Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

Kiwanja Kinauzwa Bunju ‘A’ manispaa ya Kinondoni Dar es salaam

$
0
0
Kipo Mita 800 kutoka Barabara kubwa iendayo Bagamoyo. Kiwanja kimepimwa, kina hati na kipo katika eneo lililopangwa na kuendelezwa vizuri.
Bei: Tshs. 40m/- (maelewano yapo) na malipo yanaweza kufanywa kwa awamu

mbili.
Mawasiliano: +255 713 576464 au  +1 832 734 3292
 (ikiwa haipatikani acha sms whatsapp)
Email: roseodessa@yahoo.com

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 19.07.2017

Introducing "HAPA WAKATI TU" by Wakazi

SPORTPESA YATOA SHUKRANI KWA WANAHABARI, SERIKALI, VYOMBO VYA DOLA NA WANANCHI KUFANIKISHA ZIARA YA EVERTON

$
0
0
Habari na Picha na Richard Mwaikenda
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Tarimba alisema kuwa ziara ya Everton nchini imekuwa ni ya mafanikio makubwa kimichezo, kiuchumi, kijamii na hasa kuutangaza vilivyo utalii wa Tanzania Duniani.
Tarimba hakusita pia kuishukuru Ikulu kwa kuwapa sapoti kubwa kufanikisha ziara ya Everton hasa katika masuala ya kumpata mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pamoja na kuruhusu  vyombo vya dola kwa ajili ya usalama wa timu hiyo.
"Kwa niaba ya SportPesa ambao ndiyo wadhamini wakuu wa timu hiyo, tutakuwa wachoyo wa fadhila kama tutashindwa kuwashukuru wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walituunga mkono  katika kuhakikisha kuwa maandalizi ya ziara hii yanafanikiwa." Alisema Tarimba na kuongeza kuwa...
Napenda Kumshukuru Rais  John Magufuli kwa kutoa baraka zake, lakini pia nipende kumshukuru  Makamu wake Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa utayari wa kuwapokea wageni wetu ."
Alimshukuru pia Waziri wa Habari, Utamadjuni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe  kwa niaba ya wizara hiyo kwa kuwa bega kwabega  katika jukumu hilo hizo. Pia hakusita kutoa pole kwa waziri huyo kwa kufiwa na mkewe.
 Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo,  ambapo alitoa shukrani kwa wanahabari, vyombo vya dola, serikali na watanzania kwa kufanikisha ziara ya timu ya Everton ya Uingereza hapa nchini. 

 Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sportpesa, Tarimba Abbas akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo,  ambapo alitoa shukrani kwa wanahabari, vyombo vya dola, serikali na watanzania kwa kufanikisha ziara ya timu ya Everton ya Uingereza hapa nchini. 

Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wakipokea wapongezwa kwa kufaulu mtihani wa kidato cha sita

