Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1808 | 1809 | (Page 1810) | 1811 | 1812 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0
  0 0

  Uganda’s Social Services Parliamentary Commission, led by Ms Cecilia Barbara (MP), visited the Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) in Tanzania on Wednesday 12th July 2017, with the aim of borrowing experience from their neighboring country on how to combat heart disease and tackle a wide range of health challenges.
  Since August 2015, Uganda embarked on plans to break ground for a new 200-bed hospital, to be named the Uganda Institute of Cardiothoracic Diseases, to replace the current Uganda Heart Institute (UHI). The new hospital, if completed, is expected to have three operating theatres, cardiac catheterization laboratories, an Intensive Care Unit, and research facilities.
  As part of the mission to expand cardiologic services in Uganda, Ms Barbara, alongside a team of other 10 MPs visited Tanzania’s JKCI—touted by Tanzanians as East Africa’s largest heart institute. It has 103-bed capacity and attends to an average 700 outpatients and 100 inpatients per week. It was officially established in 2015.
  JKCI Executive Director, Professor Mohammed Janabi explains to the MPs from Uganda on how the institute operates/PHOTO-Frank Shija.
  For Source and more CLICK HERE

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, kama ishara ya kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi. Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu   umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimshuhudia Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Hamisi Mwinyimvua akijenga sehemu ya ukuta wa Zahanati mpya ya kijiji cha Rwele wilayani Kyerwa mkoani Kagera hivi karibuni, wakati wa  kuzindua ujenzi wa zahanati hiyo iliyoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi, Mfuko wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu   umetoa jumla ya shilingi milioni 125 kwa ajili ya ujenzi huo,  (katikati) ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen. Mbazi Msuya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

   Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka akipokea sadaka toka kwa waumini mbalimbali  waliohudhuria ibada kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita Leo  Julai 16, 2017

   Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka akipokea sadaka toka kwa Mke wake Mama Janeth Magufuli wakati wa kuchangia ujenzi na upanuzi wa katika kanisa la Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita leo Julai16, 2017


   Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru mmoja wa waumini wa kanisa hilo ndugu Mwita Chacha kwa  kuchangia mifuko mitano ya saruji kwaaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita 
  Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwashukuru waumini walioshiki kuchangia ya ujenzi na upanuzi wa kanisa  Katoliki la  Bikira MariaParokia ya  Chato Mkoani Geita,ambapo zilikusanywa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni kumi na tatu pamoja na ahadi mbalimbali za vikiwemo vifaa vya ujenzi. PICHA NA IKULU


  0 0

  MKAZI wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo amefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro cha droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutesa hapa nchini.

  Droo iliyompa ushindi mnono mkazi huyo wa Kigamboni maarufu kama ‘Jumadili’, imechezeshwa jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

  Akizungumza katika droo hiyo ya aina yake, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kumpata mshindi wao wa Kigamboni ni sehemu ya kuhakikisha kuwa washindi wao wanaendelea kuzoa mamilioni kutoka kwao baada ya kucheza Biko.

  Alisema kila anayecheza Biko anasehemu kubwa ya kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo pamoja kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka katika droo kubwa za Jumatano na Jumapili.

  “Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu mchezo wetu wa kubahatisha unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kupitia miamala ya kifedha kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

  “Ili mtu aweze kushinda anapaswa kucheza mara nyingi zaidi kwa kuanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo mbali na ushindi wa papo kwa hapo unaotoka kila wakati, pia ni fursa nzuri ya droo kubwa ya Sh Milioni 20 ambazo tunaamini mtu akifanikiwa kuzipata kama alivyopata mshindi wetu wa Kigamboni bwana Nyari maisha yake yatapiga hatua kubwa,” Alisema. 
  Mwakilishyi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid kushoto akiandika dondoo muhimu katika droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku' leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Temeke, Fredy Nyari alifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka Biko. Kulia ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.
  Harakati za kumtafuta mshindi wa droo ya 23 Fredy Nyari wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, zilipofikia ukomo kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja kutoa neno kwa wadau na Watanzania kwa ujumla juu ya bahati nasibu ya Biko.  0 0
 • 07/16/17--02:11: SHONZA AMWAGA MINOTI, SONGWE
 • MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza (CCM) ametimiza kwa vitendo   ahadi yake ya kuwawezesha kiuchumi wanawake ambao ni wafuasi wa CCM kwa  kukusanya zaidi ya Sh35 milioni  ambazo wanawake hao walioko kwenye vikundi vya ujasiriamali wapatiwa mtaji wa kiasi cha Sh320,000 kwa kila kikundi.
  Kati ya fedha hizo, Sh 20 milioni zilitolewa na Shonza huku wadau wanaomuunga mkono mbunge huyo wakitoa zaidi ya Sh15 milioni katika harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM kiuchimi ambao ulizinduliwa rasmi juzi na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson.
  Akizungumzia mradi wa uanzishwaji wa mfuko huo, Shonza alisema  moja ya ahadi zake wakati wa kampeni za kuomba ridha ya kuchaguliwa na wanawake mwaka 2015, aliwahakikishia kuwainua kiuchumi na baada ya kuchaguliwa alianza na utaratibu wa kukutana wanawake kwa kila kata  kwa ajili ya kuunda vikundi, kuvisajili ili viweze kukopesheka.

