Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1828 | 1829 | (Page 1830) | 1831 | 1832 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Kampuni ya mawasiliano na mahusiano ya Proaktiv Communications Ltd ya jijini Dar es salaam ambayo inahusika kutangaza makampuni na taasisi mbalimbali za nchini na kimataifa imejiunga katika mtandao wa Instagram kwa lengo la kuwafikishia wadau wake taarifa za matukio na shughuli mbalimbali zinazoratibiwa na kampuni hiyo inayojulikana kwa jina la ProaktivPR kwenye mtandao wa Instagram unaokua kwa kasi zaidi dunia nzima. 

   Akizungumza na Blogu hii, mwanzilishi wa kampuni hiyo Mwesiga Kyaruzi amesema kwamba kutokana na mahitaji ya soko la habari, mawasiliano na masoko ambapo watu wengi hivi sasa wanategemea zaidi kupata habari haraka zaidi kupitia mitandao ya kijamii, kampuni yake imeona ni vyema kufungua akaunti ya Instagram ili kupanua wigo wa usambazaji habari za bidhaa na huduma zitolewazo na makampuni pamoja na taasisi mbalimbali zinazohudumiwa na kampuni hiyo.

   “Pamoja na kuwafikia watu wengi zaidi wanaotumia huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na wateja wetu, pia hii ni hatua thabiti ya kwenda na mahitaji ya wakati uliopo kwani takwimu zinaonyesha kwamba mtandao huo hadi kufikia mwezi April mwaka huu ulikuwa unatumiwa na watu wapatao milioni 800 kuzungumza na kupashana habari kwa mwezi, hivyo basi kwa mazingira ya dunia ya sasa ni muhimu kwenda na wakati badala ya kutegemea vyombo vya habari vya asili (traditional media) pekee kama magazeti, redio na TV kwani dunia inabadilika kwa kasi,” alisema Kyaruzi. 

   Kampuni ya Proaktiv Communications inatoa huduma za kujenga taswira kwa kuratibu utoaji habari chanya kuhusu matukio, bidhaa, huduma na masuala mbalimbali kwa sekta za kibenki, kilimo, madini, mawasiliano, usafirishaji, elimu, afya, ujenzi, viwanda, nishati, huduma za kifedha, burudani, michezo pamoja na utalii. Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea tovuti ya kampuni hiyo www.proaktiv.co.tz na hakikisha unafollow akaunti ya Instagram kupitia link ya www.instagram.com/proaktivpr ili kujionea matukio na habari kemkem zinazoratibiwa na kampuni hiyo ya Kizalendo.

  0 0

  Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma TAKUKURU. Usikose kuangalia kipindi hiki uone jinsi ambavyo TEHAMA imesaidia kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma hasa kupitia sims za mkononi.

  0 0

  Mashindano ya mpira wa Miguu maarufu kama URIO CUP 2017 yamezinduliwa rasmi Jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo, yanayoratibiwa na Msonge Africa Kwa kushirikiana na Jomo International na kudhaminiwa na Times FM, yana lengo la kuzikutanisha timu 32 zinazotokea katika sehemu mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam ili kuleta hamasa katika kata ya Kunduchi na pia kuzipa timu za kata hiyo uzoefu. 

  Akizindua mashindano hayo, Diwani wa Kata ya Kunduchi, Michael Urio ambaye ndio mdhamini na mwanzilishi wa kombe hilo la Urio Cup alisema hii ni mara ya pili kwa mashindano hayo kufanyika kwani mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2015 na kuhusisha timu 16 na kuongeza kuwa Urio Cup mwaka huu inaenda sambamba na Kampeni maalumu ya ‘Wezesha Mama na mtoto Mpya wa Kuncuchi’ ambayo ilizinduliwa hivi karibuni na yenye lengo la kuboresha zahanati ya Ununio na Mtongani.  Diwani wa Kata ya Kunduchi, Michael Urio akipiga danadana ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Urio Cup mashindano ambayo yanatarajiwa kufanyika katika kata yake kuanzia mwezi ujao. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Radio Times FM, Rehure Nyaulawa, Mratibu wa Urio Cup, Deus Buhilo na Katibu wa Ligi na Mashindano wa Chama Cha Mpira Wilaya ya Kinondoni, Khalid Shehani.

