Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1823 | 1824 | (Page 1825) | 1826 | 1827 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na: Paschal Dotto - MAELEZO.

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kenya zimefanya mazungumzo ya pamoja na kutatua  vikwazo vilivyokuwa vikiikabili  sekta ya biashara baina ya nchi hizo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga ametoa taarifa juu ya kumalizika kwa tofauti za kibiashara baina ya nchi hizo. 

   “Bidhaa za Tanzania zilizowekewa vikwazo na nchi ya Kenya ni unga wa ngano pamoja na  gesi ya kupikia (LPG). Aidha juhudi, za Serikali ya Tanzania kuona vikwazo hivyo vinaondolewa na Serikali ya Kenya kwa wakati hazikuzaa matunda, hivyo Serikali ya Tanzania nayo iliweka vikwazo kwa bidhaa za maziwa na sigara kutoka Kenya kuingia katika soko la Tanzania,” amefafanua Dkt. Mahiga.

  Amesema kuwa kutokana na mahusiano mazuri ya udugu yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya na  kwa kujali manufaa mapana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli walikubaliana kuzungumza na kutoa vikwazo vya biashara hizo. 

  Aidha, Dkt. Mahiga amesema, nchi hizo zimekubaliana kuunda Tume ya pamoja ambayo itakuwa na jukumu la kuepusha tofauti za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kutolea ufumbuzi changamoto za kibiashara kati ya nchi hizo mbili pindi zinapojitokeza.

  Tume hiyo itaongozwa na Mawaziri wa mambo ya Nje wa Tanzania na Kenya na kujumuisha mawaziri wanaohusika na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Biashara, Fedha, Mambo ya Ndani ya Nchi, Kilimo, Uchukuzi na Utalii wa nchi hizo. 
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo na kushoto ni Kaimu Balozi wa Kenya nchini Tanzania Peter Sang.
   Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

  Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (hayupo pichani) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya  Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. Kulia ni mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Songwe, Erasto Zambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
   Baadhi ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao  katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya  Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea silaha za jadi kutoka kwa Chifu  Muleshwelwa Mzunda wa Mbozi ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chief wa Songwe Julai 24, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe . Kushoto kwake ni mkewe Mary na watatu kulia  ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto kwake) wakiagana na viongozi wa Mkoa wa Songwe kabla ya kuondoka kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa huo kwenda kwenye uwanja wa ndege wa Songwae baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani humo Julai 24, 2017. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanyara wilayani Mbozi ambao walikusanyika barabarani wakitaka asimame na kuzungumza nao . Alikuwa akitoka Vwawa kwenda Uwanja wa Ndege wa Songwe Julai 24, 2017.

  0 0

  Harakati za ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung uliopo Mpirani Kikwajuni Mjini Zanzibar zinaendelea karibu Miezi Miwili sasa chini ya Wahandisi wa Kampuni ya Kimataifa ya Zhengtai Group ya Jamuhuri ya Watu wa China.


  Ujenzi huo unafuatia msada mkubwa ulioidhinishwa na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa Serikali ya Zanzibar katika azma ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa pande hizo mbili ukizingatia heshima uliopewa Uwanja huo wa kuitwa jina la Muasisiwa Taifa la China Hayati Mao Tse Tung.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kutembelea Uwanja huo kujionea harakati za ujenzi huo kazi ambayo inaonyesha mafanikio mazuri.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea harakati za ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung uliopo Mpirani Kikwajuni Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Hbari, Utamaduni, Utalii na Michezo Rashid Ali Juma.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Omar Hassan Omar akimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani ramani ya Uwanja wa Mao Tse Tung utakavyokuwa baada ya kukamilika kwake.
  Balozi Seif katika picha ya pamoja na Uongozi wa ngzi ya juu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo pamoja na wahandisi wa nujenzi wa uwanja wa michezo wa Mao Tse Tung.


  Balozi Seif akiagana na Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika masuala ya Utamaduni Chimbeni Kheir baada ya kuangalia harakati za ujenzi wa uwanja wa michezo wa Mao hapo Mpirani Kikwajuni Mjini Zanzibar.  Picha na – OMPR – ZNZ.  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe 
  amewapokea Mabilionea 26 wa taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika Hifadhi ya Taifa  Serengeti kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.

  Mabilionea hao ambao wanatoka katika mabara yote duniani wapo nchini Tanzania kama sehemu ya ziara yao katika nchi 8 duniani ikiwemo Uingereza, Rwanda, Maldives, Nepal, Bhutan na Rajastan.

  Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake,  Prof. Maghembe aliwakaribisha Tanzania na kwenye Maajabu ya Dunia yanayobebwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Alisisitiza "hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivores) na wale wanaokula nyama (canivores) kama Serengeti". 

  Prof. Maghembe aliwaeleza Wageni wake kuwa kuhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia. Hivyo akawaomba wageni hao wawe mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo lenye  amani na vivutio vyenye ubora wa pekee. Hatua hiyo italeta watalii wengi na kuiongezea Tanzania mapato.

  Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokua kwa wastani wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.

  (SOURCE: WWW.WIZARAYAMALIASILINAUTALII.BLOGSPOT.COM).
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea 26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini Tanzania.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi (katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi.
  Kiongozi wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
  Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakimsikiliza Waziri Maghembe.

  0 0

    Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Kikosi cha Yanga kimeendelea tena na mazoezi mapema leo baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili kutoka kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo  Mzambia George Lwandamina.

  Yanga waliokuwa wanafanya mazoezi ya Gym kwa takribani wiki  moja na nusu ikiwa ni katika programu ya Mwalimu Lwandamina ya kuwaweka fit wachezaji hao baada ya kuwa mapumzikoni kwa kipindi kirefu.

  Leo mapema asubuhi kikosi hicho kiliingia katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017/18 huku wakitarajiwa kuwa mechi kadhaa za kirafiki.

  Mechi ya kwanza ya kirafiki itakuwa ni Agosti 5 dhidi ya timu ya Singida inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo Mholanzi Hans Van De Pluijm mchezo utakapigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
   

  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi Amis Tambwe akiwa katikati akipambana na wachezaji wa Yanga katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
   Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul akiwa amemiliki mpira akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake  katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
   Wachezaji wa Yanga wakiwa katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
  Kocha George Lwandamina akijadiliana jambo na Beki kisiki Kelvin Yondani katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.


  0 0

  Visiwa vya Zanzibar na Mauritius vina fursa ya kubadilishana uzoefu katika miradi ya Maendeleo ili kujiongezea ujuzi na maarifa yanatayowawezesha Wananchi wake kuimarika zaidi kiuchumi hali itakayosababisha Mataifa yao kuongeza mapato.


  Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Kisiwa cha Mauritius { Moneo Consulting } Bwana Devanand Virahsawmy akiuongoza ujumbe wa viongozi wa Kampuni hiyo alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.

  Bwana Devanand Virahsawmy alisema Sekta ya elimu ambayo ndiyo mama katika Taifa lolote Duniani inaweza kuwa mwanzo wa ushirikiano huo unaoweza kutoa nafasi kwa vijana wa pande hizo mbili kujipatia Elimu ya Msingi, Sekondari hadi vyuo Vikuu .

  Alisema mpango huo wa pamoja kupitia Kaisheni ya pamoja kwa Nchi zilizozunguukwa na Bahari ya Hindi utaongeza chachu ya uchumi kwa Vijana waliobobea Kitaaluma sambamba na ongezeko la ajira.

  Bwana Devanand alisema Visiwa vya Mauritius tayari vimeshapiga hatua kubwa ya maendeleo hasa katika Sekta ya Utalii kiwango ambacho wanaweza kusaidia Taaluma kwa Nchi zilizo jirani na Visiwa hivyo.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Mauritius (Moneo Consulting) Bw. Devanand Virahsawmy Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Balozi Seif na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ, Makatibu Wakuu na Watendahi Wakuu wa SMZ akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Moneo Consulting kutoka Mauritius.
  Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Mauritius (Moneo Consulting) Bw. Devanand Virahsawmy akisisitiza jambo wakati ujumbe wake ulipofanya mazungumzo na Balozi Seif.
  Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya Moneo Consulting na badhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa SMZ. Picha na – OMPR – ZNZ.


