Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

UCHAGUZI MKUU WA KUWACHAGUA VIONGOZI WAPYA WA JUMUIYA YA WATANZANIA READING JUMAMOSI YA TAREHE 29/07/2017

$
0
0

Kamati ya Uchaguzi inachukua fursa hii  kuwataarifu Watanzania wote waishio Reading na maeneo ya jirani ya kuwa  tutakuwa na *mkutano mkuu wa kuwachagua viongozi wa jumuiya yetu hapa Reading ni siku ya JUMAMOSI TAREHE 29/07/2017 kwa yoyote yule atakayependa kuwania nafasi   basi unatakiwa kujaza fomu na kuirejesha mapema iwezekanavyo.
Pia kwa wale ambao hawatakuwa na uwezo wa ku download fomu ya kugombea Uongozi, basi mnaomba mwasiliane na sisi ili tuweze kuwatumia hard copy.
Upatapo ujumbe huu basi mjulishe na mwenzako, Fomu zirudishe kwenye email ya Kamati ya uchaguzi kama ilivoahinishwa hapo chini.
Pia kwa ufafanuzi au maswali yoyote yale basi usisite kuwasilaina na kamati ya uchaguzi kwa njia ya barua Pepe tajwa hapa chini.Watanzania wote wanaoishi Reading na maeneo ya jirani mnakaribishwa kuja kuchagua Viongozi wenu.
Tuma maombi yako ya kugombea Uongozi au ufafanuzi kwa barua pepe kwenda
NAFASI ZA KUGOMBEA 
NGAZI YA JUU YA UONGOZI
1:Mwenyekiti
2:Makamu Mwenyekiti
3:Katibu
4:Katibu Msaidizi
5:Mtunza Hazina/Mtunza Hazina Msaidizi
WAJUMBE
Kuna nafasi nne za wajumbe  ambazo zinatakiwa kujazwa siku hiyo.
     UCHAGUZI : 29/07/2017
MUDA: Kuanzia saa Kumi kamili jioni (4.00pm)
UKUMBI
Bridge  Hall
Oxford Road
 Reading
 Berkshire
 RG1 7PL
MUDA : 10.00 jioni - 3.30usiku (4.00pm - 9.30pm). Mara baada ya Uchaguzi kutakuwa na Chakula, Vinywaji na Burudani Kidogo. Wasiliana na sisi kwa njia ya email tajwa hapo juu au simu nambari 07402 344004
Umoja ni Nguvu, Pamoja Tunaweza!
Tangazo hili limeletwa kwenu na Kamati ya Uchaguzi TA  Reading 2017.
Tanzania Association Reading
WOTE MNAKARIBISHWA

Wananchi wa Busokelo wafanya tafrija maalumu ya kumuaga rasmi mbunge wao mstaafu Profesa Mark Mwandosya

$
0
0
Na Mwandishi Maalumu, Lufilyo 
Jana, Jumamosi tarehe 22 Julai 2017 ilikuwa siku ya kipekee familia ya Profesa Mwark Mwandosyak kwani Wananchi wa Busokelo walifanya tafrija pale Lwangwa, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, ya kumuaga rasmi kama Mbunge wao kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015. 
Akiwa amehemewa na tukio hilo, Profesa Mwandosya alisema hiyo ni heshima iliyoje kwake, Mke wake Lucy Akiiki, watoto wao; Max Mwandosya, Sekela Mwandosya, Emmanuel Mwandosya, na wajukuu Tusekile, Lusekelo, na Queen Maria, Mkwe Digna Mwandosya, na ndugu na marafiki wa karibu. 

Katika risala iliyosomwa kwa niaba yao na Mwalimu Juma Mwakikuti, Mwalimu Mkuu wa Seminari ya Manow, Wananchi wa Busokelo, au Rungwe Mashariki kama Jimbo lilivyojulikana kabla ya kuwa Halmashauri kamili, walishukuru kwa kile walichoona kama mchango mkubwa alioutoa katika maendeleo ya Busokelo, Rungwe, Mbeya na Tanzania kwa ujumla, katika kipindi ambacho Profesa Mark Mwandosya alikuwa Mbunge wao. 