  “Moja ya ahadi nilizotoa kwa wananchi wangu ni kuimarisha sanaa na michezo kwani michezo sasa hivi ni chanzo kikubwa cha ajira hasa kwa vijana. Urio Cup iliyopita ilitoa baadhi ya wachezaji waliojiunga na timu za daraja la kwanza na nimefahamishwa kuwa kuna wengine pia wanacheza ligi kuu,” alisema Mh. Urio.

   Alitoa wito kwa wadau mbalimbali wapenda michezo wamuunge mkono katika hili ili kombe hili liweze kukua mwaka hadi mwaka na kuwafadisha vijana wengi zaidi. “Nimearifiwa kuwa tutawaalika wawakilishi kutoka timu za ligi kuu ili waweze kutafuta vipaji kutoka kwa timu zitakazoshiriki Urio Cup. 

  Hili litasaidia sana katika kuamsha ari ya vijana huku wote wakiwa na matumaini ya kusajiliwa na timu kubwa siku moja,” alisema diwani huyo. Naye mratibu wa Urio Cup, Bw. Deus Buhilo alisema maandalizi yote yamekamilika na wanatarajia kushindanisha timu 32 ambazo zinatakiwa kujisajili na kulipia ada ya Tsh 70,000 na timu zinazotakiwa kujisajili zinatakiwa kutuma maombi na kupata maelekezo kupitia namba 0652559122 na malipo kupitia namba 0628555333. 
   Diwani wa Kata ya Kunduchi, Michael Urio akizungumza wakati wa uzinduzi wa Urio Cup mashindano ambayo yanatarajiwa kufanyika katika kata yake kuanzia mwezi ujao. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Radio Times FM, Rehure Nyaulawa na Katibu wa Ligi na Mashindano wa Chama Cha Mpira Wilaya ya Kinondoni, Khalid Shehani.

  “Urio Cup ni mashindano makubwa na tumeweka vigezo ili kuhakikisha tunakuwa na mashindano bora yanayofuata kanuni zote za FIFA na TFF. Tunataka kuwajengea vijana wetu uzoefu ili waweze kufika katika ngazi za juu zaidi,” alisema mratibu huyo na kumshukuru Diwani Urio kwa kuanzisha mashindano hayo.


  0 0

   Jubilee Insurance katika kuadhimisha miaka 80 ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo ya bima imezinduwa vyoo katika shule ya  msingi Itiji iliyopo jijini Mbeya, vyoo hivyo vyenye jumla ya matundu 12 vilivyo jengwa na kampuni hiyo ya bima ya Jubilee Insurance na kuzinduliwa na  Meneja wa kanda nyanda za juu mamlaka ya bima Tanzania,  Consoleta Cabone baada ya kuguswa na changamoto ya  vyoo katika shule mbalimbali za msingi nchini.
   Meneja wa kanda nyanda za juu mamlaka ya bima Tanzania,  Consoleta Cabone akizungumza baada ya kukabidhi vyoo hivyo, ambapo alisema "Naipongeza sana Jubilee Insurance kwa kujitoa kujenge vyoo vya wanafunzi wa shule ya msingi Itiji, kwani ni jambo kubwa na linalo fanya na wacheche na badara ya kufanya sherehe kubwa katika maoteli kugawana kile kilicho baki kwenye bima na hatimae kurejeshwa kwa wananchi kwa kufanya mambo mema yenye baraka ikiwemo hili la ujenzi wa vyoo kwenye shule mbalimbali za msingi" pia Consoleta Cabone alitoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo yanayozungukwa na shule hiyo kulinda na kudhamini vyoo vilivyo jengwa na Jubilee Insurance.
  Meneja wa Tawi la  Jubilee Insurance kwa nyanda za juu kusini, Anne Qares akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi Meneja wa kanda nyanda za juu mamlaka ya bima Tanzania, Consoleta Cabone katika uzinduzi na ufunguzi wa vyoo vya wanafunzi wa shule ya msingi Itiji vyoo vilivyo jengwa na Jubilee Insurance.
   Mkuu wa Shule ya msingi Itigi Mwl Lightness E. Makundi Akitoa shukran kwa Jubilee Insurance kwa ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika shule yake.

