Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1810 | 1811 | (Page 1812) | 1813 | 1814 | .... | 3272 | newer

  0 0


  Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefuta adhabu dhidi ya wanafamilia wanne waliofungiwa kushiriki masuala la soka kwa mwaka mmoja.

  Wanafamilia hao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa, James Mwakwinya; Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Blassy Kiondo; Kaimu Katibu wake, Ayoub Nyaulingo pamoja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

  Haji Manara alitiwa hatiani Aprili 23, mwaka huu kwa makosa ya lugha chafu na za chuki kwa viongozi wa TFF na kupotosha umma dhidi ya kadi njano ya mchezaji Mohammed Fakhi wa Kagera Sugar ambako alifungiwa kushiriki masuala ya mpira kwa mwaka mmoja na faini ya Sh milioni tisa.

  Viongozi wa RUREFA walifungiwa kwa mwaka mmoja na faini ya Sh. milioni mbili kwa kila mmoja kwa makosa ya kukiuka maagizo ya viongozi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyotaka wasitishe mchakato wa uchaguzi mkoa kwa kuwa kulikuwa na rufaa iliyokatwa TFF.

  Akizungumza na Wanahabari leo Julai 17, 2017 Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas, alisema viongozi hao wamesamehewa adhabu zao kwa kuwa waliomba kupitiwa upya kwa mashauri yao na kamati imeona ni bora kuwaachia huru ili kuendeleza masuala ya soka.

  “Wapo wengi waliofungiwa wengine maisha na wengine adhabu fupi, msamaha huu ni kwa wale ambao wameomba tu kupitiwa upya kwa adhabu zao, pia milango ipo wazi kwa wengine ambao wanataka kupitiwa kwa mashauri yao, lakini si kwa wale waliopanga matokeo uwanjani,” alisema Tarimba.

  Kadhalika, Tarimba aliwaomba viongozi wa TFF kuandaa semina ya Maofisa Habari na Viongozi wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ili kuepuka maneno machafu ambayo yanasababisha wao kufungiwa.

  “Inaonekana viongozi na Maofisa Habari hawana maneno mazuri ya kuongea na wadau wa soka na ndio maana matatizo ya kufungiwa yanajitokeza mara kwa mara, naamini wakipata semina hiyo itawasaidia kujirekebisha na kupunguza kesi kama hizo,” alisema Tarimba.

  Kwa niaba ya TFF, Ofisa Habari wa Shirikisho, Alfred Lucas, wameyapokea mapendekezo hayo kutoka kwa Tarimba na kwamba tutafanyia kazi ili kurekebisha makosa hayo kwa manufaa ya soka la Tanzania.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas akizungumza na wanahabari leo mchana ikiwa ni maamuzi waliyoyafikia ya kamati ya nidhamu na kuwafungulia baadhi ya wanafamilia wa mpira waliokuwa wamefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi.

  0 0


  NA EVELYN MKOKOI.

  NAIBU  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga  Mpina ,amesitisha uchimbaji na uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo yasiyo rasmi.

  Pia ametoa siku 30 kwa Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kubaini na kutenga maeneo ya uchimbaji ya mchanga ambayo yapo ndani ya manispaa zao yatakayo ruhusiwa kwa zoezi hilo kisheria.

  Akitoa agizo hilo Dar es Salaan leo,wakati wa ziara ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju alisema kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika Kwa urahisi, manispaa zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na kuyabaini kama kunauwezekano wakuchimba mchanga.

  Alisema ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa  kuandaa utaratibu mfupi wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Halmashauri pamoja na Nemc.

  “Halmashauri zote zilizo na eneo ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufata taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”alisisitiza Mpina

  Alisema watafanya Operasheni ya  usiku na mchana kuhakikisha watu watakaoendelea kuchimba  mchanga na kuchota mchanga sehemu ambazo haziruhusiwi watachukuliwa  hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.

  Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunju Bw. Kateni Nassor Msangi alimshukuru Mpina kwa kufanya ziara katika eneo hilo na kuiomba serikali kufanya utaratibu wa kujengea mawe katika kuta za kingo yam to huo ambao umeharibika vibaya, ili kuweza kunusuru mazingira ya mto huo kuharibika pamoja na kunusuru makazi yao.
  DSC_0014
  Eneo la mto Nyakasangwe lililopo kaika kata ya Bunju linavyoonekana kuharibika vibaya kutokana na uchimbaji wa mchanga , na kupelekea makazi ya wananchi kuwa hatarini.
  DSC_0025
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina  akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukamilika kwa zoezi la kukagua mto Nyakasangwe, uliopo katika kata ya Bunju ulioharibiwa vibaya na uchimbaji wa mchanga.
  DSC_0044
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa kituo cha Radio cha Efm kinachopatikana katika masafa ya 93.7 katika jiji la Dar es Saalam alipokuwa akimuuliza maswali kuhusu uchafuuzi wa mazingira utokanao na uchimbaji wa mchanga katika eneo la Boko.

