Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

Wanawake wa Kitanzania Kufanya Kongamano la Kumuombea Rais Magufuli.

0
0
Na: Thobias Robert - MAELEZO.

Wanawake wa Jumuiya ya Tanzania Fellowship of churches kutoka makanisa mbalimbali wanatarajia kufanya kongamano la maombi na dua maalumu kwaajili ya kumuombea ulinzi Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya katika kutetea wanyonge na kulinda rasilimali za nchi.

 Hayo yamesemwa leo, Jijini Dar es Salaam na Mratibu wa kongamano hilo Mchungaji Deborah Malassy, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo la siku tatu linalotarajia  kuanza Julai 20 hadi Julai 23 mwaka huu katika ukumbi wa  Millenium Tower ulioko Jijini humo.

Mchungaji Malassy amesema kuwa, kongamano hilo linalenga kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuipatia Nchi ya Tanzania Kiongozi ambaye Watanzania walikuwa wanamhitaji kwa muda mrefu ili kulinda amani ya Nchi, kutetea wanyonge pamoja na kusimamia rasilimali za nchi pamoja na uadilifu kazini.

“Mwaka huu, ni mwaka wa Baraka na Neema kwa Taifa la Tanzania kufuatia matendo makuu ya Mungu aliyotutendea Watanzania, hasa kuwa na kiongozi mwenye uwezo, mcha Mungu, mtiifu mkweli na asiyependa mapato ya Serikali kupotea,” amesema Mchungaji Malassy.

Aidha amesema, kwa muda mfupi aliokaa madarakani, Rais Magufuli amefanya mambo mengi na kila Mtanzania ameyashuhudia kama vile kurejesha maadili kwa watumishi wa Umma, kuwaondoa viongozi wala rushwa pamoja na kutetea rasilimali za Tanzania zilizokuwa zikisafirishwa nje ya nchi, mfano mchanga wa dhahabu.

Vile vile kongamano hilo litatoa elimu kwa wanawake juu ya  kujilinda dhidi ya unyasasaji wa kijinsia, na kuwajengea Wanawake uwezo wa namna ya kujikwamua kiuchumi pamoja na kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia unaotokana na rushwa ya ngono.

Akinukuu Maneno ya kitabu kitakatifu kutoka kitabu cha Nyakati wa Pili 7:18, Mchungaji Malassy amesema, “Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu wataziacha njia zao mbaya wakajinyenyekesha na kuomba nami nitasikia kutoka mbinguni na nitaiponya nchi yao,” kwahiyo wao kama wakina mama walioitwa kulia na kuomboleza kwa ajili ya Taifa lao wanayo haki ya kufunga na kuomboleza kwaajili ya kuliombea Taifa.

Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Vile vile, viongozi wanawake kutoka nchi za Afrika ya Kusini, Marekani, Uingereza, Zambia, Kenya, Kongo na Botswana pia watakuwepo katika kongamano hilo.

 Kongamano hilo limekuwa likifanyika kila mwaka mwezi Disemba na Julai ambapo hufanyika pamoja na mkesha mkubwa wa maombi katika uwanja wa Taifa, lengo likiwa ni  kuombea amani, utulivu, upendo pamoja na kuwaombea viongozi wa Serikali ili waongoze Nchi kwa hekima na busara kutoka kwa Mwenyezi Mungu.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli

MAKONDA ATANGAZA VITA DHIDI YA WIZI WA VIFAA VYA MAGARI DAR ES SALAAM

Shule siyo "Clinic" wala "Maternity" - RC Rukwa

Balozi Seif Ali Iddi azindua Tamasha la 22 la Utamaduni wa Mzanzibari

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesisitiza umuhimu wa Jamii Nchini kuendelea kukuza maadili na kujiepusha na vitendo vya unyanyasi wa kijinsia dhidi ya Watoto na Wanawake ili irejeshea heshima yake Zanzibar. 
Alisema Visiwa vya Zanzibar havikuwa ni kituo muhimu cha Biashara katika mkarne zilizopita bali pia vilikuwa ni kitovu cha Elimu, heshima, ustaarabu na ukuzaji wa silka, mila na desturi za Utamaduni wa asili. 
Akilifungua Tamasha la 22 la Utamaduni wa Mzanzibari hapo katika Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michenzani Mjini Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwaomba wana Jamii kushirikiana na Wizara inayosimamia Utamaduni katika kuuenzi Utamaduni wa Taifa hasa kuhamasisha jamii kuepuka tabia zisizofaa zinazowadhalilisha Watoto, Wanawake na Watu wenye mahitaji Maalum. Balozi Seif alisema suala la kukuza utamaduni si jambo geni na ni vyema wazazi wa karne hii wakaiga mifano ya Wazazi wa zamani waliotumia mbinu mbali mbali zikiwemo sherehe za jando na unyago mfumo uliomtayarisha Kijana wa Kike na wa Kiume namna ya kukabiliana na maisha yake ya baadae. 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia vitu vya sanaa za mkono wakati alipotembelea maonyesho ya Wajasiri Amali kabla ya kuzindua Tamasha la 22 la Utamaduni wa Mzanzibari.
 Balozi Seif  akihitaji maelezo kutoka kwa Mjasiri amali wa sanaa ya vitu vya ufinyanzi kwenye maonyesho ya kazi za sanaa katika uwanja wa Kumbu kumbu ya Mapinduzi Kisonge Michenzani Mjini Zanzibar.
 Mjasiri amali wa utengenezaji wa vitu vya  sanaa ya asili Viatu vya Mitarawanda kutoka Shehia ya Bweleo Bwana Ali Mwinjuma Kirobo akimpatia maelezo Balozi Seif wakati alipotembelea banda lao.
 Paredi la wasanii mbali mbali kutoka Wilaya za Unguja wakionyesha umahiri wao katika udumishaji wa Utamaduni wa Mzanzibari hapo Kisonge Mnara wa Kumbu kumbu.
Balozi Seif akionyesha umahiri wake katika kucheza ngoma ya ndege kutoka Skuli ya Msingi Kisiwandui iliyokuwa ikitumbuiza kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la 22 la Utamaduni wa Mzanzibari hapo Mnara wa kumbu kumbu Michenzani Mjini Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA PWANI, AAMURU KAMANDA WA TRAFIKI MKOANI HUMO AONDOLEWE

0
0

Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Masauni akiwa ameambatana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana.
“Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;
“RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutati uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania.”
Masauni mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwauliza maswali abiria wa basi la Safari Express lifanyalo safari zake Dar es Salaam kwenda Arusha, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni aliiagiza Jeshi la Polisi kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufanya ukaguzi wa magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi, Jonathan Shana, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Mabasi Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (wapili kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani, Abdi Isango (wapili kushoto) katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiwa katika ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi cha Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani ambapo alifanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo. Masauni alimuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) kumuondoa Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) mkoani humo katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kufuata maelekezo aliyowahi kupewa ya kukagua magari na kusimamia sheria za usalama barabarani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa maelekezo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu (kulia) wakati alipokua anazungumza na askari wa usalama barabarani katika eneo la Sanzale, Bagamoyo. Masauni alifanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Mabasi Kibaha, Chalinze pamoja na kukagua barabara hadi kufika mjini Bagamoyo.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


WAZIRI LUKUVI AMSIMAMISHA MUWEKEZAJI TANGA

0
0


Waziri Lukuvi amefikia uamuzi huo baada ya wakazi wa eneo hilo kuzuia msafara wake na kupata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hao na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto wakimlalamikia Waziri kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro kwa wakazi hao.
Baada ya kupokea malalamiko hao Waziri Lukuvi aliamua kutembelea mashamba hayo na kuyakagua ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wamekuwa wanakabiliwa na mgogoro huu kwa miaka mingi.
Baada ya kutembelea na kujiridhisha Waziri Lukuvi amesema kwamba shamba hilo linastahili kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga na ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki ameshindwa kuwa na sifa za umiliki kwa kuwa hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004, hajalipa wafanyakazi wake kwa muda mrefu, miundombinu yake na mazingira ya kazi hayaridhishi na ameshindwa kuliendeleza shamba hilo tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo ileile ya mkoloni ya mwaka 1937.
Aidha, katika ziara hii Waziri Lukuvi amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo kati ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.
Waziri Lukuvi anatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya ziara yake mkoani Tanga.
Mnamo tarehe 18 Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya  ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.
Ili kutekeleza agizo hili wakuu wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesimamisha umiliki wa mwekezaji wa mashamba ya katani yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited yaliyopo kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga.

