Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live

TAMASHA LA USALAMA BARABARANI


IGP SIRRO AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA NA KUSISITIZA UWELEDI

$
0
0
Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amewataka askari wa Jeshi hilo kufanyakazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zitakazosaidia kujenga taswira chanya hasa wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.

IGP Sirro, ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na askari na maofisa wa mkoa wa Kagera, wakati akiwa kwenye muendelezo wa ziara zake zenye lengo la kujitambulisha pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao.

Alisema kuwa, kila askari analojukumu mbele yake la kuhakikisha suala la uhalifu na wahalifu linadhibitiwa hususan kwa kuimarisha usalama wa raia na mali zao huku wakizingatia kuwa, mkoa huo unapakana na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.

Hata hivyo, katika ziara yake, IGP Sirro, amewahakikishia askari na maofisa kuwa, yupo tayari kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kuwataka askari kuongeza kasi ya kukabiliana na matishio ya kiuhalifu na wahalifu ili kuifanya jamii kuishi kwa amani na utulivu.

Aidha, katika ziara hiyo, masuala mbalimbali yamejadiliwa huku mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu katika mkoa huo pamoja na wilaya zake zikiibuliwa kwa kuzingatia kuimarisha usalama wa raia na mali zao.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto), akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP) Augusine Ollomi, muda mfupi alipowasili, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.

JPM KUWASILI TABORA JUMAPILI-RC TABORA

$
0
0
Na Tiganya Vincent-RS_TABORA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kesho tarehe 23 Julai 2017 ,anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili mkoani hapa kwa ajili ya uzinduzi wa miradi ya mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisi kwake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alisema Mhe. Rais Dkt.Magufuli atawasili mkoani Tabora akitokea Kigoma ambapo wanatarajia kumpokea katika Wilaya ya Kaliua siku ya Jumapili .

Alisema kuwa mara baada ya kuwasili Wilayani Kaliua kuzindua uzinduzi wa barabara kutoka Kaliua hadi Kazilambwa na baadaye atapata fursa ya kuwahutubia wananchi.

Bw. Mwanri aliongeza kuwa akiwa njiani kuelekea Tabora Mhe Rais Magufuli atazinduza barabara ya Urambo hadi Tabora siku hiyo hiyo na ambapo pia atawahutubia wakazi wa Urambo na kisha kuelekea Tabora.

Alisema kuwa siku ya Jumatatu Rais ataweka Jiwe la Msingi ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kuja katika miji ya Nzega , Igunga na Tabora na baadae kuzindua upanuzi na ukarabati wa njia za kurikia Ndege katika Uwanja wa Tabora.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa siku hiyo hiyo ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atazindua barabara ya Tabora hadi Nzega na ile ya Tabora hadi Nyahua na mchana atawahutubia wakazi wa Tabora katika Viwanja vya Chipukizi.

Alisema ujio wa Rais Magufuli kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora ni sawa na usemi usemao Mgeni Njoo Mwenyeji Apone kwani zara yake mkoani hapa inazidisha matumaini kwa wakazi wa Mkoa wa Tabora na jirani zake ya kuendelea kufunguka milango au fursa mbalimbali za uchumi baada ya kuzindua miradi mbalimbali ya miundo mbinu.

Bw. Mwanri alitoa wito kwa niaba ya wananchi wa Tabora kuwakaribisha wananchi kujotokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Rais Magufuli.

ZSSF Yatiliana Saini na Banki Tpb Bank Utowaji wa Mikopo Kwa Wanachama wa ZSSF Zanzibar.

