Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: SERIKALI YAPONGEZA UTENDAJI KAZI KIWANDA CHA VIATU CHA MAGEREZA KARANGA MKOANI KILIMANJARO


INTRODUCING "AGNES" BY DEKULA KAHANGA

BREAKING NEWZZZ: VIONGOZI 6 WA CHADEMA AKIWEMO MBUNGE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA

0
0
Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia viongozi 6 wa kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma kupitia chama hicho Mhe Zubeda Sakuro kwa tuhuma za  kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa na kuzua vurugu wilayani Nyasa mkoani Ruvuma. Hii hapa taarifa yake.

WAZIRI LUKUVI AKESHA KUSHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI

UJENZI WA BARABARA ZA JUU UBUNGO WAENDELEA KWA KASI

Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu lazinduliwa Zanzibar

0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Ndege wakati akizindua Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu (STEM) kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed  Shein hapo Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni.
 Balozi Seif akizindua Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu (STEM) kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed  Shein.
 Baadhi ya wageni na walikwa kutoka Chuo Kikuu cha cha George Mason cha Nchini Marekani wakishuhudia  uzinduzi wa Tamasha la kushajiisha Elimu ya Mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu 
 Balozi Seif akisalimiana na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Profesa Mshimba nje ya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi wakati wa mwanzo wa mafunzo ya Sayansi, Teknolojia na Uhandisi wa Hesabu. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Walimu wa Hesabu Tanzania, Mwalimu Said Sima.
Mkuu wa Timu ya Wakufunzi kutoka Chuo Kikuu cha George Mason Nchini Marekani Profesa Padu kati kati akimpatia maelezo Balozi Seif  juu ya ufundishaji wa masomo ya Sayansi, Teknolojia na Hesabu kwa wanafunzi wa Fani hiyo. Nyuma ya Profesa Padu ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uwezeshaji kwa wote Zanzibar iliyoandaa Mafunzo hayo ya STEM  Bibi Giftness Castico. Picha na – OMPR – ZNZ.

MWIGULU NCHEMBA AMWAKILISHA RAIS KATIKA MAZISHI YA WAZIRI WA USALAMA WA KENYA

0
0
Courtesy of Citizen TV

Vijana Waja na Mapendekezo Maboresho Sera ya Taifa ya Vijana

0
0
 Asasi za Kiraia za zinazounda Umoja wa AZAKI za juu ya masuala ya Bunge kwa kushirikiana na asasi zingine waja na mapendekezo katika kuboresha Sera ya Taifa ya Vijana ya mwaka 2007 ili iendane na wakati pamoja na mabadiliko ya kiteknolojia.
Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) ambayo ni Asasi kiongozi Bw. Suleiman Makwita wakati akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera hiyo.

Makwita amesema kuwa lengo la kufanya mapitio juu ya Sera hiyo ni kuangalia namma ambapo wanaweza wakaishauri Serikali maeneo ya kufanyia maboresho katika Sera hiyo ya vijana.

“lengo la kufanya uchambuzi huu ni kuiomba Serikali na wadau wote wa maendeleo ya vijan nchini kuweka mazingira rafiki yatakayochochea maeneleo ya vijana kupitia sekta rasmi na zisizo rasmi ikijuisha masuala mtambuka na kuendana na dhana ya maelengo endelevu ya dunia” alisema Makwita.

Akizungumzia matokeo ya uchambuzi huo Makweta alisema kuwa wamebaini baadhi ya changamoto zilizopo katika Sera ya Vijana ya Mwaka 207 na hatimaye wamekuja na baadhi ya mapendekezo kama njia ya kusaidia kuiboresha Sera hiyo.

Baadhi ya mapendekezo waliyokuja nayo ni pamoja na kuanishwa kwa umri wa kijana kuwa miaka 13 -35 tofauti na sasa ambapo kijana anatambuli kuwa na umri kati ya 15 hadi 35.

