Page 1842) | 1843 | 1844 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Wetu - MAELEZO

  Kufuatia wito wa Rais John Pombe Magufuli alioutoa hivi karibuni, hadi kufikia jana tarehe 01 Agosti, 2017 jumla ya wakimbizi 6,700 raia wa Burundi wameshajiorodhesha kurejea nchini mwao kwa hiari.

  Kufuatia hatua hiyo, Mkutano wa pande tatu utakaojumuisha Serikali za Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) unatarajiwa kufanyika mwishoni wa mwezi huu kujadili namna ya kuwarejesha nchini mwao wakimbizi hao kwa kuzingatia sheria za kimataifa zinazohusu wakimbizi.
   Katika mahojiano na mwandishi wetu ofisi kwake jana, Mkurugenzi Idara ya Huduma za Wakimbizi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bwana Harrison Mseke alieleza kuwa tangu kutolewa kwa wito huo, Wizara imekuwa ikiwamahasisha wakimbizi hao wa kujiorodhesha kwa hiari ili waweze kurejea nyumbani.

  Akiwa katika ziara yake kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa, Rais Magufuli alitoa wito kuwataka wakimbizi raia wa Burundi kurejea nyumbani kwa hiari kwa kuwa hali ya usalama nchini mwao ni nzuri ambapo wakati akitoa wito huo tarehe 20 Julai, 2017 huko Ngara aliambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza ambaye nae aliwahakikishia wakimbizi hao kuwa hali ni shwari nchini Burundi. 

  Kwa mujibu wa Bwana Mseke, hivi sasa kuna wakimbizi raia wa Burundi 276,692 kati ya wakimbizi 348,019 walioko nchini. Wengine ni  wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) 70,840, Wasomali 150, na wengine (mchanganyiko) 337. 

  Alifafanua kuwa kati ya idadi hiyo ya wakimbizi raia wa Burundi 242,340 waliingia nchini baada ya mwezi Aprili, 2015 kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo.
  Akizungumzia mwendo wa uingiaji wakimbizi kutoka Burundi, alieleza kuwa kwa sasa kasi imepungua kutoka wastani wa wakimbizi 1,000 kwa siku kati ya mwezi Agosti hadi Disemba, 2016 hadi wastani wa wakimbizi kumi kwa siku katika miezi ya hivi karibuni.


  0 0

  Leo tarehe 2 Agosti, 2017, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yao nchini Vietnam, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba, wamekutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Vietnam, Mhe. NGUYEN XUAN PHUC, ambapo walijadili namna ya kuimarisha mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi na biashara baina ya nchi hizo mbili. Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya kukamilisha kongamano la tatu la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Vietnam lililofanyika siku hiyo hiyo ya tatu ya ziara yao.

  Katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu wa Vietnam aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua nzuri za kiuchumi inazoendelea kupiga kwa kuzingatia kwamba Tanzania ni kati ya nchi kumi duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi na ni ya kwanza kwa Afrika Mashariki. Aliishukuru pia serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuisaidia kampuni ya Halotel katika utoaji wa huduma zake za mawasiliano na hasa vijijini. 
  Aliwakikishia Mawaziri hao kuwa Vietnam itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinafikia malengo ya biashara yaliyowekwa na Marais wa nchi hizi hapo mwaka 2016 nchini Tanzania.

  Kwa upande wake Waziri Mwijage alieleza kuwa Serikali ya Tanzania inatambua na kuenzi urafiki na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizi mbili. Alieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuendeleza mikakati ya kutekeleza maelekezo ya viongozi wa nchi hizo mbili kwamba ifikapo mwaka 2020 biashara kati ya nchi hizi ifikie dola za marekanii bilioni 1. 


  Hivyo, kongamano la uwekezaji lililofanyika hapo mjini Hanoi, limeweza kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania wapatao 30 na wafanyabiashara wa Vietnam zaidi ya 200. Aidha, kutokana na kongamano hilo, changamoto mbalimbali zilielezwa ambazo zinarudisha nyuma jitihada za wafanyabiasha. 
  Alieleza kuwa tayari amekutana na Waziri wa Biashara na Biwanda wa Vietnam na wamekubaliana timu ya wataalmu ikutane Dar es Salaam mwezi Septemba kuanza kufanyia kazi mapungufu hayo kwa pande za nchi zote. Nae Waziri Dkt.  Tizeba alimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa nafasi aliyowapa ya kukutana pamoja na kuwa ana majukumu mengi. 

