Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI NGURUKA WILAYANI UVINZA MAPEMA LEO.

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi mbalimbali wa mji wa Nguruka mapema leo asubuhi,waliojitokeza kumshuhudia Rais akiweka jiwe la msingi la Mradi wa maji.Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuupatia maji mji wa Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma,ambapo pia ameweka jiwe la msingi la mradi huo unaotarajia kukamilika Desemba 31, 2017,ukamilishwaji wa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.
 Rais Dkt Magufuli akipeana mkono na Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini,Mh Daniel Nsanzugwako mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi mkubwa wa maji mapema leo mjini Nguruka mkoni Kigoma.Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuupatia maji mji wa Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma,na kuwamba Mradi huo unatarajia kukamilika Desemba 31,2017,kukamilika kwa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.
 Rais Dkt Magufuli akitoka kukagua mradi huo wa maji unaotarajia kukamilika Desemba 31,2017.kukamilika kwa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.Rais Dkt Magufuli yuko njiani akielekea mkoani Tabora,ambapo atasimama Wilayani Kaliua na kuzindua barabara ya Kaliua hadi Kazilambwa yenye urefu wa kilometa 50.


MKE WA WAZIRI MKUU APONGEZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI ILEJE

$
0
0
MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewapongeza wanawake wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali.

Ametoa pongezi hizo leo (Jumamosi, Julai 22, 2017) wakati akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Ileje katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi.Ametoa pongezi hizo baada ya kushiriki katika ukaguzi wa vikundi mbalimbali vya wanawake wanaojihusisha na shughuli za ujasiriamali wilayani Ileje.

Mke wa Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe, amesema ujasiriamali ni mkombozi kwa wanawake.

Mama Mary amesema amefarijika kuona wanawake wengi wakishiriki katika shughuli za ujasiriamali kwa kuwa zinalenga kuwaongezea kipato na kuwakwamua kiuchumi.Mmoja wa wajasiriamali hao, Bi. Riziki Sunday amesema shughuli hizo za ujasiriamali zimemuwezesha kumudu mahitaji ya familia yake, hivyo kuondokana na utegemezi.

Bi. Riziki amesema kuwa miongoni mwa faida alizozipata kutokana na ujasiriamali ni pamoja na kujenga nyumba, kusomesha watoto na kuongeza mashamba.

Pia Bi. Riziki ametumia fursa hiyo kuwashauri wanawake wenzake kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakitazama vifaranga wa samaki wakati alipotembelea banda la Kikundi cha wanawake cha Tukazane cha Ileje kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje Julai 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI KIGWANGALLA AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA BWENI LA WAZEE KAMBI YA KOLANDOTO NA KUZINDUA JIKO LA NISHATI YA GESI

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akilsililiza Katibu wa Baraza la wazee wa Mkoa wa Shinyanga Mzee Faustine Sengerema mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo la bweni la wazee katika makazi ya wazee waisiojiweza ya Kolandoto mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Bweni la wazee waishio katika makazi ya wazee wasiojiweza ya Kolandoto Mhandisi Harold Jackson Mtyana wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo na kuweka jiwe la msingi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akisililiza matumizi ya nishati ya jiko la gesi kutoka kwa Afisa Mfawdhi ya Makao ya wazee Kolandoto katika Manispaa ya Shinyanga, muda mfupi kabla ya uzinduzi wa matumizi ya majiko hayo katika vituo vya makao ya wazee na watoto hapa nchini.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akikata utepe katika moja ya bajaji kuashiria ugawaji na matumizi rasimi ya bajaji hizo katika makazi ya kulea wazee wasiojiweza ya Kolandoto Shinyanga kwa niaba ya Makazi mengine nchini.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akimkabidhi funguo ya bajaji Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea wazee wasiojiweza ya Kolandoto Bi Sophia Kang’ombe kwa niaba ya maafisa Wafawidhi katika makazi mengine nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akimkabidhi Sanduku la Huduma ya kwanza Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee wasiojiwezaya Kolandoto Bi Sophia Kang’ombe kwa niaba ya maafisa Wafawidhi katika makazi mengine nchini.

TENGA ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA KAMATI YA UFUNDI NA MAENDELEO CAF,TFF YAMPONGEZA.