$
0
0
Na Francis Godwin, Iringa
SERIKALI ya wilaya ya Kilolo na mbunge wa kilolo Mhe. Venance Mwamoto wamewapongeza kwa zawadi za maandalizi ya chuo kikuu mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (19) waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu. 
Wakikabidhi zawadi hizo kwa mapacha hao jana mbele ya walezi wao wa kituo cha Nyota ya asubuhi ambako wanaishi Maria na Consolata, Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah, Mhe.Mwamoto ambao waliongozana na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kilolo Bw. Alloyce Kwezi na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo Seth Moto walisema wamevutiwa na ufaulu wa mapata ambao ni yatima hivyo wamelazimika kuwaanzishia maandalizi ya chuo mapema zaidi kwa lengo la kuwawezesha kuanza chuo kwa wakati.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kilolo Kwezi alisema kwa kufanya kwao vizuri kumeongeza heshima kubwa kwa wilaya ya Kilolo ambayo ndio iliyoongoza kwa matokeo ya kidato cha sita kwa mkoa wa Iringa wenye shule 25 huku wilaya hiyo ikiongoza kimkoa kwa kuwa na shule Pomerini ndio iliibuka ya kwanza kwa shule zote 25. 
Hivyo alisema moja kati ya mkakati wa Halmashauri ya Kilolo ni kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mitihani mbali mbali pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo ili kuifanya wilaya hiyo kuwa mbele kwa kila jambo . 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo alisema kuwa pamoja na wilaya kutoa msaada huo kwa watoto hao mapacha kama sehemu yao ya maandalizi ya chuo bado milango ipo wazi kwa wadau wengine walioguswa na watoto hao kuzidi kuwasaidia kwani wao wenyewe wameonyesha nia ya kuendelea na masomo na kuwa mfano kwa baadhi ya jamii ambayo imekuwa ikiwaficha watoto wenye ulemavu kwenda shule .
 “ Wametuowezesha wilaya yetu kufanya vizuri kweli! Tunawapongeza wao ,walimu na wadau wote wa elimu zaidi wanafunzi ambao wamefanya vizuri katika mitihani hiyo.
"Kilolo ilikuwa ikitazamwa sana kuona nini matokeo ya  Maria na Consolata ila bila viongozi na wadau wengine wa elimu kujitoa kwa ajili yao yawezekana wasingefanya vizuri …..tupo pamoja nao na tutaendelea kuwa pamoja zaidi hadi chuo “ Mkuu huyo wa wilaya alisema.
Aliongezea kuwa moja kati ya mahitaji yao makubwa kwa sasa ni nyumba yao maalum kwa ajili ya kuishi pindi watakapokuwa chuo kwani wao wanahitaji nyumba maalum ambayo ni rafiki zaidi na aina ya ulemavu waliokuwa nao . 
Mbunge wa Kilolo Mwamoto mbali ya kuwapongeza mapacha hao bado alitaka wananchi wote wenye watoto wenye ulemavu kuiga mfano wa mapacha hao na hatapendezwa kuona watoto wenye ulemavu wa aina yeyote ile wanafichwa majumbani . 
Pia alisema moja kati ya mkakati wake kuona mazingira ya shule mbali mbali katika wilaya ya Kilolo yanakuwa rafiki na kuwataka wananchi kuendelea na ujenzi wa vyumba vya madarasa ,maabara ili kuepukana na changamoto ya miundo mbinu ya elimu pamoja na kwenda sawa na serikali ya Rais Dkt John Magufuli ya uboreshaji wa elimu .
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah, mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo Seth Moto wakiongea na watoto hao
mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamoto akiwapongeza mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah akiwapongeza mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Abdallah akiwapa zawadi ya laptop  mapacha walioungana mapacha Maria na Consolata Mwakikuti 
 Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wakipokea mito
 Mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti wakipokea mablanketi

BALOZI SEIF AKITAKA CHAMA CHA SKAUTI NCHINI KUWAELIMISHA VIJANA ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI

$
0
0
Na Othman Khamis Ame
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema wakati umefika kwa Chama cha Skauti Nchini kuongeza nguvu za kuwaelimisha Vijana wenzao hasa walioko Vijijini ili wajikomboe kupenda kujishughulisha na kazi au miradi ya ujasiri amali.
Alisema Vijana wengi wamekuwa na tabia ya kujihusisha na vigenge vya kihuni mitaani vinavyopelekea kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya wizi pamoja na vitendo vya kudhalilisha watoto wanawake na watu wenye mahitaji Maalum.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa Kauli hiyo wakati akizungumza na Vijana wa Chama cha Skauti Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Mkoani Dodoma kushiriki Tamasha la Wiki Moja la Maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania hapo katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Alisema zipo fursa nyingi za ajira zinazopatikana katika Sekta ya Utalii ambazo Vijana endapo wataamua kuzichangamkia zinaweza zikawapatia kipato kwa kutumia soko la bidhaa zinazotokana na kilimo cha mboga mboga na mazao ya Baharini.
Balozi alifahamisha kwamba Uskauti kwa vile hauna mafungamano ya itikadi ya Kisiasa wala Dini unalengo la kuwaunganisha Vijana katika harakati zao za kimaisha kupitia misingi ya kujenga Utaifa wao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza umuhimu wa vijana wa Skauti kufundishwa mbinu na mafunzo ya kuogelea na kuzamia kutokana na majukumu yao yaliyowazuunguka ya kuwa wao ni miongoni mwa Taasisi zinazotoa huduma wakati yanapotokea maafa au majanga.
Balozi Seif alielezea kuridhika kwake na Kanuni 10 za Skauti zinazoelekeza uzalendo unaojenga Taifa lenye Wananchi wanaopendana na kuwa na nguvu za kukabiliana na changamoto zinazowazunguuka katika misingi ya nidhamu na uwajibikaji.
Mapema Kamishna Mkuu Msaidizi wa Chama cha Skauti Zanzibar Maalim Suleiman Takadir alisema Skauti iliasisiwa Zanzibar mnamo mwaka 1912 na Mwaka 1917 ikaanzishwa upande wa Tanzania na kufifia katika miaka ya 60.
Maalim Takadir alisema Chama hicho kilianzishwa tena Mwaka 1992 chini ya Rais wa Awamu ya Tano Dr. Salmin Amour ili kufufua ari ya kuwajenga Vijana katika uzalendo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akivishwa Skafu na Kijana Omar Amour Said wa Skauti nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar kabla ya kuzungumza na Vijana wa Chama cha Sakauti Zanzibar. Kati kati yao ni Raius wa Chama cha Skauti Zanzibar ambae pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma.
Balozi Seif akiambatana na Rais wa Skauti Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma wakielekea ndani ya Ukumbi wa Mkutano kuzungumza na Vijana wa Skautio Zanzibar wanaotarajiwa kuondoka Zanzibar kuelekea Mkoani Dodoma katika maadhimisho ya Miaka 100 ya Skauti Tanzania.