  Alisema jambo lililofanywa na Shonza ni mfano tosha na kudhihiridha kwamba anafanya kazi kwa kutekeleza ilani ya CCM n azma ya Serikali ya kufikia  nchi ya viwanda.
  Katika uzinduzi, huo, Mbunge Shonza  aliungwa mkono na wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Jimbo la Mtama, Livingstone Lusinde ‘Kibajaji’, Mbunge wa Jimbo la Pangani Tanga, Jumaa Awesu, Janeth Mbene wa Ileje na Josephat Hasunga wa wa Jimbo la Vwawa Mbozi.
  “Tayari kuna kikundi kwa kila kila kata ambavyo nilivisimamia mimi kuanzia kupta usajili na vingine vimeanza kazi za ujasiriamali na vina vifanya kazi, kwa kila kikundi niliahidi kuwasaidia Sh200, 000 kama mtaji wa kuanzisha shughuli yoyote ya ujuasiamali, lakini nikaone niwakutanishe wadau wengine watakaoniunga mkono kwenye hili na nashukuru mmeonesha ukweli wenu”.
  Alisema wanawake wa Songwe hawahitaji kutafutiwa kazi maofini, kwani  ni wachapa kazi lakini changamoto waliyo nayo ni mitaji tu kwani uwezo wa kuingia shamba na kuanzisha mradi wowote wa kiujasiriamali wanao.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Tulia aliwataka wabunge wa viti maalum nchini kwenda kutekeleza ahadi walizozitoa  kwa wananchi wakati wakipigiwa kura badala ya kuwatelekeza kwa kisingizio cha kutokuwa na majimbo.
  Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kulia) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza (katikati) wakiwa wamekumbatia kitita cha fedha kiasi cha Sh35 milioni zilizotolewa katika harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha shughuli za ujasiriamali katika vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa rasmi juzi na Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko huo umeanzishwa na Shonza ambapo alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni zikichangwa na wadau wa mbunge huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa Sh320, 000 kutoka Kata zote 100 za Mkoa wa Songwe. 

  Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kulia) na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza wakipanga vizuri kitita cha fedha kiasi cha Sh35 milioni zilizotolewa katika harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha shughuli za ujasiriamali kupitia vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa rasmi juzi na Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko huo umeanzishwa na Shonza ambapo alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni zikichangwa na wadau wa mbunge huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa Sh320,000 kutoka Kata zote 100 za Mkoa wa Songwe. 
  Wabunge wakicheza muziki na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Songwe, waliofika kwenye harambee ya uzinduzi wa harambee ya kutunisha mfuko wa uwezeshaji wanawake wa CCM wa mkoa huo ili kuanzisha shughuli za ujasiriamali katika vikundi kwenye kata zao uliozinduliwa rasmi juzi na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia mjini Vwawa Mbozi. Mfuko huo umeanzishwa na Shonza ambapo alitoa Sh20 milioni huku Sh15 milioni zikichangwa na wadau wa mbunge huyo. Kila kikundi kitapata mtaji wa Sh320, 000 kutoka Kata zote 100 za Mkoa wa Songwe.

  0 0

  Timu ya Soka ya klabu ya Simba kesho alfajiri, inatarajia kwenda nchini Afrika kusini, kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao. 

  Kambi hiyo ya siku Ishirini itahusisha wachezaji wote waliosajiliwa kwenye klabu,kwa msimu huu wa ligi. 

  Kwa upande wa wachezaji waliopo kwenye Timu ya Taifa,wao wataungana na wenzao,mara baada ya mchezo wa marudiano baina Taifa Stars na Rwanda,utakaochezwa wiki ijayo kule Kigali. 