Aliongeza kuwa katika masuala ya afya Sera inapaswa kukugusia masuala yote yanayoathiri vijana kama vile afya ya uzazi, anemia,TB na Selimundu, badala ya kutilia mkazo kwenye VVU/Ukimwi pekee.

Pamoja na mapendekezo hayo Makwita aliipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa vijana kijana, pamoja nakufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya wadau mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa Baraza la Taifa la Vijana.

Uchambuzi huu wa Sera ya Taifa ya Vijana ya Mwaka 2007 umefanywa kwa ushirikiano baina ya umoja wa AZAKI za Vijana juu ya Masuala ya Bunge na Mtandao wa AZAKI za Vijana juu ya Masuala ya Afya ya Uzazi chini ya uongozi wa Asasi ya Dray a Vijana Tanzania (TYVA).

Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman Makwita akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana  ya mwaka 2007 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa pamoja na baadhi ya wananchama wa asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman Makwita akiwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana  ya mwaka 2007 mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa pamoja na baadhi ya wananchama wa asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. 
Wanachama wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakiwa katika pica ya pamoja mara baada ya kumaliza kuwasilisha muhtasari wa uchambuzi wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana  ya mwaka 2007 kwa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. 

YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO July 15, 201

0
0


Tume ya vyuo vikuu nchini TCU imetangaza mfumo mpya kwwa kuomba nafasi ya kusoma vyuo mbalimbali hapa nchini; https://youtu.be/_1aKVh0VNrA

Waziri Prof.Makame Mbarawa autaka uongozi unaosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kufanya marekebisho ndani ya uwanja huo; https://youtu.be/f76RK0Bq6Oc

Wakazi wa mkoani Lindi walia na uhaba wa mafuta kutokana na mamlaka ya mapato TRA kufunga vituo ambavyo havina mashine ya EFD; https://youtu.be/F9s6RrOtGOc

Tazama mazungumzo kwa kina kutoka kwa msanii wa muziki wa Bongofleva Barnaba akizungumzia safari yake ya muziki hapa nchini http://simu.tv/Jllvf5A

Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa awataka wakazi Tabora kulinda miundombinu ya uwanja wa ndege wa Tabora. https://youtu.be/sRAbKNGdqFk

Naibu waziri Selemani Jafoa amewataka viongozi wa halmashauri kupeleka michango ya watumishi katika mifuko ya hifadhi ya jamii; https://youtu.be/0k7Hs2h3vM8

Naibu waziri wa elimu Mhandisi Manyanya aitaka manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kuboresha miundombinu ya shule za msingi; https://youtu.be/G7BTtHJwRMw

Serikali imeanza ujenzi wa shule maalum kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia wilayani Arumeru katika kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu; https://youtu.be/46wgxBHzfWA




MAGAZETI YA JUMAPILI LEO JULAI 16,2017

NEWS ALERT: MATOKEO YA MTIHANI YA KIDATO CHA SITA SHULE ZOTE ZA SEKONDARI NCHINI

DC HOMERA ATOA MSAADA WA BATI 100 NA MIFUKO 100 YA SARUJI KWA SHULE MBILI ZA TUNDURU

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mhe. Juma Zuberi Homera ametoa msaada wa bati 100 na mifuko ya saruji 100 kwa shule ya msingi msinjili iliyopo kijiji cha msinjili kata ya Mlingoti magharibi Tarafa ya Mlingoti.
Dc Homera ameainisha matumizi ya msaada huo kama ifuatavyo, bati 25 na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya msingi msinjili Iliyopo katika kijiji cha msinjili na Bati 60 pamoja na mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kuezeka nyumba za walimu wawili wa shule ya msingi mwangaza zilizoezekwa kwa nyasi, sambamba na hayo aliagiza madarasa katika shule hio zikarabatiwe.