IGP SIRRO AKUTANA NA BAADHI YA MAKAMANDA AKIWA SAFARINI MIKOA YA KANDA YA ZIWA

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza jambo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Debora Magiligimba, IGP Sirro amepita mkoani Singida, akiwa safarini kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiweka saini katika kitabu cha wageni katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, na kuzungumza na baadhi ya askari na maofisa (hawapo pichani), IGP Sirro, amepita katika wilaya hiyo, akiwa safarini kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Manyoni (OCD) Cleophace Magesa, IGP Sirro, amepita katika wilaya hiyo, akiwa safarini kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akifurahia jambo na kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro J. Muliro, IGP Sirro, amepita mkoani humo, akiwa safarini kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kuzungumza na askari wa Jeshi hilo. Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi

PROFESA MWAMFUPE MEYA MPYA MANISPAA YA DODOMA

0
0
 
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma Balozi Job Lusinde akitoa neno kwa Meya Mpya na kwa Madiwani wa Manispaa ya Dodoma wakati wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa hiyo Julai 19 mwaka huu.
 Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi  akiwaonesha wajumbe wa Baraza la Madiwani Karatasi ya kura wakati wa zoezi la kuhesabu kura  kwa uwazi wakati wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Dodoma.
 Wadau mbalimbali wakifuatilia zoezo la uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Dodoma uliofanyika Julai 19 mwaka huu ambapo Profesa Davis Mwamfupe wa CCM aliibuka Mshindi.
 Madiwani waliogombea nafasi ya Meya wa Manispaa ya Dodoma wakitambulishwa mbele ya wajumbe. Kushoto ni Mgombea wa CCM Profesa Davis Mwamfupe na Kulia ni Mgombea wa CHADEMA Yona Kusaja.

ONYO KALI DHIDI YA UZUSHI MITANDAONI KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

DKT PEDRO KISALI PALLANGYO WA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE ASHINDA TUZO YA WATAFITI VIJANA WA KIAFRIKA MWAKA 2017

0
0
Huu ni ushindi Kwa taifa na ushindi Kwa vijana, Hongera sana Dr. Pedro Kisali Pallangyo kwa kushinda tuzo hii.

TUTAWASHUGHULIKIA WALE WOTE WANAOTOA MATAMSHI YA KICHOCHEZI - MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itawashughulikia watu wote  wanaotoa matamshi ya kichochezi nchini bila ya kujali nyadhifa zao. 

Amesema ni vema watu wakawa makini na kijiepusha kutoa matamshi ambayo yataathiri mfumo wa maisha kwa wananchi wengine.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Julai 19, 2017 wakati wa ibada ya mazishi ya mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe Bibi Linnah Mwakyembe iliyofanyika wilayani Kyela. 
Amesema Serikali haitavumilia kuona baadhi ya watu wakitoa matamshi ambayo hayana tija kwa jamii na badala yake yanalenga kuwavuruga wananchi na kuchochea migogoro.

"Tutashughulika na watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi, popote walipo bila ya kujali uwezo wao, vyeo vyao na mamlaka walizonazo." 

Pia amewaomba viongozi wa dini waendelee kuliombea Taifa na viongozi wake na kwamba Serikali inawategemea na iko pamoja nao. 
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Askofu wa Kanisa la Evarinjerical Brother Hood, Rabison Mwakanani kuonya vitendo vya baadhi ya watu kumtukana Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli. 
Amesema ni vema watu hao  wakajifunza namna ya kuwasilisha hoja zao bila ya kutumia lugha za matusi. 
“Rais Dkt. Magufuli amefanya mambo mengi makubwa kwa ajili ya maendeleo. Wanaofanya hivyo wasidhani kama wanamtukana Rais tu bali wanawatukana Watanzania wote waliomchagua wakiwemo viongozi wa dini.” 
Pia aliwaomba wananchi kufanya maandalizi mapema kwa sababu wote ni wapitaji, hivyo waandae roho zao kwa kuacha kufanya dhambi na maovu yote ili wawe na mwisho mwema. 
Vile Vile Waziri Mkuu amewaomba wananchi wote washirikiane kwa pamoja kumuombea Dkt. Mwakyembe na familia yake ili Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji katika kipindi hiki kigumu. 
“Wajibu wetu sote ni kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema. Tunajua kwa sasa Dkt. Mwakyembe yuko katika wakati mgumu, namuhakikishia kwamba hayuko peke yake kwani Serikali iko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu.” 
Naye, Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai alimpa pole Dkt. Mwakyembe huku akiitaka familia kuendelea kuwa na upendo kama ule uliokuwepo wakati wa uhai wa marehemu Bibi Linnah. 
Kwa upande wake, Mtoto mkubwa wa marehemu, George Mwakyembe alisema anaamini mama yao, alijiandaa na kifo hicho kwa kuwa alikuwa mchamungu. 
"Mama alikuwa na ratiba kila siku ifikapo saa nne usiku lazima afanye ibada, Hivyo nina matumaini makubwa kupitia Uchamungu wake, Mwenyezi Mungu atamuweka mahala pema."