$
0
0
MKURUGENZI Mkuu wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi kushoto na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Jamii Zanzibar (ZSSF) Makame Mwadini wakitiliana saini makubaliano ya kutowa mikopo ya Kielimu na Kuazia Maisha kwa Wanachama wa (ZSSF)hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ZSSF kilimani Zanzibar, wakishuhudia Mwanasheria wa ZSSF Mohammed Fakih na Afisa Mawasiliano wa Tpb Bank Chichi Banda
Mkurgenzi Mkuu wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi kushoto akibadilishana mikataba wa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF kupata mikopo kupitia Banki ya Tpb Bank, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Mwadini Makame,  kuwawezesha kupata Mkopo wa Elimu ya Juu na kuaza maisha kwa Wanachama wa ZSSF, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Kilimani Zanzibar.wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa pande hizo mbili.
Maofisa wa Tpb Bank wakifuatilia mkutano huo wa utilianaji saini ya kutowa mikopo kwa Wanachama wa ZSSF Zanzibar kupitia benki hiyo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za ZSSF Kilimani Zanzibar.
Maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF wakifuatila mkutano huo wa utilianaji wa saini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MPIGA PICHA KAZINI

$
0
0
Mpiga picha wa kujitengemea ambaye jina lake halikupatikana haraka akimuweka sawa mteja wake wakati akimchukua picha kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama alivyokutwa na Kamera ya Globu jamii katika moja ya viunga vya Mji wa Dodoma mchana huu.
  Mteja keshakaa sawa na picha inapigwa.
muda mfupi baadae mteja mwingine kaingia.

ONYO KALI KWA WAUZA PEMBEJEO FEKI, HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA WATAKAOBAINIKA.

$
0
0

Wauzaji wa pembejeo ambao sio waaminifu wamepewa onyo kali na endapo atabainika yeyote anayewalaghai wakulima na kuwauzia pembejeo ambazo sio hali hatua kali dhidi yake zitachukuliwa.

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Beatus Chowaji ametoa onyo hilo wakati akizindua mradi wa Faida Mali unaoshirikiana na shirika la AMDT katika kuwasaidia wakulima wa alizeti Mkoani Singida ili kulima zao hilo kibiashara zaidi.

Chowaji amesema kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya wakulima ambao hukumbana na wauzaji wa pembejeo ambao sio waaminifu na kuwalaghai kwakuwa wakulima hao hawana elimu na uelewa hasa wa viuatilifu au mbegu ambazo ni halisi.

Ameongeza kuwa mkono wa serikali ni merfu na utawabaini popote walipo hivyo waache mara moja kwani kwa kufanya hivyo wanakirudisha nyuma kilimo cha alizeti ambacho ni tegemeo kwa ajili ya uchumi wa viwanda Mkoani Singida.

“Singida tuna Viwanda vya kuamua mafuta ya alizeti vikubwa viwili, vya kati vitatu na vidogo 115 na kufanya jumla ya viwanda vya alizeti kuwa 120, vyote hivyo vinategemea alizeti ya mkulima, lakini pia mkulima anakuwa na matarajioa makubwa, hao wauzaji pembejeo wasio waaminifu hatutawavumilia, tena waache mara moja”, amesisitiza Chowaji.

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida Beatus Chowaji akisoma bango mara baaa ya kuzindua mradi wa Faida Mali unaoshirikiana na shirika la AMDT katika kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida.

Mkurugenzi wa Shirika la AMDT Michael Kayombo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Faida Mali wenye lengo la kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida kulima kibiashara.

Baadhi ya wadau waliohudhuruia uzinduzi wa mradi wa Faida Mali wenye lengo la kuwasaidia wakulima wa Alizeti Singida kulima kibiashara.

Mkurugenzi wa mradi wa Faida Mali mkoa wa Singida Tom Silayo akisoma taarifa ya mradi huo kwa wajumbe waliohudhuria uzinduzi wa mradi utakaowasaidia wakulima kulima alizeti kibiashara.

Mtendaji Mkuu wa Chama cha wasindikaji wa Mbegu za alizeti Tanzania Daud Musa Mwasantaja akiwahakikishia wakulima wa alizeti upatikanaji wa soko katika uzinduzi wa Mradi wa Faida Mali.


Serikali Yapongezwa kwa Kuwaleta Pamoja wadau wa Mazingira na Wazalishaji Mifuko ya Plastiki

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Wadau wa Mazingira na Wazalishaji wa Mifuko ya Plastiki hapa nchini wameipongeza Serikali kwa kuwakutanisha pamoja ili kujadili kuhusu matumizi ya mifuko ya plastiki na kutoa maoni yao kwa Serikali juu ya kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira.