  0 0

  Leo ni Siku kubwa kwa mchezo wa mpira wa miguu nchini hususan washabiki na mchezo huo murua, baada ya kamati ya nidhamu kuitengua adhabu yangu ya kufungiwa mwaka mmoja,kujihusisha na masuala ya kandanda ndani na nje ya nchi. 

  Adhabu hii ilikuwa inaiumiza sana klabu yangu na kuiondolea haki yake muhimu, ya kuwapa habari kwa wakati watanzania juu ya kinachoendelea kwenye klabu. 

  Kiukweli niishukuru kamati ya nidhamu chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas kwa kuiondoa adhabu hii, kiukweli alioondolewa adhabu sio Haji, ni Simba na mchezo wenyewe wa Soka. 

  Hakika hawa wamesikia kilio cha wengi, na kilio cha wengi kina nguvu ya Mungu Mwenyezi, Shukran kwa Mola kwa kuwapa nguvu hii kina Tarimba na wenzake. 

  Niwashukuru pia viongozi wa TFF kwa utashi wao kwenye hili. 

  Nitakuwa mjinga nisipowashukuru wanasimba wenzangu ambao siku zote wamekuwa upande wangu, hawa ninawaahid kuwatumikia kwa moyo na dhamira ileile ya Haji ya kuhakikisha haki na wajibu wetu kama klabu unatekelezwa. 

  Kipekee niwashukuru viongozi wangu wa Simba ambao walihakikisha jambo hili linapatiwa ufumbuzi wa haraka na linamalizika kwa njia ya amani. 

   Mwisho

  niwashukuru watu wote mliokuwa nami ktk sala na dua zenu,hususan kwenye kipindi kigumu cha adhabu. 

  Sitapenda kufukua makaburi, yatupasa sote tusonge mbele, hakuna aliyeshinda, umeshinda mchezo wa soka. 

  Nawaahidi kuendelea kufanya kazi zangu kwa weledi,nidhamu na kwa kuzingatia miiko ya mchezo huu unaobeba dhamana za maisha ya watu walio wengi, sambamba na kuendelea kuitetea na kuilinda klabu yangu kwa nguvu zote. 

  Haji S Manara
  Mkuu wa Habari na mawasiliano
  SIMBA SPORTS CLUB

  SIMBA NGUVU MOJA

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akifafanua jambo mbele ya nwaandishi wa habari (hawapo pichani) akitangaza uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) pamoja na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola na kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano wao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) alipokuwa akitangaza uamuzi wa kusitisha uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na wajumbe saba wa Bodi ya baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam.Picha na: Frank Shija - MAELEZO.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Dk. Jane Goodall, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Katika Ujumbe wake Dk. Goodall aliambata na Mama Getrude Mongela na Hadija Simba ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Roots and Shoots pamoja na watendaji wengine wa Taasisi hiyo.

  Katika mazungumzo yao Dk. Goodall pamoja na mambo mengine amezungumzia uharibifu wa shoroba za wanyama pamoja na makazi yao katika hifadhi ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma ambayo ni maarifu kwa uhifadhi wa Sokwe. Alisema kwa sasa hifadhi hiyo imezungukwa na maakazi ya binadamu hali iliyosababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wanyama hao.

  Aidha Dk. Goodall alimuelezea Makamu wa Rais jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kupambana na uharibifu wa mazingira katika hifadhi ya Gombe ikiwemo kuhimiza uwepo wa mipango bora ya matumizi ya ardhi.

  “inawezekana tatizo kubwa linalosababisha uharibu wa mazingira ni umasikini na uelewa mdogo wa wananchi” alieleza Dk.Goodall. Hata hivyo alisema zipo jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kutoa elimu kwa umma. Kwa sasa wananchi kutoka katika vijiji zaidi 52 mkoani wa Kigoma wanapatiwa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira. Vilevile, jumla ya shilingi Milioni 400 zimekopeshwa kwa wananchi wa vijiji 32 ili kujiwezesha kiuchumi na kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira hususan yenye leno la kulinda shoroba na makazi ya Sokwe. Hali hii imeanza kuleta mafanikio.