Article 3

HAFLA YA SIKU YA TANZANIA KATIKA JIJINI OTTAWA, CANADA, YAFANA SANA

0
0
Tarehe 14 Julai, 2017 ilikuwa ni siku ya Tanzania Jijini Ottawa, Canada. Siku hii ilikuwa ni mwendelezo wa sherehe za kuazimisha miaka 150 ya uwepo wa Taifa la Canada. Mamlaka ya Jiji la Ottawa ilitoa fursa kwa ofisi mbalimbali za kibalozi kushiriki katika sherehe hizo ambazo zimekuwa zikiendelea tangu Januari 2017. Tarehe 14 Julai ilipangwa kwa ajili ya Tanzania.  Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Ottawa ulitumia siku hiyo kuitangaza nchi yetu katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi, utalii na utamaduni.

Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka akiwa na mkewe Bi. Esther Zoka, akikata utepe kuashiria kuanzishwa kwa shughuli mbalimbali zilizofanyika siku hiyo.

Bi. Petronilla Lyimo, Mshereheshaji wa siku hiyo ambaye ni mke wa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya ya Wana-diaspora wa Tanzania Jijini Ottawa (TAO)
Mhe. Balozi Jack Zoka akimtembeza Meya Jim Watson kwenye maonyesho ya vikundi mbalimbali vilivyoshiriki siku hiyo.
Afisa wa Ubalozi Bw. Leonce Bilauli akitoa zawadi kwa Meya wa Jiji la Ottawa Jim Watson alipotembelea ukumbi wa maonyesho akishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka.

 Afisa wa Balozi Bi. Aziza Bukuku akiwa kwenye banda la Ubalozi akielezea wageni kuhusu Tanzania. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

TANZIA: WAZIRI HARRISON MWAKYEMBE AFIWA NA MKEWE


Wahitimu waliosoma China waombwa kuisaidia Tanzania katika uchumi wa viwanda

0
0
WAZIRI wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga amesema wanafunzi wahitimu kutoka vyo vya nje ya nchi waunde umoja wa mataifa waliyotoka ili kuwa na jukwaa la kuvuna wataalamu pamoja na wao kutambuana.
Alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizindua Chama cha wanafunzi waliosoma China (CAAT), jijini hapa ambapo alibainisha vyama vingi vya aina hiyo vimeanzishwa na kupotea kutokana na kukosa msukumo kutoka serikalini.
“Nyinyi mtakua kiungo kati ya wasomi kutoka China, serikali na jamii, hiki ni chama cha kwanza cha wanafunzi waliosoma  China. Matarajio yangu ari iliyowafanya kujipanga pamoja itabaki daima na naamini chama hiki kitakua jukwaa la wanafunzi wanaoendelea kusoma na waliohitimu,” alisema Balozi Mahiga.
Aliongeza kuwa: “Najua kuna Wachina nchini walioanzisha viwanda na wangependa kupata vijana wasomi, hii ni fursa pekee ya kuendeleza sekta binafsi na kudumisha urafiki wetu. Ningeshauri idara za serikali na sekta binafsi kuwa karibu na chama hiki.
“Nimezungumza nao na nimeona aina ya utaalamu waliokuwa nao, utaalamu huu utasaidia kuleta tija kwa idara mbalimbali na wizara pamoja na taasisi za umma. Nitaangalia namna wizara yangu itakavyokisaidia chama hiki ili tusiwaache peke yao ubunifu waliofanya ni wa ahali ya juu kabisa.”
Balozi  msaidizi wa China nchini, Bw.

 Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine Mahiga Wa kwanza (kushoto) ni  Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong  wa pili (kulia) ni  Balozi wa Tanzania Nchini China Bwana. Mbelwa Kairuki wakinena jambo kwenye  hafla  fupi ya kuzinduzi wa Ofisi za umoja wa wahitimu Wanafunzi   Watanzania walio Soma nchini China au China Alumni Association of Tanzania(CAAT) iliyofanyika
jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine akinena jambo na  Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye hafla  fupi ya kuzindua Chama cha umoja wa wahitimu, Wanafunzi    Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT)  jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine akiambatana  na  Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye uzinduzi wa ofisi za  umoja wa wahitimu, Wanafunzi  Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT) ) iliyo fanyika Posta  jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Mhe, Dkt, Augustine Katikati akipata picha ya pamoja na  wanaumoja wa (CAAT)  wapili (kulia) ni Balozi wa Tanzania Nchini China Bwas.  Mbelwa Kairuki  wa kwanza (kushoto) ni Mwenyekiti wa  (CAAT)  DKT.Liggy Vumilia  wa pili (kushoto) ni Balozi msaidizi wa China Bwana. Gao Haudong kwenye  hafla  fupi ya kuzindua Ofisi za  Chama wa wahitimu, Wanafunzi   Watanzania walio Soma Nchini China (CAAT) iliyo fanyika  jijini Dar es salaam.Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Treni ya kitalii ya Rovos Rail yawasili Dar es Salaam na watalii 65

0
0
KUWASILI kwa watalii 65 kwa treni inayoshikilia nafasi ya pili kwa ufahari duniani Rovos Rail, kumeendelea kuiweka Tanzania katika ramani nzuri kama sehemu salama kwa utalii na mapumziko.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo katika kituo cha TAZARA jijini hapa, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devota Mdachi amesema fursa kama hizo zinapojtokeza ni wakati wao kuonyesha ukarimu wa watanzania.
“Sisi ndio wenyeji wao lazima tuonyeshe hawakukosea kuchagua kuja Tanzania, hivyo nawaasa wananchi kuwapa mapokezi mazuri na kuwakirimu wageni hawa ambao wengine watakwenda Zanzibar na wengine watabaki hapa kwa siku kadhaa kabla ya kuondoka,” alisema Bi. Mdachi na kusisitiza:
“Tanzania ina vivutio vingi, kama nilivyowahi kueleza siku za nyuma treni hii ambayo imeanza safari yake katika mji wa Pretoria Afrika wiki kadhaa zilizopita na kukanyaga reli ya TAZARA katika kituo cha Kapiri Mposhi nchini Zambia Julai 11, kisha ikakanyaga ardhi ya Tanzania Julai 12 imepitia vituo kadhaa vya kiutalii ikiwemo Mbuga ya Selous.”
TTB ipo katika mazungumzo na uongozi wa TAZARA ili kutumia nafasi ya wageni wanaotoka mataifa mbalimbali kujifunza utamaduni wa Tanzania pamoja na kutembelea vivutio vya kiutalii ili wanaporejea katika mataifa yao kuelezea uzuri wa nchi hii.
 Mkurugezi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bibi Devota Mdachi akisalimiana  na mmoja wa watalii waliowasili Jijini Dar es salaam kwa treni kutokea Afrika ya kusini. Jumla ya watilii 65 wamewasili Tanzania kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini. Hivi ni jitihada za TTB katika kutangaza vivutio vya utalii.

Mkuuwa Idara ya Masoko  wa TAZARA,Bwana Hemed Msangi(wapili kulia)akisalimiana na Meneja wa Treni ya Rovos Rail Bi. Daphne Mabala(kushoto) mara baada ya kuwasili na treni hiyo Jijini Dar es salaam ikiwa na watalii 65 kutokea Afrika ya kusini waliokuja kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya utalii Tanzania(TTB) Bi.Devota Mdachi. Hizi ni jitihada za Bodi ya utalii nchini katika kujitangaza.

 Watalii 65 wakishuka kwenye Treni  aina ya Rovos Rail jijini Dar es salaam wakitokea Afrika ya Kusini. Ikiwa ni jitihada za Bodi ya Utalii Nchini (TTB) na TAZARA katika  kufanikisha ujio wa watalii hao waliokuja kujionea  vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.
 Mmoja wa watalii kutoka Afrika ya Kusini akicheza ngoma ya kitamaduni ikiwa ni sehemu ya mapokezi kwa ujumbe wa watilii 65 waliowasili nchini kwa kutumia Treni aina ya Rovos Rail ambayo ni treni ya pili kwa ubora Duniani.

