Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

ELIMU SAHIHI ITUMIKE KWANZA KABLA YA MATUMIZI YA SHERIA KWA WAKEKETAJI

$
0
0
Elimu sahihi juu ya madhara ya ukeketaji ya muda mfupi na mrefu inatakiwa itolewe kwa jamii kabla ya kuwachukulia hatua baadhi yao wanaoendelea kufanya vitendo vya ukeketaji licha ya uwepo wa sheria kali.

Rai hiyo imetolewa mapema leo na Mratibu wa Mradi wa Kupinga Ukeketaji (WOWAP) Nasra Suleiman katika semina ya kupinga Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya Msange Wilayani Singida, kwa ushirikiano wa Ofisi ya Ustawi wa Jamii Mkoa wa Singida na mradi huo kwa ufadhili wa shirika la WAAF-Japan.

Mratibu huyo amesema nguvu ya sheria itasaidia kuondoa ukeketaji endapo wananchi wengi watakuwa na uelewa wa kutosha juu ya madhara ya ukeketaji na kuamua kwa hiyari kuachana na mila hiyo.

“Sheria isiwe nguvu pekee ya kupambana na ukeketaji, tukifanya hivyo itafikia kipindi tutakwama kwa kiasi kikubwa kwa kuwa watu wataendelea kukeketa kwa kificho ili wasikamatwe, lakini kila mwana jamii akiwa na elimu ya kutosha ya madhara hayo, nguvu ya sheria itatumika tu kwa wachache watao kaidi”, amesisitiza Nasra.

Ameongeza kuwa Watendaji wa kata na vijiji wana uwezo mkubwa wa kubadilisha mtazamo na mila ya ukeketaji kwa kuelimisha wananchi wao hasa baada ya semina zinazoandaliwa na miradi au mashirika Fulani kwakuwa zinawajengea uwezo ili waweze kutoa elimu sahihi na mbinu za kuelimisha.

Nasra amesisitiza kuwa jukumu la elimu lisiachwe kwa sekta binafsi kama mradi wake wa WOWAP pekee bali liwe jukumu la jamii nzima huku akifafanua kuwa elimu inayotakiwa kutolewa ni ile inayoelezea madhara ya ukeketaji na sio kuwakataza kwa kigezo cha kutii sheria pekee.
 Mzee maarufu na mwenyeji wa Msange Bi Greta Musa Nyonyi akichangia hoja katika semina ya kupinga Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya Msange Wilayani Singida.
 Mratibu wa Mradi wa Kupinga Ukeketaji (WOWAP) Nasra Suleiman akizungumza na washiriki wa semina ya kupinga Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya Msange Wilayani Singida.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Msange Magni Oisso akichangia hoja katika semina ya kupinga Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya Msange Wilayani Singida.
 Washiriki wa semina ya kupinga ukeketaji iliyoandaliwa na Mradi wa WOWAP wakifuatilia kwa umakini filamu fupi ya Ukeketaji iliyofanyika katika Kata ya Msange Wilayani Singida.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA MAJI AFANYA ZIARA CHALINZE

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza jambo wakati wa ziara yake  ya kukagua hatua iliyofikiwa katika mradi wa ukarabati  na upanuzi wa mtambo wa maji chalinze na na ujenzi wa mfumo wa kusafirishia maji pamoja na matenki yakuhifadhia maji. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA)Mhandisi Christer Mchomba na kushoto ni Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya WAPCO inayotekeleza mradi huo.
Mafundi wakiendelea na Kazi ya ujenzi wa matanki ya kuhifadhi na kusambaza maji katika Jimbo la Chalinze.
Baadhi ya mitambo ikiwa katika moja ya maeneo unakotekelezwa mradi  huo utakaonufaisha wakazi wa Jimbo la chalinze na sehemu ya Wilaya ya Handeni.
Sehemu ya mabomba yakiwa katika moja ya maeneo unakotekelezwa mradi huo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe (wapili kushoto) akioneshwa ramani ya mradi huo na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wake wakati wa ziara yake  ya kukagua mradi huo  wa ukarabati  na upanuzi wa mtambo wa maji chalinze na na ujenzi wa mfumo wa kusafirishia maji pamoja na matenki yakuhifadhia maji.

(Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO)

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI MKUTANO MKUU WA ALAT TAIFA JIJINI MBEYA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Alat Taifa ,Gulamhafeez Abubakar Mukadam akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Mkutano mkuu wa Alat Taifa unaotarajia kufanyika Jijini Mbeya Mwezi ujao,  ambao Rais Dkt John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi ,kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Alat ,Stephene Mhapa akifuatiwa na Diwani wa kata ya Maboga Iringa Veny Muyinga
 Kaimu Katibu Mkuu wa -Alat Abdallah Shaban akizungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo juu ya mkutano Mkuu wa Taifa wa Alat
 Makamu Mwenyekiti wa Alat ,Stephene Mhapa  akisisitiza jambo kwa Wandishi wa habari juu mkutano mkuu wa taifa utakao fanyika Jijini Mbeya Mwezi ujao Mwaka huu.

CHAMA CHA WAPANGAJI CHAWAJIA JUU MADALALI WASIO JISAJILI KATIKA MFUMO WA KAMPUNI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Wapangaji nchini Dumey Mukama akizungumza na Waandishi wa habari juu ya tamko lao la kupinga Madalali ambao hawajasajiliwa katika mfumo wa kampuni ,ambao wamekuwa kero kwa wanachama wao.
Mwanasheria wa Chama cha Wapangaji nchini, Pamela Kihumo akisisitiza jambo juu ya hatua watakazochukua kwa madalali wote ambao awajajisajiri katika mfumo wa makampuni katika kuendesha biashara ya upangishaji nyumba
Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwa makini katika kuchukua taharifa hiyo kutoka chama cha Wapangaji ndani ya ukumbi wa idara ya haabari maelezo.

JAFO:TUNATAKA KASI KATIKA UTEKELEZAJI MIRADI

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka wakandarasi wa ujenzi wa miundombinu ya barabara na majengo katika halmashauri zote nchini kuzingatia mikataba ya ujenzi, huku akiwaonya tabia ya kuchelewesha kukamilisha miradi kwa wakati.

Jafo aliyasema hayo katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya barabara na madaraja wilayani Kisarawe.Amesema Ofisi ya Rais, Tamisemi haitofumbia macho wakandarasi ambao wameshinda tenda za ujenzi na kuonesha uwezo mdogo.

“Pia hatutafumbia macho ucheleweshaji wa miradi bila sababu yeyote ya msingi kinyume na matarajio yaliyoainishwa ndani ya mkataba,”amesema Jafo.

Naibu Waziri Jafo katika ziara zake hivi karibuni ikiwemo ujenzi wa daraja la Twangoma lililopo wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam amekuwa akisisitiza wakandarasi kuzingatia ubora wa madaraja yanayojengwa  nchini ili yaweze kudumu kwa muda mrefu. 

Jafo amemaliza ziara yake leo wilayani Kisarawe na anatarajia kuendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro, Songwe, Njombe, Singida, Tabora, Kagera, Mwanza na Mara.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wataalam wa ujenzi wa daraja la Kologombe linalounganisha Kijiji cha Gwata na Dololo wilayani Kisarawe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za mji wa Kisarawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata maelekezo kuhusu ujenzi wa barabara ya kisarawe mjini kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri Mbena.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa daraja la Kologombe wilayani Kisarawe.

CHINA YAIJENGEA UWEZO IDARA YA FORODHA YA TANZANIA

$
0
0
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam.

Kiwango cha biashara kati ya Tanzania na China kimefikia Dola bilioni 4.7 katika kipindi cha mwaka 2015 na kwamba kiwango hicho kinatarajiwa kuongezeka zaidi.

Mwakilishi Mkuu Mkazi wa Masuala ya Uchumi na Biashara, kutoka Ubalozi wa China hapa nchini, Bw. LIN Zhiyong, amesema hayo Jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya forodha kuhusu Maboresho na Vihatarishi hatari vya kiforodha, yanayotolewa kwa maafisa wa forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na wataalamu kutoka Chuo cha Forodha cha Shanghai-China.

Bw. Zhiyong amesema kuwa uhusiano wa Tanzania na China ni wa kihistoria na kwamba hivi karibuni nchi yake iliipatia Tanzania seti 3 za makontena ya vifaa vya kisasa kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam, vyenye uwezo mkubwa wa kugundua pembe za ndovu, dawa za kulevya na silaha zinazosafirishwa kimagendo kutoka ndani na nje ya nchi.

 Alisema pia kuwa hivi sasa nchi yake ni kama imeondoa kabisa kodi kwa bidhaa za Tanzania zinazosafirishwa kwenda China hadi kufikia asilimia 97, na kwamba anatarajia kuona wafanyabishara wa Tanzania wakichangamkia fursa hiyo na kuongeza kiwango cha bidhaa za Tanzania zenye ubora zinazosafirishwa kwenda nchini mwake.