  Dk. Goodall ametaja changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira ya Gombe kuwa ni kuwepo kwa wakimbizi kutoka Burundi ambao kwa kiasi kikubwa hushiriki katika shughuli ambazo husababisha uharibu wa mazingira kama vile kilimo na ufugaji usio endelevu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na akiwa kwenye kikao na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu kinachomuelezea Jane Goodall na miaka 50 alioishi Gombe kutoka kwa Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall. Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava.  0 0

  UONGOZI wa Klabu ya Yanga umejaza nafasi zilizoachwa wazi kwa mujibu wa katiba ibara ya 28:(1)d  ikiwa ni maazimio ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokaa tarehe 15/7/2017.

  Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji kikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga kimeweza kufikia maazimio hayo kutokana na ibara hiyo anakuwa na mamlaka ya kujaza nafasi zile zilizoachwa wazi na wajumbe wa kamati.

  Kikao hicho kimeweza kuwateua wajumbe watatu ambao ni Mohamed Nyenge, Tonny Mark na Majid Suleiman ambao wataanza majukumu yao yataanza moja kwa moja wakichukua nafasi za wajumbe wawili walioamua kujiweka pembeni pamoja na  mjumbe aliekuwa mwenyekiti wa kamati ya mashindano Mhandisi Malume aliekwenda nje ya nchi kwaajili ya masomo.

  Pamoja na hilo, uongozi wa Yanga mapema wiki hii iliweza kukutana na kufanya kikao na wachezaji wa zamani wa timu hiyo na kufikia maazimio mbalimbali yenye malengo ya kuisaidia timu yao na kushirikiana nao bega kwa bega.
  Maazimio hayo ni :

  1.Kuwashirikisha katika masuala ya klabu na kuwaweka karibu na klabu.

  2.Kujenga umoja wa wana Yanga kwa ujumla.

  3.Kuunda safu ya uongozi wao itakayorahisisha mawasiliano baina yao na uongozi wa klabu.

  4.Kuweka kumbu kumbu kwaajili ya historia ya klabu na vizazi vijavyo kupitia wao.

  5.Kusaidiana katika suala zima la ugunduzi wa vipaji vya wachezaji kwa manufaa ya klabu.  0 0
  0 0

  MBUNGE wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo kuongeza bidii ikiwemo kujikita kwenye masomo ya sayansi ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ilivyopo hapa nchini. Balozi Adadi aliyasema hayo jana wakati alipokabidhi vifaa vya maabara kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya ElimuSayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa chini. 
  Alisema vifaa hivyo ambayo vimetolewa katika shule 7 kati ya 24
  wilayani humo vitakuwa ni chachu ya wanafunzi kuweza kufikia malengo yao ya kufanya vizuri katika masomo yao katika hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya Muheza. “Jambo hilo ni nzuri na hasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kutaka vifaa hivyo vikabidhiwe katika shule ambazo zitakuwa zimekamilisha ujenzi wa maabara na vitaweza kuwapa mwanga mzuri kusoma kwa bidii “Alisema. 
  Alisema ni jambo la ajabu iwapo vifaa ambazo vimekabidhiwa vitatumika vibaya kitendo ambacho kitakwamisha juhudi za serikali za kutaka wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kuendana na sera ya viwanda. “ Vifaa hivi ambavyo mmekabidhiwa leo hii vinagharama kubwa hivyo niwaombe ndugu zangu mhakikishe mnavitunza ili viweze kutumika katika matumizi yaliyokusudiwa lakini pia niwatake wanafunzi mhakikishe mnasoma kwa bidii “Alisema .
  Mbunge huyo alisema lipo tatizo la kubwa la kutokuwepo vifaa vya maabara katika shule nyingi za sekondari hapa nchini jambo ambalo limeanza kupatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya elimu ili kuona namna ya kulimaliza. 
  Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akionyesha moja kati ya vifaa vya maabara ambayo wilaya ya Muheza imepatiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari wilayani humo juzi wakati alipokwenda kukabidhi kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Luiza Mlelwa kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wilaya hiyo Julitha Akko 
  Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Muheza High School,Luqman Mustapha akimueleza Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu juzi namna wanayotumia vifaa vya maabara walivyopatiwa wakati alipokabidhi vifaa vya maabara kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa nchini 


  0 0
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wafanyakazi wakati wa mafunzo ya kuandaa mpango mkakati wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

  Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfuatilia kwa makini mwenzeshaji kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Andrew Mbwambo wakati wa mafunzo ya kuandaa mpango mkakati wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

  Wawezeshaji wa kuandaa mpango mkakati wa utendaji kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miaka mitano kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe wakimsililiza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfuatilia kwa makini mwenzeshaji kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. AndrewMbwambo wakati wa mafunzo ya kuandaa mpango mkakati wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

  Picha na JKCI.