$
0
0
Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace John Karia amempongeza Leodegar Chilla Tenga - Rais wa Heshima wa TFF kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Leodegar Chilla Tenga aliteuliwa Ijumaa iliyopita katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mjini Rabat nchini Morocco ambako katika kamati hiyo muhimu, Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya.

“Hii ni sifa kwa nchi. Na ni sifa kwa Mheshimiwa Tenga. Tunajisikia fahari Tanzania kung’ara katika medani za uteuzi katika vyombo vya kimataifa kama CAF. Uteuzi wake ni kwamba anafungua njia kwa nchi na wengine ili kufanya vema,” anasema.

Karia amesema ana imani na Tenga na Bwalya katika kamati yao kwa sababu ni wachezaji na manahodha wa zamani wa timu za taifa. Itakumbukwa kwamba Tenga alikuwa akicheza kama mlinzi Bwalya alikuwa mshambuliaji. “Wote ni wataalamu. wanajua, tutafanikiwa.”

Katika mkutano huo mbali na kuteua akina Tenga na kuunda kamati nyingine, pia ulifanya marekebisho ya muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na sasa yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni mwa mwaka. 

Kwa miaka ya nyuma hadi mwaka huu ambako michuano hiyo ilifanyika Gabon, ilikuwa ikifanyika kuanzia katikati ya Januari hadi Februari. Mbali na kuzitoa Fainali za AFCON katikati ya mwaka hadi mwanzoni, pia idadi ya timu za kushiriki zimeongezwa kutoka 16 hadi 24 ambako sasa utakuwa na timu washindwa 10 badala ya mbili kama ilivyokuwa awali.

“Watanzania wasikate tamaa, hata kama kwa mfumo wa sasa unaofutwa au tuseme kubadilishwa, bado tuna malengo yetu yalikuwa ni kufuzu, Tunajipanga kwa hali ya sasa na hatujaanza vibaya na Lesotho. Bado tuna nafasi,” amesema Karia.

Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon.

Hii si mara ya kwanza kwa Tenga aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), bali amekuwa akiteuliwa mara kwa mara kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF. Hongera sana Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Chilla Tenga.

MAKONDA: KAMPUNI YA PROPERTY INTERNATIONAL INASAIDIA KUONDOA TATIZO LA MIGOGOLO YA ARDHI

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema miongoni mwa Makampuni Binafsi yanayoisaidia Serikali kwa kufanya kazi ya uuzaji na upimaji wa Viwanja vya Viwanda na Makazi, ni Kampuni ya Property International pekee ambayo mpaka sasa kama mkuu wa mkoa bado hajapata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu migogolo ya ardhi.

Akizungumza katika Kipindi cha Sema Kweli kinachorushwa kila Ijumaa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, alisema kuwa, amekuwa akipata malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi juu ya migogolo hiyo inayotokana na kuuziwa ama kupimiwa viwanja na makampuni ambayo hayajajitosheleza katika kufanya kazi hiyo baada ya kuidhinishwa na Serikali.

Aidha alisema kuwa kutokana na suala hilo kumekuwa na ugumu wa Serikali kukusanya mapato 'Kodi ya majengo' kutokana na wananchi kujijengea makazi holela bila kupata vibali vya ujenzi, baada ya kuuziana maeneo kienyeji bila kupimwa na kupatiwa hati, jambo ambalo kwa sasa linafanyiwa kazi kwa kasi na baadhi ya makampuni binafsi ikiwamo ya Property International, yanayoshirikiana na Selikali katika kifanya kazi hiyo.

Makonda alimpongeza Waziri William Lukuvi, kwa kazi ngumu anayofanya ikiwa ni pamoja na ya ulasimishaji wa makazi ili kwenda na viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya kuzitambua nyumba na kuzipa madaraja tofauti kurahisisha upatikanaji wa kodi ya majengo, na mpangilio wa miji unaotakiwa huku Serikali ikiendelea kuwakaribisha wapimaji biasfi ili kuendana na kasi.