  Ikiwa huko nchini Afrika kusini, kikosi hicho pia kitapata fursa ya kucheza michezo kadhaa ya kujipima nguvu,kabla ya mchezo wake wa tarehe nane mwezi ujao(SIMBA DAY),Mechi ambayo klabu huitumia kutambulisha wachezaji wake na jezi mpya ya msimu,mchezo huo utapigwa hapa jijini Dar es salaam,kwenye uwanja wa Taifa. 

  Wakati huo huo klabu ya Simba inaungana na wanamichezo na watanzania wengine,kumpa pole Waziri wetu mwenye dhamana ya michezo nchini Dr Harrison Mwakyembe kwa kuondokewa na Mkewe bi Linnah Mwakyembe. 

  Tunamuomba Waziri Mwakyembe awe na subira yeye na familia yake katika kipindi hiki kigumu,na klabu itashiriki shughuli zote za msiba wa mama yetu Linnah. 

  IMETOLEWA NA 
  IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO 
  SIMBA NGUVU MOJA

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuachana na nguo za mitumba imewadia kutokana na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo nchini.

  Pia amesema uwepo wa viwanda hivyo utasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika hivyo amewataka walime pamba ya kutosha ili viwanda vipate malighafi.

  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo  jana (Jumamosi, Julai 15, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar Es Salaam.

  Alisema viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.

  Alisema kwa sasa wanunuzi wa pamba hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.

  “Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la uhakika ipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba.”

  Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha saruji cha Lake kinachozalisha saruji ya nyati ambapo aliwapongeza wawekezaji wote nchini kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.

  Katika kiwanda hicho ambacho kinazalisha tani 700,000 kwa mwaka kimeajiri watu 2000 na kinalipa kodi ya  sh. bilioni 81.312 kwa mwaka, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wake wawe waaminifu, wafanye kazi kwa weledi na wawe waadilifu.

  Pia Waziti Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na viwanda sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akingalia mitambo ya kutengeneza Nguo katika Kiwanda cha NIDA kilichopo Tabata Jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu alifanya ziara katika kiwanda hicho Jumamosi Julai 15, 2017. kushoto anayetoa maelezo ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza Nguo cha NIDA, Muhammad Hamza Rafiki na kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Muhammad Waseem.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati)  akionyeshwa Ubora wa Kanga zinazotengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha NIDA wakati alipofanya ziara kiwandani hapoJumamosi Julai 15, 2017. wanao muonyesha kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza Nguo cha NIDA Muhammad Hamza Rafiki na kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda, Muhammad Waseem. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amempa muda wa miezi kumi Mkandarasi wa Kampuni ya CICO anayejenga barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30 kwa kiwango cha lami kukamilisha kazi hiyo.

  Prof. Mbarawa ameyasema hayo mkoani Tabora mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kuelezea kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake.

  “Nakupa miezi kumi tangu sasa hadi mwezi Mei mwakani uwe umeikabidhi Serikali barabara hii”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

  Ameongeza kuwa ukamilishaji wa barabara hiyo uendane na viwango na ubora vinavyoendana na thamani ya fedha waliyopewa ili barabara hiyo iweze kudumu kwa muda uliopangwa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi, amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa kuufuatilia kwa karibu mradi huo ambao utachochea kasi ya maendeleo mkoani humo.


  Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi wa barabara ya Tabora –Nyahua KM 85, wakati alipokagua ujenzi wake, Mkoani humo jana. 
  Muonekano wa sehemu ya KM 6 ya barabara ya Tabora–Nyahua yenye jumla ya urefu wa KM 85, inayojengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani humo. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitazama mchoro wa ujenzi wa kalvati itakayojengwa katika barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30, Mkoani humo jana. 
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi anayesimamia ujenzi wa barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30 Eng. Golam Shahid, kumaliza mradi huo kwa viwango na ubora unaostahili, Mkoani humo jana. 
  Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw. Abeli Busalama, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokuwa akikagua barabara ya Kaliua-Kazilambwa yenye urefu wa KM 56 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani humo jana.


