Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

INTRODUCING Number 1 Official Video by Phillz ft Darassa


WAFANYAKAZI NMB WASHIRIKI MASHINDANO YA MOTHLY MUG, GOFU

$
0
0
Mchezaji wa timu ya gofu ya NMB, George Kivaria ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Huduma Mbadala za Kibenki wa NMB akishiriki mashindano ya gofu ya Mothly Mug yanayoandaliwa na Klabu ya Gofu ya Lugalo. Mchezaji wa timu ya gofu ya NMB, Gibson Mlaseko ambaye pia ni Meneja Mahusiano ya Wateja wa NMB akishiriki mashindano ya gofu ya Mothly Mug yanayoandaliwa na Klabu ya Gofu ya Lugalo. Mchezaji wa timu ya gofu ya NMB, Michael Misabo ambaye pia ni Meneja wa Huduma kwa Njia ya Mtandao akishiriki mashindano ya gofu ya Mothly Mug yanayoandaliwa na Klabu ya Gofu ya Lugalo. Wafanyakazi wa benki ya NMB Tanzania wameshiriki mashindao ya gofu ya kila mwezi yanayoandaliwa na Klabu ya Gofu ya Lugalo yanayofahamika kama Mothly Mug ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya gofu vya Lugalo. Mchezaji wa timu ya gofu ya NMB, Gibson Mlaseko ambaye pia ni Meneja Mahusiano ya Wateja wa NMB akishiriki mashindano ya gofu ya Mothly Mug yanayoandaliwa na Klabu ya Gofu ya Lugalo.

MAMA WA MINUSO YOTE WASHINGTON DMV 2017 SEPTEMBA 1 HAD SEPTEMBA 3

$
0
0

TWENZETU WASHINGTON D.C. 
DMV LABOR DAY WEEKEND
Inquiries:
 (301) 404-6901
(240) 423-3331
(240) 595-5100
1 (202) 957-2157
1 (202) 629-7841
(301) 404-0413
DMV KAMA ZAMANI

NEWS ALERT: JPM ATEUA MAKAMISHNA WAWILI JESHI LA ZIMAMOTO

"Exim kuimarisha ushirikiano na China kwa ajili ya wafanyabiashara wa Tanzania"

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Exim Dinesh Arora [kulia] akitia saini kwenye kitabu cha wageni akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Exim Tanzania Yogesh Manek walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini China. Pamoja nao ni Balozi anayewakilisha Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki.

Ujumbe wa kiwango cha juu kutoka EXIM Bank Tanzania wametembelea China wakijaribu kuunda ushirikiano na taasisi za kifedha muhimu za nchi hiyo kwa lengo la kuwezesha biashara kwa urahisi kati ya China na Afrika, haswa kwa biashara ndogo na kati (SME) zinazoendeshwa nchini Tanzania, Uganda, Djibouti na Comoros ambako benki ya Exim inafanya biashara.

Mikutano iliyofanyika nchini China ilifanikishwa na Balozi Mbelwa Kairuki ambaye anawakilisha Tanzania nchini humo kwa kuunganisha ujumbe huo na taasisi muhimu za kifedha za China. Ujumbe huo ulifanya mikutano yenye mafanikio makubwa na benki zinazoongoza za biashara na taasisi za fedha za maendeleo (DFIs).

Safari hii ilikuwa ni muhimu haswa ukizingatia uhusiano unaokua wa kiuchumi kati ya Afrika Mashariki hususani nchi za Tanzania, Uganda, Djibouti na China. Nchi hizi zimeshuhudia mwongezeko mkubwa wa uwekezaji na biashara katika miaka ya hivi karibuni kupitia makampuni makubwa ya kiserikali na binafsi ambayo yanafanya biashara katika nchi hizi.

Biashara za kati na ndogo (SMEs) zinatambulika kwa umuhimu wake katika kuchangia ukuaji na maendeleo ya uchumi katika nchi zinazoendelea. Huko China biashara hizi zinachangia hadi asilimia 60 ya mapato ya taifa. Katika Afrika mchango unakuwa mdogo kwa sababu mbali mbali zikiwemo ukosefu wa vifaa, teknolojia na uwekezaji wa kutosha. Ugumu wa kupata fedha au mtaji unaendelea kuwa changamoto kubwa katika ukuaji wa biashara hizi ambapo inasababisha biashara hizi kufa au kupungua.

Afrika kwa ujumla na zaidi hasa Tanzania, ina fursa kubwa katika maeneo kama ngozi, nguo, usindikaji, kilimo na viwanda. Fursa ni kubwa na juhudi za pamoja zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali na sekta binafsi.Safari kama hii iliyofanyika hivi karibuni ni hatua nzuri katika kufanikisha juhudi hizi.