    Mgeni rasmi akiwa katika zoezi  la uzinduzi wa vyoo shule ya msingi Itiji iliyopo jijini mbeya.


  0 0

  Na Teresia Mhagama, Arusha

  Katika mkutano wa Kimataifa wa Kamati ya Kikanda inayohusika na upigaji vita uvunaji haramu wa madini katika Ukanda wa Maziwa Makuu uliofanyika jijini Arusha 25-27, Julai, 2017, Tanzania ikiwa ni nchi Mwanachama, ilieleza jinsi ilivyotekeleza malengo Sita ya Kamati hiyo ambayo yanapaswa kutekelezwa na nchi wanachama 12 ili kufanikisha udhibiti wa uvunaji haramu wa madini.

  Awali, Kamishna Msaidizi wa Madini, Mhandisi John Nayopa alieleza kuwa malengo ya ICGLR ni pamoja na kuwianisha sheria za nchi wanachama ili kuweka uwiano katika sheria za kudhibiti uvunaji haramu wa madini, kuwa na hati moja ya usafirishaji madini ya Tin, Tantalum, Tungsten na dhahabu (3TG) ili kuhakikisha kuwa madini hayo yanachimbwa na kutumika kihalali na lengo la Tatu ni kurasimisha shughuli za wachimbaji wadogo.

  Alisema kuwa malengo mengine ya ICGLR ni pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake katika shughuli za uchimbaji madini, kuimarisha uwazi na uwajibikaji na kuwa na mfumo wa kanzidata utakaowezesha kufuatilia taarifa za uvunaji, usafirishaji na uuzaji wa madini.

  Kuhusu uchimbaji wa madini ya 3TG, alisema kuwa, Serikali imeendelea kutoa leseni za uchimbaji wa madini hayo ambapo mpaka sasa zimetolewa leseni 236 za uchimbaji wa madini ya Bati (Tin), leseni 18 za uchimbaji wa madini ya Tantalite, leseni 2 za madini ya wolframite na leseni 11,826 kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ambapo asilimia 95 ya leseni hizo zimetolewa kwa wachimbaji wadogo.

  Kuhusu suala la kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji, Mhandisi Nayopa alieleza kuwa Tanzania imeshajiunga na Mpango wa Kimataifa wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji (EITI) mwaka 2009 na kuthibitishwa mwaka 2012 ambapo mpaka sasa imeshatoa Ripoti Saba zinazoonesha mapato yanayoingia serikalini kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini, gesi asilia na mafuta na sasa inafanyia kazi ripoti ya mwaka wa Fedha wa 2015/2016 ambapo wananchi sasa wanapata fursa ya kufahamu mapato yanayotokana na uwepo wa Rasilimali hizo.

  Kuhusu lengo la ICGLR la kurasimisha shughuli za uchimbaji mdogo wa madini na kuongeza ushiriki wa wanawake katika Sekta ya Madini, Mhandisi Nayopa alisema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha kuwa suala hilo linatekelezwa kwa ufanisi ambapo mpaka kufikia mwezi Mei, 2017, takriban leseni za madini 35,000 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo huku ikiendelea kutenga maeneo ya uchimbaji madini na kuhimiza uundwaji wa vyama vya ushirika vya wachimbaji wadogo.

  Aliongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa kuna makundi na vyama vya wachimbaji wadogo 143 vinavyomiliki leseni za madini ambapo makundi 6 kati ya hayo ni wachimbaji wanawake.

  Kuhusu lengo la kuingiza taarifa za madini katika mfumo wa kieletroniki wa kanzidata, Mhandisi Nayopa alisema kuwa Tanzania inao mfumo wa utoaji leseni (Mining Cadastre database) ambao una taarifa za kijiolojia na takwimu mbalimbali za madini na sasa Serikali iko katika hatua za kuboresha mfumo huo ili uendane na mahitaji ya ICGLR.