  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Morogoro
    NDEGE zinazorushwa bila rubani kwa ajili ya kupiga picha (Drone) ni marufuku kutokana na msuala ya anga, Mwanasheria wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Bi. Maria Makalla amesema, wakati wa semina ya waandishi ya wahabari iliyofanyika mjini Morogoro mwisho mwa juma.
  Semina hiyo ilihusu kuwaelimisha wanahabari hao juu ya majukumu ya TCAA pamoja na matokeo ya ukaguzi wa kimataifa baada ya Mamlaka hiyo kukaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO).
   Bi Makalla amesema ndege zisizo rubani hazitakiwi zirushwe kiholela kwani kama ilivyo sehemu zote duniani zinatakiwa kuwekewa kanuni kutokana na usalama wa anga.
  "Wanaomiliki drones kwa sasa wasizitumie mpaka utaratibu mahususi wa namna ya kuzitumia utakapotoka, ikiwa  ni pamoja na mamlaka kujua wamiliki wote wa ndege hizo na jinsi ya kuzitumia.
  "Drones ni ndege ndogo na zina athari kubwa endapo huko angani zitakutana na ndege nyingine na kusababisha ajali," amesema mwanasheria huyo wa TCAA.
  Ameweka bayana kwamba utaratibu unaandaliwa  na kwamba wadau wote wanaomiliki drones itabidi kwanza  kuelimishwa masuala ya usalama wa anga na kujua kanuni zake zitazotungwana kutolewa  kwa mujibu wa sheria.
  "Masuala ya anga ni mapana na kila siku teknolojia zinabadilika katika matumizi ya anga hivyo inatupasa sote kwenda kwa mujibu wa  kanuni za teknolojia hizo", alisema.
   Mwanasheria Mwandamizi waMamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Maria Makalla akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari juu ya majukumu ya  Mamlaka hiyo pamoja na matokeo ya ukaguzi wa kimataifa Mamlaka ilivyokaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wa semina iliyofayika mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina  hiyo iliyofayika mjini Morogoro mwishoni mwa juma.


   Meneja  Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), BestinaMagutu  (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya majukumu ya Mamlaka hiyo

  Mwanasheria Mwandamizi waMamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bi. Maria Makalla akiwa na 
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria semina ya majukumu ya  TCAA pamoja na matokeo ya ukaguzi wa kimataifa Mamlaka ilivyokaguliwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) wakati wa semina iliyofayika mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina  hiyo iliyofanyika mjini Morogoro mwishoni mwa juma.  0 0

  Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) imepata viongozi baada ya kufanyika uchaguzi huru wa kidemokrasia siku ya Jumamosi ya tarehe 15 July 2017 katika jiji la London. Mgeni rasmi alikua ni Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa.
  Viongozi waliochaguliwa ni: Dada Lynne Kimaro (Mwenyekiti), Ndg. Omwami George Ndibalema (Makamu Mwenyekiti), Ndg. Lazaro Matiku (Katibu), Dada Halima Yusuph (Naibu katibu), na Dada Edith Kimaro (Mweka Hazina)
  Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Diaspora Community United Kingdom of Great Britain & NI, kila jumuiya za matawi zinatakiwa kuchagua wawakilishi wawili (2) katika Baraza (The Council) la Tanzania Diaspora UK. Wajumbe watachaguliwa hapo baadae. 
  Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana katika hatua hio kubwa na ya muhimu katika ujenzi wa Umoja wa Watanzania UK 
   Asanteni, 
  Uongozi Tanzania Diaspora Community/Association 
  United Kingdom of Great Britain & Northern Ireland
  Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa (wa pili kulia) akiwa na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa London
  Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania London Dada Lynne Kimaro
  Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa akiwa katikia picha ya pamoja na wanachama na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania London. Picha kwa hisani ya  TZUK

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri  Julai 16, 2017.
   Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alip hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri Julai 16, 2017.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri Julai 16, 2017. 
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


  0 0  0 0
  0 0

   Waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako alifanya ziara ya ghafla katika shule Mkoani Iringa. Alitembelea shule zinazo fundisha watoto wenye mahitaji maalum za Makala Wilaya ya Mfundi, Shule ya viziwi Mtwivila, Shule ya sekondari ya wasichana Mtwivila na shule ya sekondari ya Lugalo.