Mazungumzo yaliyofanyika yalihusisha kuwepo kwa ushirkiano kati ya benk ya Exim na taasisi za kifedha za China katika kuendeleza sekta ya biashara za kati na ndogo nchini Tanzania. Ilidhihirika kuwa benki ya Exim ikiwa kama moja ya benki zinazoongoza nchini Tanzania katika sekta binafsi inaweza kuwa kichocheo na mstari wa mbele katikakufakikisha mipango hii

Mwakilishi wa benki ya Exim wa dawati la China Katusime Nzarombi amesema, “Tulipokelewa vizuri sana na wenyeji wetu kutoka benki za China na uhusiano ulioanzishwa utaendelea kuboresha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili. Tutaendelea kufanyia kazi ushirikiano huu na kuhakikisha kuna faida za uhakika katika sekta ya SME nchini Tanzania.”

Benki ya Exim Tanzania ni moja kati ya benki za biashara zinazoongoza ikiwa na matawi katika nchi nne Afrika. Benki hii inaendelea kuwa mstari wa mbele katika utoaji suluhisho kwenye huduma za kibenki kwa watu binafsi, biashara ndogo na makampuni makubwa. Benki ya Exim ina msingi wa mali wenye thamani ya shilingi za Kitanzania trilioni 1.8 na ina matawi 45 na wafanyakazi 942 katika nchi hizo nne.

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI CHUNYA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Dennis Dillip ambaye ni Mjiolojia kuhusu mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni ya Sunshine Mining Limited uliopo Chunya wakati alipoutembelea Agosti 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakipata Maelezo kutoka kwa Afisa Madini wa Mkoa wa Mbeya Mhandisi Said Mkwawa kuhusu taarifa za Kampuni ya Sunshine Gold Mininga Limited wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni hiyo wilayani Chunya Agosti 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia wimbo maalum unaozungumzia utendaji wa serikali ya Awamu ya Tano ulioimbwa na Kwaya maarufu ya Kiwete katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Sabsaba mjini Chunya Julai 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba mjiini Chunya Agosti 1, 2017. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mkuki kutoka kwa Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaso ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chifu wa makabila ya Wakimbu na Wasafa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Chunya Agosti 1, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya SUNSHINE GROUP, Betty Mkwasa wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa Sunshine Mining Limited uliopo Chunya Agosti 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

NGURUWE RUKSA KIBAHA BAADA YA KUPIGA MARUFUKU.

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani ,imesitisha zuio la kuingiza na kufanya biashara ya nguruwe na mazao yake ,:"ambapo juni mwaka huu ilipiga marufuku biashara hiyo ili kuepuka  na ugonjwa wa homa ya nguruwe(AFRICAN SWINE FEVER) .

Halmashauri hiyo ilichukua hatua hiyo kutokana na idara ya mifugo na uvuvi kubaini kuingia kwa ugonjwa huo katika baadhi ya maeneo .

Akizungumzia suala hilo ofisini kwake mjini humo,ofisa habari wa halmashauri ya mji wa Kibaha,Innocent Byarugaba,alisema  idara hiyo imefanya uchunguzi na kujiridhisha kuwa hakuna tena viashiria hivyo na kuamua kusitisha zuio hilo.

Aidha alieleza jumla ya nguruwe 71 wenye thamani ya sh.mil.4.970 walikufa kutokana na ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Kwa mujibu wa Byarugaba ,uwepo wa kuzuia na kusitisha kipindi hicho kulisaidia kupunguza na hatimae kudhibiti ongezeko na kuenea kwa ugonjwa huo .

"Halmashauri hii kuanzia sasa inapenda kuutarifu umma kuendelea na shughuli zake kama kawaida na kwamba zuio limeondolewa rasmi "alisema Byarugaba.
Alieleza sababu iliyosababisha kupigwa marufuku kuingia mnyama huyo na kuathiri hasa wauza kitimoto kwamba ni ugonjwa wa homa ya nguruwe kuingia kwenye kata mbili za Picha ya Ndege na Viziwaziwa eneo la Mikongeni. 

Nae Afisa mifugo na uvivu wa halmashauri ya mji wa Kibaha, Charles Marwa ,alisema hatua za awali zilizochukuliwa ikiwemo kuzuia nguruwe kuingia na kutoka katika maeneo yaliyokuwa na viasharia.
"Sampuli mbalimbali za nguruwe waliokufa zilichukuliwa na kupelekwa maabara kuu ya mifugo Temeke Jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi na kubaini uwepo wa ugonjwa huo ,” alisema Marwa.