  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipenya ili kuvuka katika daraja la mto Songwe kwenye mpaka wa mikoa ya Mbeya na Songwa baada ya Lori lililokuwa limebeba vinywaji baridi kupinduka katika daraja hilo na kuziba barabara. Ajali hiyo ilisababisha msururu mrefu wa magari yaliyokuwa yakitoka Tunduma na yale yaliyokuwa yakitoka Mbeya Julai 24, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  Msururu wa magari uliosababishwa na ajali ya lori lililopinduka kwenye daraja la mto Songwe katika barabara Mbeya- Tunduma Julai 24, 2017. Lori hilo lilikuwa limebeba vinywaji baridi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Kulia kwa Mh Rais ni Balozi wa India Nchini Mhe Sandeep Arya, Kulia kwa Mh Rais ni Waziri Maji Mhandisi Gerson Lwenge, akifuatiwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na viongozi balimbali wa Mkoa wa Tabora wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mradi wa Maji toka Ziwa Victoria Kwenda Kwenye Mji wa Tabora, Igunga na Nzega Julai 24, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Balozi wa India Nchini Mhe Sandeep Arya,wakiteta jambo mara baada ya Rais kuweka Jiwe la Msingi na Ufunguzi rasmi wa mradi wa Maji toka Ziwa Victoria Kwenda Kwenye Miji ya Tabora, Igunga na Nzega leo Julai 24, 2017.
  Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa mara baada ya ufunguzi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Tabora leo Julai 24, 2017.
  Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo ya Mradi Ukarabati, Ujenzi na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege Tabora toka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Uwanja huo Mhandisi Neema Joseph.
  Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akikata utepe kwenye Ufunguzi wa barabara ya Tabora -Puge -Ngeza yenye Urefu wa Kilometa 114.9 akiwa na  Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa na viongozi wengine wa mkoa wa Tabora.
  Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia wananchi wakati wa ziara mkoani Tabora.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yamefikia katika hatua ya nusu fainali kwa timu nne kuumana mwishoni mwa wikiendi iliyopita huku Mchenga Bball Stars na Kurasini wakiibuka na ushindi.

  Michezo hiyo iliyochezwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay ilikuwa ni hatua ya kwanza ya mechi za nusu fainali ambapo wikiendi ijayo itaendelea tena ikiwa ni hatua ya pili.

  Baada ya kumalizika kwa hatua tatu za mechi ya nusu fanilai, mshindi wa jumla wa mechi hizo ataingia moja kwa moja katika fainali ya Sprite BBall Kings inayotarajiwa kufanyika mwezi Agost mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.

  Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za wikiendi iliyopita, wiki ijayo timu hizo zitaumana tena mpaka katika hatua ya tatu na timu zilizopata alama nyingi ndiyo zitafanikiwa kuingia hatua iya fainali.
  Mchezaji wa timu ya Mchenga (jezi nyeusi) akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Flying Dribblers katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.
  Mchezaji wa timu ya Flying Dribblers (jezi nyeupe) akiwa amemiliki mpira katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.
  Mchezaji wa timu ya Flying Dribblers (jezi nyeupe) akiwa amemiliki mpira katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na madereva wanaofanya safari zao kati ya Masiwani,Magomeni,Majengo na Raskaone Jijini Tanga   waliogoma kutoa huduma kwa siku nzima wakiishinikiza Halmashauri kuikarabati barabara wanazozitumia kutokana na ubovu ambapo Mbunge huyo aliwataka kuendelea shughuli zao wakati kilio chao kikifanyiwa kazi
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani (RTO)Nassoro Sisiwaya akizungumza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku
   Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza na waansdishi wa habari kuhusu namna halmashauri ilivyoweza kulitatua tatizo hilo mara moja kwa kupitisha greda kuichonga
  Kaimu DTO wa wilaya ya Tanga,Imani Raphael akizungumza na  madereva hao ambapo aliwataka kuendelea na shughuli zao wakati suala lao likishughuliwa na mamlaka husika.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Tarehe 16-18 Julai, 2017 Tanzania iliwakilishwa na Timu ya wanafunzi saba katika Mashindano ya Ubunifu yajulikayao kama First Global Robotic Challenge yaliyofanyika jijini Washington D.C

  Timu hiyo iliongozwa na wakufunzi wawili, Bi. Mkufu Shaban Tindi na Bi. Carolyne Eryarisiima.

  Tarehe 19 Julai, 2017 Timu hiyo ilitembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzaniani Washington, DC nchini Marekani kwa ajili ya kusalimia na kujitambulisha.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Mtwara HALIMA DENDEGO Kwa kushirikana na mkuu wa mkoa wa RUVUMA DKT BILINITH MAHENGE wamesema watahakikisha wanaboresha mahusiano mema kati ya TANZANIA na pamoja na MAJIMBO YA NIASSA,na CABO DELGADO nchini MSUMBIJI hususani katika kuboresha miundombinu ili kuweza kutoa fursa wa wananchi katika pande hizo mbili hayo yamesemwa wakati wa kuitimisha mkutano wa ujirani mwema katika ya majimbo hayo kutoka MSUMBIJI na mikoa ya ruvvuma na mtwara.