Waliorodhesha mambo mengi ikiwa ni pamoja na: elimu; afya; mawasiliano; miundombinu; utamaduni; utawala (kuanzishwa kwa Halmashauri); maji safi karibu kila kijiji; umeme kila kata kuanzia mwaka 2002; mshikamano wa Jimbo; michezo; Kituo cha Utamaduni, Mila, Historia, na Desturi za Wanyakyusa; Benki ya NMB; Ujenzi kupitia Shirika la Nyumba la Taifa; na kadhalika. Kipekee walimshukuru Mama Lucy Mwandosya kwa kulea watoto yatima na kuwasomesha kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu, na kujenga kituo cha ufundi cha watoto hao ambacho amekikabidhi kwa Serikali na sasa kimekuwa Chuo cha Ufundi cha VETA. 
Mzee Mwakihwanja kutoka Lupata akimvishaProfesa Mark Mwandosya wakati wa tafrija maalumu ambayo  Wananchi wa Busokelo waliandaa jana Jumamosi Julai 22, 2017 ili kumuaga rasmi kama Mbunge wao kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015, Lwangwa, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, mkoani Mbeya mgolole Profesa Mark Mwandosya wakati wa tafrija maalumu ambayo  Wananchi wa Busokelo waliandaa jana Jumamosi Julai 22, 2017 ili kumuaga rasmi kama Mbunge wao kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015, Lwangwa, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, mkoani Mbeya.

Profesa Mark Mwandosya akifurahia zawadi yake ya mkuki na mgolole
Picha ya kumbukumbu iliyopigwa Jumamosi,tarehe 22 Julai 2017 kwa heshima ya Profesa Mark Mwandosya baada ya Wananchi wa Busokelo kuandaa  tafrija Lwangwa, Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, ili kumuaga rasmi kama Mbunge wao kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015. 

RAIS DKT. MAGUFULI AANZA ZIARA MKOANI TABORA NA KUZINDUA MIRADI YA BARABARA

$
0
0

  Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora Mhe Rais yupo mkoani humo kwa  ziara ya kiserikali
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mke wake Mama Janeth Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Agrey Mwanri wakiondoa kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Tabora Ndono - Urambo yenye urefu wa kilometa  94 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 

Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Tabora Ndono - Urambo yenye urefu wa kilometa  94 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 

 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiondoa kitambaa kwenye jiwe la Msingi kuashiria kufunguliwa kwa Barabara Kariua - Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,akiwapungia Mikono kwa Kuwasalimia Wananchi wa Kariua na Viunga vyake Walio jitokeza kumsikimsikiliza Mh Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
 Maelfu ya wananchi wa Kariua na Viunga vyake Wakimsikiliza Mh Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwahutubia wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Wananchi wa Kariua Mkoani Tabora wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora. Picha na IKULU
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

In loving memory of the late franco kabigi

$
0
0
Today marks five long years since you left us daddy. Oh Lord you know how much we still love him and miss him. He is irreplaceable indeed. 

Daddy, I remember all the things you taught me especially the brave words you used to tell me; "my daughter  Joyce, always remember usikimbie zaidi ya miguu yako". 

Those words keep me going in my ups and downs. Thank you daddy. You forever remain  my star.
May our merciful Lord continue to rest you in eternal peace.

AMEN!

OLD SCHOOL RE- UNION BASH 2017 September 1-3 in Columbus, Ohio

MAJIMBO YA NIASSA,CABO DELGADO YA MSUMBIJI YATAENDELEZA MAHUSIANO NA MIKOA YA RUVUMA ,MTWARA

$
0
0
Mikoa ya Ruvuma, Mtwara pamoja na majimbo ya Niassa, Cabo Delgado ya Msumbiji ykubaliana kuendeleza vyema mahusiano ya ujirani mwema ili kuleta fursa za watu wa nchi hizo mbili. Katibu Tawala mkoa wa Ruvuma Bw. Hassan Bendeyeko ameongea  wakati wa kufungua mkutano wa ujirani uliofanyika mkoani Ruvuma kwa siku mbili habari kamili ni hii hapa.