Balozi Seif akimpongeza Kijana Kassim Yussuf Msoma Mashairi ghibu baada ya kughani kwenye Mkutano wa Skauti Zanzibar uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Kikwajuni.
Baadhi ya Skauti wa Zanzibar wakifuatilia Mkutano wa Chama hicho uliohutubiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi uliokuwa wa matayarisho ya mwisho wa Vijana wake kujiandaa kuelekea Dodoma katika Tamasha la Miaka 100 ya Skauti Tanzania.
Baadhi ya Makatibu wa Skauti wa Mikoa ya Unguja wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif ambaye hayuko pichani hapo katika Ukumbi wa zamia wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwahutubia VBijana wa Chama cha Skauti Zanzibar wanaojiandaa kuelekea Dodoma katika Tamasha la Miaka 100 ya Skauti Tanzania.Picha na – OMPR – ZNZ.

Utalii wa Ndani : Ikorojia na Maporomoko ya Nkondwe

NAIBU WAZIRI MANYANYA :AWATA WAZAZI KUFUATILIA MAENDELEO YA WATOTO WAO SHULENI

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya wa pili kutoka kulia akitembelea shule ya Msingi Bagamoyo wakati wa ziara yake wilayani Korogwe kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel na anayefuatia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akiwa ameshika mtoto wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Jumanne Shauri
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia, Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Bagamoyo iliyopo wilayani Korogwe ambapo aliwataka kusoma kwa bidii ili waweze kupata mafanikio

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe,Jumanne Shauri akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Matondoo wakati wa ziara hiyo ambapo aliwataka kutilia mkazo masomo ya sayansi. 

INTRODUCING "NADONDOKA" BY MASTA ROBATT ft. KAYUMBA

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AHIZIMIZA USHIRIKIANO KUKABILI UKATILI DHIDI YA ALIBINO

$
0
0
Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Mhe. George  Masaju ametoa wito  kwa Asasi zisizo za kiserikali ( NGO)    kushirikiana na kufanya kazi kwa  karibu na Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu wa Serikali    ili  kupitia ushirikiano huo kukomesha   na hatimaye kumaliza kabisa  changamoto zinazowakabili  watanzania wenye albinism.

Mwanasheria Mkuu ametoa  wito huo  leo  ( Jumatano)wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi  Ikponwosa Ero,  Mtaalamu Huru wa Baraza la  Haki za Binadamu  la Umoja wa Mataifa kuhusu  watu wenye albinism

“  Ningependa  kutoa shukrani zako kwa kuamua kuja Tanzania  na kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali,  hii ni fursa  muhimu kwako    ya kupata taarifa sahihi na rasmi kuhusu  jitihada , juhudi na mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali na taasisi zake katika kukabili  vitendo vya jinai dhidi ya watanzania wenzetu wenye  albinism” akasema Mhe. Mwanasheria Mkuu

Na Kuongeza “ kupitia kwako nikuombe basi  uwahimize   viongozi wa asasi zisizo za kiserikali hususani zile zinazojihusisha na  watanzania wenye  albinism kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na  Ofisi yangu  na Taasisi nyingine za serikali kwa sababu wote tuna nia na lengo moja la  kuwasaidia  watanzania wenzetu”..