  Kuhusu suala la kuwianisha sheria za madini kwa nchi wanachama wa ICGLR na kutumia hati moja ya usafirishaji madini, Mhandisi Nayopa alieleza kuwa, rasimu za marekebisho katika Sheria ya Madini na kanuni zake zimeashaandaliwa ili kuendana na muongozo wa ICGLR kuhusu Rasilimali zilizopo katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu .

  Kuhusu suala la kuwa na hati ya pamoja ya usafirishaji wa madini ya 3TG ifikapo mwaka 2018, Mhandisi Nayopa alieleza kuwa, sambamba na mabadiliko ya hivi karibuni katika sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo yamelenga kuboresha usimamizi katika Sekta ya Madini hali itakayopeleka mabadiliko katika masuala ya utawala kwenye Sekta ya Madini, bado jitihada zinafanyika ili kutimiza lengo la ICGLR la kuwa na hati hiyo ya pamoja.

  Akizungumzia Mkutano huo kwa ujumla, Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka alisema kuwa mkutano huo umejikita katika kujadili madini ya 3TG ambayo yanapatikana Tanzania na katika nchi wanachama ili madini hayo yachimbwe kwa mujibu wa taratibu, kuuzwa katika mkondo halali na kuwa na mfumo wa ufuatiliaji wa jinsi madini hayo yanavyochimbwa mpaka yanapofika kwa mlaji wa mwisho.

  Vilevile alisema kuwa mkutano huo pia umejadili suala la ajira kwa watoto katika shughuli za uchimbaji madini ambapo alisema kuwa kwa upande wa Tanzania suala hilo lipo katika sheria ya madini ya mwaka 2010 ambayo sasa imefanyiwa marekebisho ambayo inakataza mtu aliye chini ya miaka 18 kuhusika katika shughuli za madini.
  Baadhi ya Wajumbe kutoka Tanzania, Sudan, Sudan Kusini na Rwanda waliohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa 15 wa Kamati ya ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya uvunaji haramu wa madini katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika unaofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na wa pili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Mhandisi John Nayopa.

  0 0

  WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB wilayani Kilosa, Morogoro kwa kushirikiana na Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) cha benki hiyo wametoa msaada kwa mtoto Sheila Bushiri (7) ambaye alizaliwa akiwa mlemavu wa mguu mmoja kufanyiwa upasuaji na kumnunulia mguu wa bandia ili aweze kutembea kama watu wengine. 

  Akizungumza kuhusu msaada huo, Meneja wa tawi la benki ya NMB KIlosa, Dismas Prosper alisema walimjua mtoto huyo kupitia Bi. Shalphina Lipinga ambaye alikwenda ofisini kwao kuomba msaada wa kusaidia watoto wenye uhitaji na baada ya kuwaonyesha mtoto huyo waliona kuna haja ya kumsaidia. 

  Alisema baada ya kumwona wao kama wafanyakazi walichangishana pesa na kutokana na utaratibu wa benki hiyo kuwa iwapo wafanyakazi wakichangishana pesa kitengo cha CSR kuwaongezea pesa sawa na kiwango walichotoa walifanikisha mtoto huyo kufikishwa kwenye hospitali ya CCBRT iliyopo Dar es Salaam ambapo alipatiwa matibabu.

  Sheila akiwa katika picha na wafanyakazi wa tawi la NMB wilayani Kilosa, Morogoro ambao ndiyo waliotoa msaada kwa kushirikiana na Mkuu Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kumsaidia mtoto huyo kufanyiwa upasuaji kwenye hospitali ya CCBRT na kupewa mguu wa bandia ambao kwa sasa unamwezesha kutembea tofauti na awali.