  Alieleza kuwa changaoto nyingi zilizoelezwa na wafanyabiashara katika kongamano la biashara zingeweza kutatuliwa iwapo hati za makubaliano zilizopendekezwa na nchi hizo zingekuwa zimekamilishwa na kuwekwa saini. 
  Hivyo, alimuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu asaidie kwa upande wa Serikali ya Vietnam ili hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya taasisi mbali mbali za Tanzania na Vietnam zikamilishe na kurahisisha biashara.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZRB na Uongozi wa ZRB katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZRB Bw.Saleh Sadik (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)akiwa Mwenyekiti wa kikao cha Siku moja cha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZRB na Uongozi wa ZRB katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,(kulia) Mshauri wa Rais Ushirikiano wa Kimataifa na Uchumi Mhe,Mohamed Ramia Abdiwawa.
  Kamishna wa Mapato ZRB Nd,Amour Hamil Bakari (katikati) akichangia wakati wa kikao cha siku moja kilichowajumuisha Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZRB na Uongozi wa ZRB na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja, wengine (kulia) Naibu Kamisha wa ZRB Nd,Halima Shamte na (kushoto) Mhasibu Mkuu wa Serikali Mwanahija Almasi Ali.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Nd,Khamis Mussa (kulia) akitoa maelezo wakati wa kikao cha Siku moja cha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZRB na Uongozi wa ZRB katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,mweyekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),(kushoto) Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalis Salum Mohamed.
  Mshauri wa Rais maswala ya Uwezeshaji Mhe. Abdulrahman Mwinyijumbe akichangia katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,mweyekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),ambacho kiliwajumuisha Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango,Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZRB na Uongozi wa ZRB. Picha na Ikulu, Zanzibar.

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

  WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba, amewataka askari wa uhamiaji nchini kuhakikisha wanataifisha magari na vyombo vya usafiri wanavyokutwa navyo wahamiaji haramu, wakati wanapokamatwa. Aidha amewaagiza askari hao kuwakamata watu wanaowalipia faini wahamiaji haramu na kuwafungulia mashitaka.

  Mwigulu aliyasema hayo, wakati alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) na ofisi mpya ya uhamiaji ya mkoa wa Pwani ambazo zote zipo wilayani Kibaha. Alisema magari na vyombo vinavyosafirishia wahamiaji haramu ikiwemo boti vitaifishwe na kutumika katika kazi za ujenzi wa taifa.


  "Haiwezekani mtu aingie nchini kwa makusudi bila kibali halafu inapotakiwa kulipa faini kutokana na kosa hilo atokee mtu kuwalipia faini kwa haraka jambo linalosababisha vitendo hivyo kuenea kwa kasi” alisema Mwigulu.

  Mwigulu alieleza kwamba, ni lazima iangaliwe, jamii inapaswa kujiepusha na kushirikiana na kundi hilo ili kupunguza wimbi kubwa la wahamiaji haramu nchini. Waziri huyo alisema, iangaliwe njia  za kudhibiti wahamiaji hao pale inapotokea kukamatwa ama kushtakiwa  na kuhukumiwa pasipo kuwalinda kwa kuwalipia faini.

  "Mkiwakamata pia na magari myataifishe siku hiyo hiyo na kuyapeleka magereza ili yakabebe mawe, na hata mkiwakamata kwenye boti taifisheni hizo boti hakuna kuweka viporo"alisema Mwigulu.

  Awali akitembelea ofisi mpya katika jengo la vitambulisho vya taifa (NIDA), Mwigulu aliwaagiza watendaji wa ofisi hiyo kuhakikisha wanafanyia kazi agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuunganisha utambulisho wa jumla kwa wananchi.

  "Wananchi wanatakiwa wawe na utambulisho wa aina moja pekee unaojumuisha taarifa zao zote" alisisitiza Mwigulu.

  Nae afisa Uhamiaji Mkoani Pwani, Plasida Mazengo alisema ofisi yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa vitendea kazi hali inayosababisha kufanyakazi kwenye mazingira magumu. Alimuomba waziri huyo kuangalia namna ya kusaidia kutatua changamoto hizo ili waweze kufanya kazi zao kifanisi zaidi kwa maslahi ya watanzania.

  Kaimu mkurugenzi wa uzalishaji vitambulisho (NIDA) Alfonce Malibiche alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 99.9, na utakapokamilika utawarahisishia wananchi kupata huduma kirahisi na jengo litaanza kazi rasmi mwishoni mwa mwezi huu .

  0 0

  Wakulima mkoani RUVUMA wametakiwa kuzalisha mazao yeye tija ili kukuza sekta ya kilimo na kupanua uzalishaji ili kuifanya nchi ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo mkoa wa ruvuma ni kati ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi hapa nchini Tanzania.HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wana familia wa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri katikl idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wana 
  familia wa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri katikl idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapa pole wana 
  familia wa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri katikl idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka sini katika kitabu cha maombolezi nyumbani kwa Marehemu Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu ambaye alikuwa ni mhadhiri katikl idara ya Kemia, ameacha mjane na watoto watatu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Mama Mary Mdachi, mjane wa Marehemu  Dkt. Stephen Juma Mdachi aliyefariki Jumanne Agosti 1, 2017 katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Picha na IKULU

  0 0

  BAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, droo ya 28 imefanyika leo, huku mkazi wa Goba, jijini Dar es Salaam, Moses Matagili, akifanikiwa kuibuka kidedea kwa kushinda Sh Milioni 20.

  Droo hiyo iliyofanyika jana, ilichezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.