TAZAMA YALIYOJILI MKOANI RUVUMA KUANZIA JUL 17 – JUL 23, 2017

$
0
0
Tumekusogezea karibu matukio sita ya kihabari yaliyojili mkoani Ruvuma kuanzia Jul 17 – Jul 23, 2017 .

Airtel yatoa vitabu masomo ya sayansi vya thamani ya shilingi milioni 15 kwa shule za sekondari Mbeya

$
0
0
Shule tano kufaidika na vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 5 

Mbeya; Katika kuinua sekta ya elimu nchini , kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa msaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa shule 5 za sekondari mkoani Mbeya.

Vitabu hivyo vimetolewa na Airtel kwa kushirikiana na Tulia Ackson foundation kwaajili ya shule za sekondari za Ikuti, Kayuki , Bujeli, Ntaba na Ikupa

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Naibu Spika Mh Dkt, Tulia Ackson alisema aliwapongeza Airtel kwa kushirikiana na taasisi yake ya Tulia Ackson ili kusaidia shule za sekondari zenye uhaba wa nyenzo za kujifunzia mkoani Mbeya. Dr. Ackson alisema” ni muhimu kwa makapuni binafsi ya umma kushirikiana katika kuinua sekta ya elimu nchini ili kuweka mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi

Tumeshuhudia uhaba mkubwa wa vitabu katika mashule ambapo uwiano upo kati ya kitabu kimoja kwa wanafunzi 5 hadi 10. Tunaamini msaada huu tunaoutoa leo utasaidia kuzalisha nguvukazi yenye ueledi itakayowawezesha kujiajiri au kuajiriwa na kujenga uchumi wenye nguvu. Natoa wito kwa makapuni mbalimbali kuungana nasi na kuzifikia shule zenye uhitaji wa vifaa vya kufundishia nchini

Kwa upande wake Meneja Mauzo mkoani Mbeya, Bartholomew Masatu alisema” Airtel tunaamini jamaa iliyoelimika inajengwa kutoka katika shule zenye vifaa vya kufundishia vyakutosha hususani vitabu. Ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi hapa Mbeya”.

Tunaamini msaada utachochea ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi katika mkoa wetu.” Aliongeza Masatu

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa sekondari ya Kayuki Bi Bertha Sarufu Kwa niaba ya shule zilizofaidika na msaada wa vitabu alisema “ Tunashukuru sana Airtel kwa kutufikishia msaada huu na napenda kutoa wito kwa wanafunzi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa lengo la kuboresha ufaulu. Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".


WAZIRI wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamja na Naibu Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Akson wakipokea vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.Anayewakabidhi vitabu hivyo ni Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mbeya bw, Bartholomew Masatu. Airtel imekabidhi vitabu hivyo mwishoni mwa wiki hii ikiwa ni ahadi yake ya kuendeleza masomo ya sayansi nchini.

WAZIRI wa Elimu Profesa, Joyce Ndalichako (Kushoto)akiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania , Dkt.Tulia Akson , wakimkabidhi vitabu vya sayansi kwa Mkuu wa sekondari ya Kayuki, Bertha  Sarufu, vitabu vilivyotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. Mbali ya Kayuki, shule nyingine za sekondari zilizonufaika na msaada huo ni Ikuti, Bujela, Ntaba na Ikapu, zote zipo wilayani Rungwe. Airtel imekabidhi vitabu vya sayansi mwishoni mwa wiki vyenye thamani ya shilingi milioni 15.