''Wapimaji binafsi watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa Watumishi na Vifaa vya kisasa vinavyorahisisha upimaji wa haraka na kwa wakati, lakini Manispaa zinatakiwa kuwapa ushirikiano makampuni hayo kwa kuwapa na kuwatambua ili Serikali inapotoa Hati isitokee mgongano kutokana na maeneo husika kupimwa na watu watatu tofauti''. alisema.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO

$
0
0
Na Editha Karlo- Globu ya Jamii Kigoma

RAIS Wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ,David Kafulila kwa kujitoa Muhanga kutetea Watanzania kupitia sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo Mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nguruka,leo Katika uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza, alisema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua Ubadhilifu uliofanywa na Kampuni ya IPTL ambapo kwasasa suala hilo ameanza kulifanyia kazi na mafanikio yameanza kuonekana.

Amesema Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwasababu ya uzalendo wake wa kutetea Taifa.

"Mimi ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo ninampongeza Kafulila kwa uzalendo wake kwa nchi na nitaendelea kumpongeza maisha yangu yote"alisema Magufuli.Magufuli alisema maendeleo hayana chama ndio maana Kafulila alijitoa kwa hali ya juu na kutetea fedha za Wananchi zilizo kuwa zikiibiwa na mafisadi wachache na kujinufaisha wao.

"Ninajua Kafulila ulitukanwa sana wakati wa kuibua sakata la Escrow, wapo watu walikuita tumbili mimi najua wewe sio tumbili ,matumbili ni wao wewe najua ni wa Chama kingine lakini umefanya kazi kubwa ya kulinda maslahi ya nchi, kwahiyo nitakuwa mnafiki sana nisipo kupongeza kitu ulichokifanya ni kikubwa Kwa,Taifa naomba nikupongeze kwa hilo",

Alisema Kiongozi mzuri ni yule ambae anatetea wananchi bila kujali chama wala siasa za uchochezi , hivyo atahakikisha kuwa Wananchi hawateseki na Wale ambao wameiba fedha za serikali na Wananchi wanazirudisha bila kujali nyadhifa walizonazo, ili pesa hizo zitumike katika kuleta maendeleo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mh.David Kafulila

BARABARA YA MPEMBA/ISONGOLE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto) wakisalimiana na wanakwaya baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje mkoani Songwe, Julai 22 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Ileje kwamba Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mpemba-Isongole.

Amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 58 ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwani itafungua fursa za kiuchumi na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Julai 22, 2017) alipozungumza na wananchi wa wilaya ya Ileje kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi.

Waziri Mkuu alisema barabara hiyo itawawezesha wananchi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe, ambao wana mazao mengi kuyafikia masoko kwa urahisi.

“Ujenzi wa barabara hiyo utaongeza fursa za kiuchumi katika Wilaya ya Ileje, hasa kufungua biashara za mipakani kati ya nchi ya Tanzania na Malawi.”Alisema Serikali imedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto mbalimbali hasa miundombinu ya barabara, hivyo aliwaomba waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.

Awali Mkuu wa wilaya hiyo, Bw. Joseph Mkude alisema kiasi cha fedha kinachotolewa kwa matengenezo ya barabara hakitoshi ukilinganisha na ubovu wa barabara zao.

Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa wilaya aliiomba Serikali kuipa kipaumbele miradi ya ujenzi wa barabara iliyo kwenye ukanda wa mvua nyingi ili zipitike wakati wote.Pia alisema wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo la uharibifu wa barabara unaofanywa na wananchi wasio waadilifu, hivyo kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.

Hata hivyo alisema kwa sasa wanatoa elimu ya utunzaji na ulinzi wa miundombinu ya barabara kwa wananchi ili kupunguza gharama za matengenezo ya kila mara.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 23, 2017

Mahojiano ya TBC JamboTanzania kati ya Angela Msangi na Peter Msechu


MAMBO YA GADO

TAMASHA KUBWA LA CASTLE LITE UNLOCKS LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Msanii Vanessa Mdee akiwa jukwaani akiwakonga mashabiki.

 Msanii Diamond Platinumz akiwa katika jukwaa la castle lite unlocks akiwakonga wapenzi wa burudani  usiku wa kuamkia leo

Msanii Casper Nyovest akiwa jukwaani akiwakonga mashabiki.
Msanii toka Marekani FUTURE akiwa jukwaani kwenye tamasha kubwa la castle lite unlocks usiku wa kuamkia leo. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI ASEMA NCHI INAHITAJI WAZALENDO, AMPONGEZA KAFULILA KWA IPTL

$
0
0
RAIS Wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ,David Kafulila kwa kujitoa Muhanga kutetea Watanzania kupitia sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo Mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania. 
 Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nguruka, Katika uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza, amesema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua Ubadhilifu uliofanywa na Kampuni ya IPTL ambapo kwasasa suala hilo ameanza kulifanyia kazi na mafanikio yameanza kuonekana.Hii hapa Video yake.