Bw. Zhiyong, amezishauri Idara za Forodha za Tanzania na China kuimarisha ushirikiano na kukuza biashara na uwekezaji kwa faida ya pande zote mbili.
 Naibu Kamishna wa Forodha na Maboresho ya Vihatarishi Hatari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. James Mbunda, akizungumza na na watoa mafunzo ya Takwimu na Udhibiti Vihatarishi hatari vya Forodha, yanayotolewa na Chuo cha Forodha cha Shanghai-China, Jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Mwakilishi Mkazi wa Ubalozi wa China anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Bw. Lin Zhiyong.
 Naibu Kamishna wa forodha na Maboresho ya Vihatarishi Hatari wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. James Mbunda (Kushoto) na akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Ubalozi wa China anayeshughulikia Uchumi na Biashara, Bw. Lin Zhiyong, wakati wa kufungua mafunzo kuhusu Takwimu na kudhibiti Vihatarishi hatari vya Forodha, yanayotolewa na Chuo cha Forodha cha Shanghai-China, Jijini Dar es Salaam.


 Mkufunzi Mkuu wa masuala ya forodha kutoka Chuo cha Forodha cha Shanghai, China, Profesa Sun Hao (kulia) akizungumza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya siku 14 ya maafisa wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dae Salaam.

 Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Grace Sheshui akiwakaribisha watoa mafunzo ya Takwimu na Udhibiti Vihatarishi hatari vya Forodha, yanayotolewa na Chuo cha Forodha cha Shanghai-China, Jijini Dar es Salaam.
 Maafisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na wengine (kulia) na wakufunzi wa Takwimu na Udhibiti Vihatarishi hatari vya Forodha wakisikiliza maelezo ya awali wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UVUVI USIO RASMI KATIKA BONDE LA JANGWANI JIJINI DAR

$
0
0
 Katika pita pita ya leo, Kamera ya Glogu ya Jamii imezinasa taswira za vijana hawa (majina yao hayakupatikana kwa haraka) wakiwa katika eneo la Bonde la Jangwani jijini Dar es salaam wakivua samaki ambao haikufahamika kwa haraka ni wa aina gani, katika maji mengi yaliyotuwama katika eneo hilo. Uvuvi wa aina hii katika maji hayo unaweza kuhatarisha afya yao kwa kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu na Kichocho. 
 Vijana hao wakiendelea kusaka vitoweo.
Wakitega nyavu.

PROFESA MWANDOSYA AMZUNGUMZIA MAREHEMU LINA GEORGE MWANDOSYA


INTRODUCING: MBIGILI BY NAS B Ft. JAY MALLEY

SHAKA APONGEZA WAGANGA NA WAUGUZI MKOANI KIGOMA

$
0
0
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema serikali ya awamu ya tano itaendelea kuwajali na kuwahudumia wagonjwa kwa kupeleka idadi ya waganga, wauguzi, dawa na utoaji wa vifaa tiba katika zahanati vituo vya afya na hospitali za wilaya nchini .

Pia Serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha katika kila Kata na Wilaya kunajengwa zahanati na vituo vya afya ili kunusuru pia kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano .

Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipotembelea katika kituo cha Afya cha kijiji cha Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma katika siku ya pili ya ziara yake kuona utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm katika maendeleo ya kisekta.
Shaka alisema serikali ya Chama Cha Mapinduzi zina wajibu wa kufuatilia kwa karibu na kujua kama yale yote yalioahidiwa katika ilani , yanayotimizwa na iwapo yanawafikia na kuwahudumia wananchi kama inavyokusudiwa na serikali Kuu kwa wananchi wake. 

Alisema pamoja na kukabiliwa na upungufu wa idadi ya Waganga na Wauguzi katika Kituo cha Afya Nguruka, waliopo wamekuwa wakijituma bila kuchoka huku wakitoa huduma kwa njia makini na sahihi ili kunusuru na kutibu wagonjwa . 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SONGWE, AMPA MIEZI MIWILI DED SONGWE KUBADILI UTENDAJI WAKE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa miezi miwili kuanzia leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe, Bw. Elias Nawera abadili mwenendo wake kiutendaji na ashirikiane vizuri na  Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Samwel Jeremiah.

Amesema Serikali ya awamu ya Tano inawataka watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuheshimiana na atakayeshindwa kufanya hivyo hatavumiliwa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Julai 20, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Songwe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.