  Akizungumza baada ya kumpata mshindi huyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema sasa ni wakati wa kuchangamkia fursa ya kuibuka na mamilioni kwa kucheza Biko inayotoa ushindi wenye fursa ya kiuchumi.

  Kajala Masanja Balozi wa Biko Tanzania.
  Alisema kwamba droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 inafanyika Jumatano na Jumapili, huku Jumatano hii ikienda kwa Matagili, ambaye ni mkazi wa Goba, sanjari na washiriki kuvuna zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

  “Tunampongeza mshindi wetu wa droo ya 28, Matagili kwa kuvuna donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko, hivyo tunawaomba Watanzania wengine waendelee kucheza Biko ili waweze kujipatia zawadi mbalimbali kutoka kwetu.

  “Jinsi ya kucheza ni rahisi maana bahati nasibu yetu inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money, ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456,”Alisema.

  Naye mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, alisema mchezo wa Biko unachezwa kwa kufuata sheria zilizowekwa, jambo linaloongeza ufanisi kwa Watanzania wote kucheza na kushinda zawadi za Biko.

  “Tunawakumbusha Watanzania kuwa Biko ni mchezo rahisi na ambao unachezeshwa kwa uangalizi mkubwa wa bodi yetu, hivyo kwa wale wanaocheza waelewe kuwa huu ni mhcezo salama,” Alisema.

  Wakati Matagili akiibuka kidedea kwa kuzoa Sh Milioni 20 kutoka Biko huku akitarajiwakukabidhiwa fedha zake mapema iwezekanavyo, tayari mshindi wa droo ya 27, Viane Kundi wa Irnga, akiwa ameshapokea fedha zake Jumatatu iliyopita.


  0 0


  Moja ya Benki inayokua kwa kasi nchini, Benki ya FINCA Microfinance, leo imetangaza kampeni ya miezi miwili inayofahamika kama 'FikaNaFINCA' Kampeni hii itampa fursa anayefwatilia kurasa za kijamii ya benki hiyo nafasi ya kujishindia tiketi ya kwenda na kurudi bure baada ya kuposti picha ya bahasha ya tiketi yenye nembo ya FIKA NA FINCA na pia kupendwa na watu wengi.

  Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance, Nicholus John alisema kuwa washindi watakuwa na nafasi ya kupata tiketi za usafiri wa anga na barabara ya kwenda na kurudi kutoka mashirika ya usafiri wa anga ya ndani ya Air Tanzania (ATCL) na Auric Air na pia kwa mabasi yanayoenda bara yakiwemo mabasi ya kampuni za Ngorika, New Force na Isamilo.

  "FINCA inathamini wateja wake na jamii kwa ujumla, katika kuonyesha hilo, ndo maana tumeleta kampeni hii itakayoenda kwa miezi miwili huku mshindi kutangazwa kila wiki. Jinsi ya kushinda ni rahisi sana, piga picha tiketi yako yenye nembo ya FIKA NA FINCA, posti kwenye kurasa ya Facebook na Instagram ukiweka #FikaNaFINCA kwenye caption, alafu aalike ndugu jamaa na marafiki kuipenda."alisema John.

  John aliongeza: "Ninatoa wito kwa Watanzania kuchukua fursa hii ya kipekee na kushiriki kwa wingi ili kushinda ofa hii ya kusafiri bure".

  Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, Benki ya FINCA Microfinance Bwana Nicholous John akionyesha mfano wa tiketi ya ndege itakayotumika katika kampeni yao iliyopewa jina la FikaNaFINCA iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian Fungamtama

  Kutoka kushoto ni Meneja usafirishaji wa kampuni ya Super Feo Bw Masumbuko akifuatiwa na Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian Fungamtama Bi. Lilian Fungamtama na Mtaalamu wa Masoko wa Benki ya FINCA Bw. Noel Mulumba wakionyesha mifano ya tiketi za usafirishaji ambazo wateja watapaswa kupiga picha na kushirikisha  wafuasi wako katika mitandao ya kijamii ili kujishindia tiketi ya bure katika kampeni iliyopewa jina la FikanaFINCA .


  0 0


  Shirika la chakula Duniani (WFP) limetambulisha mikakati yake mitano yakutokomeza njaa nchini itakayofanyika ndani ya miaka minne kuanzia
  mwaka huu hadi 2021.

  Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha WFP na waandishi wa Habari za mtandaoni, mkurugenzi wa WFP Tanzania,Michael Danford ameitaja mikakati hiyo kuwa, ni kuwasaidia wakimbizi na jamii zao, kutoa msaada wa lishe hasa katika maeneo ya Dodoma na Singida. 

  Aidha alitaja mikakati mingine kuwa ni, kuimarisha mfumo wa chakula Serikalini na ubunifu wa namna ya kupata chakula cha ziada. 
  Akifafanua namna ya utekelezaji wa mikakati hiyo, amesema, watatoa
  msaada wa fedha kwa wakimbizi wapatao 400,000 kwa ajili ya kuwawezesha kupata mahitaji yao wanayotaka pia kuiongezea serikali kipato. 