   Nia ya ziara hiyo ni pamoja na kukagua vifaa vya kufundishia ambavyo serikali imetoa. Pia alipta fursa ya kusalimia wanafunzi na walimu. Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza, Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Bi wamoja Ayoub, Wakuu wa wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri David na Iringa Mhe.Richard Kasesela. Pia wabunge waheshimiwa, Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mch Peter Msigwa​.
  Waziri Ndalichako akipokelewa na Mkuu wa wilaya ya Iriga mjini Mh Richard Kasesela pamoja na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mh.Peter Msigwa mara baada ya kuwasili ndani ya Manispaa ya Iringa 
  Waziri Prof.Ndalichako  akisikiliza jinsi ya kufundisha watoto wenye ulemavu wa kusikia​.
  ​Waziri Prof. Ndalichako akiongea na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini,Mhe.Peter Msigwa katika Shule ya Viziwi, Mbunge Viti Maalum Mhe Zainab Mwamwindi akisikiliza​
  Waziri  Profesa Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Iringa girls 
  picha ya pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum
  Waziri Profesa Ndalichako akiongea na wananfunzi wa Shule ya sekondari Lugalo kidato cha 5

  0 0


   Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart ikishirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),sambamba na Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,wanatarajia kuanzisha msako mkali kwa wale wote wanaofanya biashara ya uharamia wa kazi za Wasanii hapa nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,Mkurugenzi wa Msama Auction Mart,Alex Msama alisema kuwa tayari wameishapata kibali na kupewa baraka zote za kuifanya kazi hiyo,ya kuhakikisha wizi/uharamia wa kazi za Wasanii unapungua ama kufika kikomo kabisa.

  “Tayari tumepata kibali,hivyo Sisi kama kampuni tumejipanga vyema kukabiliana na hayo mapambano ya wizi wa kazi za Wasanii,tutakae mkuta anauza nyimbo za CD feki,ama anauza nyimbo za wasanii kwa kuziweka kwenye flash,kwenye simu sambamba na wale wote wanaomiliki kompyuta kwa kufanyia kazi hiyo ya kuuza nyimbo za wasanii kinyume cha sheria, tutawakamata popote pale walipo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria”alisema Msama.

  Amesema kuwa Wasanii wameibiwa vya kutosha,ifike mahali nao sasa wanufaike na jasho la kazi yao,na si kumnufaisha mtu mwingine,alisema na kuongeza kuwa Wasanii wamekuwa wakilalamika muda mrefu kuhusiana na hili jambo la kuibiwa kazi zao na kusambazwa hovyo hovyo bila utaratibu wa aina yoyote,wao kama kampuni watalibeba jukumu hilo huku wakiamini ushirikiano ndio jambo kubwa la kuifanikisha kazi hiyo  yenye changamoto kubwa.

  “Tunawaomba wasanii mbalimbali na Wadau wa sanaa ya Muziki,watuunge mkono ikiwemo na kutupa ushirikiano wa taarifa,zikihusu maeneo yoyote ambako uharamia wa kazi zao unafanyika,nasi tutachukua hatua za haraka na kuwakamata wahusika”alisema Msema.

  Msama alimaliza kuwa kuwapa tahadhari ya mapema kwa wale wote wanaouza kazi wasanii kinyume cha sheria,hasa katika vituo vya mabasi,nyumbani,kwenye Maduka ya biashara waache mara moja,wakipuuza wajue kabisa kiama chao kimefika.

  0 0


  Siku ya Ijumaa 28 Julai 2017 Saa 2.00 Usiku ,Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni au Viumbe wa ajabu “Anunnaki Aliens” yenye makao yake

  nchini Ujerumani inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho la wazi la Orient-Afrika litakalo fanyika mjini Bonn,Ujrumani siku ya Ijumaa 28.Julai 2017

  saa 2.00 Usiku(20.00 hrs),bendi hiyo inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja inadumu katika medani ya muziki kwa miaka 24 na kufanikiwa kuteka washabiki wa kimataifa,pamoja na kuachia nyimbo na CD kadha

  bendi hiyo imejizolea umaarufu katika majukwaa ya kimataifa wa mdundo wa Extraordinary “Bongo Dansi” unaowatia kiwewe washabiki barani ulaya. Usikose kujumuika nao at www.ngoma-africa.com au www.instagram.com/ngomaafricaband

  0 0  0 0   Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka (kushoto)akisalimiana na Katibu wa CCM Wilaya ya UVINZA ndg Evarist Mkuluge alipopokelewa Katika kata ya Nguluka Wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma.
   Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka (katikati) akikaribishwa rasmi na gwaride la vijana wa Green Guard Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza
   Shamrashamra za Vijana wa Boda boda katika mapokezi ya Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza
   Shamra Shamra za wanachama wa Chama cha mapinduzi katika mapokezi ya Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1808 | 1809 | (Page 1810) | 1811 | 1812 | .... | 3278 | newer