Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 182 | 183 | (Page 184) | 185 | 186 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Wasanii Raymond Kigosi na Steven nyerere wakiwafurahisha washabiki wao kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza
   Wasanii wakibadilishana mawazo na baadhi ya wasanii chipukizi wa jiji la Mwanza kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza.
   
   Wananchi mbalimbali wa jiji la Mwanza wakishangilia kwa nguvu kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza
   Wasanii wakiwa katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillm Festival jijini Mwanza, ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza.

  0 0

  Meneja wa Mradi wa kuwawezesha wananawake wa “MWEI” Grace Lyon akiwaelimisha baadhi ya wateja waliotembelea banda la Vodacom katika maonesho ya 37 ya sabasaba ,namna ya mradi huo unavyofanya kazi kwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo wanawake kupata mikopo isiyokuwa na riba mradi huo hadi sasa umewawezesha wanawake zaidi ya 7,000.
  Afisa wa Vodacom akimueleimisha moja ya wateja waliojitokeza kupata huduma katika banda la Vodacom lililopo katika maonesho ya 37 ya sabasaba jijini Dar es Salaam, Kampuni hiyo sasa imewawezesha wateja wake kulipia bidhaa kupitia huduma ya M pesa katika maonyesho hayo.
  Hili ndilo Banda la Vodacom linavyo onekana kwa nje katika viwanja vya Sabasaba.
  Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walioko katika maonesho ya 37 ya sabasaba jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja tayari kabisa kwa kutoa huduma kibandani hapo.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura na Mama Salma Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  Wageni wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU 

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama wakipokea saluti wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa Marekani leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Nyuma yao ni Mama Salma Kikwete na Mama Michelle Obama pamoja na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na IGP Saidi Mwema . Kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage na Mkuu wa Itifaki wa Ikulu ya Marekani (White House) Balozi Capricia Marshall. Ziara ya Rais Obama nchini imetajwa kuwa moja ya ziara za viongozi wa nje zilizofanikiwa sana, ambapo maelfu ya Watanzania walijitokeza kumlaki na kumuaga.
   Rais Barack Obama akiagana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam huku Mstahiki Meya wa Ilala pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakisubiri zamu zao
   Rais Obama na mkewe wakikwea pipa lao la Air Force One
   Rais Obama na mkewe wakipunga mikono kuaga Watanzania
   Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiaga wageni wao
  Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Adam Malima (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe  Alfonso Lenhardt wakipungia kuaga wageni wao. 

  0 0


  0 0

   Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume, akitoa ufafanuzi wa huduma za NSSF wakati wa Maonesha ya Sabasaba. 
   Issac Peter, akitoa maelezo ya huduma za bima katika banda la NSSF. 
   Mshiriki wa Maonesha ya 37 ya Biashara ya Kimataifa akipata maelezo kutoka kwa Mhasibu Mwandamizi wa NSSF, Madhehebi Tuli (kulia). 
  Ofisa Uhusiano Mwandamizi NSSF, Theopista Muheta akiwapa madaftari baada ya kujibu maswali kwa ufasaha yanayohusiana na huduma za NSSF.
  Mmoja wa wanachama wa Saccos zilizopata mkopo kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Shapilly Abdallah (kulia) akimuhudumia mteja katika banda la NSSF.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mratibu wa Tamasha la RAHA ZA JANA NA LEO Bw.Kahabi Ng'wendesha akilitambulisha rasmi Tamasha hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar katika hoteli ya Chichi iliyopo manispaa ya kinondoni jijini Dar.
  Bw. Kahabi alizungumzia namna kampuni ya Yuneda namna ilivyojiandaa kufanikisha tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na wakazi wa jiji la Dar jumamosi hii katika viwanja vya posta kijitinyama.
  Baadhi ya viongozi wa bendi tofauti wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuthibitisha ni namna gani wamejiandaa naTamasha  hilo linalokutanisha bendi sita za muziki wa dansi nchini Tanzania.Bendi hizo ni Mashujaa,Bantu group,Twanga pepeta,Msondo,Sikinde na king kikii"wazee sugu".
   Mwanamuziki Bichuka(Sikinde) akifafanua namna watakavyoiburuza Msondo Ngoma jukwaani ikiwa ndiyo waasimu wao wa siku nyingi kwa mara nyingine wanakutana jukwaa moja viwanja vya posta.Pia kutakuwa na silent moment kuwakumbuka wanamuziki wote wa mziki wa dansi waliotangulia mbele ya haki nchini Tanzania.
  King Kikii(kushoto) akielezea namna alivyojipanga kuteka mashabiki siku ya jumamosi hii katika viwanja vya posta .kulia ni mwanamuziki mkongwe Hamza Kalala.Milango ya uwanja itakuwa wazi kuanzia saa tano asubuhi hadi usiku mnene,Watoto bureeee mpaka saa kumi na mbili,wakubwa Tsh 8,000/= tu mpaka chwee.Michezo ya watoto,nyama choma na vinywaji vyakutosha vitakuepo.

