Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1826 | 1827 | (Page 1828) | 1829 | 1830 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya  Nishati na Madini,  Prof. James Mdoe, tarehe 25/7/2017, amefungua rasmi Mkutano wa Kimataifa wa 15 wa Kamati ya ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya uvunaji haramu wa madini katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika.
  Mkutano huo unaofanyika jijini Arusha kwa siku tatu umehudhuriwa na nchi wanachama 12 ambazo ni Tanzania, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda, Zambia, Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan  na Kenya.
  Akifungua mkutano huo, Prof Mdoe alisema kuwa baadhi ya masuala muhimu yatakayojadiliwa ni pamoja na matumizi ya hati moja ya usafirishaji madini, kuwianisha sheria za nchi wanachama ili kuwa na uwiano katika kudhibiti utoroshaji madini, pamoja na urasimishaji wa shughuli za wachimbaji wadogo.
  Masuala mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na uongezaji wa ushiriki wa wanawake katika shughuli za uchimbaji madini, uwazi na uwajibikaji katika tasnia ya uziduaji (EITI)  pamoja na uzuiaji wa watoto katika shughuli za uchimbaji madini.
  Pamoja na kujadili utekelezaji wa malengo  mbalimbali ya kamati hiyo na kupeana uzoefu wa shughuli za udhibiti wa uvunaji wa haramu wa madini katika nchi hizo, ICGLR itatoka na maazimio yanayopaswa kutekelezwa na nchi wanachama ili lengo la udhibiti wa uvunaji  haramu wa madini lifanikiwe.
   Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya  Nishati na Madini,  Prof. James Mdoe akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa 15 wa Kamati ya ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya uvunaji haramu wa madini katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika unaofanyika jijini Arusha.
   Baadhi ya Wajumbe  kutoka Tanzania, Sudan, Sudan Kusini na Rwanda waliohudhuria Mkutano wa Kimataifa wa 15 wa Kamati ya ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya uvunaji haramu wa madini katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika unaofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka na wa pili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, John Nayopa.
  Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya  Nishati na Madini,  Prof. James Mdoe (katikati,) akiwa na Wajumbe wa Mkutano wa Kimataifa wa 15 wa Kamati ya ICGLR ambayo inahusika na mapambano dhidi ya uvunaji haramu wa madini katika nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika.

  0 0

   Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem wa (pili kushoto) akikabidhi watendaji wa wilaya ya mkuranga mabeseni hamsini pamoja na vifaa vya akina mama wakati wa kujifungua katika hospital ya wilaya hiyo.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
   Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akizindua kisima  katika kijiji cha Mpafu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega.
   Picha ya pamoja
  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem wakionja maji baada ya kuzindua kisima  katika kijiji cha Mpafu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah ulega.

  0 0
  0 0

  Vijana wa Kitanzania wenye umri wa kuanzia miaka 14 hadi 17 wameshiriki katika michezo ya Mbio Fupi (800m) na ndefu (3000m) na pia kwenye kuogelea katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola (The Commonwealth of The Bahamas) yaliyoanza Julai 13-23, 2017 huko Bahamas, ambapo waliweza kutika hatua ya fainali na kufanya vizuri. Kijana wetu mmoja mwenye umri wa miaka 17 anayeitwa Francis Damiano Damas alishinda nafasi ya tatu kwenye fainali za mita 3000 na kuchukua medali ya shaba. Vijana hawa na wengine kama hao ni vyema wakaendelezwa ili waliwakilishe vyema Taifa letu na kuitangaza Tanzania kimataifa.
  Wa kwanza kutoka kushoto ni Colins (14 years), wa pili kutoka kushoto ni Fancis Damiano (17 years), wa katikati ni Kiongozi wa Msafara, wa kwanza kulia ni Selina Itatiro (14 years) na wa pili kulia ni Regina (15 years).

  0 0


  Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

  WAZIRI wa afya, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi, Dk. Mpola Tamambele, kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo ya serikali ya kuhakikisha mama mjamzito, mtoto chini ya miaka mitano na mzee wanapata huduma bure.