Amesema watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yaweze kufikiwa. Pia waheshimiane sehemu za kazi na kila mtu azingatie mipaka ya madaraka yake.

"Mkurugenzi hapa hamsikilizi Mkuu wa wilaya anaondoka kituo cha kazi bila ya kuaga na amewagawa wakuu wa Idara. Namtaka afanye mabadiliko ya utendaji wake ndani ya miezi miwili na Mkuu wa Mkoa fuatilia jambo hili."

Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote wasimamie utendaji wa wakurugenzi wa Halmashauri kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.”Serikali hii si ya mchezo. Serikali hii inahitaji watumishi waadilifu wa kuwatumikia Watanzania.”

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bibi Chiku Galawa amesema wamejipanga kuhakikisha changamoto zote zinazoukabili mkoa zinaboreshwa pamoja na kufikia malengo ifikapo 2020.

Ametaja malengo hayo kuwa ni kuhakikisha mkoa huo unakuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato, kila mwananchi awe na bima ya afya pamoja na kuwa na hospitali katika kila wilaya.

Kuhusu mpango wa Serikali wa kuwa na uchumi wa viwanda amesema tayari wameshaanzisha viwanda vya maziwa, kukamua alizeti ikiwa ni kuunga mkono mpango huo.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe, Elias Nawela  baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. 
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimia wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  (kulia) alipozungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini  kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha  Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 20117. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini wa mkoa wa Songwe kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkewe Mary na Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA MUWEKEZAJI WA MKONGE MKOANI TANGA.

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesimamisha umiliki wa mwekezaji wa mashamba ya katani yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited yaliyopo kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Waziri Lukuvi amefikia uamuzi huo baada ya wakazi wa eneo hilo kuzuia msafara wake na kupata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hao na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto wakimlalamikia Waziri kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro kwa awakazi wa Mnazi.

Baada ya kupokea malalamiko hao Waziri Lukuvi aliamua kutembelea mashamba hayo na kuyakagua ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wamekuwa wanakabiliwa na mgogoro huu kwa miaka mingi.

Baada ya kutembelea na kujiridhisha Waziri Lukuvi amesema kwamba shamba hilo linastahili kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkoa wa Tanga na ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki ameshindwa kuwa na sifa za umiliki kwa kuwa hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004, hajalipa wafanyakazi wake kwa muda mrefu, miundombinu yake na mazingira ya kazi hayaridhishi na ameshindwa kuliendeleza shamba hilo tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo ileile ya mkoloni ya mwaka 1937.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa kata ya Mnazi wilaya ya Lushoto mkoni Tanga waliozuia msafara wake na kumpa malalamiko kuhusu mashamba matatu yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro.  
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua miundombinu na mazingira ya kazi ya mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997. 
Mazingira ya shamba yaliyotelekezwa na mmiliki wake wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997. 
Baadhi ya mitambo iliyochakaa ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937. 
Baadhi ya mitambo iliyochakaa ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937.

NANO ENERGIZER NOW IN TANZANIA / KICHOCHEO CHA NANO SASA KINAPATIKANA TANZANIA

$
0
0
Kwa ajili ya kuikarabati na kuipa ulinzi Injini na gearboxya gari yako bila kuifungua. Huziba mikwaruzo yote ndani ya Injini na gearboxna kuirudisha nguvu ya Injini kama ilivyokuwa mpya. Hupunguza matumizi ya mafuta 5%hadi 21%. Huongeza nguvu ya Injini na hutoa ulinzi wa Injini hadi kufikia kilomita 40,000. Hupatikana kwa injini na geabox za aina zote.
Hupatikana kwa aina zote za magari, Compressor, Jenereta,Bajaji na Pikipiki
KIMETHIBITISHWA NA:
SHIRIKA LA UBORA LA KIMATAIFA – ISO
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA – TBS
MKEMIA MKUU WA SERIKALI TANZANIA
KIMEPENDEKEZWA NA WATENGENEZAJI MAGARI:
TOYOTA
MERCEDES BENZ
GM DAEWOO
VOLVO
HONDA
HYUNDAI
AUDI
KIMEFANYIWA MAJARIO NA KUTHIBITISHWA NA TAASISI:
CHUO KIKUU CHA TAIFA KYUNGPOOK - KOREA
CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA SEOUL - KOREA
TAASISI YA MASHINE NA VIFAA YA KOREA
CHUO KIKUU CHA YEUNGNAM - KOREA
TAASISI YA KOREA YA TEKNOLOJIA YA MAGARI
JESHI LA ULINZI LA TAIFA LA KOREA
KITUO CHA JESHI LA ANGA LA INDIA
KIMETENGENEZWA NA NANO TECH INTERNATIONAL KOREA KINASAMBAZWA NA POWER ENERGY ENGINEERING LTD:
KWA MAWAKALA WASILIANA NASI KWA NAMBA ZIFUATAZO
                               0715 480174 / 0719346060
INAPATIKANA:
UBUNGO MATAA JENGO LA OILCOM - O715 480174
MWENGE JAPAN AUTO SPARE (MARRYLAND BAR) -  0714 363637
BK JAPAN AUTO SPARE PARTS SEGEREA STAND - 0653 519653
KARIAKOO - DUBAI TRADERS, LUESHA GENERAL (KISANGANI), ZANLUB