   “Alikuja ofisini Shalphina kusema kuwa anasaidia watoto ambao hawajiwezi na katika maongezi alisema kuna mtoto alizaliwa na ulemavu wa mguu mmoja na anaishi na bibi yake na anampeleka shule kila siku akimbeba mgongoni hivyo kama kuna mvua hawezi kwenda shule, mimi nikaona hapo kuna shida kubwa, “Nilipoona picha hana mguu mmoja kama mzazi iliniuma sana, niliweza kuwasilisha kwa wafanyakazi wenzangu na nilipowauliza nini tumfanyie wengi walipendekeza baiskeli na tukakubaliana kuchanga, alipopelekwa CCBRT walishauri apate mguu wa bandia na wafanyakazi wengi wakalikubali,” alisema Prosper. 

  Prosper alisema lengo la wafanyakazi hao kutoa msaada ni kumwona mtoto huyo akiwa na furaha na kuendelea na masomo yake vizuri na kwasasa wana mpango wa kuendelea kutoa msaada kwa watu wengine ambao wanahitaji kupata msaada ili kuendesha shushuli zao za kila siku kama watu wengine ambao hawana ulemavu.
   
  Mwonekano wa mguu wa mtoto Sheila Bushiri kabla ya kusaidiwa na wafanyakazi wa Benki ya NMB Kilosa kufanyiwa upasuaji na kupewa mguu wa bandia.

   “Mwisho wa siku tulifanikiwa kuweka tabasamu kwenye uso wa yule mtoto kwa kutumia kile kidogo ambacho Mungu ametusajilia tumsaidie na sio kwa yule mtoto tu tuna malengo ya kuendelea kusaidia wengine ili na wao wapate tabasamu,” alisema Prosper. Kwa upande wa bibi yake Sheila, Habiba Said ambaye ndiyo anaishi na mtoto huyo alisema mtoto huyo alizaliwa na ulemavu huo na akiwa na miezi tisa mama yake alimwacha nyumbani na kuondoka huku baba wa mtoto akiwa hajulikani. 

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiweka saini kwenye kitabu cha wageni wakati alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka, kwa lengo la kujitambulisha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
  Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, ambaye amefika katika ofisi yake kwa lengo la kujitambulisha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo, kulia ni kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Boniveture Mushongi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mwamapalala mkoani Simiyu, wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Shinyanga, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo pamoja nakujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wananchi wa Maganzo mkoani Shinyanga, wakati alipowasili akitokea mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo pamoja nakujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.

  0 0
 • 07/27/17--01:00: NHIF KUZINDUA TOTO AFYA KADI


 • 0 0
  0 0

  Dear Friends,

  Tanzania Standard Newspapers (TSN) Ltd, invites you to join and participate in the 3rd TSN Business Forum to be held in Tanga on the 17th August 2017. The Forum provides you with an opportunity to pitch your products, services, and innovations and engage the business community in the Region. It also gives you an opportunity to enjoy a well coordinated business exposure through TSN brands - The Daily News and HabariLeo and online channels including dnTV. Please come, join, and conquer. Karibuni Sana!  0 0

   Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mjini Kahama, Shinyanga jana. Klabu hiyo imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Katikati ni mmoja wa wateja, Salum Selemani na Joshua John (kulia), Ofisa Masoko wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kutoka ofisi ya Mwanza.
   Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa mjini Kahama, katika semina iliyoandaliwa kabla ya  uzinduzi  rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC hiyo iliyoanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Hafla ya uzinduzi ilifanyika mjiini Kahama, Shinyanga jana.
   Meneja wa Kanda wa NBC, Daudi Mfalla (kulia), akizungumza wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi  rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC  iliyoanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara wadogo na wakati wa NBC, Evance Luhimbo.
   Baadhi ya wateja wa NBC mjini Kahama waliohudhuria uzinduzi wa B-Club ya benki hiyo, wakijipiga picha ‘selfie’ pamoja na bango lenye picha inayoonyesha kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni baadhi ya shamrashara zilizopamba uzinduzi huo.  0 0


   Kuna mtazamo wa jumla miongoni mwa wananchi kuwa usalama nchini umeimarika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kama inavyooneshwa na zaidi ya nusu ya wananchi hao (asilimia 53). Lakini asilimia 37 ya watanzania wanasema hali ya usalama imebaki vilevile huku asilimia 10 wanasema hali imekuwa mbaya zaidi.