  “Kuna faida zaidi ya kutumia fedha kuliko chakula kwa wakimbizi kwani
  kila dola moja iyakayotumika inaweza kuimarisha uchumi wa nchi sababu
  fedha zitakazoingia zitakuwa za kigeni”. 

  Aidha ameongeza, WFP kwa kushirikiana na wadau wengine watatoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuwaunganisha kwenye masoko ya uhakika. 

  ” Tangu Tanzania ipate Uhuru, WFP ndio iliyosaidia wakulima kwa Mara ya
  kwanza kupata mikopo kutoka benki, tulikaa na taasisi za fedha
  tukawashawishi kuwaamini wakulima na kuanza kuwapa mikopo,” amesema.
   Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford akielezea kwa undani namna shirika hilo litakavyoweza kufanya kazi nchini Tanzania na kuitaja mikakati mitano waliyo iweka kwa ajili ya Shirika hilo.
   Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa Habari za Mtandaoni.
  Mmoja wa wafanyakazi wa WFP Bw. Masasa Makwasa akielezea namna Programu ya ‘Farm to Market Alliance’ inavyofanya kazi na inavyowasaidia wakulima katika shughuli zao za Kilimo.
   Mtaalam wa mambo ya usimamizi wa Fedha ambaye pia ni Blogger Bi. Monica Joseph akiuliza swali linalohusiana na maswala ya fedha hasa kwa wakulima ambao WFP wanaofanyanao kazi.
   Bi. Alice Maro kutoka WFP akielezea mambo zaidi kuhusu Shirika hilo.
   Baadhi ya Bloggers wakiwa katika mkutano huo
  Picha ya Pamoja ya watumishi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) pamoja na waandishi wa Habari za Mtandaoni (Bloggers).Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania

  0 0


  0 0

  Wakulima mkoani RUVUMA wametakiwa kuzalisha mazao yeye tija ili kukuza sekta ya kilimo na kupanua uzalishaji ili kuifanya nchi ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ambapo mkoa wa ruvuma ni kati ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi hapa nchini Tanzania.

  0 0
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana  amepokea Jumla ya kompyuta  za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 kutoka kiwanda cha utengenezaji wa nguo zitokanazo na pamba ya Tanzania cha NIDA Textile Ltd. 

  Makonda amesema kmpyuta hizo atazitoa kwa Vituo vya Polisi 20 kwa ajili ya kufungwa mfumo wa kisasa wa kuripoti taarifa za uhalifu zilizoripotiwa kwenye Vituo vya Polisi kila siku (Crime Statistic Management Information System) kupambana na uhalifu.

  Faida za Mfumo ni kumsaidia Mwananchi kupata taarifa za ndugu yake aliepotea pasipokujua yupo wapi kwa kumuangalia kwenye mfumo kama anashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi mfumo utaonyesha taarifa zake kwa wakati kwenye kila Kituo.

  Aidha mfumo utasaidia viongozi kupata taarifa za uhalifu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi kwa wakati na kupunguza uhalifu kwani taarifa zote za wahalifu zitaonekana kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Mkoa,Wilaya na Mkuu wa kituo hivyo kusaidia viongozi kufanya maamuzi.

  Mfumo pia utaondoa Rushwa na matukio ya Wananchi kubambikiziwa kesi kwani kila atakaefikishwa kituo cha Polisi viongozi wote akiwemo Mheshiniwa Makonda atapata atajua.

  Mfumo pia utamuwezesha kiongozi kujua idadi na aina ya uhalifu unaofanyika kwa siku,eneo ambapo matukio hujirudia mara kwa mara sanjari na mhalifu ambae matukio matukio yake ya uhalifu yamekuwa yakijirudia maeneo mbalimbali.

  “Tunaachana na kuandika taarifa kwenye makaratasi na makaunta au madaftari kwenye Vituo vya Polisi ambayo baada ya muda mfupi yanapotea na kumuacha Mwananchi hajui kesi yake imeishia wapi, huu mfumo ni ukombozi na mwonekano mpya wa Jeshi la Polisi na hata Wananchi wataachana na matatizo ya rushwa na watu kubambikiziwa kesi” Alisema Makonda.

  Mfumo wa CSMIS utachukuwa taarifa za Mhalifu kuanzia anapoingia kituo cha polisi CRO, Jina la Mhalifu, Aina ya kesi,jina la Mpelelezi, Hakimu, Mahakama anayopelekwa na kama amehukumiwa kulipa faini au kifungo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza amesema kampuni yao imeamua kuunga mkono jitiada za Mheshimiwa Makonda katika dhamira yake ya kufanya Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam. 
   Baadhi ya Kompyuta hizo
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,Paul Makonda(wakwanza kulia) akikabidhiwa  Computer za kisasa 100 zenye thamani ya Shillingi Million 210 na  Mkurugenzi wa Kiwanda cha NIDA Bwana Mohamed Hamza.

   

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi jana amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa maeneo ya Nakasangwe, Nakalekwa na kuwapa ujumbe kuwa mgogoro wa ardhi uliodumu eneo hilo kwa miaka 13 kiasi cha kusababisha vifo sasa suluhu yake imepatikana.