  Kutokana na kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Beda Mmbaga kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo mara moja wakati uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zikiendelea .

  Amemuelekeza Kaimu Mkurugenzi huyo pia kuwafuatilia watumishi wa afya kituoni hapo waliohusika kumuagiza mama aliyejifungua Salma Khalifan kwenda kununua vifaa vya kujifungulia vya sh.180,000 ili apate huduma .

  Aliyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi, kabla ya kukabidhiwa kwa magari ya wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo, Hamoud Jumaa.

  Waziri huyo alisema yeye hana mamlaka ya moja kwa moja kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo hivyo anaiachia mamlaka husika isimamie jukumu hilo. Alisema hatokubali kuona watumishi wachache kwenye vituo vya afya, zahanati na hospitali wanachezea maagizo ya serikali. Alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mama aliyejifungua ambae alisema amenunua vifaa vya kufanyiwa operesheni kwa gharama ya sh .180, 000.
  Ummy alisema haiwezekani kuona mama wajawazito, wanalipishwa hadi gloves na pamba ili kujifungua wakati serikali yao ilishasema watahudumiwa bure . Alieleza kwamba, kuanzia sasa waganga wakuu wa wilaya, mikoa na watumishi wa afya wote nchini wahakikishe wanatimiza maelekezo ya serikali kuhudumia akinamama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo vya uzazi . Ummy alisema kuwa ,watumishi na wauguzi wengi wanajituma na kufanya kazi zao kifanisi ila wapo wachache ambao wanakwamisha juhudi hizo .

  "Sitokubali mtumishi anakwenda kinyume na serikali ,rais wetu John Magufuli anasisimamia suala zima la kuboresha huduma za afya ,halafu akitokea mtu mmoja mzembe anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho "

  "Wananchi wamekuwa waoga hata kuingia katika suala la bima ya afya kwa sababu ya mambo kama haya ,namsimamisha mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika ." alisema Ummy .

  Mbali ya hayo Ummy alibainisha,bajeti ya dawa katika halmashauri ya  wilaya ya Kibaha imeongezeka ndani ya miaka miwili mfululizo kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya tano .
  Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akitembelea kituo cha afya Mlandizi katika ziara yake aliyoifanya jana. kushoto ni Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi, Dk. Mpola Tamambele, ambaye amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.

  Ummy alisema mwaka 2015/2016 bajeti ya madawa katika halmashauri hiyo ilikuwa mil.24 na 2017 ilifikia mil.70 na bajeti ya sasa 2017/2018 imefikia sh. mil.101 .

  Kwa upande wake mama aliyejifungua kituoni hapo ,Salma Khalfani ,alimweleza Ummy kwamba aliandikiwa orodha ya dawa za kununua kwenye maduka ya dawa ya nje .

  Alieleza ,alitakiwa kufanyiwa upasuaji na hivyo kutakiwa kununua madawa na vifaaa tiba ,pamba na gloves vya 180,000 akanunue ili aweze kujifungua .

  Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Mmbaga alisema maagizo aliyopewa na waziri ameyapokea na atayafanyia kazi .

  Nae mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaaa alisema kumekuwa na malalamiko mengi juu ya wananchi hasa akinamama kulipishwa fedha za dawa na vifaa tiba. Alisema baadhi ya wazee wamekuwa wakishindwa kupewa huduma za afya bila malipo. Jumaa alimuomba Ummy kuendelea kushirikiana nae kuwadhibiti watumishi wazembe wanaodidimiza haki za wananchi .

  0 0

  Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi),  George Simbachawene (kulia) akizungumza na wananchi baada ya kupokea malalamiko yao katika Kijiji cha Lukole kuhusu shida ya maji wanayoipata, wakati alipokwenda kwenye bomba la Kijiji kuzungumza na wakinamama ambao ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo na kuwataarifu namna ambavyo amekwishaanza kushughulikia kero hiyo.

  Na Nteghenjwa Hosseah - Kibakwe.