Akizungumza wakati akifungua kikao cha wazi cha kupokea maoni ya wadau kuhusu dhamira ya Serikali kupiga marufuku uzalishaji, uuzaji, usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema dhamira ya Serikali ni kupata maoni ya wadau na wazalishaji wa mifuko hiyo ili Serikali ifanye tathmini kabla ya kuchukua hatua na kuweka mazingira yatakayowezesha utekelezaji wa Sheria ya Mazingira kwa kila mdau.

“Changamoto imekuwa kubwa katika matumizi ya mifuko ya plastiki katika swala la mazingira kwani tumeshuhudia miundo mbinu yetu ikiathirika, mifugo na hata viumbe vya baharini na kwa mujibu wa tafiti kuna hatari baadae mifuko hii ikawa mingi zaidi baharini kuliko samaki” Alisisitiza Makamba.

Akifafanua Makamba amesema kuwa Serikali imeona ni vyema ikakutana na wadau ili ipate maoni yao kwa kuzingatia kifungu cha 178 cha Sheria ya Mazingira kinachotaka wananchi na wadau kushirikishwa na kupata taarifa kuhusu maswala ya mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifungua Kikao cha Wazi cha kupokea maoni ya wadau kuhusu dhamira ya Serikali kupiga marufuku uzalishaji,uuzaji,usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustine Kamuzora akiongea wakati wa ufunguzi wa Kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.

Sehemu ya wadau walioshiriki kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mjadala na maoni ya washiriki .(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo).

WAZIRI UMMY AZINDUA ZAHANATI NGUVUMALI JIJINI TANGA

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katika akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Zahanati ya Kata ta Nguvumali leo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa na wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Said. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katika akisisitiza jambo kwa Muuguzi wa Afya wa Zahanati ya Nguvumali baada ya kuizindua kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo,Dkt Ally Bughe 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa na kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nguvumali na wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF)Alhaj Mussa Mbaruku 
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia uzinduzi huo
Waheshimiwa madiwani kutoka Kata mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia uzinduzi huo.


VYUO NA VYUO VIKUU-UVCCM WAMKINGIA KIFUA RAIS.DK MAGUFULI

$
0
0
Na Nassir Bakari

Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kupitia Idara yake ya Vyuo na Vyuo vya Elimu ya Juu, umemkingia kifua Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli ukisema kwamba hafanyi uteuzi kwa njia za kibaguzi bali anafanya hivyo kwa kuzingatia weledi na uwezo wa anayemteua.

UVCCM imesema, hayo leo jijini Dar es Salaam, na kupinga vikali kauli iliyotolewa hivi karibuni na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, kwamba Rais Dk. Magufuli amekuwa akifanya uteuzi kwa kuzingatia ubaguzi wa ukanda, ukabila, dini na jinisa.

Akifungua Kikao cha kazi cha Viongozi wa Vyuo na Vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu- UVCCM, Daniel Zenda alisema, UVCCM kupitia Idaya yake, inapinga na kulaani vikali kauli hizo za Tundu Lissu kwa sababu ni kauli za hatarai kwa kuwa zina lengo la uchochezi, kudhalilisha na kugawa Wananchi kwa misingi ya kibaguzi.

"Ndugu Watanzania kauli hii ya Tundu Lissu ni yenye lengo la kuchonganisha, kudhalilisha na kuwagawa wananchi, Sisi Vjana wa Vyuo na vyuo Vikuu, tunalaani kwa nguvu zetu zetu kauli hii. Kwa mfano ukitazama uteuzi wa Mkuu wa Majeshi nchini anatoka Bara, lakini hupo chini ya Waziri wa Ulinzi Dk. HusseinMwinyi ambaye anatoka Zanzibar", sasa hapo ubaguzi unakujaje", alisema na kuhoji.