Marwa alibainisha ,ugonjwa wa African Swine Fever,ambao  unadaiwa kuingia  kwa nguruwe hauwezi kuambukiza binadamu ila madhara yake makubwa ni kuteketeza nguruwe wengi asilimia 100,kwa muda mfupi na kusababisha hasara kwa mfugaji.

Alitaja dalili za ugonjwa huo ni kuvuja na kusambaa kwa damu kwenye viungo vya mwili , homa kali, kupumua kwa shida na, kutapika.
Vifo ndani ya siku mbili hadi 10 na muonekano wa damu kuvilia kwenye viungo mbalimbali vya ndani vya nguruwe baada ya kumpasua.

Ugonjwa huo hushambulia nguruwe na hauna tiba kwa wanyama wanaoupata na husababisha vifo vingi unapotokea hasa kwa wanyama wakubwa.

DAWASCO YASHAURIWA KUTOA HUDUMA KWA UWAZI

$
0
0
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.  PICHA NA KAJUNASON/MMG.

Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema ameapa kuwashughulikia watumishi wachache chini ya wizara yake ambao bado wanaendekeza maisha ya ujanja ujanja kazini.

Profesa Kitila ameitoa kauli hiyo leo Jumanne wakati akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) kwenye ofisi za makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. Amesema ingawa Dawasco imefanikiwa kuboresha huduma zake, lakini wapo watumishi wa chache ambao bado wanafanya kazi kwa ubabaishaji.

Amesisitiza kuwa zama za ujanjaujanja zimekwisha na wale wachache wanaoshiriki mbinu za kulihujumu shirika hilo hawatavumiliwa na watendaji wa shirika hilo kutoa taarifa kwa watakaobainika. Wakati huo mhuo, Profesa Mkumbo amewashukuru watendaji na watumishi wa Dawasco akibainisha kuwa siku hizi simu za malalamiko anazopigiwa na wateja kuhusu huduma za maji zinazotolewa na Shirika hilo zimepungua sana.

Amesema hali hiyo inatokana na Dawasco kuboresha huduma zake. Amesema hivi sasa anatumiwa ujumbe mfupi wa kupongezwa kuhusu huduma za zinatolewa na Dawasco na kulitaka shirika hilo kuendelea kuchapa kazi ya kutoa ya kuwahudumia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

“Hongereni kwa huduma nzuri mnazitoa kwa wakazi wa mikoa hii. Nyie ndiyo taswira ya Serikali katika utoaji wa huduma za maji. Bila nyie Ukatibu wa Mkuu hauna maana kwa mkoa wa Dar es Salaam hata waziri na wizara kwa ujumla,” amesema Profesa Mkumbo. Profesa Mkumbo amesema wizara yake haina mipaka katika utendaji kazi na kwamba ipo wazi kuwasiliana mtendaji yeyote atakayetaka huduma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco).


Waziri Mhagama akutana na Balozi wa Vietnam nchini

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Kazi, Vijana Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (Mb) akisisitiza jambo pamoja na Balozi wa Vietnam Bw. Nguyen Kim Doanh ofisini kwake, Jijini Dar es Salaam Agosti 2,2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Balozi wa Vietnam Bw. Nguyen Kim Doanh kuhusu ushirikiano baina ya nchi ya Vietnam na Tanzania ofisini kwake, Jijini Dar es Salaam Agosti 2, 2017. Kulia ni Msaidizi wa Balozi Bw. Ton Ho Tri Dzung.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Vietnam Bw. Nguyen Kim Doanh baada ya mazungumzo yao, ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Agosti 2, 2017.

VETA NA AIRTEL YATHIBITISHA KUHUDUMIA WANAOTAKA KUJIFUNZA UFUNDI WALIKO

$
0
0
Afisa Matukio wa Airtel Tanzania akikabidhi simu maalum zitakazotumika kuendesha mradi wa VSOMO kwa Msajili Mkuu Veta Kipawa(Registry), Bw, Harold Mganga, (kushoto), akishuhudiwa na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi. (Project and Short Course Coordinator)Veta Kipawa Gosbert Kakiziba (katikati) simu hizo zimetolewa kwa kwaajili ya mradi wa VSOMO. VSOMO ni applikesheni maalum inayotoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya mtandao inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.
Afisa Matukio wa Airtel Dangio Kaniki (kulia) akimuonyesha applikesheni ya VSOMO Mkuu wa Usajili Veta Kipawa (Registry) Bw, Harold Mganga (katikati) pamoja na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi. (Project and Short Course Coordinator) Veta Kipaw bw, Gosbert Kakiziba (kulia). hafla fupi ya makabidhiano ya simu hizo yaliyofanyika Veta Kipawa. Aplikesheni ya VSOMO inatoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya mtandao inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.

Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania (VETA) kwa kupitia mfumo wa mafunzo kwa mtandao wa VSOMO unaodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imebainisha kuwa iko tayari kuhudumia vikundi au jamii ya wanaotaka kujifunza ufundi stadi kwa kupeleka timu yao ya mafunzo kwa vitendo popote ili kuhakikisha dhana ya uchumi wa viwanda inakamilika kwa kuwa na mafundi wazuri waliohitimu ufundi katika chuo maalumu nchini.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo cha veta kipawa ambae pia ni msimamizi wa mradi wa mafunzo kwa njia ya simu unaodhaminiwa a Airtel kwa lengo la kutoa FURSA kwa vijana wegi mjini kupata ujuzi na kujiajiri Mhandisi Lucius Luteganya.

VETA tuko tayari kuwafuata wanafunzi wetu endapo watajiandikisha na kuhamasihana kwa kikundi  kusoma kwa njia ya mtandao wa VSOMO , ikiwa watakuwa vijana kuanzia 15-20 na wakipenda kupata mafunzo waliko basi sisi tutawafuata waliko ili kuhakikisha wanahudumiwa na mobile trainers wetu”.

“sasa hivi kupitia mtandao wa Vsomo tunakozi 12, wanafunzi wanaweza wakajisomea wawapo popote mara baada ya kupakua App yetu ya VSOMO na kulipia kozi anayotaka” alisisitiza Luteganya.

Eng Luteganja alitaja kozi hizo kuwa ni “Tunampango waongeza kozi zingine  15 hivi karibuni lakini kwa sasa zilizopo tayari kwenye mtandao ni Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani , Umeme wa magari, Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu za mkononi, Ufundi Alluminium,  Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma Ufundi wa kuchomea vyuma.

Tangu VETA na Airtel walipozindua  mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao waVSOMO mwezi wa Juni 2016 Mfumo huu wa VSOMO sasani umepata umaarufu mkubwa kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application ya VSOMO, 8000 wamejiandikisha na kati yao 50 wameshasoma kozi mbalimbali  na kupata vyeti vyao vya ufundi stadi kutoka  VETA.

kujiandikisha katika mojawapo ya kozi 12 zinazopatikana katika application ya VSOMO mwanafunzi atalipia kwa simu yake gharama ndogo ya shilingi 120,000 tu kupitia huduma ya Airtel Money kwa kupiga *150*60#. na kufanya malipo ambazo gharama hizi zitamuwezesha kuja kupata mafunzo kwa vitendo bila malipo ya ziada.

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA POLISI KWA KOSA LA KUMILIKI NOTI BANDIA ILEMELA.

$
0
0


MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA TAREHE 01.08.2017 MAJIRA YA SAA 23:00HRS KATIKA BAR IITWAYO THE DREAMS ILIYOPO MTAA WA KONA YA BWIRU KATA YA KITANGIRI WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUMKAMATA RYOBA MANGULE, MIAKA 27, MKAZI WA IBUNGILO, AKIWA NA NOTI BANDIA SITA (6) ZA SHILINGI ELFU KUMI ZENYE THAMANI YA TSHS 60,000/=, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.

AWALI ASKARI WALIPATA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MAENEO TAJWA HAPO JUU YUPO MTU MWENYE NOTI BANDIA. AIDHA BAADA YA KUPOKEA TAARIFA HIYO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI HADI ENEO HILO NA KUFANYA MSAKO MAENEO HAYO KISHA BAADAE WALIFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA AKIWA NA KIASI HICHO CHA NOTI BANDIA.

POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, AIDHA MSAKO WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA BADO UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWAOMBA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA. PIA ANAWATAKA VIJANA KUACHA TABIA YA UTENGENEZAJI NA USAMBAZAJI WA NOTI BANDIA KWANI NI KOSA LA JINAI NA ENDAPO MTU ATAKAMATWA AKIWA ANAJIHUSISHA NA UHALIFU WA AINA HIYO HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

Bunge la Tanzania kuanzisha Urafiki wa Kibunge na Bunge la UAE

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo ametembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu na kufanya mazungumzo na Spika mwenzake, Dr Amal Al Qubaisi ambapo amewasilisha mapendekezo rasmi ya kuanzisha Umoja na Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mhe Spika Al Qubaisi ambae ni Spika wa kwanza mwanamke katika nchi zote za Mashariki ya Kati kwa niaba ya Bunge la nchi hiyo amekubali mapendekezo hayo na kutoa mwaliko Kwa Wabunge wa Tanzania kutembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu kwa nia ya kuona namna  UAE ilivyopiga hatua.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Abu Dhabi. kulia kwake ni Spika wa Bunge hilo, Dr Amal Al Qubaisi. 
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akiwa na mwenyeji wake, Dr Amal Al Qubaisi baada kuzungumza nae.
Spika Job Ndugai akipewa ziara ya Bunge la nchi hiyo na Spika Al Qubaisi