  Uharibifu wa vyanzo  vya maji ni tatizo lililokithiri katika maeneo mengi Nchini Tanzania huku wananchi wa maeneo hayo wakiendelea kushuhudia na kuvumilia uharibifu huo eti kwa sababu tu wahusika ni ndugu, jamaa ama  marafiki wa jamii husika.

  Pasipo kujali athari zinazoweza kutokea kutokana na uharibifu wa mazingira hususan vyanzo vya maji wananchi wameendelea kulima, kufuga, kuchunga  pamoja na kuishi katika maeneo hayo pasipo kuwa na shaka yoyote na kusababisha ukosefu wa maji kwa jamii inayotegemea vyanzo hivyo. 

  Athari zaidi zimethibitija katika Kijiji cha Chinyika na Lukole  vilovyopo kata ya Chinyika kwa kukosa maji kutokana na Uharibifu uliofanywa na baadhi wa wananchi katika chanzo cha maji kwenye milima ya wota ambacho ndio chanzo kikuu cha maji ya mtiririko kwa wananchi zaidi ya elfu saba.
  Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi),  George Simbachawene (katikati aliyekaa) akisimikwa kuwa Chifu wa Kigogo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kingiti.

  Hali hii imepelekea wananchi wa vijiji hivyo vyenye vitongoji zaidi ya kumi na tano kuwekeana zamu ya kuchota maji ambapo kwa wiki kila Kijiji hupata maji kwa siku tatu na kila kaya huchota Ndoo nne kwa siku ya zamu yao ambapo kiasi hicho hakiwajawahi kuwatosha mahitaji ya Kaya.

  Wananchi wa Kijiji cha Chinyika wamepaza sauti zao kwa Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi),  George Simbachawene wakati wa ziara yake katika vijiji hivyo na kulalamikia tatizo la upungufu wa maji na adha wanayopata kutokana na hali hiyo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Dismas Ten


  Na Agness Francis, Globu ya Jamii.


  Winga machachari wa timu ya Yanga Simon Msuva anatarajiwa kuondoka kuelel]kea nchini Morocco kwa ajili ya vipimo ili kujiunga na timu ya ya Difaa Hassani Eljadidi (DHJFC) inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.

  Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Yanga, Dismas Ten amesema kuwa mchezaji Saimon Msuva anatarajia kuondoka kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya zoezi la vipimo vya afya ili kukamilisha mchakato mzima wa usajili wa mchezaji huyo katika timu ya Difaa Hassani Eljadidi (DHJFC).

  Ten amesema kuwa, walishamaliza mazungumzo na klabu hiyo kwa ajili ya kujiunga nao na wamempa baraka zote kijana wao kwa ajili ya kuanza maisha mapya ya soka nchini Morocco.

  Timu hiyo iliyomaliza msimu uliopita huku ilishikilia nafasi ya pili katika nmsimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 59, huku WCA Casablanca wakiwa kilelelni kwa point 66 ligi kuu ya morocco, Ambayo inajumuisha timu 16 kama ilivyo ligi kuu ya Tanzania bara. 

  Hata hivyo uongozi wa yanga unasubiri majibu ya vipimo vya Msuva na kuendelea na taratibu zote za kuuzwa kwa mchezaji huyo ambaye ameitumikia club hiyo misimu 5 akiwa kiungo mshambuliaji mwenye jezi namba 27.