  Hapi amesema kuwa ikiwa ni muendelezo wa utatuzi wa migogoro ya ardhi wilayani Kinondoni ofisi yake ilizikutanisha pande mbili za wenye mashamba na wakazi ambazo kwa miaka kadhaa zimekua kwenye mgogoro mkubwa na kufanya nao mazungumzo yaliyoweka msingi mzuri wa kumaliza mgogoro huo.

  Hapi amewahakikishia wananchi hao kutokuwa na wasiwasi na kwamba serikali wilayani Kinondoni imeamua kutumia falsafa ya

  "pata kidogo poteza kidogo" (win win)ili kumaliza mgogoro huo baina ya pande mbili na kurejesha hali ya amani kayila eneo hilo.

  "Tumeamua sasa eneo hili lote lipimwe viwanja, ili wakazi wote mliohakikiwa kila mmoja apate kipande cha ardhi cha kuishi na familia yake na viwanja vinavyobaki wapate wenye mashamba. Hii ndiyo njia pekee ya kuweza kuwafanya muishi kwa amani katika mji uliopimwa na kupangwa vizuri."Alisema DC Hapi

  Aidha, Hapi aliwaeleza wananchi hao kuwa katika eneo hilo zaidi ya viwanja 6000 vitapatikana na hivyo kuwatoa shaka kuwa wakazi wote zaidi ya 3000 waliohakikiwa kila mmoja atapata ardhi iliyopimwa huku wenye mashamba nao wakipata viwanja vitakavyobakia ili waweze kuviendeleza au kuviuza vikiwa na hati miliki.

  DC Hapi amesema kazi ya upimaji wa ardhi katika eneo hilo inatarajiwa kuanza haraka na kumalizika ndani ya kipindi cha miezi mitatu chini ya kampuni ya Afro Map ambayo pande mbili zimeichagua kufanye kazi hiyo.

  "Nawapa kampuni hii miezi mitatu tu, kazi ya upimaji iwe imekamilika eneo hili ili wananchi wangu waishi kwa amani wakijua serikali yao ipo kuwasaidia." Alisema DC.

  Mgogoro wa Nakasangwe ulianza mwaka 2004 na hivyo kudumu kwa miaka 13 kipindi ambacho kilitawaliwa na chuki, uhasama na uadui mkubwa baina ya wenye mashamba na wananchi waliovamia mashamba hayo. Watu kadhaa walipoteza maisha katika mgogoro huo.

  Wananchi wote wanaounda pande mbili za mgogoro wamemshukuru DC Hapi na kushikana mikono kama ishara ya mwisho wa mgogoro huo na mwanzo mpya. 


   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi akizungumza jana mbele ya wananchi  wa Mtaa wa Nasarangwe, Kata ya Wazo   juu   ya kampuni ya Afro Map imepewa kazi upimaji wa viwanja  itakayokamilika  ndani ya miezi mitatu badala ya miezi nne iliyokuwa ikifahamika hapo awali.
   Diwani wa Kata ya Wazo Joel Mwakalebela akizungumza leo na wananchi wa juu ya kutoa ushirikiano katika kuchangia gharama za upimaji wa viwanja ili zoezi hilo lisikwame.
   Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi

  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM, Mtwara

  BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeelezea kuridhishwa na kasi pamoja na viwango vya miradi ya ujenzi ya barabara inayofadhiliwa na benki hiyo katika Ukanda wa Kusini, na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa na wananchi wake.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo anayesimamia Kanda wa Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, baada ya kutembelea na kukagua barabara ya Tunduru-Nangaka-Mtambaswala, mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilometa 202.2.

  Barabara hiyo yenye vipande vitatu imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 180 kupitia ufadhili wa benki hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali ya Tanzania.

  Dkt. Weggoro amesema kuwa barabara hiyo ambayo upande mmoja inaunganisha Tanzania na Msumbiji, itachochea maendeleo ya wananchi kutoka pande hizo mbili kwa kusafirisha watu na bidhaa kwa urahisi zaidi.

  “Nimeona mabadiliko makubwa sana, si tu kwa barabara, lakini maisha ya watu, mabadiliko ambayo ni dhahiri yanatokana na hii miradi ya barabara ambayo imefungua fursa nyingi za maendeleo, watu wanafanyabiashara lakini pia wanatembeleana!” alisema Dkt. Weggoro.

  Alitoa wito kwa Watanzania kuchangamkia fursa ya uwepo wa barabara hizo kujiletea maendeleo kwa kufanyabiashara hivyo kujikwamua kiuchumi.