AJALI KIMARA BARUTI

$
0
0
Gari lenye namba za usajilii namba T 129CYY imetumbukia mtaroni eneo la Bahama Mama-Kimara Baruti jijini Dar es Salaam mapema leo.Kulingana na mashuhuda wa jali hiyo wanaeleza kuwa ajali hiyo ilisababishwa na Mwendo kasi wa gari hiyo, ambapo dereva alikuwa akimkwepa mwendesha bodaboda na kujikuta akitumbukia kwenye mtaro kama ambavyo tukio hilo lilivyonaswa na Camera ya Globu ya Jamii.
 
Baadhi y mashuhuda wakishuhudia tukio la ajali hiyo,ambapo hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya kuwa na majeraha madogo na hatimaye kukimbizwa  hospitali kwa huduma ya kwanza.

Mwakilishi wa Jimbo la Tungu Mhe Simai Mohammed na Mbunge wa Jimbo Hilo Mhe Khalifa Salum Washiriki Ujenzi wa Soko la Samaki Katika Kijiji cha Tindini

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Khalafa Salum Suleima wakishiriki katika ujenzi wa Taifa wa kujenga Soko la Samaki katika ufukwe wa pwani ya Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja, wakikata majengo ya kuezekea bati katika soko hilo. Pia wamekabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi huo ili kutowa mazingira mazuri ya Soko hilo wakati wa kufanya mnada wa samaki kwa wavuvi wanaporudi baharini kuvua.
Mbunge nas Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said ma Mhe Khalifa Salum Suleiman wakikabidhi mabati kwa Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Bi. Sauda Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ya Mabati hayo na miti yamefanyika katika viwanja vya Soko hilo Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini.
Wananchi wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki wao.. 
Wananchi wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki wao
Kiongozi wa Kijiji cha Tindini akitowa maelezo ya ujenzi wa Soko hilo la Samaki katika ufukwe wa bahari yao litakalotowa huduma ya kuuzia samaki kwa wavuvi katika soko la mnada. 

SHAKA AMALIZA ZIARA YA KIKAZI WILAYA YA MAGU, ATUA WILANI UKEREWE

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akishiriki Kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Mwamanga wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akizindua shina la vijana wakereketwa wa CCM wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka,(kulia) akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Mwamanga wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akizindua shina la vijana wakereketwa wa CCM wilayani Magu.

MKUU WA MKOA WA MWANZA MHE MONGELLA AKIWA KAZINI


MKUTANO MKUU WA UJIRANI MWEMA KATI YA MIKOA YA MTWARA NA RUVUMA KWA TANZANIA NA MAJIMBO YA NIASSA NA CABO DELGADO KWA NCHI YA MSUMBIJI

$
0
0
Mkutano wa ujirani mwema ambao unakutanisha mikoa ya ruvuma na Mtwara kwa upande wa Tanzania na Majimbo ya NIASSA na CABO DELGADO kwa upande wa nchi ya MSUMBIJI umeanza leo Mkoani Ruvuma.

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI DED WA MBOZI KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Bw. Eliseyi Mgoyi pamoja na maofisa wengine watatu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma. 
 Pia amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Songwe, Bw. Damian Sutta kuwakamata na kuanza kuwachunguza haraka maofisa hao na kisha ampelekee taarifa ofisini kwake. 
 Waziri Mkuu amewasimamisha kazi maofisa hao leo (Jumapili, Julai 23, 2017) wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Vwawa, akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa  Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wa wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Vwawa wilayani Mbozi Julai 23, 2017. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa  Wapili  kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Limdi, Erasto Zambi
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe nje kidogo ya mji wa Vwawa mkoani Songwe Julai 23, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kulia kwake) wakitazama Kimondo wakati walipotembelea Kituo cha Mambo ya Kale cha Mbozi mkoani Songwe
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa wilaya ya Mbozi wakati walipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kyalele wilayani humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. 
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama nguo za batiki  wakati walipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wa Mbozi kabla ya  mkutano wa hadahara uliohutubia wa Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nalyelye wilayani Mbozi, Februari 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