  Mapema mchana huu Msuva ameenda klabu ya Yanga kwa ajili ya kuaga na kupata baraka za viongozi wake waliokuwa nae katika maisha ya soka ndani ya Klabu ya Yanga kwa miaka mitano.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan  amezipongeza juhudi zinazofanywa na taasisi ya Merck ambayo ni kampuni inayoongoza katika sayansi na teknolojia  ambayo imelenga  kushughulikia masuala  uwezeshwaji wa wanawake na huduma za afya akisema kwamba wamekuja nchini  kwa wakati mwafaka, 
  Wakati wa mkutano maalum kati ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation  Makamu wa Rais  alisema kuwa Merck Foundation  inakaribishwa na serikali inatarajia kushirikiana  na taasisi hiyo  inayoheshimika na iliyo makani katika  kuwezesha wanwake , vijana, huduma za afya  na sayansi. 
  Tunatambua mchango  unaotolewa na Merck Foundation  katika kujengea uwezo  huduma za afya barani Afrika na tunakaribisha shughuli zake  nchini Tanzania, hususani katika kampeni zinazolenga  kuuongezea umma  uelewa kuhusu ugumba. 
  Makamu wa Rais aliongeza, “Mimi binafsi nitafanya kazi na Merck katika kuwawezesha wanawake walio na uwezo duni kijamii na kiuchumi kote nchini Tanzania  na sehemu nyingine duniani ili kujenga utamaduni mpya  katika kuheshimu na kumtambua wanawake  kama sehemu ya wanajamii wanaozalisha  wawe ni kinamama na hata wasio wazazi.” 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Ofisa Mkuu Mtendaji wa Merck Foundation, Dk Rasha Kelej,  ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ofisa Mkuu Mtendaji wa Merck Foundation, Dk Rasha Kelej,  ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam.

  0 0

  Kijana Francis Damiano Damas (17)  ametwaa medaili ya shaba katika mbio za mita 3000  kwenye  mashindano ya sita  vijana kutoka  nchi za Jumuiya ya Madola yaliyomalizika mwishoni mwa juma jijini  Nassau nchini Bahamas. Picha ya juu inamuonesha Kijana Francis Damiano Damas akiwa na wenzake Collins (kushoto) Kiongozi wa msafara Mwinga Mwanjala (katikati), kulia ni Celina Itatiro (14) na wa pili kulia ni Regina (15)
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu wa Polisi, Zelote Stephen ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wale wote watakaosababisha kuibuka kwa hoja za ukaguzi wa Hesabu za serikali katika Halmashauri zao. Aliyasema hayo alipohudhuria kwenye baraza maalum la madiwani la kujadili na kujibu hoja 147 za mkaguzi wa hesabu za serikali nchini kwa mwaka wa fedha 2015/2016 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

  Akinukuu barua ya maagizo aliyoyatoa tarehe 4/5/2017 Mkuu wa Mkoa alisema kuwa kila mamlaka ya nidhamu ichukue hatua za kinidhanmu kwa mujibu wa sharia kwa watumishi ambao wamesababisha hoja za ukaguzi kwa uzembe au kwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo na taarifa juu ya hatua hizo apelekewe.
  “Kwenye hoja zilizojibiwa ningependa sana hoja ziwe na data zinazoeleweka na za uhakika, na kuacha kitu kinachoitwa tunaendelea kuishughuilikia, iseme tumefikia wapi, sio tunaendelea, Hakuna kinachoendelea, lazima kupiga hatua kuondoka kwenye hoja hiyo, nimesikia kuwa kuna watu wamechukuliwa hatua lakini sijaziona,” Mh. Zelote alibainisha.

  Aidha alibainisha kuwa wapo watu waliofanya madudu na wanapaswa kuchukuliwa hatua na kutowaachia kwani kufanya hivyo hakutasaidia kufutika kwa hoja na kusisitiza kuwa waliosababisha hoja watafutwe popote walipo ili warudi kujibu hoja walizoziibua.

  Hata hivyo, Mh. Zelote ameusifu uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa kuweka misingi imara iliyowapelekea kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2015/2016 na kuwaasa kumtumia mkaguzi mkaazi wa mkoa pamoja na wakaguzi wa ndani kutoka ofisi yake ili kuzuia hoja zisitokee.

  “Ni halmashauri pekee katika Mkoa huu ambayo imepata hati safi, kwa hilo niwapongeze sana, angalau mmenitoa kimasomaso, sijui ingekuwaje kama ingekuwa ni zote zimepata hati yenye mashaka,” Alisema.
  Na kuagiza kuwa hoja zote zilizo ndani ya uwezo wa mkoa zisijitokeze tena kwakuwa halmashauri zote zina mfumo unaojumuisha kanuni, sharia na taratibu lazima mambo hayo yasimamiwe kikamilifu.

  Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mh. Zeno Mwanakulya alisema kuwa lengo la halmashauri ni kuhakikisha kuwa hoja hizo zinafutika na hazijirudii.

  “Lengo la Halmashauri ni kuhakikisha kwamba tunazifuta hoja zote, ndio lengo letu kubwa kwahiyo wakati tunachangia lazima tujiulize kwanini hoja hizi zimejitokeza, Je, zilikuwa na sababu ya kutokea, basi ni vizuri kama wawakilishi wa wananchi tuweke msisitizo hoja hizo zifutwe” Alisema.

  Na pia aliahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ili kuhakikisha kuwa Halmashauri hiyo inaendelea kupata hati safi.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda alibainisha kuwa hoja zinasababishwa na uzembe wa watumishi katika kutekeleza majukumu yao na kukumbusha kuwa mwaka wa fedha 2014/2015 kulikuwa na hoja 80 ukilinganisha na mwaka wa fedha 2015/2016 wenye hoja 147.

  “Kila mtu katika eneo lake akiwajibika hakutakuwa na hoja kwasababu Hakuna hoja isiyo na majibu, wakaguzi wanachotaka ni majibu, ukishawaridhisha kwa kuweka kumbukumbu zako vizuri, hoja haiwezi kujitokeza,” alimalizia.

  0 0

  The delegates from Cyberspace Administration of China government were visiting Star Media (T) Ltd Headquarters in Tanzania earlier yestoday and showed some concern as one of the well-organized companies which has established its branches and employed a lot of local people.

  During the visit, Star Media (T) Ltd Vice President Mr. Carter Luo welcoming the team of delegation where they get short introduction on of Star Media (T) Ltd Tanzania and how it operates in the country as it transforms many Tanzanian family from analog to digital life.

  After the visit the delegation Team include CCTV, Xinhua agency and people’s Daily Online congratulate star times for welcoming the team to visit and its way showing good work cooperation between Tanzanian staff and Chinese.
  Director General of cyberspace Administration of china, Zhen Cheng (Left) together with StarMedia Vice President Mr. Carter Luo (Right) after visiting startimes TBC shop.  

  The main purpose is to motivate development in Media through creativity, research and development of Media Industry in Tanzania and China and how they can cooperate together to achieve this.

  “Mr. Zhen Director General of Cyberspace administration said that “The cooperation between Chinese and Tanzania is well established since many years ago. China is willing to deeper cooperation in training promoting, and developing local staff who will be working in different field”.
  StarMedia Vice President Mr. Carter Luo shows The cyberspace Administration of china delegation team around satellite transmission dishes. 

  He noted that the great effort done by Star Media (T) Ltd Tanzania in digital migration is well appreciated and provided an opportunity for Tanzanian people to develop and share their experiences about the expansion of digital technology as well as planning for the future.


  0 0


  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.  Aggrey Mwanri amezindua rasmi kambi maalum ya huduma za Afya juu ya upimaji wa Afya bure kwa wananchi mbalimbali Wilayani Nzega, ndani ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanri ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwapongeza waandaaji wa kambi hiyo kwani itasaidia kuboresha afya za wananchi ili kuwa na afya njema.

  “Wananchi wanahitaji Afya njema, tunapongeza kwa kambi hii kwani madaktari bingwa waliokuja hapa watatua matatizo ya msingi kwenye afya zetu. Hivyo wananchi mujitokeze kwa wingi” aleleza RC Mwanri. Aidha, Mh. Mwanri amewapongeza  Madaktari bingwa kutoka China ambao wanaendesha kambi hiyo ya siku Sita, iliyoanza rasmi Julai 24 na inatarajia kumalizika Julai 30.
  Hata hivyo, Mh. Mwanri aliwaagiza Wakurugenzi wote wa Mkoa wa Tabora waupokee mpango huo wa kambi za huduma za Afya ili uende mkoa mzima kwani wanakosa fursa ya kuonana na Madaktari bingwa.