EU injects TZS. 1.4 billion to counter child marriage and FGM

$
0
0
The European Union Delegation in Tanzania has funded and launched today a TZS. 1,400,000,000, equivalent to EUR 600,000, three- year project (2017 – 2020) to counter child marriage and female genital mutilation (FGM) that will be implemented by Plan International Tanzania in partnership with Children’s Dignity Forum (CDF) and New Light For Children Organisation (NELICO), Tackle Africa and Tanzania Football Federation (TFF) in Geita and Tarime Districts.

The Head of Delegation of the European Union to Tanzania Ambassador Roeland van de Geer underlined the EU's commitment to acting in genuine partnership with Tanzania, international and regional organizations, and civil society to combat violence and harmful practices against women and girls. "Child marriage and FGM are a violation of girls’ human rights. 

These harmful practices have a devastating impact on a girl's health, her well-being and personal development but they also have a detrimental ripple effect on the society as a whole. Ending child marriage means a positive effect on the health and education of girls and their children, it contributes to a lower fertility rate and increases women’s expected earnings and household welfare."

Plan International Tanzania Deputy Country Director, Ms. Gwynneth Wong, said that Child Marriage in Tanzania prevails at the rate of 37%, where three out of ten girls enter into marriage before the age of 18 with Mara having the highest rate of 55% and Geita 37%. The Deputy Country Director also revealed that while the national prevalence rate of Female Genital Mutilation is at 10%, Mara is at the rate of 32%, three times the national rate. All these practices deprive the girl child of their potential to contribute to both national and personal developments.

“The girls are deprived of their right to enjoy their childhood and reaching their goals. Subjecting them to early marriages and mutilating their genitals puts them at risk of maternal health complications and even deaths. This fuels the poverty cycle and is against the UN Sustainable Development Goals”, said Gwynneth Wong.

The project targets over 1,500 in-school and out-of-school girls aged between the age of 10 – 24, and aims to prevent the incidences of harmful traditional practices of Child Marriage and FGM through empowering girls and strengthening of community, civil society and government support systems to respond to girls’ rights violation and challenges.

TIMU YA 'TMT' IMEFANIKIWA KUIFUATA MCHENGA KATIKA FAINALI YA MPIRA WA KIKAPU.

$
0
0
 Nahodha wa timu ya Kurasini Heat Rajab Hamis ( jezi nyeupe) akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya TMT katika mchezo wa tatu wa hatua ya nusu fainali ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa alama 99 kwa 71.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
TIMU ya TMT imefanikiwa kuifuata Mchenga katika hatua ya fainali ya mpira wa kikapu ya Michuano ya Sprite Bball Kings baada ya kuiondoa Kurasini Heat kwa alama 99 dhid ya 71.

Mchezo huo uliochezwa jana katika Viwanja vya Don Bosco Oysterbay ulikuwa na ushindani mkubwa sana kwa kila timu ambapo katika nusu fainali ya kwanza na ya pili zilimalizika kwa kila upande kupata ushindi.

Mkurugenzi wa Ufundi na mashindano TBF Manase Zablon amezipongeza timu za Mchenga Bball Stars na TMT kwa kuingia katika hatua ya fainali ya michuano ya Sprite Bball Kings 2017.

Manase amesema kuwa kwa sasa hatua ya fainali inatarajiwa kuwa wiki ijayo na zitachezwa katika hatua ya michezo mitano na watawatangazia ni katika uwanja gani zitachezwa.

Kwa upande wa Nahodha wa timu ya TMT, Isihaka Masoud amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Kurasini Heat ulikuwa ni mgumu sana kwani walivyopoteza mchezo wa kwanza waliangalia wapi walipokosea na katika mchezo wa nusu fainali ya pili na ya tatu wamehakikisha wanatoka na ushindi na hilo wamefanikiwa na kuingia fainali.

Isihaka amesema kuwa, haiofii timu ya Mchenga kwani maandalizi mazuri ndiyo yatakayoonekana ndani ya Uwanja ingawa wanafahamu ni timu nzuri yenye wachezaji wazoefu na wazuri.
Piga nikupige langoni mwa timu ya Kurasini Heat Katika mchezo wa tatu wa hatua ya nusu fainali ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa alama 99 kwa 71.
Nahodha wa timu ya TMT Isihaka Masoud (jezi ya Bluu) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Kurasini Heat Katika mchezo wa tatu wa hatua ya nusu fainali ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa TMT kutoka na ushindi wa alama 99 kwa 71.