  Mhandisi Heldaus Jerome kutoka Wakala wa Barabara -Tanroads, Makao Makuu, alisema kuwa barabara hiyo ya Tunduru-Mangaka-Mtambaswala, ina vipande vitatu, kutoka Mangaka – Nakapanya (km 70.5), Nakapanya – Tunduru (66.5) na Mangaka – Mtambaswala (km 65.5)

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Klabu saba za Rotary za Dar es salaam kwa kushirikiana na Benki M jana zimezindua mbio na matembezi ya Rotary Dar Marathon ambapo kwa mwaka huu yanafanyika kwa mara ya tisa mfululizo toka kuanzishwa kwake. Matembezi hayo yanayofanyika kila mwaka yatafanyika siku ya kumbukumbu ya kifo cha mwalimu Nyerere katika viwanja vya greens, Oystebay jijini Dar es salaam.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana jijini, Mwenyekiti wa kamati ya maadalizi ya Rotary Dar Marathon Bi. Catherinerose Barretto alisema “tunayo furaha kuzindua na kusaini mkataba wa kushirikiana na Benki M kama mdhamini mkuu katika matembezi ya mwaka huu.

  Kuna mambo mapya yameongezeka katika ushiriki wa matembezi mwaka huu, kwa mara ya kwanza tutakuwa na marathon iliyokamilika ya km 42.2, pia tutaongeza urefu wa mzunguko kwa waendesha baiskeli kutoka km 21.1 kufikia km 42.2. Matembezi ya km 9 mwaka huu yatarefushwa kufikia km 10, matembezi ya km 5 tu ndio yatabaki kama yalivyo.

  Mbio na matembezi ya rotary Dar Marathon pamoja na kuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii, pia yamekuwa yakiboreshwa kila mwaka na kuvutia washiriki wengi wakiwemo wa kimataifa.

  “kila mwaka tumekuwa tukiongeza vivutio katika matembezi haya. Mwaka huu tutakuwa na marathon nzima tofauti na miaka iliyopita ambapo ilikuwa ni nusu marathon”, aliendelea Barretto Mwaka huu, mbio na matembezi hayo yatalenga katika kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika hospitali ya CCBRT ambayo huhudumia wananchi wenye matatizo mbalimbali ya ulemavu ili kuwezesha hospitali hiyo kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi.

  Akiongelea mipango ya wanachama wa Rotary katika kuwezesha huduma bora za afya, mwenyekiti wa bodi ya Rotary Dar Marathon Bi. Sharmila Bhatt amesema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo wamekuwa wakichangisha fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya na hatimaye wamefanikiwa kupata mradi ambao una manufaa zaidi kwa jamii hivyo fedha hizo zote zitaelekezwa katika mradi huu. “Tunayo furaha kuwa sehemu ya mradi huu ulioanzishwa na CCBRT wenye lengo la kuongeza huduma zilizo bora kwa watu wenye ulemavu mbalilmbali.

  Akichangia juu ya ushiriki wa Benki M katika mbio na matembezi haya, mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alisema kuwa wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali maendeleo ya jamii, hivyo wamekuwa wakishirikiana na Rotary katika Rotary Dar marathon toka ilipoanzishwa mwaka 2009.

  Aliongeza kuwa “tunasisistiza kuwa ni sera yetu kushirikiana na taasisi mbalimbali zinazoheshimika katika kuleta mageuzi kwa wahitaji hapa nchini, tunaamini kabisa kuwa kwa pamoja tukishirikiana tutafanikisha ujenzi wa kituo hiki cha afya hapo CCBRT. Hii ina maana kubwa sana kwetu kuiona sekta ya afya katika jamii yetu inapewa kipaumbele, tunaamini kuwa kuweka nguvu zaidi katika sekta ya afya ni msaada wa moja kwa moja kwa jamiii ukuaji wa uchumi kwa ujumla”.

  Tangu mwaka 2009 ilipoanzishwa, Rotary Dar Marathon kushirikiana na Benki M imefanikisha miradi mbalimbali ikiwemo upandaji wa miti, utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka mashuleni pamoja na ujenzi wa wodi ya kansa ya watoto katika hospitali ya taifa ya muhimbili, wodi hii ni moja kati ya wodi bora kabisa za magonjwa ya kansa ya watoto hapa Afrika na pia mradi wa kujenga upya kituo cha kisasa cha kujifunzia katika maktaba ya chuo kikuu cha Dar es salaam.
  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Catherinerose Barretto (kulia) akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano Dar es Salaam jana, ambapo Bank M na Rotary Clubs zitakusanya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika hospitali ya CCBRT mwezi wa Octoba kupitia matembezi ya Rotary Dar Marathon. Kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank M, Jacqueline Woiso, mwenyekiti wa bodi ya Rotary Dar Marathon Sharmila Bhatt na rais wa Rotary club ya Dsm aliyemaliza muda wake Nirmal Sheth.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Bank M, Jacqueline Woiso (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Dar Marathon Shamila Bhatt wakibadilishana mkataba wa makubaliano baada ya kutia saini katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, huku wakishuhudiwa na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon, Catherinerose Barretto (kulia) , wengine ni marais wa klabu mbalimbali za Rotary.

  0 0

  Na Bashir Yakub.

  Mwanamke ameachwa na mume wake wa zamani. Lakini hajamuacha kisheria. Hakumpa talaka isipokuwa waliachana tu kila mtu akaendelea na maisha yake tena kwa muda sasa. Wewe umekutana na huyo mwanamke na umeanzisha naye mahusiano. Umeanza kuishi naye au umeamua kabisa kumuoa.