Kaimu Katibu Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu-UVCCM Daniel Zenda akizungumza wakati wa kikao cha kazi na viongozi wa Vyuo na Vyuo Vikuu mkoa wa Dar es Salaam, leo .



Kaimu Katibu Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu-UVCCM Daniel Zenda (kulia) akiongoza kikao cha Kazi cha Viongozi wa Vyuo na Vyuo Vikuu-UVCCM mkoa wa Dar es Salaam, leo katika ukumbi wa jengo la Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar s Salaam. PICHA NA BASHIR NKOROMO .

SH. BILIONI 1.669 KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI ILEJE-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga sh. bilioni 1.669 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya ya Ileje mkoani Songwe.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Julai 22, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Itumba.

Waziri Mkuu amesema kati ya fedha hizo sh. bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika miji miwili ya Isongole na Itumba wilayani Ileje.“Kiasi kingine cha sh. milioni 669 kimetengwa kwa ajili ya maji katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ileje katika mwaka wa fedha wa 2017/2018. 


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa jengo la hospitali ya wilaya ya Ileje akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe, Julai 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kushoto) wakitazama mbegu za mahindi zinazozalishwa na Kikundi cha SAM cha Ileje wakati alipotembelea banda la kikundi hicho kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje Julai 22, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vifaranga wa samaki wakati alipotembelea banda la Kikundi cha wanawake cha Tukazane cha Ileje  kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje Julai 22, 2017.
 Baadhi ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na taasisi binafsi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao mjini Ileje Julai 22, 2017.

JAJI UPENDO MSUYA AZIKWA LEO KWENYE MAKABURI YA KINONDONI, JIJINI DAR

$
0
0
Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya enzi za uhai wake.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Prof. Ibrahim Juma (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa wakiwa wamejipanga tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya aliyewaki kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, tayari kwa mazishi yake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam leo
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya aliyewaki kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, likishushwa kaburini wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam leo
Askari Polisi wakitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya aliyewaki kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam leo.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Prof. Ibrahim Juma akiwa na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakishiriki mazishi ya Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya aliyewaki kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam leo
Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto mstari wa mbele) akishiriki mazishi ya Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya aliyewaki kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam leo

MBUNGE WA KIGOMA MJINI MHE. ZITTO KABWE AMFAGILIA RAIS MAGUFULI KWA KUFUFUA MRADI MKUBWA WA MAJI TOKA ZIWA TANGANYIKA

PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula (wa pili kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, katika hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika Hospitalini hapo, Julai 22, 2017. Wengine pichani ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge (katikati), Mjumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Sarah Mwaga (wa pili kulia) pamoja na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Caroline Damian. Mfuko huo umetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 99 kwa hospitali 16 hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Zainab Chaula (wa nne kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) wakiangalia moja ya vitanda vya kujifungulia wakina mama, vilivyotolewa na Mfuko huo, kwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017.
Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, katika hafla fupi ya makabidhiano msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano msaada wa vifaa tiba vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Julai 22, 2017. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAGIC FM BAMIZA TOP 20 COUNT DOWN JULY 22, 2017

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI WA MKOA WA KIGOMA

$
0
0

 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji toka Ziwa Tanganyika toka kwa mhandisi mshauri wa mradi huo ndugu Michael Mwamkinga 


 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Waziri Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe pamoja  na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi  wa mradi wa maji toka ziwa Tanganyika 

  Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Waziri Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe pamoja  na viongozi wengine akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi  wa mradi wa maji toka Ziwa Tanganyika 

  Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Mamia ya Wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. 
 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli,akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Bulombora Kikosi cha 821KJ. 
Maelfu ya waanchi wakimsikiliza Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati akiwahutubia a katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. 