  Takwimu za Sauti za Wananchi za mwaka 2015 zilionesha kwamba asilimia 57 ya wananchi hawakuwahi kuhisi hawako salama kutembea kwenye maeneo wanayoishi. Lakini mwaka 2017 idadi imeongezeka na kufikia asilimia 71. Kwa ujumla kwa mwaka uliopita, asilimia 29 ya wananchi hawakujisikia salama kutembea kwenye maeneo wanayoishi au waliogopa kufanyiwa uhalifu kwenye nyumba zao (asilimia 26). Asilimia 16 walikiri kukaa majumbani mwao huku wakiwa na hofu ya uhalifu.
  Pamoja na viashiria chanya kuhusu usalama, viwango vya uhalifu vinaonekana kuwa juu. Asilimia 41 ya wananchi wamewahi kushuhudia uhalifu ukifanyika hadharani ndani ya mwaka mmoja uliopita.

  Matokeo haya yametolewa na Twaweza katika utafiti wake uitwao Hapa usalama tu: Usalama, polisi na haki nchini Tanzania. Muhtasari huu unatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simuza mkononi. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,805 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) mnamo mwezi Aprili mwaka 2017.


  Vilevile takwimu hizi zinaonesha kwamba mara nyingi wananchi hawaombi msaada kwa polisi,hasa pale wanapokuwa wahanga wa uhalifu. Ni mwananchi mmoja tu kati ya wanne (asilimia 26) anayeomba msaada polisi. Hata hivyo, idadi hii inatofautiana kutokana na makundi mbalimbali: matajiri (asilimia 42) na wakazi wa mijini (asilimia 41) wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuomba msaada polisi. Wananchi wengine (asilimia 66), huenda kwanza kwa mwenyekiti wa kijiji/mtaa. Wakati huo huo, idadi kubwa ya wananchi imeripoti kutotoa kabisa taarifa za uhalifu: asilimia 21 wanasema hawatatoa taarifa za uhalifu zilizolenga kaya zao na asilimia 8 wanasema uhalifu kwenye jamii zao hautoripotiwa.
  Bila shaka wananchi huamua kutotoa taarifa za uhalifu polisi kutokana na umbali wa vituo. Asilimia 27 ya wananchi hawana kituo cha polisi kwenye kata zao. Hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya vijijini ambapo asilimia 50 wanasema hawana kituo cha polisi kwenye kata zao na asilimia 27 hutumia muda mrefu (zaidi ya dakika 30) kufika kwenye kituo cha polisi. 

  0 0


  Pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Albert Msole (CCM) ambaye amefanikiwa kushinda tena nafasi hiyo baada ya kumbwaga mpinzani wake Philemon Oyogo (Chadema).    
  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Yefred Myenzi akitoa matokeo hayo alisema kati ya madiwani 22 waliopiga kura, madiwani 14 walimpigia Msole na madiwani nane walimpigia Oyogo. 
  Myenzi alisema Msole atadumu kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2017/2018 ndipo utakapofanyika uchaguzi mwingine wa makamu Mwenyekiti. Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo Msole aliwashukuru madiwani wote kwa heshima kubwa waliyompa na kumrudishia tena nafasi hiyo hivyo ataendelea kushirikiana nao kuhakikisha kuwa halmashauri hiyo inasonga mbele kwenye maendeleo. 

  "Tuendelee kushirikiana pamoja kwani tumeshirikiana vizuri tangu mwaka 2015 na kazi yangu kubwa ni kumsaidia Mwenyekiti wa halmashauri yetu, natoa ahadi kwenu kuwa nitaendelea kuteleleza wajibu wangu kwani heshima mliyonipa ni kubwa japo mimi ni mdogo kwenu," alisema Msole.  
  Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipitieck alisema kama siyo jambo la kisheria, kanuni na taratibu, wasingeruhusu uchaguzi huo ufanyike kwani jitihada za Msole za uchapakazi kwenye halmashauri hiyo zinajulikana. 
  "Msole ni mpambanaji mzuri, muwajibikaji, muwazi na anayefanya kazi zake kwa kutenda haki bila kupendelea mtu na nadhani wote tunatambua jitihada zake kama siyo sheria angekuwa makamu Mwenyekiti kwa miaka yote mitano," alisema Sipitieck.