  Ulimuuliza kuhusu mahusiano yake ya zamani akakueleza bila kukuficha yaliyomsibu. Na wewe ukaona kwa kuwa tayari hayuko na huyo mume wake wa zamani kwa muda mrefu au muda kiasi basi haina shida. Kitu cha msingi kwako ulichozingatia ni kuwa hawa watu hawako wote tena kwa maana mahusiano yao waliyasitisha.

  Je sheria inasemaje kuhusu hali hii. Je kukaa na mwanamke wa namna hiyo kwa maana ya kuishi naye bila ndoa, au kuishi naye kwa ndoa au kuwa naye katika mahusiano bila kuishi naye kumezungumziwaje na sheria. Je uko salama. Je hakuna lolote linaweza kukutokea likakusababishia usumbufu, gharama, na kurehani mustakabali wa maisha yako. Je nini ufanye ikiwa umo katika hali kama hiyo.

  Haya na mengine yataelezwa hapa chini. Sura ya 29 ya sheria ya ndoa , iliyorekebishwa mwaka 2010 itatupatia majawabu ya maswali haya.

  1.NI WAKATI GANI NDOA HUHESABIKA IMEVUNJIKA.

  Ndoa ni zao la sheria na kufa kwake hufa kisheria. Ndoa haivunjiki isipokuwa taratibu za kisheria zimefuatwa. Ndoa inaweza kuvunjika kwa kifo cha mmoja wana ndoa, kwa kupotea kwa mda mrefu na kuihisiwa kufa kwa mmoja wa wanandoa( presumption of death), lakini pia ndoa hufa/huvunjika kwa talaka.

  Kama mojawapo ya hayo juu halijajitokeza ndoa hiyo bado inaishi. Kwahiyo mwanaume unatakiwa kujua kuwa mwanamke uliyemuoa au unayeishi nae bila ndoa au uliye naye tu katika mahusiano ya kawaida , ikiwa hapo awali alikuwa katika ndoa na mojawapo ya yaliyotajwa hapa juu hayajatokea basi mwanamke huyo ndoa yake bado inaendelea. Hapo badae itaelezwa hatari kubwa zinazokukabali .

  2. JE KUTENGANA NI TALAKA.

  Unaweza kudhani kuwa uko salama kwasababu una uhakika mwanamke uliyenaye ametengana na mme wake wa mwanzo na hivyo wewe uko salama. Kisheria kuna tofauti ya kutengana na kuachana/kutalikiana. Kutengana sio talaka. Talaka ni talaka mpaka itolewe kwa mujibu wa sheria. Pia kutelekeza sio kuachana/talaka. Watu wanaokuwa wametengana au wametelekezana bila talaka fahamu kuwa watu hao kisheria bado ni wanandoa.


  0 0

  Katika kuadhimisha maonesho hayo ya Nane Nane yanayofanyika viwanja vya Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma, banda la Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania- Tawa limekuwa kivutio kikubwa kwenye maonesho hayo ambayo yameanza rasmi tarehe 1/8/2017.

  Kivutio hicho kimetokana na kuleta wanyamapori mbalimbali wakiwepo Simba, Chui, Nyati, Chatu, Nyoka mbalimbali, Ndege mbali mbali, Fisi na Tausi. Kwa mara ya kwanza maonesho haya ya kuleta wanyamapori hai yalikuwa yanafanywa na Idara ya Wanyamapori. Safari hii TAWA wameamua kuongeza idadi ya wanyama ambayo haikuwapo hapo awali. Mfano Nyati na Mamba.

  Akizungumza katika maonesho hayo, Afisa habari na Mahusiano wa TAWA Bw. Twaha Twaibu aliwaeleza Wandishi wa Habari kuwa TAWA inashiriki kwa mara ya kwanza katika maonesho haya. Aliendelea kusema TAWA ni Mamlaka iliyoanzishwa kwa Amri ya Serikali na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Na.135 la tarehe 9 Mei, 2014. Uanzishwaji wa Mamlaka hii ni utekelezaji wa kifungu cha 8 cha Sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009. Mamlaka ya Wanyamapori imeanza kazi rasmi tarehe 1/Julai/2016. Makao Makuu yake kwa sasa yapo mjini Morogoro.
  Bw. Twaibu alielezea Wanahabari kwa kusema Mamlaka ilianzishwa na Serikali kama chombo cha utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa niaba ya Serikali chini ya uangalizi wa Serikali na kuwa na mfumo unaonesha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi. Kama ilivyo kwa Mamlaka Serikali nyingine nchini, lengo la kuanzishwa TAWA ni kutekeleza majukumu ya Idara ya Wanyamapori hasa ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini. Majukumu ya TAWA ni kusimamia shughuli za utawala, ulinzi, usimamizi wa raslimali ya Wanyamapori katika maeneo yote nje ya Hifadhi za Taifa na Hifadhi ya Ngorongoro.