  0 0

  Kamishna wa Walipa Kodi Wakubwa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Neema G. Mrema (wa tatu kutoka kulia walioketi) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Paul M. Masanja (wa pili kutoka kushoto walioketi) katika picha ya pamoja baada ya kikao cha wataalamu wa taasisi hizo mbili kujadili mikakati ya kuboresha ukusanyaji kodi kutoka sekta ya madini. Kikao hicho kimefanyika Julai 2, 2013 Giraffe Ocean View Hotel, Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka akiwa katika mazungumzo pamoja na Mke wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza,Bibi Cherie Blair wa Mkutano wao uliofanyika leo jijini Dar.
  Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka,kulia akimkabidhi zawadi ya kinyago cha kitanzania Bibi Cherie Blair baada ya kumaliza mazungumzo yao.
  Picha ya pamoja ya kumbukumbu ya Mhe.Waziri wa kazi na Ajira Bibi Gaudentia Kabaka na Bibi Cherie Blair pamoja na maofisa wao walioshiriki katika mazungumzo ya pamoja.

  Waziri wa Kazi na Ajira, Bibi Gaudentia Kabaka tarehe 2/07/2013 amekutana na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza Bibi Cherie Blair, katika mazungumzo ya kubadilishana uzoefu yaliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar-es-Salaam.

  Katika mazungumzo hayo ,Viongozi hao walijadili changamoto mbali mbali zinazowakabili akina mama wa kitanzania katika kujikwamua kiuchumi. Katika mazungumzo hayo Bibi Cherie Blair ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ijulikanayo kama “Cherie Blair Foundation” alionyesha kuguswa sana na juhudi za kinamama nchini wanajishughulisha na masuala ya ujasiria mali na kujijengea fursa za kujiajiri,kupitia taarifa ya Mhe .Waziri Kabaka iliyoelezea juhudi za kinamama waliopo katika sekta isiyo rasmi.

  Kina Mama hao wawili mashuhuri walikubaliana kushirikiana katika nafasi zao kuwasaidia kinamama hao wa Kitanzania.

  Wizara ya Kazi na Ajira inahusika na kuratibu masuala ya ajira nchini na inawasaidia Wajasiria mali waliopo katika sekta isiyo rasmi kushiriki na kutangaza bidhaa zao wanazozizalisha kupitia Maonesho

  Mashuhuri ya nchi za Afrika Mashariki yajulikanayo kama Nguvukazi/Jua kali, yanayofanyika kila mwaka kwa mzunguko katika nchi wanachama.

  0 0

  Rais Barrack Obama wa Marekani na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakizungumza na watendaji wa kuu wa sekta ya umeme nchini.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mr.Maswi,mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Sadik Meck Sadik na watatu kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati kiongozi huyo wa Marekani alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaofanywa na kampuni ya Symbion power ya Marekani huko Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Barack Obama wa Marekani akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Prof. Sospeter Muhondo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Syimbion,uliopo Ubungo jijini Dar.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakichezea mpira maalumu unaojaa nishati kila unapochezwa na nishati hiyo kutumika kuwasha taa ama kuchajia simu wakati wa uzinduzi wa Umeme kwa Afrika kwenye mtambo wa umeme wa Symbion Ubungo jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Kikwete na Mgeni wake Rais Barack Obama wa Marekani,wakisikiliza maelezo juu ya mpira unaoweza kufua umeme.
  Rais Barack Obama wa Marekani akipiga kichwa mpira huo wenye uwezo wa kufua umeme.
  Rais Barack Obama wa Marekani akizindua rasmi mpango wa marekani wa Umeme kwa Afrika kwenye mtambo wa umeme wa Symbion Ubungo jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

  0 0

  Wateja wa benki ya CRDB wakipata huduma ya kuweka na kuchukua fedha kutoka katika tawi linalotembea 'Mobile Branch' wakati wa Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Wateja wa benki ya CRDB wakipata huduma ya kuweka na kuchukua fedha kutoka katika tawi linalotembea 'Mobile Branch' 


  Wateja wa benki ya CRDB wakipata huduma za kibenki katika gari linalotembea kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 

   Ofisa Mauzo wa benki ya CRDB, Vicent Lulenga akimuhudumia mteja.
   Wateja wakipata huduma za kibenki
   Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB wakipata huduma kutoka katika banda la benki hiyo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mauzo wa benki ya CRDB, Mgeni Kabisama.
   Wateja wa benki ya CRDB wakipata huduma ya kuweka na kuchukua fedha kutoka katika tawi linalotembea 'Mobile Branch'
   Huduma za kibenki zikitolewa katika banda la benki ya CRDB.
    Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB wakifungua akaunti katika banda la CRDB wakati wa Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

  0 0

  The Tanzanian International Bongoflava Artist has signed a licensing deal with one of the world biggest and top Music labels "Universal Music, South Africa". His content will be distributed through the Kleek, a mobile streaming service available on all Samsung smart phone in Ghana, Angola, Kenya, South Africa and Nigeria. CPwaa is one of the A-List Artists signed by Universal Music from East Africa for its Kleek continental platform.