Mkuuwa Idara ya Masoko  wa TAZARA,Bwana Hemed Msangi(katikati) akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Mstaafu Thomas Mihayo walipotembelea na kuona mandhari ya Treni aina ya Rovos Rail ambayo ni treni ya pili kwa ubora Duniani ilipowasili Jijini Dar es salaam kutokea Afrika kusini ikiwa na jumla ya watalii 65 waliokuja kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini. 

Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA


Ujenzi wa Barabara ya Ipembe-Msongole Kuanza Mwezi Juni Mwaka huu.

0
0
Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 107.56 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Ipemba hadi Isongole wilayani Ileje yenye urefu wa kilomita 50.3 kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mkoa wa Songwe na Nchi jirani ya Malawi.

Naibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo amesema ujenzi huo utaanza mwezi juni Mwaka huu na kukamilka mwezi June, 2019.

“Tayari mkandarasi ameshapatikana na sasa ameanza kufanya maandalizi ya kuleta vifaa vitakavyotumika katika ujenzi huu, Serikali ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kukamilisha ahadi hii kwa miezi ishirini na nne toka pale ujenzi utakapoanza”. amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Eng. Ngonyani amesema kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ni katika hatua za kutekeleza ahadi iliyotolewa na Serikali kwa wanachi wa mkoa huu katika vipindi tofauti tofauti vya uongozi.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akipata maeleozo ya mtandao wa ramani ya barabara za Mkoa wa Songwe kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa wakati wa ziara yake ya kukagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM). 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipokea maoni ya mkazi wa wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wakati wa ziara yake ya kukagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM)  ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaanza mwezi juni Mwaka huu. 

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International ltd, Canada kuhusu kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara Mafinga-Nyigo KM 74.1 wakati alipokagua maendeleo ya mradi huo Mkoani Njombe. 


FEZA SEKONDARI YATOA ALIYEONGOZA KIDATO CHA SITA KITAIFA KWA WAVULANA KATIKA MASOMO YA SANAA

0
0
 Mwanafunzi Francis Thomas aliyemaliza kidato cha Sita katika shule ya Wavulana ya Feza akiwa amebebwa juu na wanafunzi wenzie wa shule hiyo baada ya kuibuka Mwanafunzi bora kitaifa katika Masomo ya Sanaa na Biashara katika matokeo yaliyotangazwa na baraza la mitihani Julai 15, 2017.
  Mwanafunzi Francis Thomas aliyemaliza kidato cha Sita katika shule ya Wavulana ya Feza  akiwa katika picha ya pamoja na Wazazi wake wote wawili ,Thomas Samky na Victoria Samky walipofika shuleni hapo
 Wanafunzi waliofanya vizuri katika Mitihani ya Kidato cha sita na kuwamo katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa, Kabhabhira Bukuru na Atuganile Cairo wakiwa ni wenye furaha kufuatia matokeo kutoka ambapo Atuganile amekuwa wa tatu kitaifa katika Masomo ya Sayansi na Kabhabhira amekuwa wa Saba katika masomo hayo.
 Mwanafunzi aliyefanya vizuri na kuwa wa tatu  katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa ,  Atuganile Cairo akiwa na Mama yake Mzazi  akimpongeza kwa kufanya vizuri katika mtihani huo wa kidato cha Sita
 Wanafunzi waliofanya vizuri na kuwamo katika 10 bora ya wasichana waliofanya vizuri kitaifa ,Kabhabhira Bukuru na Atuganile Cairo  wakisalimiana na Mwalimu mkuu wa Shule ya Wasichana fedha ,Ibrahim Rashid pamoja na baba yake atuganile Jimmy Cairo

MASAUNI, MKUU WA WILAYA MUHEZA WAFANYA OPARESHENI USIKU KUWASAKA WAHALIFU MSITU WA AMANI MKOANI TANGA

0
0
Na Felix Mwagara (MOHA) 
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mkoani Tanga kufanya operesheni ya kuwasaka waharibifu  wa chanzo cha maji cha Mto Zigi ambao unapeleka maji Tanga mjini.