MKE WA WAZIRI MKUU AWASIHI WANAFUNZI KUTOKATISHA MASOMO

$
0
0
MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewasihi wanafunzi wa kike nchini kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo yao.
Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa mfululizo kutoka kiwango kimoja cha taaluma kwenda kingine.
Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 23, 2017) alipozungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Vwawa wilayani Mbozi.
Mke wa Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ziara ya mkoa Songwe, aliwaasa wanafunzi hao kutumia wakati huu kwa kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo viovu.
“Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara kwa ajili ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikatishe masomo yenu.”
Mama Mary aliongeza kwamba “utumieni muda huu vizuri ili msije mkaujutia baadae, kwani wakati ni mali ukipita umepita.”
Alisema ni vizuri wakasoma hadi chuo kikuu na kwamba wasikimbilie kufanya mambo yasiyowahusu kwa sasa kwani mshika mawili moja lazima limponyoke.Mke wa Waziri Mkuu alisema wanafunzi hao wakisoma hadi elimu ya juu watakuwa na uwezo wa kutambua jambo lipi ni jema na lipi ni baya.
“Kilichonifurahisha zaidi ni kwa sababu mimi pia ni mwalimu kwa hiyo inavyoona wanafunzi wako vizuri kama hivi nafurahi sana, hivyo nawaomba msome kwa bidii.”
Serikali imetunga sheria kali dhidi ya watu wanaosababisha watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kuwapa mimba au kuwaoa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JULAI 24, 2017

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majalwa akizungumza na wanafujnzi wa Shule ya Sekondari ya Vwawa iliyop[o Mbozi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na watumishi wa umma, viongozi wa dini na viongozi wa taasisi za binafsi kwenye ukumbi wa shule hiyo Julai 23, 2017 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAGAZETI YA JUMATATU LEO JULAI 24,2017

INTRODUCING: MUPENZI BY ALLY NIPISHE

IGP SIRRO AKUTANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOANI MWANZA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (katikati), akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, wakati alipofika ofisini kwake jana. IGP Sirro, yupo mkoani humo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi, yenye lengo la kujitambulisha kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo. kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Ahmed Msangi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, kwa lengo la kujitambulisha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, alipofika kwa lengo la kujitambulisha, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa Jeshi hilo baada ya kumaliza kikao kazi na maofisa na askari ambapo aliwasisitiza kuzingatia weledi wakati wa kutekeleza majukumu yao. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.


MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI AWAHIMIZA WATANZANIA KULIPA KODI

JK AFUNGUA MKUTANO WA WATOA HUDUMA ZA AFYA NA WAMILIKI WA VITUO VYA AFYA NA WATAALAMU WA AFYA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI, JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua mkutano wa sita wa watoa huduma za afya, wamiliki wa vituo vya Afya, wataalamu wa Afya kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Uganda, Burundi, na mataifa ya nje ambao unaogozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu Pamoja na mabalozi na viongozi mbali mbali wa serikalini na sekta binafsi kujadili mustakabali wa sekta ya afya wa Tanzania na nchi shiriki hasa jinsi ya kuboresha sekta binafsi. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Picha na Kajunason, Globu ya Jamii.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wengine wa meza kuu wakimshikiliza Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akitoa hotuba yake katika kungua mkutano wa sita wa watoa huduma za afya, wamiliki wa vituo vya Afya, wataalamu wa Afya kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Uganda, Burundi, na mataifa ya nje, unaofanyika kwa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa sita wa watoa huduma za afya, wamiliki wa vituo vya Afya, wataalamu wa Afya kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Uganda, Burundi, na mataifa ya nje ambao unaogozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu Pamoja na mabalozi na viongozi mbali mbali wa serikalini na sekta binafsi kujadili mustakabali wa sekta ya afya wa Tanzania na nchi shiriki hasa jinsi ya kuboresha sekta binafsi. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Picha na Kajunason, Globu ya Jamii.

NEWZ ALERT:TUNDU LISSU AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU MCHANA HUU

$
0
0

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Rais chama cha Mawakili nchini (TLS),Mh. Tundu Lissu akishuka kwenye gari maalum mara baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema hii leo jijini Dar,akituhumiwa kwa makosa ya Uchochezi.

Tundu Lisu alikamatwa  Julai 20 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alikokuwa akielekea Kigali, Rwanda kwenye Mkutano wa Marais wa Vyama vya Mawakili Afrika Mashariki.
Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Rais wa chama cha Mawaikili nchini (TLS),Mh. Tundu Lissu akiingizwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema hii leo jijini Dar,kujibu tuhuma za kesi yake inayomkabili ya ya Uchochezi.