  “Ni jambo zuri, tunaomba Wakurugenzi wote mulipokee suala ili wa Mkoa wa Tabora ili liendelee Mkoa mzima. Pia ni wasaha kwa wananchi wote kupeana taarifa ili zienee kwa watu wote wajitokeze hapa Nzega kupatiwa huduma za upimaji na matibabu.” 
  Alieleza Mh. Mwanri huku akimuagiza Mganga Mkuu ahakikishe anaratibu mpango huo uenee Mkoa nzima wa Tabora.

  Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini ameshukuru Serikali ya China kwa kufanikisha tukio hilo ikiwemo kutoa dawa za Maralia kwani kwa msingi huo utasaidia kuokoa maisha ya wananchi wa Nzega.
  “Tunapokea kwa mikono miwili msaada huu wa kutoka Serikali ya China hasa kupitia kwa Balozi wake hapa nchini Tanzania. Dawa hizi ni nyingi nahakika zitasaidia wananchi wote kuanzia wilaya ya Nzega na Mkoa nzima wa Tabora kwa ujumla. Nawashukuru sana wananchi wanaojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuja kupata  huduma za matibabu kwenye kambi hii ya madaktari bingwa hapa Nzega” alieleza Dak. Kigwangalla.

  Zoezi hilo la Upimajj wa Afya Bure Wilayani Nzega, limeandaliwa na Wabunge wa majimbo yote ya  Nzega ambapo imeanza kuanzia hiyo Julai 24 na itatarajiakumalizika Julai 30, huku kwa wakazi wote wa Nzega na jirani wata pima afya zao bure na kupata huduma za matibabu bure, ikiwemo upasuaji. Tayari timu ya Madaktari bingwa wa kila fani ya tiba wapo kwenye kambi hiyo inayoendelea kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nzega.

  0 0

  Spika wa Bunge la Tanzania, Mh. Job Ndugai akisalimiana na Kaimu Rais wa Nigeria, Mh. Prof. Yemi Osinbajo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 18 wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika unaofanyika Mjini Abuja nchini Nigeria.
  Spika wa Bunge la Tanzania, Mh. Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Bunge la Nigeria, Mhe Alhaji Yakubu Dogara wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 18 wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika unaofanyika Abuja nchini humo.

  0 0

  The united Republic of Tanzania is supporting the initiatives taken by the Amir of Kuwait HH Sheikh Sabah Al-Jaber Al-Sabah’s mediation efforts to address the Gulf crisis and the exploration of possible solution methods.

  The diplomatic crisis began in June 5th 2017 when Saudi Arabia, United Arab Emirates, Bahrain, and Egypt abruptly cut off diplomatic relations with Qatar by withdrawing ambassadors and imposing trade and travel bans.

  Tanzania call for unity and stability of the Gulf region and it emphasis that a solution should be found within the framework of the Gulf Cooperation Council and in that regards, it joins and support the initiative of the State of Kuwait that called for the crisis to be resolved through peaceful negotiations.

  We therefore, appeal to the Gulf Nations to quickly resolve their disputes in peaceful and diplomatic manner. 

  Issued by Government Communication Unit, Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

  26 July, 2017

  0 0

  Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.

  Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeupa muda wa siku tano kuwasilisha pingamizi la awali dhidi ya maombi ya dhamana ya kesi ya  uhujumu uchumi inayomkabili  Mfanyabiashara Yusufali Maji (41) na wenzake watatu.

  Manji na wenzake, pia wanakabiliwa na  kukutwa na vitambaa vya sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)  isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.

  Hata hivyo, mfanyabiashara huyo amefungua maombi yaliyosajiliwa kwa namba 122/2017, kupinga hati iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuzuia dhamana dhidi yake na yalitajwa jana mbele ya Jaji Isaya Arufani.

  Upande wa mashtaka ukiongozwa na Paul Kadushi, Simon Wankyo na Tulumanywa Majigo, ulidai mahakamani kwamba wanaomba muda kwa sababu wana nia ya kuwasilisha pingamizi la kupinga maombi ya utetezi.

  Pia, ulidai kuwa wanaomba mahakama iwape muda wa kuwasilisha majibu ya hati ya maombi ya mshtakiwa.