Akasema  Serikali  inachukulia kwa uzito wa hali ya juu  makosa  ya kijinai dhidi ya watu wenye albinism na kwamba, watuhumiwa wote ambao wamepatikana na hatia wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na  sheria kuchukua mkondo wake.

Akasisitiza kwamba  Katiba ya  Jamhuri ya Muungano  imesisitiza sana juu ya haki ya mtu kuishi na kwamba haki hiyo ni kwa watanzania wote bila ya kubagua   wakiwamo  watu wenye  albinism au ulemavu wa aina yoyote.

“ Haki ya mtu kuishi imefafanuliwa na kuelezwa kwa kina kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na haki hiyo  haimbagui mtu mwenye albinisim au  mtanzania yoyote ile na ndio maana  makosa ya jinai  dhidi ya  haki ya mtu kuishi  awaye yeyote yule  yanachukuliwa kwa uzito ule ule”.

 Mwanasheria Mkuu wa  Serikali  Mhe. George Masaju akifafanua    kuhusu namna Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Divisheni ya Mashtaka inavyoshughulikia kwa  kupeleleza na kuendesha kesi za jinai dhidi ya watu wenye albnism. katika maelezo yake  Mwanasheria Mkuu amesema  Serikali inachukulia kwa uzito wa hali ya kipekee matatizo yanayowakabili watanzania wenye ualbino na kwamba juhudi hizo  zimesaidia sana katika kupunguza kwa  kiasi kikubwa matukio ya jinadi dhidi ya   watanzania hao ingawa bado kunachangamoto. 
Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akimsikiliza  Bi. Ikponwosa Ero, Mataalam Huru wa Baraza la Haki za Binadamu  la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye albnism. Mhe. Mwanasheria Mkuu na Bi. Ero walikutana leo  Jijini  Dar es Salaam, ambapo walibadishana mawazo  kuhusu  namna  Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu   inavyoshughulikia matukio ya kijinai dhidi ya watanzania wenye albnism.

MAKALA YA SHERIA: KAMA HAIJAPITA MIAKA 12 UNAWEZA KURUDISHA ARDHI ULIYODHULUMIWA.

$
0
0
Na  Bashir   Yakub
1.UKOMO  WA  HAKI.

Hakuna  haki  isiyo  na  ukomo wa  muda  unapokuwa  unaidai. Huwezi  kudai  haki  muda  wowote  unaotaka  wewe. Ni  lazima   udai  haki  ndani  ya  muda.Na  ni  ule  muda tu uliowekwa  na  sheria. Ipo  sheria  rasmi  inayoeleza  muda  wa  kudai  haki  mbalimbali.  Inaitwa Sheria  ya  Ukomo  wa  Muda ,  Sura  ya  89.  Katika  sheria  hiyo   hapajaelezwa tu   ukomo  wa  kudai  haki  katika  masuala  ya  ardhi  bali  pia  katika  masuala  mengine  yote  ya  haki  unazoweza  kudai.

Ndani  ya  Sheria  ya  Ukomo  wa  Muda  kumeelezwa ukomo  wa  kudai  haki  iliyotokana  na  masuala  ya  mikataba na  makubaliano, ukomo   wa  kudai  haki  katika  masuala  ya  udhalilishaji, ukomo  wa rufaa, ukomo  wa  haki  katika  masuala  ya bima, madai  ya  fedha,  rehani  za  mikopo, na mambo  mengine  mengi.


2.  HUJAPITWA  NA  MDA  BADO UNAWEZA  KUIDAI  ARDHI  YAKO.

Wako  watu  huko  nyuma  walidhulumiwa  ardhi  muda  mrefu  na  sasa  wamekata  tamaa.  Wamekata tamaa  kutokana  na  kuona   ni mda  mrefu  umepita  tangu  haki  hiyo  iporwe  na  sasa  wanadhani  kuwa   hawawezi  tena  kudai  haki  hiyo.