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA RIPOTI YA NCHI YA APRM

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amezindua Taarifa ya Nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM).
Uzinduzi huo  ulihudhuriwa na  kiongozi wa Jopo la Mchakato huo kwa Tanzania ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo  la Watu Mashuhuri Bi. Brigitte Sylvia Mabandla, Viongozi wengine wa APRM Tanzania ni Balozi Ombeni Sefue, Profesa Hasa Mlawa na Balozi Aziz Mlima aliyemuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
APRM ni mpango wa hiari wa kujipima kwa vigezo vya utawala bora uliobuniwa mwaka 2003 na Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Lengo la mpango huu ni kuziwezesha nchi  wanachama kujitathmini kwa vigezo vya utawala bora katika maeneo manne ambayo ni; Demokrasia na Utawala wa Kisiasa; Usimamizi wa Uchumi; Utendaji wa Mashirika ya Biashara; na Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi.

Akihutubia katika uzinduzi huo, Makamu Rais amewapongeza Wakuu wa Nchi na Serikali wanaoshiriki katika mchakato wa APRM kwa ujasiri wao wa kushirikishana taarifa za kuaminika kuhusu masuala ya utawala bora katika nchi zao.
 “Taarifa hizi zinaonesha wazi juu ya hali ya utawala bora katika Bara letu na kutupa nafasi ya kujirekebisha pale ambapo kuna dosari na kujipongeza pale tunapofanya vizuri na kuwapa wengine nafasi ya kujifunza zaidi’’ alisema Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionyesha kitabu chenye ripoti  ya nchi kuhusu Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa afrika kujipima kwa Vigezo vya Utawala (APRM) mara baada ya kuzindua taarifa hiyo kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. 
Baadhi ya wageni mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Mkutano huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



JPM ATOA SIKU 14 KWA WAMILIKI WA VITUO VYOTE VYA MAFUTA KUTUMIA MASHINE ZA EFD, WATAOKIUKA AGIZO KUFUNGIWA VITUO NA KUFUTIWA LESENI

MICHUZI TV: MAZISHI YA MAREHEMU LINAH GEORGE MWAKYEMBE KIJIJINI IKOLO WILAYANI KYELA, MKOA WA MBEYA

Article 1


COVENANT BANK

Article 8

RAIS DKT MAGUFULI AWATAKA WENYE MIFUGO MINGI KUIUZA BADALA YA KWENDA KUCHUNGIA HIFADHINI

KADA CCM AANZISHA KAMPENI YA MAGUFULI BAKI

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe akagua ukarabati na upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze

0
0
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isaack Kamwelwe akisisitiza jambo wakati wa ziara yake  ya kukagua hatua iliyofikiwa katika mradi wa ukarabati  na upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze  na ujenzi wa mfumo wa kusafirishia maji pamoja na matenki ya kuhifadhia maji. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA)Mhandisi Christer Mchomba na kushoto ni Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya WAPCO inayotekeleza mradi huo.
 Mafundi wakiendelea na Kazi ya ujenzi wa matanki ya kuhifadhi na kusambaza maji katika Jimbo la Chalinze.

 Sehemu ya mabomba yakiwa katika moja ya maeneo unakotekelezwa mradi huo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe (wapili kushoto) akioneshwa ramani ya mradi huo na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wake wakati wa ziara yake  ya kukagua mradi huo  wa ukarabati  na upanuzi wa mtambo wa maji chalinze na na ujenzi wa mfumo wa kusafirishia maji pamoja na matenki yakuhifadhia maji. 
Picha zote na Frank Mvungi-MAELEZO
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images