MTANDAO WA ELIMU TANZANIA, (TenMet), WAKUTANA NA BLOGGERS JIJINI DARES SALAAM

$
0
0


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.
BINADAMU ili aweze kuyakabili mazingira yake, moja ya nyenzo muhimu ni elimu, na kwa kutambua umuhimu wa elimu, wadau mbalimbali wamekuwa wakifanya juhudi kubwa katika kusaidiana na serikali ili kufikia lengo la kuwapatia elimu Wananchi wa Tanzania.
Mtandao wa Elimu Tanzania, kwa kifupi TenMet, ni moja ya taasisi zinazifanywa juhudi kub wa katika kuhakikisha malengo yaliyotajwa hapo juu yanafikiwa.
TenMet ambayo iliasisiwa miaka 18 iliyopita ikiunganisha taasisi nyingine 39 wakati huo, kwa sasa mtandao huo umepanuka na kufikia jumla ya taasisi 181 zilizojikita katika swala la kuhakikisha watanzania wanapatiwa haki yao ya elimu, lakini sio tu kupatiwa elimu bali pia elimu iliyo bora.
Ili kufikisha ujumbe kwa wahusika (jamii) TenMet hufikisha ujumbe kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na makongamano, semina na vyombo vya habari vikiwemo vile vya kisasa (social media kama vile Blogs).
Agosti 2, 2017, Maafisa wa TenMet waliwaalika bloggers ili kuangalia namna gani wanavyoweza kushirikiana katika kutekeleza malengo yaliyoanishwa hapo juu ya kusambaza taarifa mbalimbali zinazohusu masuala ya elimu.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, alisema, lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa kikazi baina ya taasisi yake na vyombo vya habari vya kimtandao kwani anaamini taarifa zitawafikia wadau wengi zaidi.

“Lakini pia tunaamini ushirikiano huu utatusaidia katika kuibua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini, kwa kuhabarisha umma, hivyo tunayo furaha kubwa kukutana nanyi leo hii.”Alifafanua.
Kwa upande wake, Afisa Programu wa TenMet, Bi. Alistidia Kamugisha, amefafanua kuwa, TenMet kama ambavyo malengo yake yalivyoainishwa, imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali kuhusu elimu hapa nchini, lakini pia kwa kushirikiana na taassi nyingine za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuratibu mikutano, maonesho na semina kuhusu masuala ya elimu.
Afisa Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bi. Alistidia Kamugisha, akizungumza wakati wa kikao cha kujenga ushirikiano baina ya taasisi hiyo na Bloggers kilichofanyika makao makuu ya TenMet, Sinza jijini Dar es Salaam, leo Agosti 2, 2017.
Meneja Programu wa TenMet, Bw.Nicodemus Shauri Eatlawe, (katikati), akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kulia ni Bi. Alistidia Kamugisha, na Afisa Programu wa taasisi hiyo, Bw. David Sizya.
 Afisa wa TenMet, Bw. Dominic Dogani, akitoa ufafanuaiz wa masuala mbalimbali yatakayojadiliwa kwenye kikao hicho.
 Majadiliano yakiendelea..
 Bw. Sizya, (kulia), akimpatia nakala ya vitabu vya TenMet mwandishi wa Mo Blog, Bw. Rabif Humwe.

ATOGS yakaribisha ushiriki kwenye mradi bomba la mafuta

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma Katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Abdulsamad Abdulrahim (katikati) akielezea mikakati ya jumuiya hiyo ya kuwezesha wadau mbalimbali wataoshiriki katika utoaji wa huduma kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 02 Agosti, 2017. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye.

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma Katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Abdulsamad Abdulrahim, amesema kuwa jumuiya inakaribisha makampuni mbalimbali nchini kujiunga na jumuiya hiyo na kuwezeshwa kwenye ushiriki katika mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Abdulrahim aliyasema hayo leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam na kushirikisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, na watendaji kutoka Jumuiya ya Watoa Huduma Katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na  Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF).

Alisema kuwa tayari baadhi ya makampuni yameshaanza kujiunga na jumuiya hiyo na kutaka watu binafsi wenye nia ya kushiriki katika utoaji huduma kwenye mradi wa bomba la mafuta kujiunga na jumuiya hiyo ili kuwezeshwa. Alisema kuwa kazi kubwa itakayofanywa na ATOGS ni pamoja na kuwawezesha washiriki kupata utaalam wa utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na namna ya kupata mikopo kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za kifedha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye (katikati) akifafanua jambo katika mkutano huo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma Katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Abdulsamad Abdulrahim.

