Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1824 | 1825 | (Page 1826) | 1827 | 1828 | .... | 3283 | newer

  0 0


   courtesy of The African Perspective Magazine

  0 0
  0 0

   Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart inatarajia kupiga mnada jengo la Abla Complex lenye urefu wa ghorofa saba lililopo Mikocheni Dar es Salaam kutokana na mmiliki wake kushindwa kulipa mkopo anaodaiwa na KCB Bank Limited.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bi. Scholastica Kevela, Yono wataendesha Mnada huo August 12, 2017 hapo hapo mjengoni, na amekaribisha yeyote mwenye nia ya kununua jengo afike kwenye mnada huo kuanzia saa nne na nusu asubuhi (From 10.30 am).

   


  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  Mwege wa uhuru kitaifa umeanza kutimua vumbi mkoani Kigoma kwa kuibua miradi lukuki iliyojengwa chini ya kiwango katika halmashauri ya wilaya ya uvinza huku kukiwa na hofu ya ufujaji wa fedha za umma katika utekelezaji wa miradi hiyo.

  Kufuatia hali hiyo Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017 Amour Amour amekataa kuweka mawe ya msingi katika miradi hiyo mitano, inayohusisha ujezi wa nyumba za walimu vyumba vya madarasa na ofisi mbalimbali na kuagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo.

  Aidha Kiongozi huyo ametoa muda wa siku tatu kwa muhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza na mkandarasi aliyejenga mradi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Nguruka iliyopo katika kata ya nguruka kurekebisha baadhi ya kasoro zilizobainika katika mradi huo kwa kutumia fedha zao .

  Maagizo hayo aliyatoa jana mara baada ya kuanza kukagua na Kuzindua Miradi sita ya halmashauri hiyo katika Shule ya Sekondari Nguruka, ambapo katika mradi wa Nyumba za shule hiyo walibaini kuwepo na nyufa katika majengo hayo na matumizi yafedha nyingi katika kukamilika kwa Mradi huo na kumuagiza mkurugenzi kuwasimamia muhandisi wa halmashauri na Mkandarasi wa mradi kufanya marekebisho ndani ya siku tatu na kupelekewa taarifa ya marekebisho hayo.

  Hata hivyo Kiongozi huyo aliahirisha zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya kijiji cha Malagalasi kata ya Nguluka Wilayani uvinza mkoani kigoma kufuatia jengo hilo kujengwa chini ya kiwango.

  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mrindoko.  0 0

  MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, jana amekabidhiwa fedha zake alizoshinda kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko, jumla ya Sh Milioni 20.

  Makabidhiano hayo yamefanyika jana mkoani Mtwara katika benki ya NMB, ambapo Lukinga aliishukuru Biko na kusema kuwa fedha hizo atazitumia vizuri kuhakikisha zinakuza uchumi wake.“Nashukuru kwa kukabidhiwa fedha hizi ambazo kwa hakika nitazitumia vizuri kama sehemu ya kupiga hatua kiuchumi kama dhamira ya Biko kuanzisha bahati nasibu yao.

  “Awali sikuamini kama naweza kushinda donge nono la Sh Milioni 20, hivyo ni wakati huu Watanzania wote kuamini kwamba Biko ni mchezo wa kubahatisha wa watu wote, maana kama hata mimi wa Mtwara nashinda, ndio kusema yoyote anaweza kushinda,” Alisema.


  Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles, alimpongeza Lukinga kwa kukabidhiwa fedha zake, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa ya Biko ili washinde zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kila wakati, sambamba na droo kubwa ya Sh Milioni 20 inayotoka Jumatano na Jumapili.


  “Jumapili hii amepata Lukinga ambapo leo tumemkabidhi fedha zake, hivyo wote mnaweza kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ya kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea kikiwa Sh 1,000 na kuendelea,” Alisema.


  Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven mwenye fulana ya Biko kushoto akiwa ameshika hundi saa chache kabla ya kumkabidhi kiasi cha fedha cha Sh Milioni 20 mshindi wa Mtwara, Ally Hassan Lukinga katikati. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.


  Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko Tanzania, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia, akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa mjini Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyeshinda katika droo ya 24 Jumapili. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Robert Hokororo

  Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango halmashauri ya wilaya ya Kishapu imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata za Lagana, Itilima na Talaga. Katika ziara hiyo wajumbe hao pamoja na wataalamu kutoka halmashauri walitembelea maendeleo ya ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Mwadulu iliyopo kata ya Lagana.

  Wakiwa eneo hilo wajumbe hao kupitia kwa mwenyekiti wa halmashauri, Boniphace Butondo walipongeza juhudi za uongozi wa shule hiyo kwa ubunifu na kutumia vizuri fedha za Serikali.

  Butondo aliwataka wanakamati ya shule kuendelea kuupa ushirikiano uongozi wa shule hiyo ili waendelee kushughulikia shughuli za maendeleo kupitia mpango wa elimu bure. Kamati hiyo iliweza pia kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Lagana ambayo inajengwa kwa nguvu ya wananchi ambapo walihimiza waendelee kuchangia.

  Ziara hiyo pia ijumuisha kata ya Itilima ambapo wajumbe na wataalamu hao walikagua ujenzi wa vyumba viwili vya darasa shule ya msingi Ipililo pamoja na kata ya Talaga ukarabati wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Nhobola.

  Waliridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi huo ambapo walimpongeza afisa elimu ufundi, Moshi Balele kwa kufuatilia kwa ukaribu shughuli zote zinazoendelea.

  Hiyo ni mojawapo ya ziara za kukagua miradi ya maendeleo zinazofanywa na kamati mbalimbali za Baraza la Madiwani katika halmashauri hiyo kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akiongozana na mchumi kutoka halmashauri hiyo, Veronica Massawe katika kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akiwaelekeza jambo mafundi waliokutwa na kamati wakiendelea na shughuli ya kusakafia mojawapo ya vyumba vya madarasa.
  Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Ungozi na Mipango wakikagua mradi wa ujenzi wa mojawapo ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Lagana wakati wa ziara hiyo.
  Ofisa elimu ufundi, Moshi Balele akiwaelekeza wajumbe wa kamati namna ujenzi wa chumba cha darasa unavyoendelea katika shule ya msingi Ipililo.
  Chumba cha darasa katika shule ya msingi Mwamadulu ata ya Lagana kikiwa katika hatua mwisho wa ujenzi wake.

  0 0


  Mashindano ya Mbio za Baiskeli katika Mikoa mitano ya Kanda ya ziwa yanataraji kufanyika AGOSTI 6, 2017 katika Viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu. Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya uzalishaji wa Vinywaji Baridi ya JAMBO FOOD PRODUCT kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.


  Mashindano hayo yatahusisha Umbali wa Kilomita 200 kwa Wanaume, Kilomita 80 kwa Wanawake na Kilomita 5 kwa watu wenye Ulemavu. Pia kutakuwa na Burudani Mbalimbali Kutoka kwa WAGIKA na WAGARO na Ngoma nyingine nyingi za Asili zitatolewa siku hiyo. Zawadi Mbalimbali zitatolewa kwa washiriki ikiwemo Pikipiki na fedha Taslimu zaidi ya Shilingi Milioni nane.

  Fomu za Ushiriki wa SIMIYU JAMBO FESTIVAL 2017 zinapatikana katika Ofisi za Maafisa Michezo katika Halmashauri za Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Mara na Geita kwa Gharama ya Shilingi 5000 tu.

  Mgeni rasmi Katika Mashindano hayo ya mbio za Baiskeli ya SIMIYU JAMBO FESTIVAL 2017 atakuwa ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Tulia Ackson Tulia.