Tundu Lisu alikamatwa  Julai 20 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alikokuwa akielekea Kigali, Rwanda kwenye Mkutano wa Marais wa Vyama vya Mawakili Afrika Mashariki.
 
HABARI ZAIDI TUTAWALETEA HIVI PUNDE. 

JAFO AZITAKA HALMASHAURI KUWAWEZESHA KINAMAMA NA VIJANA KWA VITENDO

$
0
0
NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amezitaka halmashauri kuwawezesha vijana na kinamama kwa vitendo kwa kuyapa makundi hayo baadhi ya kazi zilizo chini ya halmashauri ambazo wanao uwezo wa kuzifanya ili wajiongezee kipato.

Jafo ameyasema hayo leo katika hafla ya kukabidhi hundi ya Sh. milioni 70 iliyotolewa na Manispaa ya Dodoma kwa vikundi vya ujasiliamali vya vijana na kinamama ndani ya manispaa hiyo.

Ameeleza kwamba haipendezi kwa halmashauri yeyote kuwanyima fursa ya kazi vikundi vya vijana na kinamama ambapo kazi hizo zinaweza kufanywa na makundi hayo.

Jafo ametolea mfano kikundi cha vijana cha DOYODO ambacho kina kiwanda cha kisasa cha kufyatua Matofali lakini wanahangaika soko  la kuuzia matofali wakati kuna ujenzi mkubwa wa madarasa na vyoo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Wawakilishi wa vikundi vya vijana na kinamama wa Manispaa ya Dodoma wakipokea hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali.
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza na wajasiriamali wa Manispaa ya Dodoma katika hafla ya kukabidhi hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya vikundi vya Kinamama na Vijana.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akitoa taarifa ya mikopo ya vijana na kinamama kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Rais Dkt Magufuli afungua mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora

$
0
0
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo mafupi mara baada kufungua mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora. Rais Dkt Magufuli ameagiza Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano kujenga jengo la abiria 500 badala ya jengo lililopo la abiria 50.Pia ameagiza urefu wa uwanja uongezwe hadi kufikia kilometa 2.5 badala ya kilometa 1.9 zilizopangwa ili ndege kubwa na ndogo ziweze kuutumia uwanja huo.
Rais Dkt John Pombe Magufuli ameweka jiwe la Msingi la mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda miji ya Tabora, Nzega na Igunga. Mradi huo utagharimu Shilingi Bilioni 600 na unatekelezwa kwa fedha za mkopo nafuu kutoka India. Una uwezo wa kuzalisha lita Milioni 80 kwa ajili ya Mji wa Tabora.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo mafupi ya mradi huo wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora,kutoka kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Prof Makame Mbarawa mapema leo mkoani humo

Rais Dkt John Pombe Magufuli mapema leo amefungua mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora,Wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Rais Dkt Magufuli ameagiza Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano kujenga jengo la abiria 500 badala ya jengo lililopo la abiria 50.Pia ameagiza urefu wa uwanja uongezwe hadi kufikia kilometa 2.5 badala ya kilometa 1.9 zilizopangwa ili ndege kubwa na ndogo ziweze kuutumia uwanja huo.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AZINDUA BODI MPYA YA USHAURI YA WIZARA - TAASISI YA UHASIBU TANZANIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amezindua Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa lengo la kuimarisha ufanisi wa Taasisi  na uangalizi wa karibu.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa uzinduzi huo uliofanyika  Taasisi ya Uhasibu Tanzania kampasi ya Singida  Dkt. Kijaji amesema Bodi hiyo itamsaidia Waziri wa Fedha na Mipango kupata ushauri wa kitaalam  na hatimaye kutoa maamuzi  yenye tija kwa Taasisi na Taifa kwa ujumla.