  0 0

  Mkuu wa jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amesema kukamata viongozi wa kisiasa na dini si kosa bali ni sehemu ya majukumu ya Jeshi la polisi kukamata kama amevunja sheria. Hii hapa video yenye Kazi yetu Ruvuma TV ni kuhabarisha umma, hivyo tumekusogezea matukio sita yaliyotokea mkoani Ruvuma kuanzia Jul 17 – Jul 23, 2017. 
  .

  0 0


  0 0
 • 07/24/17--12:25: MARAIS WOTE WA MAREKANI


 • 0 0


  Wazazi na walezi mnakumbushwa kuwa TCU sasa hivi haipokei maombi ya kujiunga na vyuo vikuu. Hivyo basi imetoa maelekezo kuwa sasa hivi unaomba moja kwa. Moja kwenye chuo husika unachotaka. Na hii ni Orodha ya vyuo vikuu Tanzania na tovuti zake:

  1.    Chuo kikuu cha uongozi wa fedha (IFM)        ……..
  www.ifm.ac.tz au http://ifm.admission.ac.tz
  2.    Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)  …………..
  https://www.udsm.ac.tz
  3.    Chuo Kikuu huria cha Tanzania (OUT)        …………..
  https://www.out.ac.tz
  4.    Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)        ……….
  https://www.udom.ac.tz
  5.    Chuo kikuu cha Mzumbe (MU)             …………
  www.mzumbe.ac.tz
  6.    Chuo Kikuu cha kilimo Cha Sokoine (SUA)    …………
  www.suanet.ac.tz
  7.    Chuo kikuu cha sayansi ya tiba Muhimbili (MUHAS)  …….
  www.muhas.ac.tz
  8.    Chuo kikuu cha Tumaini Makumira (TUMA)    ………
  www.makumira.ac.tz
  9.    Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT)    ………
  https://saut.ac.tz
  10.    Chuo kikuu cha ardhi (ARU)            ……..
  www.aru.ac.tz
  11.    Chuo kikuu cha Mtakatifu Yohane (SJUT)    ………
  www.sjut.ac.tz
  12.    Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) ……. www.mustnet.ac.tz
  13.    Chuo kikuu cha kikatoliki cha Sayansi ya Tiba – Bugando (CUHAS)….. www.bugando.ac.tz
  14.    Chuo kikuu cha Zanzibari (ZU)            ……..
  www.zanvarsity.ac.tz
  15.    Chuo kikuu kishiriki cha Elimu – Mkwawa (MUCE) …….
  https://www.muce.ac.tz
  16.    Chuo kikuu cha ushirika Moshi (MoCU)        ………
  https://www.mocu.ac.tz
  17.    Chuo kikuu cha Afrika cha Nelson Mandela cha sayansi na Teknolojia  … www.nm-aist.ac.tz
  18.    Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hebert Kairuki (HKMU) …… www.hkmu.ac.tz
  19.    Chuo kikuu cha umma cha Zanzibari    (SUZA)    ……..
  www.suza.ac.tz
  20.    Chuo kikuu kishiriki cha elimu cha Dar Es Salaam (DUCE) …….    duce.ac.tz
  21.    Chuo kikuu cha Mlima Meru (MMU)        …….
  www.mmu.ac.tz
  22.    Chuo kikuu cha Mtakatifu Yosefu Tanzania (SJUIT) ………. www.mmu.ac.tz
  23.    Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) .. www.sekomu.ac.tz
  24.    Chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala (KIU)     ……..
  https://www.kiu.ac.tz
  25.    Chuo kikuu kishiriki cha askofu Mkuu Mihayo Tabora (UMUCTA) https://www.kiu.ac.tz
  26.    Chuo kikuu cha kiislamu Morogoro (MUM)    …….
  www.mum.ac.tz
  27.    Chuo kikuu kishiriki cha kikristu cha tiba Kilimanjaro (KCMC) …    kcmuco.ac.tz
  28.    Chuo kikuu kishiriki cha Jordan (JUCO)        ……
  www.juco.ac.tz
  29.    Chuo kikuu kishiriki cha Stella Maris Mtwara (STEMMUCO) … www.stemmuco.ac.tz
  30.    Chuo kikuu kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) www.smmuco.ac.tz
  31.    Chuo kikuu cha Arusha (UOA)            …….        uoa.ac.tz
  32.    Chuo kikuu cha Ekerneforde Tanga (ETU)    ……
  www.etu.ac.tz
  33.    Chuo kikuu kishiriki cha Josiah Kibira (JoKUCo)    …..
  www.jokuco.ac.tz
  34.    Chuo kikuu kishiriki cha afya na tiba cha Mt. Francis (SFUCHAS) www.sfuchas.ac.tz
  35.    Chuo kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) ……
  www.uaut.ac.tz
  36.    Chuo kikuu cha Elimu ya Biashara (CBE)        ………
  https://www.cbe.ac.tz
  37.    Chuo kikuu cha kikatoliki cha Mwenge (MWECAU) …….
  www.mwecau.ac.tz
  38.    Chuo kikuu kishiriki cha Tumaini Dar Es Salaam (TUDARCo) … www.tudarco.ac.tz
  39.    Chuo kikuu cha Iringa (UoI)            ……….
  www.uoi.ac.tz
  40.    Chuo kikuu kishiriki cha Tumaini Iringa        ……..
  www.elct.org/iringa.html
  41.    Chuo kikuu cha Theofilo Kisanji    (TEKU)        ……..
  https://www.teku.ac.tz
  42.    Chuo kikuu cha uhasibu Tanzania (TIA)        ………
  https://tia.ac.tz
  43.    Chuo kikuu cha  Tekinolojia Dar Es Salaam (DIT)    ……..
  www.dit.ac.tz
  44.    Chuo kikuu cha kimataifa cha Tiba & Tekinolojia (IMTU) …… www.imtu.edu
  45.    Chuo kikuu cha Usafirishaji cha Taifa (NIT)    …….
  www.nit.ac.tz
  46.    Chuo kikuu cha ustawi wa jamii (ISW)        ……..
  www.isw.ac.tz
  47.    Chuo kikuu cha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere (MNMA) ….. www.mnma.ac.tz