MWANZA - LIBERTY (MKABALA NA COCONUT HOTEL) - 0626 450450

NAIBU WAZIRI MPINA AFANYA ZIARA USIKU KUBAINI UHARIBIFU WA MAZINGIRA UTOKANAO NA UCHIMBAJI WA MCHANGA.

$
0
0
NA EVELYN MKOKOI

Katika hali isiyoya kawaida, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amefanya ziara ya Oparesheni maalum kwa kushirikiana na jeshi la Police kitengo cha FFU ili kuweza kubaini uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa uchimbani na uchotaji wa mchanga katika vyanzo vya maji na maeneo mengine.

Akiwa katikati ya Mto Mpigi uliopo katika mpaka wa Dar es salaam na Bagamoyo usiku wa kuamkia leo, naibu Waziri Mpina alisema kuwa watu wanaochimba na kuchota mchanga kiholelea watachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kwa mujibu wa sheria, kutaifishwa kwa magari yao na hata kufikishwa mahakamani.

“kama mnavyoona hapa na kama tulivyosikia kutoka kwa mtu wa DAWASA haya mabomba ya maji yanayopita katika mito yanaharibika kutokana na shughuli hizi na serikali inaweza kuingia gharama kubwa sana kurekebisha mabomba haya kama bomba hili Mtaalam amesema hapa itagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80 kutengeneza bomba hili.” Alisema Mpina.

Aidha Mpina alisema ukiachilia mbali uharibifu wa Miundo Mbinu hiyo ya Maji pamoja na Mazingira wananchi wnaweza pia kukosa maji kwa takribani muda wa wiki mbili.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwa na mchanga mkononi akiwasikiliza maafisa wataalam katikati Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye pia ni katibu wake Bw. Daniel Sagata, na kulia ni Afisa kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenge akieleza kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi kati kati ya mto Mpigi katika eneo la Mpaka wa Bagamoyo na Dar es Salaam, ambapo uharibifu huo Umeharibu eneo ambapo limepita Bomba kubwa la maji safi (halipo pichani) linalo safirisha maji kutoka Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini na kuhudunia seheu ya mkoa mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam, Bomba ambalo lipo hatarini kuharibika.
Afisa Mtaalam kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenje (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Sehemu ya mto Mpigi ( haipo Pichani, iliyoharibiwa vibaya kutokana na shughuli za uchimbaji wa mchanga. (Picha na Evelyn Mkokoi)

RC SHINYANGA AKUTANA NA WAWEKEZAJI NA WAFANYABIASHARA WA MKOA WA SHINYANGA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amekutana na wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kufahamiana na kujadili mambo kadha wa kadha ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mkoa wa Shinyanga.


Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga.


Akizungumza katika kikao hicho,Telack alisema huu ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2016/2017 – 2020/2021 wenye dhima ya kujenga uchumi wa viwanda ili kuchochea mageuzi ya maendeleo ya watu.


“Ili kutimiza malengo ya mpango huu lazima serikali ifanye kazi kwa ushirikiano wa karibu na sekta binafsi na nyinyi ni sehemu ya sekta binafsi na ili kudumisha ushirikiano huo serikali imeanzisha mabaraza ya biashara katika ngazi ya taifa,mikoa na wilaya”,alieleza Telack.


Aidha alisema uwekezaji ni moja ya shughuli zinazochochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla ambapo hadi sasa mkoa huo una jumla ya viwanda 81,ambapo viwanda vikubwa ni 18,viwanda vya kati 9 na vidogo 54.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba yake wakati wa kikao chake pamoja na wawekezaji na wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Julai 20,2017.
Wafanyabiashara,wawekezaji na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwa ukumbini 
Kaimu Mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga Jackton Koy akizungumza katika kikao hicho. 
Kikao kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akichangia hoja katika kikao hicho .