Aidha, alipongeza jitihada za serikali katika kuwezesha uchumi wa viwanda kupitia mradi wa bomba la mafuta hali inayoleta matumaini ya kuwa nchi kutoka kwenye orodha ya nchi masikini duniani na kuingia katika orodha ya nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa, inavyofafanua.

 Alisisitiza kuwa lengo la jumuiya ni kuwaunganisha watoa huduma wote na kuwapa elimu ya namna bora ya utoaji wa huduma ili kuweza kushiriki kikamilifu katika mradi wa bomba la mafuta. Aliongeza kuwa mradi wa bomba la mafuta utaleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kuanzia kwa mwananchi mmoja mmoja hadi kwa taifa kwa ujumla na kuwataka wananchi hasa waishio katika mikoa itakayopitiwa na miundombinu ya bomba la mafuta kuchangamkia fursa na kuondokana na umasikini.

Aliendelea kutaja mikoa itakayopitiwa na miundombinu ya bomba la mafuta kuwa ni pamoja na Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Manyara na Tanga. Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo alipongeza uanzishwaji wa ATOGS na kusema kuwa jumuiya hiyo imekuja wakati mwafaka wa mradi wa bomba la mafuta na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kupitia jumuiya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa pili kushoto) akifafanua jambo katika mkutano huo. 

Dkt. Pallangyo alitumia fursa hiyo kuwakaribusha watanzania kujitokeza katika uzinduzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kufanywa na Marais Yoweri Museven wa Uganda na Dkt. John Magufuli siku ya Jumamosi wiki hii. Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF).

Godfrey Simbeye aliyataka makampuni yatakayopata tenda ya kutoa huduma kwenye mradi wa bomba la mafuta kufanya kazi kwa umahiri na uadilifu mkubwa kwa manufaa ya nchi.

“ Kutakuwepo na kazi nyingi sana zitakazotolewa kwa watanzania hususan huduma kwa wakandarasi watakaojenga bomba, umakini na uadilifu wa hali ya juu unahitajika ili kuleta sifa njema kwa nchi,” alisema Simbeye Aliishauri serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuweka mpango maaalum wa kutoa mafunzo wa namna ya kujenga mabomba ili baadaye wataalam wa ndani ya nchi wafanye kazi ya kujenga mabomba na kupunguza gharama.

Aliendelea kusema kuwa wakati serikali ikiimarisha mazingira mazuri ya uwekezaji nchini, mabenki yajiandae kutoa mikopo mara moja kwa makampuni yatakayopata tenda kwenye mradi wa bomba la mafuta.

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA NANENNE MKOANI MOROGORO

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linashiriki maonyesho ya Kilimo yanayoendelea mkoani Morogoro, Katika maonyesho hayo wakazi wote wa Morogoro Hususan Wakulima wanakaribishwa kupata elimu kuhusu namna ya kushiriki kilimo cha miwa (Outgrowers Scheme) Mpango huu umeanziishwa mahususi ili kuwasaidia watanzania kupata kipato kwa kulima miwa na Miwa hiyo itanunuliwa moja kwa moja na Kampuni Hodhi ya Mkulazi ambayo ni ubia kati ya NSSF na PPF. 

Vile vile wananchi wote wanakaribishwa kujiandikisha na NSSF ili kupata Matibabu bure kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na Mafao mengine yatolewayo na NSSF kama vile Mafao ya uzazi, kuumia kazini, Mafao ya urithi, Pensheni ya uzeeni na mengineyo
Afisa wa NSSF Mr Shaban Salehe akimwandikisha mwanachama mpya katika banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.
Afisa wa NSSF, Mwanawetu Njozi (kulia) akiongea na mgeni alietembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.
Afisa wa NSSF, Jonathan Mkahala akimwandikisha mwanachama mpya katika banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro, Pembeni kushoto ni Afisa mwandamizi wa Matekelezo wa Shirika hilo, Bw. Salawa.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano, Amina Mbaga akizungumza na wageni walietembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.

IGP SIRRO AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KITUO CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI NA NCHI JIRANI CHA UBUNGO

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro (katika) alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo na kituo cha daladala cha Mbezi Luisi, (kushoto) ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP) Murilo Jumanne Murilo.

Na Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka madereva na wamiliki wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na wamiliki na madereva wa mabasi madogo ya abiria maarufu kama daladala kuhakikisha wanayafanyia ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara magari yao ili kupunguza ajali zinazosababishwa na ubovu na uchakavu wa magari.