  0 0

  Wahariri na Wanahabari wametakiwa kuendelea kutumia kalamu zao katika kuandika masuala mbalimbali ya utalii wa Tanzania ili kuutangaza ikiwa sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 
   'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 

  Prof Maghembe amesema katika kufanikisha kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutegemea utalii Wanahabari wanapaswa kushiriki moja kwa moja katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi kwa Watanzania na wageni kwa kutumia kalamu zao.

  "Nyinyi waandishi wa habari msikubali kuandika jambo ambalo hamlijui kitaaluma, kwani ukifanya hivyo utakuwa hujengi jamii yako,hivyo ni muhimu sana kwa wanahabari kujua habari sahihi za uhifadhi hasa kwa kuzungumza na wataalamu kutoka sekta hiyo"amesema Prof. Maghembe.

  Nae Mkurugenzi wa TANAPA, Allan kijazi amesema kuwa utalii unachangia 17.2% ya pato la Taifa na 25% ya fedha za kigeni nchini,80% ya utalii unatokana na Hifadhi za Taifa.

  Amesema kuwa TANAPA inajitegemea kwa asilimia 100, na mchango wao kwa serikali umeongezeka kutoka bilioni 27 mwaka 2015/16 mpaka bilioni 34 kwa mwaka 2016/17 sawa na ongezeko la bilioni saba.

  "Tanzania ina vivutio vingi vya kipekee ukilinganisha na nchi nyingine Duniani,Mamlaka kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini pamoja na Ofisi za Balozi zetu nchi mbalimbali inajitangaza ndani na nje ya Nchi ili kuongeza idadi ya Watalii",amesema Kijazi.

  Akielezea Uvumi wa Mlima Kilimanjaro kuwa haupo Tanzania,anasema ni ni propaganda za ushindani wa kibiashara, lakini matumizi ya Teknolojia yamesaidia kutoa elimu,anasema na kuongeza kuwa hivi sasa idadi kubwa ya watalii kutoka Nje ya nchi wanaelewa Mlima huo upo Tanzania.

  Akielezea changamoto ya Ujangili,Kijazi anaeleza kuwa kwa sasa matukio ya ujangili yamepungua kwa 80% na kwamba Mamlaka inashirikiana na Jumuia ya Kimataifa kutokomeza Soko la bidhaa zinazotokana na ujangili.

  Kijazi alimaliza kwa kusema kuwa TANAPA ilianzishwa kisheria mwaka 1959 kukiwa na hifadhi moja tu ya Serengeti,lakini mpaka sasa hifadhi zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 16 mwaka 2014.

   Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe akizungumza jambo alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
    Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia  yaliyaokuwa yakijiri kwenye mkutano huo ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe kufungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
   Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
    Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanga'.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella, akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu,lengo ikiwa ni kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Wengine ni Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mkurugenzi Mradi wa kuzuia biashara hiyo kutoka Taasisi ya Kimataifa ya RTI,Dk. Lyungai Mbilinyi.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam
  Mkurugenzi Mradi wa Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Taasisi ya Kimataifa ya RTI, Dk. Lyungai Mbilinyi, akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara hiyo,lengo ikiwa ni kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo.Wengine ni Mwenyekiti wa kamati hiyo () na Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Kamati na Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu akizungumza wakati wa mkutano wa kupitia Sheria mbalimbali zinazosimamia biashara hiyo. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) mpya na la kisasa katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo Tarafa ya Puge ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini.

  Tukio hilo la kukabidhi gari hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula ambaye alitoa agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito kuwawaisha sehemu muhimu za kutolea huduma stahiki. 