 Masauni alifika katika eneo hilo la tukio saa mbili usiku na kujionea maeneo yaliyoharibiwa kwa kuchimbwa mashimo makubwa na wahalifu hao wakidai kuwa wanatafuta madini ya dhahabu. Hata hivyo, hakuna mhalifu aliekamatwa katika eneo hilo wakati wa oparesheni hiyo. 
Akizungumza katika eneo hilo lililopo Tarafa ya Amani, wilayani humo jana, Masauni ambaye pia aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu, alisema Jeshi la Polisi litaendelea kufanya oparesheni katika eneo hilo usiku na mchana kwa kushirikiana na walinzi wa msitu  ili kuwaondoa wahalifu hao haraka iwezekanavyo. 
Masauni alisema licha ya Polisi kuendelea kufanya doria katika eneo hilo lakini wanatarajia kufungua kituo cha polisi ili kuongeza ulinzi zaidi katika eneo hilo muhimu ambalo ndio chanzo cha maji kwa sehemu kubwa ya wakazi wa Mji wa Tanga. 
“Tumepanga kuimarisha ulinzi zaidi katika eneo hili kwa kujenga kituo cha polisi ambapo askari wetu watashirikiana na walinzi wa misitu kufanya doria ya kupambana na wahalifu,” alisema Masauni na kuongeza;


“Kwa habari zisizo rasmi tulizozipata katika vyanzo vyetu, hawa wahalifu wanamtandao mkubwa wakishirikiana na watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na hata baadhi ya watumishi wa umma, tutaendelea kufanya uchunguzi huu kwa kina kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ili kuwabaini wahalifu wote haraka iwezekanavyo.”

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti), akiongozwa na Afisa Tarafa ya Amani, wilayani Muheza, Ayubu Mhina kumuonyesha eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji cha Mto Zigi ambalo linasambaza maji sehemu kubwa ya Jiji la Tanga ambalo limeharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimo wakidai kuwa wanatafuta madini ya dhahabu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi linafanya oparesheni katika eneo hilo mara kwa mara na pia linatarajia kujenga Kituo cha Polisi katika eneo hilo ili kupambana na wahalifu hao. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Muheza, Oscar Joshua, na kulia ni Mshauri wa Wagambo wilayani humo.  
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimsikiliza Mhifadhi Msaidizi Hifadhi ya Asili Amani, wilayani Muheza, Bob Matunda (wapili kushoto), alipokua anamuonyesha eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji cha Mto Zigi lililoharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimbo wakidai wanatafuta madini ya dhahabu katika eneo hilo. Masauni aliongozana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya muda wa usiku kwenda kuangalia waharibifu hao walivyoliharibu eneo hilo.  
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimfafanulia jambo Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo (kulia), mara baada ya kuangalia eneo la chanzo cha maji katika hifadhi ya Msitu wa Asili wa Amani ambalo liliharibiwa na wahalifu kwa kuchimba mashimo katika eneo la Kihara ambalo ni chanzo cha maji, wakidai wanatafuta madini ya dhahabu katika eneo hilo.  Masauni akiongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo, walifika eneo hilo la tukio muda wa usiku.  Katikati ni Afisa Tarafa ya Amani, wilayani Muheza, Ayubu Mhina. 
Mbunge wa Jimbo Muheza, Balozi Adadi Rajabu akimuonyesha  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), ameneo mbalimbali yaliyoathiriwa na wachimbaji wa madini katika eneo hilo ambalo ni muhimu kutokana kuwa na chanzo cha maji ambayo yanatumika katika eneo kubwa mkoani Tanga. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanaasha Tumbo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images