  0 0  0 0

  WITO umetolewa kwa washindi wa bahati nasibu ya Biko wanaoendelea kupatikana kila siku wafanye vitu vya maendeleo mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake.
  Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alipokuwa anamkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Jumadili (Jumapili), Fredy Nyari, akiwa ni mshindi wa droo ya 23 ya Biko.

  Akizungumzia hatua ya makabidhiano ya fedha hizo, Heaven, alisema kwamba ikiwa siku zote mtu anakosa mtaji wa kuanzisha au kuendeleza biashara zake, kupata Milioni 20 kwa mara moja si jambo la mzaha.


  Alisema ni wakati wao sasa washindi wote wa Biko wale wanaopata zawadi nono ya Sh Milioni 20 inayotoka kila Jumatano na Jumapili pamoja na zawadi za papo kwa hapo zinazoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja wanakuza uchumi wao.

  “Kwa kuanzia Sh 1,000 tu mtu anaweza kushinda 5,000 hadi Milioni 20 kwa droo zetu kubwa, ambapo ni rai yetu kwa washindi wote kuwataka maisha yao yabadilike kwa kutumia vyema fedha zao baada ya kucheza Biko, mchezo unaochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za TIGO Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya Kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.


  Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kulia akimkabidhi kiasi cha Sh Milioni 20 mshindi wao Fredy Nyari wa Kigamboni aliyeibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 katika droo ya 23 juzi. Kushoto ni Afisa wa NMB.

  Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko droo ya 23, Fredy Nyari, akiwa na uso wa furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.
  Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa na mshindi wao wa Sh Milioni 20 Fredy Nyari baada ya kumkabidhi fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam leo mchana.


  0 0
 • 07/17/17--11:32: JIONEE MAAJABU


 • 0 0

  Na Is-haka Omar, Zanzibar.  
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ameshiriki katika mazishi ya watoto wanne waliofariki dunia  jana (juzi) baada ya kuingia kwenye gari iliyokuwa sehemu ya maegesho na likajifunga hali iliyopelekea watoto hao kukosa hewa na kufariki huko Kidongo Chekundu Unguja.   
  Marehemu hao waliotambuliwa kwa majina ya Mwatma Mohamed Malawi (2), Haisam Mustafa(2), Munawar Ahmed Khamis (3) na Muslim Hamza bakar (2) wote wamezikwa leo katika maeneo tofauti ya Makaburi ya Mwanakwere na Kiembe samaki Mbuyu Mnene Unguja. 
  Akizungumza mara baada ya maziko hayo Naibu Katibu huyo huko katika makaburi ya Mwanakwerekwe, alisema CCM imepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa ya vifo vya watoto hao na inatoa mkono wa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizopata msiba huo na kuwasihi waendelee kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha msiba huo.
  Alisema watoto hao walitarajiwa kuwa ni miongoni mwa viongozi na wataalamu wa fani mbali mbali wa baadae hivyo msiba huo umeacha pengo kubwa  kwa familia na taifa kwa ujumla.
  Aidha Dkt. Mabodi aliwataka wazazi na walezi nchini kuwa karibu na watoto wao kwa kuhakikisha mazingira yanayotumiwa na watoto kucheza yanakuwa katika hali ya usalama ili kuepuka athari zinazoweza kusababisha majeraha ama vifo kwa watoto wao.
   Maiti za watoto wanne waliofariki ndani ya gari huko Kidongochekundu  Zanzibar wakitolewa msikitini na kupelekwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe kwa ajili ya mazishi.

   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akishirikiana na waombolezaji wengine katika mazishi ya watoto hao.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akishirikiana na waombolezaji wengine katika mazishi ya watoto hao. 

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awasili mkoani Tanga kutatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo pamoja na mikoa inayopakana nayo.
  Katika ziara hii Waziri Lukuvi leo amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo kati ya Wilaya ya Kiteto Iliyopo Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi iliyopo mkoani Tanga ikiwa muendeleo zo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.
  Waziri Lukuvi anatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya ziara yake mkoani Tanga.