 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania DktJohn Pombe Joseph Magufuli akisoma mabango baada ya kuhutubia  katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania DktJohn Pombe Joseph Magufuli akiwatuliza wananchi wakati akisoma mabango baada ya kuhutubia  katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma

Umati wa wananchi uliojitokeza kumsikiliza Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania DktJohn Pombe Joseph Magufuli  katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. PICHA NA IKULU
                               Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

MAGAZETI YA JUMAPILI EO LJULAI 23,2017

BALOZI KAMALA ATAKA WAKANDARASI WANAOPEWA MIRADI MISSENYI KUIKAMILISHA VIZURI

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala amewataka wakandarasi wanaopewa kutekeleza miradi ya maendeleo wilaya ya Missenyi kukamilsha miradi kikamilifu vizuri na kwa wakati. Balozi Kamala anaonekana akikagua ukarabati wa zahanati ya kata Kakunyu. Balozi Kamala amekataa kupokea mradi wa ukarabati wa zahanati hiyo baada ya kuambiwa umekamilika wiki mbili zilizopita.

ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBAINI WA UFISADI

$
0
0
KUKAMILIKA kwa mchakato wa uaandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutasaidia kuweka misingi imara na kuondoa changamoto zilizopo katika Katiba ya sasa, hivyo kukomesha ufisadi na kuinua uchumi wa Tanzania.

Aidha, kukamilika huko kwa Katiba Mpya kutaakisi jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, ambaye alimtaka Rais Magufuli kuumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, kwani alisema mbali ya kuakisi kasi yake anayoifanya ya kukuza uchumi pia kutasaidia kuhimiza uwajibikaji.

“Wakristo na Watanzania kwa ujumla tuna imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano na ni matarajio yetu kwamba mchakato wa kuandika Katiba utamalizwa kama lengo lilivyokuwa,” alisema. 

Askofu Gaville amesimikwa ili kuchukua nafasi ya Askofu Dkt. Owdenburg Mdegella ambaye amestaafu.Alisema wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dkt. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote. 
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville (kushoto).
Askofu Blaston Gaville wakati akiwekwa wakfu kuongoza Dayosisi ya Iringa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). 

UBALOZI WA JAPAN NCHINI WAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI MBALIMBALI YA KIMAENDELEO MKOANI IRINGA

$
0
0
UBALOZI wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli. 

ubalozi huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa Bweni hilo la wanafunzi shule ya sekondari ya Idodi Iringa balozi Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania. 

Alisema kuwa hatua Japan kufika kusaidia ujenzi wa bweni hilo katika shule ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Ismani Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aliloomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali kuteketea kwa Moto.

"waziri Lukuvi lileta maombi ya mradi wa kujengewa miradi hiyo ya maendeleo ambayo ni Hostel ya wasichana shale ya wasichana Ismani ambayo ilijengwa toka mwaka 2005 na mwaka2008 kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika zahanati ya Mlowa... namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi hiyo"
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo
Vitanda vilivyopo katika bweni hilo 
Hili ndilo bweni la kisasa lililojengwa na ubalozi wa Japan nchini 
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akikabidhi taa za mionzi ya jua kwa mkuu wa shule ya sekondari Idodi kulia kwake ni mbunge wa Isiman Wiliam Lukuvi na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na katibu wa CCM Iringa vijijini Dodo Sambo 

MSANII BONGO FLAVA AT MFALME WA MIDUARA BONGO, MR TZ WANOGESHA RAHA ZA PWANI COLLEGE PARK, MARYLAND

$
0
0

Msanii wa Bongo flava na mfalme wa miduara AT, akiongelea utamaduni wa kiswahili na raha za pwani kwenye jopo la kongamano la raha za pwani kwa lengo la kudumisha na kutangaza utamaduni wa Mswahili na lugha yake.na baadae kuonesha onesho kali ya nyimbo zake zilizotamba na zinazoendelea kutamba kwenye anga ya bongo na kimataifa. Kongamano hilo linaloambatana na tamasha la Mswahili na lugha yake huandaliwa na Swahili Media Network na hufanyika mara moja kila mwezi. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production.

Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT akichengua mashabiki wake kwa wimbo mmoja wapo wa mduara.

Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT usipime ni balaa

Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye  jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 Hampton Inn, College Park, Maryland.

Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye  jopo la kongamano la raha za pwani.

KUONA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live




Latest Images