  On March 13, 2013 Universal Music Group, in partnership with Samsung, as well as African and international music labels and publishers, has launched a pan-African mobile music streaming service called the Kleek.  Designed and built specifically for Africa, the Kleek will bring music lovers closer to their favorite artists, while also providing artists with valuable access to a wider pan-African audience.

  This new deal will make CPwaa not only to gain more revenues from his music but also a worldwide exposure and global outreach through the Kleek.

  To learn more about the Kleek go here

  Kind Regards.

  Ilunga Khalifa ( CPwaa)

  0 0

  Shine A Light is a group founded by KCMC (Kilimanjaro Christian Medical College)students in June 2010 aimed at helping children who are less fortunate (orphans ,street children etc ) achieve their dreams, have a chance at life and a bright future. WEBSITE : www.shine-a-light.org

  In commemorating the day of the african child shine a light in collaboration with the community and pediatric department conducted a pediatric screening event at kifaru village in mwanga on the 30th of JUNE 2013!Targeting children aged one year to seven years . a total number of 408 children were screened !!!

  JOINING HANDS TOUCHIN HEARTS!!!
  Children and their parents gather at kifaru primary school waiting to be screened.
  Dr Rahim pediatrician at KCMC at the screening event!
  Members of shine a light at work !
  Members of shine a light pose for a group photo at kifaru mwanga !

  0 0

  Mahakimu Mkoani Lindi wametahadharishwa kutojiwekea malengo makubwa ya kutaka kujipatia utajiri wa haraka haraka tofauti na vipato vya mishahara yao ili kujiepusha na uwezekano wa kujitumbukiza kwenye vitendo viovu vya kuomba rushwa na hivyo kupindisha maamuzi ya utoaji haki kwa jamii ikiwemo wanyonge kutokuwa na haki.

  Taadhari hiyo imetolewa na katibu msaidizi idara ya viongozi wa utumishi wa umma/siasa Bi Zahara Guga kwenye mafunzo ya kuwaaelimisha mahakimu Mkoani humo juu ya kusimamia utoaji wa haki kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ili kuwatendea haki wananchi.

  Aidha Bi Zahara Ameonya kuwa kama utoaji haki kwa wananchi usipofanywa kwa umakini na uadilifu mkubwa, kuna hatari kwa mahakimu hao wakawa chanzo cha kulisababishia taifa kuingia kwenye migogoro na hatimaye uvunjifu wa amani usio wa lazima.

  Akifungua Mafunzo hayo,Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Lindi,Joh Likango alitaja baadhi ya mapungufu na matatizo ya kimaadili kwa Mahakimu ni pamoja na rushwa , utoaji wa huduma usioridhisha, matumizi mabaya ya madaraka, wizi, unyanyasaji wa kijinsia pamoja na rushwa ya ngono.

  Likango alisisitiza kuwa Rushwa Imekuwa kero kubwa kwa jamii kutokana na kukithiri kwenye sekta za umma jambo ambalo linawafanya wananchi kununua haki zao na kusababisha huduma nyingi za kijamii kutolewa chini ya kiwango.

  ‘mahakama ni chombo ambacho kinatoa haki kwa jamii bila ya upendeleo hivyo basi idara hiyo inawajibu kutekeleza majukumu yake kuhudumia wananchi bila ya upendeleo ili Haki itolewe bila Chochote chenye kushawishi vinginevyo Mtapoteza Amani iliyopo”Alimalizia Likango.

  Kwa upande wake Hakimu Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Dunstan Ndunguru kwa niaba ya wenzake amewataka mahakimu wenzake kuyatumia mafunzo hayo kurekebisha kasoro zao ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki wanayostahili pale wanapohitaji msaada wa kisheria.
  Jengo la Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi Lindi
  Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Lindi akifungua mafunzo kwa mahakimu wa mkoa wa Lindi kuhusiana na Maadili.
  Mahakimu toka mahakama za mkoa wa Lindi wakiwa katika mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na Sekriterieti ya maadili ya Umma na kufanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi,John Likango,wa pili toka kushoto waliosimama akiwa katika Picha ya Pamoja na mahakimu wa mahakama za mkoa wa Lindi wakiwemo maafisa toka Sekriterieti ya maadili ya Umma.Picha na Habari zimeleta na Abdulaziz Video,Globu ya Jamii-Lindi.