Wako  watu wamedhulumiwa  ardhi  katika  masuala  ya  mirathi,  katika  masuala  ya  mikopo,  katika  masuala  ya  mikataba  na  makubaliano,  katika  masuala  ya  ndoa  na  machumo  ya mali  za  ndoa, katika  masuala  ya  uvamizi, katika  masuala  ya  kuharibu  mipaka  n.k. Na  ardhi  hapa  tunazungumzia  mashamba,  viwanja  na  nyumba. Hivi  kwa  pamoja  ndivyo  huitwa  ardhi.

Basi  yafaa  ujue  kuwa kama  wewe  ni  kati  ya  waathirika  wa  jambo  hili  basi  bado unayo  haki  ya  kudai   ardhi  yako  madhali  muda  huo  haujakupita.  Haki  yako  inaishi   mpaka  miaka  12  na  itakufa baada  ya  muda  huo.  Kama  imepita  miaka  sita,  mitano,  nane,  kumi,  n.k.  bado  muda  wako  wa  kudai  na  kurudishiwa  ardhi upo.


MISS TANGA TALK SHOW OFFICIAL LAUNCH IN PICTURES

MAGAZETI YA ALHAMIS LEO JULAI 20,2017

MAKILAGI: WATAKAOTUMIA RUSHWA UCHAGUZI HUU UWT TUTAWATIA ADABU

$
0
0
NA BASHIR NKOROMO

Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) imeapa kuwa ya mfano katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wagombea wa nafasi mbalimbali katika Jumuia hiyo watakaobainika kutumia rushwa au kufanya vitendo vyovyote vinavyokiuka kanuni za Uchaguzi.

Kiapo hicho kimetolewa jana jijini Dar es Salaam, na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Amina Makilagi wakati akitangaza maazimio ya Kikao Cha Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT kilichofanyika juzi Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jiijini.

"Tunashukuru kwamba baada ya Mwenyekiti wetu wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kuonyesha anapambana na rushwa kufa na kupona na kwa dhati kabisa, kila mtu amemuelewa na sisi UWT tunaahidi kumuunga mkono kwa kuhakikisha katika uchaguzi huu hatutakuwa na mzaha, yeyoyote atakayebainika kutumia rushwa hatutamuonea aibu hata awe nani", alisema Makilagi.

Alisema, uchaguzi kwa ngazi ya Matawi umefanyika kwa asilimia 95, ngazi ya Kata vikao vya uchujaji vinaendelea na kwa ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa uchaguzi unaendelea.

TANZIA: MAMA WA MZAZI MWENZA WA MWANAMUZIKI DIAMOND PLATNUMZ AFARIKI DUNIA LEO

$
0
0
Mama mzazi wa Zarina Hassan maarufu kama ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mzazi mwenza wa Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz, Halima Hassan (kulia) amefariki dunia asubuhi hii, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akidaiwa kusumbuliwa na maradhi ya moyo na figo.

Zari amethibitisha kifo cha mama yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI..
AMEN.

HABARI NJEMA KWA WANACHAMA WA NSSF: VIONGOZI WATENGA SIKU YA KUSIKILIZA MALALAMIKO YA WANACHAMA

RAIS DKT MAGUFULI AMPOKEA RAIS NKURUNZIZA WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe magufuli akiwa ameambatana na mgeni wake  Rais wa Burundi,Pierre Nkurunziza aliewasili mapema leo katka uwanja wa mpira wa Lemela mjini Ngara,Rais Dkt Magufuli amempokea Rais Nkurunziza akiwa kwenye ziara yake kikazi mkoani Kagera.

Aidha Rais Nkurunziza baada ya kupokelewa na Mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli,alipata wasaa wa kuwasalimia wananchi mbalimbali waliofika kumpokea katika uwanja huo wa mpira mjini Ngara.