UDAHILI WA PAPO KWA PAPO KWA VYUO VIKUU VYA NJE NDANI YA GLOBAL EDUCATIO LINK

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Baada ya Matokeo ya Kidato cha Sita , Global Education Link (GEL) ambao ni mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imesema kuwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu vya nje udahili ni papo kwa papo na vyuo hivyo viko wazi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema katika azma ya serikali ya awamu ya tano ya viwanda, inahitaji rasilimali watu ya kutosha ambao ndio watasukuma gurudumu hilo la viwanda na ujuzi upo katika vyuo vya nje ambapo nchi zenye vyuo vina uatajiri wa viwanda.

Mollel amesema kuwa vyuo ambavyo anashirikiana na vina uwezo wa kutosha katika uzalishaji wa rasilimali watu katika sekta ya viwanda.Amesema kuwa wazazi wanaotaka kupeleka wanafunzi katika vyuo vikuu vya nje hawatajutia kutokana na mazingira wanayokwenda kusoma huko.

Mollel amesema kuwa wazazi na wanafunzi wafike katika ofisi zao ziko katika mikoa ya Dar es Salaam viwanja vya Saba saba , Dodoma , Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Arusha pamoja na nchi ya Zambia.

Amesema kuwa mwanafunzi atayekuwa anapitia katika wakala hiyo atapata uangalizi kwa muda wote masomo yake katika kuhakikisha mzazi kile anachokifanya kwa kijana wake hawezi kujutia.

Mollel amesema kuwa wazazi na wanafunzi wanaweza kufika katika ofisi zao kwa maelezo na jinsi kuwafanyia udahili wa papo kwa papo.
Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Global Education Link (GEL) Damaricy Peter akiwapa maelekezo wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Hati ya Kusafiria Passport , Abdul Milanzi akimsainisha fomu ya hati ya kusafiria mteja wa Global Education Link GEL leo katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional, Love Kumas akizungumza na mteja katika ofisi za Global Education Link (GEL) leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MBUNGE VITI MAALUMU CHADEMA ASAIDIA UJENZI MWANZA

$
0
0
Na Judith Ferdinand wa BMG, Mwanza
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani Mwanza Mhe. Susan  Maselle, ametoa shilingi milioni moja ili kuchangia ujenzi wa darasa la awali (chekechea) katika shule ya msingi Nyerere, Kata ya Igoma Jijini Mwanza.
Mhe. Maselle alitoa fedha hizo jana katika harambee ya kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika katika ukumbi wa Agape Lodge katika mtaa wa Nyerere Kata ya Igoma.
Alisema pamoja na juhudi za serikali kuboresha elimu, bado sekta hiyo haijafika pale panapohitajika ambapo alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wabunge kuona umuhimu wa kuchangia masuala ya kuboresha elimu kwa kujitoa na kuchangia kama alivyofanya yeye. 
 Aidha aliwaomba wazazi wenye uwezo kuchangia elimu ili kupata viongozi wa baadae na kuwajenga katika kusaidia na kujitoa katika jamii.
Katibu wa Baraza la Vijana Chadema BAVICHA mkoa wa Mwanza, Boniphace Nkobe, aliwasihi wadau wote kuungana kwa pamoja ili kukamilisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati ili wanafunzi waweze kusoma wakiwa darasani kama wanafunzi wengine.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Igoma Mashariki, Odoyo Lan’go alisema sera ya serikali katika elimu inamtaka mtoto kabla hajaanza darasa la kwanza (elimu ya msingi) awe amepitia elimu ya awali, hivyo wadau wanatakiwa kuchangia kukamilika kwa darasa hilo la awali

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mkoa Wa Mwanza Mhe.  Susan Maselle, akizungumza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa darasa la awali katika shule ya Msingi Nyerere Jijini Mwanza..

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mkoa Wa Mwanza, Susan  Maselle akiwa na wazazi, watoto na viongozi wa Mtaa wa Nyerere Jijini Mwanza.

KITAMBAA CHEUPE NA KING KIKII

Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images