  0 0

  Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi, CUF linaloongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba limewavua uanachama wabunge nane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho.
  Mwenyekiti huyo wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam kwa makosa kama hayo.
   Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo leo wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam. Amesema wabunge hao nane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na CHADEMA kumwondoa yeye madarakani

  0 0

   Tanzania is Africa’s best safari destination, according to SafariBookings.com, the largest online marketplace for African safari tours. The website conducted an analysis of more than 2,500 expert and safari-goer reviews and declared Tanzania the best safari country in 2017. 
   “Our analysis included more than 2,500 expert and safari-goer reviews. The reviews were evaluated to find the overall favourite and decide the 2017 winner,” says a report posted on the website. 
   The reviews were written by tourists who went on a safari and some of Africa’s leading travel experts. 
  “In our original analysis in 2013, Tanzania also swept away challenges from other sub-Saharan African nations. It is the second time the country has been awarded our overall winner of the best African country for a safari.”
   The website adds that its analysis also revealed that Tanzania’s famed wild spaces made it the best country overall for wildlife too. Various celebrities have in recent months been flocking to various tourist attractions in Tanzania. 
   They include US singer Usher Raymond, former England, Manchester United and Real Madrid player David Beckham, former Liverpool player Mamadou Sakho, Everton player Morgan Schneiderlin and American movie stars Will Smith and Harrison Ford. They visited a number of spectacular tourist sites, including Serengeti National Park and Mount Kilimanjaro. SafariBookings.com named Zambia as the best country for a bush experience, with the majority of experts and safari-goers agreeing that bush landscapes in Zambia were “very special”. “Very popular with safari-goers generally, Zambia also rated as the best country for birdlife. Not surprising given the wealth of avifauna in the country’s many protected areas.” 
  The report also details the reasons reviewers and experts rate Tanzania as the best safari destination in Africa:Superb wildlife viewing in top-class parks. Two are Unesco World Heritage Sites.

  • The annual great migration where over 2.5 million wildebeest and zebra in the Serengeti National Park 
  • Authentic African wilderness with unfenced parks, dirt roads and endless plains.
  • A wide range of budget, mid-range and luxury safari options.
  • Beach holiday extensions on Zanzibar Island, including kite-surfing.
  • Best chimp tracking of Africa in Gombe- and Mahale Mountains National Park.
  • Extend your safari holiday by climbing Africa’s highest mountain; Mount Kilimanjaro.
  • Politically stable and generally safe country.
  • Direct flights from abroad make the northern and southern safari circuits easily accessible
  • Politically stable and generally safe


  Photo: Usher/Twitter Usher in Tanzania.

  0 0


older | 1 | .... | 1823 | 1824 | (Page 1825) | 1826 | 1827 | .... | 3286 | newer