  Mkoa wa Simiyu, Wilaya Moja Bidhaa Moja

  HAKUNA KIINGILIO KATIKA MASHINDANO HAYO, NYOTE MNAKARIBISHWA

  0 0

   MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Christopher Kilungu katikati akikagua mazingira ya Shule ya msingi Litola ikiwa ni pamoja na ujenzi mpya wa matundu 12 ya vyoo vya wanafunzi wa shule hiyo. Picha na Yeremias Ngerangera


  0 0

  Na Thobias Robert-Maelezo
  Sekta ya utalii nchini imeendelea kukuza na kuongeza mapato ya serikali kwa kuchangia zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa, huku ikitazamiwa kuongezeka katika mwaka huu wa fedha. 

  Hayo yalisemwa Jana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) Bwana Allan Kijazi wakati akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA” kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1).

  “Utalii unatoa mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi hii, kwa sasa hivi unakisiwa kwamba unachangia kama asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya fedha ya kigeni,” alisema Bw. Kijazi. huku akisisitiza kuwa TANAPA watazidi kulinda na kuendeleza hifadhi zilizopo nchini ili zizidi kuongeza pato la taifa kwa maendeleo ya watanzania wote.

  Mkurugenzi huyo wa TANAPA alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 TANAPA ilichangia kiasi cha billion 27 kwenda Mfuko wa Taifa wa serikali na matarajio yao katika kuchangia mfuko wa fedha wa Taifa kwa mwaka huu  wa fedha 2017/2018 ni bilioni 33.4 hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa Watalii kutoka nje ya nchi. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0  0 0


  0 0


   Balozi wa Kiswahili Afrika Mama Salma Kikwete akiongea wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili nchini Kenya katika Jengo la Kenya Institute of Curriculum Development, Nairobi, Kenya ambapo ameahidi kuitumia kwa manufaa ya Tanzania, Kenya, Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Afrika na Duniani kwa Ujumla.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili nchini Kenya katika Jengo la Kenya Institute of Curriculum Development, Nairobi, Kenya.
  Balozi wa Kiswahili Afrika Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania, Kenya, Dkt. Pindi Chana (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) wakati wa uzinduzi wa Kamusi Rasmi ya Kiswahili leo nchini Kenya.

  0 0

  KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza amekanusha madai yanayoenezwa juu ya kutokulipwa wananchi 1228 wa eneo la Katosho katika Manispaa hiyo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bandari kavu ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 12 zimetengwa kwa ajili ya gharama za fidia. 
  Hayo ameyazungumza jana Jijini Tanga alipokuwepo kwenye kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao.
  Aidha alisema jumla ya hekari 158 ndizo zilizochukuliwa na mamlaka ya bandari(TPA) kwa ajili ya mradi huo huku wananchi 1196 kati 1228 tayari wamekwisha lipwa fedha zao kama semehemu ya fidia za ardhi,mazao na makazi jambo ambalo limefanyika kwa mujibu wa kisheria na ushirikishwaji wa pande zote. 
  Mchindiuza alizidi kufafanua kuwa kutokana na hatua hiyo wananchi 32 kati yao walishindwa kulipwa fidia zao kutokana na kushindwa kuwakilisha akaunti zao katika Halmashauri ya manispaa ya Mji wa Ujiji jambo ambalo linapotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari. 
  “Yapo malalamiko mengi ya utaratibu wa ulipwaji wa fidia hizo kwa wananchi walioko katika maeneo ya ya maradi lakini labda niseme kitu tayari tumekwisha walipa wananchi 1196 kati 1228 na waliobakia ni 32 tu na fedha zao zipo wapeleke akauti zao tuweze kuwalipa”Alisema.

  KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika  kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao. Kushoto ni Maneja wa Mawasilino TPA Janeth Ruzangi.
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi, Arusha
  Jeshi la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kupunguza makosa ya jinai kwa mwaka huu 2017 toka 1,378 yaliyoripotiwa mwaka jana 2016 hadi kufikia 1,041 na kufanya idadi ya makosa yaliyopungua  kufikia 337. 
  Akitoa takwimu hizo ofisini kwake  jana mchana, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo (pichani), alisema kwamba punguzo hilo ni sawa na asilimia 24.4 huku akifafanua kwamba takwimu hizo ni kwa mujibu wa kuanzia mwezi  Januari hadi Juni mwaka huu 2017.
  “Huu upungufu wa makosa ya jinai ni takwimu za nusu mwaka, toka Januari hadi Juni mwaka huu 2017 ikilinganishwa na mwaka 2016 kwa muda kama huo, hivyo utaona tumejitahidi “. Alifafanua Kamanda Mkumbo, huku akiendelea kubainisha.
  “Mwaka jana kwa nusu mwaka makosa ya mauaji yalikuwa 45 lakini mwaka huu kwa kipindi kama hicho makosa yalikuwa 36 pungufu ya makosa 9, wakati makosa ya kubaka yalikuwa 106 kwa mwaka jana lakini mwaka huu yameshuka hadi kufikia makosa 79 pungufu ya makosa 27, huku makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha mwaka jana yalikuwa makosa 16 na mwaka huu kwa kipindi kama hicho yamekuwa makosa matatu sawa na upungufu wa makosa 13”. Alisema Kamanda Mkumbo.

  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma

  Kufuatia Kongamano kubwa la Uwekezaji linalotarajiwa kufanyika nchini Uingereza, mwezi Septemba mwaka huu, Balozi wa Tanzania nchini humo, Dkt. Asha-Rose Migiro amekutana na wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na kujadili fursa za uwekezaji nchini katika sekta husika.

  Katika kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Julai 24 mwaka huu, Balozi Migiro, alisema kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza umejipanga kulitumia vema kongamano hilo ambapo watanadi fursa za uwekezaji katika sekta zote muhimu nchini, zikiwemo za nishati na madini.

  “Ni kwa sababu hiyo, nimeona nifike hapa ili nikutane nanyi, tujadili kuhusu fursa za uwekezaji hapa nchini katika sekta za nishati na madini ili tuweze kuzinadi wakati wa kongamano hilo,” alisema Balozi Migiro.

  Akifungua majadiliano baina ya wataalam hao na Balozi Migiro, Naibu Katibu Mkuu Pallangyo, alibainisha kuwa zipo fursa nyingi za uwekezaji hapa nchini, katika sekta za nishati na madini na kupongeza hatua ya Balozi Migiro kudhamiria kuzinadi fursa hizo kwa wawekezaji nchini Uingereza.

  Aidha, kwa upande wa sekta ya nishati, Dkt. Pallangyo alimwomba Balozi Migiro kupeleka maombi kwa Serikali za Uingereza na Ireland kusaidia miradi ya usambazaji umeme vijijini inayoendelea nchini kote.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akiwa katika kikao na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro (kushoto), Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma Julai 24, 2017. Wengine pichani ni wataalam wa Wizara na Taasisi zake walioshiriki kikao hicho.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati), akiongoza kikao cha wataalam wa Wizara pamoja na Taasisi zake na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha Rose Migiro (kushoto kwa Naibu Katibu Mkuu.)

   Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha Rose Migiro (mwenye Koti la Pinki) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia kwa Balozi), wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Wizara pamoja na Taasisi zake, Makao Makuu ya Wizara, mjini Dodoma.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia), akimkabidhi Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro, Kitabu cha Mpango Kabambe wa Uendelezaji Sekta Ndogo ya Umeme (Power System Master Plan). Wanaoshuhudia ni wataalam wa Wizara pamoja na Taasisi zake.

   
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto), akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro (kulia), baada ya kikao baina yao Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Julai 24 mwaka huu.
  Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA  0 0


  0 0
  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 1824 | 1825 | (Page 1826) | 1827 | 1828 | .... | 3283 | newer