  0 0

  Waziri wa Kazi,Uwezeshaji Wananchi Uchumi na Ushiriuka na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Zanzibar.Mhe Haroun Ali Suleiman (kulia) akimsikiliza Naibu katibu Mkuu wa UVCCM,Shaka Hamdu wakati alipokuwa akizungumza mambo kadhaa yahusuyo ziara ya kuhimarisha chama,akilipokuwa katika kituo cha Mtegani FM Makunduchi,Zanzibar.
  Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar,Shaka Hamdu akizungumza kwenye kituo cha Redio FM Mtegani Makunduchi wakati wa ziara za mikoa kukiimarisha Chama hicho.

  0 0
 • 07/03/13--01:46: TAARIFA YA MSIBA
 • MWANACHAMA WA BIAFRA JOGGING CLUB DAR ES SALAAM AMBAYE PIA NI MKE WA MWENYEKITI WA BIAFRA JOGGING CLUB,BI. EVELYNE ALFRED,ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTOTO WA DADA YAKE KILICHOTOKEA JANA JIJINI DAR.

  MSIBA UKO NYUMBANI KWAO KINONDONI MKWAJUNI NA MAZISHI YATAFANYIKA SAA KUMI JIONI YA LEO KATIKA MAKABURI YA KINONDONI,JIJINI DAR.

  KWA MAWASILIANO ZAIDI 

  MOLLEL
  0717 375375

  MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI

  - AMIN.


  0 0


  0 0


  0 0

  Proffessor Calestous Juma who is a famous proffessor of the practice of international Development and director of the science ,technology and Globalization Project at Harvard Kennedy School USA gives an overview about the GMO’s during his public lecture.
  COSTECH Director General Dr Hassan Mshinda pays attention to the public lecture about the innovations in agriculture for improved productivity and socio economic development at COSTECH conference hall on 2nd July 2013.
  COSTECH Director of Finance and Administartion Hussein Shaaban(right) looks at the power point slides about the next harvest innovation in african agriculture during the public lecture presentation at COSTECH.With him is COSTECH Chief Research Officer Dr Nicholaus Nyange(left).
  A cross section of the participants of the public lecture pay attention to the presentation about the innovations in agriculture for improved productivity and socio economic development at COSTECH conference hall.Looking on from the right side is the former Miss Tanzania Faraja kota Nyarandu.

  0 0

  Mtaalamu wa mazingira wa ofisi ya bonde la maji la Pangani ,Mhandisi Arafa Maggidi akiwa na mtaalamu wa vipimo kutoka kituo cha utafiti wa kuondoa Frolide cha Ngurdoto Godfrey Mkongo wakiangalia maji yanayodaiwa kuwa na kemikali yakiingia mto Karanga .
  Mtaalamu wa mazingira wa ofisi ya bonde la maji la Pangani ,Mhandisi Arafa Maggidi akiwa na mtaalamu wa vipimo kutoka kituo cha utafiti wa kuondoa Frolide cha Ngurdoto Godfrey Mkongo wakichukua sampuli ya maji ya Mto Karanga kwa ajili ya vipimo.
  Mwananfunzi wa chuo cha maabara ya sayansi,ufundi na teknolojia Arusha Stephew Msalale akichukua maji ya mto Karanga kama sampuli kwa ajili ya vipimo.
  Mtaalamu wa mazingira wa ofisi ya bonde la maji la Pangani ,Mhandisi Arafa Maggidi akiwa na mtaalamu wa vipimo kutoka kituo cha utafiti wa kuondoa Frolide cha Ngurdoto Godfrey Mkongo wakichukua sampuli ya maji ya Mto Karanga kwa ajili ya vipimo.

  Na Dixon Busagaga waglobu ya jamii Moshi

  KUFUATIA kutolewa kwa taarifa za kutiririshwa kwa maji yanayodaiwa kuchanganyika na kemikali kutoka kwa baadhi ya viwanda vilivyoko kando ya mto Karanga ofisi ya Bonde la Pangani(PBWO) imelazimika kuchukua sampuli ya maji hayo kwa ajili ya kuyafanyia vipimo.

  Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya taarifa za kichunguzi zilizofanywa na Globu ya jamii baada ya kuwezeshwa na na mfuko wa waandishi wa habari(TMF) na kuripoti jinsi wakazi wa vijiji vya Chekeereni,Weruweru,Mijongweni na Kiyungi walivyo athirika na maji hayo.


older | 1 | .... | 182 | 183 | (Page 184) | 185 | 186 | .... | 3285 | newer