 "Bodi hii ya Ushauri inategemewa kutoa mchango  wa mawazo na  kitaalam yanayohusu uendeshaji  na uboreshaji wa  Taasisi yetu ya TIA ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea duniani katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kiteknolojia, kisiasa na kijamii", amesema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji ameongeza kuwa Bodi hiyo ina wajibu wa kujua ubora wa wanafunzi wanaohitimu katika chuo hicho ikiwa ni pamoja na ubora wa vyeti vyao kuendana na uwezo wao wa kufanya kazi katika fani walizosomea na kukabiliana na changamoto kwenye maeneo ya kazi.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Said Chiguma amesema Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchache wa miundombinu kama vile kumbi za mihadhala, madarasa, maktaba na maabara za kompyuta ambavyo ni nyenzo muhimu katika utoaji wa elimu iliyo bora.

Chiguma amesema ili kupunguza changamoto hizo, Taasisi inajitahidi kutenga fedha inazozikusanya ili kukarabati na kujenga majengo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha elimu na kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi.

Taasisi ya Uhasibu Tanzania ni chuo cha Serikali ambacho kinatoa mafunzo katika fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Rasilimali Watu, Masoko na Uhusiano wa Umma pamoja na Uhasibu wa Fedha za Umma kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashada (Diploma)  na Shahada (Degree).
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza muda mfupi kabla hajazindua Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.
 Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Said Chiguma akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Joseph Kihanda, akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi hiyo. Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa  Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA Singida mjini. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri TIA Said Chiguma na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA Joseph Kihanda na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo na Mjumbe wa Bodi Dkt. Leonada.

MSIBA MAREKANI

$
0
0

Tarifa za kusikitisha za kifo cha mwenzetu Peter M Jennings Kessy. Mtanzania alikuwa akiishi Bronx New York kilichotokea siku   July11,2017 .
Ndugu Peter Jennings ni mjomba wa Rose Gadner wa Connecticut . Taratibu za mazishi zinapangwa ambapo mwili utasafirishwa kuelekea nyumbani Kilimanjaro -Tanzania.Kabla ya kusafirishwa mwili utaangwa August 12,2017(Tentative ) .
Kama ilivyo ada yetu tushirikiane ktk kipindi hiki kigumu ,tuonyeshe umoja, upendo na udugu wetu kwa hali na mali. Tunawaombea Mungu awape nguvu na faraja.
Pole kwa ndugu , jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.

Taarifa zaidi zitatolewa kadiri zitapokuwa tayari au wasiliana na :
Rose Gadner:+12038140545



More contacts &
info to follow #UpdatesAsWeGet

Aksanteni,


Sylvester Mwingira.
Hi everyone, please click here to support my GoFundMe campaign, Peter's Tanzania Funeral Fund: 



MAFUNZO YA MFUMO MPYA WAKUANDAA MIPANGO NA BAJETI ZA SERIKALI ZA MITAA-MWANZA YAFANA

$
0
0
 Katibu Tawala Msaidizi,Uchumi na Mipango Mkoa wa Mwanza, Johansen Bukwali akifungua Mafunzo ya Mfumo Mpya wakuaandaa Mipango na Bajeti za Serikali za Mitaa (PlanRep) kwa maafisa Mipango, Wachumi, Wahasibu, Maafisa Tehema na Makatibu wa Afya wa Halmashauri kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa yaliyofanyika Jijini Mwanza, leo Tarehe 24 Julai 2017.
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka TAMISEMI,  Elisa Rwamiago akitoa mafunzo ya Mfumo Mpya wakuaandaa Mipango na Bajeti za Serikali za Mitaa (PlanRep) kwa maafisa Mipango, Wachumi, Wahasibu, Maafisa Tehema na Makatibu wa Afya wa Halmashauri kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa yaliyofanyika Jijini Mwanza, leo Tarehe 24 Julai 2017.
 Washiriki wa Mafunzo ya Mfumo Mpya wakuaandaa Mipango na Bajeti za Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia mafunzo yaliyofanyika Jijini Mwanza, leo Tarehe 24 Julai 2017.
Mgeni rasmi (katikati walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Mfumo Mpya wakuaandaa Mipango na Bajeti za Serikali za Mitaa (PlanRep) kutoka Mkoa wa Geita yaliyofanyika Jijini Mwanza, leo Tarehe 24 Julai 2017.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images