  Jaji Arufani alisema upande wa Jamhuri uwasilishe majibu na pingamizi lao Agosti Mosi na upande wa utetezi kama watakuwa na majibu ya nyongeza wawasilishe Agosti 2 na mahakama hiyo itasikiliza maombi hayo Agosti 4, mwaka huu.
  Katika maombi hayo,  Manji anaiomba Mahakama Kuu kutengua hati ya DPP ya kuzuia dhamana yake  iliyowasilishwa Julai 5, mwaka huu aliposomewa mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwamo kukutwa na sare hizo.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki katika kumfariji kipindi cha msiba wa mke wake mpendwa Bi. Linah George Mwakyembe.

  Napenda kutumia fursa hii kwanza kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa neema na baraka zake na pili kutoa shukrani zangu za dhati kwa Watanzania wote kwa upendo na ushirikiano mkubwa mlionipa mimi na familia yangu katika kuomboleza kifo cha mke wangu mpendwa Bi.Linah Widmel-George Mwakyembe na baadaye katika mazishi yake wilayani Kyela.

  Familia inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli; Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan; Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kwa mchango wao mkubwa katika kumuuguza marehemu wakati wa uhai wake.

  Aidha, familia inawashukuru viongozi hao waandamizi wa nchi pamoja na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson Mwansasu, wake wa viongozi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, viongozi wetu wa nchi wastaafu, Wabunge, Majaji, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Maaskofu wa Kanisa la Kiluteri, Makanisa ya Moravian na makanisa ya kiroho (Mito ya Baraka, Living Water, Evangelical Brotherhood nk) kwa ushirikiano wao katika maombolezi na mazishi ya marehemu.

  Wana-familia tutakumbuka daima moyo adhimu wa upendo na ushirikiano tulioupata toka kwa Katibu wa Bunge na maafisa wake, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na timu yake mzima ya Wizara, Makatibu Wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, watendaji wakuu wa taasisi, asasi na kampuni mbalimbali, na wananchi wote kwa ujumla katika kipindi hicho kigumu.

  Pia napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru Wana-Kyela wote kwa uvumilivu waliouonesha kipindi chote cha kumuuguza marehemu na ushirikiano wao wa dhati katika mazishi yake.

  Mwisho lakini si kwa umuhimu, nawashukuru sana madaktari na wauguzi waliomhudumia marehemu kwa kujituma, kwa weledi na ustahimilivu wao ili kuokoa maisha yake lakini Mungu akampenda zaidi. Vilevile wamiliki wa vyombo vya habari, waandishi na watangazaji kwa kukesha nasi kipindi chote cha msiba Dar es

  Salaam na Kyela wakitekeleza wajibu wao wa kitaaluma na vilevile kutufariji wafiwa kwa hali na mali.

  Nawaomba wote mpokee shukrani zangu za dhati na Mwenyezi Mungu awabariki kwa moyo wa ushirikiano na upendo mliouonyesha kwetu.

  Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe.

  Dkt. Harrison George Mwakyembe (Mb),
  WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO,
  26/07/2017.

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri katika jiji la Dar es Salaam ndani ya siku 20 kusiwepo nyumba za wageni pamoja na kumbi za starehe katika maeneo yanayozunguka shule.

  Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na wakuu wa shule za sekondari na Msingi uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam. ambapo amesema kuwa  shule ni kwa ajili ya kutoa elimu hivyo kuwepo kwa vitu hivyo vinafanya kuhalibu na kuwahadaa wanafunzi.

  Amesema kuwa maeneo yote ya shule yapimwe ili kusiwepo kwa mazingira ya kuweza watu kufanya kujenga maeneo hayo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na maafisa elimu, waalimu wakuu shule za sekondari na msingi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akizungumza na katika Mkutano wa Walimu Wakuu Shule za Sekondari na Msingi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Shule Kisarawe 11, Elieshi Emmanuel akizungumza katika Mkutano wa Wakuu wa Shule juu.
  Mkutano ukiendelea.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

older | 1 | .... | 1826 | 1827 | (Page 1828) | 1829 | 1830 | .... | 3270 | newer