  Ikumbukwe mnamo tarehe 18 Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya  ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.
  Ili kutekeleza agizo hili wakuu wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.
  Aidha, wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto walimlalamikia Waziri Lukuvi kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo ajulikanae kwa jina la Le-Mash Enterprises Limited.
  Baada ya Waziri Lukuvi kusikiliza malalamiko hayo, ameahidi kutembelea mashamba hayo kesho ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wanakabiliwa na mgogoro huu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera wakiwasikiliza wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi katika kutatua mgogoro wa mpaka unaoikabili mikoa hiyo.
   Wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto wakiwasilisha malalamiko yao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi baada ya kukutana nae.
   Eneo la Mji wa Lushoto mkoani Tanga.
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi  (katikati) alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela (wanne kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera na (watatu kushoto) pamoja na viongozi wengine.
   Wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto wakiongozwa na Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Shangazi (wasita Kulia) walipokutana Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi

  0 0


  0 0  0 0

   Mbunge wa Manonga / Igunga Seif Khamis Gulamali akimpokea na kumpa sapoti ya safari yake Muigizaji wa Filamu za Kihindi Sanjay Dutt kwenda Mapumzikoni Mbuga za Wanyama Ngorongoro Mkoani Arusha Mapema leo
   Mbunge wa Manonga / Igunga Seif Khamis Gulamali akimpokea na kumpa sapoti ya safari yake Muigizaji wa Filamu za Kihindi Sanjay Dutt kwenda Mapumzikoni Mbuga za Wanyama Ngorongoro Mkoani Arusha Mapem leo  Muingizaji wa Filamu za Kihindi Sanjay Dutt akipanda ndege tayari kwa kuruka  kwenda Mapumzikoni Mbuga za Wanyama Ngorongoro Mkoani Arusha Mapema leo

  0 0

   Rais Mtaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akilakiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipofika kumpa pole kwa msiba wa mke wa Waziri huyo mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Rais Mtaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiongea na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipofika kumpa pole kwa msiba wa mke wa Waziri huyo mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz (kulia) akimpa mkono wa pole  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati walipoenda kumpa pole Waziri Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam, kulia ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu na kushoto ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe.  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametoa siku saba kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam DCP Lucas Mkondya kuhakikisha wizi wa vifaa vya Magari unakomeshwa mara moja.

  Akitoa maagizo hayo, Mheshimiwa Makonda amesema wizi wa vifaa vya magari vikiwemo Vioo, Radio, Side mirrow, Power Window,Taa pamoja na Shoo ya mbele na nyuma ya Gari vimekuwa vikishamiri kila kukicha jambo linalowakera wananchi na kuwapa hofu ya kuweka magari yao kwenye maegesho kwa kuhofia kuibiwa kitendo ambacho amesema hakivumiliki.

  “Sitaki kusikia watu wanaibiwa vifaa vya Magari yao,watu wanaibiwa Vioo, Power Window,Radio, Taa,Side Mirror na wakati mwingine wanavunja vioo vya gari na kuiba Pochi na Laptop, sasa haiwezekani wizi wa namna hii uendelee kwenye Mkoa  wangu, sasa Kaimu Kamanda Kanda Maalumu nakuagiza na ninakupa siku saba sitaki kusikia wizi wa vifaa vya magari ukiendelea, nataka ifikie hatua mtu aweze kuegesha Gari lake na kulikuta likiwa salama” Alisema Makonda.

  “Mwananchi yoyote atakaeibiwa na akapeleka taarifa Polisi na hatua za kisheria zichukuliwe atoe taarifa kwangu bahati nzuri wananchi wana namba zangu, haiwezekani Mwananchi anajikusanya na kununua gari alafu anaibiwa watu wanaiba vifaa vyake, wizi wa namna hii nasema Mwisho ndio umefika leo," Alisisitiza Makonda.

  Aidha Makonda ameagiza Maduka na Vijiwe vyote vinavyouza vifaa vya Magari kujisajili mara moja iliviweze kutambulika na Serikali.“Kinachoshangaza ni kwamba hawa wanaoiba wana vijiwe vyao ambapo wanauza hivyo vifaa, ukienda Kariakoo, Magomeni na pia Temeke (Keko) kuna vijiwe ambavyo ukienda kule unakuta kifaa kilichoibiwa kwenye Gari lako kipo mtaani kinauzwa” Aliongeza Makonda.

  Akipokea Maagizo hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  DCP Lucas Mkondya amesema kuwa maagizo hayo yanaanza kutekelezwa leo ambapo msako utaanza leo kuhakikisha Genge la wezi wa vifaa vya magari vinasambaratishwa.

  Aidha amewaagiza Makamanda wa polisi Temeke, Ilala na Kinondoni kuanza utekelezaji wa maagizo hayo kuanzia leo na kuwataka wote wanaouza vifaa vya wizi kujisalimisha mara moja kwa Jeshi la Polisi.

  0 0


older | 1 | .... | 1810 | 1811 | (Page 1812) | 1813 | 1814 | .... | 3272 | newer