IGP Sirro aliyasema hayo jana wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani pamoja na kituo cha daladala cha Mbezi Luisi kwa lengo la kuangalia hali ya usalama wa kituo hicho, kuona namna ukaguzi wa mabasi ya abiria unavyofanyika kabla hayajaanza pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za abiria.

“Nimefarijika kuona watendaji wa kituo hiki pamoja na askari wangu wakifanya kazi vizuri kwa ushirikiano mkubwa hali inayosaidia kupunguza kero mbalimbali kwa watumiaji wa kituo hiki” alisema IGP Sirro.

Aliongeza kuwa Ubungo ni salama na itaendelea kuwa salama kwa sababu vibaka wamepungua na wale wanaofanya utapeli katika kituo hicho waache mara moja na kutafuta kazi nyingine kwa kuwa mwisho wa siku wataacha familia zao baada ya kukumbana na mkono wa sheria.

Pia ameelekeza magari yote ya abiria yabandikwe namba simu zote za makamanda wa mikoa wa Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Wakuu wa Polisi wa wilaya zote sehemu ambazo itakuwa ni rahisi kuonekana na abiria ili iwe rahisi kwao kutoa taarifa pindi wanapoona dereva anaendesha gari kwa kukiuka sheria na kanuni za usalama barabarani.

Aliwataka wananchi kuendelae kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ikiwa ni pamoja kutii sheria bila shuruti na kutoa wito kwa wamiliki wa magari, madereva pamoja na abiria kuwa wastaabu na kuhakikisha wanaheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani kwa kuwa kila mmoja anafahamu madhara ya ajali.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizungumza na madereva wa mabasi ya abiria pamoja na abiria wanaosubiri usafiri wa kwenda mikoa mbalimbali na nchi jirani baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, pamoja na kituo cha daladala cha Mbezi Luis.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akimuelekeza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Muslim kuhakikisha kuwa magari na mabasi yote ya abiria yanakaguliwa mara kwa mara. IGP Sirro alifanya ukaguzi wa kushtukiza jana katika Kituo Kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo na Kituo cha Daladala cha Mbezi Luis.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro ( katika) akiwa katika ukaguzi wa kushtukiza kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, (wa kwanza kushoto) ni Kaimu Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es salaam, Naibu Kamishna wa Polisi ( DCP) Lucas Mkondya akifuatiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Awadhi Haji.

Ufunguzi Banda la Nafasi Art Space Chini ya Udhamini wa NMB

$
0
0
BENKI ya NMB Tanzania imedhamini ujenzi wa duka la Nafasi Art litakalotumiwa na watoto kujifunza mambo mbalimbali ambayo yanahusu sanaa ili kukuza vipaji walivyonavyo vya sanaa ili watakapokua waweze kuvitumia kutengeneza kipato. 
Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa duka hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke alisema udhamini huo ni sehemu ya malengo ya benki kuhakikisha inatenga pesa ambazo zitatumika kusaidia jamii.

 "Benki yetu imekuwa ikitumia kitengo cha CSR kusaidia jamii kwa kutenga pesa kila mwaka ambazo zinatumika kusaidia jamii, tunaamini kuwa ujenzi huu utasaidia kuinua vipaji vya watoto ambao wanapenda sanaa ili wainue vipaji vyao," alisema Ineke. 
Naye Mkurugenzi wa Nafasi Art Space, Rebecca Correy aliishukuru NMB kwa uufadhili ambao wamewapa na kuwa banda hilo litawasaidia watoto wanaopenda sanaa kuonyesha vipaji vyao kwani kwa kipindi kirefu watoto wamekuwa wakikosa nafasi ya kushiriki kufanya kazi mbalimbali za sanaa lakini kwa sasa wataweza kuonyesha vipaji vyao. 

Kwa upande wa mgeni rasmi kwenye halfa hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu aliipongeza NAFASI Art Space kwa jitihada ambazo inazifanya za kukuza sanaa nchini na kuwa Serikali ya awamu ya tano itandelea kushirikiana nao.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu, Mwenyekiti wa Bodi ya Nafasi Art Space, Davie Kitururu, Mkurugenzi wa Nafasi Art Space, Rebecca Correy na Balozi wa Denmark nchini, Einar Jensen wakifungua banda la NAFASI ya Watoto.
Mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa banda la NAFASI ya watoto, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Joyce Hagu akikata utepe kufungua duka la kuhifadhia kumbukumbu la NAFASI Art Space. Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker akizungumza kuhusu udhamini wa NMB na jinsi ambavyo wamejipanga kutoa misaada kwa jamii zenye uhitaji.

TUSIRUHUSU WAGENI KUINGIA HOVYO NCHINI - WAZIRI MKUU

Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images