VIJANA WA ZAMANI COLUMBUS, OHIO WAKIJIFUA TAYARI KWA OLD SCHOOL REUNION BASKETBALL BONANZA

$
0
0
Image may contain: 8 people, people smiling, people standing and outdoor
Siku ya kwanza walivyojitokeza kujifua hii ilikua siku ya Jumanne July 18, 2017 Columbus, Ohio.
Image may contain: 9 people, people smiling, people standing, shoes, basketball court and outdoor
Mazoezi yakiendelea siku ya pili Jumatano July 19, 2017 Cloumbus, Ohio

WAZIRI MWAKYEMBE AWASHUKURU WATANZANIA KWA KUMFARIJI KUTOKANA NA MSIBA WA MKEWE.

$
0
0
Na Shamimu Nyaki-WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amewashukuru viongozi wote wa Serikali, Sekta binafsi, Taasisi za Kidini vyombo vya habari na watanzania wote waliomfariji katika msiba wa mke wake Bibi Linah Mwakyembe uliotokea Julai 15 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa Misa ya mazishi ya mke wake huyo iliyofanyika jana nyumbani kwake Kyela Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa amefarijika sana kwa upendo ulioonyeshwa na kila mtu kwa nafasi yake katika kipindi hiki kigumu na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kila jambo.

“Mimi na wanangu tumefarijika sana kwa kuona jinsi ambavyo Watanzania na wana Kyela mlivvyokuwa na upendo kwetu mmetupa faraja na mmetutia nguvu na mmetuoshesha ushirikiano mkubwa katika jambo hili tunaomba mwenyezi Mungu awabariki sana na asanteni sana”Alisema Mhe Waziri Mwakyembe.

Kwa Upande wake Mhe.Amos Makala Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati akitoa salamu za pole kwa niaba ya wanachi wa mkoa wake amesema wananchi wa Mbeya watamkumbuka marehemu  mama Linah Mwakyembe kwa moyo wake wa kujitolea kusaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo kufundisha jamii kumcha Mungu pamoja na Ujasiriliamali uliosaidia wanawake wa Kyela kujiajiri.

“Wananchi wa Mbeya tunakupa pole sana Mhe. Mwakyembe pamoja na familia yako lakini pia tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya mama Linah hapa duniani ambayo yameleta faida kwa jamii tunamuomba mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi amina lakini na wewe pia tunakuombea Mungu aendelee kukupa uvumilivu na uamini kuwa hili nalo litapita”.Alisema Mhe Makala.

Marehemu Bibi Linah Mwakyembe ameagwa na kuzikwa jana nyumbani kwake Kyela na ameacha watoto watatu.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe

SITAVUMILIA HATI CHAFU KATIKA HALMASHAURI YOYOTE MKOANI KWANGU-DKT NCHIMBI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singia Dkt Rehema Nchimbi amesema hatavumilia kuona halmashauri inafanya uzembe na kupata hati chafu ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Fedha za Serikali kwakuwa itamchafua yeye na taswira ya uongozi wote wa Mkoa wa Singida.

Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo mapema jana wakati wa baraza maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali ambazo amesema hoja nyingi zimetokana na uzembe.

Amesema licha ya kuipongeza Manispaa ya Singida kwa kupata hati safi, uwepo wa hoja umedhihirisha kuwa kuna baadhi ya watendaji wanafanya kazi kwa uzembe na kutofuata taratibu na sheria hivyo wajirekebishe haraka.

Dkt Nchimbi ameongeza kuwa hoja nyingi zinajitokeza kwa kukosa umakini na watendaji kufanya kazi kwa mazoea hali ambayo ikiendelea inaweza kuipelekea manispaa kupata hati isiyoridhisha hivyo kupata hati safi kuwaongezee nguzu ya kuboresha utendaji kazi wao.

Aidha amewashauri wakuu wa idara na watumishi wengine kuitendea haki manispaa yao kwa kuchapa kazi kuwa wadilifu na kufuata sheria kwani wakifanya hivyo wataepuka hoja zisizo za lazima na kuharakisha maendeleo.
 Mkuu wa Mkoa wa Singia Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na Meya wa Manispaa ya Singida Gwae Chima Mbua kabla ya kuanza kwa baraza Maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bravo Kizito Lyampembile akifungua baraza Maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali.
 Baadhi ya Viongozi wa Manispaa ya Singida wakifuatilia baraza Maalumu la madiwani wa Manispaa ya Singida kujadili hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images