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UHAMISHO WA WATUMISHI WA UMMA UFANYIKE KWA MAKINI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amezitaka Taasisi za Serikali kuratibu suala la uhamisho wa watumishi wa umma kwa makini pale inapohitajika kufanya hivyo Ili kuepuka kero na usumbufu kwa watumishi. 

Waziri Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala eneo la Segerea, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kairuki amesema uhamisho lazima ufanyike kwa mtumishi wa umma endapo kukiwa na sababu za msingi sana. “Naomba ieleweke kuwa uhamisho una taratibu zake hivyo kila mwajiri ni mwajiri akazifuata.” Mhe. Kairuki alisisitiza.

Ameongeza kuwa imebainika wapo baadhi ya watumishi wa umma wanawasilisha sababu mbalimbali kwa waajiri kuomba kuhama wakiwa na nia ya kukwepa kukaguliwa sifa zao za elimu. 
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Segerea alipofanya ziara ya kikazi  ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw. Edward Mpogolo akiwatambulisha baadhi ya watumishi na viongozi wa Segerea waliohudhuria kikao kazi kilichowakutanisha na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) Jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Jimbo la Segerea, Mhe. Bonnah Kaluwa akitoa salamu wakati wa kikao kazi na kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), leo Jijini Dar es Salaam.  
 Mkazi wa Segerea, Bw. Juma Kali akiwasilisha hoja maalum wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala - Segerea  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SADC Kuendelea Kusimamia Amani Katika Nchi Wanachama

$
0
0
Na. Bushiri Matenda- MAELEZO

Serikali ya Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhakikisha kunakuwa na amani na mshikamano miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Jumuiya hiyo leo Jijijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga alisema kuwa Tanzania itaendeleza jitihada zinazofanywa na SADC kwa nchi wanachama katika kuendelea kuimarisha  Ushirikianao katika Siasa, Ulinzi na Usalama.

“Nawasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wetu wa SADC ambaye anaamini kuwa mkutano huu unatuleta pamoja katika kujenga ushirikiano wetu zaidi kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa na amani, umoja, mshikamano na ustawi kati ya nchi wanachama,” alisisitiza Dkt. Mahiga

Dkt. Mahiga alisema kuwa nchi wanachama zimeendelea kuwa eneo lenye usalama na ustawi kwa kuzingatia hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na umoja huo kupitia kamati mbalimbali zilizoundwa kushughulikia mageuzi katika nchi za Lesotho hali iliyosaidia Taifa hilo kufanya uchaguzi wa wabunge mwezi June 2017 kwa amani. 
 Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dr. Stergomena Tax akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa 19 wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya hiyo inayojadili ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama mapema hii leo Jijini Dar es SalaamA.
 Waziri wa Mambo ya nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (hawapo pichani) wakati akifungua mkutano wa 19 wa Kamati hiyo unaojadili ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama mapema hii leo Jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa 19 wa Kamati hiyo unaojadili ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama mapema hii leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa – MAELEZO)

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KAMANDA MKONDYA AWATAKA MAJAMBAZI WALIOMALIZA VIFUNGO VYAO KUJISALIMISHA

FEMINA HIP NA NGUVU YA BINTI

$
0
0
Ni muda wetu sasa! Ndio ni muda wetu. Karibu katika Jukwaa la Nguvu ya Binti  2017, litakalounganisha mabinti, vijana na jamii kwenye mijadala inayomtazama Mtoto wa kike na changamoto zake za kila siku.
Enhe! Mwambie rafiki  aje tujifunze, ushauri na tuulize maswali katika mada zinazobeba Ajenda mpya ya Nguvu Ya BINTI 2017
Kila jumatano ya pili na ya mwisho wa mwezi katika kurasa za Femina Hip : Facebook,Instagram na Twitter @feminahip
#SautiYaNguvuYaBinti

TAMASHA LA USALAMA BARABARANI KUFANYIKA AGOSTI 5 MWAKA HUU UWANJA WA TAIFA

$
0
0
 Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Tamasha la Usalama Barabarani linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi wa nane, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi,Fortunatus Musilimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Fortunatus Musilimu, akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu Tamasha la Usalama Barabarani linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi wa nane, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli. Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni. 
Waandishi wa  Habari wakimisikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Mkutano uliohusu Tamasha la Usalama Barabarani linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi wa nane,mwaka huu katika Uwanja wa Taifa,Jijini  Dar es Salaam, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. John Magufuli.Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi,Fortunatus Musilimu.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images