  Wandishi wa Habari walitaka kupata kauli ya TAWA na Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme wa Stiglers Gorge uliyoko ndani ya Pori la Akiba Selous, kama TAWA na Wizara wanasemaje?


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la utawala la Polisi wilaya ya Longido, kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo na kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Longido Bw. Daniel Chongolo.

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo amewashukuru na kuwapongeza wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wamejitoa na kuhakikisha wanakamilisha jengo la utawala la Polisi wilaya ya Longido.

  Akizindua jengo hilo jana, alisema kwamba litawezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi kwa utulivu sambamba na kukabiliana vyema na masuala ya uhalifu katika wilaya hiyo, na kuongeza kuwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa anajisikia furaha na fahari kuona wadau wanashirikiana na kuagiza meneja wa Tanesco wilaya ahakikishe ameweka mita ya umeme ambapo gharama hizo aliahidi atazitoa yeye mwenyewe.

  “Lazima tuimarishe mipaka na Polisi wawe na vituo vya uhakika vya kufanyia kazi ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za uhalifu na Jeshi hilo litaendelea kutumia mbinu shirikishi”. Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

  Bw. Gambo aliwaasa baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji  pamoja na wananchi kutoficha wageni ambao wanaishi nchini bila kufuata sheria na kuongeza kuwa yeyote atakayegundulika anafanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

  “Kila kiongozi anapaswa kutambua watu wote wanaoishi katika eneo lake na kuhakikisha mgeni yoyote amefuata sheria na kama akigundua (Anaishi bila utaratibu) atoe taarifa kupitia kamati za ulinzi na usalama za kata ili hatua ziweze kuchukuliwa”. Alisisitiza Bw. Gambo.

  Akizungumza katika uzinduzi huo mwenyeji wa shughuli hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Omari Mkumbo mbali na kuwashukuru wadau hao, alisema kwamba tukio la uchangiaji na ukamilishaji wa jengo hilo limeonyesha kwamba wana Longido wana mshikamo wa hali juu.

  Kamanda Mkumbo alisema kwamba wananchi waendeleze mshikamo huo ili kuweza kuimarisha kituo kingine cha Polisi kilichopo tarafa ya Kamwanga na kutaja majengo mengine ambayo yanajengwa na kukaribia kukamilika kwa hamasa ya Mkuu wa mkoa kuwa ni kituo cha Polisi cha Kwa Morombo pamoja na kituo cha Polisi cha Utalii ambacho ujenzi wake unafadhiliwa na TATO (Tanzania Tourist Operators).

  “Kazi kubwa ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha uhalifu unakomeshwa na japokuwa takwimu za matukio ya uhalifu katika wilaya hiyo yapo chini lakini bado kuna tatizo la madawa ya kulevya aina ya Bhangi na Mirungi hivyo wananchi endeleeni kutoa ushirikiano kwa askari kwani madhara ya madawa hayo ni makubwa”. Alisema Kamanda Mkumbo.

  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Daniel Chongolo alisema ongezeko la ukamataji wa madawa ya kulevya umetokana na udhibiti mzuri na kuahidi kuimarisha zaidi usalama kwa kutumia Polisi na vyombo vingine vya usalama huku akitoa shukrani zake kwa Kamanda wa Polisi mkoa kwa kutoa gari ambalo litasaidia kuimarisha ulinzi katika tarafa ya Kamwanga.

  Awali akitoa taarifa ya uhalifu pamoja na mchakato wa ujenzi huo, Mkuu wa Polisi wilaya ya Longido Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joswam Israel Kaijanante alisema kwamba ujenzi huo umegharimu zaidi ya Milioni 80 ambazo zilichangwa na viongozi, askari pamoja na wananchi na kuongeza kwamba bado jengo hilo halina samani na “Kompyuta , Printer” pamoja na mfumo wa maji taka ambapo gharama zake ni Milioni 16.

  Mchakato wa ujenzi wa jengo hilo ambao una ofisi tatu ambazo ni za Mkuu wa Polisi wilaya, Mkuu wa Upelelezi wilaya na Mwendesha Mashtaka wa Polisi ulianza mwaka 2015 na kukamilika mwezi Julai mwaka huu uliwashirikisha kikamilifu jumla ya wadau wapatao 20 ambao pia walipewa vyeti vya shukrani.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakati akifungua jiwe la msingi lililowekwa katika ujenzi wa jengo la utawala la Polisi wilaya ya Longido.
  Jengo jipya la utawala Polisi wilaya ya Longido ambalo lilizinduliwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo jana katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).

  0 0

  Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI), Ismail Ngolinda, akitoa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mathew Mtigumwe (kushoto), alipotembelea banda hilo. Katikati ni Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, HusseinMansour.
  Watafiti wakijadiliana jambo kwenye maonesho hayo. Kutoka kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Filbert Nyinondi, Bestina Daniel, mdau wa kilimo, Flaviana, Dk. Emmarold Mneney, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro na Christina Kidulile.
  Taswira ya banda hilo katika maonyesho hayo.

older | 1 | .... | 1840 | 1841 | (Page 1842) | 1843 | 1844 | .... | 3353 | newer