  Mkuu wa Wilaya huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk. Kigwangalla kwa kuweza kuwasaidia wananchi wa Jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia gari hilo la Wagonjwa kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi hao ambao wapo maeneo ya mbali na kituo cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa msaada kwa kuwapeleka wateja katika ngazi za juu za huduma hiyo ikiwemo Hospitali za Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa.

  Aidha, alisema ni marufuku wagonjwa kuombwa kuchangia mafuta ya ambulance hiyo au gharama yoyote ile, gari hili wagonjwa walitumie bure kwani limetolewa bure na pia huduma zote zikiwemo za mafuta zinalipwa na Halmashahuri hiyo. 

  “Gari hilo lipatikane kituoni wakati wote pamoja na dereva. Tumeshahakikishiwa hapa Halmshauri imesema ina mafuta ya kutosha litakuwa linajazwa lita 90, kila yatakapokuwa yametumika hivyo kusiwe na kisingizio kingine cha kuweza kudai mafuta ama kuwatoza wananchi gharama na atakayefanya hivyo Serikali hii si ya mchezo hatua kali zitafuata , tutakutumbua tu” alieleza Mh. Ngupula.
  Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
  Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge, lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.


  0 0


   Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa eneo la stendi ya mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro akitokea mkoani Dodoma leo Julai 27, 2017.

   Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wananchi wa eneo la stendi ya mabasi ya Msamvu  mkoani Morogoro akitokea Dodoma leo Julai 27, 2017.
   Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akimsikiliza Bi Maria Gabrieli aliyemweleza kero za wafanyabiasahara ndogondogo wa Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro kunyanyaswa. Julai 27, 2017.

  Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Bi Halima Ali akimweleza juu ya kero za wafanyabiasahara ndogondogo wa Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro kunyanyaswa. Julai 27, 2017.

  Picha na IKULU

  0 0

  Na. Hassan Mabuye.

  Mawaziri watano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watembelea mpaka wa Tanzania na Uganda ili kutatua changamoto zinazoukabili mpaka huo na kuuboresha.

  Mawaziri hao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleman Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe.

  Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na Mawaziri hao ni eneo la mpaka ya Tanzania na Uganda kwa upande unapo pita mto Kagera na eneo la kivuko cha mpaka wa Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula mkoani Kagera.

  Katika ziara hii Mawaziri hao wameweza kujionea hali halisi ya maisha ya wakazi wa mipakani na jinsi wanavyohusiana na wenzao wa nchi ya jirani ya Uganda ambapo wamekuwa wakishirikiana na kuishi kwa amani katika shughuli zao za kila siku.


  Aidha, ziara hii ni maandalizi ya Mkutano wa ujirani mwema kati ya Mawaziri wa serikali ya Uganda na Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 Julai 2017, Bukoba mkoani Kagera. 
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni Kanali Denice Mwila kuhusu changamoto za mpaka huo wngine ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleman Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba.
   Jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba 30.
    Ujumbe wa Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwa juu ya Jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba 30.
   Moja ya jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda ambalo Mawaziri wamefanya ziara ya kuliona. 


  0 0


  Mwenye picha katika kitambulisho hapo juu ni Bi. Loveness Herman (69), Mbelgiji mwenye asili ya Tanzania ambaye alifariki huko Liege, Ubelgiji tokea tarehe 18 Mei 2.

  Marehemu Loveness Herman kabla ya kuhamia Ubelgiji na kuchukuwa uraia wa nchi hiyo katika miaka ya 1980 alikuwa akiishi Dar es Salaam. Tokea alipohamia Ubelgiji, Marehemu alikuwa akiishi peke yake na hakuwahi kupata mtoto. 

  Kwa taarifa hii, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wake wa Brussels inawatafuta ndugu zake ili wape taarifa kamili za msiba huo

  Kwa maelezo zaidi piga simu katika namba hii +3226406500 au barua pepe brussels@nje.go.tz. 

  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, baada ya wananchi hao kusimamisha msafara wake alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
  Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
  Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimshangilia Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017. PICHA NA IKULU.

older | 1 | .... | 1828 | 1829 | (Page 1830) | 1831 | 1832 | .... | 3272 | newer